MKUTANO MKUU WA 10 WA KAUKI

MKUTANO MKUU WA 10 WA KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

KAUKI-Kidamali, Iringa

KAUKI-Kidamali, Iringa
Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Tuesday, March 19, 2013

KAUKI NI NINI?

E-mail: kauki2006@gmail.comKAUKI ni Umoja wa Ukoo wa Kivenule, ulioanzishwa rasmi mwaka 2005, kukabiliana na changamoto mbalimbali za maendeleo, zinazoikabili jamii inayounda umoja huu; hususani katika kujikwamua na ugumu wa maisha na pia kutumia fursa zinazopatikana ili kukabiliana na kuondokana na wimbi la umaskini, ujinga, maradhi na utegemezi. Kuanzishwa kwa KAUKI kuliambatana na maandalizi yaliyojumuisha mikutano zaidi ya 10 ya mashauriano iliyofanyika sehemu mbalimbali Jijini Dar es Salaam na Kidamali, Iringa.
Dira ya KAUKI
Kuwa na jamii elewa, angavu na inayowajibika kwa kujitegemea.
Maono ya KAUKI
Kujengeana uwezo kwa kutumia raslimali, stadi, ujuzi, maarifa na weledi, kupitia mafunzo, kongamano, mijadala na mikutano ili kuboresha maisha.
Malengo ya KAUKI
Lengo Kuu
Kuinua na kuboresha maisha ya wanaukoo wa Kivenule, kielimu, kiuchumi na kisayansi kwa kutumia ujuzi, maarifa na raslimali zinazotunguka.
Malengo mengine mahsusi
§        Kuujua na kuelewa kwa kina Chimbuko na Historia ya Ukoo wa Kivenule;
§        Kuzikusanya, kuziratibu na kuzihifadhi kumbukumbu mbalimbali za Ukoo wa Kivenule.
§        Wanaukoo kupata fursa ya kufahamiana na kutambuana;
§        Kufanya senza ya ndugu/wanaukoo wanaounda Ukoo wa Kivenule kila inapobidi kufanya hivyo na Senza hiyo itajumuisha watu waliohai na wafu;
§        Kuanzisha Mfuko wa Ukoo wa Kivenule utakaosaidia kuinua kiwango cha Elimu na pia kusomesha wanaukoo wasio na uwezo wa kumudu kulipa ada za shule au vyuo;
§        Kuboresha Elimu ndani ya Ukoo wa Kivenule ili ndugu/wanaukoo wawe na uelewa wa hali juu na kumudu mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia katika Dunia ya Utandawazi;
§        Kusuluhisha na kutatua matatizo yanayojitokeza katika Ukoo wa Kivenule kwa kupitia vikao vinavyokubalika;
§        Kuelimisha Wanaukoo/ndugu kuhusiana na madhara ya ugonjwa wa UKIMWI, matumizi ya Madawa ya Kulevya na Ulevi wa kupindukia;
§        Kuinua viwango vya maisha vya wanaukoo wa Kivenule na kuishi maisha mbadala yenye milo kamili, furaha na nyumba bora na nadhifu;
§        Kuongeza na kuimarisha mahusiano mazuri ndani na nje ya ukoo kwa kushirikiana katika matatizo mfano raha, ugonjwa, misiba pamoja na majanga makubwa;
§        Kuwa na nguvu ya kurekebisha tabia zisizostahili kwa wanaukoo/ndugu ndani ya Ukoo na kutafuta suluhu ya migogoro/migongano baina ya mtu au jamii inayotuzunguka;
§        Wanaukoo kuutambua na kuuelewa mtawanyiko/mgawanyiko wa Ukoo wa Kivenule;
§        Wanaukoo/ndugu kushirikiana katika shughuli za uzalishaji mali pamoja na utendaji kazi wa kila siku;
§        Kushirikiana na umoja au vikundi vingine vilivyoungana ili kuuletea Ukoo wa Kivenule maendeleo endelevu;
§        Kuanzisha Mfuko wa kukopeshana (SACOSS); na
§        Kupunguza au kuondoa kabisa tabia ya uvivu na uzembe ndani ya Ukoo wa Kivenule.
Muundo wa KAUKI
KAUKI inaundwa na Kanda sita ambazo ni Kidamali, Irole, Nduli, Magubike, Mufindi na Dar eS Salaam. Kwa mujibu wa Katiba ya KAUKI, kuna Mkutano Mkuu ambao ndio mkutano mkubwa kuliko yote. Hufanyika mara moja kwa mwaka. Pia KAUKI ina mikutano ya Kamati ya Utendaji ambayo hufanyika mara nne kwa mwaka kwa vipindi vya miezi mitatu mitatu. Katika Kanda pia kuna mikutano midogo midogo ambayo jukumu lake ni kujadili masuala yanayohusiana na maendeleo ya kanda. Muundo wa Uongozi wa KAUKI upo kama ifuatavyo:
 Nafasi za Uongozi Mkuu wa KAUKI
§        Mwenyekiti:                  Donath P. Mhapa       0658 843 565
§        Makamu Mwenyekiti:     Christian J. Kivenule   0714 146 382
§        Katibu Mkuu:                        Adam A. Kivenule       0713 270 364
§        Mweka Hazina               Justin D. Kivenule      0784 855 739
Nafasi za Uongozi wa Kanda
Kila kanda ina kiongozi wake ambaye ni Mwenyekiti, ambaye naye husaidiana na Katibu. Pia ndani ya Kanda kuna viongozi wa Kamati mbalimbali ambazo zipo kwa mujibu wa Katiba ya KAUKI.
Katiba ya KAUKI ndiyo mwongozi mkuu wa shughuli zote zinazofanywa na umoja huu. Katiba ya KAUKI ilipitishwa rasmi katika Mkutano MKuu wa Pili wa KAUKI uliofanyika Kidamali, Iringa.
Historia Fupi ya Kuanzishwa kwa KAUKI
Harakati za kuanzishwa kwa KAUKI zilianza kwa kuratibu mawazo ya wana-ukoo wawili, yaani Ndugu Faustino Kivenule na Ndugu Christian Kivenule mwezi Desemba 2004. Mawazo hayo yalifanyiwa kazi kwa kumshirikisha pia Ndugu Adam Kivenule, ambaye bila kuchelewa, waliweza kuandaa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mashauriano, Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa River Side, tarehe 6 Februari, 2005 – Jijini Dar es Salaam.
Harakati nyingine za maandalizi zilielekezwa upande wa Kidamali, Irore na Nduli. Kwa upande wa Kidamali, Mkutano wa Kwanza wa Mashauriano kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule, ulifanyika mwezi Mei ambapo wajumbe toka Dar es Salaam walisafiri kwenda huko ili kuwasilisha hoja, kufanya mashauriano na majadiliano, kuchagua viongozi wa kusimamia uratibu na kuunda kamati ya maandalizi.
 
Maeneo mengine kama Nduli na Irore hazikuweza kufanya maandalizi ya moja kwa moja japo taarifa toka Dar es Salaam ziliweza kufikishwa na baadhi ya wanaukoo wanaishi huko. Mjumbe mmoja tu ndugu Augustino Kivenule, toka Mgongo, Iringa ndiye aliyeweza kumudu kushiriki katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule.

No comments:

Post a Comment