Iringa ni mji mkubwa uliopo Nyanda za
Juu Kusini mwa Tanzania.
Ni makao makuu ya Mkoa wa Iringa na eneo lake ni Wilaya ya Iringa Mjini. Idadi ya wakazi ni
mnamo 112,000.
Asili ya jina la Iringa ni neno
la Kihehe "liliga" lenye maana ya boma. Mji umejengwa juu ya mlima
ukitazama mto
Ruaha bondeni.
Mji uko kando la barabara kuu
ya Tanzania Zambia na kuna usafiri wa kila siku kwenda Dar es
Salaam na Mbeya.
Njia kwenda Dodoma
ni sehemu ya barabara ya kale ya "Cape-Cairo" kati ya Rasi ya Afrika
Kusini na Kairo
wa Misri lakini
kwa sasa ni barabara ya udongo tu.
Iringa ilianzishwa mwaka 1892
kama kambi la jeshi la kikoloni wakati wa vita ya
Wajerumani dhidi ya Wahehe. Mji wa leo upo mahali pa "Neu Iringa"
au Iringa mpya ya Wajerumani waliotumia jina hili baada ya kuharibu boma la
mtemi Mkwawa huko Kalenga
waliloita "Iringa" tar. 31 Oktoba 1894.
KABILA la Wahehe ambalo linapatikana mkoani Iringa, ni miongoni mwa
makabila maarufu nchini ambalo halipo nyuma katika suala zima la kuenzi Mila na
Tamaduni zake.
Wakati huo eneo ambalo sasa
linaitwa Iringa lilikuwa na makabila mbalimbali. Walikuwepo ‘Wahafiwa’ katika
Bonde la Milima Welu, Luvango, Wutinde, Lugulu, Makongati, Kalenga, Kipagala,
Kihesa, Tambalang’ombe, Ibanagosi, Tipingi, Ikolofya, Nyambila, Kibebe na
Isanzala.
‘Vanyategeta’ wao walioishi
Udzungwa, Kitelewasi na Lundamatwe, ambao walikuwa wahunzi hodari. ‘Vanyakilwa’
walilowea Mufindi wakitokea Kilwa; ‘Vasavila’ waliishi milima ya Welu huko
Makungu (Kihanga ya sasa), Magubike na Malangali; na ‘Vadongwe’ waliishi kando
ya milima ya Uhambingeto, Ipogolo, Nyabula na Luhota.
Mbali
na Kabila la Wahehe, Mkoa wa Iringa pia unakaliwa na Kabila la Wabena,
Wapangwa, Wawanji na Wakinga. Japo sasa una mchanganyiko wa makabila
mengine.
Kihehe ni lugha ya Kibantu
nchini Tanzania
inayozungumzwa na Wahehe.
Hali kadhalika, Lugha ya Kihehe ya Kabila la
Wahehe imegawanyika kutokana na Lahaja. Lahaja ni
vilugha vidogovidogo vya lugha moja ambavyo hubainika kijamii au kijiografia.
Lahaja za lugha moja zatofautiana katika matamshi, miundo ya sarufi na
msamiati. Kama lugha hutofautiana katika matamshi tu, tofauti hizo huitwa
lafudhi na siyo lahaja. Uchambuzi na uchanganuzi wa lahaja ni tawi la
isimujamii.
Wahehe
wenyewe wanaweza kusikilizana bila tatizo lolote ila huweza kutambua ni mahali
gani Mhehe huyu anatoka mfano Wahehe Vasungwa ambao wengi wao wanatoka eneo la
Dabaga.
Suala
la kuthamini tamaduni wanazorithi toka kizazi kimoja hadi kingine, ni moja ya
sababu zilizowafanya Wahehe wajizolee sifa sehemu mbalimbali ndani na nje ya
nchi.
Miongoni
mwa sifa ambazo kabila hili limejizolea ni pamoja na uvumilivu, ujasiri, uchapaji kazi ambapo kwao kilimo cha mazao
ya chakula ni msingi mkubwa wa maendeleo katika familia.
Anapobainika mtu mvivu,
hudharauriwa na kuchekwa na ukoo mzima pamoja na jamii inayomzunguka.
Baadhi
ya mazao yanayolimwa mkoani humo ni pamoja na mahindi, mtama, mihogo, alizeti,
kunde, maharage, viazi vitamu, viazi mviringo, karangaa na ulezi.
Katika
kilimo, kabila hili hufanya ushirikiano kwa namna ya kualikana baina ya mtu
mmoja na mwingine na ushirikiano wa namna hii, hujitokeza wakati wa kupalilia
na kuvuna.
