MKUTANO MKUU WA 10 WA KAUKI

MKUTANO MKUU WA 10 WA KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

KAUKI-Kidamali, Iringa

KAUKI-Kidamali, Iringa
Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Wednesday, March 20, 2013

RIPOTI YA MKUTANO MKUU WA SABA WA KAUKI















RIPOTI YA
MKUTANO MKUU WA SABA WA
UMOJA WA UKOO WA KIVENULE
(KAUKI)













Anuani

Umoja wa Ukoo wa Kivenule- KAUKI),

Eneo la Mlafu, Kando ya Barabara ya Hifadhi ya Ruaha,

Sanduku la Posta 742, Kidamali - Iringa, TANZANIA

Simu:+255-713270364/+255-658843565

Simu ya Kiganja:+255-713270364

Barua pepe: kauki2006@gmail.com / tagumtwa@gmail.com  

 


DIBAJI


Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) umetokana na muungano wa jamii mbalimbali kutoka zaidi ya Vijiji 20 vya Kidamali, Magubike, Idete, Nyamihuu, Nyamahana, Kalenga, Idodi, Nzihi, Igowole, Itagumtwa, Mgongo, Nduli, Lugalo, Iringa Mjini, Kihesa, Igowole (Mufindi), Mafinga,Igominyi na Irole; pamoja na maeneo mengine ya Morogoro, Dar es Salaam, Dodoma na Mkoa wa Iringa kwa ujumla. Umoja huu umekuwa na utaratibu wa kufanya mikutano ya siku mbili kila mwaka. Takwimu zinaonesha kuwa tayari mikutano Saba ya KAUKI imekwishafanyika katika kanda za Kidamali, Irole, Nduli na Magubike. Kanda ambayo haijapata fursa ya kuandaa mikutano hii ni Dar es Salaam pekee. Kanda ya Kidamali pekee ndiyo iliyopata fursa ya kuandaa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa KAUKI mara tatu mfululizo, yaani mwaka 2005, 2006 na 2007.

Umoja huu, ulianzishwa rasmi mwaka 2005, kukabiliana na changamoto mbalimbali za maendeleo, zinazoikabili jamii katika kujikwamua na ugumu wa maisha na pia kutumia fursa zinazopatikana ili kukabiliana na kuondokana na wimbi la umaskini, ujinga, maradhi na utegemezi.

Malengo ya KAUKI ni mengi, lakini lengo lake kuu ni kuinua na kuboresha maisha ya jamii inayounda ukoo wa Kivenule, kielimu, kiuchumi na kisayansi kwa kutumia ujuzi, maarifa na raslimali zinazotunguka. KAUKI hushirikisha mawazo, fikra, ujuzi na maarifa ya kila mwanaukoo, katika mikutano mikuu na mikutano midogo midogo, ambayo huandaliwa na wanaukoo wenyewe. Kwa kukutana pamoja, fikra za kujenga, ujuzi, uzoefu na maarifa, huunganishwa pamoja na kisha kupanga mikakati mbadala ya kuweza kukabiliana na changamoto zilizojitokeza katika maisha ya kila siku.

Majumuisho ya Ripoti ya Mikutano Mikuu Saba ya KAUKI ambayo imekwisha fanyika inavigusa vipaumbele mbalimbali ambavyo ilibidi vitekelezwe katika kipindi cha mwaka 2005 – 2012 ambavyo ni Uanzishwaji wa Miradi ya Maendeleo katika kila kanda; Kuwepo kwa Kalenda ya Shughuli na Vikao vya Kamati Kuu ambavyo kwa mujibu wa Katiba ya KAUKI, inabidi vifanyike kila baada ya miezi mitatu; kuanzisha tovuti au blogs kwa ajili ya kutangaza mambo mbalimbali yanayohusiana na Tagumtwa, kufungua akaunti na kuanzisha mfuko wa maendeleo (Tagumtwa Fund), Kuchapisha Kitabu cha Historia ya Uhehe, Kufungua ofisi katika Kanda, na kipaumbele cha mwisho ni kupokea Taarifa ya Maendeleo KAUKI kutoka katika Kanda zote kabla ya Mkutano Mkuu wa KAUKI kufanyika kila mwaka. Shukrani ziwaendee wote waliojitoa kwa hali na mali hadi kufanikisha kuandaliwa kwa majumuisho ya ripoti hii ya Mikutano Mikuu Saba ya KAUKI.
Imesainiwa na:


Donath Mhapa
Mwenyekiti - KAUKI
 
SHUKRANI


Uongozi wa KAUKI kwa niaba ya jamii inayounda umoja huu, inachukua fursa hii kutoa shukrani zake kwa jamii yote inayooishi katika Kanda za Kidamali, Magubike, Irole, Nduli, Mufindi na Dar es Salaam kwa kila aina ya ushirikiano wanayoionesha katika kutekeleza maono na malengo ya KAUKI kwa minajili ya kufikia dira ya umoja huu.

Ni changamoto kubwa kwa jamii kuweza kuandaa na kufanikisha shughuli kubwa kama kuandaa Mikutano Mikuu Saba wa KAUKI. Ni shughuli inayohitaji raslimali watu, fedha na zana ili kuweza kufikia lengo. Ni jambo la kujivunia na pia kutia moyo kwa wale wote ambao wameshiriki kikamilifu na kwa hali na mali katika jukumu hili.

Licha ya kuwepo kwa watu wachache ambao wameshindwa kuonesha uzalendo wa dhati na hivyo kutotoa aina yeyote ya ushirikiano katika harakati na mchakato mzima wa kuweza kufanikisha Mikutano Saba ya KAUKI, uongozi unawapongeza wote walioshiriki kwa hali na mali.

Malengo ya KAUKI ni mengi na Mikutano hii imejikita kikamilifu katika kutelekeza yale ambayo tumeyakusudia yaisaidie jamii hususani katika suala zima la maendeleo. Mipango, mikakati na vipaumbele vilivyowekwa vitaisaidia jamii inayounda KAUKI kubadilika katika nyanja zote za uchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni.

Uongozi wa KAUKI pia unachukua fursa hii kutuma shukrani zake za dhati kwa Kanda ya Mufindi kwa kuweza kufanikisha jukumu hili zito, sambamba na hilo kuwatia moyo wajumbe kutoka Kanda ya Dar es Salaam katika harakati za maandalizi ya kufanikisha Mkutano Mkuu wa Nane wa KAUKI mwaka 2012.


Imeandaliwa na kutolewa na:


Adam Kivenule
Katibu - KAUKI

 
Utangulizi
Harakati endelevu za kuleta mabadiliko ya kisayansi, kiteknolojia, kiuchumi, kisiasa na kijamii, zinakua kwa kasi kubwa, huku zikichochea mabadiliko ya maisha ulimwenguni. Harakati hizi zinazoambatana na msukumo wa mifumo ya kiuchumi kutoka nchi za magharibi, zinahimiza ukuzaji na udumishaji wa demokrasia, kulindwa kwa haki za binadamu na utawala bora; zinatoa fursa na hamasa kwa jamii huria nazo kubuni na kutafuta mbinu mbadala za kuweza kujiinua ili kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii. Changamoto tunazozizungumzia ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa, kukua kwa sayansi na teknolojia ya habari na mawasiliano, utandawazi na soko huria, na mabadiliko ya mifumo ya watawala wa kisiasa ambayo imeiathiri nchi za Kaskazini mwa Afrika. Msukumo wa Mataifa ya Magharibi unachochea sana mabadiliko, hususani katika suala zima la demokrasia na utawala bora.

Matumizi ya Kompyuta yamekuwa makubwa sana tofauti na awali, ambapo yamejikita hasa katika usambazaji wa habari; na matumizi ya jumla ya teknolojia ya habari na mawasiliano mfano mitandao ya kijamii (social forum). Matumizi ya mawasiliano ya Intaneti (Internet), kutengeneza mifumo na mitandao ya mawasilino (systems and networks of communications), matumizi ya kompyuta katika shughuli za kiofisi, takwimu, maabara mahospitalini, viwandani na katika vyombo vya usalama kama jeshi, viwanja vya ndege na vitengo vya kijasusi (intelligence unit) vimechochea maendeleo na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

Mabadiliko mengine ambayo yameiathiri jamii yetu ni pamoja na kupanuka kwa wigo wa soko duniani (soko huria) ambapo ushindani baina ya mataifa katika sekta mbalimbali za ajira, biashara, uchumi umeongezeka kwa kiwango cha juu. Utandawazi umeongeza maingiliano ya jamii na hivyo kusababisha mabadiliko makubwa katika suala la maadili, mila na tamaduni, na desturi. Sambamba na hilo, dunia imebadilika na kuwa kama kijiji ambapo watu wanaweza kwenda mahali popote au kuwasiliana kwa muda mfupi kwa kutumia usafiri wa ndege, meli, magari; na matumizi ya vyombo vya mawasiliano kama simu za mkononi, mawasiliano ya kompyuta (Internet), barua pepe (e-mail), mitandao ya kijamii (social forums) na chats.

Soko huria limeathiri mataifa mengi ya kiafrika na kusababisha nchi hizo kushindwa kusimamia uchumi wake na hivyo kutoa fursa kwa mataifa tajiri ya kibepari kuweza kumiliki uchumi wa nchi maskini. Kwa mfano kushindwa kuendesha na kuviendeleza viwanda vya umma hapa Tanzania kumetoa fursa kwa mabepari kujipenyeza na kufanya ubia na serikali zetu na hivyo kupelekea upunguzaji wa wafanyakaji, ili kuleta tija kwenye uzalishaji na upatikanaji wa faida. Kwa hali hii Watanzania wengi wamepoteza ajira na kubaki wakihaha huku na huku bila shughuli yeyote. Kwa muktadha huo, huu ndiyo tunaouita ubinafsishaji.

Kwa kutambua yote haya, jamii za Kitanzania zimekuwa katika harakati mbalimbali za kujikwamua na matatizo ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kimaendeleo wanayowakabili ili kuwa na mustakabali bora wa maisha ya mbeleni. Hii imetokana na changamoto za dunia ambazo zimejipenyeza kila kona, hususani baada ya ongezeko la uvumbuzi wa sayansi na teknolojia ya habari na mawasiliano; na hivyo kuongeza ushindani baina ya mataifa ya dunia.  Jitihadi hizi zipo za aina nyingi na kila jamii zimechukua jitihadi za makusudi ambazo imeona zina tija na itanufaika nazo. Harakati za Maendeleo zinazofanywa na Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) katika kujikwamua na kuondokana na matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii hii zimekuwa zikifanyika toka mwaka 2005. Kupitia mikutano mbalimbali katika kanda, na kumekuwa kukiibuka masuala kadhaa ambayo yamekuwa yanaiathiri jamii hii kwa namna mbalimbali.

Kwa mara kwanza katika historia, Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule, ulifanyika, tarehe 17 – 18 Desemba 2005, katika Ukumbi wa Sanga, Kijijini Kidamali, mkoani Iringa.

Katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI), jumla ya ndugu/wanaukoo wapatao 129 toka sehemu mbalimbali mkoani Iringa na kwingineko hapa Tanzania waliohudhuria. Mkutano Mkuu wa Pili wa KAUKI ulihudhuriwa na jumla ya ndugu/wanaukoo wapatao 140. Baadhi ya ndugu/wanaukoo waliohudhuria mikutano hiyo walitoka sehemu za Kidamali, Nyamihuu, Ilala-Simba, Nyamahana, Magubike, Kipera, Nduli, Iringa Mjini, Morogoro, Mikumi, Dar es Salaam, Mufindi, Mbeya, Kilimanjaro, Tosamaganga, Mseke, Mwanga, Kalenga, Idodi, Mgongo, Ilole, Itagutwa, Kipera, Idete na Nzihi.

