Jina Iringa lilitokana na neno la Kihehe Lilinga
ambalo tafsiri yake kwa Kiingereza ni Observation Post. Wahehe walianzisha
lilinga sehemu hii ilipo Iringa ya sasa, ilikuweza kuwaona maadui kwa urahisi
na kuweza kutoa taarifa za kulinda Ikulu iliyokuweko Kalenga. Wajerumani
walijenga Boma juu ya kilima hicho hicho baada ya ushindi uliopatikana baada ya
kupigana na Wahehe kwa mara ya pili. Katika pambano la kwanza Wajerumani chini
ya Von Zelewiski waliuwawa wote akabakizwa mmoja akatoe taarifa kuwa Uheheni kuna
wanaume. Vita hiyo ilipigwa eneo la Lugalo mpaka Lundamatwe Kaburi la Zelewiski
liko pale Lugalo. Kuboma ni jina walilotumia Wahehe kupaita pale ambapo
Wajerumani walijenga Boma lao.
WASIFU WA WAZEE WAANZILISHI WA KIHESA
(1) MZEE JUMBE OMARY
Huyu mzee makazi yake ya mwanzo yalikuwa Kigonzile,
baadae aliamia Kihesa karibu na mlima lilipo
kanisa la Kilutheli la Kihesa. alichaguliwa kuwa JUMBE,
Kazi yake aliamua kesi mbalimbali na kuwahamisha
watu kuja eneo ilipo Kihesa kutoka
milimani, kwa mfano mlima Mafifi.
Kesi zilizo mshinda alizipeleka Kalenga wakati huo
ndiko kulikwepo mahakama ya mwanzo. Mwandishi wa habari hii alimuona Mzee JUMBE
OMARY mara ya mwisho mwishoni mwa miaka ya 1970. Alikuwa na ngeu usoni ambayo
inasemekana aliwahi kupigana na simba.
(2) AZIZA SEMGENI
Bibi huyu ni
mmoja wa waanzilishi wa Kihesa, yeye alikuwa anatibu kwa miti shamba, Eneo lake
ndipo palipo jegwa shule ya msingi Kihesa. Wajukuu wa Bibi Aziza ni Mzee Jonas
Mgeni ( Baba Zacho) Mzee Lwinusu Mgeni (Baba Riziki)
(3) SEMTEMA KUUKINGA
Mama huyu wa kabila la Kikinga aiifariki miaka
michache aliopita ni mmoja wa waanzilishi wa Kihesa na alikuwa anamiliki eneo
ambalo mpaka leo maarufu kwa jina la SEMTEMA
karibu kabisa na Chuo Kikuu cha Tumaini
(4) SALUMU SOSOVELE
Huyu mzee kwa waliobahatika kumuona alikuwa
pandikizi la mtu. mwenye kuongea kwa tabasamu. Baba yake mzazi ndie aliyemiliki
eneo kilipo jegwa Chuo Cha Elimu Kleruu.Na kaburi la baba wa Salum lipo jirani
na Kanisa Katoliki Kihesa.
WAJUE WAZEE WA KIHESA 6
MZEE ERNEST MWANDANZI
Mzee huyu
Mhehe wa Mufindi aliyestaafu uaskari akiwa na cheo cha Inspekta, ni mmoja wa
wanzilishi wa Kihesa, alifanikiwa kuwa moja ya madiwani wa eneo hili. Mzee Ndanzi ndiye baba mzazi wa Gerald Ndanzi
wa Majembe Auction Mart.
MZEE MARTIN MLOWE
Mzee huyu
Mbena wa Kifanya - Njombe ni mmoja wa waanzilishi wa Kihesa. Pamoja na
kujishughulisha na kilimo eneo la Mangao Ismani, aliku.wa na bucha pale Kihesa alibarikiwa kupata watoto wengi
kama Gaspar, Oscar, Gerard, mtoto wa mwisho wa kiume Afred Mlowe alikuwa
mchezaji kiungo wa Kihesa Stars, mchezaji mwenzie Robert Nyato hudai kuwa
anamfananisha na Steven Gerald Alfred ndiye mtunza hazina wa Umoja wa wana
Kihesa. Kwa sasa ni mfanyakazi wa Manispaa ya kinondoni
Leo tutazungumzia wasifu wa wazee wa kihesa ambao
ni wazazi wa ndugu Faustini Mdesa cosmas na tutamzungumzia Mzee wa kijana
mhamasishaji wa siku ya wana kihesa Ali
mduba.
