MKUTANO
MKUU WA SITA WA UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI)
Kuhusu KAUKI
KAUKI ni Umoja wa Ukoo wa
Kivenule, ulioanzishwa rasmi, katika Mkutano Mkuu wa Kwanza Ukoo wa Kivenule;
uliofanyika kwa siku mbili, Kijijini Kidamali, tarehe 17 -18, mwezi Desemba, 2005.
Harakati za kuanzishwa kwa KAUKI zilianza mwezi Februari 06, 2005 Jijini Dar es
Salaam kwa kufanya mkutano mkuu wa kwanza wa mashauriano. Mikutano 10 ya
mashauriano ilifanyika kutoka mwezi Februari hadi Novemba, 2005.
Dira ya
KAUKI
Kuwa na jamii elewa, angavu na inayowajibika kwa kujitegemea.
Maono ya
KAUKI
Kujengeana
uwezo kwa kutumia raslimali, stadi, ujuzi, maarifa na weledi, kupitia mafunzo,
kongamano, mijadala na mikutano ili kuboresha maisha.
Malengo ya KAUKI
Lengo Kuu
Kuinua na
kuboresha maisha ya wanaukoo wa Kivenule, kielimu, kiuchumi na kimaisha kwa
kutumia ujuzi, maarifa na raslimali zinazotunguka.
Malengo mengine mahsusi
1. Kuujua na
kuuelewa kwa kina Chimbuko na Historia ya Ukoo wa Kivenule;
2. Kuzikusanya,
kuratibu na kuhifadhi kumbukumbu mbalimbali za Ukoo wa Kivenule.
3. Wanaukoo
kufahamiana na kutambuana;
4. Kufanya
senza ya ndugu/wanaukoo wanaounda Ukoo wa Kivenule kila inapobidi kufanya hivyo
na Senza hiyo itajumuisha watu waliohai na wafu;
5. Kuanzisha
Mfuko wa Ukoo wa Kivenule utakaosaidia kuinua kiwango cha Elimu na pia
kusomesha wanaukoo wasio na uwezo wa kumudu kulipa ada za shule au vyuo;
6. Kuboresha
Elimu ndani ya Ukoo wa Kivenule ili ndugu/wanaukoo wawe na uelewa wa hali juu
na kumudu mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia katika Dunia ya Utandawazi;
7. Kusuluhisha
na kutatua matatizo yanayojitokeza katika Ukoo wa Kivenule kwa kupitia vikao
vinavyokubalika;
8. Kuelimisha
Wanaukoo/ndugu kuhusiana na madhara ya ugonjwa wa UKIMWI, matumizi ya Madawa ya
Kulevya na Ulevi wa kupindukia;
9. Kuinua
viwango vya maisha vya wanaukoo wa Kivenule na kuishi maisha mbadala yenye milo
kamili, furaha na nyumba bora na nadhifu;
10.
Kuongeza na kuimarisha mahusiano mazuri ndani na
nje ya ukoo kwa kushirikiana katika matatizo mfano raha, ugonjwa, misiba pamoja
na majanga makubwa;
11.
Kuwa na nguvu ya kurekebisha tabia zisizostahili
kwa wanaukoo/ndugu ndani ya Ukoo na kutafuta suluhu ya migogoro/migongano baina
ya mtu au jamii inayotuzunguka;
12.
Wanaukoo kuutambua na kuuelewa mtawanyiko/mgawanyiko
wa Ukoo wa Kivenule;
13.
Wanaukoo/ndugu kushirikiana katika shughuli za
uzalishaji mali pamoja na utendaji kazi wa kila siku;
14.
Kushirikiana na umoja au vikundi vingine
vilivyoungana ili kuuletea Ukoo wa Kivenule maendeleo endelevu;
15.
Kuanzisha Mfuko wa kukopeshana (SACOSS);
16.
