Maana ya Mahusiano ni hali ya ukaribu, ujirani, urafiki, umoja au ushirikiano unaojengeka baina ya Ndugu, Jamaa au Marafiki. Mahusiano ni hali ya kuwa pamoja Kifikra, Kimwili, Kimawasiliano, Kiimani, Kiitikadi, Kimaendeleo, Kikazi, Kijamii na Kimichezo.
Kutoka kushoto ni Ndugu Christian Kivenule (Makamu Mwenyekiti wa KAUKI) na anayefuata Ndugu Adam Kivenule (Katibu wa KAUKI) kwa sasa; ni mmoja wa Waanzishili wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule-KAUKI |
Mahusiano
hujengwa kwa misingi/namna mbalimbali. Baadhi ya njia au vitu vinavyosababisha
kukawepo na mahusiano ni pamoja na:
1. Ujirani: Ujirani mara
nyingi katika jamii zetu huchangia sana katika kujenga Mahusiano. Mahusiano
yenyewe huonekana katika sura mbili tofauti. Yaani Mahusiano Mazuri kwa maana
ya Sura Nzuri au Mahusiano Mabaya kwa maana ya Sura ya Ubaya.
2. Undugu: Hii ni aina ya
nyingine ya Mahusiano ambapo ndugu wa Damu Moja au wanachangia damu, hujenga
Mahusiano ya Moja kwa Moja (Automatic Relationship). Mara nyingi Mahusiano ya
aina hii huwa na Sura ya Uzuri zaidi (Mahusiano Mazuri). Japo kuna kipindi
Fulani hata Sura ya Ubaya (Mahusiano Mabaya) hujitokeza.
3. Imani: Pia watu huweza
kujenga Mahusiano kupitia Imani zao, mfano watu wanaoabudu katika dhehebu moja
huweza kujenga mahusiano ya aina yao tofauti na dhehebu jingine. Mara nyingi
Mahusiano ya Kiimani huwa na mwelekeo wa Mahusiano memo. Mahusiano mabaya mara
nyingine hutokea na hata kusababisha vita vya kiimani (dini).
4. Itikadi: Mahusiano ya
Kiitikadi nayo hujengeka kwa kufuata Mlengo wa Vyama Vyao. Na zaidi Mahusiano ya
Kiitikadi huegemea zaidi kwenye siasa na hupungua au kutoweka kabisa baada ya
mmoja wao kubadili Itikadi yake yaani kuhama toka chama cha kimoja cha siasa na
kwenye chama kingine cha siasa. Mahusiano ya Kiitikadi hujengwa kwa misingi ya
Chuki, Fitina na Vitisho baina wa watu wa Itikadi moja na wale wa Itikadi
nyingine.
5. Maendeleo: Watu wenye hali fulani
ya kimaendeleo huweza kujenga aina fulani ya mahusiano yenye nia ya kuinuia
hali zao za kimaisha. Na mara nyingi wanaojumuika hapa ni wale ambao tayari
wameonesha nia na mwelekeo. Lakini pia hata wale waliopiga hatua kimaendeleo
huweza kuja mahusiano yao yakiwa nia ya kuimarisha hali walizonazo. Msingi
mkubwa wa mahusiano ya aina hii huwa ni kupeana mbinu na mikakati ya kuleta au
kujiimarisha zaidi katika maendeleo ambayo wanayatarajia au ambayo wamekwisha
yapata.
Pia hata kwa upande wa wale wenye hali duni ya kimaendeleo nao hujenga
aina Fulani ya mahusiano kulingana na hali na uwezo wao. Kasoro ambayo
hujitokeza hapa huwa ni mahusiano duni baina wenye uwezo (matajiri) na wale na
wasio na uwezo (maskini). Katika kujiimarisha zaidi kimaendeleo, maskini huwa
mtumishi (kibarua) na tajiri huwa mtumikiwa (mtwana).
6. Elimu: Watu wenye elimu
nao mara nyining hujenga mahusiano yao. Mara nyingi katika mahusiano yao
huwatenga wale wenye elimu kidogo au wasio na elimu kabisa. Hii hutokea zaidi
kwa wale waliobahatika kupata Elimu ya Juu mfano Chuo Kikuu. Mazungumzo na
mipango yao huwatenga zaidi wale wenye elimu kidogo. Kuwatenga hujitokeza
katika matumizi ya lugha za kigeni, kutowashirikisha katika mawazo mbalimbali
ambayo wanadhani yanaweza kuwainua watu wa hali zote (wasomi na wasio wsomi).
