MKUTANO MKUU WA 10 WA KAUKI

MKUTANO MKUU WA 10 WA KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

KAUKI-Kidamali, Iringa

KAUKI-Kidamali, Iringa
Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Friday, May 17, 2013

MATUKIO MBALIMBALI YA KIJAMII YA WANA-KAUKI KATIKA PICHA

Wana-KAUKI katika moja ya shughuli za kijamii, kutoka kushoto ni Mke wa Onesmo Kivenule, Onesmo Kivenule, Bi Anyesi Sigatambule Kivenule na Bi Asia John Kivenule

Hawa wote ni Kivenule Hazina ya KAUKI, wakiwa katika sherehe ya kijamii, kutoka kushoto ni Magreth,..., Frank, Theopista, Emmanuel na Lucy


Ndugu Onesmo Kivenule katikati akiwa na Shangazi yake Kulia na Mke wake Kushoto katika moja ya hafla

Kutoka Kushoto ni Ndugu Innocent Kivenule, Ignus Kivenule na Delfinus Kivenule

Wana-KAUKI wakiwa katika Vikao vya Kijamii

Hii ni moja ya maombolezi ya msiba wa Mama Mzazi wa Katibu wa KAUKI huko Mseke Iringa

Hapa ni nyumbani Mafinga kwa Katibu wa sasa wa KAUKI, ilikuwa ni wakati wa msiba wa Mama yake Mzazi

Katibu wa sasa wa KAUKI, Ndugu Adam Kivenule (wa kwanza kushoto) akiwa na jamaa zake katika moja ya Hoteli ya Kitalii huko Windhoek, Namibia wakati anahitimisha mafunzo yake ya Elimu ya Masafa kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano na habari. Anayefuata kutoka kushoto ni Banda kutoka Zambia, aliyesimama Simon- Kenya, Rose-Kenya na mwisho kulia ni kutoka Zambia

Katibu wa sasa wa KAUKI, Ndugu Adam Kivenule (wa tatu kushoto) akiwa na jamaa zake katika moja ya Hoteli ya Kitalii huko Windhoek, Namibia wakati anahitimisha mafunzo yake ya Elimu ya Masafa kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano na habari.

Katibu wa sasa wa KAUKI, Ndugu Adam Kivenule (wa kwanza kushoto) akiwa na jamaa zake katika moja ya matembezi katika hifadhi za wanyama, Windhoek, Namibia wakati anahitimisha mafunzo yake ya Elimu ya Masafa kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano na habari.

Katibu wa sasa wa KAUKI, Ndugu Adam Kivenule (mwenye tisheti nyeusi na miwani) akiwa na jamaa zake katika moja ya Hoteli ya Kitalii huko Windhoek, Namibia wakati anahitimisha mafunzo yake ya Elimu ya Masafa kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano na habari.



Wana-KAUKI katika mmoja ya mikutano ya KAUKI iliyofanyika Katika Kanda ya Kidamali

Wana-KAUKI katika mmoja ya mikutano ya KAUKI iliyofanyika Katika Kanda ya Kidamali

Wana-KAUKI katika mmoja ya mikutano ya KAUKI iliyofanyika Katika Kanda ya Kidamali

Wana-KAUKI katika mmoja ya mikutano ya KAUKI iliyofanyika Katika Kanda ya Kidamali

Wana-KAUKI katika mmoja ya mikutano ya KAUKI iliyofanyika Katika Kanda ya Kidamali

Wana-KAUKI katika mmoja ya mikutano ya KAUKI iliyofanyika Katika Kanda ya Kidamali

Wana-KAUKI katika mmoja ya mikutano ya KAUKI iliyofanyika Katika Kanda ya Kidamali

Wana-KAUKI katika mmoja ya mikutano ya KAUKI iliyofanyika Katika Kanda ya Kidamali

Wana-KAUKI katika mmoja ya mikutano ya KAUKI iliyofanyika Katika Kanda ya Kidamali

Ndugu Donath Mhapa, Mwenyekiti wa KAUKI

Mzee William Kivenule na Ndugu Christian Kivenule wakibadilishana mawazo katika Mkutano Mkuu wa 8 wa KAUKI uliofanyika Jijini Dar es Salaam, mwaka 2012

Mwenyekiti wa KAUKI na Mweka Hazina wa Kanda ya Dar es Salaam, wakibadilisha mawazo wakati wa Mkutano Mkuu wa KAUKI Kanda ya Dar es Salaam, 2012

Wana-KAUKI kutoka Kanda ya Dar es Salaam wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza mkutano wa KAUKI uliofanyika Katika Kanda ya Dar es Salaam

Wana-KAUKI katika mmoja ya mikutano ya KAUKI iliyofanyika Katika Kanda ya Dar es Salaam

Mzee William Kivenule kutoka Kidamali. Ni mmoja wa watoa mada katika Mikutano ya KAUKI. Ni mtu muhimu sana.

