UTAFITI WA KAUKI
Umoja wa Ukoo wa
Kivenule (KAUKI) upo katika mchakato wa utafiti kuhusiana na chanzo, muundo na
mgawanyiko wa Ukoo wa Kivenule, na pia mwingiliano na jamii zingine. Utafiti
huu umechukua takribani miaka nane na bado unaendelea kufanyika katika maeneo
mbalimbali.
Utafiti huu pia
utaangalia Koo mbalimbali ambazo zimeingiliana na Ukoo wa Kivenule na pia Ukoo
wa Kivenule ulivyoweza kuingia katika koo nyingine. Pia, utafiti utatathmini
athari hasi na chanya za mwingiliano huu na pia uhusiano wa Koo mbalimbali
katika himaya ya Uhehe.
Pia utafiti utagusa maeneo ya chimbuko la koo mbalimbali ndani ya uhehe, miiko na historia mbalimbali za koo zilizopo katika mkoa wa Iringa. Pia utaangalia uhusiano uliopo baina ya Kabila la Wahehe na Wabena.
Utafiti utaenda mbali zaidi na kuangalia mila na desturi za wahehe, aina za vyakula, tamaduni mbalimbali zinazotawala kabila hili na mengine mengi.
Kwa kuzingatia umuhimu wake, KAUKI inawaomba wakazi wote wa Mkoa wa Iringa, ambao ni Wahehe kwa Asili, kushiriki kikamilifu katika kujaza dodoso lililopo chini ya kipande hiki cha maelezo.
Kama una swali au maoni, naomba ututumie kupitia anuani hizi:
E-mail: kauki2006@gmail.com
kivenule@gmail.com
tagumtwa.kauki@gmail.com
Blog:
http://www.kauki-kauki.blogspot.com
http://www.tagumtwa.blogoak.com
http://www.adamkivenule.blogspot.com
Facebook:
http://www.facebook.com/kivenule
Twitter:
http://www.twitter.com/kivenule
Simu: +255 0713 270364
Bonyeza link hii kufungua dodoso
http://adamkivenule.blogspot.com/2013/01/dodoso-la-utafiti-wa-kauki.html
No comments:
Post a Comment