I:
UTANGULIZI
Harakati endelevu za kuleta mabadiliko
na maendeleo zinakua kwa kasi kubwa na hivyo kuchochea mabadiliko ya haraka ya
hali bora za maisha ulimwenguni kote. Harakati kama hizo zinazotegemea sana
uwepo wa Sayansi na Teknolojia, Elimu na Uchumi endelevu; zinatoa fursa na
hamasa kwa jamii huria nazo kubuni na kutafuta mbinu mbadala za kuweza kujiinua
ili kuweza kukabiliana na hali hiyo. Mabadiliko hayo yanayozungumziwa ni pamoja
na kukua kwa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kupitia Kopyuta yaani Internet
na simu za mkononi (computer, Internet and cellphones), Soko Huria, Utandawazi
na Ubinafsishaji.
Jamii huria kwa upande wake zinapata
hamasa na changamoto ya kuweza kutafuta mustakabali wake kutokana na hali
halisi ya maendeleo inavyoendelea kukua kwa kasi na athari zake kuonekana moja
kwa moja katika maisha yetu ya kila siku kwa upande mmoja; na pia mafanikio
kuonekana kwa upande mwingine.
Wimbi la umaskini uliokithiri, janga la
UKIMWI, ujinga na rushwa vimekuwa ni vikwazo vikubwa vya maendeleo na ambavyo
vinazidi kudidimiza harakati mbalimbali za kuweza kujiinua na kujikwamua katika
hali hiyo. Harakati hizi za kutafuta maendeleo zimegawanyika katika makundi
mbalimbali ya kijamii hususani makundi ya wasomi, wafanyabiashara, wanawake na
wananchi wa kawaida.
Kutokana na harakati hizo, wanajamii
wanaounda Ukoo wa Kivenule nao hawako nyuma katika kuhakikisha kuwa jamii yao
inaondokana na umaskini, ujinga pamoja na UKIMWI; na hivyo kupata fursa ya
kuishi katika Dunia Mbadala [Alternative World] iliyojisheheneza katika sayansi
na teknolojia.
Kwa kutambua hilo, wanajamii na ndugu
wanaounda UKOO wa KIVENULE, kwa pamoja toka mwezi Februari 06, 2005,
walianzisha harakati za kuinasua jamii yao kutoka kwenye lindi la umaskini,
ujinga na maradhi kwa kuunda Kamati ya kuuza na kuratibu Maandalizi ya Mkutano
Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa KIVENULE; ambao ulipangwa kufanyika katika Kijiji cha
Kidamali, Wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa, hapo tarehe 17 hadi 18
Desemba 2005. Katika mapendekezo ya awali, Uongozi uliochaguliwa kuunda kamati
ya maandalizi na uhamasishaji, ilipanga kuwepo na Kamati Tatu za Maandalizi ya
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, yaani Kamati iliyopo mkoani Dar es
Salaam, Kamati ya Kijijini Kidamali na ya Ilole – Iringa, zote zikiwa zimepewa
majukumu mazito ya kusaidia kufanikisha mkutano huo.
Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Kivenule awali ulitegemea
kuwaalika ndugu na wageni wapatao mia mbili (200) toka Kijijini Kidamali, Ilole,
Nduli, Kihesa, Ilula, Magubike, Kinyamlewa, Nzihi, Iringa Mjini, Kalenga,
Ipogolo, Museke, Kitwilu, Igowolo, Kiponzelo, Mafinga, Mufindi, Maduma, Wasa,
Ifunda, Tosamaganga, Kilombero, Morogoro, Dodoma na Dar es Salaam; na sehemu
nyingine nyingi ambako wanajamii wanaounda ukoo huo wanaishi ili waweze kupata
fursa ya kushiriki kikamilifu.
Ukoo wa Kivenule ukiwa umejiwekea
malengo mahususi katika kuandaa mkutano huo, pia uliazimia pamoja na mambo
mengine, kufundisha jamii inayounda ukoo huo, Mada Tano zenye msukumo wa kimaendeleo.
Mada zilizopendekezwa kufundishwa katika siku mbili za mkutano huo zilikuwa ni pamoja
na:
1. HISTORIA NA CHIMBUKO LA UKOO
• Ukoo ni Nini na Unapatikanaje?
• Dhana ya Kuenea na Kukua kwa Ukoo.
• Mgawanyiko wa Ukoo (Chora Mchoro Kuonyesha
Ukoo unavyoundwa).
• Kupotea kwa Ukoo.
2. MAHUSIANO BAINA YA NDUGU NDANI YA UKOO
• Ukaribu wa Wana Ndugu.
• Ushirikiano Katika Nyanja Mbalimbali.
• Kutembeleana kama Sehemu ya Kudumisha
Mahusiano.
• Kuondoa Tofauti na Kusaidiana.
3. ELIMU NA MUSTAKABALI WA UKOO
• Nafasi ya Ukoo wa Kivenule katika Elimu.
• Umuhimu wa Elimu.
• Dunia ya Utandawazi.
• Nini Kifanyike Kuinua Elimu Katika Ukoo
Wetu.
4. UKIMWI NDANI
YA UKOO NA ATHARI ZAKE
• UKIMWI ni nini?
• Namna gani UKIMWI
unavyoenea/kuambukizwa?
• Njia Mbadala za Kujilinda na
Maambukizi?
• Jukumu la Ukoo/Familia
Kukabiliana na Janga la UKIMWI.
5. DINI KATIKA UKOO
• Maana ya Dini
• Umuhimu wa Kuwa na Imani
• Maadili na Dini
• Ukoo Uliojengeka katika Misingi
ya Dini
Wawezeshaji mbalimbali
wenye ujuzi katika mada hizo walipatikana baada ya kamati kuchukua jukumu la
kuwatafuta ikiwamo kupata Mtaalam wa UKIMWI toka TAHEA.
Mojawapo ya hamasa
kubwa ya kuandaa mkutano huu ilikuwa ni pamoja na suala nzima la mahusiano
ndani ya wanandugu, wanaukoo na jamii kwa ujumla. Suala la ELIMU, ATHARI ZA
UKIMWI katika jamii ya ukoo wa Kivenule na taifa nzima. Pia haja ya kufahamiana
baina ya wanajamii na ndugu wanaounda ukoo, pamoja na kuujua Ukoo kwa ujumla.
Pamoja na mambo
mengine, kamati ilifikiria pia uwezekano wa kufanya senza ili kujua idadi ya
ndugu wanaounda ukoo husika toka kona mbalimbali hapa Tanzania; kujua nini
wanakifanya na kujua idadi sahihi ya wanandugu ambao wanahitaji msaada wa namna
moja au nyingine.
Katika suala nzima la
Kufahamu Historian na Chimbuko la Ukoo, Mahusiano baina ya wanandugu ndani ya
ukoo, Elimu, Maadili na Dini na gonjwa hatari la UKIMWI, Kamati ilionelea kuwa
ni mojawapo ya mambo msingi sana kuyaangalia katika shughuli nzima ya
maandalizi na wakati wa Mkutano Mkuu.
Changamoto zitakazopatikana
baada ya kuyagusia mambo haya ya msingi na hivyo kuwawezesha washiriki wa
mkutano mkuu kujenga ajenda mpya.
Mahusiano duni baina
ya wana ndugu, kukosekana kwa ushirikiano katika mambo mbalimbali ya
kimaendeleo, hali duni ya kiuchumi na kijamii, matatizo ya kifamilia na kiukoo
ni kati ya masuala ya msingi yaliyofikiriwa sana kabla ya kuanza kufanya
maandalizi ya Mkutano Mkuu.
Mwelekeo na nafasi ya
ukoo wa Kivenule katika suala nzima la Elimu hasa katika dunia hii ya
Utandawazi (Globalization). Maendeleo ya sayansi na teknolojia ambapo
yameifanya dunia kuwa kama kijiji kisicho na mipaka na kila mtu anaruhusiwa
kuingia na kutoka; kuongezeka kwa viwanda vinavyotumia teknolojia ya hali ya
juu; kuongezeka kwa teknolojia ya habari na mawasiliano (Internet); kupanuka na
kujengeka kwa miji, pamoja na soko huria.
Mambo yote haya ndiyo
yanayoweza kuonyesha mustakabali na nafasi ya ukoo wa Kivenule kwa maisha ya
baadaye. Ilionekana kuwa ukoo wetu upo nyuma sana katika suala nzima la elimu,
hii linajidhihirisha kutokana na kuwa na ndugu wachache sana ambao wameweza
kupata elimu kwa kiwango kinachostahili.
Hii ni hatari kwa
sababu tunajenga ukoo tegemezi ambayo baadaye utakosa mwelekeo. Mabadiliko ya
Sayansi na Teknolojia yanayojitokeza kila kukicha yanaibadili dunia na hivyo
kutulazimisha nasi katika ukoo wa Kivenule kubadilika. Matumizi ya teknolojia
ya habari na mawasiliano katika simu za mikononi, Internet, kompyuta, redio na
satelaiti ni changamoto kubwa katika Ukoo wa Kivenule.
Maambukizo ya ugonjwa
wa UKIMWI ambayo kwa kiasi kikubwa yameathiri familia nyingi zikiwemo familia
zetu sisi wana ukoo, yanapaswa kutopuuzwa bali kuwekewa mikakati madhubuti.
Ufahamu kuhusiana na gonjwa lenyewe livyoenea na madhara yake katika jamii,
njia mbadala za kujilinda na maambukizi ya ugonjwa wenyewe pamoja na kuitikia
mialiko mbalimbali ya wanajamii wanaopambana na janga hili ni mambo ya msingi
sana ambayo yalijadiliwa kwa kina kwenye mkutano huo.
Ilipendekezwa kuwa,
wakati wa mkutano huo kutakuwa na nafasi kutoa uzoefu katika mambo mbalimbali
ya kitaalum na maendeleo. Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Ukoo yalianza mapema
ili kumpa fursa kila mwanajamii/mwanaukoo kutafakari na kujadili kwa kina,
kujiandaa pamoja na kuwasilisha mchango wake wa mawazo kwa kamati husika za
kuratibu maandalizi.
Mkutano Mkuu wa Ukoo umeazimia kutoka na kitu muhimu ambacho ndicho
kitakuwa mwongozo na dira ya shughuli mbalimbali zitakazokuwa zinafanyika
katika ukoo.
Licha ya kuwa na malengo na makusudio mbalimbali, pia tunategemea mwisho wa
mkutano kutakuwa na mambo kadhaa ambayo yatakuwa ni makubaliano kutoka pande
mbalimbali za ukoo wa Kivenule. Yote hayo kwa pamoja yatakuwa ni maazimio ya
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule.
Kati ya Maazimio ambayo Kamati iliyategemea kuyatekeleza katika Mkutano Mkuu
wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ni pamoja na:
- Kufanyika kwa Senza ya Ukoo wa Kivenule ili kupata idadi kamili ya ndugu.
- Kuanzisha Mfuko wa Ukoo ambao utasaidia katika kusomesha watoto wanaofaulu pamoja na kusaidia katika matatizo mbalimbali yanayojitokeza au uhitaji wa msaada.
- Kuchagua Viongozi wa Ukoo pamoja na Wajumbe Wawakilishi watakaounda Kamati ya Ukoo ya Kuratibu mambo mbalimbali ya ukoo. Nafasi za Viongozi watakaochaguliwa zitajumuisha Mwenyekiti, Makamu wa Mwenyekiti, Katibu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina na Msaidizi wake pamoja na Walezi Watatu wa kushauri uongozi uliopo madarakani.
- Kuzitaja/kutamka bayana kazi/majukumu mbalimbali ambayo Uongozi utakaoundwa utakuwa unazifanya mfano kufanya mashauriano na usuluhishi wa matatizo mbalimbali ya ukoo yaliyojitokeza. Lakini pia jukumu lao kubwa ni kuongoza na kusimamia majukumu mbalimbali yanayojitokeza au kuhitaji usimamizi ndani ya ukoo.
- Kukusanya taarifa mbalimbali za ukoo; na
- Kuangalia na Kutathmini usalama wa mali mbalimbali zinazomilikiwa na ukoo nk.
II: UUNDAJI WA KAMATI ZA
MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA
KWANZA WA UKOO
Kamati mbili za kuratibu Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa
Kivenule ziliundwa. Kamati ya Kwanza ilikuwa ni Kamati ya Dar eS Salaam ambayo
uliundwa mwezi Februari 06, 2005 na Kamati ya Pili kuundwa ni ile ya Kidamali
ambayo iliundwa mwezi Mei 2005. Uundaji wa Kamati ya Dar es Salaam na ile ya
Kidamali uliendana na uchaguzi wa viongozi wa kuziendesha na kuzisima-mia
kamati hizo. Kwa upande wa wanaukoo na ndugu wanaoishi Dar es Salaam na mikoa
ya karibu kama Morogoro, Dodoma na Mikumi waliingia kwenye Kamati ya Dar es
Salaam.
Kamati ya Kidamali iliwaunganisha wanaukoo na ndugu wote wanaoishi maeneo
ambayo yapo karibu na Kidamali mfano Magubike, Nzihi, Kalenga, Nyamihuu, Idete
na kwingineko.
Kwa upande wa Kamati ya Dar es Salaam, viongozi walikuwa kama ifuatavyo:-
1. Christian
Kivenule Mwenyekiti
2. Adam
Kivenule Katibu
3. Athuman
Mtono Makamu
Mwenyekiti
4. Edgar
Kivenule Mshauri wa Kamati
5. Innocent
Kivenule Mweka Hazina
6. Ignas Kivenule Mshauri
Kamati ya Ilole
Na kwa upande wa Kamati ya Kidamali, viongozi waliochaguliwa walikuwa kama
ifuatavyo:-
1. Faustin
Kivenule Mwenyekiti
2. Augen
Kivenule Makamu Mwenyekiti
3. Jovin
Kivenule Katibu
4. Carolina
Kivenule Katibu Msaidizi
5. Justin
Kivenule Mweka Hazina
6. Donati
Mhapa Mshauri
7. Pyela
Kivenule Mshauri
8. Daniel Kivenule Mshauri
Kamati zote mbili zilikuwa na washauri,
ambao nao pia walichaguliwa siku hiyo hiyo ya kuwachagua viongozi. Kazi ya
washauri ilikuwa ni kuzishauri Kamati zote mbili katika kutekeleza majukumu
yake.
A: KUHAMASISHA/UHAMASISHAJI
Mwezi Mei
2005, viongozi wanaounda Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo
wa Kivenule toka Dar es Salaam, walisafiri kwenda Kidamali – Iringa wakiwa na
lengo mahsusi la Kuhamasisha wanaukoo wanaoishi Kidamali na maeneo ya Karibu
kuhusiana na Maandalizi ya Mkutano wa Ukoo.
Tendo la Uhamasishaji lilienda sambamba
na kuundwa kwa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa
Kivenule kwa Upande wa Kidamali. Jukumu la Kamati hiyo iliyoundwa ilikuwa ni:
Kuhamasisha wanaukoo toka maeneo
mbalimbali yanayozunguka Kidamali kujitokeza kwa wingi siku ya Mkutano Mkuu wa
Kwanza wa Ukoo wa Kivenule;
Kutoa michango ili kufanikisha
maandalizi ya Mkutano Mkuu; na
Kusambaza kadi za michango kwa wanandugu
na wadau mbalimbali ambao wanaweza kusaidia kuchangia maandalizi ya Mkutano
Mkuu.
B: UCHANGAJI WA MICHANGO
Kamati zote mbili ya Kidamali na Dar es
Salaam zilitekeleza ipasavyo jukumu la uchangiaji wa michango. Kwa upande wa
Kamati ya Dar es Salaam, zoezi la uchangiaji michango halikuwa na mafanikio
sana ukilinganisha na mafanikio yaliyojitokeza upande wa Kidamali.
Ukusanyaji wa michango ulifanyika kwa
kusambaza kadi za kuomba mchango wa kufanikisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa
Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Viwango wa vichango vilitofautiana kwa wale
wanaoishi mijini na pia kwa wale wanaoishi vijijini.
Kwa wanandugu wanaoishi mijini waliombwa
wachangie shilingi Elfu Kumi na Tano tu (15,000/=); na kwa wenzetu wanaoishi
maeneo ya vijijini waliombwa wachangie shilingi Elfu Tano tu (5,000) au kitu
chochote chenye thamani ya fedha hiyo mfano kutoa kuku au mazao (mahindi au
maharage).