Friday, May 10, 2013

TATHMINI YA KAUKI KUELEKEA MKUTANO MKUU WA 9 WA KAUKI, 2013

Kuelekea Mkutano Mkuu wa 9 wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI), kama mtendaji Mkuu wa umoja huu, ninakuja na tathmini ifuatayo:
  • Hatukufahamiana miongoni mwetu, 
  • Hatukuwa karibu kama ilivyo sasa, 
  • Hatukushirikiana baina yetu kama inavyofanyika sasa katika shida na raha,
  • Hatukutembeleana majumbani mwetu kama inavyofanyika leo hii.

Kwa muda wa miaka 8 ya KAUKI, tunashuhudia yafuatayo:
  1. Undugu, ushirikiano na mahusiano baina yetu yameboreka vilivyo:
  2. Tumefahamiana kama wana-ukoo na ndugu kutoka maeneo ya Irore, Nduli, Itagutwa, Mgongo, Igominyi, Isimani, Iringa Mjini, Kalenga, Kalenga, Nzihi, Kipera, Kidamali, Magubike, Nyamihuu, Idete, Ibogo, Nyamahana, Ipogolo, Mufindi, Dar na Morogoro;
  3. Kila mwaka tuna uhakika wa kukutana, kupongezana na kufarijiana kutokana na matukio mengi ya kijamii yaliyotokea katika jamii yetu;
  4. Hamasa na wahamasishaji wa kujitolea wapo na wenye moyo wa kujituma.

Tuiunge mkono KAUKI kwa nguvu zote ili isife, kwa kutoa michango na kushiriki Mkutano Mkuu wa 9 wa KAUKI, Kidamali - Iringa.

Imeandaliwa na kutolewa na:



KAUKI
Kanda ya Dar es Salaam

CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO WA KIVENULE



Toleo la Kwanza
UKOO NI NINI?
Ukoo ni muungano wa familia kadhaa zenye utambulisho fulani. Unaweza kuwa utambulisho wa jina, alama au mwelekeo mmoja. Utambulisho wowote kati ya hizo nilizotaja, unaufanya ukoo utambulike miongoni mwa jamii mbalimbali. Mara nyingi utambulisho ambao huufanya ukoo utambulike baina ya jamii za Kiafrika ni Jina. Pamoja na jina, halikadhalika kuna tunu (values) mbalimbali ambazo huheshimiwa na ukoo husika na jamii kwa ujumla.

Tunu hubeba mambo mengi, ikiwa ni pamoja na miiko, maadili, heshima, vyakula na tamaduni. Sambamba na tunu, pia kuna Mila na Desturi, ambazo huzingatiwa sana katika masuala ya kijamii, mfano wakati wa kuoa au kuoza, misiba, sherehe za jadi mfano matambiko na masuala ya kimila.

Ukoo wa Kivenule ni mmojawapo wa koo nyingi kubwa zilizopo katika Himaya ya Uhehe katika Mkoa wa Iringa. Ukoo wa Kivenuloe ulianza kutambulika toka Karne ya 18. Historia inaonesha kuwa Ukoo huu asili yake ni kutoka kwa Wabena-Manga, waliopo Kusini mwa Mji wa Iringa; yaani maeneo ya Mufindi na Njombe. Ni mchanganyiko wa Wahehe na Wabena wanaojulikana kama Wabena-Manga.

Wahehe ni moja kati ya makabila makubwa hapa Tanzania ambalo kiasili linaishi katika Wilaya za Kaskazini mwa Mkoa wa Iringa, yaani Iringa Vijijini, Iringa Mjini, Kilolo na Mufindi. Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali zinazopatikana na kutafitiwa, inasemekana kuwa ni moja kati ya makabila yaliyotokea kwenye bonde la mto Rufiji; yaani Wahehe wenye Asili ya Ungazija. Pengine hata ile sababu ya kuzika wafu wao wakielekea mashariki inapewa uzito.

