MUHTASARI WA
MKUTANO WA KWANZA WA KUUNDA
KAMATI KUU
YA
MAANDALIZI YA MKUTANO
MKUU
WA
UKOO WA KIVENULE
DESEMBA 17 – 18, 2005
MUHTASARI
WA MKUTANO
WA KWANZA WA KAMATI KUU YA MAANDALIZI YA
MKUTANO MKUU WA UKOO WA KIVENULE, DESEMBA 17 – 18, 2005
Mahali
Ulipofanyika: Ubungo - River Side Bar
Tarehe: Februari 06, 2005
Muda: 10:32 Jioni
Waliohudhuria:
Jina
Kamili
|
Mahali
Anapoishi
|
Namba ya Simu
|
1.
Christian Kivenule
|
Morogoro
|
0744 031 675
|
2.
Adam A. Kivenule
|
Ubungo, Dar es Salaam
|
0741 270 364
|
3.
Innocent Kivenule
|
Ubungo, Dar es Salaam
|
0748 663 315
|
4.
Edgar S. Kivenule
|
Mwenge, Dar es Salaam
|
0741 215 724
|
5.
Ignas Kivenule
|
Tabata, Dar es Salaam
|
0744 060 183
|
6.
Raphael Kivenule
|
Mbezi Beach, Dar es Salaam
|
0745 949 218
|
7.
Philemon Kivenule
|
Buguruni, Dar es Salaam
|
0744 757 844
|
8.
Priskus F. Kivenule
|
Mbezi, Dar es Salaam
|
|
9.
Bakhita A. Kivenule
|
Ubungo, Dar es Salaam
|
|
10.
Tenus F. Kivenule
|
Dar es
Salaam
|
|
11.
Valenia Kivenule
|
Dar es
Salaam
|
0745 555 521
|
12.
Monica Kivenule
|
City Center, Dar es Salaam
|
0745 409 138
|
13.
Phesto Ngimba
|
Dar es
Salaam
|
|
14.
Hamidu Mtono
|
Mabibo, Dar es Salaam
|
0748 443 319
|
15.
Athuman Mtono
|
Kibamba, Dar es Salaam
|
0748 708 708
|
16.
Nuhu Js Mtono
|
Mabibo, Dar es Salaam
|
|
KUFUNGUA
MKUTANO
Mkutano ulifunguliwa mnamo saa 10:32 jioni kwa Mwenyekiti wa muda wa Kamati
ya Muda ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Kivenule, ndugu Christian
Kivenule, na baadaye kuuombea kwa Sala iliyochukua muda wa dakika mbili hivi. Baada ya Sala, pia Mwenyekiti wa muda aliitumia
fursa hiyo kuomba msamaha kwa Ndugu Edgar Kivenule ambaye ni Baba na Mkubwa wa
Ukoo wa akina Kivenule wote waishio Dar es Salaam na mikoa ya karibu, kwa
kushindwa kumshirikisha kikamilifu katika hatua za awali za Mashauriano na
Maandalizi ya Mkutano huo pamoja na suala zima la kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa
Kwanza wa Ukoo wa akina Kivenule.
UTAMBULISHO
Mwenyekiti wa muda pia aliitumia fursa hii
kumwomba na kumkaribisha Ndugu Edgar Kivenule ambaye ni Mkubwa wa Ukoo wa
Kivenule waliishio Dar es Salaam,
kutoa utambulisho kwa wajumbe waliojitokeza kuhudhuria mkutano huo.
Utambulisho ulianza kama
ifuatavyo:
1.
Christian Kivenule (Baba yake John toka Kidamale) anaishi
Matombo, Morogoro
2.
Adam Kivenule (Baba yake Alphonce toka Kidamale) anaishi
Ubungo, DSM
3.
Innocent Kivenule (Baba yake Mareh. Samwel toka Ilole)
anaishi Ubungo, DSM
4.
Edgar S. Kivenule (Baba yake Sigatambule toka Kidamale) anaishi
Mwenge, DSM
5.
