RIPOTI
YA
MKUTANO
MKUU WA TATU WA KAUKI
(2007)
DIBAJI
Mkutano Mkuu wa Pili wa UMOJA WA UKOO WA
KIVENULE (KAUKI), ni mfululizo wa mikutano ya namna hii, ambayo imekuwa
ikifanyika Kijijini, Kidamali, kutoka Desemba 18, 2005, na kuwajumuisha wanajamii
wanaunda ukoo Kivenule na pia jamii nyingine zilizo karibu na jamii hii.
Mkutano Mkuu wa Pili wa KAUKI, ulikuwa ni muhimu sana kwa sababu ndiyo uliotoa
taswira mpya ya mwelekeo wa umoja huu, kwa kufanikisha kufikia maamuzi mazito
ya kuwa na Katiba.
KAUKI, ni jina la Katiba na pia Umoja wa
Wanaukoo wa Kivenule, ambalo lilipitishwa na pia kubaliwa na jumuiya nzima
iliyoshiriki Mkutano Mkuu wa Pili wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule. Lengo kuu la
KAUKI limebaki pale pale, ikiwa ni kujaribu kwa kila hali kutumia ujuzi na
maarifa, kuinua uwezo wa kielimu, kiuchumi, kijamii na kimaisha, kwa wanajamii
wanaunda umoja huo, kwa kutumia rasimali mbalimbali zinazopatika katika nchi ya
Tanzania na hususani katika maeneo wanayoishi.
KAUKI imeundwa ili kukidhi mahitaji ya
jamii iliyounda umoja huu, kwa kushirikisha mawazo, fikra, ujuzi na maarifa ya
kila mwanaukoo, katika mikutano mikuu na mikutano midogo midogo, ambayo huandaliwa
na wanaukoo wenyewe. Kwa kukutana pamoja, fikra za kujenga, ujuzi, uzoefu na
maarifa, huunganishwa pamoja na kisha kupanga mikakati mbadala ya kuweza
kukabiliana na changamoto zilizojitokeza katika mkutano huo.
Ripoti hii ya pili, imejaribu kuainisha
kwa mapana yake yale yote yaliyojitokeza katika mkutano mkuu wa pili, na
hususani, suala la Katiba ya Umoja wa Ukoo wa Kivenule. Kama zilivyo Katiba za
vikundi mbalimbali hapa nchini, ripoti hii, inabainisha uwazi na uangavu
ulitumika katika kuandaa Katiba ya KAUKI. Ushirikishwaji wa wanajamii wa Umoja
wa Ukoo wa Kivenule katika kuijadili, kuipitisha na hadi kukubaliwa kutumika;
na pia jamii ya Ukoo wa Kivenule imeelezwa kinagaubaga na hasa katika Dibaji ya
Katiba yenyewe.
Ripoti hii, inaeleza wazi, kuwa maamuzi
yaliyofanyika siku ya Jumamosi na Jumapili ya tarehe 24 na 25 Juni 2006, katika
Mkutano Mkuu wa Pili wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule, yalikuwa ni shirikishi
ambapo, jumla ya wanaukoo wapatao 140 walihudhuria mkutano huo.
Mambo mbalimbali yanayohusu jamii ya Ukoo
wa Kivenule yamewekwa bayana katika vifungu vya KAUKI na pia nyadhifa kadhaa za
uongozi katika Ukoo nazo zimebainishwa, ili kumfanya msomaji yeyote wa Katiba,
kuielewa vizuri.
Shukrani ziwaendee ndugu wote waliojitoa
kwa hali na mali hadi kufanikisha kuandaa ripoti ya Mkutano Mkuu wa Pili wa
KAUKI.
I.
UTANGULIZI
Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo wa Kivenule
ni mojawapo ya Harakati za Maendeleo zinazofanywa na Ukoo wa Kivenule ili
kujikwamua na kuondokana na matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii hii. Huu ni
mwendelezo wa Mikutano ya namna hii, ambapo kwa mara kwanza Mkutano Mkuu wa Kwanza
wa Ukoo wa Kivenule, ulifanyika mwaka jana, tarehe 17 – 18 Desemba 2005, katika
Ukumbi wa Sanga, Kijijini Kidamali Iringa.
Katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa
Kivenule, jumla ya ndugu/wanaukoo wapatao 129 toka sehemu mbalimbali mkoani
Iringa na kwingineko hapa Tanzania waliohudhuria. Baadhi ya ndugu/wanaukoo
waliohudhuria mkutano huo walitoka sehemu za Kidamali, Nyamihuu, Ilala-Simba,
Nyamahana, Magubike, Nduli, Iringa Mjini, Morogoro, Mikumi, Dar es Salaam,
Mufindi, Idete na Nzihi.
Umoja wa Ukoo wa Kivenule umezinduliwa
Rasmi mwaka huu, katika Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo wa Kivenule uliofanyika
tarehe 24 – 25 Juni 2006 katika Ukumbi wa Sanga Kijijini Kidamali, Iringa.
Kuzinduliwa kwa Umoja wa Ukoo wa Kivenule, kulienda sambamba na uzinduzi wa Mfuko
wa Ukoo pamoja na Kuipitisha Rasimu ya Katiba ya Umoja wa Ukoo wa Kivenule na
kuwa Katiba Rasmi. Pia, pamoja na mambo mengine, katika Mkutano Mkuu wa Pili wa
Ukoo, kulifanya uchaguzi wa Viongozi wa Kanda, uchaguzi wa Walezi wa Ukoo na
kuwasilishwa kwa Mada ya Historia na Chimbuko la Ukoo wa Kivenule.
Jumla ya ndugu/wanaukoo wapatao 140 toka
sehemu za Kidamali, Nyamihuu, Ilala-Simba, Nyamahana, Magubike, Nduli, Iringa
Mjini, Morogoro, Mikumi, Dar es Salaam, Mufindi, Idete, Ipogolo, Kalenga,
Mgongo, Ilole, Mbeya, Kilimanjaro, Idodi, Mseke, Tosamaganga na Nzihi
walihudhuria mkutano huo. Safari hii, ndugu/wanaukoo waonaishi sehemu za mbali
mfano Dar es Salaam, Kilimanjaro, Mbeya, Morogoro na Ilole, waliohudhuria kwa
wingi. Kwa mfano, kwa upande wa Dar es Salaam pekee, jumla na ndugu/wanaukoo 11
walihudhuria Mkutano Mkuu.
Upande mwingine ambao nao pia ulikuwa na
uwakilishi mkubwa ulikuwa ni Ilole, Nduli, Kigonzile na Mgongo, ambapo kwa
ujumla, ndugu/wanaukoo wapatao 12 walihudhuria mkutano huo, tofauti na
uwakilishi wa mwaka jana, ambapo ndugu mmoja (1) alihudhuria Mkutano Mkuu.
Kwa upande wa ndugu/wanaukoo
waliohudhuria Mkutano Mkuu toka mbali, ndugu/wanaukoo toka Mwanga mkoani
Kilimanjaro, walikuwa ni baadhi ya ndugu waliosafiri safari ndefu kuja kwenye
Mkutano Mkuu wa Pili wa Kivenule. Safari hii jumla ya ndugu/wanaukoo wapatao
wawili (2) walihudhuria Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo wa Kivenule tofauti na
mwaka jana ambapo tulikuwa hatuna uwakilishi wa aina yoyote toka
Mkoani Kilimanjaro.
Kwa wastani uwakilishi wa ndugu/wanaukoo
waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo wa Kivenule ulikuwa ni wa mtawanyiko
zaidi. Hii kwa Umoja wa Ukoo wa Kivenule ni jambo la kufurahisha na kujivunia
kwani baadhi ya malengo ya umoja huu ni kuwakusanya ndugu toka sehemu mbalimbali
hapa Tanzania. Viongozi wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule bado wanaamini kuwa hawajatimiza
lengo lao la kuandaa mikutano ya namna hii kwani wanaamini kuwa bado kuna idadi
kubwa ya ndugu/wanaukoo ambao bado hawajapata fursa ya kuhudhuria mikutano hii.
Ndiyo maana, Umoja wa Ukoo wa Kivenule bado unahamasisha ndugu/wanaukoo
wahamasishane kuhudhuria mikutano hii.
Vijiji ambavyo vimeonyesha mwelekeo mzuri
na ambapo kwa Viongozi wa Ukoo ni mafanikio makubwa ni pamoja na Kidamali,
Nyamihuu, Ilala-Simba, Nyamahana, Magubike, Idete na Nzihi. Umoja wa Ukoo wa
Kivenule unadhani kuwa hii changamoto tosha kwa viongozi pamoja na
ndugu/wanaukoo toka sehemu mbalimbali hapa Tanzania.
Mapambano na harakati endelevu za kukabiliana
na mabadiliko ya dunia kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni, kisayansi na
teknolojia, utandawazi na soko huria hayawezi kukwepeka. Yote haya kwa pamoja
inabidi yatafutiwe mbadala/mwafaka kwa kuunda jamii shirikishi katika masuala
mbalimbali yanayohusu maendeleo hasa suala la kupata elimu, kuwa na hali nzuri
kiuchumi na kuyakubali mabadiliko ya dunia na hivyo kuchukua hatua mahsusi
kuweza kukabiliana nayo.
Ongezeka la watu wanaoathirika na gonjwa
hatari la UKIMWI, milipuko ya magonjwa yanayoambatana na UKIMWI mfano Kifua
Kikuu, njaa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, uharibifu wa mazingira ni
mojawapo ya changamoto ambayo Ukoo wa Kivenule unawajibu wa kuyakabili.
Madhara ya majanga haya tayari
yanaonekana katika zetu na katika maisha yetu ya kila siku. Mfano ongezeko la
watoto yatima, watoto wa mitaani wasio na walezi, kuongezeka kwa utegemezi
kutokana na wajane kutokuwa na msaada baada ya kupoteza/kufiwa na ndugu/wanaume
zao kutokana na maradhi ya UKIMWI bado ni tatizo kubwa.
Jamii hii tegemezi tunayoijenga na ambayo
tunaishuhudia ikikua pole pole siku hadi siku, inatutegemea sisi ndugu/wanaukoo
wa kila kitu. Kwa mfano jamii yetu ina wajibu wa kuhudumiwa chakula, malazi,
mavazi, madawa, nyumba nzuri za kuishi na elimu. Je, jamii hii itaweza
kukabiliana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia kama sisi kama wanajamii
husika tutashindwa kukubali kuwajibika kwa kuwapa elimu na huduma zingine za
msingi? Hii ni changamoto kubwa ambayo hatuna budi kuifanyia kazi, na kila
ndugu/mwanaukoo kukubali kila jukumu ambalo atakuwa amepewa na jamii inayomzunguka.
Nasi kama jamii inayounda Ukoo wa
Kivenule tuna wajibu wa kushirikiana na asasi za kijamii na kiserikali katika
kuleta maendeleo. Wimbi la umaskini uliokithiri, janga la UKIMWI, ujinga na
rushwa vimekuwa ni vikwazo vikubwa vya maendeleo na ambavyo vinazidi kudidimiza
harakati mbalimbali za kuweza kujiinua na kujikwamua katika hali hiyo. Harakati
hizi za kutafuta maendeleo zimegawanyika katika makundi mbalimbali ya kijamii
hususani makundi ya wasomi, wakulima, wafugaji, wafanyabiashara, wanawake na
wananchi wa kawaida.
Pia haja ya kufahamiana baina ya
wanajamii na ndugu wanaounda ukoo, pamoja na kuujua Ukoo kwa ujumla.
Pamoja na mambo mengine, kamati
ilifikiria pia uwezekano wa kufanya senza ili kujua idadi ya ndugu wanaounda
ukoo husika toka kona mbalimbali hapa Tanzania; kujua nini wanakifanya na kujua
idadi sahihi ya wanandugu ambao wanahitaji msaada wa namna moja au nyingine.
Katika suala nzima la Kufahamu Historia
na Chimbuko la Ukoo, Mahusiano baina ya wanandugu ndani ya ukoo, Elimu, Maadili
na Dini na gonjwa hatari la UKIMWI, Kamati ilionelea kuwa ni mojawapo ya mambo
msingi sana kuyaangalia katika shughuli nzima ya maandalizi na wakati wa
Mkutano Mkuu.
Changamoto zitakazopatikana baada ya
kuyagusia mambo haya ya msingi na hivyo kuwawezesha washiriki wa mkutano mkuu
kujenga ajenda mpya.
Mahusiano duni baina ya wana ndugu,
kukosekana kwa ushirikiano katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo, hali duni ya
kiuchumi na kijamii, matatizo ya kifamilia na kiukoo ni kati ya masuala ya
msingi yaliyofikiriwa sana kabla ya kuanza kufanya maandalizi ya Mkutano Mkuu.
Mwelekeo na nafasi ya ukoo wa Kivenule
katika suala nzima la Elimu hasa katika dunia hii ya Utandawazi
(Globalization). Maendeleo ya sayansi na teknolojia ambapo yameifanya dunia
kuwa kama kijiji kisicho na mipaka na kila mtu anaruhusiwa kuingia na kutoka;
kuongezeka kwa viwanda vinavyotumia teknolojia ya hali ya juu; kuongezeka kwa
teknolojia ya habari na mawasiliano (Internet); kupanuka na kujengeka kwa miji,
pamoja na soko huria.
Mambo yote haya ndiyo yanayoweza
kuonyesha mustakabali na nafasi ya ukoo wa Kivenule kwa maisha ya baadaye.
Ilionekana kuwa ukoo wetu upo nyuma sana katika suala nzima la elimu, hii
linajidhihirisha kutokana na kuwa na ndugu wachache sana ambao wameweza kupata
elimu kwa kiwango kinachostahili.
Hii ni hatari kwa sababu tunajenga ukoo
tegemezi ambayo baadaye utakosa mwelekeo. Mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia
yanayojitokeza kila kukicha yanaibadili dunia na hivyo kutulazimisha nasi
katika ukoo wa Kivenule kubadilika. Matumizi ya teknolojia ya habari na
mawasiliano katika simu za mikononi, Internet, kompyuta, redio na satelaiti ni
changamoto kubwa katika Ukoo wa Kivenule.
Kati ya Maazimio ambayo Kamati
iliyategemea kuyatekeleza katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ni
pamoja na:
1.
Kufanyika
kwa Senza ya Ukoo wa Kivenule ili kupata idadi kamili ya ndugu.
2.
Kuanzisha
Mfuko wa Ukoo ambao utasaidia katika kusomesha watoto wanaofaulu pamoja na
kusaidia katika matatizo mbalimbali yanayojitokeza au uhitaji wa msaada.
3.