Umoja wa Ukoo wa Kivenule ulizinduliwa rasmi mwaka 2006, katika Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo wa Kivenule uliofanyika tarehe 24 – 25 Juni 2006 katika Ukumbi wa Sanga Kijijini Kidamali, Iringa. Kuzinduliwa kwa Umoja wa Ukoo wa Kivenule, kulienda sambamba na uzinduzi wa Mfuko wa Ukoo pamoja na Kuipitisha Rasimu ya Katiba ya Umoja wa Ukoo wa Kivenule na hivyo kuwa Katiba Rasmi. Kuwepo kwa Katiba ya KAUKI kulitoa fursa ya kuanza kwa utekelezaji wa shughuli na mipango mbalimbali ya maendeleo. Pia, pamoja na mambo mengine, katika Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo, kulifanya uchaguzi wa Viongozi wa Kanda, uchaguzi wa Walezi wa Ukoo na hivyo utendaji rasmi wa KAUKI kuruhusiwa kuanza.

Mkutano mkuu wa tatu wa KAUKI ulizidi kupanua wigo, maono na mipango inayohusiana na maendeleo ya umoja huu. Mahudhurio ya washiriki katika mkutano pia nayo yamepanuka kutokana na kupata washiriki wapya wengi zaidi kutoka maeneo ya Irore, Nduli, Mgongo na Mufindi.

Jambo la kufurahisha zaidi ni kupanuka kwa wigo wa mahudhurio na mwitikio katika mikutano hii; na pia kuanza kutolewa kwa fursa ya kufanya mikutano ya namna hii sehemu nyingine mfano Mkutano Mkuu wa Nne wa KAUKI utafanyika Irore, Mkutano wa Tano wa KAUKI ulifanyika Nduli, Mkutano wa Sita wa KAUKI ulifanyika Magubike, Mkutano wa Saba wa KAUKI ulifanyika Igowole, Mufindi na Mkutano wa Nane wa KAUKI utafanyika Dar es Salaam. KAUKI inaamini hii ni fursa nzuri ya jamii husika kutoka katika maeneo ambako mkutano unafanyika kuhamasishana wenyewe kwa wenyewe na hivyo kuongeza ari na moyo wa ushirikiano na pia kubadilisha uzoefu katika tasnia ya maendeleo.

Viongozi wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule bado wanaamini kuwa hawajatimiza lengo lao la kuandaa mikutano ya namna hii kwa kiwango cha juu; kwani wanaamini kuwa bado kuna idadi kubwa ya ndugu/wanaukoo na jamii kwa ujumla haijapata fursa ya kuhudhuria mikutano hii. Ndiyo maana, Umoja wa Ukoo wa Kivenule bado unahamasisha ndugu/wanaukoo na jamii kwa ujumla yenye nia ya kujifunza, kuhamasishaneakuhudhuria mikutano hii.


Vijiji ambavyo vimeonyesha mwelekeo mzuri na ambapo kwa Viongozi wa Ukoo ni mafanikio makubwa ni pamoja na Kidamali, Nyamihuu, Ilala-Simba, Nyamahana, Magubike, Idete na Nzihi. Pia, maeneo ya Nduli, Irore na Mgongo, zimeonyesha mwelekeo mzuri na ndiyo maana Mkutano Mkuu wa Nne wa KAUKI unafanyika Irore ikiwa ni mzunguko uliopangwa kuanza kutekelezwa baada ya mikutano mitatu (3) ya KAUKI kufanyika Kidamali. Umoja wa Ukoo wa Kivenule unadhani kuwa hii changamoto tosha kwa viongozi pamoja na ndugu/wanaukoo toka sehemu husika kudhihirisha ari yao na jinsi wanavyohamasika kuutumia umoja huu wa KAUKI kuunganisha ukoo na nguvu zao.

Kuendelea kufanyika kwa mikutano ya KAUKI ni sehemu ya mapambano na pia harakati endelevu za kukabiliana na mabadiliko ya kisera, kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni, kisayansi na teknolojia, na hususani utandawazi na soko huria ambayo yanapelekea jamii kubwa ya Watanzania kuwa tegemezi. Kwa kutambulia hilo, KAUKI inajaribu kutafuta mbadala/mwafaka wa changamoto hizi kwa kuunganisha nguvu ya wanajamii wanaounda KAUKI kushiriki kikamilifu katika masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo hasa suala la kupata elimu, kuwa na hali nzuri kiuchumi na kimaisha na kuyakubali mabadiliko ya dunia na hivyo kuchukua hatua mahsusi kuweza kukabiliana nayo.

Jamii hii tegemezi tunayoijenga na ambayo tunaishuhudia ikikua pole pole siku hadi siku, inatutegemea sisi ndugu/wanaukoo na jamii kwa ujumla kwa kila kitu. Kwa mfano jamii yetu ina wajibu wa kuhudumiwa chakula, malazi, mavazi, madawa, nyumba nzuri na nadhifu za kuishi na elimu. Je, jamii hii itaweza kukabiliana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia kama sisi kama wanajamii husika tutashindwa kukubali kuwajibika kwa kuwapa elimu na huduma zingine za msingi watoto wetu? Hii ni changamoto kubwa ambayo hatuna budi kuifanyia kazi, na kila ndugu/mwanaukoo lazima akubali jukumu ambalo atakuwa amepewa na jamii inayomzunguka.

Nasi kama jamii inayounda Ukoo wa Kivenule tuna wajibu wa kushirikiana na asasi za kijamii na kiserikali katika kuleta maendeleo. Wimbi la umaskini uliokithiri, janga la UKIMWI, ujinga na rushwa vimekuwa ni vikwazo vikubwa vya maendeleo na ambavyo vinazidi kudidimiza harakati mbalimbali za kuweza kujiinua na kujikwamua katika hali hiyo. Harakati hizi za kutafuta maendeleo zimegawanyika katika makundi mbalimbali ya kijamii hususani makundi ya wasomi, wakulima, wafugaji, wafanyabiashara, wanawake, makundi yaliyo pembezoni, wanasiasa na wananchi wa kawaida.

Pia kuna haja ya kufahamiana baina ya wanajamii na ndugu wanaounda ukoo, pamoja na kuujua Ukoo kwa ujumla kama sehemu ndogo tu ya changamoto japo ina madhara makubwa zaidi kama wanaukoo hawafahamiani. Kuwa wengi katika jamii ni sehemu ya raslimali. Kama tunahitaji maendeleo, tunahitaji watu, uongozi bora na siasa safi. Japo suala la fedha ni muhimu, lakini kama huna mipango thabiti, fedha inaweza isiwe muhimu kwani itapotea bure bila kufanya jambo la msingi.

Kuna baadhi ya majukumu muhimu bado hayajafanyiwa kazi. Mfano sensa haijafanyika ili kuweza kujua idadi ya ndugu/wanaukoo wanaounda KAUKI. Bila kujitambua sisi wenyewe hatuwezi kutekeleza mipango yetu kama wana-KAUKI. Sensa ni muhimu sana kwa kuandaa mipango yetu na pia kujiwekea malengo yetu kama wana-KAUKI. Kurudiana kwa majina ni moja ya changamoto za KAUKI. Hii itakuwa na athari siku za usoni ambapo mfanano wa majina utakuwa na athari katika sekta mbalimbali na mifumo ya kuhifadhi kumbukumbu (database). Hivyo umuhimu wa kuwa na majina yasiyojirudiarudia ni muhimu sana.

Changamoto zitakazopatikana baada ya kuyagusia mambo haya ya msingi katika mikutano hii inayofanyika, pia inawapa fursa washiriki wa mikutano hiyo kujenga ajenda mpya za maendeleo zitakazojadiliwa katika mikutano ijayo.

Mkutano mkuu wa kwanza wa KAUKI uliyaangalia kwa kina mahusiano duni baina ya wana jamii, kukosekana kwa ushirikiano katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo, hali duni ya kiuchumi na kijamii, matatizo ya kifamilia na kiukoo.

Mwelekeo na nafasi ya ukoo wa Kivenule katika suala nzima la Elimu hasa katika dunia hii ya Utandawazi (Globalization). Maendeleo ya sayansi na teknolojia ambapo yameifanya dunia kuwa kama kijiji kisicho na mipaka na kila mtu anaruhusiwa kuingia na kutoka; kuongezeka kwa viwanda vinavyotumia teknolojia ya hali ya juu; kuongezeka kwa teknolojia ya habari na mawasiliano (Internet); kupanuka na kujengeka kwa miji, pamoja na soko huria. Mambo yote haya ndiyo yanayoweza kuonyesha mustakabali na nafasi ya ukoo wa Kivenule kwa maisha ya baadaye. Bado inajidhihirisha kuwa ukoo wetu upo nyuma sana katika suala nzima la elimu, hii linajidhihirisha kutokana na kuwa na ndugu wachache sana ambao wameweza kupata elimu kwa kiwango kinachostahili. KAUKI inakabiliwa na changamoto za mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia yanayojitokeza kila kukicha na yanayoibadili dunia na hivyo kutulazimisha nasi katika ukoo wa Kivenule kubadilika. Matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano katika simu za mikononi, Internet, kompyuta, redio na satelaiti ni changamoto kubwa katika Ukoo wa Kivenule.

Ajenda kuu katika Mikutano Mikuu Sita ya KAUKI ambayo imekwishafanyika imekuwa kama ifuatavyo:

§        Kuwasilishwa kwa mada: “CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO”. Wawezeshaji wa mada hii walikuwa ni Ndugu William S. Kivenule toka Kidamali, Ndugu Augustino Kivenule toka Mgongo na Benard Kivenule toka Irore; Pia taarifa mbalimbali za kihistoria zilitafutwa kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya taarifa na kuendelea kuboresha katika kila Mkutano.

§        Kusomwa kwa Ripoti ya Mikutano Mikuu ya KAUKI ya kila mwaka– Katibu Msaidizi wa KAUKI;

§        Kusomwa kwa Taarifa za Mipango na Maendeleo ya KAUKI – Katibu Mkuu wa KAUKI;

§        Kuwasilishwa kwa mada: “CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI KAUKI KATIKA KUJILETEA MAENDELEO”. Mwezeshaji alikuwa ni Mheshimiwa Diwani – Stephan Mhapa; pamoja na baadhi ya watendaji wa KAUKI na walimu wa masuala ya maendeleo ya jamii.

§        Kupeana uzoefu wa shughuli mbalimbali za Kiuchumi na Maendeleo kutoka katika maeneo mbalimbali wanakoishi ndugu/wanaukoo. Uzoefu mkubwa ulikuwa ni Kilimo cha Nyanya Magubike; na

§        Uchaguzi wa Viongozi wa Kamati Ndogo na Kamati ya Utendaji.

§        Kuwasilishwa kwa Taarifa za Mipango na Maendeleo kutoka katika Kanda – Viongozi wa Kanda;


Kwa ujumla ratiba inayoonesha mpangalio wa shughuli zote zilizopangwa kufanyika katika siku mbili za mkutano hufuatwa kikamilifu. Msisitizo ulitolewa kwa masuala ambayo yalihitaji uangalizi wa karibu. Japo kuna baadhi ya majukumu ambayo bado hayajafanyika, hii imebaki kuwa ni changamoto kwa KAUKI. Kutofanyika kwa sensa bado hili ni tatizo na inabidi liendelea kushughulikiwa kwa umakini. Ukusanyaji wa taarifa za ukoo unaendelea kufanyika. Viongozi wapo na wanaendelea na shughuli zao. Msukumo wa hali ya juu unahitajika sana kutoka kwa viongozi wa KAUKI na pia wana-KAUKI wenyewe.
Ufunguzi wa Mikutano ya KAUKI
Mikutano Mikuu ya Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) imekuwa ikifunguliwa na Mgeni Rasmi kwa mujibu wa ratiba. Aliwafahamisha washiriki wa mkutano huo kuwa alikuwa darasani kwa sababu ni kitu kigeni ambacho hajawahi kuona. Ndugu Mihale alijitambulisha kuwa yeye ni mhamia kama zilivyo jamii nyingine mfano ndugu Kivenule ambaye alikuwa na jukumu la kuundaa mkutano katika kanda yake ya Mufindi. Ndugu Mihale anajivunia kwa kuwa amefundisha sehemu ya jamii inayounda KAUKI, lakini pia kwa mara nyingine amealikwa kushiriki kama Mgeni Rasmi.