Ignas Kivenule (Baba yake Pangayena toka Ilole) anaishi
Tabata, DSM
6.
Raphael Kivenule (Baba yake Pangayena toka Ilole) anaishi
Club Oasis, DSM
7.
Philemon Kivenule (Baba Mareh. Gwelino toka Ilole) anaisha
Buguruni, DSM
8.
Priskus F. Kivenule (Baba yake Mareh. Francis toka Magubike)
anaishi Mbezi, DSM
9.
Bakhita A. Kivenule (Baba yake Alphonce toka Kidamali)
anaishi Ubungo, DSM
10.
Tenus F. Kivenule
11.
Valeria Kivenule (Mke wa Innocent Kivenule) anaishi Ubungo,
DSM
12.
Monica Kivenule (Baba yake Mareh. Francis toka Magubike)
anaishi Zanaki, DSM
13.
Phesto Ngimba
14.
Hamidu Mtono (Baba yake Juma toka Nzihi) anaishi Kibamba,
DSM
15.
Athuman Mtono (Baba yake Juma toka Nzihi) anaishi Kibamba,
DSM
16.
Nuhu Js Mtono (Baba yake Juma toka Nzihi) anaishi Kibamba,
DSM
DHUMUNI
LA MKUTANO
Mwenyekiti alianza kuwaeleza wajumbe kwa
kusema kuwa Wazo la Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Kivenule, lilibuniwa na Ndugu
Faustin Kivenule ambaye ni Baba yake mdogo pamoja na yeye mwenyewe Christian
Kivenule, alipokuwa likizo kijijini, Kidamali mwishoni mwaka jana (2004). Mtu
wa tatu kulipata wazo alikuwa ni ndugu Adam Kivenule, anayeishi Ubungo, mjini
Dar es Salaam kutoka kwa Christian Kivenule mwaka huo huo wa jana.
Mambo mbalimbali yalijitokeza kutokana na
wazo (kusudio) la kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza
wa Ukoo wa Kivenule, Desemba 17-18, 2005 kijijini Kidamale. Kati ya mambo hayo ya msingi ni pamoja na
suala nzima la mahusiano ndani ya wana ukoo, suala la elimu, suala la UKIMWI, kufahamiana
na kuujua ukoo kwa ujumla, kufanya senza ili kujua idadi ya ndugu na mahali
wanapoishi pamoja na mambo mbalimbali ambayo tunayategemea yatajitokeza.
Suala la Ukoo pamoja na Mahusiano baina ya
wanandugu ndani ya ukoo, suala la elimu na gonjwa hatari la UKIMWI ni mambo ya
msingi pia ni kiini na changamoto ya mambo mengi ambayo yatajitokeza katika
mkutano huo mkuu. Mahusiano duni baina ya wana ndugu, kukosa kwa ushirikiano
katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo, kiuchumi na kijamii, matatizo ya kifamilia
na kiukoo ni kati ya masuala msingi yaliyofikiriwa sana kabla ya kuletwa kwa wazo hili katika
kikao hiki.
Mwelekeo wa ukoo wa Kivenule kuhusiana na
suala nzima la Elimu hasa katika dunia hii ya Utandawazi (Globalization) ambapo
dunia imekuwa kama kijiji kisicho na mipaka na kila mtu anaruhusiwa kuingia na
kutoka, kuongezeka kwa viwanda vinavyotumia teknolojia ya hali ya juu,
kuongezeka kwa teknolojia ya mawasiliano, kupanuka na kujengeka kwa miji,
pamoja na soko huria. Mambo yote haya ndiyo yanayoweza kuonyesha mustakabali na
nafasi ya ukoo wa Kivenule kwa maisha ya baadaye. Ilionekana kuwa ukoo wetu upo
nyuma sana
katika suala nzima la elimu, hii linajidhihirisha kutokana na kuwa na ndugu
wachache sana
ambao wameweza kupata elimu kwa kiwango kinachostahili. Hii ni hatari kwa
sababu tunajenga ukoo tegemezi ambayo baadaye utakosa mwelekeo. Mabadiliko ya
Sayansi na Teknolojia yanayojitokeza kila kukicha yanaibadili dunia na hivyo
kutulazimisha nasi katika ukoo wa Kivenule kubadilika. Matumizi ya teknolojia
ya habari na mawasiliano katika simu za mikononi, computer, radio na satellite
ni changamoto kwetu.