Lugha ya Kabila hili ni Kihehe na limegawanyika kiasi fulani katika lahaja (matamshi) tofautitofauti kutokana na maeneo ambayo huzungumzwa. Inafanana kimatamshi na kimaana na lugha ya Kibena iliyopo wilayani Njombe. Pamoja na Wabena wanahesabika kuwa zaidi ya watu milioni moja. Wengi wao ni wafuasi wa Ukristo, hasa wa Kanisa Katoliki (Jimbo Katoliki la Iringa). Kihistoria Wahehe ni maarufu kwa jinsi walivyopambana na Wajerumani walioteka maeneo yao, k.m. katika pigano la Lugalo mwaka 1891. Kiongozi wao alikuwa Chifu Mkwawa.

Katika kuenzi na kutunza tunu za asili za Uhehe, Ukoo wa Kivenule hauli nyama ya Mbawala (kwa lugha ya Kihehe Mato/Imato). Imani kubwa imejengeka miongoni mwa jamii ya Ukoo wa Kivenule kuwa kula Mbawala ni kuvunja miiko ya Ukoo ambayo iliyowekwa na Waasisi wetu (Babu zetu). Mara mwanaukoo anapokiuka miiko hii na kula nyuma ya Mbawala (Imato) basi huweza kufikwa na matatizo mbalimbali, mfano kudhurika afya yake. Mara nyingi huwapata matatizo kama ya kuvimba miguu na pengine kuoza kabisa.

Tunu nyingine ambazo Ukoo wa Kivenule unazienzi kama zilivyo koo nyingine katika Uhehe ni Miitikio (Midikiso). Tunu hii huutambulisha Ukoo wa Kivenule miongoni mwa Koo za Wahehe. Mwitikio (Mwidikiso) wa Ukoo wa Kivenule ni 'MLIGO'. Mwitikio huu hutumika katika maeneo mbalimbali mfano katika salamu, kuapa (kufanya viapo) na pia kujitofautisha na koo nyingine. Miitikio (Midikiso) huutambulisha Ukoo wa Kivenule katika koo nyingine katika ardhi ya Uhehe.

CHIMBUKO LA UKOO WA KIVENULE
Kwa Asili, Ukoo wa Kivenule ni maarufu kama Wapiganaji wa Vita. Ukoo wa Kivenule ulikuwa hodari sana katika vita vya msituni ambavyo viliwahusisha Babu zetu akina TAGUMTWA. Enzi hizo za Mababu zetu vita za Koo na Kabila zilipiganwa maeneo mengi ya himaya ya Uhehe kwa lengo la kupata mali, mifugo na heshima.

Babu TAGUMTWA BALAMA (KIVENULE) ndiye aliyewazaa Babu TAVIMYENDA KIVENULE na Babu KALASI KIVENULE. Ikumbukwe kuwa, jina halisi la ukoo wa Kivenule ni BALAMA. Kama ilivyokwisha julikana katika mada iliyowasilishwa katika Mkutano Mkuu wa Kwanza na wa Pili wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule, ambapo ilielezwa kuwa, neno KIVENULE linamaanisha sifa ya kuwa jasiri Vitani na hasa katika kutumia silaha za Mishale na Mikuki yaani kwa Lugha Asilia ya Kihehe “KUMIGOHA”.  Yaani kwa maana nyingine LIGALU yenye maana ya Kwihoma ImigohaKuhoma Watavangu au Kuvenula Avatavangu. LIGALU maana yake Vita. Kuhoma maana yake Kuchoma na Migoha maana yake Mikuki. Venula maana yake ua, fyeka maadui.

LIGALU ndiyo iliyochangia kuzaliwa kwa jina la Ukoo la KIVENULE. KIVENULE maana yake ni Ushujaa kutokana na Shabaha ya Mikuki.
KUVENULA likiwa na maana halisi ya kuwa na shabaha ya kuwaangamiza maadui kwa kutumia silaha ya Mishale na Mikuki. Babu zetu akina TAGUMTWA BALAMA walilidhihirisha hili katika Vita na Watavangu na hivyo kusababisha kuzawadiwa kwa jina la KIVENULE kama jina la sifa kutokana na ushujaa katika Vita.