C: MWITIKIO KATIKA UCHANGAJI MICHANGO
Wanaukoo wanaoishi Kidamali na maeneo ya
karibu walionyesha mwitikio wa hali juu sana kwa kutoa michango yao kwa moyo.
Karibu robo tatu ya michango iliyofanikisha Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa
Kivenule ilitoka Kidamali na maeneo yake ya Karibu. Jamii kuna sehemu kadhaa
zilionyesha kusita katika kutoa michango yao katika kipindi cha awali,
ilibadili msimamo wake katika dakika za mwisho.
Kamati iliamini kuwa kutokuwa na hamasa
wakati wa awali pengine ilitokana na kutoelewa dhumuni la michango hiyo. Mara
baada ya kubandika matangazo ya kuutangaza Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa
Kivenule, wanaukoo wengi toka maeneo mbalimbali walijitokeza kutoa michango
yao.
Wanaukoo wanaoishi Dar es Salaam
hawakufanya vizuri katika kutoa michango. Ni ndugu wachache tu ndio
waliojitokeza kutoa michango yao. Wengi wa wanandugu/wanaukoo walitoa sababu mbalimbali
za matatizo mfano kutokuwa na ajira na pia kutomudu kutoa kiasi hicho cha pesa.
Tatizo la utoaji wa michango lilienda sambamba na mahudhurio duni kwenye vikao
vilivyoitishwa. Hadi dakika za mwisho za maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza
wa Ukoo wa Kivenule, ni wanaukoo chini ya kumi ndiyo waliokuwa wametoa michango
yao.
III: TATHMINI YA MAANDALIZI
YA MKUTANO MKUU WA KWANZA WA
UKOO KIVENULE
Kamati zote mbili za
maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ile ya Kidamali nay a
Dar es Salaam, zilikaa pamoja ili kuweza kufanya tathmini ya shughuli nzima ya
maandalizi ya Mkutano Mkuu yaliyofanyika kati ya mwezi Februari na Novemba
2005.
Lengo la kuzikutanisha Kamati
zote mbili ilikuwa ni kufanya tathmini ya hatua za maandalizi zilizofikiwa kwa
ajili ya kufanikisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule.
Ilionekana dhahiri kuwa Kamati ya Maandalizi ya Kidamali ilifanya vizuri zaidi,
huku Kamati ya Maandalizi toka Dar es Salaam – ikionyesha kuelemewa kutokana na
mwitikio duni wa wanaukoo waishio eneo hilo la mjini.
Kamati zote mbili za
Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ya Kidamali na Dar es
Salaam, zilifanikiwa kukusanya jumla ya shilingi 345,350.00 mpaka siku ya mwisho ilipofanyika tathmini ya ukusanyaji
wa michango wa Kamati zote mbili.
Kamati ya Dar es Salaam
ilijitahidi kufanya maandalizi ya moja kwa moja katika harakati za Maandalizi
ya Mkutano Mkuu wa kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Maandalizi hayo yalihusisha
uandalizi wa Kadi za Michango (Kadi za Kawaida na Kadi Maalum). Kadi za kawaida
ziligawanyika katika makundi mawili, yaani kadi za Shilingi Elfu Kumi na Tano
(15,000/=) na kadi za Shilingi Elfu Tano (5,000/=). Kadi Maalum zilikuwa
mahsusi kwa watu au taasisi maalum zilizoombwa kuuchangia Mkutano Mkuu wa
Kwanza wa Ukoo wa Kivenule.
Jukumu jingine lilifanyika na
Kamati ya Dar es Salaam ilikuwa ni uandaaji na uchapaji wa minitisi za vikao
mbalimbali na kuzisambaza, uandaaji wa Mabango ya kuutangaza Mkutano Mkuu wa
Kwanza wa Ukoo wa Kivenule kwa ajili ya kubandikwa maeneo mbalimbali.
Pia Kamati ya Dar es Salaam
iliandaa vitambulisho kwa ajili ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo
wa Kivenule. Lengo ilikuwa ni kuhakikisha kuwa kila mshiriki anakuwa na
kitambulisho wakati Mkutano ukiendelea.
IV: UUNDAJI WA KAMATI ZA KURATIBU MKUTANO
Kamati mbalimbali ziliundwa ili kuweza
kufanikisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Kamati
kadhaa ziliundwa ili kuratibu shughuli na majukumu mbalimbali wakati Mkutano
ukiendelea. Kamati hizo zilizoundwa ni pamoja na:
1. Kamati ya Chakula
2. Kamati ya Ulinzi
3. Kamati ya Vinywaji
4. Kamati ya Mapokezi
5. Kamati ya Burudani
Kila Kamati ilikuwa na msimamizi wake
ili kuhakikisha kuwa kila jambo linafanyika kama ilivyopangwa katika Ratiba.
Kwa kiwango kikubwa, kila Kamati iliyopewa jukumu la kutekeleza wakati wa
Mkutano Mkuu ilifanya vizuri na kwa ufanisi wa hali ya juu. Kamati zilizoundwa
zilishirikisha wanaukoo, majirani na marafiki na hivyo kutoa hamasa kubwa
katika kutekeleza majukumu. Majirani na marafiki waliwaomba wanandugu/wanaukoo
toka Ukoo wa Kivenule kuwa mstari wa mbele katika kutekeleza majukumu yao ili
wawe chacho kwa wengine wasio wanaukoo.
V:
UTEUZI WA WAWEZESHAJI WA MADA
Wawezeshaji mbalimbali waliteuliwa na
Kamati zote mbili, yaani Kamati ya Dar es Salaam na ile ya Kidamali kuwa
Wawezeshaji wa Mada Tano zilizopendekezwa kuwasilishwa kwenye Mkutano Mkuu wa
Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Baadhi ya Wawezeshaji hao pamoja na Mada walizopewa
kuwasilisha ni:
1. CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOOO
§
Christian J. Kivenule
§
Augustino Kivenule
§
Daniel S. Kivenule
2. MAHUSIANO YA NDUGU NDANI YA UKOO
§
Stephan Mhapa
§
Ignas P. Kivenule
§
John S. Kivenule
3. ELIMU NA MUSTAKABALI WA UKOO WA KIVENULE
§
Christian J. Kivenule
§
Donath Mhapa
4. UKIMWI NA
ATHARI ZAKE NDANI YA UKOO
§
Maria Milimo
§
Adam A. Kivenule
5. DINI KATIKA UKOO
§
Jovin D. Kivenule
§
George S. Kivenule
§
Stephan Mhapa
VI:
MIALIKO KWA WANANDUGU, WANAUKOO PAMOJA NA WASHIRIKI WENGINE
Mialiko ya wanandugu pamoja na wanaukoo
kwa ujumla, kuhudhuria MKutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ilifanyika wazi
kwa kila mtu bila upendeleo, kila mwanaukoo alipewa taarifa za kufanyika kwa Mkutano
Mkuu wa Ukoo na kuombwa kuhudhuria. Aidha kamati zote mbili za maandalizi ya
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, zilikubaliana kwamba, kila
mwanandugu au mwanaukoo anapaswa kuhudhuria mkutano huo bila kukosa.
Mialiko ilifanyika kwa namna mbalimbali
ikiwemo ile ya mdomo. Yaani kumwalika mwanaukoo au ndugu moja kwa moja kwa
kumpa maelekezo kuhusiana na mahali unapofanyika mkutano mkuu, tarehe pamoja na
muda. Familia yote, yaani baba, mama na watoto, wote walipaswa kuhudhurio
mkutano mkuu huo.
Pia mialiko ilifanyika kwa kubandika
matangazo ya kuutangaza Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule sehemu
mbalimbali Kijijini Kidamali pamoja na maeneo mengine ambako Kamati ziliamini
ndugu na wanaukoo wanaishi kule.
Kila ndugu aliyefika na kuhudhuria
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, alipewa kitambulisho cha kuweza
kumtambulisha kwa ndugu wengine. Kitambulisho hicho kilionyesha namba ya
kitambulisho, jina la ndugu, mahali anapoishi na simu au sanduku la posta.
Kamati ziliepuka ile hali ya kuulizana maswali ya kuwa wewe unaitwa nani,
unaishi wapi na simu yako iko wapi? Hii ilikuwa ni sababu ya msingi ya kutoa
kitambulisho kwa kila mwanaukoo au ndugu.
VII:
UBANDIKAJI WA MATANGAZO
Ubandikaji wa matangazo ya kuutangaza
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ulifanyika sehemu mbalimbali
Kijijini Kidamali pamoja na maeneo mengine ambako Kamati ziliamini ndugu na
wanaukoo wanaishi kule, ulifanyika kwa lengo la kuwajulisha ndugu kuhusu uwepo
wa Mkutano Mkuu na wapi unafanyika.
Baadhi ya sehemu kulikobandikwa
matangazo ni pamoja na Kidamali, Magubike, Nzihi, Nyamihuu, Ipogolo na
Nyamihono. Ubandikaji wa matangazo ya Mkutano Mkuu wa Ukoo, uliibua hisia ya
kushawishika kuhudhuria kwa wanaukoo na wasio wanaukoo kuhusiana na kufanyika
kwa Mkutano huo. Wapo majirani, marafiki na watu wasio wanaukoo waliokuwa na
shauku kubwa ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule.
VIII: SIKU YA KWANZA YA MKUTANO MKUU WA KWANZA WA
UKOO WA KIVENULE, DESEMBA 17, 2006
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa
Kivenule ulifunguliwa na Mgeni Rasmi Ndugu Daima Luvanda, ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kidamali.
Awali kabla ya yote, Mwenyekiti wa
Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Mkuu wa Ukoo Ndugu Faustino Kivenule,
aliwakaribisha ndugu, jamaa na wanaukoo kwa ujumla kwenye mkutano huo.
Kabla ya kusoma hotuba ya Ufunguzi wa
Mkutano Mkuu wa Ukoo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa
Kwanza wa Ukoo, alimkaribisha Ndugu George Kivenule, kuuombea Mkutano Mkuu kwa
sala.
Baada ya Sala ya kuuombea Mkutano Mkuu,
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Ukoo, alitumia fursa hiyo
kuisoma Hotuba ya Ufunguzi.
Alianza kwa kuwajulisha ndugu, wanaukoo
na wageni waalikuwa kuwa, lengo la Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule
ni kuwaunganisha wanaukoo wote, wanaoishi sehemu mbalimbali hapa Tanzania, ili
wafahamiane, waelimishane na kupeana ujuzi katika nyanja mbalimbali za
maendeleo na kupeana uzoefu.
Pia, lengo jingine la Mkutano Mkuu wa
Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ilikuwa ni kutolewa na kufundishwa kwa Mada kadhaa
zenye nia ya kuujengea ukoo na kuwa na msimamo imara. Kwa kuwakusanya ndugu
pamoja, Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu, iliamini itasaidia kuujenga Ukoo
katika misingi ya Ushirikiano na Upendo na hiyvo kuwa na ukoo wenye umoja.
Lengo jingine la kufanya mkutano mkuu wa
ukoo ilikuwa ni kufanya senza ili kujua idadi ya wanaukoo na mwishoni kufanya
uchaguzi wa viongozi, watakaunda Uongozi wa Ukoo na pia watashirikiana na
Kamati ya Ukoo wa Kivenule katika kutekeleza majukumu mbalimbali.
Kamati itakayoundwa itakuwa na jukumu la
kuratibu mambo mbalimbali na matatizo yanayohusu ukoo.
Jumla ya Mada Tano ziliwasilishwa na
kufundishwa katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Mada
zilizowasilishwa ni pamoja na:
1. CHIMBUKO
NA HISTORIA YA UKOO;
2. MAHUSIANO
BAINA YA NDUGU NDANI YA UKOO;
3. ELIMU NA MUSTKABALI KATIKA UKOO;
4. UKIMWI NDANI YA UKOO NA ATHARI ZAKE; NA
5. DINI KATIKA UKOO.
Harakati za maandalizi
ya Mkutano Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, zilianza toka mwezi
Februari 05, 2005. Harakati hizi zilifanyika Kijijini Kidamali kwa upande mmoja
na kwa upande mwingine jijini Dar es Salaam.
Kamati zote mbili
zilizoundwa zilijipa majukumu mbalimbali, likiwemo lile la kuwaalika na
kuwashirikisha ndugu na wanaukoo katika suala zima la maandalizi ya Mkutano
Mkuu wa Ukoo katika vikao, na pia utoaji wa michango.
Katika harakati za
maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa UKoo wa Kivenule, kamati zote mbili
zilizipata vikwazo mbalimbali likiwemo tatizo la mwitikio duni katika kulipokea
wazo hili. Kwa ujumla, katika kuliuza suala/wazo hili la kuandaa na kuwa na
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, kamati ilibidi zitumiea nguvu na
mbinu za ziada ili kuweza kufanikiwa.
Mahudhurio duni
yalitoa changamoto kwa Kamati za Maandalizi ya Mkutano Mkuu, kuongeza
juhudi/jitihada na kutafuta njia mbadala za kufikia lengo. Kwa upande wa
Kijijini Kidamali, ushawishi ulizaa matunda, kwa sababu ongezeko la wanaukoo na
ndugu kuliunga mkono wazo la kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo lilivuna
washiriki wengi.
Kwa upande wa Dar es
Salaam, suala la mahudhurio duni, liliendelea kuwa ni kikwazo kwa kipindi chote
cha maandilizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Wapo waliodiliki
kusema Mkutano Mkuu wa Ukoo ufanyike kwanza Dar es Salaam na ndipo ufanyike na
kijijini Kidamali. Licha ya kupewa sababu na maelezo ya kina ya kuufanya
Mkutano huo ufanyike Kijijini Kidamali, hawakutilia maanani.
Katika suala la utoaji
wa michango, watu wamekuwa na ari na mwitikio wa hali ya juu hapa Kijijini
Kidamali, na kwa kiwango kikubwa ndio waliosaidia kufanikisha kufanyika kwa
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule.
Licha ya wanaukoo
waishio Dar es Salaam kuchangia, lakini mchango wao umesaidia kidogo sana, kwa
sababu kiwango kikubwa cha fedha pamoja na mahitaji mengine, yamepatikana hapa.
Sehemu nyingine, nje
ya Kidamali, utoaji wa michango hapo mwanzo ulikuwa wa wastani, lakini kadiri
siku zilivyokuwa zinakaribia, ari na kasi mpya ilijitokeza na kuwa kubwa hasa
toka sehemu za Magubike pamoja na Nyamihuu.
Majirani na watu
wengine wasio wanaukoo wamejitolea kutoa michango katika kuusaidia Ukoo wa
Kivenule, kufanikisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule.
Majirani na marafiki waliojitokeza kwa hali na mali katika kutoa fedha, vyombo
na vifaa mbalimbali.
IX: HOTUBA YA MGENI RASMI
Mgeni Rasmi
aliishukuru Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule
kwa kumwalika kuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Kivenule.
Alisisitiza kwa kusema kuwa, kuna watu wengi muhimu ambao tumewaacha na kuamua
kwenda kumwalika yeye.
Mgeni Rasmi alisema
amefarijika sana kutokana na kuwashirikisha jamaa/wanaukoo wote. Pia
alisisitiza kuwa anahisi yupo karibu na ukoo wa Kivenule kutokana na baadhi ya
jamaa zake wa karibu kuwepo kwenye mkutano huo. Pia hata rafiki zake nao
walihudhuria kwenye Mkutano Mkuu wa Ukoo; hii ilimpa faraja sana.
Kutokana na ukoo kuwa
na mtandao mkubwa sana, ni muhimu kukawa na shughuli za pamoja kama hizi.
Wakati anaongea na Mwenyekiti, amefurahi sana kusikia mikakati ya wanaukoo hasa
lile la kufanya senza na pia mkakati wa kufahamiana zaidi.
Mgeni Rasmi
aliwashukuru wale wote waliotoa wazo la kuwepo kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa
Ukoo wa Kivenule na jinsi walivyoshirikisha wanaukoo katika shughuli hii.
