HISTORIA FUPI YA KAUKI
KAUKI ni Umoja wa Ukoo wa Kivenule, ulioanzishwa rasmi
mwaka 2005, kukabiliana na changamoto mbalimbali za maendeleo, zinazoikabili
jamii inayounda umoja huu; hususani katika kujikwamua na ugumu wa maisha na pia
kutumia fursa zinazopatikana ili kukabiliana na kuondokana na wimbi la
umaskini, ujinga, maradhi na utegemezi. Kuanzishwa
kwa KAUKI kuliambatana na maandalizi yaliyojumuisha mikutano zaidi ya 10 ya
mashauriano iliyofanyika sehemu mbalimbali Jijini Dar es Salaam na Kidamali, Iringa.
Dira ya KAUKI
Kuwa
na jamii elewa, angavu na inayowajibika kwa kujitegemea.
Maono ya KAUKI
Kujengeana uwezo kwa kutumia
raslimali, stadi, ujuzi, maarifa na weledi, kupitia mafunzo, kongamano,
mijadala na mikutano ili kuboresha maisha.
Malengo ya KAUKI
Lengo Kuu
Kuinua na kuboresha maisha ya
wanaukoo wa Kivenule, kielimu, kiuchumi na kisayansi kwa kutumia ujuzi, maarifa
na raslimali zinazotunguka.
Malengo mengine mahsusi
§
Kuujua na kuelewa kwa kina
Chimbuko na Historia ya Ukoo wa Kivenule;
§
Kuzikusanya, kuziratibu na
kuzihifadhi kumbukumbu mbalimbali za Ukoo wa Kivenule.
§
Wanaukoo kupata fursa ya
kufahamiana na kutambuana;
§
Kufanya senza ya
ndugu/wanaukoo wanaounda Ukoo wa Kivenule kila inapobidi kufanya hivyo na Senza
hiyo itajumuisha watu waliohai na wafu;
§
Kuanzisha Mfuko wa Ukoo wa
Kivenule utakaosaidia kuinua kiwango cha Elimu na pia kusomesha wanaukoo wasio
na uwezo wa kumudu kulipa ada za shule au vyuo;
§
Kuboresha Elimu ndani ya Ukoo
wa Kivenule ili ndugu/wanaukoo wawe na uelewa wa hali juu na kumudu mabadiliko
ya Sayansi na Teknolojia katika Dunia ya Utandawazi;
§
Kusuluhisha na kutatua
matatizo yanayojitokeza katika Ukoo wa Kivenule kwa kupitia vikao
vinavyokubalika;
§
Kuelimisha Wanaukoo/ndugu
kuhusiana na madhara ya ugonjwa wa UKIMWI, matumizi ya Madawa ya Kulevya na
Ulevi wa kupindukia;
§
Kuinua viwango vya maisha vya
wanaukoo wa Kivenule na kuishi maisha mbadala yenye milo kamili, furaha na
nyumba bora na nadhifu;
§
Kuongeza na kuimarisha
mahusiano mazuri ndani na nje ya ukoo kwa kushirikiana katika matatizo mfano
raha, ugonjwa, misiba pamoja na majanga makubwa;
§
Kuwa na nguvu ya kurekebisha
tabia zisizostahili kwa wanaukoo/ndugu ndani ya Ukoo na kutafuta suluhu ya
migogoro/migongano baina ya mtu au jamii inayotuzunguka;
§
Wanaukoo kuutambua na kuuelewa
mtawanyiko/mgawanyiko wa Ukoo wa Kivenule;
§
Wanaukoo/ndugu kushirikiana
katika shughuli za uzalishaji mali pamoja na utendaji kazi wa kila siku;
§
Kushirikiana na umoja au
vikundi vingine vilivyoungana ili kuuletea Ukoo wa Kivenule maendeleo endelevu;
§
Kuanzisha Mfuko wa kukopeshana
(SACOSS); na
§
Kupunguza au kuondoa kabisa
tabia ya uvivu na uzembe ndani ya Ukoo wa Kivenule.
Muundo wa KAUKI
KAUKI inaundwa na Kanda sita
ambazo ni Kidamali, Irole, Nduli, Magubike, Mufindi na Dar eS Salaam. Kwa
mujibu wa Katiba ya KAUKI, kuna Mkutano Mkuu ambao ndio mkutano mkubwa kuliko
yote. Hufanyika mara moja kwa mwaka. Pia KAUKI ina mikutano ya Kamati ya
Utendaji ambayo hufanyika mara nne kwa mwaka kwa vipindi vya miezi mitatu
mitatu. Katika Kanda pia kuna mikutano midogo midogo ambayo jukumu lake ni
kujadili masuala yanayohusiana na maendeleo ya kanda. Muundo wa Uongozi wa
KAUKI upo kama ifuatavyo:
Nafasi za Uongozi Mkuu wa
KAUKI
§
Mwenyekiti: Donath P. Mhapa 0658 843 565
§
Makamu Mwenyekiti: Christian J. Kivenule 0714 146 382
§
Katibu Mkuu: Adam A. Kivenule 0713 270 364
§
Mweka Hazina Justin D. Kivenule 0784 855 739
Nafasi
za Uongozi wa Kanda
Kila kanda ina kiongozi wake
ambaye ni Mwenyekiti, ambaye naye husaidiana na Katibu. Pia ndani ya Kanda kuna
viongozi wa Kamati mbalimbali ambazo zipo kwa mujibu wa Katiba ya KAUKI.