Ukifika
wakati wa mavuno, mtu anayesaidiwa kazi kwa siku hiyo huandaa pombe, togwa na
kande kwa ajili ya wasaidizi wake. Kitendo hicho cha kualikana katika kazi
huitwa ‘Mugove’.
Kulingana
na mila za kabila hilo, hususan katika suala la kuandaa chakula, ni kwamba
endapo mzazi mmoja atakuwa hayupo, mzazi anayekuwepo humsubiri mwenzake ili
aungane naye katika mlo. Hii mara nyingi hufanyika kama kuna uhakika wa mzazi
huyo kurudi mapema.
Hali ni tofauti kwa watoto kwani endapo mtoto
wa kiume au wa kike atakuwa hayupo bila sababu maalumu, kimila haikubaliki hata
kidogo kuwekewa chakula.
Chakula
hicho ambacho huandaliwa na mwanamke au msichana hugawanywa katika makundi
matatu. Mafungu haya ni pamoja na fungu la
wazazi, wavulana na kundi la tatu ni watoto wa kike.
Katika kabila hilo, afikapo
mgeni hushikana mkono wa kulia na mwenyeji wake na kila mmoja huanza
kuubusu mkono wa mwezake kwa kupokezana mmoja baada ya mwingine zaidi ya mara tatu
na kitendo hicho huitwa ‘Kinonela’/Kwinonela.
Mhehe
katika kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo, mara nyingi hupenda
kujisimamia mwenyewe ambapo huamini kuwa kusimamiwa ni kudhalilishwa au kudharauliwa.
Kabila
hili pia, bado lina imani za kishirikina ambapo baadhi ya maeneo mkoani humo
watoto wa vikongwe pamoja na ukoo wao huogopwa kwa namna moja au nyingine,
hususan katika suala la kugombea
mashamba likiwemo la wanafunzi.
Vile
vile wanafunzi hushindwa kufanya vizuri katika mitihani yao kwa kuhofia kufa. Siyo hivyo tu, hata
kufanya shughuli za maendeleo mfano kujenga nyumba nzuri lilikuwa ni hatari
sana siku nyuma, japo kwa sasa linapungua. Pengine mchanyiko wa makabila
umepunguza imani hizi na kuchochea maendeleo.
Pamoja
na kuwaogopa vikongwe miongoni mwa kabila hili huamini kuwa “Kufa
konoga” wakimaanisha “kufa kupendeza”
.
Usemi
huu wa 'kufa kunoga' kwa Mhehe ni
sehemu ya kujitia moyo na humuondolea hofu katika kukabiliana na matatizo
mbalimbali ambapo kufa kwao ni jambo la kawaida kama ilivyopangwa na Mungu‘Nguluvi’.
Ugomvi
mkubwa unaweza kutokea endapo mtu mmoja
kutoka ukoo fulani atamnyooshea kidole mtu wa ukoo mwingine kwa lengo la
kumkemea ‘Kufingulisa’/kufingula.
Kitendo
hicho kikitokea yule aliyenyoshewa kidole huamini kuwa endapo atatokewa na baya
lolote, litakuwa limetokana na yule aliyemnyooshea kidole.
Kabila hili la Wahehe, pia lipo mstari wa mbele katika suala la
imani ambapo huomba baraka toka kwa Mwenyezi Mungu ili kuweza kutatuliwa
matatizo mbalimbali na kuomba neema na msamaha.
Kwa mujibu wa maelezo kutoka kwa Mzee Albeto Lyakumba (63), kutoka Kijiji cha Lungemba mkoani
humo, katika kabila hilo mtu anapokufa ndugu zake hawatakiwi kulia mapema mno,
badala yake wanatakiwa kutulia kimya takribani saa moja baada ya kifo hicho./
Hufanya hivyo kwa lengo la kupata muda wa kutosha kuuweka vizuri mwili wa
marehemu (maiti).
“Kitendo
cha mtu kufa akiwa amekodoa macho au viungo vyake havijakaa sawia huwa
tunakilaani sana, hivyo tunatumia muda huo kuuweka vizuri kwa kutumia mafuta ya
samli kuhakikisha kuwa vinakaa jinsi inavyotaakiwa,” anasema Mzee Lyakumba.
Anasema
mwili wa marehemu huzikwa kwa kutazama Mashariki kwa kuaamini kuwa, ndiko
walikotokea Wahehe ‘kwetuhumile’ tulikotoka na katika baadhi ya
koo ndani ya kabila hili, mfu hukalishwa kwenye kiti anapozikwa.