Katika shughuli yoyote
ile, vikwazo vipo, suala la msingi ni kuelimishana na kuwashawishi wale ambao
hawakuhudhuria ili kuwepo na umoja na mshikamano. Suala mshikamano na umoja ni
muhimu sana katika jamii yetu kwani itasaidia kuleta maendeleo na wana-ndugu wanatakuwa
karibu. Pia, kuwa pamoja kunasaidia kushirikiana katika magonjwa, furaha na
matatizo mbalimbali ya kila siku. Mgeni Rasmi, alitoa mfano wa Abraham na Lutha
katika ugomvi wao wa mifugo, lakini mwisho walijaliana katika shida licha ya
kutengana. Ndugu ni muhimu sana na hawawezi kutengana.
Mkutano huu unatoa
changamoto ya kuwa na mshikamano na kuwa na nguvu zaidi katika kuleta
maendeleo. Mgeni Rasmi aliushukuru Ukoo wa Kivenule kwa kuelimishana kuhusu
umuhimu wa kuwa na ushirikiano wakati wote nasi tu wakati wa matatizo. Huu ni
mfano mzuri kwa jamii nyingine. Mgeni Rasmi aliutakia kila la kheri Mkutano
Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, na kuahidi kuwa yuko nyuma ya wanaukoo
sambamba wakati wote wa Mkutano huo.
Baada ya hotuba ya Mgeni Rasmi, MKUTANO MKUU WA KWANZA WA UKOO WA KIVENULE,
ulitangazwa Kufunguliwa Rasmi Mnamo saa
4:45 Asubuhi, Siku ya Jumamosi, tarehe 17 Desemba 2005
X: UTAMBULISHO WA WANAUKOO
Kwa mujibu wa ratiba
ya siku ya kwanza ya MKUTANO MKUU WA
KWANZA WA UKOO WA KIVENULE, utambulisho wa Wanaukoo ulifanyika kwa kila
ndugu/mwanaukoo kujitambulisha mwenyewe. Mwenyekiti aliwaelewesha washiriki wote jinsi
ambavyo wanapaswa kujitambulisha.
Kila anajitambulisha alipaswa/alitakiwa
kutaja jina lake la mwanzo, jina la baba yake, babu na jina la mwisho la ukoo.
Lakini, pia wanaukoo walijitambulisha kwa kutaja majina ya Mama zao, Waume au
Wake zao.
Kila mshiriki katika Mkutano Mkuu wa
Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, alipewa kitambulisho cha kumtambulisha kwa ndugu
wengine. Kitambulisho hicho kilionyesha jina lake kamili, mahali anapoishi,
namba ya simu pamoja na sanduku la posta. Hii ilifanyika makusudi ili kupunguza
kuulizana majina kutokana na washiriki kuwa wengi.
Yafuatayo hapa
chini ni majina ya wanaukoo waliojitambulisha siku/ kwenye Mkutano Mkuu wa
Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. (refer
registration forms).
XI:
UWASILISHAJI WA MADA KATIKA MKUTANO MKUU WA UKOO
Katika MKUTANO MKUU WA KWANZA WA UKOO WA KIVENULE, jumla ya Mada Tano
ziliwasilishwa. Mada ya kwanza kuwasilishwa katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ilikuwa ni “CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO”.
Wawasilishaji wa Mada hii walikuwa ni ndugu:
1. Christian J. Kivenule
[Toka Kidamali]
2. Augustino Kivenule [toka Nduli (Kigonzile)]
MADA YA KWANZA
CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO WA KIVENULE
Maana ya Ukoo (Tafsiri)
Ukoo ni muungano wa familia kadhaa zenye utambulisho fulani, aidha wa
jina, alama au mwelekeo mmoja. Tunapozungumzia utambulisho fulani uwe wa
jina,alama au mwelekeo mmoja; tunamaanisha kwamba ukoo wa Kivenule unatambulika
kati ya jamii nyingine mbalimbali kwa jina la “KIVENULE”, jina ambalo
linatuunganisha na jamii nyingine au ndugu kujiona sisi ni kitu kimoja.
Tunapomuona mtu mgeni machoni petu lakini ana mweleko wa ukoo wa
Kivenule, tunamwuliza, mwenzetu mwiko wako ni nini kwa upande aidha wa chakula.
Bila shaka akitueleza kuwa hali nyama ya Mbawala “Asisile Ukulya Mato” yaani
mwiko wake ni kula nyama ya Mbawala, basi sote tunaafikiana kuwa huyu ni ndugu
yetu.
Hivyo Ukoo wa Kivenule uzila kula nyama ya Mbawala, na huu ndiyo mwiko
mkubwa au alama ya utambulisho tuliyorithishwa na Babu zetu.
Alama nyingine ndani ya Ukoo wa Kivenule ni ile ya Mwitikio, kwa lugha ya
fasaha ya asili yaani Kihehe toka kwa wakazi wa mkoa wa Iringa tunaita
MWIDIKISO. Mwitikio wa Ukoo wa Kivenule ni MLIGO. Hii ni alama nyingine nyeti
inayotambulisha Ukoo wa Kivenule.
Chimbuko
la Ukoo wa Kivenule
Chimbuko la Ukoo wa KIVENULE ni kutoka
sehemu ya Malangali iliyopo katika Wilaya ya Mufindi, kusini mwa mkoani Iringa.
Asili ya ukoo wa KIVENULE ni mchanganyiko wa WAHEHE na WABENA; ambapo
mchanganyiko huu hujulikana kama WABENAMANGA.
WABENAMANGA wapo katika maeneo
mbalimbali mkoniani Iringa ikiwemo Mgololo, Mtwangu, Idunda, Ilole na
kadhalika.
Historia inaonyesha kwamba, Ubini wa
KIVENULE ilikuwa ni zawadi iliyotolewa kwa Ukoo wa MWIBALAMA au BALAMA kutokana
na umaarufu na uhodari wao katika kulenga shabaha wakati wa mapigano vitani
(KWIMIGOHA). MWIBALAMA walikuwa ni Mashujaa katika Shabaha ya Mishale (MIGOHA)
kutokana na kuwatekeleza (kuwaua) maadui katika hali isiyo ya kawaida tofauti
na wapiganaji wengine.
Kitendo cha kulenga shabaha kikamilifu
bila kukosea walikiita KUVENULA. Uhalisia wa KUVENULA ni kuua kikamilifu maadui
katika vita. Kwa hiyo KIVENULE limetokana na neno KUVENULA na lilipatikana kama
Zawadi toka kwa Wakubwa wa Vita siku hizo za mapigano vitani. KIVENULE ni jina
la sifa ya kuwa na uwezo wa kumvua adui kwa kutumia shabaha ya Mishale (Migoha)
bila vikwazo.
Mzee TAGAMTWA ambaye alitoka katika Ukoo
wa MWIBALAMA alikuwa ni ni mtu na Kaka na TAVIMYENDA KIVENULE. TAGAMTWA alifia
vitani na mwili wake haukuweza kupatikana. Mzee TAGAMTWA ndiye aliyemzaa
SALAMALENGA aliyekwenda kueneza Ukoo wa Kivenule maeneo ya ILOLE. Kwa maana
hiyo, Mzee TAGAMTWA alikuwa ni Baba yake SALAMALENGA.
Historia inaonyesha kuwa, Mzee
TAVIMYENDA na Mzee SALAMALENGA wakitokea
maeneo ya Malangali - Mufindi walifikia Kalenga, ambapo walikutana na Mzee KIKOTI.
KIKOTI alikuwa ana mifugo yake eneo la MAGUBIKE na ULEFI. Hivyo, KIKOTI
alimwomba TAVIMYENDA aende MAGUBIKE ili aweze kumwangalia mifugo yake. Hali
kadhalika Mzee SALAMALENGA katika kutafuta maisha, aliamua kwenda ILOLE.
TAVIMYENDA ndiye alieneza ukoo kwa
upande wa KIDAMALI na hali kadhalika SALAMALENGA alifanya hivyo kwa upande wa
ILOLE.
Babu TAVIMYENDA yeye alikuja upande wa
Magubike yaani ULEFI enzi hizo. Babu TAVIMYENDA KIVENULE na Mke wa wake MKAMI
waliishi ULEFI na baada ya kufa walizikwa pale pale ULEFI. Babu SIGATAMBULE
KIVENULE pamoja na Babu wengine KAVILIMEMBE KIVENULE, MGAYIFAIDA KIVENULE,
HUSENI KIVENULE na BIBI MGASI walizaliwa katika eneo la ULEFI - MAGUBIKE.
Katika uhai wao muda mwingi waliishi eneo la ULEFI kabla ya Wazungu kufika
wakitafuta eneo la kuishi na wakapewa sehemu ya ULEFI. Mzungu huyo alikuwa ni
JIM, Mgiriki wa kwanza kufika eneo la ULEFI.
Kutokana na hali hiyo, Babu SIGATAMBULE
KIVENULE alihamia sehemu ya MLAFU pamoja na Babu mwingine MGAYAFAIDA. Kufika
MLAFU, Babu SIGATAMBULE alikuna na Mzungu mwingine aliyeitwa SPELO. Kwa hiyo
Wazungu hao wakampimia eneo la MLAFU na hivyo akawa amepakana na wazungu pande
zote. Kwa chini akawa amepakana na Giriki MICHO. Babu HUSENI KIVENULE yeye
alihamia MAGUBIKE.
Maana halisi ya MAGUBIKE ni kuwa kuna
jiwe liliwafunika watu hapo siku za mwanza ambapo watu walikuwa wanaishi
mapangoni.
KIVENULE waliopo ILOLE na NDULI wa wale
waliopo KIDAMALI na MAGUBIKE wote ni asili moja.
MGAWANYIKO WA UKOO WA KIVENULE
1.
Kavilimembe Kivenule Kazikwa Magubike (Me)
2.
Myagafaida Kivenule Kazikwa Mlafu (Me)
3.
Sigatambule Kivenule Kazikwa Mlafu (Me)
4.
Huseni Kivenule Anaishi Magubike (Me)
5.
Abdalah Kivenule Kazikwa Mlafu (Me)
6.
Sikimbilavi Semabiki Kazikwa Mlafu (Ke)
7.
Mgasi Kivenule Kazikwa Mlafu (Ke)
8.
Sigungilimembe
Kivenule Kazikwa Mjini (Ke)
9.
Malibora Kivenule Kazikwa Mkimbizi (Ke)
A: WATOTO WA BABU KAVILIMEMBE KIVENULE
1.
Salikuwaganga
Kivenule Anaishi Nzihi (Ke)
2.
Dalikimali Kivenule Anaishi Nzihi (Ke)
3.
Francis Kivenule Amezikwa Mlafu (Me) (Monica Kivenule)
4.
Pangalasi Kivenule Anaishi Ilula (Me)
5.
Sandra Kivenule Amezikwa
(Ke) (Mama Mapembe)
6.
Elizabert Kivenule Amezikwa (Ke)
B: WATOTO WA BABU MGAYAFAIDA KIVENULE HAKUWA NA FAMILIA
C: WATOTO WA BABU SIGATAMBULE KIVENULE
WATOTO WA BABU SIGATAMBULE |
||
Bibi
SIWANGUMHAVI SINGAILE
|
Bibi
NYANYIMALE SINGAILE
|
Bibi
PANGULIMALE SETWANGA
|
1.
Gidagumhindi
(Cecilia) Kivenule (Ke)
2.
Semyamba
(Khadija) Kivenule (Ke)
3.
Sivinitu
(Alphonce) Kivenule (Me)
4.
Kadungu
(William) Kivenule (Me)
5.
Fibumo
(Zavery) Kivenule (Me)
6.
Mlagile
(Anyesi) Kivenule (Ke)
7.
John Kivenule (Me)
|
1.
Mgulwa
(Mama Agatha) Kivenule(Ke)
2.
Luhanage
(Ponsiano) Kivenule (Me)
3.
Mgendwa
(Eusebio) Kivenule(Me) Baba Kaini
4.
Msinziwa
(Daniel) Kivenule(Me)
5.
Kanolo
(Edward) Kivenule(Me)
|
1.
Conjeta
Kivenule – Magubike
2.
Pyela
Kivenule
3.
Faustino
Kivenule
4.
George
Kivenule
5.
Carolina
Kivenule
|
D: WATOTO
WA BABU HUSENI KIVENULE
WATOTO WA BABU HUSEN |
|
Bibi
YIMILENGERESA (Mume yuko) Vitani) SEMSISI
|
Bibi
DALIKA SETALA
|
1.
Nyakudila
(Benjamin) Kivenule(Me) – Gangimali
2.
Sekiyavile
(Modesta) (Ke) Kivenule – Magubike
3.
Dominikus
Kivenule (Me) – Magubike
4.
Emmanuel
Kivenule
5.
Luciana
Kivenule (Dead)
|
1.
Kabogo
(Bernardi) Kivenule (Me) – Magubike
2.
Sembata
(Josephina) Kivenule (Ke) – Nyamahana
3.
Brandino
Kivenule (Me) – Kidamale
4.
Batromeo
Kivenule (Me) (Dead)
5.
Tavina
Kivenule (Ke) – Nyamahana
6.
Masikitiko
Kivenule (Dead)
|
1.
Gisapa
Kigereso (Ke) [dead]
2.
Sinatoga Kigereso (Ke)
3.
Mtogapawene
Kigereso
(Ke) [dead]
4.
Chesilemungu
Kigereso
(Ke) [dead]
5.
Ronjino Kigereso (Me) [dead]
MGAWANYIKO WA UKOO WA
TAGAMTWA MWIBALAMA
1.
CHOGAVANU KIVENULE
2.
PANGAYENA KIVENULE
3.
JONAS KIVENULE
4.
SAMWEL KIVENULE
5.
MUNGUATOSA KIVENULE
6.
GALASAMANENO KIVENULE
7.
WILLIAM KIVENULE
8.
TINDASULANGA KIVENULE
9.
GUNGAMESA KIVENULE
10.
SIGONGOLA KIVENULE
11.
SHABAN KIVENULE
12.
BARTON KIVENULE
1. CHAGAVANU S. KIVENULE
1.
NOSOLO C. KIVENULE
2.
MADESTUS C. KIVENULE
3.
PAULINA C. KIVENULE
2. PANGAYENA S. KIVENULE
1.
GWELINO P. KIVENULE
2.
PASCAL P. KIVENULE
3.
STELINA P. KIVENULE
4.
PAUSTINA P. KIVENULE
5.
BERNADI P. KIVENULE
6.
CHELINA P. KIVENULE
7.
IGNUS P. KIVENULE
8.
CONSOLATA P. KIVENULE
9.
RAPHAEL P. KIVENULE
1. GWELINO P. KIVENULE
1.
Fausta G. Kivenule
2.
Julius G. Kivenule
3.
Delia G. Kivenule
4.
Vasisile G. Kivenule
5.
Christopher G. Kivenule
6.
Farida G. Kivenule
7.
Michael G. Kivenule
8.
Machelina G. Kivenule
9.
Stumai G. Kivenule
10.
Philimon G. Kivenule
11.
Lugina G. Kivenule
12.
Agnes G. Kivenule
13.
Anitha G. Kivenule
14.
Frola G. Kivenule
15.
Bosco G. Kivenule
16.
Olive G. Kivenule
17.
Tegemeo G. Kivenule
18.
Yovita G. Kivenule
2. PASCAL P. KIVENULE
1.
Mage P. Kivenule
2.
Seuginge P. Kivenule
3. STELINA P. KIVENULE
1.
Eluda Nyemba
2.
Anjila Nyemba
4. PAUSTINA P. KIVENULE
1.
Yudita Kiteve
2.
Daniel Kiteve
3.
Etta Kiteve
4.
Wuliana Kiteve
5.
Kalumelita Mkeng’e
6.
Charles Kiteve
7.
Valendino Mkeng’e
5. BERNADI P. KIVENULE
1.
Damas B. Kivenule
2.
Kamimi B. Kivenule
3.
Laheli B. Kivenule
4.
Kalo B. Kivenule
5.
Kulwa B. Kivenule
Damas B. Kivenule
·
Nasuma D. Kivenule
6. CHELINA P. KIVENULE
1.
Tecla Kisumbe
2.
Gibson Kitu
3.
Carson Kisumbe
4.
Lilian Kisumbe
5.
