Utangulizi
Harakati endelevu za kuleta mabadiliko
na maendeleo zinavyokua kwa kasi kubwa na hivyo kuchochea mabadiliko ya haraka
ya hali bora za maisha ulimwenguni. Harakati hizo zinazotegemea sana kuwepo wa sayansi
na kiteknolojia na uchumi endelevu; zinatoa fursa na hamasa kwa jamii huria
nazo kubuni na kutafuta mbinu mbadala za kuweza kujiinua ili kuweza kukabiliana
na hali hiyo. Mabadiliko hayo ninayoyazungumzia ni pamoja na kukua kwa
teknolojia ya habari na mawasiliano (computer, Internet na cellphones), soko
huria, utandawazi na ubinafsishaji.
Jamii huria kwa upande wake
zinapata hamasa na changamoto ya kuweza kutafuta mustakali wake kutokana na
hali halisi ya maendeleo inavyoendelea kukua na athari kuonekana kwa upande
mmoja na pia mafanikio kuonekana kwa upande mwingine.
Wimbi la umaskini uliokithiri,
janga la UKIMWI, ujinga na rushwa vimekuwa ni vikwazo vikubwa vya maendeleo na
ambavyo vinazidi kudidimiza harakati mbalimbali za kuweza kujiinua na
kujikwamua katika hali hiyo. Harakati hizi za kutafuta maendeleo zimegawanyika
katika makundi mbalimbali ya kijamii hususani makundi ya wasomi,
wafanyabiashara, wanawake na wananchi wa kawaida.
Kutokana na harakati hizo,
wanajamii wanaounda Ukoo wa Kivenule nao hawako nyuma katika kuhakikisha kuwa
jamii yao
inaondokana na umaskini, ujinga pamoja na UKIMWI; na hivyo kupata fursa ya
kuishi katika dunia mbadala iliyojisheheneza katika sayansi na teknolojia.
Kwa kutambua hilo, wanajamii
wanaounda Ukoo wa Kivenule, kwa pamoja toka mwezi Februari 06, 2005,
walianzisha harakati za kuinasua jamii yao kutoka kwenye lindi la umaskini,
ujinga na maradhi kwa kuunda Kamati Tatu kuratibu Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa
Ukoo huo; ambao umepangwa kufanyika katika Kijiji cha Kidamali, Wilaya ya
Iringa Vijijini mkoani Iringa, hapo tarehe 17 hadi 18 Desemba 2005. Kwa
kushirikisha Kamati Tatu za Maandalizi ya Mkutano Mkuu, yaani Kamati iliyopo
mkoani Dar es Salaam,
Kamati ya Kijijini Kidamali na ile ya Ilole – Iringa, zote zimepewa majukumu
mazito ya kusaidia kufanikisha mkutano huo.
Mkutano Mkuu wa Ukoo unategemea
kuwaalika ndugu na wageni wapatao mia mbili (200) toka Kijijini Kidamali, Ilole,
Nduli, Kihesa, Ilula, Magubike, Kinyamlewa, Nzihi, Iringa Mjini, Kalenga,
Ipogolo, Museke, Kitwilu, Igowolo, Kiponzelo, Mafinga, Mufindi, Maduma, Wasa,
Ifunda, Tosamaganga, Tanangozi, Sadani, Isimani, Kilombero, Morogoro, Dodoma na
Dar es Salaam; na sehemu nyingine nyingi ambako wanajamii wanaounda ukoo huo
wanaishi ili waweze kupata fursa ya kushiriki kikamilifu.
Kamati hizo zikiwa chini ya
viongozi wahamasishaji ambao ni:
1.
Adam Kivenule Katibu
– DAR 0741 270364/0748 270364
2. Christian
Kivenule Mwenyekiti – DAR 0744
031 675
3. Athuman Mtono Makamu Mwenyekiti – DAR 0748 708 708
4. Edgar Kivenule Mshauri wa Kamati – DAR 0748488523 / 0741215724
5. Innocent Kivenule Mweka Hazina – DAR 0748 663 315
6. Ndugu Ignas
Kivenule (Mshauri Kamati ya Ilole); 0744 060 183
7. Ndugu Faustin
Kivenule Mwenyekiti (Kamati ya Kidamali)
8. Augen Kivenule Makamu Mwenyekiti (Kamati ya
Kidamali) 0748859936
9. Jovin Kivenule Katibu (Kamati ya Kidamali)
10. Carolina Kivenule Katibu Msaidizi (Kamati
ya Kidamali)
11. Justin Kivenule Mweka Hazina (Kamati ya
Kidamali) 0748 855 739
12. Donati Mhapa Mshauri (Kamati ya Kidamali) 0748 481 954
zimepewa jukumu la kuhakikisha
kuwa Mkutano Mkuu unafanyika na kufanikiwa.