Mgeni rasmi alikuwa na mawazo ya ziada kwa kuhusianisha idadi ya mikutano ambayo tayari imekwishafanyika tangu kuanzishwa kwa KAUKI. Alisisitiza kuwa KAUKI imetoka mbali na ina jukumu la kudumisha ushirikiano katika nyanja zote za kijamii, kiuchumi, kielimu na kitamaduni. Hii ni dalili za ukomavu na mnapaswa kujivunia kwa hatua hii ambayo mmefikia kwa sababu ni jamii chache ambazo zimeweza kufanya kama mnafanya ninyi.

Ndugu Mihale aliiasa jamii inayounda KAUKI kuwekeza katika nyanja za uchumi, mfano alihimiza kuendeleza kilimo hususani katika maeneo ambapo ardhi bado ina nguvu na rutuba, na inatoa mazao mazuri. Kilimo ni kipana na wana-KAUKI wasio na mtazamo wa kilimo cha nafaka tu, bali pia hata kilimo cha miti na mazao mengine yenye tija na soko.

Kwa kutathmini historia ya KAUKI, ndugu Mihale alikiri uwepo wa ukomavu kwa kurejea idadi ya mikutano ambayo tayari imekwishafanyika. Alihimiza kuendelea kutekeleza malengo na madhumuni ya kuanzishwa kwa KAUKI na pia mipango ambayo tumejiwekea kama vipaumbele. Kupanga ni kuchagua. Yote ambayo tumejipangia kama sehemu ya mkakati ni vyema tukaendelea kuyatekeleza, japo ni lazima pawepo na vipaumbele ili kuweza kufikia dira yetu.

Ndugu Mihale alihitimisha hotuba yake kwa kutathmini uhusiano na ushirikiano wake na jamii inayounda KAUKI kwa miaka kadhaa sasa na anajiona kama sehemu ya jamii hii. Anafarijika kwa kualikwa na kuweza kushirikiana na wana-KAUKI katika Mkutano Mkuu wa Saba wa KAUKI. Alihitimisha pongeza zake kwa kuwapongeza wana-KAUKI kwa kuanzisha umoja huu, na pia kuwatakia kila kheri katika MKutano Mkuu wa Saba ambao ulifanyika kwa siku mbili, yaani Jumamosi ya tarehe 25 na Jumapili ya tarehe 26 Juni, 2011, Igowole-Mufindi, Iringa.


Salamu za Mwaka za Mwenyekiti wa KAUKI
Salaam za Mwenyekiti wa KAUKI katika Mkutano Mkuu wa Saba wa KAUKI, uliofanyika Igowole–Mufindi, Iringa – 2011
Kama Mwenyekiti, ninayo heshima kubwa sana kuandika ujumbe huu kwenu wapendwa wana ukoo. Nina amini wote mliofika kwenye mkutano huo ni kutokana na moyo wa dhati kabisa mlio nao kwa ajili ya kujenga umoja na mshikamano wa ukoo wetu ili jina hili kubwa na lenye hadhi lisipoteee bure.

Naleta ujumbe huu kuomba msamaha kwa kushindwa kuhudhuria mkutano kutokana na kuumwa. Inaniumiza sana kutoonana na ndugu zangu mlio wengi, wapo ambao sijaonana nao tangia mkutano uliopita, wapo ambao ni miezi kadhaa. Lakini najua Mungu ni mwema - atatukutanisha tena.

Kama Mwenyekiti najua kuna mambo ambayo tumeshindwa kutekeleza ndani ya makubaliano ya mikutano mbalimbali, hii ni kutokana na mwaka huu kuwa mgumu sana. Kikazi na kiuchumi. Sipendi nionekane kama najitetea ila kwa niaba ya viongozi wenzangu naomba tusamehewe.

Naomba wana ukoo mtuamini ya kwmaba mwaka huu tutajitahidi kufanya kadri ya yote yatakayoongelewa kwenye mkutano huu.

Nawatakia Mkutano Mwema.

Na Mungu Awatangulie



Donath Mhapa
Mwenyekiti – KAUKI


Taarifa ya Utendaji wa KAUKI
Taarifa ya Utendaji wa KAUKI ya mwaka 2010/2011, ni mkusanyiko wa taarifa mbalimbali ambazo hukusanywa na viongozi Wakuu na viongozi wa Kanda kwa lengo la kuifahamisha jamii inayounda umoja, kutambua michakato mbalimbali ya maendeleo inayoendelea ndani ya jamii hiyo. Taarifa ya utendaji hugusa maeneo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kimaendeleo. Ni utaratibu wa KAUKI kutoa taarifa ya michakato mbalimbali ya maendeleo inayotokea Tanzania na hususani katika Kanda ambako matukio ya kila aina kuhusiana na maisha ya kila siku ya watu hutokea. Lengo lake kubwa ni kuwahabarisha wana-KAUKI kutambua mambo mbalimbali yaliyofanyika, hususani mipango ya maendeleo, mafanikio, matatizo na changamoto na namna walivyokabiliana na vizingiti mbalimbali kuelekea kupata mafanikio na maendeleo tarajiwa.

Taarifa ya Utendaji wa KAUKI imegawanyika katika sehemu kandaa kama inavyobainishwa hapa chini:

Maana ya KAUKI

KAUKI ni Umoja wa Ukoo wa Kivenule, ulioanzishwa rasmi mwaka 2005, kukabiliana na changamoto mbalimbali za maendeleo, zinazoikabili jamii inayounda umoja huu; hususani katika kujikwamua na ugumu wa maisha na pia kutumia fursa zinazopatikana ili kukabiliana na kuondokana na wimbi la umaskini, ujinga, maradhi na utegemezi. Kuanzishwa kwa KAUKI kuliambatana na maandalizi yaliyojumuisha mikutano zaidi ya 10 ya mashauriano iliyofanyika sehemu mbalimbali Jijini Dar es Salaam na Kidamali, Iringa.

Dira ya KAUKI
Kuwa na jamii elewa, angavu na inayowajibika kwa kujitegemea.
Maono ya KAUKI
Kujengeana uwezo kwa kutumia raslimali, stadi, ujuzi, maarifa na weledi, kupitia mafunzo, kongamano, mijadala na mikutano ili kuboresha maisha.

Malengo ya KAUKI
Lengo Kuu
Kuinua na kuboresha maisha ya wanaukoo wa Kivenule, kielimu, kiuchumi na kisayansi kwa kutumia ujuzi, maarifa na raslimali zinazotunguka.

Malengo mengine mahsusi
1.      Kuujua na kuelewa kwa kina Chimbuko na Historia ya Ukoo wa Kivenule;
2.  Kuzikusanya, kuziratibu na kuzihifadhi kumbukumbu mbalimbali za Ukoo wa Kivenule.
3.    Wanaukoo kupata furs ya kufahamiana na kutambuana;
4.  Kufanya senza ya ndugu/wanaukoo wanaounda Ukoo wa Kivenule kila inapobidi kufanya hivyo na Senza hiyo itajumuisha watu waliohai na wafu;
5.     Kuanzisha Mfuko wa Ukoo wa Kivenule utakaosaidia kuinua kiwango cha Elimu na pia kusomesha wanaukoo wasio na uwezo wa kumudu kulipa ada za shule au vyuo;
6.    Kuboresha Elimu ndani ya Ukoo wa Kivenule ili ndugu/wanaukoo wawe na uelewa wa hali juu na kumudu mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia katika Dunia ya Utandawazi;
7.     Kusuluhisha na kutatua matatizo yanayojitokeza katika Ukoo wa Kivenule kwa kupitia vikao vinavyokubalika;
8.    Kuelimisha Wanaukoo/ndugu kuhusiana na madhara ya ugonjwa wa UKIMWI, matumizi ya Madawa ya Kulevya na Ulevi wa kupindukia;
9.    Kuinua viwango vya maisha vya wanaukoo wa Kivenule na kuishi maisha mbadala yenye milo kamili, furaha na nyumba bora na nadhifu;
10.           Kuongeza na kuimarisha mahusiano mazuri ndani na nje ya ukoo kwa kushirikiana katika matatizo mfano raha, ugonjwa, misiba pamoja na majanga makubwa;
11.  Kuwa na nguvu ya kurekebisha tabia zisizostahili kwa wanaukoo/ndugu ndani ya Ukoo na kutafuta suluhu ya migogoro/migongano baina ya mtu au jamii inayotuzunguka;
12.Wanaukoo kuutambua na kuuelewa mtawanyiko/mgawanyiko wa Ukoo wa Kivenule;
13.Wanaukoo/ndugu kushirikiana katika shughuli za uzalishaji mali pamoja na utendaji kazi wa kila siku;
14.Kushirikiana na umoja au vikundi vingine vilivyoungana ili kuuletea Ukoo wa Kivenule maendeleo endelevu;
15. Kuanzisha Mfuko wa kukopeshana (SACOSS); na
16.Kupunguza au kuondoa kabisa tabia ya uvivu na uzembe ndani ya Ukoo wa Kivenule.

Muundo wa KAUKI
KAUKI inaundwa na Kanda sita ambazo ni Kidamali, Irole, Nduli, Magubike, Mufindi na Dar eS Salaam. Kwa mujibu wa Katiba ya KAUKI, kuna Mkutano Mkuu ambao ndio mkutano mkubwa kuliko yote. Hufanyika mara moja kwa mwaka. Pia KAUKI ina mikutano ya Kamati ya Utendaji ambayo hufanyika mara nne kwa mwaka kwa vipindi vya miezi mitatu mitatu. Katika Kanda pia kuna mikutano midogo midogo ambayo jukumu lake ni kujadili masuala yanayohusiana na maendeleo ya kanda. Muundo wa Uongozi wa KAUKI upo kama ifuatavyo:


Nafasi za Uongozi Mkuu wa KAUKI
1.      Mwenyekiti:            Donath P.  Mhapa
2.    Makamu Mwenyekiti:     
3.    Katibu:                             Adam A.    Kivenule
4.    Makamu Katibu:              Christian J.         Kivenule
5.     Mweka Hazina                 Justin D.    Kivenule

Nafasi za Uongozi wa Kanda
Kila kanda ina kiongozi wake ambaye ni Mwenyekiti, ambaye naye husaidiana na Katibu. Pia ndani ya Kanda kuna viongozi wa Kamati mbalimbali ambazo zipo kwa mujibu wa Katiba ya KAUKI.

Katiba ya KAUKI ndiyo mwongozi mkuu wa shughuli zote zinazofanywa na umoja huu. Katiba ya KAUKI ilipitishwa rasmi katika Mkutano MKuu wa Pili wa KAUKI uliofanyika Kidamali, Iringa.



Historia Fupi ya Kuanzishwa kwa KAUKI

Harakati za kuanzishwa kwa KAUKI zilianza kwa kuratibu mawazo ya wana-ukoo wawili, yaani Ndugu Faustino Kivenule na Ndugu Christian Kivenule mwezi Desemba 2004. Mawazo hayo yalifanyiwa kazi kwa kumshirikisha pia Ndugu Adam Kivenule, ambaye bila kuchelewa, waliweza kuandaa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mashauriano, Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa River Side, tarehe 6 Februari, 2005 – Jijini Dar es Salaam.



Harakati nyingine za maandalizi zilielekezwa upande wa Kidamali, Irole na Nduli. Kwa upande wa Kidamali, Mkutano wa Kwanza wa Mashauriano kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule, ulifanyika mwezi Mei ambapo wajumbe toka Dar es Salaam walisafiri kwenda huko ili kuwasilisha hoja, kufanya mashauriano na majadiliano, kuchagua viongozi wa kusimamia uratibu na kuunda kamati ya maandalizi.