Maambukizo ya ugonjwa wa UKIMWI ambayo kwa
kiasi kikubwa yameathiri familia nyingi zikiwemo familia zetu sisi wana ukoo,
yanapaswa kutopuuzwa bali kuwekewa mikakati madhubuti. Ufahamu kuhusiana na
gonjwa lenyewe livyoenea na madhara yake katika jamii, njia mbadala za
kujilinda na maambukizi ya ugonjwa wenyewe pamoja na kuitikia mialiko
mbalimbali ya wanajamii wanaopambana na janga hili ni mambo ya msingi sana ambayo yatajadiliwa
kwenye mkutano huo.
Ilipendekezwa kuwa, wakati wa mkutano huo
kutakuwa na nafasi kutoa uzoefu katika mambo mbalimbali ya kitaalum pamoja na
mada ambazo tutazijadili kwenye agenda za mkutano huu wa leo, nazo zitawasilishwa
kwenye mkutano huo.
Maandalizi ya mkutano mkuu wa ukoo
yameanza mapema ili kutupa nafasi kubwa zaidi ya kujadili, kuandaa pamoja na
kuwasilisha michango yetu ndani ya wakati unaotakiwa.
AGENDA
ZA KIKAO
Agenda mbalimbali zilijadiliwa kwenye
kikao zikiwa na mwelekeo na malengo mahususi ya kufanikisha kufanyika kwa
mkutano mkuu wa ukoo. Agenda zilizojitokeza ni:-
1.
Kuunda
Kamati ya Maandalizi ya Mkutano huo itakayoratibu shughuli mbalimbali za
wanaukoo wanaoishi Dar es Salaam.
2.
Kulitoa
kwa wajumbe wazo la Mkutano Mkuu wa Kwanza wa
Ukoo wa Kivenule unaotegemewa kufanyika kijijini Kidamale, Desemba 17 – 18,
2005.
3.
Mashauriano
baina ya Ndugu wa Ukoo wa Kivenule waishio ILOLE, NDULI, ILULA NA ENEO LA
KIDAMALI kama wanakubali kuwepo na kufanyika
kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza Ukoo wa Kivenule, hapo Desemba 17 hadi 18, 2005.
4.
Kupitia
viwango vya michango vilivyopendekezwa.
5.
Kuweka
Mikakati mbalimbali ya kufanikisha mkutano huo.
6.
Kupitia
Mada zilizopendekezwa kuwasilishwa kwenye Mkutano Mkuu.
KUJADILI
AGENDA ZA MKUTANO
1.
Kuunda Kamati ya Maandalizi ya Mkutano huo itakayoratibu shughuli mbalimbali za
wanaukoo wanaoishi Dar es Salaam
Ndugu Ignas Kivenule alianza kwa kutoa
mapendekezo kuwa Kamati iliyoandaa kikao cha kwanza cha maandalizi ya mkutano
mkuu wa ukoo wa Kivenule iendelee kufanya kazi kwani imeshaonyesha nia. Pia
Ndugu Edgar Kivenule alipendekezwa awepo mbele kwa waongoza mkutano kama kiungo muhimu cha wana ukoo waishio Dar es Salaam. Pia aliuliza swali, je
kutakuwa na vikao vingapi kabla ya mwezi wa kumi (12) wakati wa Mkutano Mkuu?
Ndugu Edgar Kivenule alipendekeza kuwa
kuundwe Kamati. Alipendekeza yeye awe mshauri tu katika masuala mbalimbali
ambayo yatakuwa yanajitokeza kuhusiana na maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, Desemba 17-18, 2005 kijijini
Kidamale. Pia alishauri kupata viongozi ambao wataunda Kamati itakayokuwa na kazi
ya kuyaratibu yote ambayo yatakuwa yanajadiliwa na wajumbe kuhusiana na
maandalizi ya mkutano. Kazi nyingine ya kamati itakuwa kuwaunganisha ndugu wote
wa ukoo wa Kivenule wanaoishi mjini Dar
es Salaam na mikoa ya karibu pamoja na kushughulikia
majukumu mbalimbali kama itakavyotakiwa
kufanya hivyo. Alipendekeza achaguliwe Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu na
Mweka Hazina.