Tagumtwa alijulikana kama anatoka Ukoo wa Balama na alikuwa na Shabaha sana ya Mikuki katika uwanja wa Vita. Alikuwa hakosei shabaha (target) na hivyo hupelekea kuwaangamiza na kuwaua sana maadui. Wakati akiwamaliza/fyeka/au adui zake kwa Mikuki, Wakuu wa Vita (Vatavangu) walikiita kitendo hicho 'KUVENULA'. Taarifa za Tagumtwa kuua (Kuvenula) adui zake katika uwanja wa vita, zilizagaa kila mahali na hivyo kupelekea Wakuu (Viongozi) wa Vita (Vatavangu) kumzawadia Jina la KIVENULE, kama jina la sifa na heshima kwa kuwa shujaa wa Vita.

Ikumbukwa kuwa asili ya Ukoo wa Kivenule ni kutoka katika ukoo wa BALAMA (MWIBALAMA). Hawa ni ndugu wa karibu wa Kivenule kabisa na hawapaswi kuoana. Koo za Mwibalama zinapatikana maeneo mengi katika Mkoa wa Iringa hususani katika Wilaya  za Mufindi, Iringa Vijijini, Iringa Mjini na Kilolo; hali kadhalika kama ilivyo ukoo wa kina Mwakivenule.

TAGUMTWA KIVENULE alifia katika uwanja wa mapambano (vita) na mwili wake haukuweza kupatikana. Kama zilivyo koo za machifu au watu maarufu miili yao ilikuwa haizikwi. Baada ya kufa iliegemezwa kwenye miti mikubwa na kuliwa na wanyama. Wakija watu wasiukute mwili basi huamini kuwa mwili umechukuliwa na Mungu.

KUKUA NA KUZAGAA KWA UKOO WA KIVENULE
Kwa mujibu wa taarifa mbalimblai za kitafiti ambazo zimekuwa zikifanyika toka mwaka 2005 hadi sasa 2013; kupitia mikutano mbalimbali ya KAUKI; zinabainisha kuwa, BABU   NYAKUDIRA BALAMA  alimzaa BABU KANOLO BALAMA. Hali kadhalika BABU KANOLO BALAMA alimzaa MTENGELINGOMA BALAMA.

Baada ya hapo, tunaona sasa Kizazi cha TAGUMTWA KIVENULE kinaanza kujitokeza. Hii ilikuwa ni Karne ya 18. TAGUMTWA KIVENULE alizaa watoto wawili (2).  Bado utafiti unafanyika kumfahamu Mama wa watoto hawa. Watoto wa Tagumtwa Kivenule walikuwa TAVIMYENDA KIVENULE na KALASI KIVENULE. Kwa mujibu wa taarifa kadhaa tulizonazo kwa sasa; hawa ni vinara wa Ukoo wa Kivenule ulioenea maeneo mbalimbali hapa Tanzania.

Tavimyenda Kivenule na Kalasi Kivenule katika harakati za kutafuta maisha walifika katika eneo la Kalenga, mahali alipoishi Mkwawa na kukutana na na Mwamyinga, aliyekuwa mfugaji maarufu katika eneo la Ulefi huko Magubike, Iringa Vijijini. Tavimyenda Kivenule alibahatika kupata kazi kwa Mwa-Myinga baada ya kuombwa kwenda kumwangalizia mifugo yake huko Magubike, huku akimwacha mwenzake Kalasi pale Kalenga.

Kalasi Kivenule yeye hakupata fursa hiyo ya kazi na hivyo akaamua kuelekea eneo Irore katika Wilaya Iringa Vijijini (kwa sasa Kilolo) kutafuta maisha. Huu ukawa ni mwanzo wa kugawanyika kwa watoto hawa wawili wa Tagumtwa Kivenule.

Tavimyenda Kivenule akielekea upande wa Magharibi mwa Mji wa Iringa na Kalasi alielekea upande wa Mashariki mwa Mji wa Iringa.

Historia inabainisha kuwa pamoja na Babu hawa kugawanyika kutokana na utafutaji wa maisha, mahusiano na ushirikiano baina yao haukuvunjika. Babu zetu waliendelea kushirikiana na kutembelea licha ya ukoo kukua na kuwa mkubwa sana.