Ukoo wa Kivenule ukiwa umejiwekea
malengo mahususi katika kuandaa mkutano huo, pia umeazimia pamoja na mambo
mengine, kufundisha jamii inayounda ukoo huo kwa kutoa Mada Tano zenye msukumo
wa maendeleo. Mada zilizopendekezwa kufundishwa katika siku mbili za mkutano ni
pamoja na UKIMWI, ELIMU, MAHUSIANO BAINA YA WANANDUGU, KUKUA NA KUENEA KWA UKOO
NA DINI.
Wawezeshaji mbalimbali wenye
ujuzi katika mada hizo tayari kamati zimechukua jukumu la kuwatafuta ikiwamo
kupata wataalam toka Tume ya UKIMWI ya Taifa (TACAIDS).
Mojawapo ya hamasa kubwa ya
kuandaa mkutano huu ni pamoja na suala nzima la mahusiano ndani ya wanandugu,
wanaukoo na jamii kwa ujumla. Suala la ELIMU, ATHARI ZA UKIMWI katika jamii ya
ukoo wa Kivenule na taifa nzima kwa ujumla, haja ya kufahamiana baina ya
wanajamii wanaounda ukoo, pamoja na kuujua ukoo kwa ujumla.
Pamoja na mambo mengine, kamati
ilifikiria pia uwezekano wa kufanya senza ili kujua idadi ya ndugu wanaounda
ukoo husika toka kona mbalimbali hapa Tanzania; kujua nini wanakifanya na
kujua idadi sahihi ya wanandugu ambao wanahitaji msaada wa namna moja au
nyingine.
Katika suala nzima la Kufahamu
Chimbuko la Ukoo, Mahusiano baina ya wanandugu ndani ya ukoo, Elimu, Maadili na
Dini na gonjwa hatari la UKIMWI, Kamati ilionelea kuwa ni mojawapo ya mambo
msingi sana kuyaangalia
katika shughuli nzima ya maandalizi na wakati wa Mkutano Mkuu.
Changamoto zitapatikana baada
ya kuyagusia mambo haya ya msingi na hivyo kuwawezesha washiriki wa mkutano
mkuu kujenga ajenda mpya.
Mahusiano duni baina ya wana
ndugu, kukosa kwa ushirikiano katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo, hali duni
ya kiuchumi na kijamii, matatizo ya kifamilia na kiukoo ni kati ya masuala
msingi yaliyofikiriwa sana
kabla ya kuanza kufanya maandalizi ya Mkutano Mkuu.
Mwelekeo na nafasi ya ukoo wa
Kivenule katika suala nzima la Elimu hasa katika dunia hii ya Utandawazi
(Globalization). Maendeleo ya sayansi na teknolojia ambapo yameifanya dunia
kuwa kama kijiji kisicho na mipaka na kila mtu anaruhusiwa kuingia na kutoka;
kuongezeka kwa viwanda vinavyotumia teknolojia ya hali ya juu; kuongezeka kwa
teknolojia ya habari na mawasiliano (Internet); kupanuka na kujengeka kwa miji,
pamoja na soko huria.
Mambo yote haya ndiyo
yanayoweza kuonyesha mustakabali na nafasi ya ukoo wa Kivenule kwa maisha ya
baadaye. Ilionekana kuwa ukoo wetu upo nyuma sana katika suala nzima la elimu, hii
linajidhihirisha kutokana na kuwa na ndugu wachache sana ambao wameweza kupata elimu kwa kiwango
kinachostahili.
Hii ni hatari kwa sababu
tunajenga ukoo tegemezi ambayo baadaye utakosa mwelekeo. Mabadiliko ya Sayansi
na Teknolojia yanayojitokeza kila kukicha yanaibadili dunia na hivyo
kutulazimisha nasi katika ukoo wa Kivenule kubadilika. Matumizi ya teknolojia
ya habari na mawasiliano katika simu za mikononi, Internet, computer, redio na
satelaiti ni changamoto kubwa katika Ukoo wa Kivenule.