AINA ZA MAHUSIANO
Kuna
aina mbalimbali za mahusiano, lakini tunaweza kugawanya mahusiano haya katika
sehemu kuu mbili.
1. Mahusiano
Mazuri; na
2. Mahusiano
Mabaya.
Aina
mbalimbali za mahusiano ambayo yapo katika jamii zetu ni pamoja na mahusiano
ya:
§
Kikazi;
§
Kijamii;
§
Kisiasa; na
§
Kiuchumi.
MAHUSIANO MAZURI
Mahusiano
Mazuri ni hali ya kuwa pamoja kwa kushirikiana katika nyanja mbalimbali za
maisha. Mahusiano Mazuri huwa katika shida au raha. Raha hujumuisha hali zozote
zenye kuashiria mafanikio na maendeleo katika maisha ya binadamu. Hii ni pamoja
na kufaulu mitihani mbalimbali ya darasani na ya maisha; kujenga nyumba,
kununua gari, kapata kazi nzuri, kufanikiwa katika kilimo, Jubilei, kupandishwa
cheo pamoja na kupata nishani.
Shida
huwa ni hali ya kuwa na mashaka, kutokuwa na uhakika wa maisha, kutokuwa na
kipato, kutofanikiwa katika elimu, ugonjwa, misongamano (Depression), misusuko
(stress), kutokuwa na ajira, kutofadhiliwa kwa hali yoyote (Promotion au
Scholarship) na kadhalika.
MAHUSIANO MABAYA
Mahusiano
Mabaya ni hali ya kutokuwa na ushirikiano, huruma au wema katika nyanja
mbalimbali za maisha. Mahusiano Mabaya nayo hali kadhalika huwa katika ubaya au
uzuri au shida na raha. Tofauti na katika Mahusiano Mazuri, Mahusiano Mabaya
hubaki kuwa ni swa katika shida na raha. Kwa ujumla ushirikiano na mawasiliano
hukosekana kabisa. Huwa hakuna huruma, maelewano, kuvumiliana na kuwasiliana.
Kikubwa
ambacho hujengeka ni chuki, majivuno, wivu, ugomvi na kutakiana shari. Hamna
hata mmojawapo ambaye huombewa kheri. Kwa yule aliyenacho, huombea au hutamaini
yeye aendelee kuwa nacho peke yake na kutomwombea kheri ya kupata yule ambaye
hana kitu.
Na kwa
yule ambaye hana, humwombea shari, bahati mbaya kupotteza au kwa namna yoyote
ambayo haina kheri kwa yule ambaye anacho. Baadhi huomba mfano kama ni gari
lipate ajari, nyumba iungue na kama anasoma anafeli. Katika aina hii ya
mahusiano hakuna nafasi ya kutakiana mema au maendeleo.
MAHUSIANO BAINA YA NDUGU NDANI YA UKOO
Ukoo wa
Kivenule ni mkubwa sana na kwa haraka unakadiriwa kuwa na ndugu karibia elfu
mbili (2000). Ni ukoo ambao unaweza kufanya mambo makubwa nay a kimaendeleo
kama utaungana na kuwa kitu kimoja.
Tatizo
kubwa ambalo linaonekana kwa wanaukoo ni kuwa na mwamko mdogo. Kwa mfano
wanaukoo wanaohudhuria Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ni theluthi
au robot u ya wanaukoo wote. Tumaini la Kamati za Maandalizi ya MKutano Mkuu ni
kuhudhuriwa na Ndugu pamoja na Wanaukoo wa Kivenule kwa wingi zaidi.
Kwa
upande wa Dar es Salaam, mwamko wao ni mdogo sana. Tumaini na tegemeo la awali
ilikuwa Dar es Salaam ingekuwa ni mfano, lakini imeshindika na hii ndiyo hali
halisi. Tunasikitika na Kamati ya maandalizi ya Dar es Salaam inaomba samahani.
Kwa
wanaukoo toka Ilole, nao wamesema tatizo kubwa kwao ni suala na nauli kuwa ni
kubwa. Lakini cha msingi kufanyika ni kuzidi kuwahamasisha na kuwapa mojyo wa
kutambua umuhimu wa Mkutano Mkuu wa Ukoo pamoja na mikutano mingine.