Wajumbe waliochaguliwa kuunda Kamati ni:
1.
Christian Kivenule Mwenyekiti
2.
Athuman Mtono Makamu
Mwenyekiti
3.
Adam Kivenule Katibu
4.
Innocent
Kivenule Mweka
Hazina
5.
Edgar
Kivenule Mshauri Mkuu wa Kamati
Ndugu Edgar Kivenule alipendekezwa kuwa
Mshauri na Kiungo cha wanaukoo wa Kivenule wanaoishi Dar es Salaam na mikoa ya karibu.
Kuhusu suala vikao vingapi vitafanyika
hadi mwezi wa kumi na mbili! Ilikubaliwa kuwa umuhimu wa vikao utatokana na
mahitaji ya kamati ambayo ndiyo yenye jukumu kubwa la maandalizi ya mkutano
mkuu. Kuchangamka au kudorora kwa maandalizi ya mkutano huo ndio kutakako amua
ni vikao vingapi vifanyike.
2.
Kulitoa kwa wajumbe wazo la Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule
unaotegemewa kufanyika kijijini Kidamale, Desemba 17 – 18, 2005
Wazo la kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule lilikubaliwa na wajumbe wote.
3.
Mashauriano baina ya Ndugu wa Ukoo wa Kivenule waishio ILOLE, NDULI, ILULA NA
ENEO LA KIDAMALI kama wanakubali kuwepo na kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza
Ukoo wa Kivenule, hapo Desemba 17 hadi 18, 2005
Wajumbe wote toka Ilole, Nduli, Ilula,
Kidamali na Dar es Salaam
walikubali kwa kauli moja umuhimu wa kuwepo kwa mkutano huo, pia waliaahidi kuhudhuria
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule.
4.
Kupitia viwango vya michango vilivyopendekezwa
Hapo awali ilipendekezwa kuwa kila mjumbe anayeishi
mjini na wale wanaoishi vijijini wenye uhakika wa kipato pia watoe kiasi cha
Tsh. 15,000.00; na vijijini watoe kiasi cha Tshs. 5,000. Kwa upande wa vijijini
pia ilipendekezwa kuwa kwa wale wasio na uwezo wanaweza kutoa mifugo mfano kuku
wawili au mifugo yoyote mingine. Na mwisho wa kutoa michango ilipendekezwa iwe
mwezi wa tisa mwaka huu.
Kati ya wajumbe waliotoa/waliochangia
mawazo yao
alikuwa ni Priskus Kivenule wa Magubike ambaye aliahidi kutoa kiasi hicho licha
ya kuwa na hali ngumu ya kiuchumi, lakini anadhani mkutano una umuhimu sana. Naye Rafaeli Kivenule toka Ilole, alihoji ni kiasi
gani cha fedha kinakadiriwa kugharimu Mkutano huo mkuu? Mwenyekiti wa Kamati
alifafanua kwa kusema, kiasi cha shilingi laki tisa na elfu kumi (910,000.00)
kinakadiriwa kutumika baada ya kuchambua gharama za mahitaji na vitu mbalimbali
ambavyo ni muhimu kuwepo kwenye mkutano huo mkuu.
