MKUTANO
MKUU WA KWANZA WA MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU
WA UKOO WA KIVENULE – DESEMBA 17 – 18, 2005
Mahali
ulipofanyika: Kidamali, Iringa
Tarehe: 07 Mei, 2005
Muda: 9:30 Alasiri
A. WALIOHUDHURIA
KWENYE MKUTANO MKUU WA KWANZA WA MAANDALIZI YA
MKUTANO MKUU WA UKOO
1.
Christian
J. Kivenule 0744
2. Justin D. Kivenule 026
2702590
3. George S. Kivenule
4. Augen W. Kivenule 0748
859936
5. Mateso W. Kivenule
6. Izabela Mgimwa
7. Balunaba P. Kivenule
8. Galino P. Kivenule
9. Aginesy S. Kivenule
10. Henli Mgimba
11. Baraka W. Kivenule
12. Lehm P. Kivenule
13. Malino W. Kivenule
14. Kaini E. Kivenule
15. Danieli S. Kivenule
16. Kalolina S. Kivenule
17. Jahneti D. Kivenule
18. Nesya S. Kivenule
19. Christina P. Kivenule
20. Mama Ameli Msigala
21. Faustino S. Kivenule
22. Adam A. Kivenule 0741
270364/0748270 364
23. Jovin. D. Kivenule
24. Donald P. Mhapa 0748
481954
25. Poziano S. Kivenule
26. Jonsiya Mkwambe
B. AGENDA ZA MKUTANO MKUU WA KWANZA WA MAANDALIZI YA
MKUTANO MKUU
1.
Kufungua
Mkutano
2. Utambulisho
3. Kuchagua Viongozi
4. Yatokanayo: Lengo Kuu la Mkutano
5. Kupitia Vifaa Mbalimbali
6. Mengineyo
7. Kufunga mkutano
C. KUFUNGUA MKUTANO
Mkutano ulianza mnamo saa 9:30 alasiri na ulifunguliwa na
Mwenyekiti wa muda Ndugu Faustin Kivenule, kwa kuwakaribisha wageni na wanaukoo
wengine, mahali ambapo mkutano ulikuwa unafanyika (Nyumbani kwa Ndg. Daniel
Kivenule). Aliwaombe wajumbe wajiandikishe kwenye karatasi ya mahudhuria ili
kujua idadi ya wajumbe wanaohudhuria mkutano.
Pia alitumia fursa hii
kuwakaribisha wajumbe wageni toka Dar es Salaam ambao walikuwa wamekuja na
shughuli moja tu ya kuhamasisha maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Ukoo hapo tarehe
17 – 18 Desemba, 2005. Wajumbe hao ni Ndugu Christian Kivenule ambaye ni
Mwenyekiti na Ndugu Adam Kivenule ambayo ni viongozi wa Kamati ya Maandalizi ya
Mkutano Mkuu kwa upande wa Dar es
Salaam.
Baada ya kuwakaribisha wageni,
Mwenyekiti wa Muda (Faustino) alichukua fursa hiyo kusoma ajenda za mkutano huo
wa maandalizi ya mkutano mkuu. Baada ya kuzisoma aliuliza wajumbe kama wanazikubali? Wote kwa ujumbe walisema wanakubaliana
nazo.
D. UTAMBULISHO
Utambulisho ulifanyika kwa kila
mjumbe kujitambulisha mwenyewe mbele ya wajumbe wa mkutano. Kila mjumbe
(mwanaukoo) alisimama na kujitambulisha akitaja majina yake mwenyewe na ya
wazazi wake, Bibi au Babu zake. Hii ilifanyika kwa wajumbe wote waliokuwepo
kwenye mkutano.
E. KUCHAGUA VIONGOZI
Hatua hii ilikuwa ni ya muhimu sana kwenye mkutano huo
kwani viongozi ambao walichaguliwa walikuwa walengwa na majukumu mazito ambayo
yalikuwa mbele yao.
Ndugu Adam Kivenule toka Dar es Salaam
alisimamia zoezi zima la uchaguzi wa viongozi. Kazi ya kwanza ilikuwa ni
kuchagua Mwenyekiti, Katibu na Mweka Hazina. Hatua ya pili ilikuwa ni kuchagua
Makamu wa Mwenyekiti, Katibu Msaidizi na Washauri wa Kamati.
Uchaguzi wa viongozi ulifanyika
kwa kuwauliza wajumbe kupendekeza majina ya wagombea uongozi na pia kuwauliza kama wanakubaliana naye. Uchaguzi haukuwa wa kupiga kura
moja baada ya nyingine, ila ulifanyika kwa kupata kura za jumla toka kwa
wajumbe. Waliulizwa kama wanakubali kupendekezwa kwake au wanakataa. Majibu ya
wajumbe wote yalikuwa ndiyo kwa kila mjumbe aliyependekezwa kushika nafasi
fulani kwenye uongozi.