Maambukizo ya ugonjwa wa UKIMWI
ambayo kwa kiasi kikubwa yameathiri familia nyingi zikiwemo familia zetu sisi
wana ukoo, yanapaswa kutopuuzwa bali kuwekewa mikakati madhubuti. Ufahamu
kuhusiana na gonjwa lenyewe livyoenea na madhara yake katika jamii, njia
mbadala za kujilinda na maambukizi ya ugonjwa wenyewe pamoja na kuitikia
mialiko mbalimbali ya wanajamii wanaopambana na janga hili ni mambo ya msingi sana ambayo yatajadiliwa
kwa kina kwenye mkutano huo.
Ilipendekezwa kuwa, wakati wa
mkutano huo kutakuwa na nafasi kutoa uzoefu katika mambo mbalimbali ya kitaalum
na maendeleo. Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Ukoo yalianza mapema ili kumpa
fursa kila mwanajamii/mwanaukoo kutafakari na kujadili kwa kina, kujiandaa
pamoja na kuwasilisha mchango wake wa mawazo kwa kamati husika za kuratibu
maandalizi.
Mkutano
Mkuu wa Ukoo umeazimia kutoa kitu muhimu ambacho ndicho kitakuwa mwongozo na
dira ya shughuli mbalimbali zitakazokuwa zinafanyika katika ukoo.
Licha
ya kuwa na malengo na makusudio mbalimbali, pia tunategemea mwisho wa mkutano
kutakuwa na mambo kadhaa ambayo yatakuwa ni makubaliano kutoka pande mbalimbali
za ukoo wa Kivenule. Yote hayo kwa pamoja yatakuwa ni maazimio ya Mkutano Mkuu
wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule.
Kati
ya Maazimio ambayo tunayategemea katika mkutano huo ni:
- Kufanya Senza ya Ukoo wa Kivenule ili kupata idadi kamili ya ndugu.
- Kuanzisha Mfuko wa Ukoo
- Kuchagua Viongozi wa watakaounda Kamati ya Ukoo ya Kuratibu mambo mbalimbali ya ukoo. (Mwenyekiti, Katibu, Mweka Hazina pamoja na viongozi wengine ambayo wana umuhimu na kupewa majukumu kuwepo).
- Kuzitaja kazi mbalimbali ambazo Uongozi utakaoundwa utakuwa unazifanya mfano kufanya mashauriano na usuluhishi wa matatizo mbalimbali ya ukoo yaliyojitokeza.
- Kukusanya taarifa mbalimbali za ukoo; na
- Kuangalia na Kutathmini usalama wa mali mbalimbali zinazomilikiwa na ukoo nk.
Katika kuhakikisha kuwa Mkutano Mkuu wa Kwanza
wa Ukoo unafanyika na kufanikiwa, kamati mbalimbali ndogondogo zinategemea
kuundwa ili kusaidia uratibu maandalizi ya mkutano huoo kabla ya kuanza na
wakati wa mkutano huo. Mojawapo wa kamati hizo ni: Kamati ya Mapokezi; Kamati
ya Malazi; Kamati ya Chakula; Kamati ya Vinywaji; Kamati ya Burudani; Kamati ya
Usafiri; Kamati ya Ulinzi na Usalama; Huduma ya Kwanza
na Kamati ya Uratibu wa Shughuli za Mkutano.
Kwa kushirikiana na Kamati Kubwa (ile iliyoundwa Dar es Salaam, ya Kidamale na ile ya Ilole) katika kuratibu maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo, kamati ndogondogo zitajumuika kutekeleza majukumu mbalimbali kabla na siku ya Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Kivenule. Kwa hiyo Kamati zote kwa pamoja zitakuwa na wajibu wa kufanya yafuatayo ili kuhakikisha shughuli nzima inaenda kama ilivyopangwa. Mojawapo ya majukumu hayo ni pamoja na:-
·
Kuoganaizi (kuandaa) huduma ya usafiri toka Iringa Mjini
hadi Kidamali kwa wageni mbalimbali ambao watakuwa wanakuja kwenye Mkutano
Mkuu wa Kwanza wa Ukoo; huo pamoja na kuandaa
orodha ya wageni na tarehe zao kufika Kidamale. Hii itakusaidia sana kwenye zoezi zima la
kuoganaizi huduma ya usafiri kwa wageni mbalimbali ambao wengi wao watakuwa
hawapajui vizuri kidamali.
·
Kufanya matayarisho ya sehemu ya Malazi kwa wageni mbalimbali
ambao watawasili kutoka sehemu mbalimbali. Hii inajumuisha sehemu salama na
nadhifu za kulala wageni husika ambapo tunategemea tutapata vyumba, magodoro
pamoja na kuwepo kwa vyoo na mabafu ya kuogea.
