Maana ya Mahusiano ni hali ya
ukaribu, ujirani, urafiki, umoja au ushirikiano unaojengeka baina ya Ndugu,
Jamaa au Marafiki. Mahusiano ni hali ya kuwa pamoja Kifikra, Kimwili,
Kimawasiliano, Kiimani, Kiitikadi, Kimaendeleo, Kikazi, Kijamii na Kimichezo.
Mahusiano hujengwa kwa misingi/namna
mbalimbali. Baadhi ya njia au vitu vinavyosababisha kukawepo na mahusiano ni
pamoja na:
1.
Ujirani: Ujirani mara nyingi
katika jamii zetu huchangia sana katika kujenga Mahusiano. Mahusiano yenyewe
huonekana katika sura mbili tofauti. Yaani Mahusiano Mazuri kwa maana ya Sura
Nzuri au Mahusiano Mabaya kwa maana ya Sura ya Ubaya.
2.
Undugu: Hii ni aina ya
nyingine ya Mahusiano ambapo ndugu wa Damu Moja au wanachangia damu, hujenga
Mahusiano ya Moja kwa Moja (Automatic Relationship). Mara nyingi Mahusiano ya
aina hii huwa na Sura ya Uzuri zaidi (Mahusiano Mazuri). Japo kuna kipindi
Fulani hata Sura ya Ubaya (Mahusiano Mabaya) hujitokeza.
3.
Imani: Pia watu huweza
kujenga Mahusiano kupitia Imani zao, mfano watu wanaoabudu katika dhehebu moja
huweza kujenga mahusiano ya aina yao tofauti na dhehebu jingine. Mara nyingi
Mahusiano ya Kiimani huwa na mwelekeo wa Mahusiano memo. Mahusiano mabaya mara
nyingine hutokea na hata kusababisha vita vya kiimani (dini).
4.
Itikadi: Mahusiano ya Kiitikadi
nayo hujengeka kwa kufuata Mlengo wa Vyama Vyao. Na zaidi Mahusiano ya
Kiitikadi huegemea zaidi kwenye siasa na hupungua au kutoweka kabisa baada ya
mmoja wao kubadili Itikadi yake yaani kuhama toka chama cha kimoja cha siasa na
kwenye chama kingine cha siasa. Mahusiano ya Kiitikadi hujengwa kwa misingi ya
Chuki, Fitina na Vitisho baina wa watu wa Itikadi moja na wale wa Itikadi
nyingine.
5.
Maendeleo: Watu wenye hali fulani
ya kimaendeleo huweza kujenga aina fulani ya mahusiano yenye nia ya kuinuia
hali zao za kimaisha. Na mara nyingi wanaojumuika hapa ni wale ambao tayari
wameonesha nia na mwelekeo. Lakini pia hata wale waliopiga hatua kimaendeleo
huweza kuja mahusiano yao yakiwa nia ya kuimarisha hali walizonazo. Msingi
mkubwa wa mahusiano ya aina hii huwa ni kupeana mbinu na mikakati ya kuleta au
kujiimarisha zaidi katika maendeleo ambayo wanayatarajia au ambayo wamekwisha
yapata.
Pia hata kwa upande wa
wale wenye hali duni ya kimaendeleo nao hujenga aina Fulani ya mahusiano
kulingana na hali na uwezo wao. Kasoro ambayo hujitokeza hapa huwa ni mahusiano
duni baina wenye uwezo (matajiri) na wale na wasio na uwezo (maskini). Katika
kujiimarisha zaidi kimaendeleo, maskini huwa mtumishi (kibarua) na tajiri huwa
mtumikiwa (mtwana).
6.
Elimu: Watu wenye elimu nao
mara nyining hujenga mahusiano yao. Mara nyingi katika mahusiano yao huwatenga
wale wenye elimu kidogo au wasio na elimu kabisa. Hii hutokea zaidi kwa wale
waliobahatika kupata Elimu ya Juu mfano Chuo Kikuu. Mazungumzo na mipango yao
huwatenga zaidi wale wenye elimu kidogo. Kuwatenga hujitokeza katika matumizi
ya lugha za kigeni, kutowashirikisha katika mawazo mbalimbali ambayo wanadhani
yanaweza kuwainua watu wa hali zote (wasomi na wasio wasomi).
AINA ZA
MAHUSIANO
Kuna aina mbalimbali za mahusiano,
lakini tunaweza kugawanya mahusiano haya katika sehemu kuu mbili.
1.
Mahusiano Mazuri; na
2.
Mahusiano Mabaya.
Aina mbalimbali za mahusiano ambayo
yapo katika jamii zetu ni pamoja na mahusiano ya:
§
Kikazi;
§
Kijamii;
§
Kisiasa; na
§
Kiuchumi.
MAHUSIANO
MAZURI
Mahusiano Mazuri ni hali ya kuwa
pamoja kwa kushirikiana katika nyanja mbalimbali za maisha. Mahusiano Mazuri
huwa katika shida au raha. Raha hujumuisha hali zozote zenye kuashiria
mafanikio na maendeleo katika maisha ya binadamu. Hii ni pamoja na kufaulu
mitihani mbalimbali ya darasani na ya maisha; kujenga nyumba, kununua gari,
kapata kazi nzuri, kufanikiwa katika kilimo, Jubilei, kupandishwa cheo pamoja
na kupata nishani.