Kupunguza au kuondoa kabisa tabia ya uvivu na
uzembe ndani ya Ukoo wa Kivenule; na
Kuanzishwa kwa KAUKI
Harakati za kuanzishwa kwa KAUKI zilianza kwa kuratibu mawazo ya
wana-ukoo wawili, yaani Ndugu Faustino Kivenule na Ndugu Christian Kivenule
mwezi Desemba 2004. Mawazo hayo yalifanyiwa kazi kwa kumshirikisha Ndugu Adam
Kivenule, ambaye bila kuchelewa, waliweza kuandaa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa
Mashauriano, jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa
River Side, tarehe 6 Februari, 2005 – jijini Dar es Salaam.
Harakati nyingine za maandalizi zilielekezwa upande wa Kidamali, Ilole
na Nduli. Kwa upande wa Kidamali, Mkutano wa kwanza wa mashauriano kwa ajili ya
maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule, ulifanyika
mwezi Mei ambapo wajumbe toka Dar es Salaam walisafiri kwenda huko ili
kuwasilisha hoja, kufanya mashauriano na majadiliano, kuchagua viongozi wa
kusimamia uratibu na kuunda kamati ya maandalizi.
Maeneo mengine kama Nduli na Ilole hazikuweza kufanya maandalizi ya
moja kwa moja japo taarifa toka Dar es Salaam ziliweza kufikishwa na baadhi ya
wanaukoo wanaishi huko. Mjumbe mmoja tu ndugu Augustino Kivenule, toka Mgongo
ndiye aliyeweza kumudu kushiriki katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Umoja wa Ukoo
wa Kivenule.
Mkutano Mkuu wa Sita wa
KAUKI
Huu ni Mkutano Mkuu wa Sita wa KAUKI; na tayari mikutano mingine mitano
imekwisha fanyika, mitatu kijijini Kidamali na mkutano moja kijijini Irole na
Nduli. Kwa utaratibu uliokubalika katika Mkutano Mkuu wa Pili na wa Tatu wa
KAUKI, kuwa itabidi mikutano hii pia ifanyike sehemu nyingine. Na leo hii ni
zamu yenu na ndiyo maana mkutano huu wa sita unafanyika hapa Magubike. Katika
Mkutano Mkuu wa Tano wa KAUKI uliofanyika Nduli, washiriki wa mkutano huo kwa
pamoja walikubaliana kuwa Mkutano Mkuu wa Sita ufanyike Magubike, leo tarehe 26
na 27 ya Mwezi Juni mwaka 2010.
Maandalizi ya Mkutano
Mkuu wa Sita wa KAUKI - Magubike
Ili kuhakikisha kuwa Mkutano Mkuu wa Sita unafanyika na kufanikiwa,
kila Kanda ililazimika kufanya maandalizi kwa utaratibu wake. Kwa hiyo kulikuwa
na kanda za Kidamali, Magubike, Irole, Nduli na Dar es Salaam ambazo mara
nyingi Uongozi umekuwa ukipokea taarifa zake. Kila kanda inaelewa majukumu yake
ambayo ni pamoja na kukusanya michango, kuhamasisha ushiriki wa wanandugu katika Mkutano wa Sita wa KAUKI
huko Magubike na pia utoaji wa michango.
Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Sita wa KAUKI ilibidi yaanze mapema tu
mara baada ya kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Tano wa KAUKI. Maandalizi ya
mkutano huu ni jukumu la kila mwana-ukoo ambapo atashiriki kwa kutoa mchango,
nafaka, mfugo au nguvu zake katika kuhakikisha kuwa maandalizi ya mkutano
yanaenda vizuri.
Shughuli za KAUKI zinafanyika chini ya mwongozo ambao ni Katiba ya
Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI). Katiba hii ilishaanza kutumika mara tu baada
ya Mkutano Mkuu wa Pili wa KAUKI uliofanyika tarehe 24 na 25 Juni 2006. Nakala
kadhaa za KAUKI tayari zimetolewa, kusambazwa na zinaendelea kutumika.