Kuchagua
Viongozi wa Ukoo pamoja na Wajumbe Wawakilishi watakaounda Kamati ya Ukoo ya
Kuratibu mambo mbalimbali ya ukoo. Nafasi za Viongozi watakaochaguliwa
zitajumuisha Mwenyekiti, Makamu wa Mwenyekiti, Katibu, Katibu Msaidizi, Mweka
Hazina na Msaidizi wake pamoja na Walezi Watatu wa kushauri uongozi uliopo
madarakani.
4.
Kuzitaja/kutamka
bayana kazi/majukumu mbalimbali ambayo Uongozi utakaoundwa utakuwa unazifanya
mfano kufanya mashauriano na usuluhishi wa matatizo mbalimbali ya ukoo
yaliyojitokeza. Lakini pia jukumu lao kubwa ni kuongoza na kusimamia majukumu
mbalimbali yanayojitokeza au kuhitaji usimamizi ndani ya ukoo.
5.
Kukusanya
taarifa mbalimbali za ukoo; na
6.
Kuangalia
na Kutathmini usalama wa mali mbalimbali zinazomilikiwa na ukoo nk.
II:
MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA TATU WA KAUKI
Kamati zote mbili za maandalizi ya
Mkutano Mkuu wa Pili wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule ile ya Kidamali na ya Dar es
Salaam, zilikaa pamoja ili kuweza kufanya tathmini ya shughuli nzima ya maandalizi
ya Mkutano Mkuu yaliyofanyika kati ya mwezi Januari na Mei 2006.
Lengo la kuzikutanisha Kamati zote mbili
ilikuwa ni kufanya tathmini ya hatua za maandalizi zilizofikiwa kwa ajili ya
kufanikisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Pili wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule.
Ilionekana dhahiri kuwa Kamati ya Maandalizi ya Kidamali ilifanya vizuri zaidi,
huku Kamati ya Maandalizi toka Dar es Salaam – ikionyesha kuelemewa kutokana na
mwitikio duni wa wanaukoo waishio eneo hilo la mjini. Hii ilikuwa na mara ya
pili kwa Kamati ya Dar es Salaam kuzidi kujidhihirisha kwake kushindwa kabisa
kuunga mkono harakati hizi wanajamii wanaunda ukoo Kivenule. Ni idadi ya watu
wachache tu ndio waliotoa michango yao.
Kamati zote mbili za Maandalizi ya
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ya Kidamali na Dar es Salaam,
zilifanikiwa kukusanya jumla ya shilingi 250,000.00 mpaka siku ya
mwisho ilipofanyika tathmini ya ukusanyaji wa michango wa Kamati zote mbili;
tofauti na jumla ya shilingi 345,350.00 zilizopatikana
katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule.
Kamati ya Dar es Salaam ilijitahidi
kufanya maandalizi ya moja kwa moja kwa kuandaa ripoti ya mkutano mkuu wa
kwanza na kuandaa mabango, katika harakati za Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Pili
wa Ukoo wa Kivenule. Maandalizi hayo yalihusisha uandalizi wa Rasimu ya Katiba,
Mabango na Ripoti ya mkutano huo.
Pia Kamati ya Dar es Salaam iliandaa
vitambulisho kwa ajili ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo wa
Kivenule. Lengo ilikuwa ni kuhakikisha kuwa kila mshiriki anakuwa na
kitambulisho wakati Mkutano ukiendelea.
III: MIALIKO KWA WANAUKOO PAMOJA NA WASHIRIKI
WENGINE
Mialiko ya wanandugu pamoja na wanaukoo
kwa ujumla, kuhudhuria MKutano Mkuu wa Pili wa Ukoo wa Kivenule ilifanyika wazi
kwa kila mtu bila upendeleo, kila mwanaukoo alipewa taarifa za kufanyika kwa
Mkutano Mkuu wa Ukoo na kuombwa kuhudhuria. Aidha kamati zote mbili za
maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, zilikubaliana kwamba,
kila mwanandugu au mwanaukoo anapaswa kuhudhuria mkutano huo bila kukosa.
Mialiko ilifanyika kwa namna mbalimbali
ikiwemo ile ya mdomo. Yaani kumwalika mwanaukoo au ndugu moja kwa moja kwa
kumpa maelekezo kuhusiana na mahali unapofanyika mkutano mkuu, tarehe pamoja na
muda. Familia yote, yaani baba, mama na watoto, wote walipaswa kuhudhurio
mkutano mkuu huo.
Pia mialiko ilifanyika kwa kubandika
matangazo ya kuutangaza Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo wa Kivenule sehemu
mbalimbali Kijijini Kidamali pamoja na maeneo mengine ambako Kamati ziliamini
ndugu na wanaukoo wanaishi kule.
Kila ndugu aliyefika na kuhudhuria
Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo wa Kivenule, alipewa kitambulisho cha kuweza
kumtambulisha kwa ndugu wengine. Kitambulisho hicho kilionyesha namba ya
kitambulisho, jina la ndugu, mahali anapoishi na simu au sanduku la posta.
Kamati ziliepuka ile hali ya kuulizana maswali ya kuwa wewe unaitwa nani,
unaishi wapi na simu yako iko wapi? Hii ilikuwa ni sababu ya msingi ya kutoa
kitambulisho kwa kila mwanaukoo au ndugu.
IV: UBANDIKAJI WA MATANGAZO
Ubandikaji wa matangazo ya kuutangaza
Mkutano Mkuu wa Pili wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule ulifanyika sehemu mbalimbali
Kijijini Kidamali pamoja na maeneo mengine ambako Kamati ziliamini ndugu na
wanaukoo wanaishi kule, ulifanyika kwa lengo la kuwajulisha ndugu kuhusu uwepo
wa Mkutano Mkuu na wapi unafanyika.
Baadhi ya sehemu kulikobandikwa matangazo
ni pamoja na Kidamali, Magubike, Nzihi, Nyamihuu, Ipogolo na Nyamihuu.
Ubandikaji wa matangazo ya Mkutano Mkuu wa Ukoo, uliibua hisia ya kushawishika
kuhudhuria kwa wanaukoo na wasio wanaukoo kuhusiana na kufanyika kwa Mkutano
huo. Wapo majirani, marafiki na watu wasio wanaukoo waliokuwa na shauku kubwa
ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo wa Kivenule sambamba na
ilivyojitokeza katika mkutano mkuu wa kwanza wa ukoo wa Kivenule.
V.
HOTUBA YA UFUNGUZI
Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo wa Kivenule
ni sehemu ya harakati za maendeleo zilizoanza toka mwaka jana, mwezi Februari 05, 2005
zikiwa na jukumu la kuinua hali za maisha za wanaukoo wa ukoo wa Kivenule
wanaoishi katika maeneo mbalimbali hapa Tanzania. Harakati hizo ndizo
zilizopelekea kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo wa Kivenule hapa Juni
24 na 25, 2006.
Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo wa
Kivenule ulifunguliwa na
Mgeni Rasmi Ndugu John Sungu, ambaye
pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kidamali. Awali ya yote, Mwenyekiti
wa Ukoo wa Kivenule ambaye pia alikuwa ni msimamizi wa Maandalizi ya Mkutano
Mkuu wa Pili wa Ukoo, Ndugu Faustino Kivenule, aliwakaribisha ndugu, jamaa,
mgeni rasmi, wageni waalikwa na wanaukoo kwa ujumla kwenye mkutano huo.
Kabla ya kusoma hotuba ya Ufunguzi wa
Mkutano Mkuu wa Ukoo, Mwenyekiti wa Ukoo alimkaribisha Ndugu George Kivenule,
kuuombea Mkutano Mkuu kwa sala. Baada ya Sala ya kuuombea mkutano huo, Mwenyekiti
wa Ukoo, alitumia fursa hiyo kuisoma Hotuba ya Ufunguzi.
Alianza kwa kuwajulisha ndugu, mgeni
rasmi, wanaukoo na wageni waalikuwa kuwa, lengo la Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo
wa Kivenule ni kuwaunganisha wanaukoo wote, wanaoishi sehemu mbalimbali hapa
Tanzania, ili wafahamiane, waelimishane na kupeana ujuzi katika nyanja
mbalimbali za maendeleo na pia kupeana uzoefu.
Pia, lengo jingine la Mkutano Mkuu wa Pili
wa Ukoo wa Kivenule ilikuwa ni kutolewa na kufundishwa kwa Mada ya HISTORIA NA
CHIMBUKO LA UKOO WA KIVENULE ambayo kwa siku hiyo iliwasilishwa na William
(Kadungu) Sigatambule Kivenule kutoka upande wa maeneo ya Kidamali; na Ndugu
Augustino Kivenule kutoka maeneo ya Ilole.
Jukumu jingine la Mkutano Mkuu wa Pili wa
Ukoo ilikuwa ni kuwasilishwa na kujadiliwa kwa Rasimu ya Katiba, Kufungua Mfuko
wa Ukoo, Kusoma na Kuijadili Ripoti ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa
Kivenule na Kuusimika upya Uongozi. Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo ulifanyika
sambamba na hitma ya marehemu Edgar (Kanolo) Sigatambule Kivenule ambaye kwa
bahati mbaya Mwenyezi Mungu alimchukua mwezi Aprili 2006. Pia ilikuwa ni fursa
nyingine ya kumbukumbu ya kumpoteza mmoja wa wanaukoo marehemu Alphonce
(Mwanitu) Sigatambule Kivenule ambaye pia Mwenyezi Mungu alimwita tarehe 9
Januari 2006. “Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi; Amina”.
Pia mkutano mkuu wa pili ulikusudia
kufanya senza ili kujua idadi ya wanaukoo na mwishoni kutoa hoja ya kuvunja au
kuendelea na uongozi uliochaguliwa kuandaa Rasimu ya Katiba ya Umoja wa Ukoo wa
Kivenule.
Harakati hizi zilifanyika
Kijijini Kidamali kwa upande mmoja na kwa upande mwingine jijini Dar es Salaam.
Kamati zote mbili zilizoundwa
zilijipa majukumu mbalimbali, likiwemo lile la kuwaalika na kuwashirikisha
ndugu na wanaukoo katika suala zima la maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Ukoo
katika vikao, na pia utoaji wa michango.
Katika harakati za maandalizi
ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa UKoo wa Kivenule, kamati zote mbili zilizipata
vikwazo mbalimbali likiwemo tatizo la mwitikio duni katika kulipokea wazo hili.
Kwa ujumla, katika kuliuza suala/wazo hili la kuandaa na kuwa na Mkutano Mkuu
wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, kamati ilibidi zitumiea nguvu na mbinu za ziada
ili kuweza kufanikiwa.
Mahudhurio duni yalitoa
changamoto kwa Kamati za Maandalizi ya Mkutano Mkuu, kuongeza juhudi/jitihada
na kutafuta njia mbadala za kufikia lengo. Kwa upande wa Kijijini Kidamali,
ushawishi ulizaa matunda, kwa sababu ongezeko la wanaukoo na ndugu kuliunga
mkono wazo la kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo lilivuna washiriki
wengi.
Kwa upande wa Dar es Salaam,
suala la mahudhurio duni, liliendelea kuwa ni kikwazo kwa kipindi chote cha
maandilizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Wapo waliodiliki
kusema Mkutano Mkuu wa Ukoo ufanyike kwanza Dar es Salaam na ndipo ufanyike na
kijijini Kidamali. Licha ya kupewa sababu na maelezo ya kina ya kuufanya
Mkutano huo ufanyike Kijijini Kidamali, hawakutilia maanani.
Katika suala la utoaji wa
michango, watu wamekuwa na ari na mwitikio wa hali ya juu hapa Kijijini
Kidamali, na kwa kiwango kikubwa ndio waliosaidia kufanikisha kufanyika kwa
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule.
Licha ya wanaukoo waishio Dar
es Salaam kuchangia, lakini mchango wao umesaidia kidogo sana, kwa sababu
kiwango kikubwa cha fedha pamoja na mahitaji mengine, yamepatikana hapa.
Sehemu nyingine, nje ya
Kidamali, utoaji wa michango hapo mwanzo ulikuwa wa wastani, lakini kadiri siku
zilivyokuwa zinakaribia, ari na kasi mpya ilijitokeza na kuwa kubwa hasa toka
sehemu za Magubike pamoja na Nyamihuu.
Majirani na watu wengine wasio
wanaukoo wamejitolea kutoa michango katika kuusaidia Ukoo wa Kivenule,
kufanikisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Majirani
na marafiki waliojitokeza kwa hali na mali katika kutoa fedha, vyombo na vifaa
mbalimbali.
VI.
HOTUBA YA MGENI RASMI
Mgeni Rasmi aliwashukuru wanandugu wa
Ukoo wa Kivenule wa kumwalika kuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano Mkuu wa Pili wa
Ukoo wa Kivenule. Awali ya yote alitumia fursa hiyo kuomba radhi kwa niaba ya Mwenyekiti
wa Kijiji Ndugu Daima Luvanda kutoweza kuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa mkutano
huo kutokana na kuwa na majukumu ya kikazi. Badala yake alimuomba yeye
amwakilishe katika ufunguzi wa mkutano huo.
Pia aliwaomba radhi Wanaukoo wa Ukoo wa
Kivenule kwa sababu alikuwa hajajiandaa kuwa mgani rasmi hivyo hakuwa na ajenda
au kitu mahsusi cha kuwasilisha katika Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Pili wa
Ukoo. Nimeshtukizwa, nilikuwa kwenye shughuli zangu, na nasikitika sitakuwa
nanyi kwa muda wote wakati Mkutano huo ukiendelea kutokana na majukumu ya
kikazi. Naomba mnisamee. Ila naahidi kuwa kesho tutakuwa wote na yale machache
ambayo niliyapanga niyaseme leo, nitayasema siku ya kesho.
Akiwahutubia Wanaukoo wa Ukoo wa
Kivenule, Mgeni Rasmi aliwashukuru na kuwapongeza ndugu/wanaukoo waliobuni mikutano
ya aina hiyo. Hii ni hamasa kwa jamii nyingine na mfano mzuri kuwa na mikutano
kama hii. Natumaini jamii nyingine zinazotuzunguka zinapata fundisho kubwa.
Binafsi mwenyewe nimepata fundisho kubwa
sana katika Mkutano huu wa leo. Nilipokuwa naongea na Mwenyekiti wa Ukoo,
nimeelezwa malengo na faida mbalimbali za kuunda Umoja wa Ukoo wa Kivenule. Baadhi
ya faida za kufanya Mkutano Mkuu ambazo nimeelezwa na Mwenyekiti wa Ukoo ni pamaja
na ndugu/wanaukoo kufahamiana. Kutokana na Ukoo kupanuka sana, ndugu/wanaukoo
kuongezeka na kuwa wengi, ilionekana haja ya kuwakusanya ndugu/wanaukoo kwa
pamoja na kuweza kufahamiana. Ukoo umetambua hatari ya maingiliano baina ya
wanandugu mfano kuchumbiana na kuoana.