Pia Rafaeli Kivenule aliuliza kama kutakuwa na wawakilishi wowote toka Dar es Salaam au kuna utaratibu gani wa
kwenda kwenye mkutano huo? Mwenyekiti alimjibu kuwa toka Dar es Salaam au sehemu yoyote nyingine
hakutakuwa na usafiri wa moja kwa moja. Ila kuna utaratibu umepangwa wa kuwa na
usafiri kuanzia Iringa Mjini mpaka Kidamali kwa wageni mbalimbali wanaishi nje
ya Kidamali. Kiasi cha Tshs. 50,000.00 kimewekewa bajeti kuwasafirisha wageni to
ka Iringa mjini hadi Kidamali na 50,000 nyingine kuwarudisha toka Kidamali hadi
Iringa mjini. Hakutakuwa na mwakilishi yeyote toka Dar es Salaam kwenye kwenye kikao hicho, ila
kila ambaye atachanga kiasi cha Tshs. 15,000 atakuwa amejipa tiketi ya
kushiriki na itabidi agigharamie nauli toka hapa hadi Iringa Mjini na toka
Iringa Mjini hadi Dar es Salaam.
Swali jingine lilikuwa ni kigezo gani kimetumika
kupitia viwango vya michango? Swali hili lilijibiwa na Mwenyekiti pamoja na
Mshauri Mkuu, huduma mbalimbali zilizopendekezwa kuwepo kwenye mkutano mkuu
ndiyo kigezo na utaratibu mahsusi uliotumika kupendekeza viwango vya michango.
Pia Adam Kivenule, Katibu wa Kamati aliongeza kwa kusema kuwa makadirio
yaliyopendekezwa mwanzo yanaweza yasikidhi haja, kwani kuna mambo mbalimbali
yanaweza kujitokeza na hivyo kuongeza gharama. Hata hivyo kiwango cha michango
kikizidi lengo hamna ubaya wowote, kuna ununuzi wa vifaa vya kudumu
vitakavyotumika wakati wa shughuli. Tunategemea vifaa hivyo vitaendelea
kutumika katika shughuli mbalimbali za kiukoo zitakazokuwa zinajitokeza kama misiba
na masuala mengine ya kiukoo ambayo yatakuwa yanawakusanya ndugu wengi. Baadhi
ya vifaa hivyo ni pamoja na vyombo vya chakula (sahani, vijiko, vikombe,
sufuria, visu), viti (vya plastiki na mbao) pamoja, meza pamoja na magodoro.
5.
Kuweka Mikakati mbalimbali ya kufanikisha mkutano huo
Mikakati mbalimbali imewekwa ili
kufanikisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza
wa Ukoo wa Kivenule. Kamati imepanga kuandaa kadi za kuchangisha michango ndani
ya wanaukoo na nje ya wanaukoo. Mwenyekiti aliahidi kuwapelekea kadi ya kuomba
michango Askofu wa Jimbo la Iringa Ngalaleku Mtwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa
Iringa. Pia kwa makadirio ya haraka haraka kama watapatikana watu 50 toka Dar
es Salaam na wakalipa shilingi 15,000.00 kila mmoja, tunategemea kupata Tsh.
750,000.00. Kwa hiyo tutakuwa tunatakiwa kukamilisha kiasi cha Tshs. Tshs.
160,000.00. Kwa hiyo Kamati imeona ni
vyema kama tarehe ijayo ya Februari 26, 2005
ya kufanya kikao, pia itumike kusambaza kadi za kuomba michango.
Mikakati mingine ni kuwahamasisha wale
wenye uwezo kuchangia zaidi, na pia tunashauri wajumbe waangalie baadhi ya
maeneo ambayo wanadhani kuna uwezekano wa kusaidiwa kama
wakipeleka barua, miniti, kadi za michango pamoja na wazo zima la mkutano.
Kupatikana kwa wingi wa michango kutasaidia pia kuboresha baadhi ya mambo/huduma
ambazo zimeminywa kutokana na ufinyu wa bajeti.
Pia kamati itakayochaguliwa itakuwa na
jukumu la kwenda kijijini Kidamali na vijiji vingine wanakoishi wana ukoo kwa
lengo la kuwahamasisha jamii nzima ya ukoo ya Kivenule ione umuhimu wa mkutano
huo, na pia ichukue jukumu la kuuchangia kwa namna moja au nyingine. Pia
tutaandaa vipeperushi mbalimbali ambavyo vitakuwa ni sehemu ya hamasa pamoja na
mabango ya kubandika sehemu mbalimbali vijijini yakiwa yamejaa ujumbe mzito
kuhusiana na mkutano huo.