Kwa mujibu
wa Katiba ya KAUKI, kuna viongozi mbalimbali waliochaguliwa katika Mkutano Mkuu
wa Pili. Viongozi hao wanajulikana kama Viongozi wa Kanda. Kila Kanda ambayo
ilikubalika kuwepo, katika Mkutano Mkuu wa Pili wa KAUKI, ina viongozi siyo
zaidi ya mmoja. Viongozi hawa, wanawajibika kwa wanaukoo wanaotoka katika Kanda
husika.
Wajibu wa
viongozi hawa, ni kushirikiana pamoja na Viongozi wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule
katika kutekeleza masuala mbalimbali ya maendeleo yanayouhusu ukoo. Pia, ni
wajibu wa viongozi hawa, kuwashauri Viongozi wa KAUKI katika masuala mbambali
yanayoukabili ukoo wetu kwa mfano masuala ya ugonjwa, elimu, uchumi na
maendeleo.
Viongozi wa
Kanda wana nguvu ya Kikatiba katika kutimiza wajibu wao na pia wana wajibu wa
kuhakikisha kuwa mipango mbalimbali inayopangwa kupitia Kamati Kuu au Mkutano
Mkuu wa KAUKI inatekelezwa.
Viongozi wa
ngazi nyingine za juu kama Katibu, Mwenyekiti, Makamu wa Katibu, Makamu wa
Mwenyekiti, Mweka Hazina na Msaidizi wake, wana wajibu wa kuwahimiza viongozi
wa Kanda, kushirikiana baina yao wenyewe na pia kushirikiana na viongozi wakuu
kutekeleza wajibu na majukumu mbalimbali ambayo yanatukabili.
Kwa mujibu
wa KAUKI, viongozi wa Kanda, wana wajibu kuhudhuria vikao mbalimbali kama
inavyoainishwa kwenye Katiba ya KAUKI. Wajibu huo pia unawagusa viongozi
wengine wa KAUKI na wanawajibika ipasavyo kutekeleza na kutimiza wajibu wao.
MICHANGO YA MFUKO WA KAUKI
Kama
ilivyokubaliwa kwenye Mkutano Mkuu wa Pili wa KAUKI na kama Katiba inavyoeleza,
kila mwanaukoo, anawajibika kulipa michango kama inavyoanishwa kwenye Katiba ya
KAUKI . Katiba ya KAUKI inafafanua kwa mapana kuhusiana na michango hiyo ya
kila mwezi. Katiba ya KAUKI, inaeleza wazi kuhusiana na wajibu wa kila
mwanaukoo kuchangia maandalizi ya Mkutano Mkuu wa KAUKI (Ibara ya 5:3(ii). Matumizi
ya michango hiyo ni kuwasaidia wanaukoo katika matatizo mbalimbali ya ugonjwa,
masomo na pia kiuchumi pindi mfuko huo utakuwa umetuna kutokana na kila
mwanaukoo kuuchangia ipasavyo. Pia michango hiyo itasaidia gharama mbalimbali
mfano kufanya mikutano.
Viongozi wa
Kanda, walipewa jukumu la kukusanya michango hiyo. Kwa mujibu wa makubaliano
yaliyofikiwa katika Mkutano Mkuu wa Tatu wa KAUKI, stakabadhi zikiwa na mhuri
wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI), zilisambazwa kwa viongozi husika wa Kanda
kwa ajili ya shughuli za ukusanyaji wa michango hiyo. Kila anayetoa mchango ni
lazima apewe stakabadhi ya malipo halali na si vinginevyo.
Taarifa kuhusiana na suala la michango, viongozi wa kanda watatoa taarifa
zaidi.
Lakini
viwango hivi vinavyotajwa kwenye Katiba havimfungi mwanaukoo kutoa zaidi. Mara
nyingi katika utoaji wa michango kwa ajili ya maandalizi ya Mikutano Mikuu,
kadi huandaliwa na kusambazwa kwa wana ndugu mbalimbali na pia kwa jamaa na
marafiki zetu. Jambo hili ni nzuri kwa sababu linaonyesha heshima kwa yule
unayemwomba atoe mchango wako. Kwa sababu hiyo, kadi maalum huandaliwa na kila
mmoja wetu ambaye anahitaji kadi hupewa kwa kiwango kile kinachotakiwa.