Sisi kama Viongozi wa Kijiji tunapata
fundisho na hamasa ya kuzihamasisha jamii nyingine kujifunza na kufanya
mikutano ya namna hii. Pia nilielezwa baadhi ya malengo ni pamoja na kuanzisha
MFUKO WA MAENDELEO YA UKOO ambao utazinduliwa wakati wa Mkutano huu; pamoja na
Kuijadili Rasimu ya Katiba ya Umoja wa Ukoo wa Kivenule.
Baadhi ya Mikakati ambayo imeelezwa na
Mwenyekiti katika hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo wa
Kivenule ni pamoja na kuhamasisha suala la Elimu kwa ndugu/wanaukoo. Ukoo wa
Kivenule unatambua suala la umuhimu wa Elimu kwa kila ndugu na mwanaukoo na
hivyo unahamasika kufanya kila linalowezekana kuhakikisha kiwango cha elimu
kinakua ili Ukoo uweze kupambana na mabadiliko ya dunia yaani Sayansi na
Teknolojia, Utandawazi na Soko Huria.
Baada ya kuzungumza hayo machache,
napenda kusema kuwa MKUTANO MKUU WA PILI WA UKOO WA KIVENULE umefunguliwa rasmi
mnamo saa 04:24 Asubuhi tarehe 24 Juni
2006.
VII. UTAMBULISHO
Kwa mujibu wa Ratiba ya Mkutano Mkuu wa Pili
wa Ukoo, Mwenyekiti wa Ukoo Ndugu Faustino Sigatambule Kivenule alitumia fursa
hii kuwaalika ndugu/wanaukoo kujitambulisha. Utambulisho ulifanyika kwa kila
ndugu/mwanaukoo kujitambulisha mwenyewe Jina lake na pia kutaja majina matatu
au zaidi ya hapo akimjumuisha Baba, Mama, Bibi na Babu zake.
Utambulisho ulifanyika kwa rika zote,
toka mtoto mdogo hadi mtu mzima wa makamo. Lengo la kujitambulisha ni
kuwawezesha ndugu wengine walioshiriki mkutano mkuu kuwatambua na kuwafahamu
ndugu zao wanaoishi maeneo mengine.
Pia utambulisho ulifanyika kwa kuandaliwa
vitambulisho ambavyo kila mshiriki wa Mkutano Mkuu wa Pili wa Umoja wa Ukoo wa
Kivenule, alipewa. Kitambulisho kiliandikwa jina la mshiriki wa mkutano
kikitaja majina matatu yaani jina lake, jina la baba na jina la ukoo. Pia
anuani nyingine nazo ziliandikwa kwenye kitambulisho ili kuwarahisishia ndugu
wengine kuzitambua kirahisi anuani za ndugu zao wengine.
Sambamba na hilo pia uandikishaji
(kujisajili) kwenye daftari kulifanyika ikiwa ni sehemu ya kutunza kumbukumbu
za washiriki wa mkutano mkuu wa pili. Mahudhurio yote yameambatanishwa kwenye
ripoti hii.
VIII. HISTORIA YA UKOO:
WILLIAM KIVENULE NA AUGUSTINO KIVENULE
Mada hii Historia na Chimbuko la Ukoo wa
Kivenule, iliwasilishwa na Ndugu William Sigatambule Kivenule kutoka Kidamali
kwa kushirikiana na Ndugu Augustino Kivenule kutoka Nduli. Wote kwa ujumla wao walijitahidi
kueleza na kufafanua kiini cha Chimbuko la Ukoo huu. Kwa kuanza Mwezeshaji
kutoka Kidamali Ndugu William, aliwaeleza washiriki wa mkutano huo kuwa Babu
MTELINGOMA BALAMA ndiye aliyekuwa mwanzilishi halisia wa ukoo wa Kivenule. MTELINGOMA
ndiye aliyemzaa Babu TAGUMTWA BALAMA (KIVENULE).
Babu TAGUMTWA BALAMA (KIVENULE) ndiye
aliyewazaa Babu TAVIMYENDA KIVENULE na Babu KALASI KIVENULE kivenule. Ikumbukwe
kuwa, jina halisi la ukoo wa Kivenule ni BALAMA. Kama ilivyokwisha julikana
katika mada iliyowasilishwa katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Umoja wa Ukoo wa
Kivenule, ambapo ilielezwa kuwa, neno KIVENULE linamaanisha sifa ya kuwa jasiri
Vitani na hasa katika kutumia silaha za Mishale na Mikuki yaani kwa Lugha
Asilia ya Kihehe “KUMIGOHA”.
KUVENULA likiwa na maana halisi ya kuwa
na shabaha ya kuwaangamiza maadui kwa kutumia silaha ya Mishale na Mikuki. Babu
zetu akina TAGUMTWA BALAMA walilidhihirisha hili katika Vita na hivyo
kuzawadiwa jina la KIVENULE kama jina la sifa kutokana na ushujaa katika Vita.
Baada ya kuwazaa watoto hawa wawili yaani
TAVIMYENDA na KALASI, walisafiri na kufika hadi sehemu ya KALENGA, wakiwa
katika harakati za kutafuta maisha. Ndipo Babu TAVIMYENDA KIVENULE alipoombwa
na Mzee MYINGA aende akamsaidie kumchungia mifugo yake eneo la MAGUBIKE na pia
Babu KALASI KIVENULE naye kuamua kwenda eneo la ILOLE kutafuta maisha.
Akiwa eneo la MAGUBIKE, Babu Tavimyenda
Kivenule akafanikiwa kupata watoto Saba (7), yaani BABU KAVILIMEMBE KIVENULE, BABU
MGAYAFAIDA KIVENULE, BABU SIGATAMBULE KIVENULE, BIBI MGASI KIVENULE, BIBI MALIBORA
KIVENULE, BIBI SIGINGULIMEMBE KIVENULE, BABU ABDALAH KIVENULE NA BIBI
SIKIMBILAVI SEMABIKI. Huyu Bibi
Sikimbilavi Semabiki hakuwa mtoto wa Babu Tavimyenda ila alikuwa ni mtoto wa
kufikia kwa Bibi yetu.
Baadhi ya akina Babu walifanikiwa kuwa na
wake zaidi ya mmoja na hawa walikuwa ni Babu SIGATAMBULE KIVENULE, ambaye mke
wake wa kwanza alikuwa anaitwa SIWANGUMHAVI SINGAILE, mke wake wa pili alikuwa
anaitwa NYANYILIMALE SINGAILE na mke wa
Tatu, PANGULIMALE SETWANGA. Mke wa pili na tatu wa Babu Sigatambule bado wapo
hai.
Babu HUSEIN KIVENULE naye alikuwa na wake
wawili ambao ni YIMILENGERESA SEMSISI na DALIKA SETALA. Taarifa za wake wa Babu
wengine bado zinaendelea kufanyiwa utafiti. Babu MGAYAFAIDA KIVENULE yeye
hakubahatika kuoa wala kuwa na mtoto. Alikuwa ni mlemavu na ndiyo maana ya jina
lake MGAYAFAIDA.
Kwa upande wa ILOLE, Babu KALASI KIVENULE
alibahatika kuwa na watoto watatu ambao ni Babu SALAMALENGA (KAHENGULA)
KIVENULE, MGUBIKILA (NYAKUNGA) KIVENULE NA SEKINYAGA KIVENULE.
BABU SALAMALENGA KIVENULE alikuwa
mwanaume peke yake na wawili waliobaki walikuwa ni wanawake. Babu Salamalenga
Kivenule alioa wake watatu ambao ni Bibi NYANGALI, BIBI SEMFILINGE MHENGAATOSA
NA BIBI SEMKONDA CHOGAVANU. Kupitia kwa wake zake watu, Babu Salamalenga ndiye
aliyeeneza Ukoo wa Kivenule katika maeneo ya Nduli, Ilole, Mgongo na Kigonzile.
Tafsiri
za Majina Mbalimbali yaliyopo katika Ukoo wa Kivenule
Kidagamhindi Heka
heka za kukimbia kodi wakati wa mkoloni
Tunyahindi Kupigwa
pigwa na wakoloni
Mwanitu Alizaliwa
kweusi (kwa kutumia lung’ali). Kuwasha moto ili kupata mwanga kwa kutumia kuni
au aina fulani ya nyasi. Mara nyingi ving’ali vinakuwa vinazimika.
Kadungu Kuwa
na Dungu kubwa (kuwa na kitovu kikubwa)
Kibumo Mvefi
(Mtu anayelialia)
Mlagile Alizaliwa
wakati Bibi yake hayupo. Wakati anaonyeshwa Bibi yake akisema Mlagile akaitwa Mlagile.
Fatamali Alifuata
mali
Yamkopita Bibi
alipomzaa mtoto wa kwanza na kisha kufariki, akapata jina la ya Mkopite
Luhanage Wakati
Bibi anazaa watoto wanakufa, alipomzaa mtoto na akaugua sana basi akaitwa
Luhanage. Luhanage maana yake ni kuugua sana.
Mgendwa Alizaliwa
kwa taabu. Alizaliwa kwa waganga wa kienyeji kwa tabu wakiwa safarini
Msinziwa
Kanolo Wakati
ameugua, anapiga ramli huki akitembea kwa waganga.
Yimilengeresa Mzee
Babu Husein alichukuliwa kwenye Vita ya Pili ya Dunia. Wahindi walikufa sana na
Waingereza wakashinda Vita.
Misamiti ya Lugha ya Kihehe
Mhisive Binamu
Nyavana Degedege
MUUNDO
WA UKOO WA KIVENULE (MWIBALAMA)
IX. KUSOMA RIPOTI YA
MKUTANO MKUU WA PILI WA UKOO WA KIVENULE
Pamoja na mambo mengine yaliyojitokeza
katika Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo wa Kivenule, ilikuwa ni pamoja na Kuisoma
Ripoti ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule uliofanyika Desemba 17 –
18, 2005 Kidamali – Iringa. Ripoti ya Mkutano Mkuu wa Kwanza ilikuwa na kurasa
Tisini na Nane (98), huku ikiwa imegawanyika katika Vipengele Kumi na Tisa (19),
picha mbalimbali za matukio wakati mkutano huo na senza ya Ndugu/Wanaukoo toka
Ilole.
Vipengele vilivyopo kwenye Ripoti ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa
Kivenule ni pamoja na:
I.
Utangulizi
II.
Uundaji
wa Kamati za Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo Wa Kivenule
A:
Kuhamasisha/Uhamasishaji
B:
Uchangiaji wa Michango
C:
Mwitikio Katika Uchangiaji Michango
III.
Tathmini
ya Maandalizi Ya Mkutano Mkuu Wa Kwanza Wa Ukoo Wa Kivenule
IV.
Uundaji
wa Kamati Za Kuratibu Mkutano
V.
Uteuzi
wa Wawezeshaji Wa Mada
VI.
Mialiko
kwa Wanandugu, Wanaukoo Pamoja Na Washiriki Wengine.
VII.
Ubandikaji
wa Matangazo
VIII. Siku ya Kwanza ya Mkutano Mkuu wa Kwanza
wa Ukoo wa Kivenule, Des. 17, 2005
IX.
Hotuba
ya Mgeni Rasmi
X.
Utambulisho
wa Wanaukoo
XI.
Wawasilishaji
wa Mada Katika Mkutano Mkuu Wa Ukoo
XII.
Ratiba
ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, Desemba 17 – 18, 2005
XIII. Kamati Iliyoratibu Shughuli Katika
Mkutano Mkuu Wa Kwanza Wa Ukoo Wa Kivenule
XIV. Tathmini ya Mkutano Mkuu wa Kwanza Wa
Ukoo Wa Kivenule
XV.
Mapendekezo/Maoni
Yaliyojitokeza Wakati wa Mkutano Mkuu Wa Ukoo
XVI. Uchaguzi wa Viongozi Wa Ukoo
XVII.
Shukrani
XVIII.
Kufunga
Mkutano
XIX.
Matukio
Katika Picha Siku Ya Mkutano Mkuu Wa Ukoo
X. KUIJADILI RIPOTI
Ripoti ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Umoja
wa Ukoo wa Kivenule, ilisomwa na Katibu Mkuu na Makamu wa Mwenyekiti kabla ya
wajumbu wa Mkutano Mkuu wa Pili wa KAUKI, kupata fursa ya kuijadili. Ripoti
ilikuwa na kurasa zipatazo mia moja (100). Kutokana na ukubwa wa ripoti hiyo,
viongozi hao wa KAUKI, walivisoma vipengele muhimu vya ripoti kwa kupokeza na
hivyo kuwapa washiriki wa mkutano kile kilichokuwa na umuhimu na kwamba kama
ilivyokubaliwa wakati mkutano, kutunza kumbukumbu ilikuwa ni mojawapo ya jukumu
mpya la Umoja wa Ukoo wa Kivenule unaoundwa.
Mada zote tano zilizowasilishwa
zilijumuishwa katika ripoti pamoja na majadiliano yaliyofanyika katika vikundi
na hivyo kumpa fursa msomaji wa ripoti kupata taswira ya mkutano ulivyokuwa.
Baada ya kuwajulisha wajumbe wa mkutano baadhi ya vipengele vinavyojumuisha
ripoti na kuvifafanua kimoja baada ya kingine kutokana na umuhimu wake, ulifika
wakati wa wanaukoo kuijadili ripoti hiyo.
Wajumbe waliopata fursa ya kutoa michango
yao, bila kusita waliisifu ripoti hiyo kwa jinsi ilivyofikia lengo na kuweza
kuhifadhi yale yote yaliyotokea katika mkutano mkuu wa kwanza wa KAUKI yakiwemo
matukio katika picha. Waliusifu utaratibu wa namna hiyo ya kuhifadhi kumbukumbu
kwani kichecheo na kivutio kwa wanaukoo wengine ambao bado hawapata fursa ya
kuhudhuria mikutano kama hii.
Waliomba nakala nyingi zaidi za ripoti
hiyo zitolewe na kusambazwa kwa ndugu wengine ili waweze kujua nini kinafanyika
katika mikutano hii. Awali ya yote kabla ya kusoma ripoti hiyo, viongozi wa
KAUKI waliomba msamaha kwa kutokuwa na nakala nyingi kutokana na bajeti kuwa
finyi ukilinganisha na gharama na kutoa nakala nyingi zaidi. Ili waliwaahidi
wanashiriki wa mkutano huo kuwa uongozi wa KAUKI utajitahidi kufanya hivyo na
ikibidi kila kanda ipate nakala ya ripoti hiyo.
Kila mjumbe aliyepata fursa ya kutoa
mchango wake wa mawazo, alikubaliana na yote yaliyojumuishwa katika ripoti
hiyo, na kisha kuomba nakala nyingi zaidi kwa kila mmoja wao kujisomea mwenyewe
nyumbani kwake.