Baada ya kumaliza kufanya
uchaguzi wa viongozi, Ndugu Adam Kivenule alitangaza matokeo ya uchaguzi kama ifuatavyo: Nafasi za uongozi wa kuunda Kamati ya
Kidamali ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Ukoo zimechukuliwa na hawa wafuatao:
1.
Mwenyekiti Faustino Kivenule
2. Makamu
wa Mwenyekiti Aujen Kivenule
3. Katibu Jovin Kivenule
4. Katibu
Msaadizi Carolina Kivenule
5. Mweka
Hazina Justin Kivenule
6. Washauri Ponsian Kivenule
7. Washauri Pyela Kivenule
8. Washauri Donati Mhapa
F. CHIMBUKO LA MKUTANO
Mwenyekiti alianza
kuwaeleza wajumbe kwa kusema kuwa Wazo la Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Kivenule,
lilibuniwa na Ndugu Faustin Kivenule ambaye ni Baba yake mdogo pamoja na yeye
mwenyewe Christian Kivenule, alipokuwa likizo kijijini, Kidamali mwishoni mwaka
jana (2004). Mtu wa tatu kulipata wazo alikuwa ni ndugu Adam Kivenule,
anayeishi Ubungo, mjini Dar es Salaam kutoka kwa Christian Kivenule mwaka huo
huo wa jana.
Mambo mbalimbali
yalijitokeza kutokana na wazo (kusudio) la kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, Desemba 17-18, 2005 kijijini
Kidamale. Kati ya mambo hayo ya msingi
ni pamoja na suala nzima la mahusiano ndani ya wana ukoo, suala la elimu, suala
la UKIMWI, kufahamiana na kuujua ukoo kwa ujumla, kufanya senza ili kujua idadi
ya ndugu na mahali wanapoishi pamoja na mambo mbalimbali ambayo tunayategemea
yatajitokeza.
Suala la Ukoo pamoja
na Mahusiano baina ya wanandugu ndani ya ukoo, suala la elimu na gonjwa hatari
la UKIMWI ni mambo ya msingi pia ni kiini na changamoto ya mambo mengi ambayo
yatajitokeza katika mkutano huo mkuu. Mahusiano duni baina ya wana ndugu,
kukosa kwa ushirikiano katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo, kiuchumi na
kijamii, matatizo ya kifamilia na kiukoo ni kati ya masuala msingi
yaliyofikiriwa sana
kabla ya kuletwa kwa wazo hili katika kikao hiki.
Mwelekeo wa ukoo wa
Kivenule kuhusiana na suala nzima la Elimu hasa katika dunia hii ya Utandawazi
(Globalization) ambapo dunia imekuwa kama kijiji kisicho na mipaka na kila mtu
anaruhusiwa kuingia na kutoka, kuongezeka kwa viwanda vinavyotumia teknolojia
ya hali ya juu, kuongezeka kwa teknolojia ya mawasiliano, kupanuka na kujengeka
kwa miji, pamoja na soko huria. Mambo yote haya ndiyo yanayoweza kuonyesha
mustakabali na nafasi ya ukoo wa Kivenule kwa maisha ya baadaye. Ilionekana
kuwa ukoo wetu upo nyuma sana
katika suala nzima la elimu, hii linajidhihirisha kutokana na kuwa na ndugu
wachache sana
ambao wameweza kupata elimu kwa kiwango kinachostahili. Hii ni hatari kwa
sababu tunajenga ukoo tegemezi ambayo baadaye utakosa mwelekeo. Mabadiliko ya
Sayansi na Teknolojia yanayojitokeza kila kukicha yanaibadili dunia na hivyo
kutulazimisha nasi katika ukoo wa Kivenule kubadilika. Matumizi ya teknolojia
ya habari na mawasiliano katika simu za mikononi, computer, radio na satellite
ni changamoto kwetu.
Maambukizo ya
ugonjwa wa UKIMWI ambayo kwa kiasi kikubwa yameathiri familia nyingi zikiwemo
familia zetu sisi wana ukoo, yanapaswa kutopuuzwa bali kuwekewa mikakati
madhubuti. Ufahamu kuhusiana na gonjwa lenyewe livyoenea na madhara yake katika
jamii, njia mbadala za kujilinda na maambukizi ya ugonjwa wenyewe pamoja na
kuitikia mialiko mbalimbali ya wanajamii wanaopambana na janga hili ni mambo ya
msingi sana
ambayo yatajadiliwa kwenye mkutano huo.
Ilipendekezwa kuwa,
wakati wa mkutano huo kutakuwa na nafasi kutoa uzoefu katika mambo mbalimbali
ya kitaalum pamoja na mada ambazo tutazijadili kwenye agenda za mkutano huu wa
leo, nazo zitawasilishwa kwenye mkutano huo.
