MKUTANO MKUU WA 10 WA KAUKI

MKUTANO MKUU WA 10 WA KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

KAUKI-Kidamali, Iringa

KAUKI-Kidamali, Iringa
Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Thursday, April 11, 2013

TAARIFA YA UGONJWA KWA WANA-KAUKI

Uongozi wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) kwa niaba ya Wanaukoo wote, unawataarifu ndugu, jamaa na marafiki, kuwa Bi. Gidagamhindi (Cecilia) Sigatambule Sekivenule (maarufu kama Mama Severin Nyangalima), anaumwa na hali yake ya afya siyo ya kuridhisha.

Bi. Gigadamhindi alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Ipamba-Tosamaganga, Iringa kwa takribani wiki mbili, hadi tarehe 10 Aprili aliporuhusiwa kurudi nyumbani. 

Taarifa zilizopatikana zinasema kuwa licha ya kuruhusiwa kurudi nyumbani, bado hali siyo ya kuridhisha. Bado tunaendelea kufuatilia taarifa za mgonjwa licha ya kuwa bado hatujawapata Ndugu wa karibu wa akina Nyangalima baada ya simu zao kutopatikana kabisa. 

Baada ya mazungumzo na Ndugu Faustino Sigatambule Kivenule siku ya Alhamisi ya tarehe 11 Aprili 2013, ambaye ni Kaka wa Bi Gidagamhindi, aliniahidi leo tarehe 12 Aprili 2013, Ijumaa, ataenda nyumbani kwake Kijijini Magubike na kisha kutupatia taarifa kamili.

Bi Gidagamhindi ni mmoja wa mihimbili ya Ukoo wa Kivenule ambao wamebakia akiwa ni mtoto wa Kwanza wa Sigatambule Tavimyenda Kivenule. Pamoja na afya yake kudorora, Bi Gidagamhindi anakabiliwa na uzee kutokana na kuwa na umri mkubwa. 

Uongozi wa KAUKI unatoa wito kwa Wana-KAUKI wote kumwombea na ikibidi kutoa kila aina ya msaada unaohitajika.

Imetolewa na:


Adam Alphonce Kivenule
Katibu Mkuu - KAUKI











 

No comments:

Post a Comment