XI. KUIPITISHA RIPOTI
Ripoti ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo
wa Kivenule ilipitishwa bila kipingamizi baada ya kujadiliwa kwa kina na
wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Pili wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule. Japokuwa hawakuwa
na nakala za ripoti hii, ila waliweza kusikiliza kwa umakini mkubwa yale yote
yaliyosomwa na viongozi na kisha kuikubali bila kipingamizi.
Waliopata fursa ya kukubali kutumika kwa
ripoti hiyo walisema kuwa kila kilichofanyika wakati wa mkutano kimejumuishwa
na pia kiwango cha uandishi wa ripoti hii inadhirisha. Ila walipendekeza, kwa
siku zijazo, nakala nyingi zaidi itabidi zitolewe ili kuwawezesha wajumbe
mbalimbali wa mkutano mkuu kuifuatilia usomaji mzima wa ripoti hizi.
|
XV. UCHAGUZI WA VIONGOZI WA
KANDA WA KAUKI
Uchaguzi wa Viongozi wa Kanda ulifanyika sambamba na uchaguzi wa Walezi
wa KAUKI. Kuna baadhi ya kanda zinaendelea kuwa na viongozi wake wa zamani. Kanda
chache bado hazijapata viongozi wake, lakini tunategemea kufanya utaratibu wa
kuweza kufanikisha upatikana wa viongozi hao.
Wafuatao hapa chini ni viongozi wapya wa Kanda wa KAUKI.
A. Ilole
- Pius Kivenule
- Bernadi Kivenule
- Titus Kivenule
B. Nduli
- Anna Kivenule
- Augustino Kivenule
C. Itagutwa
- Anyesi Kivenule
- Gipson Kitu
D. Dar es Salaam
- Ilole
- Ignas Kivenule
- Innocent Kivenule
- Delphinus Kivenule
- Kidamali
- Athuman Mtono
- Sijali Kivenule
E. Nyamihuu
- Benjamin Kivenule
F. Nyamahana
- Otavina Kivenule
G. Ilala Simba
H. Kidamali
- George Kivenule
- Jovin Kivenule
- Jermana Kivenule
- Pyela Kivenule
XVI. WALEZI WA KAUKI
Mkutano Mkuu wa Pili wa KAUKI uliitumia
fursa hiyo kufanya uchaguzi wa viongozi wa ngazi mbalimbali zikiwemo zile za walezi
wa umoja huo. Lengo la kuwa na walezi ni kuusaidia uongozi unaounda timu ya
uendeshaji wa KAUKI kwa kutoa ushauri pale panapoonekana panapwaya au kuyumba
ili lengo na makusudio ya KAUKI yaweza kufikia lengo.
Walezi waliochaguliwa jukumu lao jingine
ni kuhamasisha jamii inayounda umoja huo kuujua na pia kutoa ushirikiano baina
ya wanandugu katika mambo mbalimbali yanayofanyika kwa manufaa ya KAUKI.
Waliochaguliwa kuwa walezi wa KAUKI ni
pamoja na:
1.
Ignas Kivenule Dar
es Salaam
2.
Augustino Kivenule Ilole
3.
Stephan
Mhapa Kidamali
4.
John Kivenule Kilombero
XVII.
SENZA
Mojawapo ya mipango iliyokuwa imefikiriwa
kufanyika ilikuwa ni kufanya senza ya wanaukoo wakati wa Mkutano Mkuu wa Pili
wa KAUKI, lakini kutokana na ufinyu wa muda pamoja na mwingiliano wa majukumu
mbalimbali likiwemo lile la Arobaini ya Marehemu Edgar Kivenule, muda haukuweza
kutosha kuifanya senza hiyo.
Lakini jukumu la kufanya senza lilikuwa
mahsusi katika kuuwezesha Umoja wa Ukoo wa Kivenule kutekeleza malengo na
mipango yake ya mbeleni. Hii pia ingesaidia katika kufanya tathmini ya
makusanyo ya michango endapo nusu au robo tatu ya wanaukoo wangelipa michango
yao.
Pia hii ingesaidia kujua asilimia ya
wanaukoo ambao wanapata fursa ya kuhudhuria mikutano mikuu kama hiyo pamoja na kutambua
mgawanyiko/kusambaa kwa ukoo huu kwa ujumla. Senza pia ingesaidia kujua
mahitaji muhimu ya jamii hii yakiwemo matatizo ya kielimu yanayowakumba jamaa
mbalimbali ya jamii hii.
|
XVIII. UONGOZI MPYA WA
KAUKI
Baada ya kutolewa kwa kauli ya Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi ya Rasimu ya Katiba ya KAUKI, wajumbe wa kikao (ndugu/wanaukoo)
kwa kauli moja waliipinga kauli hiyo, na hivyo kuuomba uongozi wote ulioifanya
kazi hiyo nzuri kuendelea kushikilia nyadhifa zao kwa kipindi cha kwanza cha
miaka mitatu kwa mujibu wa Katiba mpya ya KAUKI. Walitoa hoja kuwa, kuuvunja
uongozi hakutajenga wala kusaidia kuuboresha kwa sababu viongozi waliopo ndio
wenye uzoefu wa shughuli hizi na wamejituma kwa kipindi chote, kuanzia
kuanzishwa Umoja wa Wanaukoo hadi hatua hii ya Kupitishwa kwa Katiba.
Chini ya Mwenyekiti, ilibidi uongozi wote
wa zamani kukubali kubeba dhamana ya uongozi kwa ngazi husika waliyopewa na
wanaukoo rasmi kuanzia tarehe 25 Juni 2006, Katika Mkutano Mkuu wa Pili wa
Umoja wa Ukoo wa Kivenule, uliofanyika katika Ukumbi wa Sanga, Kijijini
Kidamali-Iringa. Sambamba na hilo, Makamu wa Mwenyekiti wa Ukoo, ndugu
Christian Kivenule alitumia fursa hiyo kuwajulisha wanaukoo waliohudhuria
mkutano huo kuwa, Kamati Kuu ya Ukoo, ilifanya mabadiliko katika nyadhifa za
uongozi kulingana na mahitaji na hali halisi ya utendaji kazi wa kila siku.
Mabadiliko yalifanyika katika ngazi zote
za uongozi wa juu wa KAUKI isipokuwa katika nafasi ya Mwenyekiti, Mweka Hazina
na Msaidizi wake. Nafasi za uongozi zilizofanyiwa mabadiliko ni pamoja na
nafasi ya Makam wa Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Katibu Msaadizi. Mabadiliko hayo
yamebainishwa kama ifuatavyo:
1.
Mwenyekiti Ndugu Faustino Sigatambule Kivenule
2.
Makamu
Mwenyekiti Ndugu Christian John Kivenule
3.
Katibu
Mkuu Ndugu Adam Alphonce Kivenule
4.
Katibu
Msaidizi Ndugu Donath Peter Mhapa
5.
Mweka
Hazina Ndugu Justin Daniel Kivenule
6.
Mweka
Hazina Msaidizi Ndugu Carolina Sigatambule Kivenule
Picha za Viongozi Wakuu wa Umoja wa Ukoo
wa Kivenule (KAUKI)
|
|
|
|
|
|
||||||||||||
XIX.
MIPANGO NA MIKAKATI YA KAUKI KWA MWAKA 2006/7
Uongozi wa KAUKI ulioapishwa rasmi wakati
wa Mkutano Mkuu wa Pili wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule, kuanza kutekeleza wajibu
na majukumu mbalimbali yaliyopangwa kutekelezwa katika mwaka 2006/2007, ulipanga
kutekeleza yafuatayo:-
1.
Kusambaza
Ripoti ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule kwa Viongozi wa
Kanda na pia kwa wanaukoo wa ujumla;
2.
Kutoa
nakala nyingi za Ripoti ya Mkutano Mkuu wa Kwanza;
3.
Kuandaa
Kalenda ya Shughuli za Mwaka 2006/2007;
4.
Kufanya
uchaguzi wa Viongozi wa Kamati Ndogo;
5.
Kufanya
vikao vya Kamati Kuu;
6.
Kutolewa
nakala nyingi za Katiba ya KAUKI na kusambazwa;
7.
Kusambaza
stakabadhi za malipo kwa viongozi wa kanda;
8.
Kuonyesha
ushirikiano baina ya viongozi wa ngazi mbalimbali wa KAUKI;
9.
Viongozi
wa KAUKI kutekeleza wajibu wao;
10. KAUKI kuwa na sanduku lake la posta;
11. KAUKI kufungua Akaunti kwa ajili michango
mbalimbali ambayo inachangwa na wanachama wake.
|
XX.
TATHMINI YA MKUTANO MKUU
Mahudhurio: Safari hii, ndugu/wanaukoo waonaishi
sehemu za mbali mfano Dar es Salaam, Kilimanjaro, Mbeya, Morogoro na Ilole,
waliohudhuria kwa wingi. Kwa mfano, kwa upande wa Dar es Salaam pekee, jumla na
ndugu/wanaukoo 11 walihudhuria Mkutano Mkuu.
Upande mwingine ambao nao pia ulikuwa na
uwakilishi mkubwa ulikuwa ni Ilole, Nduli, Kigonzile na Mgongo, ambapo kwa
ujumla, ndugu/wanaukoo wapatao 12 walihudhuria mkutano huo, tofauti na
uwakilishi wa mwaka jana, ambapo ndugu mmoja (1) alihudhuria Mkutano Mkuu.
Kwa upande wa ndugu/wanaukoo
waliohudhuria Mkutano Mkuu toka mbali, ndugu/wanaukoo toka Mwanga mkoani
Kilimanjaro, walikuwa ni baadhi ya ndugu waliosafiri safari ndefu kuja kwenye
Mkutano Mkuu wa Pili wa Kivenule. Safari hii jumla ya ndugu/wanaukoo wapatao
wawili (2) walihudhuria Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo wa Kivenule tofauti na
mwaka jana ambapo tulikuwa hatuna uwakilishi wa aina yoyote.
Kwa wastani uwakilishi wa ndugu/wanaukoo
waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo wa Kivenule ulikuwa ni wa mtawanyiko
zaidi. Hii kwa Umoja wa Ukoo wa Kivenule ni jambo la kufurahisha na kujivunia
kwani baadhi ya malengo ya umoja huu ni kuwakusanya ndugu toka sehemu
mbalimbali hapa Tanzania. Viongozi wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule bado wanaamini
kuwa hawatimiza lengo lake la kuandaa mikutano ya namna hii kwani wanaamini
kuwa bado kuna idadi kubwa ya ndugu ambao bado hawajapata fursa ya kuhudhuria
mikutano hii. Ndiyo maana, Umoja wa Ukoo wa Kivenule bado unahamasisha ndugu
wahamasishane kuhudhuria mkutano huu.
Vijiji ambavyo vimeonyesha mwelekeo mzuri
na ambapo kwa Viongozi wa Ukoo ni mafanikio makubwa ni pamoja na Kidamali,
Nyamihuu, Ilala-Simba, Nyamahana, Magubike, Idete na Nzihi. Umoja wa Ukoo wa
Kivenule unadhani kuwa hii changamoto tosha kwa viongozi pamoja na
ndugu/wanaukoo toka sehemu mbalimbali hapa Tanzania.
Chakula
na vinywaji: Katika hali
ya kawaida, Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Pili wa Umoja wa Ukoo wa
Kivenule, chini ya uongozi wa ukoo, ilikusudia kuwapa huduma ya chakula na
vinywaji ndugu/wanaukoo pamoja na wageni waalikwa wote waliohudhuria mkutano
huo. Kwa ujumla, huduma hizo zimetolewa kwa kadri bajeti ilivyoruhusu. Huduma
ya chakula na chai ilitolewa kwa kila mshiriki na viongozi walihakikisha kuwa
kila mshiriki anapata huduma zote. Licha ya ufinyu wa bajeti uliojitokeza,
huduma bora ya chakula ndiyo ilikuwa kauli mbiu yetu.
Bajeti: Mkutano Mkuu wa Pili wa Umoja wa
Ukoo wa Kivenule, umekuwa na tatizo la ufinyu wa bajeti yake. Tumeshindwa kutoa
huduma zaidi mfano maji na soda wakati wote wa mkutano na badala yake, huduma
hiyo imetolewa wakati wa chakula tu. Vinywaji kama soda vimeweza kutolewa mara
tu tofauti na mipango na matarijio ya uongozi wa KAUKI. Kwa ujumla Kamati ya Maandalizi chini ya
Uongozi wa KAUKI, walijitahidi sana kuweka kipaumbele kwenye huduma za msingi.
Kwa mfano, baadhi ya huduma hazikutolewa
kutokana na ufinyu wa bajeti. Ripoti ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa
Kivenule, haikuweza kudurufiwa (kutolewa nakala nyingi); kuwaleta waandishi wa
habari wa magazeti, redio na televisheni; uchukuaji wa picha za video na picha
za mnato.
Mojawapo ya malengo ya kufanya mikutano
hii ni kutunza kumbukumbu hizo kwa njia mbalimbali mfano mikanda ya video,
vitabu, magazeti pamoja na kuandika ripoti kama hii iliyosomwa katika Mkutano
Mkuu wa Pili wa KAUKI.
Ufinyu wa bajeti umetufanya tuwe na aina
moja tu ya utunzaji wa kumbukumbu za matukio mkutanoni. Wanaukoo ndio
wachangiaji wakubwa wa bajeti zinazoaandaa mikutano hii. Kutokana na hali duni
ya miahsa, tunashindwa kufikia malengo. Kwa mfano, kuna uhaba wa vitendea kazi
kama kompyuta, printa, photokopi, projekta na televisheni kwa ajili ya
kufundishia. Tunafikiria zaidi, kuwa na miradi ya kujijengea uwezo ambayo
itasaidia uongozi wa KAUKI, kumudu baadhi ya gharama.
Ushiriki katika Mkutano: Kwa ujumla,
ndugu/wanaukoo walishiriki kikamilifu wakati wote katika siku mbili za Mkutano
Mkuu wa Pili wa KAUKI. Kamati ya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Pili wa KAUKI
iliteua Kamati Ndogo Ndogo zilizosaidia kuratibu shughuli zote za mkutano.
Mfano, Kamati ya Mapokezi ilifanya kazi yake ipasavyo pamoja na Kamati nyingine
kama Kamati ya Ulinzi na Usalama na Kamati ya Chakula. Kamati zote hizi,
zilishirikiana vyema na wawezeshaji wa Mkutano Mkuu wa Pili wa KAUKI,
kuhakikisha kuwa ratibu inafuatwa ipasavyo.
Mikutano Mikuu ya KAUKI, huendeshwa kwa
kumshirikisha kila mshiriki ili kuweza kuibua hisia na mawazo toka miongoni mwa
washiriki. Mikutano hii, huwa katika mfumo wa darasa, ambapo, huwepo na
mchanganyiko wa matukio mfano warsha, ambapo mada mbalimbali huwasilishwa na
kufundishwa, majadiliano katika vikundi hufanyika na pia mrejesho toka katika
makundi huwasilishwa mbele ya washiriki.