Pia,
viongozi wa KAUKI walipendekeza wanaukoo kuwa wabunifu katika kutoa michango
yao, hii ni pamoja na kutoa bidhaa au mazao ambayo yatajulikana kama mchango.
Kama ni nafaka au mifugo, inaweza kutumika kama chakula moja kwa moja au
ikauzwa na zikapatikana fedha ambazo zitajumuishwa kwenye bajeti inayoandaliwa.
MICHANGO TOKA VYANZO VINGINE
Tubuni
miradi ambayo inaweza kutuboreshea mapato ya KAUKI na pia kila mwana-ukoo
ahusike kikamilifu. Pia, hii kazi kwa viongozi wa mipango ya maendeleo kuwa
wabunifu wa shughuli mbalimbali za uzalishaji mali. Tunaweza kubuni miradi ya maandazi,
chapati, mama lishe, kilimo au miradi yoyote ambayo mnadhani itatusadia
kupata fedha kwa ajili ya kuweza kufanikisha mikutano kama hii.
TAREHE YA MKUTANO MKUU WA SITA WA KAUKI
Tarehe 26 ya
Jumamosi na 27 Jumapili Juni 2010, ilipendekezwa kuwa ndiyo siku ambapo Mkutano
Mkuu wa Sita wa KAUKI utafanyike Magubike.
YATAKAYOJIRI KATIKA MKUTANO MKUU WA SITA WA KAUKI
Kwa
mujibu wa ratiba ya mkutano, kutakuwa na shughuli mbalimbali katika siku mbili
za mkutano. Pamoja na mambo mengine, kutakuwepo na uwasilisha wa mada kadhaa na
pia taarifa mbalimbali kutoka kwa wana-KAUKI na viongozi, mfano:
·
Mada: 1.CHIMBUKO
NA HISTORIA YA UKOO WA KIVENULE
2. CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI KAUKI KUJILETEA
MAENDELEO
3. HISTORIA YA WAHEHE
·
TAARIFA YA UTENDAJI WA KAUKI
·
TAARIFA YA SHUGHULI ZA MAENDELEO KATIKA
KANDA
·
KUSOMA RIPOTI YA MKUTANO MKUU WA TANO
WA KAUKI
·
UZOEFU WA WANAUKOO KATIKA SHUGHULI ZA
MAENDELEO
·
MAJADILIANO YA HOJA MBALIMBALI AMBAZO
ZIMEWASILISHWA NA WASHIRIKI KATIKA MKUTANO
·
MAHITAJI YA KAUKI NA JINSI YA
KUFANIKISHA KUPATIKANA KWA MAHITAJI HAYO: Huu ni mjadala wa jumla na kila
mjumbe wa mkutano anashiriki moja kwa moja kutoa mawazo yake. Katibu na
watendaji wengine wa KAUKI wana jukumu ya kuyanakili maswali na majibu yote kwa
ajili ya kufanyiwa kazi
·
MAJUMUISHO NA TATHMINI YA MKUTANO
·
MIPANGO NA MIKAKATI YA MBELENI
·
KUTANGAZWA KWA TAREHE YA MKUTANO MKUU
WA SABA
·
SHUKRANI
·
KUFUNGA MKUTANO
Utambulisho
baina ya wanaukoo utafanyika kwa kina na kila ndugu/mwanaukoo atakuwa na
kitambulisho ambacho atakivaa kifuani kwake. Kutakuwa na fursa mbalimbali kwa
wanandugu kupeana uzoefu mbalimbali wa utafutaji wa maisha bora. Mbinu za
kujiinua kimaisha zitafundishwa na wadau wenye uzoefu pamoja na aina mbalimbali
za miradi ambayo ndugu wanaweza kufanya.