Elasto Kisumbe
7. CONSOLATA P. KIVENULE
1.
Colado Ngwenga
2.
Sixtus Ngwenga
3.
Thdey Ngwenga
4.
Felista Ngwenga
5.
Stani Ngwenga
8. IGNUS P. KIVENULE
1.
Pelis I. Kivenule
2.
Bernadelt I. Kivenule
3.
Theopista I. Kivenule
4.
Vestina I. Kivenule
5.
Lilian I. Kivenule
9. RAPHAEL P. KIVENULE
1.
Geofrey R. Kivenule
2.
Muhomela R. Kivenule
3.
SAMWEL S. KIVENULE
1.
MARTIN S. KIVENULE
2.
LUCAS S. KIVENULE
3.
ALOYCE S. KIVENULE
4.
ERENESTO S. KIVENULE
5.
INNOCENT S. KIVENULE
6.
MICHAEL S. KIVENULE
7.
MONICA S. KIVENULE
8.
ANNA S. KIVENULE
9.
ANNETA S. KIVENULE
10.
FELINA S. KIVENULE
1. MARTIN S. KIVENULE
1.
Anesia M. Kivenule
2.
Festo M. Kivenule
3.
Msso M. Kivenule
4.
Nelson M. Kivenule
5.
Saida M. Kivenule
6.
Neema
M. Kivenule
7.
Faraja M. Kivenule
8.
Teresia M. Kivenule
2. LUCAS S. KIVENULE
1.
Efrehem L. Kivenule
2.
Uzuni L. Kivenule
3.
Kibanile L. Kivenule
3. ALOIS S. KIVENULE
1.
Kissa A. Kivenule
2.
Zawadi A. Kivenule
3.
Siwazuki A. Kivenule
4.
Sitamini A. Kivenule
5.
Levina A. Kivenule
6.
Asha A. Kivenule
4. ERENESTO S. KIVENULE
5. INNOCENT S. KIVENULE
1.
Vicky I. Kivenule
2.
Frank I. Kivenule
3.
Magreth I. Kivenule
4.
Grace I. Kivenule
5.
Emmanuel I. Kivenule
6. MICHAEL S. KIVENULE
7. MONIKA S. KIVENULE
8. ANNA S. KIVENULE
9. ANNETA S. KIVENULE
10. FELINA S. KIVENULE
4. JONAS S. KIVENULE
1.
TITUS J. KIVENULE
2.
PAULO J. KIVENULE
3.
EMMNUEL J. KIVENULE
4.
ANALOIDA J. KIVENULE
5.
ARDO J. KIVENULE
6.
EMILYANA J. KIVENULE
7.
GWIDO J. KIVENULE
8.
JONISIA J. KIVENULE
9.
PIUS J. KIVENULE
10.
EMILYO J. KIVENULE
1. TITUS J. KIVENULE
1.
Yustina T. Kivenule
2.
Evaristo T. Kivenule
3.
Castory T. Kivenule
4.
Atanasi T. Kivenule
5.
Patricia T. Kivenule
6.
Jachinda T. Kivenule
7.
Johakimu T. Kivenule
8.
Letisia T. Kivenule
2. EMILYO J. KIVENULE
1.
Jamila E. Kivenule
2.
Dolla E. Kivenule
3.
Mwahen E. Kivenule
3. PIUS J. KIVENULE
1.
Frank P Kivenule
2.
Fotte P. Kivenule
3.
Verlo P. Kivenule
4.
Mkutwa P. Kivenule
5.
Niva P. Kivenule
4. PAULO J. KIVENULE
1.
Costandino P. Kivenule
2.
Lenzia P. Kivenule
5. ARDO J. KIVENULE
1.
Lembula A. Kivenule
2.
Kandia A. Kivenule
6. EMMANUEL J. KIVENULE
1.
Mgilinde E. Kivenule
7. GWIDO J. KIVENULE
1.
Sikweli G. Kivenule
2.
Frida G. Kivenule
3.
Reginandi G. Kivenule
ANALOIDA J. KIVENULE
1.
Fahamu A. Kivenule
2.
Rojasi A.
Kivenule
5. MUNGUATOSA S. KIVENULE
1.
MARIAM M. KIVENULE
2.
6. GALASAMANENO S. KIVENULE
1.
CHELINA G. KIVENULE
2.
DOMINICUS G. KIVENULE
3.
DAVID G. KIVENULE
7. WILLIAM S. KIVENULE
1.
MUSA W. KIVENULE
2.
HASSAN W. KIVENULE
3.
ANSEREM W. KIVENULE
4.
PAULINA W. KIVENULE
5.
YESOFINA W. KIVENULE
6.
RIDIA W. KIVENULE
8. TINDASULANGA S. KIVENULE
9. GUNGAMESA S. KIVENULE
10. SIGONGOLA S. KIVENULE
11. SHABAN S. KIVENULE
1.
AUGUSTINO S. KIVENULE
12. BURTON S. KIVENULE
1.
MASUDI B. KIVENULE
2.
STEPHAN B. KIVENULE
3.
JOHN B. KIVENULE
4.
BONIPHASI B. KIVENULE
5.
FABIAN B. KIVENULE
6.
LOSINA B. KIVENULE
7.
MALUKUS B. KIVENULE
8.
JULIO B. KIVENULE
MALUKUSI B. KIVENULE
1.
Jalibu M. Kivenule
2.
Kulwa M. Kivenule
3.
Doto M. Kivenule
4.
Fatuma M. Kivenule
JULIO B. KIVENULE
1.
Siyaleo J. Kivenule
2.
Gude J. Kivenule
3.
Tuma J. Kivenule
4.
Monika J. Kivenule
5.
Pelida J. Kivenule
6.
Kulusumu J. Kivenule
7.
Ajina J. Kivenule
8.
Vailes J. Kivenule
MASUDI B. KIVENULE
1.
Evaristo M. Kivenule
2.
Shedlack M. Kivenule
STEPHAN B. KIVENULE
1.
Aida S. Kivenule
2.
Rajabu S. Kivenule
3.
Kimbembe S. Kivenule
4.
Ambaa S. Kivenule
5.
Fanula S. Kivenule
JOHN B. KIVENULE
1.
Wick J. Kivenule
2.
Simbion J. Kivenule
3.
Mtitu J. Kivenule
KUPOTEA
KWA UKOO
Siku zote katika harakati za kutafuta
maisha, ukoo hujikuta unajitenga na mazingira yake ya asili, yaani nyumbani na
kujikuta ukoo husika upo sehemu nyingine. Sababu kubwa ya ukoo kuwa sehemu
nyingine ni kutafuta mkate wa kila siku; lakini pia kutafuta unafuu wa uchumi
na kupata maendeleo ya kuendesha familia zao.
Siwezi kusema moja kwa moja kuwa kuna
kupotea kwa ukoo; isipokuwa wanandugu siku zote hupuuzia mawasiliano baina ya
wanandugu na kuweka/kujenga ukuta baina yao na hivyo kufanya ndugu wawe na
mfumo mbaya wa mawasiliano. Kutokuwa na mawasiliano huleta matatizo mengine
kama vile kutosaidiana pindi shida zinapotokea na pia kutokujua upande mwingine
wanafanya nini!
Mfumo huu dume wa kutotafuta mtandao wa
mawasiliano na kutokuwa karibu baina ya wanandugu huleta mgawanyiko, na tabaka
ndani ya ukoo, lakini mbaya ziaid kutakuwa na pengo kubwa la maendeleo baina ndugu
yaani wenye nacho na wasio nacho. Hivyo basi japokuwa wanandugu tunaishi maeneo
tofauti tofauti hatuna budi kuimarisha mtandao wa mawasiliano na kuwa karibu
siku zote. Kuna usemi wa Kiingereza usemao: “People are lonely because they
build walls instead of bridges”. Kwa lugha rahisi ya hapa kwetu ni kwamba
“Avanu vakivakwa kuva vasengite ulukanzi badala ya kisumbo au kilowoko”!!!...
Na kwa nini tujenge ukuta baina yetu?!!!. Hatuna budi tujenge daraja
litakalotuunganisha yaani tuweze kuvuka kutoka upande mmoja hadi mwingine ili
tuweze kufahamu upande mwingine wanafanya nini cha katika kujiletea maendeleo.
HASARA
ZA KUPOTEA KWA UKOO
Kuna hasara nyingi zipo ambazo tunaweza
kuzipata endapo ukoo utapotea; kati ya hasara hizo ni pamoja na:
§
Kuleta
umaskini na ndugu/mwanaukoo kuwa tegemezi; kwa mfano ndugu aliyetoka nyumbani
kwenda Kigoma au popote kwa miaka mingi; hivyo anapoteza mawasiliano na
wenzake, pindi maisha yanapomuelemea basi anaanza kuwa omba omba. Kwa sababu
hana msaada wa karibu kutoka kwa wanandugu.
§
Kudumaa
kimaendeleo kwa sababu ya kuridhika na mfumo mmoja wa maisha. Hakuna ushindani
wa maendeleo kwa sababu hajifunzi kwa ndugu wenine kutokana na hatua za
maendeleo walizozifikia. Matokeo yake ndugu anaridhika na kujipa moyo eti kwa
sababu yupo ugenini na hana shida.
§
Kuna
hatari kubwa ya kujiingiza katika matukio mabaya mfano ujambazi, utumiaji wa
madawa ya kulevya kama bangi, cocaine, mandrax na kujidunga sindano. Pia ndugu
huwa katika nafasi ya kujihusisha na uasherati au umalaya katika madangulo
(kasino).
§
Hukosa
msaada tosha wa mawazo na hata jeki ya kujiletea maendeleo
§
Kutokea
kwa mgongano wa mapenzi. Hii inamaanisha kwambaa vijana ndani ya ukoo wanaweza
kujikuta wanatafutana wao kwa wao ndani ya ukoo, kwa sababu wote wapo ugenini
kwa muda mrefu na hawana mawasiliano na nyumbani kwao.
FAIDA
ZA WANAUKOO KUWA KARIBU
Faida ambazo wanaukoo wanaweza kuzipata
kama watakuwa karibu ni pamoja na:
§
Kudumisha
undugu na upendo baina ya wanandugu ndani ya ukoo.
§
Huchochea
maendeleo ya kasi ndani ya wanaukoo kwa kuangalia ndugu mwingine anafanya nini,
na pia ndugu nao kujifunza kutoka kwake na kuomba mawazo kutoka kwake au kwa wengine.
§
Hupunguza
ugumu wa tatizo, na kuonekana tatizo ni dogo na lenye kutatulika endapo kuna
ushirikiano wa dhati ndani ya wanandugu. Hii ni kwa sababu wanandugu ni kitu
kimoja na mtu kuchukulia tatizo la mwenzake kuwa lake mfano wa jamii zilizopiga
hatua katika hili ni Wahindi, Waarabu na hapa nyumbani kwetuTanzania ni
Wachaga. Familia nyingi katika jamii hii wamepiga hatua katika maendeleo.
§
Ni
rahisi kuanzisha miradi ya pamoja ya maendeleo kwa kuwa tunakuwa na itikadi zenye
mlengo mmoja na wa kufanana; tofauti na kuwa na mradi na mtu tofauti
msiyejuana, inaleta utata na ugumu zaidi.
Ni vizuri wanaukoo wakaanza kuwa kitu
kimoja kuanzia sasa. Tuache tofauti baina yetu. Tumwombe Mwenyezi Mungu
atujalie roho ya kuwapenda wengine na kuwapenda ndugu zetu kama tunavyojipenda
sisi. Tuwe tayari kuwasaidia ndugu wanaoelemewa na maisha, tuwape fara na
msaada wa vitu na hata mawazo katika kuhakikisha kila mmoja anapta unafuu wa
maisha.
MAJADILIANO YA KWENYE VIKUNDI
KUNDI NA. 1
Ukoo ni Nini?
Ukoo huanza na mtu
mmoja, ambaye huzaa watoto na pia watoto nao kuwa na familia zao (yaani nao kuzaa
watoto). Mwishoni muunganiko huu huwa ni kitu kimoja ambacho ni Ukoo.
§
Kuoa au kuolewa ndiyo msingi mkubwa wa kuwa au kuunda Ukoo
kwa sababu kuoa au kuolewa ndiko kunakojenga familia ambazo zinachangia
kupatikana kwa Ukoo.
§
Ukoo pia unaweza kuenea hata nje ya mipaka mfano Ulaya,
America na kwingineko ulimwenguni.
KUNDI NA. 2
Kuenea kwa Ukoo
Maana yake ni
§
Mtu yupo mahali fulani, ukamtembelea mfano Mbeya, Dar es
Salaam, Kenya na kwingineko.
§
Mtu yupo mahali fulani lakini usitake kumtembelea.
Kuenea/Kukua kwa Ukoo
§
Kuoa
au Kuolewa
§
Kufahamiana
§
Elimu/Kusoma
kutapelekea kujulikana
§
Kusaidiana
na kushirikiana
§
Mawasiliano,
mfano mtu wa Mwanza, alioa na akaleta mawasiliano kuwa ana mtoto Mwanza na
kumleta.
KUNDI NA. 3
Mgawanyiko
wa Ukoo
Ukoo unaweza kugawanyika kutokana na ndugu
au wanaukoo kuamua kuishi sehemu fulani kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo
zile za kiuchumi, hali ya hewa nzuri na maendeleo.
|
§
Watoto
kujaliana upande wa mama na si upande wa baba ambaye ni mwanzo wa ukoo.
§
Kuongeza
matawi na Kidamali pawe ni mzizi wa ukoo.
§
Wanawake
wapunguze tofauti kwani wao ndiyo chanzo cha kuugawa ukoo.l
Katika kuunganisha mgawanyiko huu wa
Ukoo ni Mawasiliano baina ndugu wanaoishi sehemu mbalimbali. Mfano katika
kipindi hiki mawasiliano ya simu za mkononi yameenea kila mahali, cha msingi ni
kuwa na mkakati thabiti katika kuhakikisha kuwa ndugu wanakuwa na mawasiliano
yaliyo sahihi. Bila kuwa na mawasiliano ina maana kuwa tunakuwa tumejiwekea
ukuta mnene wa kututenganisha wanaukoo.
KUNDI NA. 4
Kupotea
kwa Ukoo
Kupotea kwa ukoo husababishwa na sababu
kadha wa kadha mojawapo zikiwa zimeainishwa hapa chini:
§
Kutosaidiana
katika shida mbalimbali mfano misiba na ugonjwa.
§
Kutotembeleana
toka sehemu moja hadi sehemu nyingine mfano ndugu mmoja anakaa Morogoro na
ndugu mwingine anakaa Dar es Salaam, Tabora na kadhalika.
§
Kudharauliana
kutokana na kutofautiana katika kipato (fedha), umaskini, utajiri na elimu.
§
Kukosekana
kwa mawasiliano mfano kupigiana simu; kutotambulishana na kutotembeleana.
§
Watoto
kutotembelea kwa ndugu.
§
Wanawake
wanaoolewa kwenye ukoo kutotembeleana
§
Maskini
wasio na kipato (hana kitu) kuona aibu kufika kwa ndugu mwenye uwezo (kipato
kizuri) bila ya kufahamu kuwa wote ni ndugu wa ukoo mmoja.
§
Kupeana
taarifa mapema za matatizo kwa ndugu wote ili tuwe kitu kimoja.
Jambo la msingi kufanyika katika
kuhakikisha kuwa Ukoo haupotei ni kuundwa kwa Kamati itakayoratibu matatizo ya
Ukoo pamoja na wanandugu.
MADA YA PILI
MAHUSIANO
BAINA YA WANANDUGU NDANI YA UKOO
Utangulizi
Maana ya Mahusiano ni hali ya ukaribu,
ujirani, urafiki, umoja au ushirikiano unaojengeka baina ya Ndugu, Jamaa au
Marafiki. Mahusiano ni hali ya kuwa pamoja Kifikra, Kimwili, Kimawasiliano,
Kiimani, Kiitikadi, Kimaendeleo, Kikazi, Kijamii na Kimichezo.
Mahusiano hujengwa kwa misingi/namna
mbalimbali. Baadhi ya njia au vitu vinavyosababisha kukawepo na mahusiano ni
pamoja na:
1. Ujirani:
Ujirani mara nyingi katika jamii zetu huchangia sana katika kujenga Mahusiano.