Katika
suala zima la mahusiano, ukaribu wa wanandugu na wanaukoo linaangaliwa kwa
karibu zaidi. Mahusiano yanagusa mambo muhimu katika maisha ya kila siku mfano
Elimu, Ugonjwa, Vifo pamoja na Starehe (Harusi, Send-Off, Kipaimara na
Komunio). Elimu ni muhimu sana kwani inaongeza upeo na ufahamu wa kuweza
kukabiliana na matatizo ya maisha ya kila siku.
Suala
jingine ni ushirikiano katika nyanja mbalimbali mfano Biashara, kazi na kilimo.
Hapa tunamaanisha kuunda kikundi ambacho kitakuwa na mfuko utakaokuwa
unachangiwa na watu mbalimbali kulingana na shughuli na kipato.
Katika
kujenga mahusiano imara, kutembeleana ni muhimu sana. Faida ya kutembeleana ni
kujuliana hali, kusaidiana, kushauriana na kupeana mbinu na mwongozo wa kufauli
katika maisha. Pia katika kutembeleana huwapa fursa wanaukoo/ndugu kuangalia
mazingira mapya anayotembelea kama yanaweza kumfaa kuishi akilinganisha na
mazingira aliyotoka.
Pia
katika kushirikiana kuna haja ya kuwashawishi na kuwabembeleza wale wasio na
uwezo ikiwa ni pamoja na kuwapa moyo, kuwashauri waondoe aibu na wajenge tabia
ya kushirikiana. Katika kushirikiana inakuwa ni rahisi kuweza kutatua matatizo
mbalimbali baina ya wenye nacho na wasionacho.
Kwa
mfano katika shughuli nzima ya kuandaa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa
Kivenule, inakuwa kitu kizuri na mfano kwa wengine kama tutaonyesha kwa vitendo
haya tunayozungumza hapa. H
SIKU YA KWANZA YA MKUTANO MKUU WA KWANZA
WA UKOO WA KIVENULE, DESEMBA 17, 2006
Mkutano
Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ulifunguliwa na Mgeni Rasmi Ndugu Daima
Luvanda, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kidamali.
Awali kabla
ya yote, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Mkuu wa Ukoo
Ndugu Faustino Kivenule, aliwakaribisha ndugu, jamaa na wanaukoo kwa ujumla
kwenye mkutano huo.
Kabla
ya kusoma hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Ukoo, Mwenyekiti wa Kamati ya
Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo, alimkaribisha Ndugu George
Kivenule, kuuombea Mkutano Mkuu kwa sala.
Baada
ya Sala ya kuuombea Mkutano Mkuu, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano
Mkuu wa Ukoo, alitumia fursa hiyo kuisoma Hotuba ya Ufunguzi.
Alianza
kwa kuwajulisha ndugu, wanaukoo na wageni waalikuwa kuwa, lengo la Mkutano Mkuu
wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ni kuwaunganisha wanaukoo wote, wanaoishi sehemu
mbalimbali hapa Tanzania, ili wafahamiane, waelimishane na kupeana ujuzi katika
nyanja mbalimbali za maendeleo na kupeana uzoefu.
Pia,
lengo jingine la Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ilikuwa ni kutolewa
na kufundishwa kwa Mada kadhaa zenye nia ya kuujengea ukoo na kuwa na msimamo
imara. Kwa kuwakusanya ndugu pamoja, Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu,
iliamini itasaidia kuujenga Ukoo katika misingi ya Ushirikiano na Upendo na
hiyvo kuwa na ukoo wenye umoja.
Lengo
jingine la kufanya mkutano mkuu wa ukoo ilikuwa ni kufanya senza ili kujua
idadi ya wanaukoo na mwishoni kufanya uchaguzi wa viongozi, watakaunda Uongozi
wa Ukoo na pia watashirikiana na Kamati ya Ukoo wa Kivenule katika kutekeleza
majukumu mbalimbali.
Kamati
itakayoundwa itakuwa na jukumu la kuratibu mambo mbalimbali na matatizo
yanayohusu ukoo.