Tutakuwa na
kipindi cha kupeana uzoefu wa shughuli mbalimbali za kiuchumi kutoka katika
maeneo mbalimbali ambako ndugu wanaishi. Kama ilivyofanyika katika Mkutano Mkuu
wa Tatu wa KAUKI, maeneo yatakayotolewa uzoefu Kilimo, biashara na ajira kutoka
katika maeneo mbalimbali. Kwa kupeana elimu ya ujasiliamali itasaidia kutufungua
macho na hivyo kuongeza uwezo wa kufikiri na kwenda kutafuta maisha katika
maeneo ambayo ni mbadala kwetu. Pia taarifa hizi zitawasaidia wanandugu toka
maeneo mengine kupata mwanga wa shughuli mbadala zitakazosaidia kupata kipato
na kuboresha maisha.
Pia huu ni
mwaka wa uchaguzi. Tunategemea kuwa wana-ukoo wataitumia fursa hii ipasavyo
kuwachangua viongozi wanaoona wanafaa kuiongoza jumuiya yetu.
UCHAGUZI MKUU WA VIONGOZI WA KAUKI
Taarifa
kuhusu uchaguzi wetu tayari ilikwisha tolewa kwenye tovuti yetu inayoitwa: http://www.tagumtwafoundation.wetpaint.com
. Natumaini ni watu wachache tu wamemudu kuiangalia na lakini bado kama
viongozi tuna wajibu wa kuwatambulisha katika mkutano huu. Wafuatao ni viongozi
wapya waliochaguliwa:
VIONGOZI WAKUU WA KAUKI
1. Mwenyekiti Donath Mhapa
2. Makamu
Mwenyekiti
3. Katibu Mkuu Adam Kivenule
4. Katibu
Msaidizi Christian Kivenule
5. Mweka Hazina Justine
Kivenule
6. Mweka Hazina
Msaidizi
UCHAGUZI WA WALEZI WA KAUKI
Wafuatao ni
Walezi wa KAUKI………………………………….
VIONGOZI WA KANDA
Kila Kanda
itakuwa na wawakilishi wawili
1. Mwenyekiti
2. Katibu
3. Mweka Hazina
Kutakuwa na Viongozi wa Kamati mbalimbali
A. Mipango
na Maendeleo
- Mwenyekiti:
- Katibu:
B. Mahesabu
na Fedha
- Mwenyekiti:
- Katibu:
C. Maafa na
Matatizo
- Mwenyekiti:
- Katibu:
D. Nidhamu
na Maadili
- Mwenyekiti:
- Katibu:
Angalizo: Viongozi wa Kamati ya
Mahesabu na Fedha, watashirikiana na Mweka Hazina katika kuratibu shughuli zote
za ukusanyaji wa michango mbalimbali, wakati wa maafa, wakati wa mkutano mkuu,
mikutano na pia mchango wa kila mwezi.
MIPANGO YA KAUKI
KAUKI inajikita kujiimarisha katika ngazi zote za kiutendaji,
kiuendeshaji na kuleta mabadiliko ya kiuchumi, kielimu, kisiasa, kimaendeleo,
na kimapinduzi. Baadhi ya mikakati KAUKI ni pamoja na:
1. KAUKI kuwa
na ofisi yake Kijijini Kidamali na pia sehemu nyingine za Kanda ambapo wanaukoo
wanadhani ni muhimu kuwa na ofisi. Jambo hili
lilishaanza kufanyiwa kazi na pia eneo ambalo inabidi ofisi iwepo lilishapatikana
katika majadilian ya awali ya mwaka 2008. Viongozi toka eneo ambalo ofisi
inabidi ifunguliwe watatuhabarisha zaidi wapi wamefikia.
2. Suala na
pili ni kupata usajili ili tuwe na fursa ya kufanya shughuli kubwa zaidi. Bado suala hili lipo katika mchakato, na taratibu nyingine
zote za namna ya kupata usajili zilikwisha fuatiliwa. Ni matumaini yetu uongozi
mpya uliochaguliwa, unalifanyia kazi kazi jukumu hili muhimu.