Maandalizi ya
mkutano mkuu wa ukoo yameanza mapema ili kutupa nafasi kubwa zaidi ya kujadili,
kuandaa pamoja na kuwasilisha michango yetu ndani ya wakati unaotakiwa.
Vikao vitatu vimeshafanyika
chini ya Kamati ya Maandalizi ya Dar es Salaam.
MCHANGO
TOKA KWA WAJUMBE
Jovin Kivenule, ambaye ni Katibu wa Kamati ya
Maandalizi, ameukubali mkutano huo na akasema ni muda muafaka kuwa na kitu kama hicho. Akawaomba wana ndugu kuwa na ushirikiano katika
jukumu hili.
Donati Mhapa
·
Mawazo
haya yalishakuwepo muda mwingi. Ni vizuri kuwa na kitu kama
hiki. Ni vizuri kujuliana hali, kushirikiana na kusaidiana baina ya wana ndugu.
·
Jambo
lingine la msingi ni kushirikiana katika matatizo na raha. Kupeana mialiko
katika kupata chakula, sherehe, shughuli za mashamba nk. Kumbukumbu zinaonyesha
kuwa enzi za kule Mlafu ndugu tuliishi katika maadili ya hali juu sana. Tulishirikiana
katika milo (chakula), katika shida na raha na tukaishi maisha mazuri.
·
Mawazo
ya mtu kuhifadhi fedha isiyo tatizo. Cha msingi ni kuwa na imani na viongozi
tuliowachagua ili azma ya mkutano ifikie kilele.
·
Kila
anayesoma siyo lazima afanye kazi ya kuajiliwa. Ila inaongeza ufahamu (kupanua
mawazo). La muhimu ni kumwezesha mtu yeyote anayefaulu au kuonyesha ari ya
kujiendeleza.
·
Naunga
mkono mada zote zilizopendekezwa.
·
Anashukuru
kwa kazi nzuri inayofanywa na Kamati ya Dar
es Salaam na anatumaini pia kwa upande wao kazi
itakuwa nzuri.
·
Anashukuru
kuwa kiwango cha mchango ni kidogo na pia kulifanyia kazi suala hili. Pia
ukumbi wa Justin ni muhimu kwa shughuli nyingine za kibiashara labda pia tuangalie suala la kumbi sehemu
nyingine.
·
Suala
la malazi ni msingi sana
na pia kuna umuhimu wa kujua idadi ya wageni watakaokuja kwenye mkutano.
Faustin Kivenule
Ukoo wetu umegawanyika kwa
kiwango cha hali ya juu sana.
Kuna korongo limejitokeza katika ukoo wetu ambalo linazidi kurefuka kadri ya
siku zinavyozidi kwenda mbele. Ni korongo refu ambalo linatutenga wanaukoo na
kutugawa katika makundi tofauti kiasi cha kutisha. Lazima kuwe juhudi mahsusi
za kulifukia shimo hilo.
Jitihada mojawapo ambayo tumeamua kuichukua ni kuandaa Mkutano Mkuu pamoja na
mambo mengine, kuyajadili mambo mbalimbali ambayo yamekuwa ni chanzo au chachu
ya kurefusha korongo ambalo tayari limeshajengeka. Korongo limeshajengeka na
limekuwa likikua mwaka baada ya mwaka.
Sasa tufukie.
Tulichukulie kwa umakini mkubwa
wazo hili. Suala la ushirikiano, kujaliana, kurudisha mwelekeo mzuri wa familia
hii ni mambo ya msingi sana
kwa maisha yetu ya kila siku.
Shangazi Agnes
·
Kumbukumbu
za fedha zilizopita zinaonyesha kuwa huko nyumba hakukuwa na utunzaji mzuri wa
fedha kwani hata zile tulizozikusanya hazikuonekana. Japo Ndugu Daniel Kivenule
alisema baadhi ya fedha zilitumika kumtibu Shangazi (Khadija) wakati wa ugonjwa
wake.
Justin Kivenule
·
Umuhimu
wa elimu ni pamoja na kujiajiri ili kujikomboa kiuchumi. Inasaidia kila mahali.
·
Je
malazi na ukumbi viko kwenye bajeti. Ni muhimu vikawepo kwenye bajeti ila
tusipate shida siku za mbeleni.
George Kivenule
·
Mada
ya Dini katika Ukoo ingeongezwa. Hii itasaidia Ukoo kuwa na imani na kumwogopa.
Mungu. Dini inasaidia kuimarisha mahusiano baina ya ndugu na majirani. Inazuia
utengano. Inapendekeza kufariji, kusaidia, ushirikiano na nk.
·
Upinzani
hujitokeza katika harakati za maendeleo. Mfano katika jambo hili lazima
tutapata wapinzani. Cha msingi ni kuwa imara katika maamuzi na utekelezaji wa
shughuli mbalimbali.
Aujen Kivenule
·
Suala
la michango halina tatizo. Kiwango kilichopendekezwa hakina tatizo na anadhani
wengi wetu tutamudu kulipa.