Maeneo mengine kama Nduli na Ilole hazikuweza kufanya maandalizi ya moja kwa moja japo taarifa toka Dar es Salaam ziliweza kufikishwa na baadhi ya wanaukoo wanaishi huko. Mjumbe mmoja tu ndugu Augustino Kivenule, toka Mgongo, Iringa ndiye aliyeweza kumudu kushiriki katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule.




Mkutano Mkuu wa Saba wa KAUKI
Huu ni Mkutano Mkuu wa Saba wa KAUKI ambao unafanyika nyuma ya mikutano mingine sita ambayo imekwisha fanyika, mitatu kijijini Kidamali na mkutano moja moja kijijini Irole, Nduli na Magubike. Kwa mujibu wa makubaliano na utaratibu ambao umewekwa na Wana-KAUKI, mikutano hii itakuwa inafanyika katika ngazi ya Kanda, ili kuipa fursa jamii inayounda KAUKI kushiriki moja kwa moja. Lakini pia, vipaumbele huwekwa pale ambapo kuna idadi kubwa ya wana-KAUKA, lakini huridhiwa wakati wa Mkutano Mkuu. Kwa msingi huo, Mkutano Mkuu wa Sita wa KAUKI, kwa kauli moja, uliazimia kuwa Mkutano Mkuu wa Saba ufanyike katika eneo la Igowole, Mufindi, tarehe 25 – 26 ya Juni, 2011.

Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Saba wa KAUKI – Igowole, Mufindi
Utaratibu umewekwa na Wana-KAUKI kuwajibika kufanya maandalizi ya hali na mali ili kuwezesha kufanikisha kufanyika kwa mikutano hii. Kama ilivyokwishafanyika katika mikutano iliyotangulia, utaratibu huo huo umeendelea kutumika katika kuandaa Mkutano Mkuu wa Saba wa KAUKI. Maandalizi yamekuwa yakifanyika kwa ngazi ya Kanda, ambayo viongozi wa kanda husika wamebeba jukumu la kukusanya michango ya hali, fedha na nafaka ili isaidie katika kutoa huduma katika siku mbili za mkutano huu. Kanda zilizopaswa kushiriki katika mchakato wa maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Saba wa KAUKI ni Kidamali, Magubike, Irole, Nduli na Dar es Salaam. Hizi ni kanda ambazo katika mikutano mingi zimekuwa zikiwasilisha taarifa zake. Kila kanda inaelewa majukumu yake ambayo ni pamoja na kukusanya michango, kuhamasisha ushiriki wa wanandugu katika Mkutano wa Saba wa KAUKI huko Igowole, Mufindi na pia utoaji wa michango.

Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Saba wa KAUKI yalianza mapema tu mara baada kumalizika kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Sita wa KAUKI. Maandalizi ya mkutano huu ni jukumu la kila mwana-ukoo ambapo atashiriki kwa kutoa mchango, nafaka, mfugo au nguvu zake katika kuhakikisha kuwa maandalizi ya mkutano yanaenda vizuri.


URATIBU WA SHUGHULI ZA KAUKI NA MIKUTANO
Shughuli za KAUKI zinafanyika chini ya mwongozo ambao ni Katiba ya Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI). Katiba hii ilishaanza kutumika mara tu baada ya Mkutano Mkuu wa Pili wa KAUKI uliofanyika tarehe 24 na 25 Juni 2006. Nakala kadhaa za KAUKI tayari zimetolewa, kusambazwa na zinaendelea kutumika.

Kwa mujibu wa Katiba ya KAUKI, kuna viongozi mbalimbali ambao huchaguliwa kila baada ya kipindi cha miaka mitatu. Kuna viongozi wakuu wa KAUKI na Viongozi wa Kanda. Kila kanda ina kiongozi zaidi ya mmoja. Viongozi hawa, wanawajibika kwa wanaukoo wanaotoka katika Kanda husika.

Wajibu wa viongozi hawa, ni kushirikiana pamoja na Viongozi wa KAUKI katika kutekeleza masuala mbalimbali ya maendeleo yanayouhusu wana-KAUKI. Pia, ni wajibu wa viongozi hawa, kuwashauri Viongozi wa KAUKI katika masuala mbambali yanayoukabili ukoo wetu kwa mfano masuala ya ugonjwa, elimu, uchumi na maendeleo.

Viongozi wa Kanda wana nguvu ya Kikatiba katika kutimiza wajibu wao na pia wana wajibu wa kuhakikisha kuwa mipango mbalimbali inayopangwa kupitia Kamati Kuu au Mkutano Mkuu wa KAUKI inatekelezwa.

Viongozi wa ngazi nyingine za juu kama Katibu, Mwenyekiti, Makamu wa Katibu, Makamu wa Mwenyekiti, Mweka Hazina na Msaidizi wake, wana wajibu wa kuwahimiza viongozi wa Kanda, kushirikiana baina yao wenyewe na pia kushirikiana na viongozi wakuu kutekeleza wajibu na majukumu mbalimbali ambayo yanatukabili.

Kwa mujibu wa KAUKI, viongozi wa Kanda, wana wajibu kuhudhuria vikao mbalimbali kama inavyoainishwa kwenye Katiba ya KAUKI. Wajibu huo pia unawagusa viongozi wengine wa KAUKI na wanawajibika ipasavyo kutekeleza na kutimiza wajibu wao.

MICHANGO YA MFUKO WA KAUKI

Kama ilivyokubaliwa kwenye Mkutano Mkuu wa Pili wa KAUKI; na kama Katiba ya KAUKI inavyoainisha katika Ibara ya 5:3(ii), kuhusiana na wajibu wa kila mwanaukoo, kuwa kila mwanaukoo, anawajibika kulipa michango na kuchangia maandalizi ya Mkutano Mkuu wa KAUKI kama atakavyoelekezwa na uongozi. Katiba ya KAUKI inafafanua kwa mapana kuhusiana na michango mbalimbali hususani michango ya kila mwezi. Katiba ya KAUKI, inaeleza wazi Matumizi ya michango hiyo ni kuwasaidia wanaukoo katika matatizo mbalimbali ya ugonjwa, masomo na pia kiuchumi pindi mfuko huo utakuwa umetuna, kama kila mwanaukoo kuuchangia kikamilifu. Pia michango hiyo itasaidia gharama mbalimbali mfano kufanya mikutano.

Viongozi wa Kanda, walipewa jukumu la kukusanya michango hiyo. Kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa katika Mkutano Mkuu wa Tatu wa KAUKI, stakabadhi zikiwa na mhuri wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI), zilisambazwa kwa viongozi husika wa Kanda kwa ajili ya shughuli za ukusanyaji wa michango hiyo. Kila anayetoa mchango ni lazima apewe stakabadhi ya malipo halali na si vinginevyo.

Lakini viwango hivi vinavyotajwa kwenye Katiba havimfungi mwanaukoo kutoa zaidi. Mara nyingi katika utoaji wa michango kwa ajili ya maandalizi ya Mikutano Mikuu, kadi huandaliwa na kusambazwa kwa wana ndugu mbalimbali na pia kwa jamaa na marafiki zetu. Jambo hili ni nzuri kwa sababu linaonyesha heshima kwa yule unayemwomba atoe mchango wako. Kwa sababu hiyo, kadi maalum huandaliwa na kila mmoja wetu ambaye anahitaji kadi hupewa kwa kiwango kile kinachotakiwa.

Pia, viongozi wa KAUKI walipendekeza wanaukoo kuwa wabunifu katika kutoa michango yao, hii ni pamoja na kutoa bidhaa au mazao ambayo yatajulikana kama mchango. Kama ni nafaka au mifugo, inaweza kutumika kama chakula moja kwa moja au ikauzwa na zikapatikana fedha ambazo zitajumuishwa kwenye bajeti inayoandaliwa.

MICHANGO TOKA VYANZO VINGINE

Vipaumbele viliwekwa hususani katika kubuni miradi ambayo inaweza kusaidia kuboreshea mapato ya KAUKI na pia ya kila mwana-KAUKI. Licha ya kuwa ni kazi ya kamati ya mipango ya maendeleo, katika Mkutano Mkuu wa Saba wa KAUKI, itabidi kuweka vipaumbele kwa mwaka ujao, yaani 2011 – 2012. Lazima wana-KAUKI katika kanda zao, kuwa wabunifu wa shughuli mbalimbali za uzalishaji mali. Tunaweza kubuni miradi ya maandazi, chapati, mama lishe, kilimo au miradi yoyote ambayo mnadhani itatusadia kupata fedha kwa ajili ya kuweza kufanikisha mikutano kama hii na kutunisha Mfuko.

TAREHE YA MKUTANO MKUU WA SABA WA KAUKI

Mkutano Mkuu wa Sita wa KAUKI kwa kauli moja uliazimia Mkutano wa Saba wa KAUKI, ufanyike tarehe 25 ya Jumamosi na 26 Jumapili ya mwezi Juni mwaka 2011, sehemu ya Igowole, Mufindi - Iringa.

YALIYOJIRI KATIKA MKUTANO MKUU WA SABA WA KAUKI

Kwa mujibu wa ratiba ya mkutano, kutakuwa na shughuli mbalimbali katika siku mbili za mkutano. Pamoja na mambo mengine, kutakuwepo na uwasilisha wa mada kadhaa na pia taarifa mbalimbali kutoka kwa wana-KAUKI na viongozi, mfano:
·        Mada:    1.CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO WA KIVENULE
2. CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI KAUKI KUJILETEA MAENDELEO
3. HISTORIA YA WAHEHE
·        TAARIFA YA UTENDAJI WA KAUKI
·        TAARIFA YA SHUGHULI ZA MAENDELEO KATIKA KANDA
·        KUSOMA RIPOTI YA MKUTANO MKUU WA TANO WA KAUKI
·        UZOEFU WA WANAUKOO KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO
·        MAJADILIANO YA HOJA MBALIMBALI AMBAZO ZIMEWASILISHWA NA WASHIRIKI KATIKA MKUTANO
·        MAHITAJI YA KAUKI NA JINSI YA KUFANIKISHA KUPATIKANA KWA MAHITAJI HAYO: Huu ni mjadala wa jumla na kila mjumbe wa mkutano anashiriki moja kwa moja kutoa mawazo yake. Katibu na watendaji wengine wa KAUKI wana jukumu ya kuyanakili maswali na majibu yote kwa ajili ya kufanyiwa kazi.
·        MAJUMUISHO NA TATHMINI YA MKUTANO
·        MIPANGO NA MIKAKATI YA MBELENI
·        KUTANGAZWA KWA TAREHE YA MKUTANO MKUU WA SABA
·        SHUKRANI
·        KUFUNGA MKUTANO

UTAMBULISHO NA KUBALISHANA MAWAZO
Utambulisho baina ya wanaukoo utafanyika kwa kina na kila ndugu/mwanaukoo kuwa na kitambulisho ambacho atakivaa kifuani kwake. Kutakuwa na fursa mbalimbali kwa wanandugu kupeana uzoefu mbalimbali wa utafutaji wa maisha bora. Mbinu za kujiinua kimaisha zitafundishwa na wadau wenye uzoefu pamoja na aina mbalimbali za miradi ambayo ndugu wanaweza kufanya.

Tutakuwa na kipindi cha kupeana uzoefu wa shughuli mbalimbali za kiuchumi kutoka katika maeneo mbalimbali ambako ndugu wanaishi. Kama ilivyofanyika katika Mikutano Mikuu ya KAUKI iliyotangulia, maeneo yatakayotolewa uzoefu Kilimo, biashara na ajira kutoka katika maeneo mbalimbali. Kwa kupeana elimu ya ujasiliamali itasaidia kutufungua macho na hivyo kuongeza uwezo wa kufikiri na kwenda kutafuta maisha katika maeneo ambayo ni mbadala kwetu. Pia taarifa hizi zitawasaidia wanandugu toka maeneo mengine kupata mwanga wa shughuli mbadala zitakazosaidia kupata kipato na kuboresha maisha.