3. KAUKI kuwa
na sanduku lake la posta. Bado jambo hili halijatekelezwa
na natumaini hatua za makusudi inabidi zichukuliwe. Hakuna masharti makubwa
zaidi ya kulipa fedha tu. Ni changamoto kwa viongozi wa KAUKI na nadhani hatuna
haja ya kusubiri zaidi ya kuchukua hatua zinazostahili kulikamilisha hili.
4. Kuwa na
Akaunti katika Benki yeyote. Ufunguzi wa Akaunti
ulikwisha fanyika kabla ya Mkutano Mkuu wa Nne wa KAUKI uliofanyika Irole. Hima
wanaukoo tutoe michango yetu na pia tusaidie kuitunisha akaunti yetu. Wangapi
wanalipa mia tano za kila mwezi? Mnapata stakabadhi? Wangapi bado hawajalipa?
Kwa nini? Hizi ndizo changamoto kwetu. Bila kujitoa hatuwezi
kufanikiwa. Msitegemea watu wachache tu ndio wanaoweza kubadili maisha ya
wanaukoo wote. Inabidi tuunganishe nguvu zetu wote. Wahenga walisema, ‘Umoja ni
nguvu na utengano ni udhaifu’.
5. KAUKI kuwa
na vitendea kazi mfano Kompyuta, Printa, Simu, Meza na Viti. Bado kutekelezwa kutokana na uhaba wa fedha na pia bado
wanaukoo hawajaonesha mwito wa kutoa michango ya kila mwezi. Hivyo tunawahimiza
kutoa michango hiyo ili baadhi ya mipango na malengo ya KAUKI yakamilike.
Tutafanya harambee ili tuweze kununua vifaa hivyo, mfano Kompyuta na printa
yake. Wangapi mpo tayari kuchangia?
6. KAUKI kuanza
kutoa elimu mbalimbali kwa wadau wake. Tumeanza na
sehemu ndogo na mojawapo ni wakati wa mikutano hii. Lakini bado tunadhani
inabidi tutafute fursa nyingine. Kama tungekamilisha suala la ofisi, natumaini
fursa nyingi za kupata masomo kwa wana-ukoo zingetafutwa kwa hali na mali.
7. KAUKI kubuni
na kutekeleza miradi mbalimbali ambayo itawasadia wanajamii. Sijapata taarifa rasmi labda viongozi wa Irole wanaweza
kutupa taarifa. Mwenyekiti wa kipindi kilichopita Bwana Nyakunga aliahidi kuwa
wangeanzisha mradi wa alizeti, Sijui walifikia wapi? Tupatieni taarifa.
Tuanzishe mashamba ya KAUKI na kila kanda iwe na shamba lake. Mazao yatakayopatikana
yatatumika kama sehemu ya chakula wakati wa mikutano hii. Na pia iliyobaki
itauzwa na fedha kuwekwa katika mfuko wa KAUKI.
8. KAUKI kuwa
na kitengo cha Utaalam wa Kitaaluma na Kiujuzi ambacho kitafanya shughuli za
kuiletea fedha KAUKI, pamoja na miradi mbalimbali. Tunasubiri
kukamilika kwa ofisi na kazi itaanza mara moja. Binafsi nipo tayari kujitolea
kuhakikisha tunafanikiwa katika suala hili.
9. KAUKI
kujitangaza kwa asasi nyingine za ndani ya nchi na nje kwa kutumia teknolojia
ya kisasa yaani kuwa na tovuti. Tumeanzisha tovuti (blog) na natumaini bado haijafikiwa na
wengi. Mpango mzuri ni sisi wenyewe kulisajili jina la KAUKI (Domain
Registration) kwa wamiliki wa mitandao na kuiweka hewani tovuti yetu kwa watoa
huduma za mawasiliano ya tovuti na mitandao.
10.