MZEE COSMAS MDESA
Mzee huyu
Mhehe wa Ifunda ni mwana Kihesa ambaye alijishughulisha na kilimo huko
Kihologota Ismani akiwa na mjomba wake mzee Mwang’ingo. Mzee huyu ndiye baba
mzazi wa mwenyekiti wa maandalizi ya siku ya wana kihesa Ndugu Faustine Cosmas
Mdesa
MZEE JIMMY MWAMBAGO
Mzee huyu Mbena wa Njombe ambaye alitinga Kihesa 1962,
akitokea Tanga ambako alikuwa akifanya kazi upimaji na ramani. Mzee Jimmy
alijiunga na kufanya kazi TANCUT na kusaafu mwishoni mwaka 1979. Bingwa huyu
ambaye ni mzazi wa mwenyekiti wa Mkusanyiko wa wana Kihesa wa dar es Salaam
Ndugu Nordrick Mwambago. Kwa sasa mzee Mwambago bado yupo anaishi Kihesa
nyumbani kwake. Mwanae Nodrick Jimmy
Mwambago ndie mwenyekiti wa wana KIHESA
na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya
siku ya wana Kihesa 2/12/2012
Katika hii orodha ya wazee wa Kihesa hawa pia
wanatakiwa kuongezwa:
1. Mzee Mtwivila,
2. Fabian,
3. Bibi Semtema,
4. Mzee Lwaho,
5.
Victo Mwibalama,
6. Mzee Mwambua (Baba Mussa),
7. Mzee Ally Ngimba,
8. Edward Wissa,
9. Mgeni (Baba Jenifa),
10.
Kavilwa (Mourise),
11.
Msigomba,
12.
Balama (Baba Vero),
13.
Balama (mnyakilabu),
14.
Kibassa (Baba John),
15.
King Miking Kibassa (Babu yangu),
16.
Mzee Ng'owo,
17.
Ngogo (Mwanji),
18.
Tenga's wote (kuanzia Ngimonyi hadi wengine),
19.
Kalinga (Baba Moses),
20.
Nyalusi (Baba Mercy wa Timber),
21.
Mgeni (MZALENDO),
22.
Kigahe,
23.
G.G. Shambe,
24.
John Mbegalo,
25.
Gwegime (watoto wake hadi leo machampion),
26.
Sambala (Baba Marcelino),
27.
Mzee Luhanga (Baba yake Mwanyenza),
28.
Mzee Cheka (Baba ya Cheka Club Semtema),
29.
Mzee Gohage (Babu Fredy),
30.
Mzee James (Baba Baldo),
31.
Mwanzo Mgumu (Chao),
32.
Abel Lulandala (Baba Aidan),
33.
Fivawo,
34.
Mzee Kisonga.
WAZEE MAARUFU WALIOIJENGA KIHESA
1. MZEE JUMBE OMARY
2. MZEE LOTTI LUPEMBE
3. MZEE ZABRON KIPANDULE
MWANYATO
4. MZEE PHOLIPO SAWANI
5. MZEE RUBEN NYARUSI
6. MZEE ANDREW MKOCHA
7. MZEE METUSALA SINZIA
MWAMOTTO
8. MZEE NIKOLAI CHAWE
9. MZEE PESAMBILI RAIS
10.
MZEE JUMANNE MWANDAMIZI
11.
MZEE JIMMY MWAMBAGO
12.
MZEE CAPRO MAHANJAM MDEGELA
13.
MZEE JOHN MAUYA
14.
MZEE FEDRICK KIHADE
15.
MZEE SHEM MAINGARA
16.
MZEE VICENT MSEMWA MFARANYAKI
17.
MZEE LUBAFU LWASOMBA
18.
MZEE ELEUTEL KIMILIKE
19.
MZEE RUPI SABA MKUSA
20.
MZEE GARUS KING'UNZA
21.
MZEE GARUS MWANYAKUNGA
22.
MZEE JAMES CHOMI
23.
MZEE WILLIAM MNG'ONG'O
24.
MZEE MATHAYO MNG'ONG'O
25.
MZEE METUSALA MNG'ONG'O
26.
MZEE PETER MSILU
27.
MZEE EDWARD MMASI
28.
MZEE GEORGE SAWALA
29.
MZEE LUCAS MKUSA
30.
MZEE MUSSA MWACHANG'A
31.
MZEE AUGUSTINO MWACHANG'A
32.
MZEE EMMANUEL MWACHANG'A
33.
MZEE MARTIN MLOWE
34.
MZEE JOHN NZALI BALANCE
35.
MZEE MKINGA SAFI MBILINYI
36.
MZEE AMOSI MPOGOLE
37.
MZEE SAID KITENGE
38.
SHEKHE MDOKA MAULID
39.
SHEKHE SAID KALELA
40.
SHEKHE SAID WANGUVU
41.
MAMA DIANA MAGRETH
42.
MZEE MPOGOLE (BABA SAREHE)
43.
MZEE ALEX SANGA
44.
MZEE ISAYA KAGAHE
45.
MZEE SAMSON NYATO
46.
MZEE SAMWEL KINYUNYU
47.
MZEE MALIO MSILU
48.