Siku ya tatu baada ya maziko, ukoo huhesabu idadi ya vyombo na nguo
alizoacha marehemu na kupanga siku ya matanga ambayo hutumika pia, kugawa vitu hivyo.
Mkubwa katika familia aliyoiacha marehemu hupewa nafasi ya kwanza
kuchukua kitu kimoja baada ya kingine anachokipenda. Hufuatiwa na wadogo zake
na baadhi ya watu kama mjomba, bibi, babu, kwa kufuata taratibu za kimila.
Kwa
upande wa ngoma, kabila hilo hucheza ‘kwa
kufunga kengele na njuga ‘Mangala’
miguuni huku wakicheza kwa kumzunguka
mpiga ngoma.
Aidha,
ngoma hizo huchezwa wakati wa kufanya tambiko pamoja na siku ya kugawa vyombo
vya marehemu na endapo marehemu ameacha watoto, familia ile huamini watatunzwa
pasipo kushindwa ‘vana vakiva nunzaa sivandema’ yaani watoto
yatima nitawatunza hawatanishinda ni sehemu ya wimbo anaoimbiwa marehemu
aliyeacha watoto.
Kwa
kufuata mila na desturi za Kabila hili,
nafasi ya mwanamke awali alikuwa kama kichwa cha familia ambapo
alitegemewa na watoto kuwalipia ada na mambo mengine mengi tofauti na sasa.
Katika
enzi hizo mwanamke alitakiwa kufanya
kazi nyingi zaidi kuliko mwanamume.
Alijishughulisha na mambo mbalimbali kikiwemo kilimo, kupika,
kuokota kuni, kuchota maji, kumbembeleza mtoto pamoja na kujishughulisha na biashara
ndogo ndogo kwa ajili ya kuitunza familia.
Vile
vile, si jambo la ajabu kwa mwanamke wa kabila hili kutumiwa na mme wake kwa
ajili ya kumtongezea mwanamke ambaye wakati mwingine anaweza kuwa mke mwenza.
Asili ya nyumba za kabila hili ni za udongo ambapo paa la nyumba huezekwa kwa
kutumia nyasi kavu tu, na nyingine
hutupiwa mchanga juu yake ili kuepuka kuunguzwa.
Ujenzi
wa nyumba hujengwa kulingana na familia
iliyopo kwa kuzingatia jinsia.
Kuhusu
suala la mifugo, wanaume ndio wanaoipeleka malishoni huku wakiwa wamebeba mkuki
au mundu na fimbo.
Mvulana
wa kabila hili akifikia hatua ya kubarehe huingizwa katika kundi la watu
wazima kwani sasa anachukuliwa kuwa anao uwezo wa kufanya kazi mbalimbali
hususan kilimo na katika ujenzi wa nyumba.
Pia,
hufundishwa namna ya kuishi na watu
mbalimbali katika mazingira tofauti.
Aidha,
kijana huyo hupewa shamba lake ili kumuandalia maisha ya kujitegemea.
Sambamba na hayo, msichana akipewa mimba wakati bado yupo kwa
wazazi na endapo atakataa kumtaja aliyempa mimba, basi huaminika kuwa
amechafua nyumba ikiwa na maana kwamba mimba hiyo imetoka ndani ya nyumba
anayoishi.
Katika kumtia msukosuko zaidi familia husika, ukifika wakati wa
kujifungua msichana huyo hutishiwa kuwa
asipomtaja mwanaume aliyempa mimba atakufa.
Na kwa kuogopa kifo, hulazimika kumtaja mhusika wa hiyo mimba.
Juu ya suala la uchumba, kabila hili huzingatia mambo
mbalimbali ikiwemo tabia ya uchapaji
kazi hususan kilimo na kuangalia kama ana uwezo wa kuimarisha familia.
Posa ikishakubalika,upande wa mwanaumme hutoa Jembe kama kitanguliza Uchumba
‘Mkaja’ .
Mwanamke
anapopata mimba akiwa ndani ya ndoa
baada ya miezi saba tangu aolewe, mama yake anaenda kuomba ruhusa kule
aliko olewa ili akaishi naye hadi siku atakapo jifungua na baada ya kujifungua
hurudishwa kwa mumewe. Kuna mengi ya kujifunza katika kabila hili kwa ajili ya
faida ya kizazi kijacho.
No comments:
Post a Comment