Mahusiano yenyewe huonekana katika sura mbili tofauti. Yaani Mahusiano Mazuri
kwa maana ya Sura Nzuri au Mahusiano Mabaya kwa maana ya Sura ya Ubaya.
2. Undugu:
Hii ni aina ya nyingine ya Mahusiano ambapo ndugu wa Damu Moja au wanachangia
damu, hujenga Mahusiano ya Moja kwa Moja (Automatic Relationship). Mara nyingi
Mahusiano ya aina hii huwa na Sura ya Uzuri zaidi (Mahusiano Mazuri). Japo kuna
kipindi Fulani hata Sura ya Ubaya (Mahusiano Mabaya) hujitokeza.
3. Imani:
Pia watu huweza kujenga Mahusiano kupitia Imani zao, mfano watu wanaoabudu
katika dhehebu moja huweza kujenga mahusiano ya aina yao tofauti na dhehebu
jingine. Mara nyingi Mahusiano ya Kiimani huwa na mwelekeo wa Mahusiano mema.
Mahusiano mabaya mara nyingine hutokea na hata kusababisha vita vya kiimani
(dini).
4. Itikadi:
Mahusiano ya Kiitikadi nayo hujengeka kwa kufuata Mlengo wa Vyama Vyao. Na
zaidi Mahusiano ya Kiitikadi huegemea zaidi kwenye siasa na hupungua au
kutoweka kabisa baada ya mmoja wao kubadili Itikadi yake yaani kuhama toka
chama cha kimoja cha siasa na kwenye chama kingine cha siasa. Mahusiano ya
Kiitikadi hujengwa kwa misingi ya Chuki, Fitina na Vitisho baina wa watu wa
Itikadi moja na wale wa Itikadi nyingine.
5. Maendeleo:
Watu wenye hali fulani ya kimaendeleo huweza kujenga aina fulani ya mahusiano
yenye nia ya kuinuia hali zao za kimaisha. Na mara nyingi wanaojumuika hapa ni
wale ambao tayari wameonesha nia na mwelekeo. Lakini pia hata wale waliopiga
hatua kimaendeleo huweza kuja mahusiano yao yakiwa nia ya kuimarisha hali
walizonazo. Msingi mkubwa wa mahusiano ya aina hii huwa ni kupeana mbinu na
mikakati ya kuleta au kujiimarisha zaidi katika maendeleo ambayo wanayatarajia
au ambayo wamekwisha yapata.
Pia hata kwa
upande wa wale wenye hali duni ya kimaendeleo nao hujenga aina Fulani ya
mahusiano kulingana na hali na uwezo wao. Kasoro ambayo hujitokeza hapa huwa ni
mahusiano duni baina wenye uwezo (matajiri) na wale na wasio na uwezo
(maskini). Katika kujiimarisha zaidi kimaendeleo, maskini huwa mtumishi
(kibarua) na tajiri huwa mtumikiwa (mtwana).
6. Elimu:
Watu wenye elimu nao mara nyining hujenga mahusiano yao. Mara nyingi katika
mahusiano yao huwatenga wale wenye elimu kidogo au wasio na elimu kabisa. Hii
hutokea zaidi kwa wale waliobahatika kupata Elimu ya Juu mfano Chuo Kikuu.
Mazungumzo na mipango yao huwatenga zaidi wale wenye elimu kidogo. Kuwatenga
hujitokeza katika matumizi ya lugha za kigeni, kutowashirikisha katika mawazo
mbalimbali ambayo wanadhani yanaweza kuwainua watu wa hali zote (wasomi na
wasio wsomi).
AINA
ZA MAHUSIANO
Kuna aina mbalimbali za mahusiano,
lakini tunaweza kugawanya mahusiano haya katika sehemu kuu mbili.
1. Mahusiano
Mazuri; na
2. Mahusiano
Mabaya.
Aina mbalimbali za mahusiano ambayo yapo
katika jamii zetu ni pamoja na mahusiano ya:
§
Kikazi;
§
Kijamii;
§
Kisiasa; na
§
Kiuchumi.
MAHUSIANO
MAZURI
Mahusiano Mazuri ni hali ya kuwa pamoja
kwa kushirikiana katika nyanja mbalimbali za maisha. Mahusiano Mazuri huwa
katika shida au raha. Raha hujumuisha hali zozote zenye kuashiria mafanikio na
maendeleo katika maisha ya binadamu. Hii ni pamoja na kufaulu mitihani
mbalimbali ya darasani na ya maisha; kujenga nyumba, kununua gari, kapata kazi
nzuri, kufanikiwa katika kilimo, Jubilei, kupandishwa cheo pamoja na kupata
nishani.
Shida huwa ni hali ya kuwa na mashaka,
kutokuwa na uhakika wa maisha, kutokuwa na kipato, kutofanikiwa katika elimu,
ugonjwa, misongamano (Depression), misusuko (stress), kutokuwa na ajira,
kutofadhiliwa kwa hali yoyote (Promotion au Scholarship) na kadhalika.
MAHUSIANO
MABAYA
Mahusiano Mabaya ni hali ya kutokuwa na
ushirikiano, huruma au wema katika nyanja mbalimbali za maisha. Mahusiano
Mabaya nayo hali kadhalika huwa katika ubaya au uzuri au shida na raha. Tofauti
na katika Mahusiano Mazuri, Mahusiano Mabaya hubaki kuwa ni swa katika shida na
raha. Kwa ujumla ushirikiano na mawasiliano hukosekana kabisa. Huwa hakuna
huruma, maelewano, kuvumiliana na kuwasiliana.
Kikubwa ambacho hujengeka ni chuki,
majivuno, wivu, ugomvi na kutakiana shari. Hamna hata mmojawapo ambaye huombewa
kheri. Kwa yule aliyenacho, huombea au hutamaini yeye aendelee kuwa nacho peke
yake na kutomwombea kheri ya kupata yule ambaye hana kitu.
Na kwa yule ambaye hana, humwombea
shari, bahati mbaya kupotteza au kwa namna yoyote ambayo haina kheri kwa yule
ambaye anacho. Baadhi huomba mfano kama ni gari lipate ajari, nyumba iungue na
kama anasoma anafeli. Katika aina hii ya mahusiano hakuna nafasi ya kutakiana
mema au maendeleo.
MAHUSIANO
BAINA YA NDUGU NDANI YA UKOO
Ukoo wa Kivenule ni mkubwa sana na kwa
haraka unakadiriwa kuwa na ndugu karibia elfu mbili (2000). Ni ukoo ambao
unaweza kufanya mambo makubwa na ya kimaendeleo kama utaungana na kuwa kitu
kimoja.
Tatizo kubwa ambalo linaonekana kwa
wanaukoo ni kuwa na mwamko mdogo. Kwa mfano wanaukoo wanaohudhuria Mkutano Mkuu
wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ni theluthi au robot u ya wanaukoo wote. Tumaini
la Kamati za Maandalizi ya MKutano Mkuu ni kuhudhuriwa na Ndugu pamoja na
Wanaukoo wa Kivenule kwa wingi zaidi.
Kwa upande wa Dar es Salaam, mwamko wao
ni mdogo sana. Tumaini na tegemeo la awali ilikuwa Dar es Salaam ingekuwa ni
mfano, lakini imeshindika na hii ndiyo hali halisi. Tunasikitika na Kamati ya
maandalizi ya Dar es Salaam inaomba samahani.
Kwa wanaukoo toka Ilole, nao wamesema
tatizo kubwa kwao ni suala na nauli kuwa ni kubwa. Lakini cha msingi kufanyika
ni kuzidi kuwahamasisha na kuwapa mojyo wa kutambua umuhimu wa Mkutano Mkuu wa
Ukoo pamoja na mikutano mingine.
Katika suala zima la mahusiano, ukaribu
wa wanandugu na wanaukoo linaangaliwa kwa karibu zaidi. Mahusiano yanagusa
mambo muhimu katika maisha ya kila siku mfano Elimu, Ugonjwa, Vifo pamoja na
Starehe (Harusi, Send-Off, Kipaimara na Komunio). Elimu ni muhimu sana kwani
inaongeza upeo na ufahamu wa kuweza kukabiliana na matatizo ya maisha ya kila siku.
Suala jingine ni ushirikiano katika
nyanja mbalimbali mfano Biashara, kazi na kilimo. Hapa tunamaanisha kuunda
kikundi ambacho kitakuwa na mfuko utakaokuwa unachangiwa na watu mbalimbali
kulingana na shughuli na kipato.
Katika kujenga mahusiano imara,
kutembeleana ni muhimu sana. Faida ya kutembeleana ni kujuliana hali,
kusaidiana, kushauriana na kupeana mbinu na mwongozo wa kufauli katika maisha.
Pia katika kutembeleana huwapa fursa wanaukoo/ndugu kuangalia mazingira mapya
anayotembelea kama yanaweza kumfaa kuishi akilinganisha na mazingira aliyotoka.
Pia katika kushirikiana kuna haja ya
kuwashawishi na kuwabembeleza wale wasio na uwezo ikiwa ni pamoja na kuwapa
moyo, kuwashauri waondoe aibu na wajenge tabia ya kushirikiana. Katika
kushirikiana inakuwa ni rahisi kuweza kutatua matatizo mbalimbali baina ya
wenye nacho na wasionacho.
Kwa mfano katika shughuli nzima ya
kuandaa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, inakuwa kitu kizuri na
mfano kwa wengine kama tutaonyesha kwa vitendo haya tunayozungumza hapa. Hii
utaufanya Mkutano Mkuu kuwa na maana sana. Kivenule kwa tabia ni wapole sana na
wenye huruma. Ni vizuri tuwajali wenzetu kwa sababu hali zetu zinajulikana. Cha
msingi ni kuwa karibu na kusaidiana.
Mahusiano ambayo ukoo wa Kivenule
utarajie ni kama haya ya kuitikia kuja kwenye Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa
Kivenule. Bila kuwa na hatua madhubuti ukoo utaparaganyika. Katika vitabu vya
dini kuna mfano mmoja unasema “Mtu mmoja aliandaa sherehe na akaalika watu
kwenda kula, lakini watu wakakataa”. Kwa nini watu walikataa kwenda kula. Kila
mmoja ana sababu zake. Mungu awabariki kwa kukubali mwaliko huu.
Tafsiri sahihi ya mahusiano ipo katika
maeneo mbalimbali kama ilivyoainishwa pale mwanzo. Kila mwanaukoo anawajibika
na anawajibu kushiriki kikamilifu katika hilo. Mahusiano mazuri huleta upendano
ambao huwa ni chachu ya maendeleo.
Umuhimu wa kuwa na mahusiano mazuri
baina ya wanandugu ni kuulinda ukoo na kupunguza maingiliano kutokana na
wanaukoo kutawanyika maeneo mbalimbali ndani ya mipaka na nje ya mipaka. Katika
Mkutano huu Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, ndugu na wanaukoo kwa ujumla ni
walengwa na wanufaikaji.
Katika suala zima la mahusiano ndani ya
Ukoo wa Kivenule, kinachoepukwa hapa ni mgawanyiko wenye mwenendo wa tofauti ya
kipato. Lengo mahsusi ni kuangalia kwa nini tunafanya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa
Ukoo wa Kivenule? Hapa tunachoangalia ni mguso wa kila hali baina ya wanandugu
na wanaukoo kwa ujumla kuwa sisi wote wanaukoo ni kitu kimoja. Hivyo tuwe
wepesi katika kutoa misaada wakati wenzetu wana matatizo ya ugonjwa, njaa na
vifo. Lakini pia, ni vema kushirikiana na kutoa misaada katika shughuli za
furaha kama kufanya harusi, kipaimara na komunio.
Wanaukoo wote wanatahadharishwa, baada
ya mwaka mmoja wasipotee kwa sababu na visingizio mbalimbali. Tutumie chombo
hiki cha Mkutano wa Ukoo kutoa michango yetu ya mawazo, dukuduku na hamasa ya
kuwa na ukoo imara.
MAJADILIANO KWENYE MAKUNDI
KUNDI
NA. 1
Ukaribu
wa Wanandugu
1. Ushirikiano wa wanandugu upo katika
shida mbalimbali
2. Kujitolea na kujituma kama mwanandugu
kusaidia na kuchangia kwa hali na mali shughuli mbalimbali za Ukoo mfano
misiba, ugonjwa na maandalizi ya mikutano kama huu Mkuu.
3. Kushawishi ndugu wengine ambao hawajawa
na mwamko au habari kuhusiana na kuwepo kwa Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Kivenule
4. Kudumisha mahusiano mema baina ya
wanandugu
KUNDI
NA. 2
Ushirikiano katika Nyanja Mbalimbali
1. Elimu: Tuaangalie
uwezekano wa kusaidiana katika kupata na kuinue kiwango cha Elimu katika Ukoo
bila kujali kipato kwa kujitoa zaidi.
2. Tuondoe aibu ya kuomba
msaada. Toa shida zako kwa ndugu zako ili tusaidiane katika kuzitatua.
3. Tuondoe ukiritimba
katika kuchangia hasa katika ugonjwa. Tusaidiane katika ugonjwa.
4. Iundwe Kamati ili iwe na mwelekeo kamili
wa kuuinua ukoo.
5. Tupeane taarifa wakati wa matatizo ili
kila ndugu awe na taarifa na ashiriki kikamilifu.
6. Hata katika starehe
zetu pia tusaidiane mfano Harusi.
7. Tutangulize utu
mioyoni mwetu kabla ya pesa (tuwe na moyo wa kusaidiana na kufarijiana)
8. Tusibaguane,
tusiangalie kipato. Wewe mwenye kipato tumie muda wako kumsaidia asiye na
kipato.
KUNDI NA. 3
Kusaidiana
na Kutembeleana
1. Huwezi kumfahamu au kumjua ndugu yako
kama ana matatizo au la hasha kama hujamtembelea.
2. Ujali zaidi ndugu kuliko kujali kipato
chao
3. Eleza hali halisi ya matatizo uliyonayo
hasa pale ukitemblewa na ndugu zako.
4. Ukiona ndugu yako anadorora katika
maisha, hasa pale unapomtembelea basi mpe mawazo ya kumjenga ili naye apige
hatua ya maendeleo.
KUNDI NA. 4
Kuondoa
Tofauti Baina ya Ndugu
1. Matatizo yanayoleta migogoro ndani ya ukoo
yatatuliwe mapema zaidi.
2. Tupanue wigo wa kusaidiana ndani ya
familia bila kujali huyu tupo tumbo moja au hapana.
3. Kila eneo liwe na kamati ya mipango ya
kuratibu matatizo ndani ya ukoo.
4. Kuacha ubinafsi; tuache ubinafsi ndani
ya ukoo.
5. Mtu alishukuru kwa kusaidiwa ndani ya
ukoo, jambo hili litusaidie hata kwa sisi wanaukoo kuwasaidia wengine.
6. Haki itendeke sawa katika kupanga
maamuzi bila kujali huyu ni msomi, hana kipato, mzuri n.k. tukifanikiwa hili,
ukoo utakwenda mbali.
7. Wazazi wawe waangalifu katika kutoa
maamuzi kwa watoto wao, bila kupendelea mtoto na kadhalika.
8. Tuwekane sawa bila kujali huyu ni nani,
tuambiane ukweli katika mkutano huu.
9. Watu ndani ya ukoo wanene kwa vinywa
vyao kama kuna tofauti baina ya ndugu ili tuweze kuondoa tofauti ndani ya Mkutano
huu.
10.
Tutoe
matatizo yetu leo, ili kesho tupate majumuisho. Hivyo mtu (mwanandugu) awe huru
kuongea na awe huru katika maisha yake ya kila siku.
MAJUMUISHO
§
Tusaidiane
katika nyanja mbalimbali iwe katika Elimu, Ajira, maisha na kwingineko. Tuige
mfano wa Wachaga katika kusaidiana.
§
Tofauti
ya maisha baina ya wanandugu ni kitu cha kawaida, hata vidole havipo sawa.
§
Tunapojenga
nguvu ya wanandugu tuondoe matabaka.
§
Hapa
hapa Kidamali ndugu hawaelewani, tatizo hili ni kubwa sana, hata ndugu yako wa
karibu hawezi akasema, leta watoto wapate chakula kwangu kama ilivyokuwa siku
za nyuma.