Makundi huundwa kutumia njia mbalimbali
ikiwemo ile ya kuhesabu namba 1 hadi 4 na kasha kugawanyika kutokana na namba
walizozihesabu. Baada ya kila kundi kuwasilishwa, makundi mengine huuliza
maswali au kutoa hoja au nyongeza kutokana na hisia au mawazo mbalimbali
yaliyoibuliwa miongoni mwa wanakikundi. Jinsi huzingatiwa kwa kila jambo
linalofanyika katika vikundi na mkutano mzima kwa ujumla.
Baada kila kikundi kuwasilisha, hoja
zilizoibuliwa hujumuishwa na mwezeshaji na pia baadaye kuandikwa kwenye ripoti
kwa ajili ya kumbukumbu na utekeleza hapo baadaye.
Tathmini ya Jumla: Inagusa zaidi
kuzingatiwa kwa muda na ratiba katika kipindi chote cha mkutano. Kamati ya
kuratibu mkutano huchangamka zaidi na kwenda sambamba na ratiba. Kwa mfano
chakula na chai huandaliwa na kutolewa kwa wakati kama ratiba inavyoonyeshwa.
Japo kuna matatizo ambayo hujitokeza wakati wa kuanza kwa mkutano ambapo
wanaukoo/washiriki huchelewa kufika kutokana na umbali.
Licha ya kasoro na uhaba wa vitendea
kazi, shughuli zilizopangwa kutekelezwa kwa mujibu wa ratiba, hufanyika kama
ilivyopangwa. Wawezeshaji hujitahidi kufikisha ujumbe kwa hadhira (washiriki wa
mkutano) kama ilivyokusudiwa kwa kutumia mbinu mbadala mfano vipaza sauti, mbao
wa karatasi (flip charts), stendi ya ubao wa karatasi (flip chart stand) na
kalamu za kuandikia (mark pens). Ukosefu wa kifaa cha kufundishia kwa uangavu
zaidi yaani projekta huwa ni changamoto kwetu kubuni njia bora zaidi.
Mafanikio yanajitokeza kwa ujumla na kwa
mtu mmoja mmoja kupitia mazungumzo au mahojiano. Uongozi wa Umoja wa Ukoo baada
ya kuanza shughuli zake rasmi unategema kuboresha mambo mbalimbali mfano huduma
za chakula na vinywaji, kupata vitenda kazi kama Kompyuta, Printa, Photokopi na
Projekta. Kuboresha ofisi iliyopo kwa huduma za mawasiliano za Intaneti na pia
kutafuta wafadhili wa kutusaidia kutujengea uwezo na kutupatia vifaa vya
kufanyia kazi.
Yaliyojiri katika Mkutano Mkuu wa Pili wa
KAUKI ni:
- Kusoma na kupitishwa kwa Ripoti ya Mkutano Mkuu wa Pili wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule;
- Kupitishwa kwa mabadiliko ya uongozi wa KAUKI;
- Kupitishwa kwa Rasimu ya Katiba (KAUKI);
- Kuzinduliwa kwa Mfuko wa Ukoo;
- Kuchagua Viongozi wa Kanda;
- Kuchaguliwa kwa Walezi wa KAUKI; na
- Kutangazwa kwa tarehe ya Mkutano Mkuu wa Tatu wa KAUKI.
XXI.
SHUKRANI
IGNAS
KIVENULE NA SILLA MHAPA
Ndugu Ignas Kivenule ambaye ni Mjumbe wa
Kamati Kuu ya Umoja wa Ukoo wa Kivenule, aliwashukuru wanaukoo wote waliotoa
ushirikiano na kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Pili KAUKI, kwa kuwa wameonyesha
umoja wa hali ya juu sana. Binafsi yeye anaamini jamii inayounda Ukoo wa
Kivenule ni wapole na wasio na majivuno. Ila angefurahi sana kama jamii
inayounda ukoo huu itajitokeza kwa wingi zaidi katika Mkutano Mkuu wa Tatu wa
Ukoo wa Kivenule, utakaofanyika mwakani Juni 2007.
Ukoo wa Kivenule una zaidi ya ndugu 2000
kutoka pande zote za Kidamali, Ilole, Nduli, Magubike na kwingineko. Ni wajibu
wa kila mwanaukoo kuhamasisha watu wengine wajitokeze kuhudhuria Mkutano Mkuu
ujao. Sambamba na hilo, pia aliiomba jamii ya Ukoo wa Kivenule ikalipa umuhimu
suala la kusomesha watoto ili kupunguza utegemezi na pia kuwaandalia hali bora
za maisha hapo baadaye.
Alisikitika kwa wanaukoo toka Ilole
kutohudhuria kwa wingi Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo wa Kivenule, ila angefurahi
sana kama jamii hiyo ya Ilole ingeshiriki mkutano huo kwa wingi. Kuna sababu
nyingi zimetolewa, likiwemo suala la Nauli. Lakini, kama kila mwanaukoo atakuwa
anajali ni jambo la msingi sana wangejiandaa kikamilifu kuhudhuria Mkutano
ujao.
Wanaukoo wengi wa kutoka Dar es Salaam
wamekuwa ni wazito na hii pia inakatisha tamaa. Kama ni matatizo ni vyema jamii
yote ikashirikiana. Mojawapo ya mambo mazuri na ya msingi ya kufanya Mkutano
Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ni kuiwezesha jamii inayounda ukoo huu, kuwa
na uwezo wa kukabiliana na matatizo ya kila siku. Mwishoni aliwashukuru
wanaukoo wote wa Kidamali kwa moyo wa ukarimu waliouonyesha
XXII. VIAMBATANISHO
MAHUDHURIO
KWENYE MKUTANO MKUU WA PILI WA UKOO WA KIVENULE
JINA KAMILI
|
MAHALI UNAPOISHI
|
ANUANI/SIMU
|
1. CAROLINA S. KIVENULE
|
KIDAMALI
|
S.L.P. 742
IRINGA: 078158225
|
2. CHRISTIAN J. KIVENULE
|
MOROGORO
|
0784308195/0744035675
|
3. IGNAS P. KIVENULE
|
DAR ES SALAAM
|
0744060183
|
4. DONALD S. MHAPA
|
KIDAMALI
|
07878 43565
|
5. FAUSTINO S. KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
6. ADAM A. KIVENULE
|
DAR ES SALAAM
|
0784270364/
0713270364
|
7. JUSTIN D. KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
8. GLORIA Z. KIVENULE
|
MBEYA
|
0745337263
|
9. GODFREY Z. KIVENULE
|
IGOWOLE
|
S.L.P 98,
IGOWOLE-MUFINDI
|
10. FARAJA Z. KIVENULE
|
IGOWOLE
|
S.L.P 98,
IGOWOLE-MUFINDI
|
11. RECHINA D. KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
12. NORAH E. KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
13. ASIA J. KIVENULE
|
MOROGORO
|
|
14. JAMIRA NGENG’ENA
|
MAGUBIKE
|
|
15. GEORGE S. KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
16. INNOCENT MALAMBO
|
KIDAMALI
|
|
17. OSCAR E. KIVENULE
|
DAR ES SALAAM
|
|
18. ELIAS MDONGWA
|
KIDAMALI
|
|
19. CASTILIA NZALA
|
MAGUBIKE
|
|
20. KONJETA KIVENULE
|
MAGUBIKE
|
|
21. FEDELIKA NZALA
|
MAGUBIKE
|
|
22. ANYESI KIVENULE
|
ITAGUTWA
|
|
23. ROSE NZALA
|
MAGUBIKE
|
|
24. RETISIA MDEGELA
|
NDULI
|
|
25. ANETHA KIVENULE
|
NDULI
|
|
26. ANNA KIVENULE
|
NDULI
|
|
27. AUGUSTINO KIVENULE
|
MGONGO
|
|
28. PIERA S. KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
29. FSIJALI KIVENULE
|
DAR ES SALAAM
|
|
30. MONICA KIVENULE
|
NDULI
|
|
31. BETH NYANGALIMA
|
MAGUBIKE
|
|
32. OSCAR UTENGA
|
MAGUBIKE
|
|
33. DAUD NYAKUNGA
|
KIDAMALI
|
|
34. MARTIN KIVENULE
|
NDULI
|
|
35. HALIDI KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
36. MARIA A. NGUVILA
|
KIDAMALI
|
|
37. DOMINIKA KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
38. TAUSILA KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
39. HAPPY KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
40. FESTO D. KIVENULE
|
MAGUBIKE
|
|
41. BENJAMIN KIVENULE
|
NYAMIHUU
|
|
42. MAMA DOMISIA KIVENUE
|
KIDAMALI
|
|
43. JANETH KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
44. MADESTUS KIVENULE
|
MAGUBIKE
|
|
45. ANNA KIVENULE
|
MAGUBIKE
|
|
46. STEPHEN NZALA
|
MAGUBIKE
|
|
47. FAUZIA KIVENULE
|
MAGUBIKE
|
|
48. JERUMAN S. MAHAPA
|
KIDAMALI
|
|
49. VITUSI NZALA
|
MAGUBIKE
|
|
50. THEODOSI KIVENULE
|
MAGUBIKE
|
|
51. FARAJA KIVENULE
|
IGOHOLE
–MUFINDI
|
|
52. WINNIE E. KIVENULE
|
DAR ES SALAAM
|
|
53. ROMANUS KIVENULE
|
MAGUBIKE
|
|
54. SFELIO NZALA
|
NYAMAHANA
|
|
55. FREX NYWAGE
|
KIDAMALI
|
|
56. TAVINA KIVENULE
|
NYAMAHANA
|
|
57. BERNADI KIVENULE
|
MAGUBIKE
|
|
58. JESCA KIVENULE
|
MAGUBIKE
|
|
59. ANJELA NGWETA
|
MAGUBIKE
|
|
60. RUJINA KIVENULE
|
NYAMAHANA
|
|
61. CHESI KIVENULE
|
MAGUBIKE
|
|
62. AMANI MPONZI
|
IGANGIDUNG’U
|
|
63. MELDA KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
64. DOMINICUS KIVENULE
|
MAGUBIKE
|
|
65. JOHN SUNGU
|
KIDAMALI
|
|
66. ANNETH KIVENULE
|
DAR ES SALAAM
|
|
67. DORIS P. KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
68. ATANAS E. MBUNZA
|
KIDAMALI
|
|
69. TOMAS MWIKUKA
|
NYAMIHUU
|
|
70. TOBIS MWITALA
|
NYAMIHUU
|
|
71. KASMILI KIVENULE
|
MAGUBIKE
|
|
72. KEVIN KIVENULE
|
MAGUBIKE
|
|
73. CLELIA G. KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
74. AGAPE G. KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
75. ANJELIKA A. KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
76. AUJEN W. KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
77. ANORD D. KIVENULE
|
MAGUBIKE
|
|
78. EMMANUEL H. KIVENULE
|
MAGUBIKE
|
|
79. NESIA H. KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
80. STAN SINGAILE
|
KIDAMALI
|
|
81. STEWART E. KIVENULE
|
DAR ES SALAAM
|
|
82. JOHN MKWAMBE
|
KIDAMALI
|
|
83. BITRESSY SINGAILE
|
KIDAMALI
|
|
84. ANJENTINA H. KIVENULE
|
NYAMIHUU
|
|
85. ADELAH A. KIVENULE
|
MAGUBIKE
|
|
86. GLORIA J. KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
87. HATIBU UTENGA
|
MAGUBIKE
|
|
88. HURUMA M. CHENGULA
|
KIDAMALI
|
|
89. MSAFILI W.SINGAILE
|
KIDAMALI
|
|
90. STEPHAN S. MHAPA
|
KIDAMALI
|
|
91. AIDIN LUSASI
|
IPOGOLO –MJINI
|
|
92. AIVON F. KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
93. EGLA CHENGULA
|
KIDAMALI
|
|
94. LULU S. MHAPA
|
KIDAMALI
|
|
95. FREDY NORHA KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
96. FADHILI E. KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
97. XAVERY S. KIVENULE
|
IGOWOLE-MUFINDI
|
|
98. KAINI E. KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
99. HASSAN W. KIVENULE
|
ILOLE
|
|
100.
JOHN
S. KIVENULE
|
KILOMBERO –
MORO
|
|
101.
ELIZABERT J. KIVENULE
|
KILOMBERO-
MORO
|
|
102.
SILLAH
S. MHAPA
|
MWANGA-KILIMANJ.
|
|
103.
JANNETH
D. KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
104.
NERDA
KYANDO
|
KIDAMALI
|
|
105.
FRIDA
K. KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
106.
NORAH
D. KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
107.
GIFT
Y. KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
108.
DEBORAH
L. SANGA
|
KIDAMALI
|
|
109.
PONSIANO
S. KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
110.
GRACE
KIVENULE
|
KALENGA
|
|
111.
FEDELIKA
MHAPA
|
TOSAMAGANGA
|
|
112.
BAKHITA
J. KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
113.
FELISTER
MPOSEWA
|
KIDAMALI
|
|
114.
CHRISTINA
J. KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
115.
ONORATHA
SEHAVA
|
KIDAMALI
|
|
116.
VICTORIA
KIVENULE
|
NDULI
|
|
117.
PETER
MHAPA
|
KIDAMALI
|
|
118.
SALOME
MPOSEWA
|
KIDAMALI
|
|
119.
ATHUMAN
MTONO
|
DAR ES SALAAM
|
|
120.
INNOCENT
S. KIVENULE
|
DAR ES SALAAM
|
|
121.
FRANK
I. KIVENULE
|
DAR ES SALAAM
|
|
122.
REMMY
P. KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
123.
JUSTIN
W. SINGAILE
|
KIDAMALI
|
|
124.
DANIEL
S. KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
125.
JONISIA
S. MKWAMBE
|
KIDAMALI
|
|
126.
MARKO
KIVENULE
|
MAGUBIKE
|
|
127.
KOSTER
MHUNGULU
|
KALENGA
|
|
128.
JELTHA
MVELA
|
KIDAMALI
|
|
129.
AGNESSY
S. KIVENULE
|
KIDAMALI
|
|
130.
GETRUDE
SEMASILA
|
IDODI
|
|
131.
LESANDU
S. MHAPA
|
KIDAMALI
|
|
132.
TAMIMA
NGENG’ENA
|
MAGUBIKE
|
|
133.
BELTHA
NYANGALIMA
|
MAGUBIKE
|
|
134.
JOHN
MGUMBA
|
KIDAMALI
|
|
135.
ISABELA
MGIMWA
|
KIDAMALI
|
|
136.
DINER
D. MHAPA
|
KIDAMALI
|
|
137.
PRISCA
B. KIVENULE
|
NYAMIHUU
|
|
138.