Jumla
ya Mada Tano ziliwasilishwa na kufundishwa katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa
Ukoo wa Kivenule. Mada zilizowasilishwa ni pamoja na:
1. CHIMBUKO
NA HISTORIA YA UKOO;
2. MAHUSIANO
BAINA YA NDUGU NDANI YA UKOO;
3. ELIMU
NA MUSTKABALI WA UKOO;
4. UKIMWI
NDANI YA UKOO NA ATHARI ZAKE; NA
5. DINI
KATIKA UKOO.
Harakati
za maandalizi ya Mkutano Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, zilianza
toka mwezi Februari 05, 2005. Harakati hizi zilifanyika Kijijini Kidamali kwa
upande mmoja na kwa upande mwingine jijini Dar es Salaam.
Kamati
zote mbili zilizoundwa zilijipa majukumu mbalimbali, likiwemo lile la kuwaalika
na kuwashirikisha ndugu na wanaukoo katika suala zima la maandalizi ya Mkutano
Mkuu wa Ukoo katika vikao, na pia utoaji wa michango.
Katika
harakati za maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa UKoo wa Kivenule, kamati
zote mbili zilizipata vikwazo mbalimbali likiwemo tatizo la mwitikio duni
katika kulipokea wazo hili. Kwa ujumla, katika kuliuza suala/wazo hili la
kuandaa na kuwa na Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, kamati ilibidi
zitumiea nguvu na mbinu za ziada ili kuweza kufanikiwa.
Mahudhurio
duni yalitoa changamoto kwa Kamati za Maandalizi ya Mkutano Mkuu, kuongeza
juhudi/jitihada na kutafuta njia mbadala za kufikia lengo. Kwa upande wa
Kijijini Kidamali, ushawishi ulizaa matunda, kwa sababu ongezeko la wanaukoo na
ndugu kuliunga mkono wazo la kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo
lilivuna washiriki wengi.
Kwa
upande wa Dar es Salaam, suala la mahudhurio duni, liliendelea kuwa ni kikwazo
kwa kipindi chote cha maandilizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule.
Wapo waliodiliki kusema Mkutano Mkuu wa Ukoo ufanyike kwanza Dar es Salaam na
ndipo ufanyike na kijijini Kidamali. Licha ya kupewa sababu na maelezo ya kina
ya kuufanya Mkutano huo ufanyike Kijijini Kidamali, hawakutilia maanani.
Katika
suala la utoaji wa michango, watu wamekuwa na ari na mwitikio wa hali ya juu
hapa Kijijini Kidamali, na kwa kiwango kikubwa ndio waliosaidia kufanikisha
kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule.
Licha
ya wanaukoo waishio Dar es Salaam kuchangia, lakini mchango wao umesaidia
kidogo sana, kwa sababu kiwango kikubwa cha fedha pamoja na mahitaji mengine,
yamepatikana hapa.
Sehemu
nyingine, nje ya Kidamali, utoaji wa michango hapo mwanzo ulikuwa wa wastani,
lakini kadiri siku zilivyokuwa zinakaribia, ari na kasi mpya ilijitokeza na
kuwa kubwa hasa toka sehemu za Magubike pamoja na Nyamihuu.
Majirani
na watu wengine wasio wanaukoo wamejitolea kutoa michango katika kuusaidia Ukoo
wa Kivenule, kufanikisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa
Kivenule. Majirani na marafiki waliojitokeza kwa hali na mali katika kutoa
fedha, vyombo na vifaa mbalimbali.
HOTUBA YA MGENI RASMI
Mgeni
Rasmi aliishukuru Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa
Kivenule kwa kumwalika kuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano Mkuu wa Ukoo wa
Kivenule. Alisisitiza kwa kusema kuwa, kuna watu wengi muhimu ambao tumewaacha
na kuamua kwenda kumwalika yeye.
Mgeni
Rasmi alisema amefarijika sana kutokana na kuwashirikisha jamaa/wanaukoo wote.
Pia alisisitiza kuwa anahisi yupo karibu na ukoo wa Kivenule kutokana na baadhi
ya jamaa zake wa karibu kuwepo kwenye mkutano huo. Pia hata rafiki zake nao
waliohudhuria kwenye Mkutano Mkuu wa Ukoo; hii ilimpa faraja sana.