·
Je
ni wageni wangapi watakuja? Tunapendekeza kuwa na wastani wa ndugu 200. kwa
upande wa wageni toka nje ya Kidamali labda wanaweza kufikia 50 au zaidi.
Kaini Kivenule
Kadi ziwahi kusambazwa ili
kuwapa ndugu muda zaidi wa kujikusanya na kutoa michango yao. Ni bora watu wakasambaziwa kadi mapema
ili wajue watajibana vipi ili kuweza kutoa michango.
KUHUSU RATIBA
Ratiba hii tunayoiangalia
ilitengenezwa mwanzoni kabisa wakati bado tunafanya maandalizi ya shughuli
mbalimbali ambazo zitajitokeza kwenye mkutano mkuu. Hapa mwanzo mada zilikuwa
tatu, baadaye tukaongeza zikafika nne na leo ninyi mmeongeza mada moja na
zimefika mada tano. Cha msingi ninachoweza kusema ni kuwa tutafanyia
marekebisho Ratiba na kuzijumuisha mada zote ndani yake. Halafu tutazituma
pamoja na mambo mengine.
Mkutano lazima uwe na watu wa
kuuongoza (MCs). Tupendekeze kila Kamati ichague mtu mmoja ambaye atasaidiana
na mwezake katika kuuongoza mkutano.
BAJETI NA VIFAA MBALIMBALI VILIVYOPENDEKEZWA
Vifaa vilivyopendekezwa kwenye
mkutano huo mkuu vilipitiwa na wajumbe wa mkutano huo ili kujua mapungufu na
kupata fursa ya kufanya marekebisha pale panapostahili. Marekebisho hayo
yaligusa vifaa pamoja na bajeti ya shughuli nzima ya maandalizi ya Mkutano Mkuu
wa Ukoo wa Kivenule hapo tarehe 17 – 18 Desemba 2005.
MAMBO MBALIMBALI
YALIYOJADILIWA KAMA SEHEMU YA MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA UKOO
A: Mambo ya
Muhimu ya Kuwezesha Mkutano Kufanikiwa
1.
Malazi
: Kwa Wageni wote watakaokuja kwenye Mkutano Mkuu wa Ukoo Kidamali.
2.
Usafiri:
Toka Iringa Mjini mpaka Kidamali, Iringa na kutoka Kidamali mpaka Iringa Mjini
3.
Chakula:
Kwa siku za mkutano na kabla ya mkutano
4.
Vinywaji:
Kwa siku za mkutano na kabla ya mkutano
·
Pombe
ya Asili
·
Pombe
ya Kisasa
5.
Burudani
·
Muziki
wa Asili
·
Muziki
wa Kisasa
6.
Makisio
(Makadirio) ya Washiriki wa Mkutano (Tunategemea kuwa na Wanaukoo takribani
200 watakaohudhuria mkutano)
7.
Mchango
wa Kufanikisha Mkutano
·
Waishio
Mijini (Kima cha chini kimependekezwa Tsh. 15,000/- lakini njia ni nyeupe kwa
wale ambao wataona kuna haja ya kuchangia kwa hali na mali ili kuweza kufanikisha mkutano huo)
·
Waishio
Vijijini (Kima cha chini kimependekezwa Tsh. 5,000/- pia wanashauriwa kuwa
wanaweza kutoa kitu kingine chochote chenye thamani kama
kuku wawili, mbuzi au vinginevyo)
8.
Mahali
pa kufanyia Mkutano: Kuna kumbi mbili zimependekezwa; Kwa Sanga ndiyo umepewa
asilimia kubwa. Kwenye ukumbi wa Justin kuna watu wanazungumzia imani zao
zinawasuta kufika mahali pale. Pia kibiashara inaweza kumuathiri japo nadhani
siyo suala la msingi sana.
Majukumu ya ukumbi litashughulikiwa na Kamati ya Kidamali. Lakini maoni na
mawazo yanakaribishwa kwa ajili mashauriano zaidi kuhusu sehemu ambayo
watadhani inafaa zaidi.
Kuundwa kwa Kamati za Maandalizi
1. Kamati
ya Dar es Salaam
inaongozwa na:
Kamati ya Dar es Salaam na mikoa ya karibu
inayoshirikiana na Kamati ya Kidamali katika kufanya maandalizi ya Mkutano Mkuu
wa Ukoo wa Kivenule ipo chini ya viongozo wafuatao:
1.
Mwenyekiti: Christian Kivenule
2. Makamu Mwenyekiti: Athuman Mtono
3. Katibu: Adam Kivenule
4. Mweka Hazina: Innocent Kivenule
5. Mshauri: Edgar Kivenule
2. Kamati
ya Kidamali inaongozwa na:
Kamati ya Kidamali inayoshirikiana na
Kamati ya Dar es Salaam na Mikoa ya karibu katika kufanya maandalizi ya Mkutano
Mkuu wa Ukoo wa Kivenule ipo chini ya viongozo wafuatao:
1.
