Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa
Kivenule ulifunguliwa na Mgeni Rasmi Ndugu Daima Luvanda, ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kidamali.
Awali kabla ya yote, Mwenyekiti wa
Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Mkuu wa Ukoo Ndugu Faustino Kivenule,
aliwakaribisha ndugu, jamaa na wanaukoo kwa ujumla kwenye mkutano huo.
Kabla ya kusoma hotuba ya Ufunguzi
wa Mkutano Mkuu wa Ukoo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa
Kwanza wa Ukoo, alimkaribisha Ndugu George Kivenule, kuuombea Mkutano Mkuu kwa
sala.
Baada ya Sala ya kuuombea Mkutano
Mkuu, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Ukoo, alitumia
fursa hiyo kuisoma Hotuba ya Ufunguzi.
Alianza kwa kuwajulisha ndugu,
wanaukoo na wageni waalikuwa kuwa, lengo la Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa
Kivenule ni kuwaunganisha wanaukoo wote, wanaoishi sehemu mbalimbali hapa
Tanzania, ili wafahamiane, waelimishane na kupeana ujuzi katika nyanja
mbalimbali za maendeleo na kupeana uzoefu.
Pia, lengo jingine la Mkutano Mkuu
wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ilikuwa ni kutolewa na kufundishwa kwa Mada kadhaa
zenye nia ya kuujengea ukoo na kuwa na msimamo imara. Kwa kuwakusanya ndugu
pamoja, Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu, iliamini itasaidia kuujenga Ukoo
katika misingi ya Ushirikiano na Upendo na hiyvo kuwa na ukoo wenye umoja.
Lengo jingine la kufanya mkutano
mkuu wa ukoo ilikuwa ni kufanya senza ili kujua idadi ya wanaukoo na mwishoni
kufanya uchaguzi wa viongozi, watakaunda Uongozi wa Ukoo na pia watashirikiana
na Kamati ya Ukoo wa Kivenule katika kutekeleza majukumu mbalimbali.
Kamati itakayoundwa itakuwa na
jukumu la kuratibu mambo mbalimbali na matatizo yanayohusu ukoo.
Jumla ya Mada Tano ziliwasilishwa
na kufundishwa katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Mada
zilizowasilishwa ni pamoja na:
1.
CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO;
2.
MAHUSIANO BAINA YA NDUGU NDANI YA UKOO;
3.
ELIMU NA MUSTKABALI WA UKOO;
4.
UKIMWI NDANI YA UKOO NA ATHARI ZAKE; NA
5.
DINI KATIKA UKOO.
Harakati za maandalizi ya Mkutano
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, zilianza toka mwezi Februari 05, 2005.
Harakati hizi zilifanyika Kijijini Kidamali kwa upande mmoja na kwa upande
mwingine jijini Dar es Salaam.
Kamati zote mbili zilizoundwa zilijipa
majukumu mbalimbali, likiwemo lile la kuwaalika na kuwashirikisha ndugu na
wanaukoo katika suala zima la maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Ukoo katika vikao,
na pia utoaji wa michango.
Katika harakati za maandalizi ya
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa UKoo wa Kivenule, kamati zote mbili zilizipata vikwazo
mbalimbali likiwemo tatizo la mwitikio duni katika kulipokea wazo hili. Kwa
ujumla, katika kuliuza suala/wazo hili la kuandaa na kuwa na Mkutano Mkuu wa
Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, kamati ilibidi zitumiea nguvu na mbinu za ziada ili
kuweza kufanikiwa.
Mahudhurio duni yalitoa changamoto
kwa Kamati za Maandalizi ya Mkutano Mkuu, kuongeza juhudi/jitihada na kutafuta
njia mbadala za kufikia lengo. Kwa upande wa Kijijini Kidamali, ushawishi
ulizaa matunda, kwa sababu ongezeko la wanaukoo na ndugu kuliunga mkono wazo la
kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo lilivuna washiriki wengi.
Kwa upande wa Dar es Salaam, suala
la mahudhurio duni, liliendelea kuwa ni kikwazo kwa kipindi chote cha
maandilizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Wapo waliodiliki
kusema Mkutano Mkuu wa Ukoo ufanyike kwanza Dar es Salaam na ndipo ufanyike na
kijijini Kidamali. Licha ya kupewa sababu na maelezo ya kina ya kuufanya
Mkutano huo ufanyike Kijijini Kidamali, hawakutilia maanani.
Katika suala la utoaji wa michango,
watu wamekuwa na ari na mwitikio wa hali ya juu hapa Kijijini Kidamali, na kwa
kiwango kikubwa ndio waliosaidia kufanikisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa
Kwanza wa Ukoo wa Kivenule.
Licha ya wanaukoo waishio Dar es
Salaam kuchangia, lakini mchango wao umesaidia kidogo sana, kwa sababu kiwango
kikubwa cha fedha pamoja na mahitaji mengine, yamepatikana hapa.
Sehemu nyingine, nje ya Kidamali, utoaji
wa michango hapo mwanzo ulikuwa wa wastani, lakini kadiri siku zilivyokuwa
zinakaribia, ari na kasi mpya ilijitokeza na kuwa kubwa hasa toka sehemu za
Magubike pamoja na Nyamihuu.
Majirani na watu wengine wasio
wanaukoo wamejitolea kutoa michango katika kuusaidia Ukoo wa Kivenule,
kufanikisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Majirani
na marafiki waliojitokeza kwa hali na mali katika kutoa fedha, vyombo na vifaa
mbalimbali.