6.
Kupitia Mada zilizopendekezwa kuwasilishwa kwenye Mkutano Mkuu
Mada zote zilizopendekezwa kuwasilishwa na
kufundishwa kwenye mkutano mkuu, zilikubaliwa na wajumbe wa mkutano. Mwenyekiti
wa Kamati alizitaja mada na wawezeshaji waliopendekezwa kusaidia ufanikishaji
wa ufundishaji kuwa ni:-
Mada zilizopendekezwa:-
1.
HISTORIA
YA UKOO
- Ukoo ni Nini na Unapatikanaje?
- Dhana ya Kuenea na Kukua kwa Ukoo.
- Mgawanyiko wa Ukoo (Chora Mchoro Kuonyesha Ukoo unavyoundwa).
- Kupotea kwa Ukoo.
2.
MAHUSIANO
BAINA YA NDUGU NDANI YA UKOO
- Ukaribu wa Wana Ndugu.
- Ushirikiano Katika Nyanja Mbalimbali.
- Kutembeleana kama Sehemu ya Kudumisha Mahusiano.
- Kuondoa Tofauti na Kusaidiana.
3.
ELIMU NA MUSTAKABALI WA UKOO
- Nafasi ya Ukoo wa Kivenule katika Elimu.
- Umuhimu wa Elimu.
- Dunia ya Utandawazi.
- Nini Kifanyike Kuinua Elimu Katika Ukoo Wetu.
4. UKIMWI NDANI YA UKOO NA ATHARI ZAKE
- UKIMWI ni nini?
- Namna gani UKIMWI unavyoenea/kuambukizwa?
- Njia Mbadala za Kujilinda na Maambukizi?
- Jukumu la Ukoo/Familia Kukabiliana na Janga la UKIMWI.
Wawezeshaji
Waliopendekezwa:-
1.
Agatha Mhapa
2.
Alphonce Kivenule
3.
Christian Kivenule
4.
Donath Mhapa
5.
Edger
Kivenule
6.
Florian Kivenule
7.
Ignas
Kivenule
8.
Adam Kivenule
9.
Innocent
Kivenule
10. John Kivenule
11. Justin Kivenule
12. Lizeta Kivenule
13. Piera Kivenule
14. Siha Kivenule
15. Victoria Kivenule
16. Zavery Kivenule
Rafael Kivenule aliuliza kuhusiana na mada
zilizopendekezwa kwenye mkutano mkuu wa Kidamale kama
zitahusika na kwenye vikao vyetu vitakavyokuwa vinafanyika huku? Jibu lilikuwa
kuwa Mada zinahusika kote kwani malengo ya mkutano mkuu ni yale yale ya
kudumisha mahusiano, elimu, UKIMWI, kujuana na kusaidiana.
Mshauri Mkuu wa Kamati ya Maandalizi ya
Mkutano Mkuu wa Ukoo uliufunga mkutano kwa kutoa nasaha mbalimbali ikiwemo
kuujali na kuona umuhimu wa mikutano mbalimbali itakayokuwa inaitishwa na
Kamati hii iliyoundwa. Pia alipendekeza kikao kingine kinachofuata kisiwe mbali
sana na hiki
cha mwanzo. Alisisitiza umuhimu wa kuwajulisha ndugu wengine ambao
hawakuhudhuria waje na washirikiane na wajumbe wengine ambayo tayari wana
taarifa.
Kikao cha pili cha Maandalizi ya Mkutano
Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule
kilipendekezwa kifanyika tarehe 26 Februari 2005, saa 9.00 Ubungo, River Side
Bar.
Kikao
cha kwanza kilifungwa saa 12:58
jioni
Imetiwa Saini na:
____________________ _________________
Christian Kivenule Adam
Kivenule
Mwenyekiti
wa Kamati Katibu
wa Kamati
_______________________
Edgar Kivenule
Mshauri
Mkuu wa Kamati
No comments:
Post a Comment