Kutakuwa na Viongozi wa Kamati mbalimbali
A. Mipango na Maendeleo
1.      Mwenyekiti:     
2.    Katibu:    
B. Mahesabu na Fedha
1.      Mwenyekiti:     
2.    Katibu:    
C. Maafa na Matatizo
1.      Mwenyekiti:     
2.    Katibu:    

D. Nidhamu na Maadili
1.      Mwenyekiti:     
2.    Katibu:             

Angalizo: Viongozi wa Kamati ya Mahesabu na Fedha, watashirikiana na Mweka Hazina katika kuratibu shughuli zote za ukusanyaji wa michango mbalimbali, wakati wa maafa, wakati wa mkutano mkuu, mikutano na pia mchango wa kila mwezi.

MIPANGO YA KAUKI

KAUKI inajikita kujiimarisha katika ngazi zote za kiutendaji, kiuendeshaji na kuleta mabadiliko ya kiuchumi, kielimu, kisiasa, kimaendeleo, na kimapinduzi. Baadhi ya mikakati KAUKI ni pamoja na:
1.      KAUKI kuwa na ofisi yake Kijijini Kidamali na pia sehemu nyingine za Kanda ambapo wanaukoo wanadhani ni muhimu kuwa na ofisi. Jambo hili lilishaanza kufanyiwa kazi na pia eneo ambalo inabidi ofisi iwepo lilishapatikana katika majadiliano ya awali ya mwaka 2008. Viongozi toka eneo ambalo ofisi inabidi ifunguliwe watatuhabarisha zaidi wapi wamefikia.
2.    Suala na pili ni kupata usajili ili tuwe na fursa ya kufanya shughuli kubwa zaidi. Bado suala hili lipo katika mchakato, na taratibu nyingine zote za namna ya kupata usajili zilikwisha fuatiliwa. Ni matumaini yetu uongozi mpya uliochaguliwa, unalifanyia kazi kazi jukumu hili muhimu.
3.    KAUKI kuwa na sanduku lake la posta. Bado jambo hili halijatekelezwa na natumaini hatua za makusudi inabidi zichukuliwe. Hakuna masharti makubwa zaidi ya kulipa fedha tu. Ni changamoto kwa viongozi wa KAUKI na nadhani hatuna haja ya kusubiri zaidi ya kuchukua hatua zinazostahili kulikamilisha hili.
4.    Kuwa na Akaunti katika Benki yeyote. Ufunguzi wa Akaunti ulikwisha fanyika kabla ya Mkutano Mkuu wa Nne wa KAUKI uliofanyika Irole. Hima wanaukoo tutoe michango yetu na pia tusaidie kuitunisha akaunti yetu. Wangapi wanalipa mia tano za kila mwezi? Mnapata stakabadhi? Wangapi bado hawajalipa? Kwa nini? Hizi ndizo changamoto kwetu. Bila kujitoa hatuwezi kufanikiwa. Msitegemea watu wachache tu ndio wanaoweza kubadili maisha ya wanaukoo wote. Inabidi tuunganishe nguvu zetu wote. Wahenga walisema, ‘Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu’.
5.     KAUKI kuwa na vitendea kazi mfano Kompyuta, Printa, Simu, Meza na Viti. Bado kutekelezwa kutokana na uhaba wa fedha na pia bado wanaukoo hawajaonesha mwito wa kutoa michango ya kila mwezi. Hivyo tunawahimiza kutoa michango hiyo ili baadhi ya mipango na malengo ya KAUKI yakamilike. Tutafanya harambee ili tuweze kununua vifaa hivyo, mfano Kompyuta na printa yake. Wangapi mpo tayari kuchangia?
6.    KAUKI kuanza kutoa elimu mbalimbali kwa wadau wake. Tumeanza na sehemu ndogo na mojawapo ni wakati wa mikutano hii. Lakini bado tunadhani inabidi tutafute fursa nyingine. Kama tungekamilisha suala la ofisi, natumaini fursa nyingi za kupata masomo kwa wana-ukoo zingetafutwa kwa hali na mali.
7.     KAUKI kubuni na kutekeleza miradi mbalimbali ambayo itawasadia wanajamii. Sijapata taarifa rasmi labda viongozi wa Irole wanaweza kutupa taarifa. Mwenyekiti wa kipindi kilichopita Bwana Nyakunga aliahidi kuwa wangeanzisha mradi wa alizeti, Sijui walifikia wapi? Tupatieni taarifa. Tuanzishe mashamba ya KAUKI na kila kanda iwe na shamba lake. Mazao yatakayopatikana yatatumika kama sehemu ya chakula wakati wa mikutano hii. Na pia iliyobaki itauzwa na fedha kuwekwa katika mfuko wa KAUKI.
8.    KAUKI kuwa na kitengo cha Utaalam wa Kitaaluma na Kiujuzi ambacho kitafanya shughuli za kuiletea fedha KAUKI, pamoja na miradi mbalimbali. Tunasubiri kukamilika kwa ofisi na kazi itaanza mara moja. Binafsi nipo tayari kujitolea kuhakikisha tunafanikiwa katika suala hili.
9.    KAUKI kujitangaza kwa asasi nyingine za ndani ya nchi na nje kwa kutumia teknolojia ya kisasa yaani kuwa na tovuti. Tumeanzisha tovuti (blog) na natumaini bado haijafikiwa na wengi. Mpango mzuri ni sisi wenyewe kulisajili jina la KAUKI (Domain Registration) kwa wamiliki wa mitandao na kuiweka hewani tovuti yetu kwa watoa huduma za mawasiliano ya tovuti na mitandao.
10.           Kuchapisha kitabu toleo la kwanza cha Umoja wa Ukoo wa Kivenule kwa kipindi cha mwaka 2008 – 2009. Kamati iliyoundwa imeshindwa kukutana na kuikamilisha kazi hiyo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za:
§        Kukosa pesa
§        Mtawanyiko wa wajumbe
§        Shughuli yenyewe inahitaji pesa kwa mfano kazi ya uhariri na uchapishaji
Kutokana shughuli kuwa ngumu na kushindwa kufanyika kama ilivyopangwa, inabidi kamati iwasilishe taarifa na mapendekezo kwa wajumbe kuhusu hatua ambazo imechukua na nini imekifanya; na pia nini kifanyike, kwa kurejea hadidu zake na pia majukumu yaliyopaswa kufanyika kabla ya mkutano huu wa tano.

MAPUNGUFU YA KAUKI NA WATENDAJI WAKE
Uongozi wa KAUKI bado umeonyesha mapungufu na hii pia inaathiri mfumo mzima wa utendaji kazi zake. Baadhi ya mapungufu hayo ni pamoja na kushindwa kubisa kutekeleza baadhi ya mikakati ambayo ilikuwa ni sehemu ya makubaliano na pia mipango ya mbeleni ya maendeleo ya KAUKI. Kwa mfano baadhi ya majukumu ambayo bado hayajatekelezwa ni pamoja na:-
1.      Kutokuwa na Kalenda ya Shughuli za Mwaka;
2.    Kushindwa kufanya vikao vya Kamati Kuu;
3.    Ushirikiano finyu baina ya viongozi wa ngazi mbalimbali wa KAUKI kutokuwepo kwa mpango-kazi, tathmini ya utendaji kazi na utekelezaji wa mipango ya maendeleo;
4.    Viongozi wengi wa KAUKI kushindwa kutekeleza wajibu wao;
5.     Makusanyo hafifu ya michango; Wangapi wamelipa mpaka muda huu?
6.    Viongozi kutokuwa mfano mzuri katika kutoa michango. Tunaamini kiongozi lazima awe ni mfano wa kuigwa; Je viongozi wote mnatoa michango ya kila mwezi. Wangapi wamelipa mpaka muda huu?
7.     Wanaukoo kuonesha mwitikio duni katika ushiriki wa Mikutano Mikuu. Mfano wa Wanaukoo kutoka Dar es Salaam; na
8.    KAUKI kutokuwa na ofisi. Ni mwaka wa pili sasa jambo hili ilibidi liwe limekamilika lakini mpaka sasa bado ofisi haijaanza kufanya kazi. Hii ni changamoto kwa viongozi wetu.

Walezi

1.      Stephan                   Mhapa
2.    John               Kivenule
3.    Augustino      Kivenule









HITIMISHO
KAUKI imeendelea kujikita katika kuongeza uangavu na weledi kwa wanaukoo kutokana na kutambua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika dunia hii ya utandawazi. Mazingira na hali halisi iliyopo ambayo kila mwana-KAUKI anaiona, ameguswa nayo au kuathiriwa nayo ni vigezo tosha. Propaganda na kejeli kama kauli mbiu kutoka kwa watu mbalimbali duniani hususiani kwa wanasiasa wetu yameendelea kuwaathiri wana-KAUKI na watanzania kwa ujumla. Tatizo la ufisadi wa raslimali za watanzania mkiwemo ninyi, rushwa katika huduma za jamii mfano kukosa dawa hospitalini, maji safi ya kunywa, elimu duni na ukosefu wa ajira, vyote vinamwathiri sisi. KAUKI inaamini kuwa mwana-KAUKI mwenyewe ndiye mwenye uamuzi wa mwisho ya kuamua hatma na mustakali wa maisha yake ya sasa na baadaye. KAUKI haitarajii maisha bora kwa kila mwana-KAUKI au mtanzania mwingine yataletwa na wanasiana au watu baki waliopo nje ya nchi yetu. Jukumu la maendeleo ni letu sisi wenyewe. Ndio maana tunahimiza watu kujitoa kwa hali na mali kuuchangia mfuko wetu ili uweze kuisaidia jamii yetu katika nyanja zote za kiuchumi, elimu, afya na maendeleo.

Yote yanayofanyika katika mikutano hii ni sehemu ndogo ya jitihada kubwa zinazofanywa na KAUKI. Ahadi za wanasiasa ni za mdomoni tu na hatuamini hata siku moja kama wana-KAUKI mtayafurahia maisha bora kwa kukaa mtu moja moja au kwa kutounganisha nguvu zenu. Wanasiasa wana-agenda zao ambazo mara nyingi huwa kuangalia maslahi yao na kuyalinda. Mfano wa hivi karibuni kwa Wabunge wameomba kujiongezea mshahara hadi kufikia milioni kumi na mbili kutoka milioni saba (7) wanazolipwa sasa. Mishahara hiyo ni kodi za maskini sisi wana-KAUKI na wenzetu ambao hawapo hapa. Kwa hiyo suala la kujikwamua kimaendeleo la kila mmoja wetu hapa na si vinginevyo. Hizi ni mojawapo ya harakati za kujikwamua na lindi la umaskini unaotukabili. Lakini harakati nyingine unazifanya wewe kama mwana-KAUKI wakati wa kupiga kura yako kumchagua kiongozi. Msilemae na rushwa. Tumieni vizuri fursa yenu kwa kuchagua viongozi bora. Pengine hata katika chaguzi wa viongozi wa KAUKI watu wanaweza kutoa rushwa ili wachaguliwe! Tumieni fursa zinazopatikana kwa kuwahoji wale wanaotaka nafasi za uongozi, nini kimewatuma kugombea nafasi hizo, na sisi kama wana-KAUKI tutarajie nini. Jamii yetu ni maskini wa kila kitu, wataisaidiaje?

Kama wana-KAUKI inabidi kuhimiza mabadiliko ya kiitikadi na kimaendeleo. Wajibu watu ni kuwadhihirishia nini tunakusudia kukifanya ili kuboresha maisha yetu. Maisha bora kwa kila mtanzania kama mnavyoahidiwa katika kampeni za uchaguzi ni ndoto tu.

Kwa mfano huu ni mwaka wa tano toka uchaguzi mkuu ufanyike na wananchi mliahidiwa maisha bora kwa kila mtanzania. Je haya maisha mnayoishi kweli ni maisha bora ukilinganisha na maisha mliyokuwa mnaishi siku za nyuma. Mfumuko wa bei, kupanda kwa bei za mafuta kila wakati, njaa, ufisadi, dhuluma na kejeli na hata vifo kwa wapigania haki za wanyonge. Hii ni hali ya kukatisha tamaa na sisi wana-KAUKI tuna kila wajibu na kukabiliana na hali hii.