PENINA
L. MKAMA
|
MOSHI
|
|
JINA LA MGENI
RASMI
|
MGENI RASMI
|
|
|
|
|
|
|
|
RATIBA YA MKUTANO MKUU WA
PILI WA UMOJA WA UKOO WA KIVENULE
Siku ya Kwanza ya Mkutano Mkuu wa Pili wa Umoja wa Ukoo wa KIVENULE |
||
24 Juni 2006
|
||
Muda
|
Shughuli/Jukumu
|
Wahusika
|
12:00–12:45
|
Wageni Wote Kuamka na Kufanya Maandalizi
ya Kuingia kwenye Mkutano
|
Wote |
12:45–1:45
|
Kupata Kifungua Kinywa
|
Washiriki wote
|
1:45 – 2:45
|
Kuwasili Mkutanoni na Kujisajili
|
Washiriki wote
|
2.45 – 3.00
|
Kusoma Hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano
Mkuu wa Pili wa Ukoo wa
|
Mwenyekiti wa Ukoo
|
3:00 – 3:15
|
Ufunguzi Rasmi wa Mkutano na Mgeni
Rasmi
|
Mgeni Rasmi
|
3:15 – 4:00
|
Utambulisho baina wa wana Ndugu
|
Wote
|
4:00 – 4:15
|
Pumziko la Chai /
Kahawa/Maji
|
Wote
|
4:15 – 5:00
|
Mada: CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO |
1. Mwakilishi - Kidamali2. Mwakilishi toka Ilole |
5:00 – 5:30
|
Kuijadili Mada na Kuchangia Mawazo
Mbalimbali
|
Washiriki wote
|
5:30
– 6:30
|
KUSOMA
RIPOTI YA MKUTANO MKUU WA KWANZA WA UKOO WA KIVENULE
|
Katibu
na Mwenyekiti
|
6.30 – 7.00
|
Kuijadili
Ripoti na Kuchangia Mawazo mbalimbali
|
Washiriki
wote
|
7:00 – 8:00
|
CHAKULA CHA MCHANA
|
Wote
|
8:00 – 8:20
|
KUSOMA RASIMU YA KATIBA YA UMOJA WA
KIVENULE
|
1.
Katibu Msaidizi
2.
Makamu Mwenyekiti
|
8:20 – 9:45
|
Kuijadili Rasimu ya Katiba na Kuchangia
Mawazo, Kutoa Maoni na Ushauri (majadiliano yataendelea baada ya pumziko la
chai)
|
Wanaukoo Wote
|
9:45– 10:10
|
Pumziko la Chai/Kahawa/Maji |
Wote
|
10:10-10:40
|
Majadiliano juu ya Rasimu ya Katiba
pamoja na kuchangia Mawazo, kutoa Maoni na Ushauri yanaendelea
|
Wanaukoo wote
|
10.40 – 11.00
|
Kusoma marekebisho na yote yaliyojitokeza kuhusiana na majadiliano ya
Rasimu ya Katiba
|
Katibu Mkuu
na Msaidizi wake
|
11.00
|
KUAHIRISHA KIKAO MPAKA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 25 JUNI 2006
|
Mwenyekiti
|
11.00 – 1:30
|
Burudani (Muziki wa Kisasa na Ngoma za
Asili), vinywaji, kufahamiana zaidi na kubadilisha mawazo
|
Wanaukoo wote
|
1:30 – 2:30
|
Chakula cha Usiku na
Vinjwaji
|
Wanaukoo wote
|
2:30 – 6:30 Usiku
|
Burudani (Muziki wa Kisasa na Ngoma za
Asili), vinywaji, kufahamiana zaidi na kubadilisha mawazo
|
Wanaukoo wote
|
Siku ya Pili ya Mkutano Mkuu wa Pili wa Umoja wa Ukoo wa KIVENULE |
||
25 Juni 2006
|
||
Muda
|
Shughuli/Jukumu
|
Wahusika
|
12:00–12:45
|
Wageni Wote Kuamka na Kufanya
Maandalizi Mbalimbali
|
Wanaukoo wote |
12:45–2:45
|
Kupata
Kifungua Kinywa
|
Wanaukoo
wote
|
2:45 – 3:15
|
Kujiandaa kwenda Kanisani
|
Wanaukoo
wote
|
3.15 – 6.15
|
Ibada Kanisani
|
Wanaukoo
wote
|
6.15 – 6.45
|
Kusimika Msalaba
|
Wanaukoo
wote
|
6:45 – 7:30
|
CHAKULA CHA MCHANA
|
Wanaukoo wote
|
7:30 – 8:00
|
KUISOMA KATIBA YA UMOJA WA UKOO WA KIVENULE NA KUOMBA KUIPITISHA |
Katibu Mkuu na Wanaukoo Wote |
8:00 – 8:30
|
Uchaguzi wa Viongozi wa Kamati Ndogo
Ndogo Mbalimbali
|
Washiriki wote
|
8:30 – 9:30
|
YALIYOJITOKEZA
KWENYE MKUTANO MKUU WA PILI WA UMOJA WA KIVENULE
|
Makamu
Mwenyekiti na Katibu Msaidizi
|
9.30 – 9.45
|
Kuwatangazia Wanaukoo Majina ya:
·
Viongozi wa
Umoja wa Ukoo;
·
Kamati Kuu ya
Ukoo; na
·
Kamati Ndogo
Ndogo Mbalimbali.
|
Mwenyekiti
na
Katibu Mkuu
|
9.45 – 9.50
|
Kuzindua Mfuko wa Ukoo wa Umoja wa Ukoo wa
Kivenule (Kuanza Kukusanya michango)
|
Mgeni Rasmi na Wanaukoo wote
|
9.50 – 10.20
|
KUFUNGA MKUTANO MKUU WA PILI WA UMOJA WA KIVENULE
|
Mgeni Rasmi
|
12.00
– 1:30
|
Burudani
(Muziki wa Kisasa na Ngoma za Asili), vinywaji, kufahamiana zaidi na
kubadilisha mawazo
|
Wanaukoo
wote
|
1:30 – 2:30
|
Chakula cha Usiku na
Vinjwaji
|
Wanaukoo wote
|
2:30 – 6:30 Usiku
|
Burudani (Muziki wa Kisasa na Ngoma za
Asili), vinywaji, kufahamiana zaidi na kubadilisha mawazo
|
Wanaukoo wote
|
KATIBA YA UMOJA WA UKOO WA
KIVENULE
2006
UTANGULIZI
MWANAUKOO/NDUGU
popote pale alipo katika
sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atakuwa huru kujiunga na UMOJA WA UKOO WA KIVENULE; kwa
kuwasilisha jina lake kwa Wawakilishi wa Ukoo toka sehemu husika au kwa
Viongozi wa Ukoo wanaoishi eneo hilo;
MWANAUKOO/NDUGU, kwa kutumia Haki za Kiraia pamoja na
Uhuru wa Kikatiba wa kujiunga au kujihusisha au kushirikiana na kundi lolote,
tunaamini atajiunga na UMOJA WA UKOO WA
KIVENULE ambao umejiwekea majukumu mengi likiwamo jukumu la kutekeleza
shughuli za maendeleo ya wanaukoo, kuulinda ukoo na kuuendeleza kwa kutumia
rasilimali zilizopo;
MWANAUKOO/NDUGU, kwa kutumia Haki za Kiraia na za
Kikatiba, anao Uhuru wa kwenda na kuishi mahali popote, kufanya shughuli yeyote
pasipo kuvunja sheria na kuunda au kujiunga na vikundi mbalimbali vya kijamii
ili kujiletea maendeleo;
UMOJA
WA UKOO WA KIVENULE unatoa
fursa sawa na bila masharti, kwa kila ndugu/mwanaukoo kujiunga nao, na pia
unatoa fursa sawa kwa kila mwanaukoo kushirikiana na wanaukoo wengine katika
harakati za kujiletea maendeleo;
UMOJA
WA UKOO WA KIVENULE upo,
ili kulinda mali ya ukoo, haki na uhuru wa ndugu/mwanaukoo yoyote, familia
yake, mali yake, usalama wake, maendeleo yake na pia kumsaidia pale
inapohitajika kusaidiwa;
UMOJA
WA UKOO WA KIVENULE
unaoundwa utakuwa na nguvu za kisheria na msaada katika shughuli za kujiletea
maendeleo kwa wanaukoo; na ili upate nguvu ya kisheria inabidi upate usajili wa
kudumu toka kwa mamlaka husika za kisheria ili uweze kufanya kazi ipasavyo;
Kila Mwanaukoo, ana wajibu wa kuyashika
na kuyatekeleza yale yote ambayo yamekuwa ni maazimio na makubaliano,
yaliyosaidia kuundwa kwa UMOJA WA UKOO
WA KIVENULE;
Jina la Umoja wa Ukoo wa Kivenule unaoundwa
utajulikana kama UMOJA WA UKOO WA
KIVENULE wenye kifupisho KAUKI. Umoja huu
utasajiliwa kwenye mamlaka au ofisi husika chini ya vifungu vya sheria
vinavyotambuliwa. Pia Umoja wa Ukoo wa Kivenule unaweza kusajiliwa kama MFUKO
(FOUNDATION) au vinginevyo lakini msaada wa kisheria unatakiwa zaidi ili umoja
wetu uwe na fursa na kunufaika na mikopo
au misaada mbalimbali mbalimbali; na
SISI
WANAUKOO WA UKOO WA KIVENULE, tuliokutana tarehe 24 na 25 Juni 2006, katika MKUTANO MKUU WA PILI WA UKOO WA KIVENULE, tumekubaliana kuunda UMOJA WA UKOO WA KIVENULE wenye malengo
na madhumuni mahsusi na ya msingi kama yalivyobainishwa katika Ibara ya 3.0,
sehemu ya (i) kifungu (a) – (r).
1.0
NGUVU YA KISHERIA
(i).
UMOJA WA UKOO WA KIVENULE utakuwa na Haki ya Kisheria ya kudai
fidia kutokana na kusababishiwa hasara, kuvunjiwa heshima au madhara ya aina
yoyote kutoka kwa mtu, kundi la watu, taasisi ya umma, taasisi binafsi, kampuni
au serikali. Pia, UMOJA WA UKOO WA
KIVENULE utakuwa na haki ya kisheria ya kumfikisha mahakamani mtu, kundi la
watu, taasisi binafsi, taasisi ya umma, ndugu yeyote, kampuni au serikali
itakapothibitika kuwa ameusababishia Ukoo madhara au hasara kubwa, na pia kama
kutakuwa na umuhimu wa kufanya hivyo.
2.0
USHIRIKIANO NA VIKUNDI VINGINE
(i).
UMOJA WA UKOO WA KIVENULE upo huru kuwa mwanachama wa Vikundi
mbalimbali vya Kijamii, Taasisi za Umma na Binafsi na Mitandao mbalimbali ya
Kimaendeleo; na pia upo huru kushirikiana na Umoja wa Vikundi vya Kijamii au
Jamii nyingine za ndani na nje ya nchi, vyenye mwelekeo na malengo yanayofanana
na UMOJA WA UKOO WA KIVENULE.
Ushirikiano huo utaamuliwa na Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Kivenule.
3.0
MALENGO/MADHUMUNI YA UMOJA WA UKOO WA KIVENULE
(i).
UMOJA WA UKOO WA KIVENULE umejiwekea malengo yafuatayo:
a).
Kuujua
na kuuelewa kwa kina Chimbuko na Historia ya Ukoo wa Kivenule;
b). Kufanya senza ya ndugu/wanaukoo wanaounda
Ukoo wa Kivenule kila inapobidi kufanya hivyo na Senza hiyo itajumuisha watu
waliohai na wafu;
c).
Wanaukoo/ndugu
kufahamiana na kutambuana kuwa wao ni kitu kimoja;
d). Wanaukoo/ndugu kuutambua na kuuelewa
mtawanyiko/mgawanyiko wa Ukoo wa Kivenule;
e).
Kusuluhisha
na kutatua matatizo yanayojitokeza katika Ukoo wa Kivenule kwa kupitia vikao
vinavyokubalika;
f).
Kuongeza
na kuimarisha mahusiano mazuri ndani na nje ya ukoo kwa kushirikiana katika
matatizo mfano raha, ugonjwa, misiba pamoja na majanga makubwa;
g). Wanaukoo/ndugu kushirikiana katika
shughuli za uzalishaji mali pamoja na utendaji kazi wa kila siku;
h). Kuwa na nguvu ya kurekebisha tabia
zisizostahili kwa wanaukoo/ndugu ndani ya Ukoo na kutafuta suluhu ya
migogoro/migongano baina ya mtu au jamii inayotuzunguka;
i).
Kuelimisha
Wanaukoo/ndugu kuhusiana na madhara ya ugonjwa wa UKIMWI, matumizi ya Madawa ya
Kulevya na Ulevi wa kupindukia;
j).
Kuufanya
Ukoo wa Kivenule uheshimike na kutambulika kwa sifa nzuri na Koo nyingine hapa
nchini;
k).
Ukoo
wa Kivenule uhamasishe koo nyingine kuunda umoja unaofanana na huu wa Kivenule;
l).
Kushirikiana
na umoja au vikundi vingine vilivyoungana ili kuuletea Ukoo wa Kivenule
maendeleo endelevu;
m).Kuboresha Elimu ndani ya Ukoo wa Kivenule ili
ndugu/wanaukoo wawe na uelewa wa hali juu na kumudu mabadiliko ya Sayansi na
Teknolojia katika Dunia ya Utandawazi;
n). Kuinua viwango vya maisha vya
ndugu/wanaukoo wa Kivenule na kuishi maisha mbadala yenye milo kamili, furaha
na nyumba bora na nadhifu;
o). Kuanzisha Mfuko wa Ukoo wa Kivenule
utakaosaidia kuinua kiwango cha Elimu na pia kusomesha ndugu/wanaukoo wasio na
uwezo wa kumudu kulipa ada za shule au vyuo;
p). Kuanzisha Mfuko wa kukopeshana (SACOSS);
q). Kupunguza au kuondoa kabisa tabia ya
uvivu na uzembe ndani ya Ukoo wa Kivenule; na
r).
Kuratibu,
kuzikusanya na kuhifadhi kumbukumbu mbalimbali za Ukoo wa Kivenule.
4.0
SIFA ZA MWANAUKOO
(i).
Kila
ndugu/mwanaukoo aliyezaliwa ndani ya Ukoo Kivenule au kuchangia damu na
ndugu/mwanaukoo anakuwa na sifa ya kuwa mwanaukoo wa UMOJA WA UKOO WA KIVENULE moja kwa moja;
(ii).
Hamna
kiingilio chochote kwa ndugu/mwanaukoo kujiunga na Umoja wa Ukoo wa Kivenule;
(iii).
Mwanaukoo
atathibitishwa kwa kujiandikisha/andikishwa katika orodha ya ndugu/wanaukoo
waliokwisha hesabiwa kupitia senza ya ukoo.
4.1
UKOMO WA MWANAUKOO
(i).