KIZAZI CHA TAVIMYENDA KIVENULE
Katika Karne ya 19 hadi 20, Kizazi cha Tavimyenda Kivenule kilizaliwa na kuzagaa katika maeneo ya Ulefi, Magubike na Mlafu, Wilaya ya Iringa Vijijini, Iringa Mjini na maeneo mengine mkoani Iringa.

Taarifa tulizonazo kupitia tafiti tunazofanya, hali inaonesha kuwa, Babu Tavimyenda alikuwa na wake watatu (3), ambao ni:
1.     Bibi         Mkami         Sekabogo
2.     Bibi         Senosa
3.     Bibi         Pili              Mvemba

Mke wa kwanza wa Tavimyenda Kivenule aliolewa akiwa na mtoto; aliyejulikana kama Bibi Sikimbilavi Semabiki. Kwa mke huyu wa Kwanza Sekabogo, Tavimyenda alizaa nae watoto wanne (4); ambao ni:
1.     Babu       Kavilimembe Kivenule
2.     Babu       Mgaifaida               Kivenule
3.     Babu       Sigatambule           Kivenule
4.     Babu       Hussein                 Kivenule (Bado yupo hai)

Kwa Mke wa Pili Bibi Senosa, Babu Tavimyenda akizaa nae watoto watatu (3); ambao ni:
1.     Babu       Abdallah                Kivenule
2.     Bibi         Sigungilimembe      Kivenule
3.     Bibi         Malibora                Kivenule
Watoto hawa wa Bibi Senosa waliishi maeneo ya Kihesa katika Mji wa Iringa.

Kwa upande wa mke wa Tatu wa Bibi Pili Mvemba; Babu Tavimyenda alizaa mtoto mmoja aliyejulikana kwa jina la BIBI MGASI KIVENULE (aliishi wapi). Babu Tavimyenda Kivenule amezikwa katika eneo la Ulefi.

Baada ya hapo kizazi hiki kimeendelea kukua hadi hivi sasa Karne ya 21. **Angalia Chati kuonesha Muundo wa Ukoo wa KIVENULE**

KIZAZI CHA KALASI KIVENULE
Kwa upande wa Kalasi Tagumtwa Kivenule, kizazi hiki kilienea maeneo ya Nduli, Mgongo, Itagutwa, Kigonzile, Igominyi na Irore. Taarifa zinaonesha kuwa, Babu Kalsi Kivenule alikuwa na wake wawili (2); yaani:
1.     Bibi         Semsakwa    Mnonikilwa
2.     Bibi         Mnyamtage   Sekindole

Bibi Semsakwa Mnoni Kirwa kwa Babu Kalasi Kivenule alizaa watoto wawili (2) ambao ni:
1.     Bibi Cheilaje Nginasambula Kivenule
2.     Gingilemesa Kivenule

Kwa bahati mbaya hakuna taarifa zozote za hawa watoto wawili wa Kalasi.

Kwa upande wa Bibi Mnyamtage Sekindole, Babu Kalasi Kivenule alizaa mtoto mmoja ambaye ni Salamalenga Kahengula Kivenule. Bibi Mnyatage Sekindole awali alikuwa ameolewa kwa Mwa-Mhumba na kuzaa nae mtoto mmoja aliyeitwa Bibi Mganga Semhumba na baadaye kufariki. Baada ya hapo aliolewa na Kalasi ambapo pia alizaa mtoto mmoja tu anayefahamika kwa jina la Salamalenga Kahengula Kivenule. * Angalia watoto wa Kahengula katika Chati ya Muundo wa Ukoo wa Kivenule*

Kuna taarifa nyingi kutoka kwa Babu Tavimyenda Kivenule na Kalasi Kivenule. Mwingiliano wa koo nao unaonesha simulizi hizi. Kwa upande wa Tavimyenda mke wa Kwanza Bibi Mkami Sekabogo alikuwa na mtoto wa kufikia, aliyejulikana kwa jina la Bi Sikimbilavi Semabiki. Hatujapata taarifa rasmi kuhusiana na kizazi cha Bibi huyu, kama ilivyotokea kuwa Sipanganakumtwa Mwilongo Regina Sematagi aliyekuwa mtoto wa kufikia Bibi Semkonda mke wa Salamalenga Kahengula Kivenule.