Tukikaa pembeni na kuacha yatokee basi nasi tutaangamia kwani kinachofanyika kinatuathiri sisi. Ufisadi na wizi wa mali ya umma unatuathiri sisi. Kwa mfano kukosekana kwa huduma za msingi mfano huduma za afya, shule bora, maji na bei kubwa ya umeme ni matokeo ya dhuluma hizi. Hivyo kama wana-KAUKI bado tuna jukumu kubwa la kukabiliana na kila aina ya uozo, na adui wa maisha na maendeleo yetu.

Mbadala ya maendeleo ya nchi ya Tanzania unakutegemea wewe mwana-KAUKI, dhima, uamuke toka sasa na uelekeze nguvu zako katika kuiboresha KAUKI ili jamii yetu ipate maendeleo.

Imetolewa na:

___________________           _____________________
Donath Mhapa                               Adam A. Kivenule

Mwenyekiti – KAUKI               Katibu - KAUKI




























Taarifa za Maendeleo katika Kanda
Taarifa kwa Ujumla
Kwa wastani taarifa za Maendeleo katika Kanda haidhirisha sana ukilinganisha na jitihadi ambazo zimefanywa na KAUKI kwa kipindi cha miaka saba ya uhai wake, kutekeleza majukumu yake na kuimarisha, kuoboresha na kuchagiza maendeleo katika nyanja zote, ushirikiano na mahusiano baina ya jamii. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa viongozi kanda, kumekuwepo na kusuasua kwa ushirikiano katika nyanja mbalimbali za maendeleo katika jamii, hususani kushiriki katika kuinua elimu, kuboresha michango ya Mfuko wa KAUKI, kujitolea katika maandalizi ya Mikutano Mikuu ya KAUKI, na hata katika furaha na shida.

Mfuko wa KAUKI umekuwa ukichangiwa na watu wachache kabisa tofauti na kusudio la awali, ambalo pia kwa upande mwingine lingesaidia kuboresha mapato ya mfuko na hivyo kuanza kuisadia jamii inayounda umoja huo. Licha ya kupangia kiwango kidogo cha shilingi mia tano, bado mwenendo wa makusanyo ya mwaka ni duni kabisa ukilinganisha na idadi ya jamii inayounda KAUKI katika Kanda.

Makusanyo kiduchu ya michango yanachelewesha kuanza kutumika kwa fedha za mfuko kwa sababu kiasi kilichokusanywa bado ni kidogo sana. Wakati sasa umefika kwa Wana-KAUKI kuwa na vipaumbele ambavyo vitasaidia kuboresha mfuko wa KAUKI. Kabla ilivyopendekezwa katika Mikutano Mikuu ya KAUKI iliyopita, ambapo suala la uanzishaji miradi ambayo itaongeza tija na kuboresha mifuko, ni bora ukazingatiwa zaidi, hasa baada ya kufanya tathmini ya makusanya kwa kipindi cha miaka mitano.

Zoezi la kufanya sensa ya wana-KAUKI nalo bado limeendelea kusuasua katika kanda zote, licha ya msisitizo ambao ulikuwa umewekwa wa kuhakikisha kuwa, zinakusanywa taarifa mbalimbali za jamii inayounda KAUKI kwa    





Michango ya Mfuko wa KAUKI


































CHANGAMOTO MBALIMBALI ZINAZOIKABILI KAUKI KATIKA KUJILETEA MAENDELEO

NINI KIFANYIKE
1.      Kuboresha Mfuko wa KAUKI: Michango ya kila mwezi itolewe na Viongozi wa Kanda wawe makini katika kusimamia ukusanyaji wa michango. liandaliwe jedwali ambalo litamwongoza Kiongozi wa Kanda katika makusanya hayo kama mfano wake unavyoneshwa hapa chini.

NA.
JINA LA MWANA-KAUKI ALIYETOA MCHANGO
MWEZI
JUMLA

JULAI
AGOSTI
SEPTEMB
OKTOBA
NOVEMBA
1.
Adam Kivenule
2000
5000
3000
1000
2000
13,000
2.
Christian Kivenule
2000
5000
4000
2000
1000
13,000
3.
















































Pamekuwepo na uzembe mkubwa katika kutoa michango ya kila mwezi. Kanda ya Dar es Salaam wameanza kwa kutoa hadi ya kiasi ambacho watakusanyika kwa kipindi cha mwaka 2011 – 2012. Jumla ya kiasi cha shilingi laki mbili (200,000/=) kimeahidiwa na Adam Kivenule (50,000/-), Christian Kivenule (50,000/-), Frank Kivenule (50,000/-) na Lugano Sanga (50,000/-).

2.    Ianzishwe Miradi ya Maendeleo katika kila Kanda: Kila kanda ibuni mradi ambao utawashirikisha wana-KAUKI wote katika kuutekeleza. Fedha ya KAUKI inaweza kukopeshwa. Kwa mfano kwenye miradi ya kilimo, fedha itawasaidia katika manunuzi ya mbolea na pembejeo na baada ya mavuno watairejesha. Lakini kwa wale ambao watabuni miradi ambayo ni tofauti na kilimo, wenyewe wataona ni kwa namna gani itawasaidia. Kutakuwa na utaratibu maalum wakati wa ukopeshaji na pengine, riba kidogo inaweza kutoshwa lengo ikiwa ni kuboresha mfuko.

3.    Kuandaliwa kwa Kalenda ya Vikao vya Kamati vya KAUKI kwa mwaka 2011 – 2012. Inapendekezwa kuwepo na vikao vya kamati ambavyo vitawakutanisha viongozi wa Kanda na viongozi wakuu wa KAUKI kila baada ya miezi mitatu. Jedwali lifuatalo linaonesha ratiba ya vikao hivyo na mahali vitakapofanyika.

NA
TAREHE YA KIKAO
MAHALI NA SHUGHULI MUHIMU
MWANDAAJI
1.
24 SEPTEMBA 2011
KIDAMALI, IRINGA
KANDA YA KIDAMALI
2..
31 DESEMBA 2011
NDULI, IRINGA
KANDA YA NDULI
3.
03 MACHI 2012
MOROGORO MJINI: Pamoja na Mambo mengine, Mkutano huu utapokea Ripoti za Kanda ambazo zitagusa maeneo mbalimbali ya maendeleo ya eneo husika.
KANDA YA DAR ES SALAAM
4.
26 MEI 2012
IROLE, IRINGA. Wakati wa Mkutano huu mambo yafuatayo yatapaswa kufanyika:
Kutoa Ripoti ya Utekelezaji wa yale ambayo tulijipangia kufanya hususani kuanzisha miradi na maendeleo yake.
Maendeleo ya ukusanyaji wa Michango yote. Ya Mkutano Mkuu wa Nane wa KAUKI na ile ya Mfuko wa KAUKI.
Kuona Daftari la Wanaukoo kutoka Kanda husika lililochorwa vizuri litakaloonesha Majina na Miezi ya Michango.
Viongozi wa Kanda zote kuwasilisha Majina ya Wana-KAUKI watakaohudhuria Mkutano Mkuu wa Nane wa KAUKI Jijini Dar es Salaam.
Kuandaa majina ya watoto ndani ya ukoo waliofanya vizuri katika mitihani ya Darasa la Saba, Kidato cha Nne, Sita na Vyuo Vikuu.
KANDA YA IROLE, IRINGA

4.    Kuanzisha Vikoba ndani ya Wana-KAUKI: Utaratibu wa namna ya kujiunga na vikoba na pia elimu ya mafunzo kuhusu VIKOBA itabidi iandaliwe na kutolewa kwa wana-KAUKI wote. Ni jambo la msingi elimu hii ikasambazwa kwenye kanda zote.

MKUTANO MKUU WA NANE WA KAUKI
Mkutano Mkuu wa Nane wa KAUKI ni mkutano unaoandaliwa na Kanda ya Dar es Salaam, ambao utazishirikisha jamii zote kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania, hususani mkoani Iringa Dar es Salaam na Morogoro. Mkutano huu ni mwendelezo wa mikutano ya KAUKI ambayo imekuwa ikifanyika toka mwaka 2005 katika Kanda za Kidamali, Irole, Nduli, Magubike na Mufindi, yote ikiwa imefanyika mkoani Iringa. Mkutano wa Nane wa KAUKi unaandaliwa kwa lengo mahususi ikiwa ni pamoja na kupima utekelezaji wa vipaumbele ambavyo viliwekwa wakati wa Mkutano wa Saba, uliofanyika Igowole, Mufindi Iringa.

Vipaumbele viliwekwa katika Mkutano Mkuu wa Saba wa KAUKI ni pamoja na:
·        Fedha za Mfuko wa KAUKI kuanza kusaidia kwa kutoa vimikopo vidogo vidogo kwa ajili a shughuli za uzalishaji na biashara na kasha kuzirudisha ndani ya kipindi Fulani cha makubaliano. Lengo la kuanza kuzitumia fedha za mfuko ni kuifanya akaunti iendelee kuwa hai kwa kuweka na kutoa fedha tofauti na hali awali, ambapo ilibidi isimamishwe kutokana na fedha zake kutotolewa.
·        Kuanzisha miradi mbalimbali ambayo itaboresha mfuko wetu na pia kuboresha mahitaji ya mikutano na huduma katika mikutano hiyo. Kila Kanda inategemea kuanzisha mradi wake kwa kadri watakavyoona inafaa.
·        Kuhakikisha kuwa vikao vya Kamati Kuu ya KAUKI vinafanyika kwa mujibu wa kanda.
·        Kuandaa Kalenda ya shughuli za KAUKI pamoja na vikao mbalimbali vya umoja huo.
·        Kuhamasisha Kanda ya Dar es Salaam kuanza maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Nane wa KAUKI, ambao utafanyika Dar es Salaam, tarehe 30 Juni na tarehe 01 Julai 2012.
·        Kuendelea kuuchangia mfuko wa KAUKI kwa bidii kwa kuandaa fomu maalum ambayo kila kiongozi wa Kanda atabaini watu wake na kuwajumuisha katika fomu hiyo, ili iwe rahisi kufuatilia.

Tarehe na mahali utakapofanyika
Mikakati: miradi itaanzishwa kwa lengo la kuboresha mfuko na pia kusaidia gharama za maandalizi ya Mkutano Mkuu huo. Gharama hizo ni pamoja na usafiri wa kwenda na kurudi; huduma za chakula na pia kujikimu njiani mwa safari.

Ushiriki: Kutokana na shauku kubwa ya wana-ndugu kushiriki Mkutano Mkuu wa Nane wa KAUKI, itabidi kuwe na mshikamano wa dhati hususani katika kuratibu maandalizi ya mkutano huo. Michango kama kipaumbele cha maandalizi yote itabidi watu wajitoe hasa na kwa wakati kwa sababu tunaamini kutakuwa na ushiriki mkubwa sana kutoka pembe mbalimblali za Tanzania. Pamoja na hayo, tunategemea kupata ugeni kutoka hapa hapa Dar es Salaam ambao nao pia wataongeza gharama. Mikakati mahususi itabidi iandaliwe na Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Nane wa KAUKI itakayokuwa Dar es Salaam na kuiwasilisha katika vikao mbalimbali vya kamati vitakavyo fanyika Kidamali, Nduli, Morogoro na Irole.

Mahali pa Kufanyika Mkutano Mkuu: Dar es Salaam kama zilivyo kanda nyingine nayo inawajibika kuandaa Mkutano wa Nane wa KAUKI. Mikakati mbalimbali namna ya kufanikisha jukumu hili itafanywa na Wawakilishi wa Kanda ya Dar es Salaam.




