Mwenyekiti: Faustin Kivenule
2.
Makamu
Mwenyekiti: Aujen Kivenule
3.
Katibu: Jovin
Kivenule
4.
Katibu
Msaidizi: Caroline Kivenule
5.
Mweka
Hazina: Justin Kivenule
6.
Washauri: Pyela Kivenule
Donati Mhapa
Daniel Kivenule
Kamati hii itashughulikia majukumu yote ya maandalizi
ya mkutano mkuu na shughuli zote za maandalizi ndani ya Kidamali na vijiji vya
karibu. Itasimamia usambazaji wa barua za mialiko pamoja na za michango
mbalimbali, usambazaji wa kadi za michango, ukusanyaji wa michango pamoja na
kutekeleza majukumu mengine ambayo Kamati hizi mbili zitakuwa zimeshauriana.
Kamati hii itafanya kazi chini ya uongozi ulioundwa na kutekeleza majukumu
waliyokubaliana katika vikao vyao.
B: MAJUKUMU YA KAMATI ZOTE MBILI
1.
Kusambaza
barua za mwaliko pamoja na maombi mengine kama
michango nk. Kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa Ukoo pale zitakapohitajika.
2.
Kuratibu
shughuli zote za Ukusanyaji wa Michango
3.
Kuandaa
mikutano mbalimbali za maandalizi kwa kushirikisha ndugu mbalimbali wanaoishi
sehemu tofauti. Mfano kwa Dar es
Salaam kuna ndugu toka Kidamale, Ilole, Nduli na Ilula
nk.
4.
Kuhamasisha
Wanaukoo waishio kijijini Kidamali, Ilole, Nduli, Ilula na sehemu nyinginezo
hapa Tanzania
kuhusiana na umuhimu wa kuwepo kwa mkutano huo pia kutoa ushirikiano wa hali na
mali
katika zoezi zima la maandalizi.
5.
Kuandaa
Mpango wa Kazi wa Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Ukoo
- Kufanya vikao mbalimbali vya Kamati ya Maandalizi vitakavyoshirikisha Kamati zote mbili ya Kidamali na Dar es Salaam.
- Kuwajulisha walengwa (Ndugu) umuhimu wa kujali muda wa kukusanya michango. Kwa mfano kuwaeleza Mwisho wa Ukusanyaji wa Michango (Mara baada ya kupata Barua na Kadi).
- Kuwashirikisha wadau wengine wasio ndugu katika kampeni za kukusanya michango. Mfano kuwaomba michango Wabunge, Madiwani, Maaskofu na watu wengine muhimu katika jamii zetu.
C: ORODHA YA UKOO WA AKINA KIVENULE WAISHIO DAR ES SALAAM
1.
Edgar
Kivenule (Mwenge Flats)
2.
Innocent
Kivenule (Ubungo Jeshini)
3.
Athuman
Mtono (Kibamba)
4.
Adam Kivenule (Ubungo Kibangu)
5.
Christian Kivenule (Matombo – Morogoro)
6.
Philemon Kivenule (Buguruni) 0744 029880
7.
Flora
Kivenule (Mabibo Sahara)
8.
Ignas
Kivenule (Tabata Shule)
9.
Sabina Mhapa (Buruguruni)
10. Mwanne Mtono (Ubungo
Kibangu)
11. Raphael Kivenule
(Mbezi – Club Oasis)
12. Monica Kivenule
(Zanaki Street)
13. Priskusi Kivenule
(Mbezi Juu)
14. Michael Mhapa (Ubungo Kibangu)
15. Regina Mapembe (Kinondoni)
16. Evaristo Mapembe
(Tabata)
17. Nuhu Mtono (Mabibo)
18. Hamidu Mtono
(Mabibo)
19. Sijali Kivenule Kisukuli
20. Alexander Nyangalima (Morogoro)
21. Flomina Kivenule (Mbezi)
22. Fred Mapembe (Tabata)
23. Thabit Mtono (Kigamboni)
D: ORODHA YA UKOO WA AKINA KIVENULE WAISHIO NJE YA DAR ES
SALAAM NA KIDAMALE
1.
Alphonce Kivenule (Ludewa)
2.
John Kivenule (Kilombero)
3.
Zavery
Kivenule (Igowole/Sadani)
4.
Lizeta
Kivenule (Dodoma)
5.
Victoria Kivenule (Dodoma)
6.
Goretha Kivenule (Mtera)
7.
Asia Kivenule (Morogoro)
8.
Irene Kivenule ( )
9.