Sipanganakumtwa Mwilongo Regiona Sematagi amesaidia kueneza kizazi cha Ukoo wa Mnyavanu. Taarifa zaidi na ukoo wa Mnyavanu upo katika Chati ya Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule.**

TABIA YA KIZAZI CHA TAVIMYENDA NA KALASI KIVENULE KUOA WAKE WENGI
Tabia nyingine ya kizazi hiki cha Tavimyenda na Kalasi ilikuwa ni kuoa wake wengi. Kwa mfano Tavimyenda pekee alikuwa na wake watatu. Hali kadhalika Kalasi naye alikuwa na wake wawili.

Hali hii ya kuwa na mke zaidi ya mmoja walirithi watoto wao. Kwa mfano watoto watatu wa kiume wa Tavimyenda waliozaliwa kwa Bibi Mkami Sekabogo walioa wake wawili hadi watatu. Mtoto wa kwanza wa Babu Tavimyenda Kivenule aliyejulikana kama Kavilimembe Kivenule alikuwa na wake wawili (2). Mtoto wa tatu wa Bibi Mkamai Sekabogo, aliyejulikana kwa jina la Sigatambule Matesa Kivenule, alikwa na wake watatu. Hali kadhalika mtoto wa nne wa Bibi Mkami Sekabogo anayejulikana kama Hussein Kivenule alikuwa na wake wawili. Mtoto pekee wa Pili wa Bibi Mkami hakubahatika kuwa na familia; na alijiita jina la kujinyanyapaa "Mgaifaida" Kivenule.

Sambamba na tabia ya Ukomo wa Kivenule kuoa mke zaidi ya moja; pia kuna utamaduni uliojitokeza kwa baadhi ya watoto wa Bibi Mkami Sekabogo kuoa dada na mdogo wake. Hili linajidhihirisha kwa wake wawili wa Babu Kavilimembe Kivenule ambao walikuwa ni Bibi Sikumwendinguluvi Sekusiga (Bi Mkubwa) na Bibi Gakumwalia Sekusiga (Bi Mdogo).

Hali kadhalika kwa mtoto wa tatu wa Bibi Mkami Sekabogo; Babu Sigatambule Matesa Kivenule alioa wake watatu, ambapo wake wawili wakubwa, 'Bibi Sikumwendinguluvi Singaile (Bi Mkubwa) na Bibi Nyanyilemale Singaile (Bi Mdogo wa Pili); na wa tatu aliitwa Bibi Pangulimale Setwanga.

Mtoto wa nne wa Bibi Mkami Sekabogo Hussein Kivenule, yeye alioa wake wawili kutoka familia tofauti. Wake zake waliitwa Bibi Yimilengeresa Semsisi (Bi Mkubwa) na Bibi Dalika Setala (Bi Mdogo). Kwa upande wa watoto Kalasi Kivenule, mtoto wake Salamalenga Kahengula Kivenule naye alioa wake watatu; ambao ni Bibi Semkonda, Bibi Semfilinge na Bibi Nyangali.

Hatujapata taarifa rasmi za watoto wa Kalasi kutoka kwa mke wake Bibi Semsakwa Mnonikilwa ambao ni Cheilaje Nginasambula Kivenule na Gingilemesa Kivenule. Kwa upande wa Kahengula yeye alioa kutoka katika familia tofauti.

UZAO WA BABU KAVILIMEMBE, MGAIFAIDA, SIGATAMBULE NA HUSSEIN KIVENULE
Babu Kavilimembe Kivenule aliishi eneo la Magubike, Wilaya ya Iringa Vijijini, huku akipakana na Ulefi upande wa Kaskazini, Idete na Ibogo upande wa Magharibi. Akiwa ameoa wake wawili wa familia moja, Babu Kavilimembe alibahatika kupata watoto sita (6).

Kwa upande wa mke wa kwanza Bibi Sikumwendinguluvi Sekusiga; Mzee Kavilimembe Kivenule alipata watoto wafuatao:
1.     Elizabert           Kivenule
2.     Dalikimale         Kivenule
3.     Sandra              Kivenule
4.     Pangalasi          Kivenule

Na kwa mke mdogo Bibi Gagumwalia Sekusiga, Mzee Kavilimembe alipata watoto wawili ambao ni:
1.     Salikuvaganga   Kivenule
2.     Francis             Kivenule

Watoto hao wa Babu Kavilimembe wengi wao waliishi maeneo ya Ulefu na Magubike. Baadhi yao walihamia maeneo mengine kama Nzihi, ukiacha wale waliokuwa watumishi wa serikali wakaenda kuishi maeneo mbalimbali. Babu Kavilimembe amezikwa eneo la Magubike, Iringa Vijijini.