MADA YA TATU
ELIMU NA MUSTAKABALI WA UKOO
Elimu ni kitu cha msingi sana katika
maisha ya binadamu. Elimu ni mwongozo wa fikra za binadamu katika kuyamudu,
kuyatambua, kuyadhibiti na kuyatawala mazingira ya aina yoyote yanayomzunguka.
Elimu ni dira katika maisha yetu ya kila siku. Elimu inasaidia katika utambuzi
na ufahamu wa mambo mengi katika maisha yetu ya kila siku.
Zamani koo nyingi hapa kwetu zilipuuza
sana Elimu. Umuhimu wa Elimu haukuzingatiwa kabisa. Idadi ya watu waliosoma
kadri siku zinavyozidi kwenda mbele ilipungua na imeendelea kupungua sana na
hivyo kufanya kiwango cha elimu pia kupungua katika jamii zetu. Kukosa Elimu
kumewakosesha wanaukoo nafasi katika sekta mbalimbali za kimaendeleo mfano
sekta ya binafsi, sekta ya umma (serikali) na sekta za kijamii (jamii
huria).
Ukoo wa Kivenule una vipaji vingi,
lakini Elimu inaweza kuwa ni kikwazo cha mafanikio. Kukosekana kwa elimu
pengine kunasababisha jamii ya Kivenule kushindwa kuwa mahusiano (interaction)
na jamii nyingine katika kujiletea maendeleo na hasa kutokana na kukua kwa Sayansi
na Teknolojia au vinginevyo. Mabadiliko ya sayansi na teknolojiayanauweka Ukoo
wa Kivenule njiapanda na hivyo kupoteza mwelekeo.
NAFASI YA UKOO WA KIVENULE KATIKA ELIMU
1. Tumegundua kuwa nafasi ya
ukoo wa Kivenule katika elimu ni mdogo au upo chini kwa sababu:
- Nafasi za ajira katika maofisi makubwa serikalini ni mdogo.
- Wanaukoo wachache wamepaa ajira katika mashirika makubwa (umma au binafsi) yanayozingatia kiwango elimu katika ajira.
2. Kuwa na idadi ndogo ya
wanaukoo waliofikia elimu ya kiwango cha juu mfano kidato cha 4, 6 mpaka vyuo
vikuu.
3. Wanaukoo kutojua umuhimu
wa elimu.
Ili ukoo uwe na nafasi
elimu tufanyaje?
- Tujitahidi kusomesha watoto wetu hadi elimu ya juu.
- Elimu ya ufundi pia ni muhimu ndani ya ukoo.
- Tuunde kamati katika ukoo itkayoratibu sula zima la ukoo.
- Kukusaya michango kuwasaidia waso na uwezo wa kusomesha.
- Kuwasaidia kusoma watoto wa ukoo wasio na msaada.
- Kuwatafutia watoto wafadhili ili kupata elimu.
- Kubuni miradi ya kusaidia kukua kwa elimu
UMUHIMU WA ELIMU
1. Umuhimu wa elimu ni kuondoa
umaskini ndani ya familia na jamii kwa ujumla.
2. Mtu mwenye elimu anaweza
kusaidia kuinua maisha ya mtu yeyote ambaye hana elimu katika familia.
3. Mtu mwenye elimu anaweza
kubuni mbinu yeyote itakayomwezesha kuyamudu maisha katika:
- Kilimo
- Biashara
- Ufundi
- Uongozi katika sekta mbalimbali nk.
4. Umuhimu wa elimu ni kupanua
upeo wa akili
- Kimawazo
- Kifikra
- Kujiamini katika mambo yake unayoyapanga
- Unakuwa na haiba
- Kujulikana mbele ya watu
DUNIA YA UTANDAWAZI
Utangulizi
Dhana ya utandawazi inahusu kuwepo kwa
ulimwengu usio na mipaka katika maingiliano ya jamii mbalimbali katika shughuli
zao za kiuchumi na kisiasa licha ya kuwepo kwa mipaka ya kijiografia. Dhana ya
"utandawazi" katika kiingereza inaitwa "globalisation",
neno ambalo linatokana na "globe", kwa maana ya umbile la dunia yetu.
Kama tunavyofahamu dunia yetu ina umbile la tufe.
Kwa karne nyingi, walimwengu
walitengenishwa na mipaka ya kimaumbile ya dunia kama vile mito, milima,
mabonde na bahari. Kabla havijaundwa vyombo vya usafiri vyenye mwendo wa kasi
kuliko wanyama kama vile punda na farasi, jamii nyingi zilkaa peke yake bila
kufahamu kama kuna jamii nyingine nyingi katika uso wa dunia. Na kwa sababu
hiyo jamii ziligawanyika katika makundi madogo madogo mengi, yenye tamaduni
tofauti; kwa maana ya lugha, mila na desturi. Haya ndiyo makabila ambayo
yalikuwepo katika mabara yote ulimwenguni.
Kutokana na kukosekana aina yeyote ya
mawasiliano ya lugha, au maingiliano yoyote ya kijamii, jamii nyingi zilizokuwa
jirani ziliishi kwa uadui. Kila mmoja akimshuku mwenzake ni mbaya au hana
thamani. Matokeo yake yalikuwa vita baina ya jamii hizi, mwenye nguvu alimuua
mwenzake, au alimteka kuwa mtumwa au alimgeuza kitoweo.
Kwa jamii nyingi ulimwengu wao ulikuwa
ni kijiji chao. Watu, ni wale wa kabila
lao tu - wengine wote ni "washenzi, wanyika, vyasaka, wanyamahanga,
n.k." (Hii ni mifano ya hapa kwetu Tanzania, lakini hata katika mabara ya
Ulaya na Asia hali ilikuwa ni hiyo hiyo).
Baada ya jamii kuanza kutengeneza vyombo
vya usafiri, hasa vile vya majini, ulimwengu ukaanza kupanuka watu wakaweza
kusafiri sio tu baina ya vijiji na miji ya karibu bali walivuka bahari kubwa na
kwenda kwenye mabara mbali mbali. Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa Utandawazi.
Watu wa jamii mbalimbali walianza
kueneza tamaduni zao huku na kule. Hapa kwetu Afrika tulipata watalii wa kwanza
kabisa kutoka jamii za Wayunani, Waarabu na Wachina kame nyingi kabla ya Wareno
(hawa ndiyo wazungu wa kwanza huku Afrika Mashariki.
Hata hivyo maingiliano baina ya jamii
katika mabara mbalimbali yaliendelea kwa kasi ya wastani tu, kwani nyenzo za
usafiri na kupeleka habari zilikuwa hazina kasi kubwa. Bado safari za meli
zilichukua miezi au miaka baina ya bara na bara na safari za gari moshi pia
zilikuwa za polepole.
Uliundwa mfumo wa Posta wa kimataifa
uliowezesha watu kupashana habari kwa maandishi (barua, magazeti n.k.) lakini
nao pia haukuwa wa haraka sana. Kwa hiyo basi, bado jamii nyingi ziliendelea
kuwa na lugha zao na tamaduni zao ambazo hazijaguswa na mabadiliko kutoka nje
ya jamii zao. Lakini katika kame za 19 na 20 yametokea maendeleo makubwa ya
kitekinolojia ambayo yamesababisha mageuzi makubwa katika maingiliano ya
kijamii: usafiri wa anga, simu, radio, cinema, televisheni na kompyuta.
Tekinolojia hizi mpya zimefanya mipaka ya kijiografia kuwa haina uzito tena.
Watu wanaweza kusafiri popote duniani
kwa muda mfupi tena kwa raha na starehe zaidi, taarifa za habari zinaweza
kufikishwa kwa mamilioni ya watu kwa sauti na picha kwa wakati mmoja katika
muda wa sekunde tu. Huu ndiyo uUandawazi. Huu ndiyo ulimwengu usio na mipaka.
Je, katika ulimwengu huu ulio wazi,
tunahitaji elimu ya namna gani? Tunasema kuwa elimu ni utaratibu wa kurithisha
kutoka kizazi kimoja hadi kingine, maarifa, ujuzi, utamaduni na ustaarabu wa
jamii iIi kuidumisha, kuistawisha na kuiendeleza jamii ile.
Changamoto iliyo kwetu ni kuyaelewa vema
mapana na marefu ya dhana hii ya Utandawazi, kubaini kwa usahihi jamii tunayoikusudia
ni ipi - Tanzania, Afrika Mashariki, SADC au dunia nzima? Na kuafikiana kitaifa
ni maarifa gani, ujuzi gani, utamaduni gani, na ustaarabu gani tunaotaka
kuwarithisha watoto wetu.
UTANDAWAZI KATIKA KARNE VA ISHIRINI NA MOJA
Choy (2004) anatoa maana
ya Utandawazi kwa kusema kuwa Utandawazi ni kasi ya kusambaa kwa watu, mawazo,
huduma, mitaji, bidhaa na mambo mengine kutoka nchi moja kwenda nyingine. Hali
hii inasababishwa na kukua kwa sayansi na teknolojia. Kwa kifupi Utandawazi
unasukumwa na ushindani wa kibiashara ambao umeruhusu utaratibu wa soko huria
ambao umesababisha kupanuka haraka kwa sekta binafsi katika uendeshaji wa
uchumi na kupanua biashara ya kimataifa.
Utandawazi unaendeshwa
na soko Iinalopanuka kwa bidhaa za kila aina kuvuka mipaka ya kitaifa.
Uwekezaji, biashara na habari vimefunguliwa mipaka ya kitaifa. Ripoti ya
shirika la Maendeleo la Kimataifa (UNDP) ya Maendeleo ya Binadamu (1999)
inaeleza kasi ya kuenea kwa utandawazi kwa kusema kuwa "soko likitawala
kijamii na kisiasa matokeo yake utandawazi unawanufaisha wachache wenye nguvu
za kumiliki mali wakati wengine wakiendelea kuwekwa kando katika
ushindani". Ripoti ya UNDP ya mwaka 2004 inathibitisha haya kwa kubainisha
kuwa Marekani pekee inamiliki asilimia 85 ya viwanda vyote duniani vya filamu.
Ripoti hiyo pia imetoa
mfano wa umiliki na matumizi ya mtandao wa Kompyuta duniani na kubainisha kuwa
nchi maskini zina sehemu ndogo sana. Kwa mfano mwaka 1997 nchi maskini zilikuwa
zinatumia asilimia 0.2 ya mtandao wa Kompyuta ukilinganishwa na asilimia 93.3
katika nchi tajiri. Katika mgawanyo wa namna hii ni dhahiri kuwa hakutakuwa na
usawa katika dunia ya utandawazi.
FAIDA ZA UTANDAWAZI
Utandawazi umefungua
milango na kutoa nafasi kwa mamilioni ya watu duniani kunufaika katika nyanja
mbalimbali, kama vile, Kukua kwa biashara, maendeleo ya kiteknolojia, uwekezaji
nje ya nchi na kukua kwa mawasiliano "na mitandao ambavyo vimechochea
kukua kwa uchumi na kuleta maendeleo kwa jamii. Shirika la Maendeleo la Umoja
wa Mataifa (1999) linaripoti kuwa dunia ya sasa ina utajiri mwingi na
teknolojia ya hali ya juu kushinda wakati wowote ule. Aidha utandawazi
umesababisha mataifa kuwa karibu na kufanya dunia kuwa kama kijiji kimoja. Siku
hizi ni rahisi kutoka nchi moja na kwenda nchi nyingine kufanya kazi au
biashara. Aidha, bila hata kwenda unaweza kusoma au kufanya biashara na nchi
nyingine kwa kutumia mitandao.
Kukua kwa mwingiliano
wa watu duniani kumeleta mfumo wa kimataifa ambao unathamini maendeleo ya watu
wote. Masuala ya maendeleo yanajadiliwa na kuwekewa mikakati kimataifa. Hii
inasaidia hata nchi maskini kutoa hoja zake na maslahi yake kulindwa kimataifa.
Mwingiliano wa watu duniani unajaribu kuleta maendeleo katika nchi zote na
kuondoa tofauti zilizopo ili ushirikiano uwe rahisi. Iii tunufaike na fursa
hizi zinazoletwa na utandawazi ni lazima tuwape vijana wetu elimu
itakayowawezesha kuelewa majukumu yao katika jamii yenye amani na utulivu,
inayozingatia haki za binadamu na kudhamini tofauti za mataifa mbalimbali.
USHINDANI UNAOSABABISHWA NA UTANDAWAZI
Kuenea kwa teknolojia
kumepunguza mahitaji ya wafanyakazi wanaotumia nguvu tu bila ujuzi na stadi
katika uzalishaji. Kwa hiyo tunahitaji wasomi wenye ujuzi na stadi za kutosha
iIi nchi yetu isiwe soko la bidhaa za watu wengine. Ni lazima tulenge katika
kujiongezea uwezo wa kunufaika na fursa zinazoletwa na utandawazi. Kwanza
kabisa tunahitaji kuimarisha elimu ya sayansi na hisabati, kwani masomo haya
ndiyo msingi wa teknolojia; iwe ni teknolojia ya mawasiliano (ICT) au
teknolojia ya uzalishaji viwandani.
Kwa hiyo uimarishaji
wa masomo ya sayansi na hisabati ni lazima uanzie
shule za msingi. Na
vivyo hivyo tuendeleze katika madarasa mengine. Wataalamu wa masuala ya
maendeleo wanasema "tofauti ya utajiri kati ya Kaskazini (Ulaya_ na Kusini
(Nchi zinazoendelea) ni Sayansi na teknolojia".
Elimu pia ni nyenzo ya
kuwajenga watoto katika ujasiri, kujiamini na kuthubutu. Hizi ni hulka ambazo
zinaweza kujengwa shuleni kupitia mbinu mbalimbali. Hulka hizi ni misingi imara
ya ubunifu na ushindani hata katika biashara za kimataifa.
ELIMU YENYE MWELEKEO WA UTANDAWAZI
Tujiulize, je ni elimu
gani inayotakiwa iIi kukabiliana na athari za utandawazi katika jamii yetu?
Hili ni swali kwa kila mdau wa elimu. Kila mmoja wetu ajaribu kujibu swali hili
kwa ufasaha. Mimi nitadokezea tu yale ambayo tunaweza kuyafanya.
Elimu itolewayo haina
budi kuwa yenye misingi ya sayansi na teknolojia. Hivyo ni lazima kuimarisha
ufundishwaji na usomaji sayansi na hisabati kuanzia elimu ya msingi. Hali hii
inahitaji kubadilisha mitaala yetu iIi iweze kutoa maarifa ujuzi na stadi
zinazotakiwa, na kumwezesha mhitimu kukabiliana na utandawazi
Sambamba na
ubadilishaji wa mitaala ya shule itabidi kuimarisha mafunzo ya elimu ya ualimu
kwa sababu, pamoja na maendeleo na mabadiliko ya tekinolojia hakuna mbadala ya
mwalimu darasani. Wote tunafahamu kuwa vitabu na mbinu mbalimbali za
kufundishia na kujifunzia anazotumia mwalimu darasani ni bora kuliko matumizi
ya televisheni na kompyuta. Ni kweli kuwa pamoja na utandawazi, kwa miaka mingi
ijayo mwalimu atakuwa hana mbadala darasani.
ATHARI ZA UTANDAWAZI
Hatari ya kutoweka
Utamaduni wa kitaifa: Utandawazi hufungua milango ya kuingiza mawazo na
utamaduni wa kigeni unaotoka zaidi katika nchi zilizoendelea kwenda nchi
zinazoendelea. Hii inahatarisha utamaduni wa nchi zinazoendelea kutoweka. Kwa
mfano inasemekana kuwa mwaka 1998 asilimia 80 ya bidhaa za kiutamaduni duniani
zilitokea katika nchi 13 tu duniani zikiongozwa na zile za Hollywood (UNDP,
2004). Hali hii ni ushahidi kuwa nchi zinazoendelea hupokea sehemu kubwa ya
utamaduni kutoka nje ya nchi zao. Ni jukumu letu kubuni mbinu na mikakati
sahihi na kuhakikisha kuwa utamaduni wetu ulio bora unadumishwa kwa manufaa ya
vizazi vijavyo na maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla.