Katiba ya KAUKI ndiyo mwongozi
mkuu wa shughuli zote zinazofanywa na umoja huu. Katiba ya KAUKI ilipitishwa
rasmi katika Mkutano MKuu wa Pili wa KAUKI uliofanyika Kidamali, Iringa.
Historia Fupi ya Kuanzishwa kwa KAUKI
Harakati za kuanzishwa kwa KAUKI zilianza kwa
kuratibu mawazo ya wana-ukoo wawili, yaani Ndugu Faustino Kivenule na Ndugu
Christian Kivenule mwezi Desemba 2004. Mawazo hayo yalifanyiwa kazi kwa
kumshirikisha pia Ndugu Adam Kivenule, ambaye bila kuchelewa, waliweza kuandaa
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mashauriano, Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo
ulifanyika katika ukumbi wa River Side, tarehe 6 Februari, 2005 – Jijini Dar es
Salaam.
Harakati nyingine za maandalizi zilielekezwa upande
wa Kidamali, Irore na Nduli. Kwa upande wa Kidamali, Mkutano wa Kwanza wa
Mashauriano kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Umoja wa Ukoo
wa Kivenule, ulifanyika mwezi Mei ambapo wajumbe toka Dar es Salaam walisafiri
kwenda huko ili kuwasilisha hoja, kufanya mashauriano na majadiliano, kuchagua
viongozi wa kusimamia uratibu na kuunda kamati ya maandalizi.
Maeneo mengine kama Nduli na Irore hazikuweza
kufanya maandalizi ya moja kwa moja japo taarifa toka Dar es Salaam ziliweza
kufikishwa na baadhi ya wanaukoo wanaishi huko. Mjumbe mmoja tu ndugu Augustino
Kivenule, toka Mgongo, Iringa ndiye aliyeweza kumudu kushiriki katika Mkutano
Mkuu wa Kwanza wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule.
Mkutano Mkuu wa Kumi (10) wa KAUKI
Huu ni Mkutano Mkuu wa Kumi wa
KAUKI ambao unafanyika nyuma ya mikutano mingine Tisa ambayo imekwisha fanyika,
mitatu Kijijini Kidamali na Mkutano moja moja Kijijini Irole, Nduli, (Iringa
Vijijini), Igowole (Mufindi) na mara mbili Magubike Mkoani Iringa, na Mkutano
mmoja Jijini Dar es Salaam (Karibu na Tabata Shule). Kwa mujibu wa makubaliano
na utaratibu ambao umewekwa na Wana-KAUKI, mikutano hii itakuwa inafanyika
katika ngazi ya Kanda, ili kuipa fursa jamii inayounda KAUKI kushiriki moja kwa
moja. Lakini pia, vipaumbele huwekwa pale ambapo kuna idadi kubwa ya wana-KAUKI,
lakini huridhiwa wakati wa Mkutano Mkuu. Kwa msingi huo, Mkutano Mkuu wa Tisa
wa KAUKI, kwa kauli moja, uliazimia kuwa Mkutano Mkuu wa Kumi ufanyike katika
Kanda ya Kidamali, Iringa Vijijini, tarehe 28– 29 ya Juni, 2014.
Angalia picha za matukio
katika Mkutano Mkuu wa Nane wa KAUKI uliofanyika Jijini Dar es Salaam, Juni 30
- Julai 1, 2012
http://www.facebook.com/photo.php?fbid=497523093617046&set=a.497521733617182.1073741825.100000780786862&type=1&theater
Kwa taarifa zaidi, angalia http://www.tagumtwa.blogoak.com
http://www.facebook.com/tagumtwa na http://www.twitter.com/tagumtwa
TANGAZO
MKUTANO
WA KUMI (10) WA UMOJA WA UKOO WA KIVENULE-KAUKI
Uongozi wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI), kwa heshima na taadhima,
unachukua fursa hii kuwatangazia Wana-KAUKI wote, Ndugu, Jamaa na Marafiki,
wanaoishi mijini na vijijini kutoka katika Mikoa yote ya Tanzania Bara; Mkutano
wa Mkuu wa Kumi (10) wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI), utakaofanyika katika
Kijijini Kidamali, Wilayani ya Iringa Vijijini, Mkoani Iringa; kuanzia tarehe 28
- 29 Juni, 2014.
Wana-KAUKI Wote na Wapenda Maendeleo kwa Ujumla,
na wale wote wanaoguswa na harakati zetu, wanaombwa kusaidia maandalizi ya
Mkutano huo kwa kuchangia fedha, nafaka na raslimali nyingine, ambazo zitasaidia
kufanikisha kufanyika kwa mkutano huo, pamoja na huduma muhimu kama chakula,
kabla, wakati na baada ya Mkutano huo, kwa wageni wote.
Kwa niaba ya Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu
wa 10 wa KAUKI, inakuomba/inawaomba
Pia nachukua fursa hii kuwakaribisha jamaa na
marafiki ambao wanapenda kujifunza namna KAUKI inavyofanya kazi kwa kipindi cha
miaka 8, toka umoja huu ulipoanzishwa rasmi mwaka 2005.
Kwa taarifa mbalimbali kuhusiana na shughuli za
KAUKI na matukio mbalimbali katika mikutano yetu, matatizo ya kijamii mfano
misiba na mengine mengi fungua http://www.tagumtwa.blogoak.com pia tunapatikana
kupitia http://www.facebook.com/kivenule na www.twitter.com/kivenule
Natanguliza
shukrani zangu za dhati,
Wako katika kazi,
Adam Kivenule
KATIBU MKUU-KAUKI
No comments:
Post a Comment