MZEE HAMISI KINGENG'ENA
49.
MZEE NGAIRO( BABA STIVIN)
50.
MZEE KUDINGWA MAPUNDA
51.
MZEE FRANSIS KITIME
52.
MZEE LAMEKI TUMBUKA
53.
MZEE IBRAHIM MWIBARAMA
54.
MZEE KALYIEMBE ( BABA ANYWELWISE)
55.
MZEE SIXMUND MOLAMOLA
56.
MZEE JOSEPH KASUMRI SANGA
57.
MZEE MKULU EZEKIA
58.
MZEE CHODOTA (BABA ELIABI)
59.
MZEE MTEVELA (BABA FOIDA)
60.
MZEE OBADIA NGOGO
61.
MZEE PETER NGWIVAHA
62.
MZEE EDWARD MAKWETA
63.
MZEE ADAMU KAPUNGU
64.
MZEE ELIEZA MNG'ONG'O
65.
MZEE EDSON MWAMWANI
66.
MZEE JOHN LUSUNDE
67.
MZEE ZABRON KINYAMAGOHA
68.
MZEE EPHRANI KILATU
69.
MZEE SALUM NYENZI
70.
MZEE ADAM SAJIO KADUMA
71.
MZEE JONASI MGENI
72.
MZEE ZAKARIA CHUWA
73.
MZEE MAIGE MACHIBYA
74.
MZEE KUFAKUNOGA MAHAMODU
75.
MZEE PETER LUPEMBE
76.
MZEE LINGWENDU SANGA
77.
MZEE JOHN KANYWENDA
78.
MZEE MARTINE MWAMBILINGE
79.
MZEE AMRAN MDEMU
80.
MZEE HENRY NYANYEMBE
81.
MZEE JOHN LUHANGA
82.
ZABRONI LUVINGA
83.
MZEE ALI MDUBA
84.
MZEE MARKO MFUGALE
85.
MZEE ALFREDY MBATA
86.
MZEE JOHN GILIKI
87.
MZEE JOHN EJO
88.
MZEE GALAHENGA BEATUSI
89.
MZEE MDENDEMI
90.
MZEE MWANYWAEGE
91.
MZEE DANIEL LUGENGE
92.
MZEE KIDUNU
93.
MZEE MNG'ONGO'
94.
MZEE MBILINYI
95.
MZEE MWANANGUNULE
96.
MZEE KANDANDA
97.
MZEE TITIKOO
98.
MZEE SALUM MDEGIPARA
99.
MZEE FUNGO
100. MZEE MGOMBELE
101. MZEE NZELU
102. MZEE KIDULILE
103. MZEE MBIFILE
104. MZEE ELIAS SANGA
105. MZEE NGWALE
106. MZEE MARTIN KIDUKO
107. MZEE KIWELE
108. MZEE MWITA
109. MAMA GIFT
110. MZEE NGALAWA (BABA MWAMBA)
111. MZEE DICKS DISUZA
112. MZEE MAGAVA
113. MZEE FARAHANI
114. MZEE BENARD MBIGILI
115. MZEE POYO
116. MZEE MNYAMWANI
117. MZEE KAPANDE
118. MZEE MWALIWELO
119. MZEE MALILA
120. MZEE CHENGULA
121. MZEE FURAHISHA
122. MZEE WILILO (BABA ROBERT)
123. MZEE MASENYA
124. MZEE BABA HILDA
125. MZEE MASHAKA WILLBAKI
126. MZEE KIKOSI JUMA MASOUD
127. MZEE COSMAS MDESA
128. MZEE MLIMBILA
129. MZEE MBOMBWE
130. MZEE SOSTEN KYANDO
131. MZEE NDITI
132. MZEE BABA MAYASA
133. MZEE WEEK END
134. MZEE LUGENGE
135. MZEE LUGALA
136. MZEE MWANG'INGO
137. MZEE ODO
138. MZEE RUNYASI
139. MZEE SEKAHANGA
140. MZEE MFIKWA
141. MZEE AMBROS MWANGWADA
142. MZEE KIWONAOMELA
143. MAMA SAMAMBA
144. MZEE LUCHABIKO KAPUGI
145. MCHUGAJI CHUSI
146. MZEE MACHILINA
147. MAMA SEMPOGOLE
148. MAMA GEORGE KUMBEMBA MWAKIMBENGONDO MGODAGWIVAHA MUNYIDUNDA
149. MZEE SAMUEL BWANANGONDO M.M
MWAKIMBE
NB: KUNA WAZEE WASIOPUNGUA 200 WALIO IJENGA KIHESA
TUTAENDELEE KUSAIDIANA KUWAKUMBUKA KAMA MAJINA YAO HAYAPO HAPA
IMETAYARISHWA NA ROBERT MWANYATO:
MRATIBU WA TAMASHA LA WANA KIHESA