Uharibifu wa
mazingira: Matumizi makubwa ya rasilimali katika nchi zilizoendelea
yamesababisha nchi maskini kuharibu mazingira. Kwa mfano karatasi, samaki,
madini na bidhaa nyingine zinazotokana na maliasili zimevunwa kiasi kwamba
zjnasababisha kuharibika kwa mazingira na
Baioanuai. Haya
yanathibitishwa na ripoti ya UNDP ya mwaka 2004 inayobaini kuwa kati ya mwaka
1990 na 1997 uwekezaji katika uchimbaji wa madini barani Afrika uliongezeka
maradufu.
Mada ya Elimu na Dunia
ya Utandawazi imeletwa kwenye Mkutano huu iIi tuweze kujiandaa vizuri
kukabiliana na utandawazi ambao hatuwezi kuukwepa. pamoja na mabadiliko mengi
tunayotegemea lakini tuwe na msimamo. Pale ambapo tunaona kuwa misingi yetu
kama taifa itabomolewa, tuchukue hatua za binafsi na za pamoja kuhakikisha kuwa
maadili yetu na utamaduni wetu unadumishwa kwa vijana wetu na jumuiya nzima.
Utandawazi usitufanye tuharibu yale mazuri tuliyo nayo.
NINI KIFANYIKE
KUINUA ELIMU KATIKA UKOO WETU
Umoja wa Ukoo wa
Kivenule una jukumu la kuona kuwa vijana wetu ni rasilimali na nguvu kazi
inayotayarishwa kwa ajili ya ushindani katika dunia ya utandawazi. IIi kufikia
azma hii ni lazima tuwe wabunifu na wepesi kukabiliana na mabadiliko ambayo
yatajitokeza kila mara. Ujuzi na maarifa viwe ndiyo ngao yetu kubwa. Hatimaye
matokeo halisi ya kazi yetu tutayaona tutakapofuatilia vijana wetu waliopitia
kwenye mfumo wetu wa elimu na kuona kuwa wanao ujuzi na stadi za kuwawezesha
kupata ajira katika dunia ya ushindani. Tutakuwa tumefanikiwa kama tutawakuta
wanafunzi wetu wameajiriwa na ni watu wa kutegemewa ndani na nje ya nchi.
Mikakati ambayo
inaandaliwa na Umoja wa Ukoo wa Kivenule katika kuinua elimu katika ukoo ni
pamoja na kuanzisha mfuko ambao utachangiwa na wanaukoo ili kuwasaidia
ndugu/wanaukoo ambao hawana uwezo wa kuwasomesha watoto. Pia, mfuko huo
utasaidia kuwaendeleza ndugu/wanaukoo ambao wamefaulu na hawana uwezo wa
kujisomesha. Mambo mengine muhimu kama sara za shule, vitabu, kalamu za risasi
na wino, ada na vifaa vitatolewa na Umoja wa Ukoo wa Kivenule pindi pale hali
ya mfuko itaboreka.
MAJADILIANO KWENYE MAKUNDI
KUNDI
NA. 1
Nafasi ya Ukoo wa Kivenule katika Elimu
4. Tumegundua kuwa nafasi
ya ukoo wa Kivenule katika elimu ni mdogo au upo chini kwa sababu:
- Nafasi za ajira katika maofisi makubwa serikalini ni mdogo.
- Wanaukoo wachache wamepaa ajira katika mashirika makubwa (umma au binafsi) yanayozingatia kiwango elimu katika ajira.
5. Kuwa na idadi ndogo ya
wanaukoo waliofikia elimu ya kiwango cha juu mfano kidato cha 4, 6 mpaka vyuo
vikuu.
6. Wanaukoo kutojua
umuhimu wa elimu.
Ili ukoo uwe na nafasi
elimu tufanyaje?
- Tujitahidi kusomesha watoto wetu hadi elimu ya juu.
- Elimu ya ufundi pia ni muhimu ndani ya ukoo.
- Tuunde kamati katika ukoo itkayoratibu sula zima la ukoo.
- Kukusaya michango kuwasaidia waso na uwezo wa kusomesha.
- Kuwasaidia kusoma watoto wa ukoo wasio na msaada.
- Kuwatafutia watoto wafadhili ili kupata elimu.
- Kubuni miradi ya kusaidia kukua kwa elimu
KUNDI NA. 2
Umuhimu
wa Elimu
4. Umuhimu wa elimu ni kuondoa umaskini
ndani ya familia na jamii kwa ujumla.
5. Mtu mwenye elimu anaweza kusaidia kuinua
maisha ya mtu yeyote ambaye hana elimu katika familia.
6. Mtu mwenye elimu anaweza kubuni mbinu
yeyote itakayomwezesha kuyamudu maisha katika:
- Kilimo
- Biashara
- Ufundi
- Uongozi katika sekta mbalimbali nk.
5. Umuhimu wa elimu ni kupanua upeo wa
akili
- Kimawazo
- Kifikra
- Kujiamini katika mambo yake unayoyapanga
- Unakuwa na haiba
- Kujulikana mbele ya watu
KUNDI NA. 3
Dunia
ya Utawandazi
Vigezo: Elimu ili tuweze kwenda sambamba na
wenzetu katika dunia ya Utandawazi. Utandawazi unafanya dunia kuwa kama kijiji.
·
Kupitia
elimu watu wanawezeshwa kupambana katika mazuri na mabaya.
·
Wenye
mwanga kidogo katika elimu wawasaidie wengine kuifafanua elimu ya Utandawazi
kwa kubainisha faida na hasara zake.
Udhibiti
Mienendo ya watoto iangaliwe ili kuona
kuwa haiharibiwi na Utandawazi. Kazi za watoto zifuatiliwe kwa karibuni na
wazazi ili wasipate muda mwingi wa kuangalia mambo yasiyowahusu.
Elimu ya Utandawazi kwa walioipata na
umri (wote tuna haki ya elimu, aliyeo na umri mkubwa.
KUNDI NA. 4
Nini
kifanyike ili kuinua Elimu katika Ukoo
1. Watoto wetu wapelekwe shule kwa wakati
unaostahili (Awali, msingi, sekondari nk).
2. Kudhibiti tabia za watoto wetu ili
waweze kusoma vizuri (tabia mbaya).
3. Wazazi wawe wapesi kutoa msaada
unaohitajika kwa watoto (mahiaji ya msingi) kuwajenea mazingira mazuri ya
elimu.
4. Mtoto akifaulu kwenda sekondari mzazi
atoe taarifa kwa wenzetu ili waone uwezekano wa kusaidia mtoto huyo aene
shuleni.
5. Ndugu wawe walinzi wa kila mtoto wa
ndugu anayefanya mambo ya ajabu mitaani.
6. Kubuni mfuko maalum wa elimu ili kusaidia
mapema watoto wanaofaulu, lakini mtoto anaweza kufaulu na asichaguliwe.
MAJUMUISHO
1. Katika dunia ya leo, mambo mengi
yamemezwa na Utandawazi. Jambo la msingi la kuzingatia ni kupata Elimu. Wanaukoo
wote wajitahidi kupata elimu pamoja na kujiendeleza hadi kupata elimu ya juu.
2. Wanaukoo inabidi
tuelekeze (tuwekeze) nguvu na rasilimali zetu katika Elimu.
MADA YA
NNE
UKIMWI NDANI YA UKOO NA ATHARI ZAKE
UKIMWI ni nini?
UKIMWI ni Upungufu wa
Kinga Mwilini mwa binadamu. Kwa lugha ya kigeni, Upungufu wa Kinga Mwilini
hujulikana kama AIDS; yaani kirefu chake “Acquired Immuno Deficiency Syndrome.
Na virusi vinavyoeneza ugonjwa wa UKIMWI kwa lugha ya kigeni hujulikana kama
Human Infection Virus (HIV). Kwa lugha rahisi, neno UKIMWI linaweza
kunyumbulishwa au kumegwa katika herufi za kujitegemea kama tatu hivi; yaani
U – inasimama badala
ya Upungufu;
KI – inasimama badala
ya Kinga; na
MWI – inasimama badala
ya Mwili.
Mwili wa binadamu
umeumbwa na seli za aina mbili; yaani
§
Seli Nyekundi za Damu (Red Blood Cells); na
§
Seli
Nyeupe za Damu (White Blood Cells).
Kinga za mwili ambazo huulinda mwili wa
binadamu kutokana na maambuki ya maradhi mbalimbali hutengenezwa kwenye Seli
Nyeupe za Damu (White Blood Cells). Kwa lugha ya kigeni kinga hizi huitwa
Antibodies.
Virusi vinavyoeneza ugonjwa wa UKIMWI
hukaa muda mrefu sana mwilini mwa binadamu hadi kufikia hatua ya kuweza
kutambulika. Mgonjwa aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI huweza kukao hadi miaka
kumi bila kuleta athari yoyote. Mara nyingi, mgonjwa aliyeambukizwa virusi vya
UKIMWI anaweza kuishi kwa muda mrefu bila kupata madhara yoyote kutokana na
afya ya awali ya mgonjwa, pamoja na aina za vyakula anavyokula.
Kwa wagonjwa ambao afya zao siyo
madhubuti, madhara ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI huweza kujitokeza katika
kipindi cha miezi sita (6) au pungufu ya hapo. Dalili mbalimbali ya maambukizi
ya virusi vya UKIMWI huweza kuanza kujitokeza baada ya kipindi hicho cha miezi sita. Dalili
hizo huwa ni pamoja na:
§
Kushambulia
na magonjwa mbalimbali ya maambukizi mfano Kifua Kikuu (Tuberclosis);
§
Kupungukiwa na uzito mara kwa mara;
§
Kupata
mkanda wa jeshi; na
§
Kutapika
na kuharisha.
NJIA
MBALIMBALI ZINAZOCHANGIA MAAMBUKIZI/KUENEA KWA VIRUSI VYA UKIMWI
Kuna haja kwa wanaukoo wa
Ukoo wa Kivenule pamoja na jamii inayowazunguka kutilia umuhimu suala la kupata
Elimu ya kujua jinsi maambukizi na kuenea kwa virusi vya UKIMWI kunavyotokea,
hii itasaidia jamii yetu na wanaukoo/familia kwa ujumla kuzifahamu njia
mbalimbali mbadala ambazo zinachangia kwa kiwango kikubwa maambukizi ya virusi
vya UKIMWI. Baadhi ya njia hizo zinazosaidia/changia maambukizi ya virusi vya
UKIMWI ni pamoja na:
1.
Kufanya ngoo holela na zisizo salama;
2.
Kutochukua hatua madhubuti za kupima afya na kujitambua/kujijua
kiafya kabla ya kufunga ndoa;
3.
Kushambuliwa na magonjwa mbalimbali ya zinaa bila kwenda
hospitalini kutibiwa;
4.
Kuchangia katika matumizi ya vifaa vya kutogea mfano nyembe,
sindano za mahospitalini, miswaki, mikasi ya mahospitalini na kushika vidondo
vya mgonjwa aliyeambukizwa na virusi vya UKIMWI bila kutumia kinga (gloves);
5.
Kuwekewa damu yenye virusi vya UKIMWI;
6.
Mtoto kuambukizwa virusi vya ugonjwa wa UKIMWI toka kwa mama yake
wakati wa kujifungua;
7.
Mama Mjamzito kutochukua hatua madhubuti/tahadhari ya kupima afya
yake ili kujua kama ana maambukizo ya virusi vya UKIMWI au hapana;
8.
Kurithi wajane;
9.
Wanaukoo/familia kutokuwa waaminifu katika
ndoa zao; na
10.
Mama aliyeathirika na virusi vya UKIMWI
kumnyonyesha mtoto ambaye hajaathirika na virusi vya UKIMWI.
NJIA MBADALA ZA KUJILINDA NA MAAMBUKIZI
WAnaukoo/familia
baada ya kuzifahamu njia mbalimbali mbadala zinazochangia maambukizi ya virusi
vya UKIMWI; sasa wajibu wao mkubwa ni kuielimisha jamii yao kuzitambua njia
kadhaa zinazosaidia kujilinda na maambukizi ya virusi vinavyoleta upungufu wa
kingi mwilini yaani UKIMWI. Hatua hizo madhubuti ambazo ukoo na jamii yetu kwa
ujumla inapaswa kuzichukua ni kutoa elimu kuhusu umuhimu wa:
1.
Kupima afya na kujitambua kama umeambukizwa
virusi vya UKIMWI toka katika vituo mbalimbali vya afya mfano ANGAZA na
mahospitalini;
2.
Kufanya ngono salama kwa kutumia njia mbadala
zinazoshauriwa na wataalamu au kuacha kabisa mpaka muda muafaka utakapofika;
3.
Waathirika wa virusi vya UKIMWI kutojihusisha
katika ngono au hali yoyote ambayo inaweza kuchangia maambukizi ya virusi vya
UKIMWI:
4.
Wanaukoo/familia kuwa waaminifu katika ndoa
zao;
5.
Kwenda hospitali kutibu dalili zozote za
maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Magonjwa ya zinaa huchangia sana katika
maambukizi ya virusi vya UKIMWI;
6.
Mama Wajawazito kupima afya zao kabla ya
kujifungua ili kuwanusuru watoto wanaozliwa wasiathirike na virusi vya UKIMWI
kama mama hao watakuwa wameambukizwa na virusi vya UKIMWI;
7.
Mama aliyeathirika na virusi vya UKIMWI,
kutomnyonyesha mwanae ili kupunguza uwezekano wa kumwambukiza mtoto kama
atathibitika kuwa ameambukizwa;
8.
kuacha kurithi wajane; na
9.
Kuacha mila potofu zinazopotosha mfano kupiga ramli.
JUKUMU LA UKOO/FAMILIA KUKABILIANA NA JANGA LA UKIMWI
Jukumu la Ukoo/Familia
katika kukabiliana na virusi vya maambukizi vinavyoeneza ugonjwa wa UKIMWI ni
pamoja na:
1.
Kutoa na kueneza elimu ihusuyo maambukizi ya virusi vya
UKIMWI kwa watoto na vijana wenye ufahamu na uelewa na hali hali kadhalik kwa
watu wazima;
2.
Kuwaelimisha wanaukoo/familia kuzifahamu njia mbadala za
kujikina na kujilinda a maambukizi ya virusi vya UKIMWI;
3.
Kuwaelimisha wanaukoo/familia kuzifahamu njia mbalimbali
zinazochangia maambukizi na kuenea kwa virusi vya UKIMWI;
4.
Kuwaelimisha wanaukoo/familia kujenga tabia ya kupenda
kupima afya zao na kujua kama wameambukizwa virusi vya UKIMWI au hapana;
5.
Kuwaelimisha wanaukoo/familia kuwa waaminifu katika ndoa
zao ili kupunguza hatari ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI; na
6.
Kuwaelimisha wanaukoo/familia kuishi katika misingi ya
Dini na Maadili mema.
Pia muhimu sana
kukatolewa Elimu ya kujua jinsi maambukizi na kuenea kwa virusi vya UKIMWI
kunavyotokea, hii itasaidia jamii yetu na wanaukoo/familia kwa ujumla
kuzifahamu jia mbalimbali mbadala ambazo zinachangia kwa kiwango kikubwa
maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Baadhi ya njia hizo zinazosaidia/changia
maambukizi ya virusi vya UKIMWI ni pamoja na:
1.
Kufanya
ngoo holela na zisizo salama;
2.
Kutochuku
hatua madhubuti za kupima afya na kujitambua/kujijua kiafya kabla ya kufunga
ndoa;
3.
Kushambuliwa
na magonjwa mbalimbali ya zinaa bila kwenda hospitalini kutibiwa;
4.
Kuchangia
katika matumizi ya vifaa vya kutogea mfano nyembe, sindano za mahospitalini,
miswaki, mikasi ya mahospitalini na kushika vidondo vya mgonjwa aliyeambukizwa
na virusi vya UKIMWI bila kutumia kinga (gloves);
5.
Kuwekewa
damu yenye virusi vya UKIMWI;
6.
Mtoto
kuambukizwa virusi vya ugonjwa wa UKIMWI toka kwa mama yake wakati wa
kujifungua;
7.