Ndugu/mwanaukoo
hana ukomo katika UMOJA WA UKOO WA KIVENULE;
(ii).
Labda
akifikwa na mauti.
4.2
HAKI ZA MWANAUKOO
(i).
Ana
haki ya kujiunga na Umoja wa Ukoo wa Kivenule bila masharti yeyote;
(ii).
Hana
kipingamizi katika kuushauri na kuupa
msaada Umoja wa Ukoo wa Kivenule;
(iii).
Ana
haki ya kuhudhuria na kushiriki kikamilifu katika Mkutano Mkuu wa Ukoo wa
Kivenule pamoja na mikutano mingine ambayo ataalikwa;
(iv).
Ana
haki ya kutoa dukuduku lake kwa viongozi wa ukoo au Mkutano Mkuu wa Ukoo;
(v).
Ana
haki ya kusikilizwa pindi atakapopata matatizo yoyote yale katika maisha yake
ya kila siku;
(vi).
Ana
haki na uhuru wa kutoingiliwa na Umoja wa Ukoo wa Kivenule katika shughuli zake
halali za kila siku katika kujitafutia riziki ya kuendesha maisha yake,
isipokuwa kama hatavunja miiko ya umoja huo;
(vii). Ana haki ya kuheshimiwa na kuthaminiwa na
kila ndugu/wanaukoo;
(viii).
Ana
haki ya kuwa na familia;
(ix).
Ana
haki ya kujiunga na vikundi halali au umoja wowote popote pale ulipo/alipo;
(x).
Ana
haki ya kwenda mahali popote bila kuzuiwa au kuingiliwa na viongozi au
ndugu/mwanaukoo yeyote maadamu havunji sheria;
(xi).
Ana
haki ya kutii imani ya aina yoyote bila kuingiliwa na Umoja wa Ukoo wa
Kivenule;
(xii). Hawezi kutengwa wala kujitenga na Umoja
wa Ukoo wa Kivenule kwa sababu anaingia moja kwa moja kwa mujibu wa Ibara 4.0 (i) kuhusu sifa za mwanaukoo;
na
(xiii).
Hawezi
kujitoa katika Umoja wa Ukoo wa Kivenule labda akipatwa na mauti.
4.3
WAJIBU WA MWANAUKOO
(i).
Kutoa
michango ya aina yoyote kama Katiba ya Umoja wa Ukoo wa Kivenule inavyoelekeza;
(ii).
Kutoa
michango ya dharura pindi atakapoombwa na Viongozi wa Ukoo wa Kivenule;
(iii).
Kuheshimu
maamuzi yanayotolewa kwa mujibu wa Katiba ya Umoja wa Ukoo wa Kivenule;
(iv).
Kulipa
ada ya kila mwezi kama ilivyoainishwa kwenye Katiba ya Umoja wa Ukoo wa
Kivenule;
(v).
Kushiriki
kikamilifu katika matatizo mfano ugonjwa, misiba, njaa na sherehe;
(vi).
Kuhudhuria
vikao mbalimbali kama ilivyoanishwa kwenye Katiba ya Umoja wa Ukoo wa Kivenule;
na
(vii). Ana wajibu wa kutii maagizo yoyote toka
kwa viongozi wa ukoo yenye maslahi kwa Ukoo wa Kivenule.
5.0
MICHANGO
(i).
UMOJA WA UKOO WA KIVENULE utakuwa na michango ya aina tatu (3)
itakayotambulika katika Katiba. Michango hiyo ni pamoja na:
a).
Michango
ya Kuanzia;
b). Michango Endelevu ya kila Wiki, Mwezi,
Miezi na kadhalika; na
c).
Michango
ya dharura katika Ugonjwa au Vifo.
5.1
MICHANGO YA KUANZIA
(i).
Kiasi
cha shilingi Elfu Mbili tu (2,000/=) za Tanzania kinapendekezwa kiwe ni kianzio
katika kutoa Michango ya Kunzia katika UMOJA
WA UKOO WA KIVENULE;
(ii).
Michango
ya Kuanzia ya shilingi Elfu Mbili tu (2,000/=) za Tanzania, inapendekezwa ianze
kutolewa baada ya Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo wa Kivenule, mwezi Juni hadi
Julai 31, 2006;
(iii).
Michango
ya Kuanzia inaweza kutolewa kwa awamu ili kuwawezesha wale wasio na kipato cha
uhakika waweze kulipa bila kuathiri maisha yao ya kila siku;
(iv).
Umoja
wa Ukoo wa Kivenule unamwomba kila ndugu/mwanaukoo ajitahidi kulipa Michango ya
Kuanzia itakayoanza Juni mpaka Julai 31, 2006; na
(v).
Michango
ya Kuanzia haimuzuii ndugu/mwanaukoo yeyote kutoa zaidi ya kiasi kilipendekezwa
ndani ya Katiba ya UMOJA WA UKOO WA
KIVENULE.
5.2
MICHANGO ENDELEVU
(i).
Kiasi
cha shilingi Mia Tano tu (500/=) za Tanzania kilipendekezwa kiwe kinalipwa kila
mwezi kama Mchango Endelevu ili kuchangia UMOJA
WA UKOO WA KIVENULE;
(ii).
Mchango
Endelevu wa kila mwezi wa shilingi Mia Tano tu (500/=) za Tanzania
unapendekezwa uanze kutolewa kuanzia tarehe 01 Agosti, 2006;
(iii).
Michango
Endelevu haimuzuii ndugu/mwanaukoo mwenye uwezo na ari ya kuuendeleza ukoo
kuchangia zaidi; na
(iv).
UMOJA WA UKOO WA KIVENULE unamwomba kina ndugu/mwanaukoo ajitahidi
kulipa Michango Endelevu wa kila mwezi.
5.3
MICHANGO YA DHARURA
(i).
Michango
ya dharura itatolewa pindi pale yatatokea matatizo mfano ugonjwa au kifo; na
(ii).
Michango
ya dharura itatolewa pindi litakapojitokeza jambo au shughuli ya muhimu ya
kimaendeleo inayobidi kukamilika mfano kumlipia ada, mchango kununua
shamba/nyumba na nauli au kumsaidia ndugu/mwanaukoo kulipa faini katika
mahakama ili kumweka huru na kadhalika.
5.4
ULIPAJI WA MICHANGO
(i).
Michango
ya Kuanzia ya shilingi Elfu Mbili tu (2,000/=) za Tanzania, itaanza kutolewa
baada ya MKUTANO MKUU WA PILI WA UKOO WA
KIVENULE, mwezi Juni 26 hadi Julai 31, 2006;
(ii).
Mchango
Endelevu ya kila mwezi wa shilingi Mia Tano tu (500/=) za Tanzania utaanza
kutolewa kuanzia tarehe 01 Agosti, 2006;
(iii).
Stakabadhi
itatolewa kwa ndugu/mwanaukoo kwa kila aina ya mchango utakaoutoa;
(iv).
Michango
ya aina yote italipwa kwa Mweka Hazina au Mweka Hazina Msaidizi;
(v).
Kwa
wale wanaoishi mbali na Waweka Hazina wa Ukoo, watalipa michango yao kwa
viongozi wa Ukoo wanaotambuliwa na kupewa stakabadhi yenye mhuri wa Ukoo wa
Kivenule;
(vi).
Ndugu/mwaukoo
yuko huru kulipa zaidi ya kiasi kilichopendekezwa katika Katiba ya Umoja wa
Ukoo wa Kivenule;
(vii). Michango Endelevu inaweza kulipwa kwa
mwezi, miezi, mwaka na hata miaka kadhaa; na
(viii).
Kutakuwa
na daftari maalum la kunakili michango ya dharura. Endapo Michango ya Dharura
itazidi malengo/kusudio, kiasi kinachobaki kitaingizwa kwenye Mfuko wa Umoja wa
Ukoo wa Kivenule. Kiwango cha
kumsaidia mgonjwa kibainishwa wazi
5.5
UFUATILIAJI WA MICHANGO
(i).
Viongozi
wote wa Ukoo wa Kivenule wanajukumu la kuhimiza, kuhamasisha na kufuatilia
ndugu/wanaukoo kulipa/kutoa michango yao;
(ii).
Wawakilishi
katika Kamati ya Ukoo pia nao wana wajibu wa kuhimiza, kuhamasisha na
kufuatilia ndugu/wanaukoo kulipa/kutoa michango yao;
(iii).
Viongozi
wa kutoka kila sehemu wanakoishi ndugu/wanaukoo waandae orodha ambayo itatumika
kukusanyia michango;
(iv).
Stakabadhi
yenye mhuri wa Ukoo wa Kivenule itatolewa kwa kila aina ya mchango utakaotolewa
na ndugu/mwanaukoo kutoka kwa viongozi wa ukoo wanaotambuliwa na waliopewa
jukumu la kukusanya mchango;
(v).
Viongozi
wanaokusanya michango wasiwakwaze ndugu/wanaukoo wenye moyo na ari ya kutoa
zaidi michango bali wawahamasishe na kuwapa moyo;
(vi).
Viongozi
kutoka sehemu mbalimbali wafuatilie michango ya kila mwezi ili kusiwe na
malimbikizo ya muda mrefu; na
(vii). Ukusanyaji wa michango umegawanywa katika
kanda sita (6); yaani Kanda ya Kidamali, Kanda ya Ilole, Kanda ya Magubike,
Kanda ya Morogoro, Kanda ya Nduli na Kanda ya Dar es Salaam na Mufindi. Kwa
hiyo kila mwanaukoo atakuwa anawasilisha mchango wake katika Kanda aliyo karibu
nayo.
5.6
ASIYETOA MICHANGO
(i).
Katiba
ya Umoja wa Ukoo wa Kivenule inabainisha wazi katika Ibara ya 4.3, kifungu (i),
(ii), (iv) na (vii) kinachoeleza wajibu wa mwanachama (mwanaukoo). Kwa
kushindwa kutekeleza vifungo hivyo vya Katiba, mwanachama (mwanaukoo)
atasababisha haya yafuatayo:
a).
Kukosa
au kutopata huduma muhimu na za msingi zitakazotolewa na Umoja wa Ukoo wa
Kivenule;
b). Atahojiwa na Uongozi wa Ukoo wa Kivenule ili
kubainisha tatizo linalomfanya asitoe michango au kulipa ada;
c).
Atahojiwa
na Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Kivenule na pia kubainisha kinachomfanya asiitii
Katiba.
d). Mkutano
Mkuu wa Ukoo utapewa taarifa toka kwenye Kamati nay eye atajitetea.
5.7
KUFUNGUA AKAUNTI YA UMOJA WA UKOO WA KIVENULE
(i).
UMOJA WA UKOO WA KIVENULE utafungua akaunti yake katika benki
yeyote itakayokubaliwa na Kamati Kuu ya Ukoo wa Kivenule. Kazi ya kufungua
Akaunti itafanywa na Viongozi wa Ukoo na hasa ikimjumuisha Mweka Hazina na
msaidizi wake. Masharti ya kufungua Akaunti ya Ukoo wa Kivenule yamebainishwa
kama ifuatavyo:
a).
Umoja
wa Ukoo wa Kivenule utakuwa na Akaunti itakayokuwa inahifadhi fedha pamoja na
michango mbalimbali inayochangwa na ndugu/wanaukoo;
b). Katika kufungua Benki Akaunti, wahusika
wataambatanisha Muhtasari wa Kikao kilichofanyika kubainisha dhumuni/lengo la
kufungua akaunti;
c).
Barua
ya Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji; na
d). Saini mbili (2) hadi tatu (3) za Viongozi
wa Ukoo wa Kivenule.
6.0
KUIDHINISHA MATUMIZI YA FEDHA ZILIZOPO BENKI
(i).
Katiba
ya UMOJA WA UKOO WA KIVENULE
inabainisha wazi idadi ya wajumbe watakaoidhinisha fedha za matumizi ya Kamati
ya Ukoo.
a).
Kutakuwa
na Wajumbe Sita (6)
wa Kamati Kuu ya Ukoo wa Kivenule watakaoidhinisha kuchukuliwa fedha kwa ajili
ya matumizi ya kiofisi; na
b). Matumizi makubwa yataidhinishwa na Kamati
Kuu ya Ukoo wa Kivenule pamoja na Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Kivenule.
6.1
MATUMIZI YA FEDHA ZA UMOJA WA UKOO WA KIVENULE
(i).
Katiba
ya UMOJA WA UKOO WA KIVENULE
inabainisha wazi kuhusu matumizi ya fedha na michango mbalimbali ya
ndugu/wanaukoo kama inavyoainishwa hapa chini:
a).
Kuendesha
Vikao vya Kamati Kuu, Kamati Ndogo pamoja na Mkutano Mkuu wa Ukoo;
b). Kuendesha vikao vya kawaida na vya
dharura vya Ukoo;
c).
Kununulia
vifaa vya kuendeshea shughuli za kiofisi;
d). Kulipia kodi ofisi;
e).
Kugharamia
safari za kiofisi kwa viongozi wa Ukoo;
f).
Kugharamia
chakula na malazi kwa viongozi wa Ukoo ambao watakuwa wamesafiri kikazi nje ya
makazi yake;
g). Kusaidia katika kutatua matatizo
mbalimbali yanayoupata ukoo mfano misiba, njaa na ugonjwa;
h). Kusaidia kuinua Elimu kwa ndugu/wanaukoo
ambao wamethibitishwa hawana uwezo na Kamati ya Mipango na Maendeleo; na
i).
Kutoa
motisha kwa ndugu/wanaukoo watakaouletea sifa Ukoo wa Kivenule.
7.0
MKUTANO MKUU WA UKOO
a).
Mkutano
Mkuu wa Ukoo wa Kivenule ndiyo wenye mamlaka yote yanayohusu UMOJA WA UKOO WA KIVENULE na utafanyika
mara moja kila mwaka;
b). Utahudhuriwa na ndugu/wanaukoo wote wa
Ukoo wa Kivenule;
c).
Wajumbe
wa mkutano huo ni ndugu/wanaukoo wote wa Ukoo wa Kivenule;
d). Kazi ya Mkutano Mkuu wa Ukoo ni:
(i).
Kuipokea,
kuisoma na kuipitisha Ripoti ya Mwaka ya Ukoo kuhusiana na Mipango na Maendeleo
ya Ukoo; pamoja na Ripoti ya Fedha kuhusiana na Mapato na Matumizi ya mwaka
uliopita.
(ii).
Kuidhinisha
na Kupitisha Mapato na Matumizi ya Fedha za Michango.
(iii).
Kusoma
Bajeti ya Umoja wa Ukoo wa Kivenule ya Mwaka wa Fedha.
(iv).
Kupitia
Maazimio na Mapendekezo ya Kamati Kuu ya Ukoo na kuyapitisha.
(v).
Kupokea
Ripoti ya Kamati ya Utendaji ya Umoja wa Ukoo.