Shida huwa ni hali ya kuwa na
mashaka, kutokuwa na uhakika wa maisha, kutokuwa na kipato, kutofanikiwa katika
elimu, ugonjwa, misongamano (Depression), misusuko (stress), kutokuwa na ajira,
kutofadhiliwa kwa hali yoyote (Promotion au Scholarship) na kadhalika.
MAHUSIANO
MABAYA
Mahusiano Mabaya ni hali ya kutokuwa
na ushirikiano, huruma au wema katika nyanja mbalimbali za maisha. Mahusiano
Mabaya nayo hali kadhalika huwa katika ubaya au uzuri au shida na raha. Tofauti
na katika Mahusiano Mazuri, Mahusiano Mabaya hubaki kuwa katika shida na raha.
Kwa ujumla ushirikiano na mawasiliano hukosekana kabisa. Huwa hakuna huruma,
maelewano, kuvumiliana na kuwasiliana.
Kikubwa ambacho hujengeka ni chuki,
majivuno, wivu, ugomvi na kutakiana shari. Hamna hata mmojawapo ambaye huombewa
kheri. Kwa yule aliyenacho, huombea au hutamaini yeye aendelee kuwa nacho peke
yake na kutomwombea kheri ya kupata yule ambaye hana kitu.
Na kwa yule ambaye hana, humwombea
shari, bahati mbaya kupoteza au kwa namna yoyote ambayo haina kheri kwa yule
ambaye anacho. Baadhi huomba mfano kama ni gari lipate ajari, nyumba iungue na
kama anasoma anafeli. Katika aina hii ya mahusiano hakuna nafasi ya kutakiana
mema au maendeleo.
MAHUSIANO
BAINA YA NDUGU NDANI YA UKOO
Ukoo wa Kivenule ni mkubwa sana na
kwa haraka unakadiriwa kuwa na ndugu karibia elfu mbili (2000). Ni ukoo ambao
unaweza kufanya mambo makubwa nay a kimaendeleo kama utaungana na kuwa kitu
kimoja.
Tatizo kubwa ambalo linaonekana kwa
wanaukoo ni kuwa na mwamko mdogo. Kwa mfano wanaukoo wanaohudhuria Mkutano Mkuu
wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ni theluthi au robo tu ya wanaukoo wote. Tumaini
la Kamati za Maandalizi ya MKutano Mkuu ni kuhudhuriwa na Ndugu pamoja na
Wanaukoo wa Kivenule kwa wingi zaidi.
Kwa upande wa Dar es Salaam, mwamko
wao ni mdogo sana. Tumaini na tegemeo la awali ilikuwa Dar es Salaam ingekuwa
ni mfano, lakini imeshindika na hii ndiyo hali halisi. Tunasikitika na Kamati
ya maandalizi ya Dar es Salaam inaomba samahani.
Kwa wanaukoo toka Irore, nao
wamesema tatizo kubwa kwao ni suala na nauli kuwa ni kubwa. Lakini cha msingi
kufanyika ni kuzidi kuwahamasisha na kuwapa moyo wa kutambua umuhimu wa Mkutano
Mkuu wa Ukoo pamoja na mikutano mingine.
Katika suala zima la mahusiano,
ukaribu wa wanandugu na wanaukoo linaangaliwa kwa karibu zaidi. Mahusiano
yanagusa mambo muhimu katika maisha ya kila siku mfano Elimu, Ugonjwa, Vifo
pamoja na Starehe (Harusi, Send-Off, Kipaimara na Komunio). Elimu ni muhimu
sana kwani inaongeza upeo na ufahamu wa kuweza kukabiliana na matatizo ya
maisha ya kila siku.
Suala jingine ni ushirikiano katika
nyanja mbalimbali mfano Biashara, kazi na kilimo. Hapa tunamaanisha kuunda
kikundi ambacho kitakuwa na mfuko utakaokuwa unachangiwa na watu mbalimbali
kulingana na shughuli na kipato.
Katika kujenga mahusiano imara,
kutembeleana ni muhimu sana. Faida ya kutembeleana ni kujuliana hali,
kusaidiana, kushauriana na kupeana mbinu na mwongozo wa kufauli katika maisha.
Pia katika kutembeleana huwapa fursa wanaukoo/ndugu kuangalia mazingira mapya
anayotembelea kama yanaweza kumfaa kuishi akilinganisha na mazingira aliyotoka.
Pia katika kushirikiana kuna haja
ya kuwashawishi na kuwabembeleza wale wasio na uwezo ikiwa ni pamoja na kuwapa
moyo, kuwashauri waondoe aibu na wajenge tabia ya kushirikiana. Katika
kushirikiana inakuwa ni rahisi kuweza kutatua matatizo mbalimbali baina ya
wenye nacho na wasionacho.
Kwa mfano katika shughuli nzima ya
kuandaa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, inakuwa kitu kizuri na
mfano kwa wengine kama tutaonyesha kwa vitendo haya tunayozungumza hapa.
No comments:
Post a Comment