SHUKRANI
Zilielekezwa kwa Ndugu Xavery Kivenule kwa kufanikisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Saba wa KAUKI. Mkutano wa mwaka 2001 uliofanyika Igowole, Mufindi, Mkoani Iringa ulifana sana. Tunatanguliza shukrani zetu kwa wenyeji kwa ukarimu wao hususani Mzee Xavery Kivenule aliyepigana Kiume na familia yake kukamilisha jukumu hili. Tunawaombea afya njema na Mungu Awabariki Sana.

Mwisho tutakiane afya njema, kazi njema kila mmoja wetu na safari njema.











VIAMBATANISHO
Orodha ya Washiriki
Jina                                                  Anuani                                            Simu
1.       Christian             Kivenule       S. L. P. 6030, Morogoro                0714146382
2.      Xavery                 Kivenule       S. L. P. 28, Igowole, Mufindi        0758260506
3.      George                 Kivenule       S. L. P. 108, Kidamali                    0782815862
4.      Jovin                   Kivenule       S. L. P. 193, Kidamali                     065555064
5.      Fredy                   Nywage          S. L. P. 108, Kidamali                    0782281207
6.      Vitus                    Nzala              S. L. P. 108, Magubike                   0788282046
7.      Emmanuel         Kivenule       S. L. P. 108, Magubike
8.     Shallon F.           Nywage          S. L. P.108, Kidamali                     0767281207
9.      Anodi                  Kivenule       S. L. P. 108, Magubike                   0769065568
10.  Teudos                Kivenule       S. L. P. 108, Magubike                  
11.   Konjeta               Kivenule       S. L. P. 108, Magubike      
12.  Davidika             Nzala              S. L. P. 108, Magubike      
13.  Rukia                   Nzala              S. L. P. 108, Magubike      
14.  Kaini                    Kivenule       S. L. P. 108, Kidamali                    0766663151
15.   Rehani B.                        Kivenule       S. L. P. 193, Kidamali                     0763568564
16.  Paulo                   Nzala              S. L. P. 108, Magubike
17.   Gift                      Kivenule       S. L. P. 2412, Kidamali
18.  Grolia                  Kivenule       S. L. P. 2412, Kidamali
19.  Iman                    Kisega                        S. L. P. 1243 Magubike
20. Rukia                   Nzala              S. L. P. 1243, Magubike    
21.  Frida                    Kivenule       S. L. P. 2412, Kidamali      
22. Nomsa                 Kapugi           S. L. P. 28, Igowole-Mufindi       
23. Abiba                   Juma             S. L. P. 1243, Magubike    
24. Benadeta                        Kivenule       S. L. P. 1544, Kidamali
25.  Nesia                   Kivenule       S. L. P. 742, Kidamali        
26. Augustino          Kivenule       S. L. P. 1777, Mgongo                     0688024838          
27.  Thadei                 Nyakunga     S. L. P. 250, Irole                            0652874470
28. Anodi                  Kivenule       S. L. P. 250, Irole                            0712 626235
29. Anyesi                 Kivenule       S. L. P. 108, Magubike      
30. Samwel               Mihale           S. L. P. 28, Mufindi                        0766048047
31.  Adam A.              Kivenule       S. L. P. 32505, Dar es Salaam       0713 270364
32. Martin                 Kivenule       Nduli, Iringa
33. Lugano                Sanga             S. L. P. 2991, Dar es Salaam         0768683700
34. Gloria      Z.        Kivenule       S. L. P. 2991, Dar es Salaam         0764647725
35.  Frank       I.         Kivenule       S. L. P. 76971, Dar es Salaam        0713146479
36. Clelia                   Kivenule       S. L. P. 2412, Kidamali
37.  Silenia                 Kivenule       S. L. P. 1544, Kidamali
38. Jonisia                Mkwambe     S. L. P. 742, Kidamali
39. Remija                Kivenule       S. L. P. 1544, Kidamali
40. Amalya G.           Kivenule       S. L. P. 250, Irole
41.  Faustino             Kivenule       S. L. P. 742, Kidamali                     0787626185/
                                                                                                                      0755293193 

HOTUBA YA UFUNGUZI WA MKUTANO MKUU WA SABA WA KAUKI

JUNI 25 – 26, 2011, IGOWOLE, MUFINDI – IRINGA

Ndugu Mgeni Rasmi,
Ndugu Wageni Waalikwa;
Wanaukoo na Jamii yote inayounda Ukoo wa Kivenule;
Mabibi na Mabwana;

Kamwene…, Munogage…, Makasi…,

Ni furaha iliyoje kuwa nanyi katika hadhara hii. Ni matumaini yangu kuwa, wote ni wazima wa afya na kuwepo kwenu pia kuonesha jinsi mnavyothamini shughuli ambayo tutaifanya kwa siku mbili, yaani leo na kesho katika kuhakikisha kuwa Mkutano Mkuu wa Saba wa KAUKI unafanikiwa.

Ndugu Mgeni Rasmi;  nianze kutoa historia fupi ya umoja huu. KAUKI ni Umoja wa Ukoo wa Kivenule, ulioanzishwa rasmi mwaka 2005, kukabiliana na changamoto mbalimbali za maendeleo, zinazoikabili jamii inayounda umoja huu; hususani katika kujikwamua na ugumu wa maisha na pia kutumia fursa zinazopatikana ili kukabiliana na kuondokana na wimbi la umaskini, ujinga, maradhi na utegemezi. Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI), ulianzishwa rasmi mnamo Desemba 17 - 18, 2005 Kijijini Kidamali. Harakati za kuanzishwa kwa KAUKI zilianza mwezi Februari 06, 2005 Jijini Dar es Salaam kwa kufanya mkutano wa kwanza wa mashauriano. Harakati nyingine na kuunda kamati za maandalizi zilielekezwa upande wa Kidamali, Ilole na Nduli. Kwa upande wa Kidamali, Mkutano wa kwanza wa maandalizi ya Mkutano Mkuu ulifanyika mwezi Mei ambapo wajumbe toka Dar es Salaam walishiriki katika majadiliano, kuchagua viongozi wa kuunda kamati ya maandalizi na kuhamasisha.

Ndugu Mgeni Rasmi; Umoja wa Ukoo wa Kivenule ulizinduliwa rasmi mwaka 2006, katika Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo wa Kivenule uliofanyika tarehe 24 – 25 Juni 2006 katika Ukumbi wa Sanga Kijijini Kidamali, Iringa. Kuzinduliwa kwa Umoja wa Ukoo wa Kivenule, kulienda sambamba na uzinduzi wa Mfuko wa Ukoo pamoja na Kuipitisha Rasimu ya Katiba ya Umoja wa Ukoo wa Kivenule na kuwa Katiba Rasmi; hivyo kutoa fursa ya kuanza kwa utekelezaji wa shughuli na mipango mbalimbali ya maendeleo. Pia, pamoja na mambo mengine, katika Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo, kulifanyika uchaguzi wa Viongozi wa Kanda, uchaguzi wa Walezi wa Ukoo na hivyo utendaji rasmi wa KAUKI kuruhusiwa kuanza.

Ndugu Mgeni Rasmi; Huu ni Mkutano Mkuu wa Saba wa KAUKI; na tayari mikutano mingine sita imekwisha fanyika, mitatu kijijini Kidamali na mkutano moja kijijini Irole, Nduli na Magubike. Kwa utaratibu uliokubalika katika Mkutano Mkuu wa Pili wa KAUKI na wa Tatu kuwa itabidi mikutano hii pia ifanyike sehemu nyingine ambako kuna jamii inayounda umoja huu. Na leo hii ni zamu yenu na ndiyo maana mkutano huu unafanyika hapa Igowole, Mufindi. Katika Mkutano Mkuu wa Sita wa KAUKI uliofanyika Magubike, washiriki wa mkutano huo kwa pamoja walikubaliana kuwa Mkutano Mkuu wa Saba ufanyike Igowole, Mufindi.

Malengo ya KAUKI
Ndugu Mgeni Rasmi; malengo makuu ya KAUKI ni kujaribu kwa kila hali kwa kutumia ujuzi na maarifa, kuinua uwezo wa kielimu, kiuchumi na kimaendeleo, kwa wanajamii wanaounda umoja huo, kwa kutumia rasilimali mbalimbali zinazopatika katika nchi ya Tanzania na hususani katika maeneo wanayoishi; ikiwa ni pamoja kuihamasisha jamii hii kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kupunguza umaskini unaowakabili.

KAUKI imeanzishwa kukidhi shida na mahitaji ya jamii iliyounda umoja huu na hususani katika maeneo lengwa ya elimu, afya, uchumi na maendeleo, kwa kushirikisha mawazo, fikra, ujuzi na maarifa ya kila mwanaukoo, katika mikutano mikuu na mikutano midogo midogo, ambayo inaandaliwa na wanaukoo wenyewe. Kwa kukutana pamoja, fikra za kujenga, ujuzi, uzoefu, kujengewa uwezo na maarifa, huunganishwa pamoja na kisha kupanga mikakati mbadala ya kuweza kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika maisha.

Ndugu Mgeni Rasmi; malengo KAUKI ni mengi na baadhi yake ni:
  • ·  kuwa na ofisi yake Kijijini Kidamali na pia sehemu nyingine za Kanda
  • ·        Kuisajili KAUKI na kuwa na mfuko wa kusaidia ndugu katika elimu, afya na matatizo mengine. Tayari mfuko umeanzishwa na unaendelea kuchangiwa. 
  • ·        kuwa na sanduku lake la posta, tovuti. Kwa sasa ina tovuti  inayopatika kupitia www.tagumwafoundation.wetpaint.com na inaboreshwa kupitia www.tagumtwa.blogoak.com    
  • ·        Kuwa na Akaunti katika Benki – tayari imefungua katika Benki ya NMB, Iringa Mjini
  • ·        kuwa na vitendea kazi mfano Kompyuta, Printa, Simu, Meza na Viti
  • ·        kuanza kutoa elimu mbalimbali kwa wadau wake. Inatoa elimu katika mikutano yake
  • ·        kubuni na kutekeleza miradi ambayo itawasadia wanajamii. Mpango wa Mradi wa Alizeti-Irole, ambao bado haujaanza kutekelezwa.
  • ·        kuwa na kitengo cha Utaalam wa Kitaaluma na Kiujuzi ambacho kitafanya shughuli za kuiletea fedha KAUKI, pamoja na miradi mbalimbali. Ipo katika mchakato.
  • ·        Kuchapisha kitabu toleo la kwanza cha Umoja wa Ukoo wa Kivenule kwa kipindi cha mwaka 2009-2012. Kazi inaendelea na taarifa mbalimbali zinaendelea kukusanywa.

Mafanikio
Ndugu Mgeni Rasmi; KAUKI imefanikiwa kufanya yafuatayo:
·        kuendelea kufanyika kwa mikutano mkuu. Mikutano Mikuu sita tayari imefanyika Kidamali mara tatu, Irole, Nduli na Magubike mara moja moja.
·        kupanua wigo wa ushiriki kutoka Irole, Nduli, Itagutwa, Mgongo na Mufindi; Kilimanjaro, Dar es Salaam, Morogoro na maeneo mengine.
·        Kuongezeka kwa ufahamu na uelewa wa watu kuhusu KAUKI na mada zinazofundishwa
·        kufahamiana baina ya wana-KAUKI kumeongezeka mara dufu
·        Kuanzishwa kwa Mfuko wa KAUKI
·        Imeanzisha blogs ambazo zinabeba taarifa mbalimbali za KAUKI na wana-KAUKI kwa ujumla.

Changamoto
Ndugu Mgeni Rasmi; Changamoto zinazoikabili KAUKI ni pamoja na
·        Ushiriki duni wa wanaukoo katika mikutano mikuu
·        Kasi ndogo na moyo wa kuchangia mfuko wa kusaidia wanaukoo
·        Kutokidhi gharama za kuandaa mikutano hii kwa sababu michango inakuwa ni kidogo
·        Kutofikia malengo ya mipango tunayojiwekea
·        Ndugu wa mijini kuwa na mwamko mdogo wa kuunga mkono jitihada hizi

Matarajio katika Mkutano Mkuu wa Saba wa KAUKI
Ndugu Mgeni Rasmi; Kama Ratiba inavyoonesha, hayo ndiyo yatakayofanyika katika siku mbili za Mkutano Mkuu wa Sita wa KAUKI. Lakini, tunategemea kuwa na Mada kadhaa ikiwemo ya Chimbuko Historia ya Ukoo ambapo tutaijadili kwa undani zaidi. Lakini pia, masuala mengine mfano elimu, maendeleo na ushirikiano wa dhati baina ya wanandugu yatapewa kipaumbele.