Kwa upande wa Babu Mgaifaida Kivenule, yeye hakubahatika kupata familia. Mgaifaida alikuwa na ulemavu ambao ulimfanya ashindwe kutembea katika hali ya kawaida. Muda mwingi aliishi eneo la Ulefu kabla ya sehemu kubwa ya Ukoo wa Kivenule kuhamia sehemu ya Mlafu. Baada ya kufariki, alizikwa Mlafu.

Babu Sigatambule Matesa Kivenule alikuwa ni mtoto wa tatu wa Tavimyenda Kivenule kwa Bibi Mkami Sekabogo. Babu Sigatambule aliishi Ulefi, akahamia Mlafu na baadaye Kidamali. Babu Sigatambule ndiye aliyehakikisha Ukoo wa Kivenule unapata eneo la Mlafu huku akipambana na Wagiriki. Walowezi na wawekezaji katika zao la Tumbaku.

Babu Sigatambule Kivenule katika uhai wake alibahatika kuoa wake watatu (3); huku wake zake wawili wakitoka katika familia moja ya ukoo wa Singaile. Wake zake hawa wakubwa waliitwa Bibi Sivangumhavi Singaile na Bibi Nyanyilimale Singaile. Mke wa Tatu wa Babu Sigatambule aliitwa Bibi Pangulimale Setwanga. Wote waliishi Mlafu na baadaye kuhamia eneo Kidamali.

Wake zake wawili Bibi Nyangilimale Singaile na Bibi Pangulimale Setwanga bado wapo hai na wanaishi Kidamali.

Watoto wa Babu Sigatambule Kivenule ni hawa wafuatao:
Kwa Bibi Sivangumhavi Singaile (Mke Mkubwa):
1.     Gidagumhindi    Cecilia          Kivenule
2.     Semyamba        Khadija        Kivenule
3.     Sivinitu             Alphonce      Kivenule
4.     Kadungu           William        Kivenule
5.     Fibumo             Xavery         Kivenule
6.     Mlagile             Anyesi          Kivenule
7.     John                                   Kivenule

Bibi Nyanyilimale Singaile (Mke wa Pili)
1.     Mgulwa             Agnes          Kivenule
2.     Luhanage          Ponsiano      Kivenule
3.     Mgendwa          Eusebio        Kivenule
4.     Msinziwa          Daniel          Kivenule
5.     Kanolo             Edward         Kivenule

Mke wa Tatu wa Bibi Pangulimale Setwanga
1.     Conjeta   Kivenule
2.     Pyela       Kivenule
3.     Faustino  Kivenule
4.     George    Kivenule
5.     Carolina  Kivenule

Babu Sigatambule Kivenule alifariki mwishoni mwa miaka ya 90 na kuzikwa eneo la Mlafu, Kidamali - Iringa.

Mzee Hussein Tavimyenda Kivenule alikuwa ni mtoto wa nne wa Bibi Mkami Sekabogo. Yeye aliishi eneo la Ulefi na baadaye Mlafu. Kwa sasa anaishi Magubike. Babu Hussein Kivenule kwa sasa anakadiriwa kuwa na miaka zaidi ya 113 kwa mujibu wa taarifa na tafiti ambazo tunazo.

Babu Hussein Tavimyenda Kivenule ameshiriki kikamilifu katika Vita vya Pili ya Dunia. Wakati anashiriki vita hiyo alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 44. Amepigana vita maeneo mbalimbali mfano Burma, India na Ulaya. Kwa sasa ana upofu wa macho ambao anasema ulisababishwa na Baruti. Hali kadhalika anakiri kuwa kuendelea kuwa hai ni kwa sababu alipigana upande wa Mwingereza. Anakiri vita ndiyo iliyomsababishia upofu pengine asingekuwa na hali aliyonayo kwa sasa.