Furaha Kivenule ( )
10. Bakita Kivenule (Mafinga)
11. Emmanuel Kivenule ( )
12. Agatha Kivenule (Dodoma)
13. Florian Kivenule (Mafinga)
E: RATIBA YA MKUTANO MKUU WA KWANZA WA UKOO WA KIVENULE
Mahali pa kufanyia Mkutano: _____________________________________
Tarehe: 17
– 18 Desemba 2005
Washiriki: Ukoo
Wote wa Kivenule na Wageni Waalikwa
Siku ya Kwanza ya Mkutano Mkuu wa Ukoo wa KIVENULE |
||
Muda
|
Shughuli/Jukumu
|
Wahusika
|
12:00–12:45
|
Wageni Wote Kuamka na Kufanya Maandalizi ya Kuingia
kwenye Mkutano
|
Wote |
12:45–1:45
|
Kupata Kifungua Kinywa
|
Wote
|
1:45 – 2:45
|
Kuwasili Mkutanoni na Kujisajili
|
Wote
|
2:45 – 3:15
|
Ufunguzi wa Mkutano na Mgeni Rasmi
|
Mgeni Rasmi
|
3:15 – 4:00
|
Utambulisho baina wa wana Ndugu
|
Wote
|
4:00 – 4:45
|
Pumziko la Chai / Kahawa/Maji
|
Wote
|
4:45 – 5:30
|
Mada ya Kwanza: HISTORIA YA UKOO |
Mtoa Mada na Mkubwa wa Ukoo |
5:30 – 6:00
|
Majadiliano katika Makundi
|
Makundi 4
|
6:00 – 6:20
|
Murejesho na Majumuisho
|
Mwezeshaji
|
6:30 – 8:00
|
CHAKULA CHA MCHANA
|
Wote
|
8:00 – 8:45
|
Mada ya Pili: MAHUSIANO BAINA YA NDUGU NDANI YA
UKOO WA KIVENULE
|
Mtoa MADA
(…………………)
|
8:45 – 9:15
|
Majadiliano katika Makundi
|
Makundi 4
|
9:15 – 9:45
|
Murejesho na Majumuisho
|
Mwezeshaji
|
9:45– 10:45
|
Pumziko la Chai/Kahawa/Maji |
Wote
|
10:45-1:30 Usiku
|
Mapumziko Marefu (Kusalimiana na Kufahamiana zaidi)
|
Ndugu na Wageni Wote
|
1:30 – 2:30
|
Chakula cha Usiku na Vinjwaji
|
Ndugu Wote
|
2:30 – 6:30
|
Burudani (Muziki wa Kisasa na Ngoma za Asili)
|
Wote
|
Siku ya Pili ya Mkutano Mkuu wa Ukoo wa KIVENULE |
||
Muda
|
Shughuli/Jukumu
|
Wahusika
|
12:00– 12:45
|
Kuamuka na Kufanya Maandalizi ya Mkutano
|
Wote |
12:45 – 1:45
|
Kifungua Kinywa
|
Wote
|
1:45 – 2:15
|
Kuwasili Mkutanoni na Kujisajili
|
Ndugu wote |
2:15 – 2:45
|
Mada Ya Tatu: ELIMU NA MUSTAKABILI WA UKOO WA
KIVENULE
|
Mtoa Mada |
2:45 – 3:15
|
Majadiliano kwenye Makundi
|
Makundi 4
|
3:15 – 3:45
|
Murejesho na Majumuisho
|
Kiongozi wa Kundi na Mwezeshaji
|
3:45 – 4:30
|
Pumziko la Chai/Kahawa/Maji
|
Wote
|
4:30 – 5:00
|
Mada ya Nne: UKIMWI NDANI YA UKOO NA ATHARI ZAKE |
Mtoa Mada |
5:00 – 5:30
|
Majadiliano kwenye Makundi |
Makundi 4 |
5:30 – 6:00
|
Murejesho na Majumuisho |
Kiongozi wa Kundi na Mwezeshaji |
6:00 – 7:15
|
CHAKULA CHA MCHANA
|
Wote |
7:15 – 7:45
|
Mada ya Tano: DINI KATIKA UKOO |
Mtoa Mada |
7:45 – 8:15
|
Majadiliano kwenye Makundi |
Makundi 4 |
8:15 – 8:45
|
Murejesho na Majumuisho |
|
8:45 – 9:45
|
Majumuisho:1. Yote Yaliyojitokeza
2.
Matarajio
3. Tarehe ya Mkutano Mwingine |
Mwezeshaji |
9:45 – 10:15
|
Shukurani toka kwa Ndugu Mbalimbali
|
|
10:15–11:00
|
KUCHAGUA VIONGOZI WA KUUNDA KAMATI YA UKOO
|
Ndugu Wote
|
11:00
|
Kufunga Mkutano
|
Viongozi wa
Kamati ya Ukoo
|
F: WAWEZESHAJI WA MADA (FACILITATORS)
1.
Agatha Mhapa
2.
Alphonce
Kivenule
3.
Lizeta Kivenule
4.
Ignas
Kivenule
5.
Siha Kivenule
6.
Christian Kivenule
7.
Adam Kivenule
8.