·
Kuhakikisha kuwa shughuli zote zinazohusiana na maandalizi ya
vyakula zimepangiliwa vizuri. Kula chakula katika muda uliopangwa, huduma ya
chai/kahawa na maji wakati mkutano unaendelea viende kama
ratiba itakavyokuwa imepangwa. Hii inamaanisha kuwa, RATIBA pamoja na matangazo
mbalimbali yatabandikwa sehemu mbali
kwenye eneo la mkutano (ukumbi), jikoni, maeneo mbalimbali ya Kijiji cha
Kidamali. Hii itasaidia kuwafanya washiriki wa mkutano kujali na kuona umuhimu
wa mkutano.
·
Kutaundwa kamati ndogo ndogo zenye wajibu wa kutekeleza
majukumu zitakazopangiwa na kamati kubwa. Mfano wa kamati hizo ndogo ni pamoja
na Kamati ya Ulinzi na Usalama, Kamati ya Usafi, Kamati ya Chakula, Kamati ya
Vinywaji, Kamati ya Malazi, Kamati ya Mapambo, Kamati ya Picha za Video na
Picha za Kawaida na Kamati ya Burudani. Kamati zote hizo ndogo ni muhimu sana kwani ndizo
zitakazosaidia shughuli nzima kwenda kama
ilivyokusudiwa.
·
Lazima uwepo usimamizi madhubuti ili kuwezesha shughuli
mbalimbali kuwa ndani ya ratiba (muda uliopangwa). Kwa hiyo kuna haja ya kuwepo
kwa saa za ukutani ambazo zitakuwa kama
mwongozo. Hii tunamaanisha kuwa Wawezashaji lazima wawe wachangamfu sana wakati wa kuendesha
mada mbalimbali pamoja na majadiliano.
·
Kazi nyingine kubwa ni kuhamasisha wanakoo mbalimbali
wanaishi ndani ya Kidamali na kwingineko kuwa na moyo wa kujitolea katika
shughuli mbalimbali zitakazojitokeza kwenye mkutano. Hii ni pamoja na
kuzisaidia kamati ambazo zitaonyesha hali ya kuelemewa au kuhitaji msaada wa
kiutendaji.
Baadhi
ya wawezeshaji waliopendekezwa toka katika ukoo husika ni pamoja na:
1.
Agatha Mhapa
2. Alphonce Kivenule
3. Lizeta Kivenule
4. Ignas Kivenule
5. Siha Kivenule
6. Christian Kivenule
7. Adam Kivenule
8. Justin Kivenule
9. Donath Mhapa
10. John Kivenule
11. Victoria Kivenule
12. Edger Kivenule
13. Piera Kivenule
14. Florian Kivenule
15. Innocent Kivenule
16. Stephen Mhapa
17. Severin Nyangalima
Mada zitakazowasilishwa kwenye mkutano mkuu ni pamoja na
1. CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO
- Ukoo ni Nini na Unapatikanaje?
- Dhana ya Kuenea na Kukua kwa Ukoo.
- Mgawanyiko wa Ukoo (Chora Mchoro Kuonyesha Ukoo unavyoundwa).
- Kupotea kwa Ukoo.
2. MAHUSIANO BAINA YA NDUGU NDANI YA UKOO
- Ukaribu wa Wana Ndugu.
- Ushirikiano Katika Nyanja Mbalimbali.
- Kutembeleana kama Sehemu ya Kudumisha Mahusiano.
- Kuondoa Tofauti na Kusaidiana.
3. ELIMU NA MUSTAKABALI WA UKOO
- Nafasi ya Ukoo wa Kivenule katika Elimu.
- Umuhimu wa Elimu.
- Dunia ya Utandawazi.
- Nini Kifanyike Kuinua Elimu Katika Ukoo Wetu.
4. UKIMWI
NDANI YA UKOO NA ATHARI ZAKE
- UKIMWI ni nini?
- Namna gani UKIMWI unavyoenea/kuambukizwa?
- Njia Mbadala za Kujilinda na Maambukizi?
- Jukumu la Ukoo/Familia Kukabiliana na Janga la UKIMWI.