Kutokana
na ukoo kuwa na mtandao mkubwa sana, ni muhimu kuwa na shughuli za pamoja kama
hizi. Wakati anakuongea na Mwenyekiti, amefurahi sana kusikia mikakati ya
wanaukoo hasa lile la kufanya senza na pia mkakati wa kufahamiana zaidi.
Mgeni
Rasmi aliwashukuru wale wote waliotoa wazo la kuwepo kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza
wa Ukoo wa Kivenule na jinsi walivyoshirikisha wanaukoo katika shughuli hii.
Katika
shughuli yoyote ile, vikwazo vipo, suala la msingi ni kuelimishana na
kuwashawishi wale ambao hawakuhudhuria ili kuwepo na umoja na mshikamano. Suala
mshikamano na umoja ni muhimu sana katika jamii yetu kwani itasaidia kuleta
maendeleo na wanandugu wawtakuwa karibu.
Pia,
kuwa pamoja kunasaidia kushirikiana katika magonjwa, furaha na matatizo
mbalimbali ya kila siku. Mgeni Rasmi, alitoa mfano wa Abraham na Lutha katika
ugomvi wao wa mifugo, lakini mwisho walijaliana licha ya kutengana. Ndugu ni
muhimu sana na hawawezi kutengana.
Mkutano
huu unatoa changamoto ya kuwa na mshikamano na kuwa na nguvu zaidi katika
kuleta maendeleo.
Mgeni
Rasmi aliushukuru Ukoo wa Kivenule kwa kuelimishana kuhusu umuhimu wa kuwa na
ushirikiano wakati wote nasi tu wakati wa matatizo. Huu ni mfano mzuri kwa
jamii nyingine.
Mgeni
Rasmi aliutakia kila la kheri Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, na
kuahidi kuwa yuko nyuma ya wanaukoo sambamba wakati wote wa Mkutano huo.
Baada
ya hotuba ya Mgeni Rasmi, MKUTANO MKUU WA KWANZA WA UKOO WA KIVENULE,
ulifungulia Rasmi mnamo saa 4:45, tarehe 17 Desemba 2005.
UTAMBULISHO WA WANAUKOO
Kwa
mujibu wa ratiba ya siku ya kwanza ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa
Kivenule, utambulisho wa Wanaukoo ulifanyika kwa kila ndugu/mwanaukoo
kujitambulisha. Mwenyekiti aliwaelewesha washiriki wote jinsi ambavyo wanapaswa
kujitambulisha.
Kila
anajitambulisha alipaswa/alitakiwa kutaja jina lake la mwanzo, jina la baba
yake, babu na jina la mwisho la ukoo. Lakini, pia wanaukoo walijitambulisha kwa
kutaja majina ya Mama zao, Waume au Wake zao.
Kila
mshiriki katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, alipewa
kitambulisho cha kumtambulisha kwa ndugu wengine. Kitambulisho hicho
kilionyesha jina lake kamili, mahali anapoishi, namba ya simu pamoja na sanduku
la posta. Hii ilifanyika makusudi ili kupunguza kuulizana majina kutokana na
washiriki kuwa wengi.
Yafuatayo
hapa chini ni majina ya wanaukoo waliojitambulisha siku kwenye Mkutano Mkuu wa
Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. (refer
registration forms).
UWASILISHAJI WA MADA
Katika Mkutano
Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, jumla ya Mada Tano ziliwasilishwa. Mada ya
kwanza kuwasilishwa katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ilikuwa
ni “CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO”. Wawasilishaji wa Mada hii walikuwa ni ndugu:
1. Christian J. Kivenule
2. Augustino Kivenule
VIAMBATANISHO (ANNEXTURE)
Wawezeshaji wa Mada Mbalimbali
1. Christian J. Kivenule
2. Augustino Kivenule
3. Stephan Mhapa
4. Maria Milimo
5. Adam A.
Kivenule
6. Jovin D. Kivenule
7. George S. Kivenule
8. John S. Kivenule
9. Ignas P. Kivenule
Wawezeshaji Wasaidizi
1. Lesandu Mhapa
2. Adam A. Kivenule
3. Faustin S. Kivenule
4. Christian J. Kivenule
Msimamizi wa Vyombo vya Matangazo
1. Lesandu Mhapa
2.
KAMATI IYORATIBU SHUGHULI KATIKA MKUTANO
MKUU WA KWANZA WA UKOO WA KIVENULE
No comments:
Post a Comment