Justin Kivenule
9.
Donath Mhapa
10. John Kivenule
11. Victoria Kivenule
12. Edger Kivenule
13. Piera Kivenule
14. Florian Kivenule
15. Innocent Kivenule
16. Stephen Mhapa
17. Severin Nyangalima
G: WAHUDUMU: CHAKULA, CHAI/KAHAWA NA VINYWAJI
1.
Rahel Chambula
2.
Asia Kivenule
3.
Germana Mhapa
4.
Mrs. Justin
5.
Mrs. Jovin
6.
Stewart Kivenule
7.
George Kivenule
8.
Janeth Kivenule
9.
Frola Kivenule (Supervisor)
10. Jovin Kivenule
11. Mama Tamasha
(Supervisor)
H: MAANDALIZI YA VIFAA VYA KUTUMIA
Vifaa
|
Idadi |
Bei
|
Jumla |
1. Sahani: Bati (150) na Udongo (50)
|
200
|
|
|
2. Vikombe: Plastiki (150) na Udongo (50)
|
200
|
|
|
3. Vijiko
|
200
|
|
|
4. Biki
|
100
|
|
|
5. Mark Pen
|
15
|
|
|
6. Glasi
|
200
|
|
|
7. Radio + 2 MIC
|
1*
|
|
|
8. Flip Chart
|
|
|
|
9. Meza
|
5
|
|
|
10. Viti + Fomu/Benji
|
100
|
|
|
11. Video Picture Camera
|
1
|
|
|
12. Still Picture Camera
|
2
|
|
|
13. Tissue Paper
|
20
|
|
|
14. Opener
|
10
|
|
|
Jumla
|
|
|
|
I:CHAKULA
Vifaa
|
Idadi |
Bei
|
Jumla |
15. Mchele
|
|
|
|
16. Mahindi (Unga)
|
Gunia 2
|
|
|
17. Viazi Mviringo
|
Gunia 1
|
|
|
18. Unga wa Ngano
|
|
|
|
19. Mafuta ya Kula (Alizeti)
|
Lita 40
|
|
|
20. Chumvi
|
Kgs 4
|
|
|
21. Appetizer (Kiongeza Mate)
|
Kopo 12
|
|
|
22. Maharage
|
Kgs 50
|
|
|
23. Mbuzi wa Nyama
|
2
|
|
|
24. Nyama ya Ng’ombe
|
Kgs 100
|
|
|
25. Mboza Majani
|
Maf. 20
|
|
|
26.Sukari
|
Kgs 25
|
|
|
27. Majani+Iliki
|
½ Dazani
|
|
|
28. Viungo: Nyanya
|
Tenga 3
|
|
|
29. Viungo: Vitunguee
|
Debe 1
|
|
|
Jumla
|
|
|
|
J: VINYWAJI
Vifaa
|
Idadi |
Bei
|
Jumla |
25. Soda
|
|
|
|
26. Bia
|
Kreti 10
|
|
|
27. Maji (Madogo)
|
Katoni
50
|
|
|
28. Pombe ya Kienyeji
|
Plastiki 10
|
|
|
29. Sufuria
|
|
|
|
30. Plastiki za Maji
|
|
|
|
31. Pipa
|
|
|
|
32. Bakuli za Mboga
|
|
|
|
33. Miiko
|
|
|
|
34. Kuni
|
Tela
1
|
|
|
35. Mkaa |
Gunia
2
|
|
|
Jumla |
|
|
|
K: MENGINEYO
Vifaa
|
Idadi |
Bei
|
Jumla |
29. Kutangaza Mkutano
|
Poster 2,
Vipeperushi
|
|
|
30. Kutangaza Mkutano
|
Mwandishi wa
Habari 1
|
|
|
31. Maua na Mapambo
|
|
|
|
|
|
|
|
Jumla
|
|
|
|
L: MADA ZITAKAZOWASILISHWA KWENYE MKUTANO MKUU
1.
HISTORIA
YA UKOO
- Ukoo ni Nini na Unapatikanaje?
- Dhana ya Kuenea na Kukua kwa Ukoo.
- Mgawanyiko wa Ukoo (Chora Mchoro Kuonyesha Ukoo unavyoundwa).
- Kupotea kwa Ukoo.
2.
MAHUSIANO
BAINA YA NDUGU NDANI YA UKOO
- Ukaribu wa Wana Ndugu.
- Ushirikiano Katika Nyanja Mbalimbali.
- Kutembeleana kama Sehemu ya Kudumisha Mahusiano.
- Kuondoa Tofauti na Kusaidiana.
3.
ELIMU NA MUSTAKABALI WA UKOO
- Nafasi ya Ukoo wa Kivenule katika Elimu.
- Umuhimu wa Elimu.
- Dunia ya Utandawazi.
- Nini Kifanyike Kuinua Elimu Katika Ukoo Wetu.