(vi).
Kuunda
Kamati mbalimbali za Umoja wa Ukoo wa Kivenule kama kuna haja ya kufanya hivyo.
(vii). Kutathmini Utendaji wa Kamati mbalimbali
za Ukoo.
(viii).
Kufanya
Uchaguzi wa Viongozi wa Ukoo kama kutakuwa na haja ya kufanya hivyo.
(ix).
Kuwasomea
wanaukoo Taarifa ya Mipango na Maendeleo kwa mwaka ujao.
(x).
Kutaja
tarehe ya Mkutano Mkuu wa Ukoo mwingine.
(xi).
Kuadabisha
viongozi watakaokiuka taratibu za uongozi.
7.1
KAMATI KUU YA UKOO
a).
Kutakuwa
na vikao vinne (4) vya Kamati Kuu ya Ukoo kwa Mwaka.
b). Kamati Kuu ya Ukoo inawajumuisha
Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina pamoja na Wawakilishi
wote katika Umoja wa Ukoo wa Kivenule.
c).
Ili
kikao cha Kamati Kuu kifanyike inabidi kihudhuriwe na theluthi mbili ya wajumbe
wote.
d). Kazi ya Kikao cha Kamati Kuu ya Ukoo ni
pamoja na:
(i).
Kupanga
Ajenda za Mkutano Mkuu wa Ukoo.
(ii).
Kujadili
na kutafutia ufumbuzi matatizo yanayojitokeza katika Ukoo.
(iii).
Kupendekeza
viwango vya michango.
(iv).
Kutekeleza
majukumu yaliyoagizwa na Mkutano Mkuu wa Ukoo au yanayojitokeza.
(v).
Kuhimiza
ulipaji wa michango na kuiwakilisha.
(vi).
Kutoa
taarifa katika Mkutano Mkuu wa Ukoo kuhusiana na Shughuli za Maendeleo katika
Ukoo.
(vii). Kuhakiki Mapato na Matumizi ya Fedha.
(viii).
Kutengeneza
mpango wa kazi wa kila mwaka wa shughuli za maendeleo ya Ukoo.
(ix).
Kutengeneza
Bajeti ya Ukoo kwa kusaidiana na Kamati ya Mipango na Maendeleo; na Kamati ya Mahesabu na Fedha.
(x).
Kalenda
ya Kazi
7.2
KAMATI NDOGO MBALIMBALI ZA UKOO
a).
Kamati
Kuu ya Ukoo wa Kivenule itakuwa na Kamati Ndogo mbalimbali ili kurahisisha
utendaji wa shughuli zake za kila siku. Kamati hizo zimebainishwa hapa chini
kama ifuatavyo:
(i).
Kamati
ya Utendaji;
(ii).
Kamati
ya Mipango na Maendeleo;
(iii).
Kamati
ya Maafa na Matatizo mbalimbali yanayoupata ukoo;
(iv).
Kamati
ya Nidhamu na Maadili;
(v).
Kamati
ya Mahesabu na Fedha;
b). Kazi ya Kamati Ndogo Ndogo za Ukoo
(i).
Kuisaidia
Kamati Kuu kutekeleza majukumu yake;
(ii).
Kuripoti
kwa Kamati Kuu mipango mbalimbali ya maendeleo;
(iii).
Kuandaa
Bajeti ya Kamati Kuu na Umoja wa Ukoo wa Kivenule;
(iv).
Kuripoti
kwa Kamati Kuu hali ya Nidhamu, Maadili na Mahusiano katika ukoo; na
(v).
Kuishauri
Kamati Kuu.
8.0
SIFA ZA KIONGOZI
a).
Kiongozi
wa UMOJA WA UKOO WA KIVENULE
anatakiwa awe na sifa zifuatazo:
(i).
Awe
mwaminifu na mwadilifu ndani ukoo na nje ya ukoo;
(ii).
Awe
na ufahamu wa mambo mbalimbali;
(iii).
Awe
na moyo wa kujituma na kujitolea;
(iv).
Awe
mbunifu na mwenye maarifa katika utendaji wa kazi zake;
(v).
Awe
mwepesi kushaurika na kushauri;
(vi).
Aiheshimu
jamii inayomzunguka, ndugu/wanaukoo wa Ukoo wa Kivenule;
(vii). Atoe ushirikiano kwa viongozi wenzake
pale inapobidi kufanya hivyo;
(viii).
Akubali
kukosolewa;
(ix).
Asitoe
wala kupokea rushwa;
(x).
Apende
kujenga hoja (nguvu ya hoja) na si kutumia hoja ya nguvu;
8.1
WAJIBU WA VIONGOZI
a).
Kiongozi
wa UMOJA WA UKOO WA KIVENULE anatakiwa
kutekeleza wajibu wake kama ifuatavyo:
(i).
Afanye
kazi kwa mujibu wa KATIBA YA UMOJA WA
UKOO WA KIVENULE;
(ii).
Ahudhurie
vikao mbalimbali vinavyoitishwa na viongozi wa ukoo;
(iii).
Akubaliane
na maamuzi ya Mkutano Mkuu wa Ukoo na Kamati Kuu;
(iv).
Atoe
ushirikiano kwa viongozi wenzake pale inapobidi kufanya hivyo;
(v).
Atekeleza
wajibu wake pasipo msukumo au kusukumwa;
(vi).
Asipokee
au kutoa rushwa;
(vii). Aheshimu jamii inayomzunguka,
ndugu/wanaukoo wa Ukoo wa Kivenule;
(viii).
Awe
mbunifu na mwenye maarifa katika utendaji wa kazi zake;
(ix).
Awe
na ufahamu wa mambo mbalimbali;
(x).
Apende
kujenga hoja (nguvu ya hoja) na si kutumia hoja ya nguvu;
8.3
NAFASI ZA UONGOZI
a).
Kutakuwa
na nyadhifa kadhaa za uongozi katika UMOJA
WA UKOO WA KIVENULE, ambapo viongozi wake watapatikana kwa kuchaguliwa au
kuteuliwa katika Mkutano Mkuu wa Ukoo au Vikao vya Kamati Kuu ya Ukoo. Nyadhifa
hizo zimebainishwa hapa chini:
(i).
Mwenyekiti;
(ii).
Makamu
wa Mwenyekiti;
(iii).
Katibu
Mkuu;
(iv).
Katibu
Msaidizi;
(v).
Mweka
Hazina;
(vi).
Mweka
Hazina Msaidizi;
(vii). Walezi Watatu (3);
(viii). Viongozi
toka Kifungu [i – vii] Wanaunda Kamati Kuu; na
(ix).
Viongozi
wa Kamati Ndogo za Ukoo.
9.0
MWENYEKITI
(i).
Mwenyekiti
wa UMOJA WA UKOO WA KIVENULE
atachaguliwa na Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Kivenule. Aidha anaweza kupendekezwa na
Kamati Kuu na jina lake kupitishwa na Mkutano Mkuu wa Ukoo kwa ridhaa yao;
(ii).
Mwenyekiti
wa Ukoo atadumu katika uongozi kwa kipindi cha miaka mitatu (3) toka
kuchaguliwa;
(iii).
Uchaguzi
wa Mwenyekiti utafanywa kwa kura za siri;
(iv).
Atatangazwa
kuwa Mwenyekiti halali kama atapata kura zaidi ya theluthi mbili za
wanachama/wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Ukoo.
(v).
Atawajibika
kwa wanaukoo wote.
9.1
KAZI ZA MWENYEKITI
(i).
Atakuwa
Msemaji Mkuu wa shughuli mbalimbali katika Ukoo;
(ii).
Atasimamia
Vikao vyote, Mkutano Mkuu wa Ukoo na Kamati Kuu ya Ukoo;
(iii).
Atakuwa
na Kura ya Upendeleo wakati wa kufikia maamuzi fulani. Upendeleo huo ulete
faida na uwe wa busara na maslahi katika ukoo; na
(iv).
Mhakiki
na muidhinishaji wa matumizi madogo endapo ataridhika na kukubaliana na maombi.
9.2
UKOMO WA UONGOZI
a).
Mwenyekiti
wa UMOJA WA UKOO WA KIVENULE atakoma
katika nafasi hiyo ya uongozi endapo ataguswa/kukumbwa na mojawapo ya sababu
zifuatazo:
(i).
Kwisha
kwa muda wa uongozi ambao ni vipindi viwili vya miaka mitatu (3);
(ii).
Kufariki;
(iii).
Kuachishwa;
(iv).
Akishindwa
kuwajibika; na
(v).
Akiugua/akipata
ugonjwa utakomfanya ashindwe kufanya kazi kama inavyostahili.
(vi).
Akishindwa
kuhudhuria vikao vitatu mfululizo bila sababu ya msingi.
10.0
KATIBU MKUU
(i).
Jina
la Katibu Mkuu wa UMOJA WA UKOO WA
KIVENULE atapendekezwa na Kikao cha Kamati Kuu na kuchaguliwa na Mkutano
Mkuu wa Ukoo wa Kivenule;
(ii).
Katibu
Mkuu wa Ukoo atadumu katika nafasi ya uongozi kwa kipindi cha miaka mitatu toka
kuchaguliwa;
(iii).
Katibu
Mkuu atachaguliwa kwa kura za siri na wanaukoo wote.
(iv). Atatangazwa kuwa Katibu halali kama
atapata zaidi ya theluthi mbili ya kura za wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Ukoo; na
(v).
Atawajibika
kwa wanaukoo wote.
10.1
KAZI ZA KATIBU MKUU
a).
Katibu
Mkuu wa UMOJA WA UKOO WA KIVENULE
atakuwa na majukumu yafuatayo:-
(i).
Ataitisha
Vikao vya Kamati Kuu na vya Wanaukoo;
(ii).
Atatunza
Nyaraka na Majarida ya Vikao;
(iii).
Atakuwa
mwandishi mkuu wa minitisi za vikao vya Kamati Kuu na Mkutano Mkuu wa Ukoo;
(iv).
Atawajibika
kwa wanaukoo wote; na
(v).
Muidhinishaji
wa matumizi madogo na kuhakiki mapato.
10.2
UKOMO WA UONGOZI
a).
Katibu Mkuu wa UMOJA WA UKOO WA KIVENULE atakoma katika nafasi hiyo ya uongozi
endapo ataguswa/kukumbwa mojawapo ya sababu zifuatazo:
(i).
Kuisha
kwa muda wa uongozi ambao ni vipindi viwili vya miaka mitatu (3);
(ii).
Kufariki;
(iii).
Kuachishwa;
(iv).
Akishindwa
kutoa taarifa sahihi mbele ya Kamati Kuu na Mkutano Mkuu wa Ukoo;
(v).
Akishindwa
kuwajibika kiutendaji;
(vi).
Akiugua/akipata
ugonjwa utakaomfanya ashindwe kufanya kazi kama inavyostahili;
(vii). Asipohudhuria vikao vitatu mfululizo bila
kutoa taarifa.
10.3
Mwenyekiti na Katibu
Mkuu wakishindwa kuwajibika kiutendaji kama ilivyobainishwa kwenye
Katiba ya UMOJA WA UKOO WA KIVENULE,
Makaimu wao watachukua nafasi zao na
kufanya kazi mpaka tarehe ya kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Ukoo.
11.0
MTUNZA HAZINA
(i).
Mweka
Hazina wa UMOJA WA UKOO WA KIVENULE
atachaguliwa na Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Kivenule. Aidha anaweza kupendekezwa na
Kikao cha Kamati Kuu na kupitishwa na Mkutano Mkuu wa Ukoo;
(ii).
Mweka
Hazina wa Ukoo atadumu katika nafasi ya uongozi kwa vipindi viwili vya miaka
mitatu toka kuchaguliwa;
(iii).
Mweka
Hazina atachaguliwa kwa kura za siri na wanaukoo wote.
(iv). Atatangazwa kuwa Mweka Hazina halali kama
atapata zaidi ya theluthi mbili ya kura za wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Ukoo; na
(v).
Atawajibika
kwa wanaukoo wote.
11.1
KAZI ZA MWEKA HAZINA
a). Mtunza hazina atakuwa na
wajibu ufuatao:-
(i).
Kutunza
fedha zote za wanachama (Wanaukoo) Benki, kwenye Akaunti ya Umoja wa Ukoo na
pia kwa maandishi.
(ii).
Kutunza
michango ya viingilio, ya kila mwezi na michango dharura.
(iii).
Kutoa
taarifa ya Mahesabu na Fedha kwenye Kamati Kuu ya Ukoo na Mkutano Mkuu wa Ukoo.
(iv).
Kusoma
taarifa ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwenye Kamati Kuu ya Ukoo na Mkutano
Mkuu wa Ukoo.
(v).
Kuidhinisha
malipo madogo pale inapohitajika kufanya hivyo.
11.2
UKOMO WA UONGOZI
a). Mweka Hazina wa UMOJA WA UKOO
WA KIVENULE atakoma katika nafasi hiyo ya
uongozi endapo ataguswa/kukumbwa
na mojawapo ya sababu zifuatazo:
(i).
Kuisha
kwa muda wa uongozi ambao ni vipindi viwili vya miaka mitatu (3);
(ii).
Kufariki;
(iii).
Kuachishwa;
(iv).
Akishindwa
kutoa taarifa sahihi kuhusiana na Mapato na Matumizi ya Fedha mbele ya Kamati
Kuu ya Ukoo na Mkutano Mkuu wa Ukoo;
(v).
Akishindwa
kuwajibika kiutendaji;
(vi).
Asipohudhuria
vikao vitatu mfululizo bila kutoa taarifa; na
(vii). Akibainika na ubadhirifu wa fedha,
michango au mali ya ukoo.
(viii).
Akiugua/akipata
ugonjwa utakaomfanya ashindwe kufanya kazi kama inavyostahili.
12.0
TANBIHI
Fedha za UMOJA WA UKOO WA KIVENULE zinazopatikna kutokana na michango ya
wanaukoo, dharura na vyanzo vyovyote vya mapato, zitatunzwa benki katika
Akaunti ya Umoja wa Ukoo wa Kivenule. Mtunza Hazina hatatakiwa kubaki na fedha
zaidi ya Tshs. 50,000/= ofisini kwake. Matumizi yoyote ya fedha iliyopo benki
katika Akaunti ya Umoja wa Ukoo wa Kivenule, yataidhinishwa na Mwenyekiti,
Katibu na Mweka Hazina pamoja na Wajumbe Wawili (2) wa Kamati Kuu kwa
maandishi.
Taarifa za matumizi ya michango
mbalimbali itatolewa na Mweka Hazina katika Vikao ya Kamati Kuu na Mkutano Mkuu
wa Ukoo.
Pia, Katiba ya UMOJA WA UKOO WA KIVENULE inatoa fursa kwa viongozi wa Ukoo
kuitisha kikao cha dharura cha wanaukoo wakati wowote.
No comments:
Post a Comment