HOTUBA YA
MGENI RASMI
Mgeni Rasmi aliishukuru Kamati ya
Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule kwa kumwalika kuwa
Mgeni Rasmi katika Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Kivenule. Alisisitiza kwa kusema
kuwa, kuna watu wengi muhimu ambao tumewaacha na kuamua kwenda kumwalika yeye.
Mgeni Rasmi alisema amefarijika sana
kutokana na kuwashirikisha jamaa/wanaukoo wote. Pia alisisitiza kuwa anahisi
yupo karibu na ukoo wa Kivenule kutokana na baadhi ya jamaa zake wa karibu
kuwepo kwenye mkutano huo. Pia hata rafiki zake nao waliohudhuria kwenye
Mkutano Mkuu wa Ukoo; hii ilimpa faraja sana.
Kutokana na ukoo kuwa na mtandao mkubwa
sana, ni muhimu kuwa na shughuli za pamoja kama hizi. Wakati anakuongea na
Mwenyekiti, amefurahi sana kusikia mikakati ya wanaukoo hasa lile la kufanya
senza na pia mkakati wa kufahamiana zaidi.
Mgeni Rasmi aliwashukuru wale wote
waliotoa wazo la kuwepo kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule na jinsi
walivyoshirikisha wanaukoo katika shughuli hii.
Katika shughuli yoyote ile, vikwazo
vipo, suala la msingi ni kuelimishana na kuwashawishi wale ambao hawakuhudhuria
ili kuwepo na umoja na mshikamano. Suala mshikamano na umoja ni muhimu sana
katika jamii yetu kwani itasaidia kuleta maendeleo na wanandugu wawtakuwa
karibu.
Pia, kuwa pamoja kunasaidia
kushirikiana katika magonjwa, furaha na matatizo mbalimbali ya kila siku. Mgeni
Rasmi, alitoa mfano wa Abraham na Lutha katika ugomvi wao wa mifugo, lakini
mwisho walijaliana licha ya kutengana. Ndugu ni muhimu sana na hawawezi
kutengana.
Mkutano huu unatoa changamoto ya
kuwa na mshikamano na kuwa na nguvu zaidi katika kuleta maendeleo.
Mgeni Rasmi aliushukuru Ukoo wa
Kivenule kwa kuelimishana kuhusu umuhimu wa kuwa na ushirikiano wakati wote
nasi tu wakati wa matatizo. Huu ni mfano mzuri kwa jamii nyingine.
Mgeni Rasmi aliutakia kila la kheri
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, na kuahidi kuwa yuko nyuma ya
wanaukoo sambamba wakati wote wa Mkutano huo.
Baada ya hotuba ya Mgeni Rasmi,
MKUTANO MKUU WA KWANZA WA UKOO WA KIVENULE, ulifungulia Rasmi mnamo saa 4:45,
tarehe 17 Desemba 2005.
UTAMBULISHO
WA WANAUKOO
Kwa mujibu wa ratiba ya siku ya kwanza
ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, utambulisho wa Wanaukoo
ulifanyika kwa kila ndugu/mwanaukoo kujitambulisha. Mwenyekiti aliwaelewesha
washiriki wote jinsi ambavyo wanapaswa kujitambulisha.
Kila anajitambulisha
alipaswa/alitakiwa kutaja jina lake la mwanzo, jina la baba yake, babu na jina
la mwisho la ukoo. Lakini, pia wanaukoo walijitambulisha kwa kutaja majina ya Mama
zao, Waume au Wake zao.
Kila mshiriki katika Mkutano Mkuu
wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, alipewa kitambulisho cha kumtambulisha kwa ndugu
wengine. Kitambulisho hicho kilionyesha jina lake kamili, mahali anapoishi,
namba ya simu pamoja na sanduku la posta. Hii ilifanyika makusudi ili kupunguza
kuulizana majina kutokana na washiriki kuwa wengi.
Yafuatayo hapa chini ni majina ya
wanaukoo waliojitambulisha siku kwenye Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa
Kivenule. (refer
registration forms).
UWASILISHAJI
WA MADA
Katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa
Ukoo wa Kivenule, jumla ya Mada Tano ziliwasilishwa. Mada ya kwanza
kuwasilishwa katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ilikuwa ni
“CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO”. Wawasilishaji wa Mada hii walikuwa ni ndugu:
1.
Christian J. Kivenule
2.
Augustino Kivenule
VIAMBATANISHO
(ANNEXTURE)
Wawezeshaji
wa Mada Mbalimbali
1.
Christian J. Kivenule
2.
Augustino Kivenule
3.
Stephan Mhapa
4.
Maria Milimo
5.
Adam A. Kivenule
6.
Jovin D. Kivenule
7.
George S. Kivenule
8.
John S. Kivenule
9.
Ignas P. Kivenule
Wawezeshaji
Wasaidizi
1.
Lesandu Mhapa
2.
Adam A. Kivenule
3.
Faustin S. Kivenule
4.
Christian J. Kivenule
Msimamizi wa
Vyombo vya Matangazo
1.
Lesandu Mhapa
2.
KAMATI
IYORATIBU SHUGHULI KATIKA MKUTANO MKUU WA KWANZA WA UKOO WA KIVENULE
No comments:
Post a Comment