5. DINI KATIKA
UKOO
- Maana ya Dini
- Umuhimu wa Kuwa na Imani
- Maadili na Dini
- Ukoo Uliojengeka katika Misingi ya Dini
RATIBA YA MKUTANO MKUU WA KWANZA WA UKOO WA KIVENULE
Siku ya Kwanza ya Mkutano Mkuu wa Ukoo wa KIVENULE |
||
Muda na tarehe
17 Des. 2005
|
Shughuli/Jukumu
|
Wahusika
|
12:00–12:45
|
Wageni Wote
Kuamka na Kufanya Maandalizi ya Kuingia kwenye Mkutano
|
Wote |
12:45–1:45
|
Kupata
Kifungua Kinywa
|
Wote
|
1:45 – 2:45
|
Kuwasili
Mkutanoni na Kujisajili
|
Wote
|
2:45 – 3:15
|
Ufunguzi wa
Mkutano na Mgeni Rasmi
|
Mgeni Rasmi
|
3:15 – 4:00
|
Utambulisho
baina wa wana Ndugu
|
Wote
|
4:00 – 4:45
|
Pumziko la
Chai / Kahawa/Maji
|
Wote
|
4:45 – 5:30
|
Mada ya Kwanza: CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO |
Mtoa Mada na Mkubwa wa Ukoo |
5:30 – 6:00
|
Majadiliano
katika Makundi
|
Makundi 4
|
6:00 – 6:20
|
Murejesho na
Majumuisho
|
Mwezeshaji
|
6:30 – 8:00
|
CHAKULA CHA
MCHANA
|
Wote
|
8:00 – 8:45
|
Mada ya Pili:
MAHUSIANO BAINA YA NDUGU NDANI YA UKOO WA KIVENULE
|
Mtoa MADA (…………………)
|
8:45 – 9:15
|
Majadiliano
katika Makundi
|
Makundi 4
|
9:15 – 9:45
|
Murejesho na
Majumuisho
|
Mwezeshaji
|
9:45– 10:45
|
Pumziko la Chai/Kahawa/Maji |
Wote
|
10:45-1:30 Usiku
|
Mapumziko
Marefu (Kusalimiana na Kufahamiana zaidi)
|
Ndugu na
Wageni Wote
|
1:30 – 2:30
|
Chakula cha
Usiku na Vinjwaji
|
Ndugu Wote
|
2:30 – 6:30
|
Burudani
(Muziki wa Kisasa na Ngoma za Asili)
|
Wote
|
Siku ya Pili ya Mkutano Mkuu wa Ukoo wa KIVENULE |
||
Muda
18 Des. 2005
|
Shughuli/Jukumu
|
Wahusika
|
12:00– 12:45
|
Kuamuka na
Kufanya Maandalizi ya Mkutano
|
Wote |
12:45 – 1:45
|
Kifungua
Kinywa
|
Wote
|
1:45 – 2:15
|
Kuwasili
Mkutanoni na Kujisajili
|
Ndugu wote |
2:15 – 2:45
|
Mada Ya Tatu:
ELIMU NA MUSTAKABILI WA UKOO WA KIVENULE
|
Mtoa Mada |
2:45 – 3:15
|
Majadiliano
kwenye Makundi
|
Makundi 4
|
3:15 – 3:45
|
Murejesho na
Majumuisho
|
Kiongozi wa
Kundi na Mwezeshaji
|
3:45 – 4:30
|
Pumziko
la Chai/Kahawa/Maji
|
Wote
|
4:30 – 5:00
|
Mada ya Nne: UKIMWI NDANI YA UKOO NA ATHARI ZAKE |
Mtoa Mada |
5:00 – 5:30
|
Majadiliano kwenye Makundi |
Makundi 4 |
5:30 – 6:00
|
Murejesho na Majumuisho |
Kiongozi wa Kundi na Mwezeshaji |
6:00 – 7:15
|
CHAKULA CHA
MCHANA
|
Wote |
7:15 – 7:45
|
Mada ya Tano: DINI KATIKA UKOO |
Mtoa Mada |
7:45 – 8:15
|
Majadiliano kwenye Makundi |
Makundi 4 |
8:15 – 8:45
|
Murejesho na Majumuisho |
|
8:45 – 9:45
|
Majumuisho:1. Yote Yaliyojitokeza
2. Matarajio
3. Tarehe ya Mkutano Mwingine |
Mwezeshaji |
9:45 – 10:15
|
Shukurani
toka kwa Ndugu Mbalimbali
|
|
10:15–11:00
|
KUCHAGUA
VIONGOZI WA KUUNDA KAMATI YA UKOO
|
Ndugu Wote
|
11:00
|
Kufunga
Mkutano
|
Viongozi wa Kamati ya Ukoo
|
No comments:
Post a Comment