4. UKIMWI NDANI YA UKOO NA ATHARI ZAKE
- UKIMWI ni nini?
- Namna gani UKIMWI unavyoenea/kuambukizwa?
- Njia Mbadala za Kujilinda na Maambukizi?
- Jukumu la Ukoo/Familia Kukabiliana na Janga la UKIMWI.
5. DINI KATIKA
UKOO
- Maana ya Dini
- Umuhimu wa Kuwa na Imani
- Maadili na Dini
- Ukoo Uliojengeka katika Misingi ya Dini
M: MADA ZA KUJADILI KWENYE MAKUNDI
Mada ya Kwanza: HISTORIA YA UKOO
·
KUNDI
LA KWANZA: Ukoo ni Nini
na Unapatikana
·
KUNDI
LA PILI: Kuenea na Kukua kwa Ukoo
·
KUNDI
LA TATU: Mgawanyiko wa Ukoo (Chora Mchoro
Kuonyesha Ukoo unavyoundwa)
·
KUNDI
LA NNE: Kupotea kwa Ukoo
Mada ya Pili: MAHUSIANO BAINA YA NDUGU NDANI YA UKOO
·
KUNDI
LA KWANZA: Ukaribu wa
Wana Ndugu
·
KUNDI
LA PILI: Ushirikiano Katika Nyanja
Mbalimbali
·
KUNDI
LA TATU: Kutembeleana
·
KUNDI
LA NNE: Kuondoa Tofauti na Kusaidiana
Mada ya Tatu: ELIMU NA MUSTAKABALI
WA UKOO
·
KUNDI
LA KWANZA: Nafasi ya Ukoo wa Kivenule katika Elimu
·
KUNDI
LA PILI: Umuhimu wa Elimu
·
KUNDI
LA TATU: Dunia ya Utandawazi
·
KUNDI
LA NNE: Nini Kifanyike Kuinua Elimu Katika
Ukoo Wetu
Mada ya Nne: UKIMWI NDANI YA UKOO NA
ATHARI ZAKE
·
KUNDI
LA KWANZA: UKIMWI ni nini?
·
KUNDI
LA PILI: Namna gani UKIMWI
unavyoenea/kuambukizwa?
·
KUNDI
LA TATU: Njia Mbadala za Kujilinda na Maambukizi?
·
KUNDI
LA NNE: Jukumu la Ukoo/Familia Kukabiliana na
Janga la
UKIMWI.
Mada ya Tano: DINI KATIKA UKOO
·
KUNDI
LA KWANZA: Nini Maana ya Dini?
·
KUNDI
LA PILI: Umuhimu wa Kuwa na Imani
·
KUNDI
LA TATU: Maadili na Dini
·
KUNDI
LA NNE: Ukoo Uliojengeka katika Misingi ya
Dini
N: MAAZIMIO YA MKUTANO
Licha ya kuwa na malengo na makusudia mbalimbali, pia
tunategemea mwisho wa mkutano kutakuwa na mambo kadhaa ambayo yatakuwa ni
makubaliano kutoka pande mbalimbali za ukoo wa Kivenule. Yote hayo kwa pamoja
yatakuwa ni maazimio ya Mkutano Mkuu wa Kwanza
wa Ukoo wa Kivenule.
Kati ya Maazimio ambayo tunayategemea katika mkutano
huo ni:
- Kufanya Senza ya Ukoo wa Kivenule ili kupata idadi kamili ya ndugu.
- Kuanzisha Mfuko wa Ukoo
- Kuchagua Viongozi wa watakaounda Kamati ya Ukoo ya Kuratibu mambo mbalimbali ya ukoo. (Mwenyekiti, Katibu, Mweka Hazina pamoja na viongozi wengine ambayo wana umuhimu na kupewa majukumu kuwepo).
- Uongozi utakaoundwa kufanya mashauriano na usuluhishi wa matatizo mbalimbali ya ukoo yaliyojitokeza.
- Kukusanya taarifa mbalimbali za ukoo
- Kuangalia na Kutathmini usalama wa mali mbalimbali zinazomilikiwa na ukoo nk.
O:
KAMATI MBALIMBALI ZITAKAZOUNDWA KUFANYA KAZI KABLA NA
WAKATI WA
MKUTANO
1.
Kamati
ya Mapokezi
2.
Kamati
ya Malazi
3.
Kamati
ya Chakula
4.
Kamati
ya Vinywaji
5.
Kamati
ya Burudani
6.
Kamati
ya Usafiri
7.
Kamati
ya Ulinzi na Usalama
8.
Huduma
ya Kwanza
9.
Kamati
ya Uratibu wa Shughuli za Mkutano
P:
VITAMBULISHO KWA AJILI YA MKUTANO MKUU WA UKOO
Kitambulisho kitakuwa na:
·
Jina
la Mkutano
·
Jina:
·
Tarehe
Mkutano:
·
Mahali
Anapoishi:
No comments:
Post a Comment