Mzee Hussein Kivenule alioa wake wawili na kubahatika kupata watoto kumi na tatu (13). Kwa mke wake wa kwanza Bibi Yimilengeresa Semsisi. Babu Hussein alipata watoto wafuatao:
1.     Nyakudila          Benjemin      Kivenule
2.     Sekiyavile          Modesta       Kivenule
3.     Dominicus                            Kivenule
4.     Emmanuel                            Kivenule
5.     Luciana                                Kivenule
6.     Ajendina                              Kivenule

Kwa upande wa mke wa pili wa Bibi Dalika Setala, Mzee Hussein Kivenule alipata watoto wafuatao:
1.     Kabogo Bernadi           Kivenule
2.     Sembata Josephine      Kivenule
3.     Necia                         Kivenule
4.     Batromeo                   Kivenule
5.     Brandino                    Kivenule
6.     Tavina                       Kivenule
7.     Masikitiko                  Kivenule

Asilimia kubwa ya familia ya Babu Hussein Kivenule inaishi maeneo ya Magubike, Idete na Ibogo. Pia wapenda historia mnakaribishwa kwenda kumtembelea Babu Hussein Kivenule.

UZAO WA SALAMALENGA KAHENGULA KIVENULE
Babu Salamalenga Kahengula Kivenule alikuwa ni mtoto pekee wa kiume wa Babu Kalasi kwa mke wake wa pili Bibi Mnyamtage Sekindole. Kahengula pia ni kaka wa Bibi Mganga Semhumba, aliyekuwa mtoto pekee kwa Mwamhumba, aliyefariki mara tu baada ya kumzaa Bibi Mganga kwa Sekindole.

Babu Salamalenga Kahengula Kivenule alio wake watatu ambao ni:
1.     Bibi Semkonda
2.     Bibi Semfilinge
3.     Bibi Nyangali

Salamalenga anapomuoa Bibi Semkonda alimkuta na mtoto wa kufikia Sipanganakumtwa Mwilongo Regina Sematagi. Kwa wake zake hawa watatu, Babu Salamalenga alibahatika kupata watoto kumi na tatu (13). Kwa Bibi Semkonda alibahatika kupata watoto wafuatao:
1.     Pangayena        Kivenule
2.     Jonas               Kivenule
3.     Samwel             Kivenule
4.     Galasamaneno   Kivenule
5.     Daud (William)  Kivenule
6.     Barton              Kivenule

Kwa mke wa pili Bibi Semfilinge, Babu Salamalenga alizaa nae watoto watatu ambao ni:
Chagovanue Kivenule
Munguatosa Kivenule
Mwilimilisa Kivenule

Na kwa mke wa tatu Bibi Nyangali, Babu Salamalenga alizaa nae watoto wanne (4) ambao ni:
1.     Tindasulanga              Kivenule
2.     Sigongola                   Kivenule
3.     Shaban                      Kivenule
4.     Gungamesa                 Kivenule

MWINGILIANO NA KOO NYINGINE KATIKA HIMAYA YA UHEHE
Zaidi ya Koo mbalimbali 50 zinachangamana na Ukoo wa Kivenule. Hii ni kutoka Karne ya 18 ambapo kizazi hiki kilianza kujitambua na kujikusanya. Baadhi ya Koo ambazo zimechangamana na ukoo huu ni pamoja na koo za:
1.     Kabogo
2.     Kamtawa
3.     Katowo
4.     Kigereso
5.     Kindole
6.     Kisumbe
7.     Kiteve
8.     Kitu
9.     Kusiga
10. Lawa
11. Luhwavi
12. Lupola
13. Madembwe
14. Manimu
15. Matagi
16. Mdongwe
17. Mfilinge
18. Mhapa
19. Mhumba
20. Mkeng'e
21. Mkonda
22. Mnonikirwa
23. Mnyavanu
24. Msisi
25. Mtono
26. Mvemba
27. Myalla
28. Ngeng'ena
29. Ngolo
30. Ngwenga
31. Ngweta
32. Nyakunga
33. Nyangali
34. Nyangalima
35. Mvemba
36. Nzala
37. Sambagi
38. Senosa
39. Setala
40. Singaile
41. Utenga

Taarifa hizi ni sehemu kidogo ya taarifa tulizonazo na ambazo bado zinafanyiwa utafiti wa kina. Kwa maana hiyo, tumeiita ni Toleo la Kwanza. Tunatarajia kuwa na matoleo mengine yaliyoboreka zaidi.

Imeandaliwa na kusambazwa na:


Adam Alphonce Kivenule
Katibu Mkuu - KAUKI