Utambulisho baina ya wanaukoo utafanyika kwa kina na kila ndugu/mwanaukoo atakuwa na kitambulisho ambacho atakivaa kifuani kwake. Kutakuwa na fursa mbalimbali kwa wanandugu kupeana uzoefu mbalimbali wa utafutaji wa maisha bora. Mbinu za kujiinua kimaisha zitafundishwa na wadau wenye uzoefu pamoja na aina mbalimbali za miradi ambayo ndugu wanaweza kufanya.

Tutakuwa na kipindi cha kupeana uzoefu wa shughuli mbalimbali za kiuchumi kutoka katika maeneo mbalimbali ambako ndugu wanaishi. Kama ilivyofanyika katika Mkutano Mkuu wa Tatu, Nne, Tano na wa Sita wa KAUKI, maeneo yatakayotolewa uzoefu Kilimo, biashara na ajira kutoka katika maeneo mbalimbali. Kwa kupeana elimu ya ujasiliamali itasaidia kutufungua macho na hivyo kuongeza uwezo wa kufikiri na kwenda kutafuta maisha katika maeneo ambayo ni mbadala kwetu. Pia taarifa hizi zitawasaidia wanandugu toka maeneo mengine kupata mwanga wa shughuli mbadala zitakazosaidia kupata kipato na kuboresha maisha.

Matarajio ya Mbeleni
Ndugu Mgeni Rasmi; Mipango ya KAUKI kwa mwaka uliopita 2010 na 2011
·        Kuendeleza jitihada za kufungua ofisi Kidamali na kununua vifaa vya ndani ya ofisi kama vile kompyuta, printa na fenicha
·        Kuchapisha kitabu cha historia ya wahehe ambapo ndani yake pia kutakuwa na taarifa za KAUKI
·        Kuongeza wigo wa ushiriki katika mikutano; na
·        Kuhamasisha wana-KAUKI kuchangia mfuko

Hitimisho
Ndugu Mgeni Rasmi; KAUKI imeendelea kujikita katika kuongeza uangavu na weledi kwa wanaukoo kutokana na kutambua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika dunia hii ya ushindani. Ugumu wa maisha, mfumuko wa bei, ukosefu wa ajira, na changamoto mbalimbali ambazo kila mwana-KAUKI anaiona, ameguswa nayo au kuathiriwa nayo. Tatizo la ufisadi wa raslimali za watanzania, rushwa katika huduma za jamii mfano kukosa dawa hospitalini, maji safi na salama, elimu duni na ukosefu wa ajira, vyote vinatuathiri sisi. KAUKI inaamini kuwa mwana-KAUKI mwenyewe ndiye mwenye uamuzi wa mwisho ya kuamua hatma na mustakabali wa maisha yake ya sasa na baadaye. KAUKI haitarajii maisha bora kwa kila mwana-KAUKI au mtanzania mwingine yataletwa na wanasiasa au watu baki waliopo nje ya nchi yetu. Jukumu la maendeleo ni letu sisi wenyewe. Ndio maana tunahimiza watu kujitoa kwa hali na mali kuuchangia mfuko wetu ili uweze kuisaidia jamii yetu katika nyanja zote za kiuchumi, elimu, afya na maendeleo.

Ndugu Mgeni Rasmi, baada ya kusema hayo machache, kwa niaba ya Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu ya Igowole, Mufindi, nakuomba Ufungue Rasmi Mkutano Mkuu wa saba wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI).

Karibu Sana


Imetolewa na:

Ndugu Donath Mhapa
Mwenyekiti
Kwa Niaba ya Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Saba wa KAUKI





   RATIBA YA MKUTANO MKUU WA SABA WA UMOJA  
  WA UKOO WA KIVENULE-KAUKI

Siku ya Kwanza ya Mkutano Mkuu – Igowole: Tarehe 25 Juni 2011

Muda
Shughuli/Jukumu
Wahusika
12.00 – 12.45
Wageni Wote Kuamka na Kufanya Maandalizi ya Kuingia kwenye Mkutano

Wote

12.45 – 01.15
Kupata Kifungua Kinywa
Washiriki wote
01:15 – 02:00
Kuwasili Mkutanoni na Kujisajili na kupata vitambulisho
Washiriki wote
02.00 – 02.20
Kusoma Hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Sita wa KAUKI
Mwenyekiti wa KAUKI
02.20-02.45
Ufunguzi Rasmi wa Mkutano na Mgeni Rasmi
Mgeni Rasmi
02.45-03.15
Utambulisho baina wa Ndugu na Wageni Waalikuwa
Wote
03.15 – 04:00
Mada: CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO WA KIVENULE
(a). Washiriki wasambaziwe nakala ya muundo wa Ukoo na kisha kuujadili na kutoa mawazo yao katika makundi

Mwakilishi toka  Kidamali

Mwakilishi toka Ilole
mwakilishi toka Nduli
Washiriki wote
04:00– 04:30

Pumziko la Chai / Kahawa/Maji

Washiriki Wote

04.30-04.45
Mada Inaendelea.
(b). Washiriki waijadili mada na kutoa mapendekezo
(c). Washiriki waijadili mada na kupendekeza nini kifanyike kutunza kumbukumbu hizo
(d). Washiriki wazijadili njia mbadala za kutunza taarifa zinazohusiana na ukoo
Wawezeshaji na Washiriki wote
04.45-05.05

Kuwasilisha majadiliano katika Makundi

Washiriki wote na Wawezeshaji
05.05-05.30
Majumuisho ya yote yaliyojitokeza katika Mada
Wawezeshaji
05:30 – 06:30
TAARIFA YA UTENDAJI WA KAUKI:
1. Mipango na Shughuli zilizokusudiwa kufanywa na KAUKI 2009/2010;
2. Taarifa ya Utendaji kwa Ujumla;
3. Taarifa ya Mahesabu na Fedha; na
1.                   Mafanikio na Matatizo ya KAUKI
4. Matarajio ya KAUKI 2010/2011
Katibu Mkuu
Mhasibu
06.30 – 07.00
TAARIFA YA SHUGHULI ZA MAENDELEO KATIKA KANDA
1. Uhamasishaji
2. Mwitikio wa Jamii inayounda Ukoo
3. Ushirikiano miongoni mwa wanajamii
4. Mafanikio na Matatizo
Viongozi wa Kanda zote
07.00-08.00
CHAKULA CHA MCHANA
Washiriki wote
8:00 – 8:45
KUSOMA RIPOTI YA MKUTANO MKUU WA SITA WA KAUKI
Kujadili Mapungufu, Kutoa Ushauri, Nyongeza
Kupitisha Ripoti
Katibu Msaidizi
Washiriki wote
08:45 – 09:15
Salaam mbalimbali kutoka kwa Washiriki wa Mkutano Mkuu (Wastani watu 6 na dakika @ 5)
Washiriki wa Mkutano
09:15– 09:45

Pumziko la Chai/Kahawa/Maji

Washiriki wote
09.45 -11:00
UZOEFU WA WANAUKOO KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO
1.Kidamali/Magubike: Kilimo cha Nyanya /Tumbaku na shughuli nyingine za kiuchumi dakika 25
2. Irole/Nduli/Itagutwa/Mgongo: Uzoefu wa Shughuli za Kiuchumi dakika 25
3. Dar/ Morogoro/ Kilombero / Moshi dakika 15
4. Kalenga, Ifunda, Ilala Simba, Wasa, Idodi na Nyamihuu
Washiriki wote; viongozi wa Kanda au wajumbe watakaochaguliwa kutoa uzoefu wa shughuli hizo za kiuchumi
11.00
KUAHIRISHA MKUTANO
Mwenyekiti wa KAUKI
2:30 – 6:30 Usiku
Burudani (Muziki wa Kisasa na Ngoma za Asili), vinywaji, kufahamiana zaidi na kubadilisha mawazo
Wanaukoo wote

Siku ya Pili ya Mkutano Mkuu – Igowole: Tarehe 26 Juni 2011

Muda
Shughuli/Jukumu
Wahusika
12.00 – 12.45
Wageni Wote Kuamka na Kufanya Maandalizi ya Kuingia kwenye Mkutano

Wote

12.45 – 01.15
Kupata Kifungua Kinywa
Washiriki wote
01:15 – 02:00
Kuwasili Mkutanoni na Kujisajili
Washiriki wote

02.00-02.45
MADA: CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI KAUKI KUJILETEA MAENDELEO
1. Nini kifanyike kwa wana-KAUKI kujiletea Maendeleo?
2. Mnadhani ni vitu gani vipewe Kipaumbele kwa wanaukoo kunufaika na KAUKI!
3. Baadhi ya Malengo ya KAUKI ambayo mnayafahamu mnadhani yatasaidia kuleta mabadiliko? Na ni kwa namna gani? Jadili
4. KAUKI ni sehemu tu ya vikundi vingi vinavyofanya jitihada za kujiinua kiuchumi na kimaendeleo, mnadhani ni changamoto gani tunaipata ukilinganisha na mafanikio au matatizo ambayo yamevipata vikundi vingine? Yajadili na kuyatoa mapendekezo hayo
Wawezeshaji na washiriki wote
02.45-03.15

Majadiliano katika Makundi : Kila mshiriki ajidiliane na wana kundi kikamilifu na kutoa hoja za msingi za kujenga. Kila hoja ya msingi iwasilishwe ila kila mwanaukoo asikie.

Washiriki wote wagawanyike katika makundi

03.15-03.45
Makundi kuwasilisha hoja kutoka katika makundi yao

Washiriki wote

03.45-04.30

Majumuisho ya yote yaliyojitekeza katika Mada

Wawezeshaji

04:30 – 05:00

Pumziko la Chai / Kahawa/Maji

Washiriki Wote

05.00-06.00

Washiriki wote na Viongozi wa KAUKI
06.00-07.00
MAHITAJI YA KAUKI NA JINSI YA KUFANIKISHA KUPATIKANA KWA MAHITAJI HAYO: Huu ni mjadala wa jumla na kila mjumbe wa mkutano anashiriki moja kwa moja kutoa mawazo yake. Katibu na watendaji wengine wa KAUKI wana jukumu ya kuyanakili maswali na majibu yote kwa ajili ya kufanyiwa kazi
Washiriki na Viongozi wa KAUKI
07.00-08.00
CHAKULA CHA MCHANA
Washiriki wote
08:00–09.00
HISTORIA YA WAHEHE
1.       Kuibuka kwa tawala mbalimbali ndani ya Uhehe (Wanitole, Wahabeshi, Wangazija)
2.       Chimbuko la Koo mbalimbali mkoani Iringa
3.       Mahusiano yaliyopo baina ya koo zilizoibuka wakati wa vita za kikabila na wageni
4.       Mgawanyiko wa Koo katika Mkoa wa Iringa

1.       Mwl. Israel Mposiwa
2.       Ndg. Adam Kivenule
3.        
4.        
09:00–09:30

Pumziko la Chai/Kahawa/Maji

Washiriki wote
09.30-11:00
1.       MAJUMUISHO NA TATHMINI YA MKUTANO
2.       MIPANGO NA MIKAKATI YA MBELENI
3.       KUTANGAZWA KWA TAREHE YA MKUTANO MKUU WA SABA
4.       SHUKRANI
5.       KUFUNGA MKUTANO
VIONGOZI WA KAUKI NA Washiriki wa Mkutano Mkuu



MUUNDO WA UKOO WA KIVENULE

No comments:

Post a Comment