Kuchapisha kitabu toleo la kwanza cha Umoja wa
Ukoo wa Kivenule kwa kipindi cha mwaka 2008 – 2009. Kamati
iliyoundwa imeshindwa kukutana na kuikamilisha kazi hiyo kutokana na sababu
mbalimbali zikiwemo za:
- Kukosa pesa
- Mtawanyiko wa wajumbe
- Shughuli yenyewe inahitaji pesa kwa mfano kazi ya uhariri na uchapishaji
Kutokana shughuli kuwa ngumu na kushindwa kufanyika kama
ilivyopangwa, inabidi kamati iwasilishe taarifa na mapendekezo kwa wajumbe
kuhusu hatua ambazo imechukua na nini imekifanya; na pia nini kifanyike, kwa
kurejea hadidu zake na pia majukumu yaliyopaswa kufanyika kabla ya mkutano huu
wa tano.
MAPUNGUFU YA KAUKI NA WATENDAJI WAKE
Uongozi wa
KAUKI bado umeonyesha mapungufu na hii pia inaathiri mfumo mzima wa utendaji
kazi zake. Baadhi ya mapungufu hayo ni pamoja na kushindwa kubisa kutekeleza
baadhi ya mikakati ambayo ilikuwa ni sehemu ya makubaliano na pia mipango ya
mbeleni ya maendeleo ya KAUKI. Kwa mfano baadhi ya majukumu ambayo bado
hayajatekelezwa ni pamoja na:-
1. Kutokuwa na
Kalenda ya Shughuli za Mwaka;
2. Kushindwa
kufanya vikao vya Kamati Kuu;
3. Ushirikiano
finyu baina ya viongozi wa ngazi mbalimbali wa KAUKI kutokuwepo kwa mpango-kazi,
tathmini ya utendaji kazi na utekelezaji wa mipango ya maendeleo;
4. Viongozi
wengi wa KAUKI kushindwa kutekeleza wajibu wao;
5. Makusanyo
hafifu ya michango; Wangapi wamelipa mpaka muda huu?
6. Viongozi
kutokuwa mfano mzuri katika kutoa michango. Tunaamini kiongozi lazima awe ni
mfano wa kuigwa; Je viongozi wote mnatoa michango ya kila mwezi. Wangapi wamelipa
mpaka muda huu?
7. Wanaukoo
kuonesha mwitikio duni katika ushiriki wa Mikutano Mikuu. Mfano wa Wanaukoo
kutoka Dar es Salaam; na
8. KAUKI
kutokuwa na ofisi. Ni mwaka wa pili sasa jambo hili ilibidi liwe limekamilika
lakini mpaka sasa bado ofisi haijaanza kufanya kazi. Hii ni changamoto kwa
viongozi wetu.
VIONGOZI WAKUU WA KAUKI
1. Mwenyekiti Donath P. Mhapa
2. Makamu
Mwenyekiti
3. Katibu Mkuu Adam A. Kivenule
4. Makamu Katibu
5. Mhasibu Mkuu Justin D. Kivenule
Walezi
1. Stephan Mhapa
2. John Kivenule
3. Augustino Kivenule
HITIMISHO
K
|
AUKI imeendelea kujikita katika kuongeza uangavu na weledi kwa wanaukoo
kutokana na kutambua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika dunia hii ya
utandawazi. Mazingira na hali halisi iliyopo ambayo kila mwana-KAUKI anaiona,
ameguswa nayo au kuathiriwa nayo ni vigezo tosha. Propaganda na kejeli kama
kauli mbiu kutoka kwa watu mbalimbali duniani hususiani kwa wanasiasa wetu yameendelea
kuwaathiri wana-KAUKI na watanzania kwa ujumla. Tatizo la ufisadi wa raslimali
za watanzania mkiwemo ninyi, rushwa katika huduma za jamii mfano kukosa dawa
hospitalini, maji safi ya kunywa, elimu duni na ukosefu wa ajira, vyote
vinamwathiri sisi. KAUKI inaamini kuwa mwana-KAUKI mwenyewe ndiye mwenye uamuzi
wa mwisho ya kuamua hatma na mustakali wa maisha yake ya sasa na baadaye. KAUKI
haitarajii maisha bora kwa kila mwana-KAUKI au mtanzania mwingine yataletwa na
wanasiana au watu baki waliopo nje ya nchi yetu. Jukumu la maendeleo ni letu
sisi wenyewe. Ndio maana tunahimiza watu kujitoa kwa hali na mali kuuchangia mfuko
wetu ili uweze kuisaidia jamii yetu katika nyanja zote za kiuchumi, elimu, afya
na maendeleo.
Yote yanayofanyika katika mikutano hii ni sehemu ndogo ya jitihada
kubwa zinazofanywa na KAUKI. Ahadi za wanasiasa ni za mdomoni tu na hatuamini
hata siku moja kama wana-KAUKI mtayafurahia maisha bora kwa kukaa mtu moja moja
au kwa kutounganisha nguvu zenu. Wanasiasa wana-agenda zao ambazo mara nyingi
huwa kuangalia maslahi yao na kuyalinda. Mfano wa hivi karibuni kwa Wabunge wameomba
kujiongezea mshahara hadi kufikia milioni kumi na mbili kutoka milioni saba (7)
wanazolipwa sasa. Mishahara hiyo ni kodi za maskini sisi wana-KAUKI na wenzetu
ambao hawapo hapa. Kwa hiyo suala la kujikwamua kimaendeleo la kila mmoja wetu
hapa na si vinginevyo. Hizi ni mojawapo ya harakati za kujikwamua na lindi la
umaskini unaotukabili. Lakini harakati nyingine unazifanya wewe kama
mwana-KAUKI wakati wa kupiga kura yako kumchagua kiongozi. Msilemae na rushwa.
Tumieni vizuri fursa yenu kwa kuchagua viongozi bora. Pengine hata katika
chaguzi wa viongozi wa KAUKI watu wanaweza kutoa rushwa ili wachaguliwe!
Tumieni fursa zinazopatikana kwa kuwahoji wale wanaotaka nafasi za uongozi,
nini kimewatuma kugombea nafasi hizo, na sisi kama wana-KAUKI tutarajie nini.
Jamii yetu ni maskini wa kila kitu, wataisaidiaje?
Siasa za porojo zimepitwa na wakati. Kama wana-KAUKI inabidi kuhimiza
mabadiliko ya kiitikadi na kimaendeleo. Wajibu watu ni kuwadhihirishia nini
tunakusudia kukifanya ili kuboresha maisha yetu. Maisha bora kwa kila mtanzania
kama mnavyoahidiwa katika kampeni za uchaguzi ni ndoto tu.
Kwa mfano huu ni mwaka wa tano toka uchaguzi mkuu ufanyike na wananchi
mliahidiwa maisha bora kwa kila mtanzania. Je haya maisha mnayoishi kweli ni
maisha bora ukilinganisha na maisha mliyokuwa mnaishi siku za nyuma. Mfumuko wa
bei, kupanda kwa bei za mafuta kila wakati, njaa, ufisadi, dhuluma na kejeli na
hata vifo kwa wapigania haki za wanyonge. Hii ni hali ya kukatisha tamaa na
sisi wana-KAUKI tuna kila wajibu na kukabiliana na hali hii.
Tukikaa pembeni na kuacha yatokee basi nasi tutaangamia kwani
kinachofanyika kinatuathiri sisi. Ufisadi na wizi wa mali ya umma unatuathiri
sisi. Kwa mfano kukosekana kwa huduma za msingi mfano huduma za afya, shule
bora, maji na bei kubwa ya umeme ni matokeo ya dhuluma hizi. Hivyo kama
wana-KAUKI bado tuna jukumu kubwa la kukabiliana na kila aina ya uozo, na adui
wa maisha na maendeleo yetu.
Mbadala ya maendeleo ya nchi ya Tanzania unakutegemea wewe mwana-KAUKI,
dhima, uamuke toka sasa na uelekeze nguvu zako katika kuiboresha KAUKI ili
jamii yetu ipate maendeleo.
Mwisho
Imetolewa
na:
___________________________
___________________________
Donath Mhapa Adam
A. Kivenule
No comments:
Post a Comment