Mama
Mjamzito kutochukua hatua madhubuti/tahadhari ya kupima afya yake ili kujua
kama ana maambukizo ya virusi vya UKIMWI au hapana;
8.
Kurithi
wajane;
9.
Wanaukoo/familia kutokuwa waaminifu katika ndoa zao; na
10.
Mama aliyeathirika na virusi vya UKIMWI kumnyonyesha
mtoto ambaye hajaathirika na virusi vya UKIMWI.
WAnaukoo/familia baada
ya kuzifahamu njia mbalimbali mbadala zinazochangia maambukizi ya virusi vya
UKIMWI; sasa wajibu wao mkubwa ni kuielimisha jamii yao kuzitambua njia kadhaa
zinazosaidia kujilinda na maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Hatua hizo madhubuti
ambazo ukoo na jaii yetu kwa ujumla inapaswa kuzichukua ni kutoa elimu kuhusu
umuhimu wa:
1.
Kupima afya na kujitambua kama umeambukizwa virusi vya
UKIMWI toka katika vituo mbalimbali vya afya mfano ANGAZA na mahospitalini;
2.
Kufanya ngono salama kwa kutumia njia mbadala
zinazoshauriwa na wataalamu au kuacha kabisa mpaka muda muafaka utakapofika;
3.
Waathirika wa virusi vya UKIMWI kutojihusisha katika
ngono au hali yoyote ambayo inaweza kuchangia maambukizi ya virusi vya UKIMWI:
4.
Wanaukoo/familia kuwa waaminifu katika ndoa zao;
5.
Kwenda hospitali kutibu dalili zozote za maambukizi ya
magonjwa ya zinaa. Magonjwa ya zinaa huchangia sana katika maambukizi ya virusi
vya UKIMWI;
6.
Mama Wajawazito kupima afya zao kabla ya kujifungua ili
kuwanusuru watoto wanaozliwa wasiathirike na virusi vya UKIMWI kama mama hao
watakuwa wameambukizwa na virusi vya UKIMWI;
7.
Mama aliyeathirika na virusi vya UKIMWI, kutomnyonyesha
mwanae ili kupunguza uwezekano wa kumwambukiza mtoto kama atathibitika kuwa
ameambukizwa;
8.
kuacha
kurithi wajane; na
9.
Kuacha
mila potofu zinazopotosha mfano kupiga ramli.
Wanaukoo/familia wana jukuu pia la
kuwahudumia wale ambao tayari wameambukizwa na virusi vya UKIMWI ili waendelee
kujihusisha na shughuli za uzalishaji mali na kupunguza utegemezi. Baadhi ya
majukuu hayo ya wanaukoo/familia ni pamoja na:
1.
Kuwapenda
na kuwasaidia wagonjwa wote waliathirika na virusi vya UKIMWI;
2.
Kutowanyanyapa
wagonjwa walioathirika na virusi vya UKIMWI;
3.
Kuchukua
hatua madhubuti za kuwasaidia waathirika wa virusi vya UKIMWI kupata dawa za
kurefusha maisha. Mfano wa dawa hizo ni RVA,
4.
Kuwathamini
wagonjwa waliambukizwa na virusi vya UKIMWI; na
5.
Kuwasaidia
wagonjwa waliambukizwa na virusi vya UKIMWI kupata vyakula vya kuujenga na
kuulinda mwili.
Kuna Hamasa, Mbinu au Falsafa mbalimbali
ambazo wanaukoo/familia wanaweza kuzitumia katika kupambana na gonjwa hili. Hii
ni pamoja na kuzingatia matumizi ya J&; yaani waone umuhimu wa:
1. KUJITAMBUA;
2. KUJIHESHIMU;
3. KUJIPENDA;
4. KUJITHAMINI;
5. KUJIAMINI;
6. KUJILINDA;
na
7. KUJIDHIBITI.
Medani kadhaa ambazo wanaukoo/familia
wanaweza kuzitumia kuepukana au kuwa mbali na maambukizi ya virusi vya UKIMWI
ni pamoja na:
1. Kusema
hapana (kukataa) ushawishi wa aina yoyote;
2. Kuongea
na kutokukubali kuburuzwa;
3. Kuondoa
woga na kupima afya yako;
4. Kupunguza matumizi ya vileo au kuacha
kabisa;
5. Wanaukoo/familia kuwa waaminifu katika ndoa
zao;
6. Wanaukoo/familia
kujiepusha na vishawishi;
7. Wanaukoo/familia
kuulinda ujana na utu uzima wao;
8. Kujibidisha
katika kazi na hivyo kupunguza fikra zisizo za msingi; na
9. Kusoma
vitabu na magazeti baada ya kazi.
Kwa kufanya hivyo, yote hayo
yaliyopendekezwa katika makala hii, nafasi hii, nafasi ya jaii hii ya ukoo wa
KIVENULE itakuwa imepiga hatua muhimu katika kukabiliana na kupambana na
maambukizi ya virusi vinavyoeneza gonjwa la UKIMWI.
MAJADILIANO KWENYE MAKUNDI
KUNDI
NA. 1
UKIMWI
ni nini?
1. Maana: Upungufu wa Kinga Mwilini
2. Upungufu wa kinga unasababisha
kukosekana au kuuawawa kwa chembechembe nyeupe za damu (white blood cells)
ambazo husaidia kuzuia maambukizo ya magonjwa mbalimbali mwilini
3. Kinga hiyo inapopungua mwilini
husababisha mtu kuugua magonjwa mbalimbali mfano malaria, TB Kifua Kikuu,
Kuharisha na kadhalika.
KUNDI
NA. 2
Namna gani UKIMWI unavyoweza kuenea
1. Kurithi wajane
2. Ngono uzembe
3. Ulevi wa kupindukia
4. Kutokuwa waaminifu katika ndoa
5. Kukosa maadili ya dini
6. Michilizi ya damu
7. Kushirikiana katika matumizi ya sindano
na vifaa vya kutibia visivyo salama.
8. Kuongezewa damu yenye virusi.
9. Kwa njia ya kunyonyesha.
10.
Wakati
wa kujifungua
11.
Kwa
njia ya kushirikiana miswaki.
KUNDI
NA. 3
Njia Mbadala za Kujilinda na Maambukizi ya UKIMWI
1. Kuanzisha shughuli mbalimbali.
2. Kupunguza ulevi wa kupindukia mfano: mtu
alisema kunywa Pombe si starehe ila kwenye Pombe kun starehe.
3. Wanandoa kuwa waaminifu.
4. Kuepukana na utumiaji wa vifaa visivyo
salama.
5. Kufuata Maadili ya Mungu.
6. Kuwa wazi katika mazungumzo yanayohusu
UKIMWI.
7. Kupima afya.
8. Kutumia zana za kujilinda na maambukizi
ya Virusi vya UKIMWI.
9. Kukimbilia mijini.
10.
Kutumia
Madawa ya Kulevya.
11.
Wazazi
na wakubwa kuwa wazi kwa watoto wao.
12.
Kuepuka
vishawishi mbalimbali.
13.
Kurithi
wajane au kurithiwa.
14.
Kuweka
wazi mtu akifariki.
KUNDI NA. 4
Jukumu la Ukoo/Familia Kukabiliana na Janga la UKIMWI
1. Elimu itolewe kwa wana
ndugu wote juu ya UKIMWI.
2. Wanandoa kuwa
waaminifu katika ndoa zao.
3. Wanandugu kujihusisha
katika kazi na kushiriki michezo mbalimbali.
4. Kuhimiza matumizi ya mipira
ya plastiki (gloves) katika uoshaji wa maiti, nguo na kadhalika.
5. Kuwatimizia watoto
wanaosoma mahitaji yao mfano fedha nk.
6. Kutozalia majumbani (Wakunga)
7. Ukeketaji ukomeshwe
8. Kubusu maiti.
9. Kuficha maradhi.
MADA YA TANO
DINI KATIKA UKOO
UTANGULIZI
Tuna msemo unaotukumbusha
hivi, hakuna mtu anayependa kuishi peke yake, au aliye kama kisiwa na hakika
kweli. Hatuishi wala hatuwezi kuishi hivyo, yaani kuishi watu pekee, watu
waliotengwa na wenzao kama vile kisiwa kilichotengwa na nchi kavu.
Twawahitji wengine wengi ili
tujisikie tumeungana na watu tumkuwa kitu kimoj na wanadau wenzetu.
Tunaangalia maisha yetu ya
kila siku tunaona mifano mingi. Nikiona furaha nahitaji kushirikiana na mtu
mwingine. Tukipatwa na misib, magonjwa tunahitji kutulizwa, kufarijiwa na
kusaidiwa na wengine.
Tena kuna vifungo
vinavyotuunganisha vyaweza kuwa ni urafiki, ujamaa, ujirani uhusiano wa kikazi
na kadhalika. Kati yangu na watu wengine.
Pamoja na vifungo hivyo
tulivyovitaja vinavyotuunganisha katika maisha ya kawaida, kuna kifungo kikuu
ambacho kinaweza kutuunganisha au kuniunganisha mimi, na hicho kifungo si
mwingine ila ni Mungu. Mungu ndiye kifungo pekee kinachotulte uhusiano wa
kawaida uliopo kati ya Mungu na Mimi au wewe, ndio tunachokiita Dini.
NINI
MAANA YA DINI?
Neno hili Dini ni neno ambalo pengine umelisikia
mara nyingi, na pengine hatuelewi maana yake lakini linaweza kuwa na maana
nyingi sana. Endapo ukimwuliza ndugu yeyote maana ya dini, natumaini utapata
majibu mengi sana na yote yatakuwa yanaelezea maana halisi ya dini.
Dini ni Imani ya Kuamini kitu
au jambo fulani kuwa linaweza kumsaidia binadamu kupata mahitaji yake. Ndani ya
Dini kuna kitu ambacho huwa ni nguzo kwa yule anayeamua kuwa katika dini fulani.
Nguzo hiyo ni Imani. Imani inampelekea binadamu kuweza kujitengenezea utaratibu
wa kutolea heshima, kufanya ibada ikibidi hata kuitolea Sadaka.
Maana hii ya
pili; Dini ina maana hasa ya kufungamana na kuhusiana. Kwa maneno mengine Dini
ni uhusiano, urafiki, ushirikiano uliopo Kati ya Mungu na Binadamu. Maana hii
ya pili inamweleza hasa Mungu Mmoja Muumba Mbingu na Nchi.
Maana hii ya pili
inaonyesha utofauti wa maana ya kwanza ambayo inaonyesha inaweza kuhusisha
Miungu zaidi ya mmoja. Maana ya pili ya dini ndiyo inayoaminiwa na watu wengi
au mamilioni ya watu katika ulimwengu huu.
Msingi mkuu wa Dini ni
Imani. Kila mtu ana dini. Mtu mwingine anaamini kukaa peke yake na hiyo
ndiyo dini yake. Imani ni tabia ya ndani
aliyonayo mtu. Imani ya ndani huzaa tabia. Tabia huonekana nje. Dhehebu ni
muunganiko wa watu wenye tabia. Kama ukoo tunaweza kutengeneza dhehebu letu.
Dini ilianza lini
Hili linaweza kuwa ni
swali karibu kwa mmoja wetu kuwa Dini ilianza lini? Kwa kweli Dini imeanza zama
za kale kabisa, binadamu alipoanza kuwa binadamu.
Watu wa Sayansi
walichunguza mianzo ya binadamu, wanatuambia kwamba binadamu alipovumbua
ulimwengu na kujitambua mwenyewe, pale pale alitamua pia mtu aliye mkubwa
kuliko binadamu, na huyo si mwingine ila ni Mungu.
Aina ya Miungu
Kabla ya Mungu
hajajionyesha, kuna Miungu ambayo watu wa kale waliiabudu na kuitumikia Miungu
hiyo ni ile iliyotokana na vitu vilivyoumbwa na Mungu navyo ni:
ANU Mungu Mbingu
EA Mungu Maji
ENIL Mungu Upepo
SHAMASH Mungua
Juan a Dunia na kadhalika
Hii ndiyo Miungu waliyoiabudu hapo kale
lakini haikuwa Miungu ya Kweli.
Dini
za Kiulimwengu
Baada ya kuona Miungu waliyoiabudu hapo
kale imepitwa na wakati, hapo baadaye watu walianzisha Dini za Kiulimwengu
ambazo zilianza huku Bara la ASIA katika nchi za China na India. Mawazo hayo
yaliyojitokeza kabla Mungu hajajifunua au kujionyesha kuanzisha dini yake
Mungu. Mawazo yao juu ya kumtafuta Mungu yalikuwa mazuri isipokuwa namna zao
zilikuwa kinyume na Mungu.
Dini
Zenyewe za Kiulimwengu
Dini ya Kihindu ilianza mwaka 2500 KK.
Imani ya Dini hiyo waliamini uwepo wa Mungu katika kila kiumbe kilicho hai
mfano……. Hivyo kutokana na Imani hiyo walithamini sana Uhai wa kila Kiumbe.
Dini ni KIBUDHA hii ilianzishwa mwaka
560 KK. Imani yao waliamini kuwa maisha ya binadamu ni mateso, mateso kutokana
na kutamani mambo yasiyo kidhi mahitaji ya Roho.
Hivyo walijitahidi kuepuka mates ohayo
kwa kutimiza maneno nan. Maoni halisi – misemo halisi - mndo mzuri wa maisha – amaa nzuri – na
kadhalika. Hivyo walijitahidi sana kuongea na kutenda vizuri kila wakati.
Dini
ya Mungu
Baada ya dini hizo za kiulimwengu Mungu
saa anajionyesha au kujifunua, japo hakujifunu katika kila taifa. Alijifunua
katika taifa la Israel kwa KUMWITA IBRAHIMU. MUNGU alijionyesha kwa mpango huo
ili watu wamtambue jinsi alivyo, watu waone kuwa yeye ni Mungu wa namna gani
mwa 12 – 13.
Mungu alijitambulisha kwa Ibrahi katika
Taifa la Israel kwa msimamo huu kuwa
MUNGU NI MOJA NA HAKUNA MWINGINE; ila ni
yeye tu, nah ii ndiyo imani kwa Israel kuwa Mungu I mmoja tu.
Msingi huo wa Imani kwa Israel
uliandikwa katika maandiko ya Kiyahudi na iliitwa kifungu cha Sikiliza Ee Israel.
Hili ilikuwa SALA ya Asubuhi kila siku na ni muhimu waifahamu na kuisali.
SALA YENYEWE: Sikiliza Ee Israel Bwana
Mungu ni mmoja. Nawe umpende Bwana Mungu wako kwa moyo wake wote na kwa Roho
yako yote, na kwa Nguvu zako zote… Kumb 6:4 – 5, 13 – 14.
Dini
Kubwa zinazofuata Mpango wa Mungu Mmoja
1.
Dini ya Kikristo
Dini hii Asili yake na Mpango wake ni
Mungu Mmoja Muumba Mbingu na Nchi. Tukianzia na Ibrahim pamoja na historia
nzima ya Ukoo wa Yesu na Kanisa lake yaani Mitume.
Dini hii ya Kikristo ina madhehebu yake
ambayo yanamwamini MUNGU mmoja kwa njia ya Yesu Kristo. Na kila anayemwamini
MUNGU hana budi kufuat Mwongozo wake kwa kushika NENO LA MUNGU kulifuaa na kuwa
na maisha nao, kwa kushika kiaminifu Amri 10 za Mungu na sheria zake. Pamoja na
hayo kumheshimu, kumwabudu, kumwomba, kumpenda katika siku zote za maisha.
2.
Dini ya Kiislamu
Hii pia inamwamini Mungu Mmoja ALLAH, na
mjumbe wake ni Mtume MOHAMED SALLALEI WASALAM Dini hii pia ina madhehebu yake.
Dini hii inahimiza kila Mwislamu anayemwamini MUNGU (ALLAH) anahimizwa kuisoma
KORAN au MSAHAFU na kushika maagizo ya Mungu (ALLAH) kutoka kwa mjumbe wake
aliyefunuliwa Mtume MOHAMED, pamoja na kufuata Nguzo Tano (5) za Uislamu.
Dini hizi mbili na madhehebu yake
zinazomwamini Mungu Mmoja, zinawahimiza waamini wake pamoja na watu wote kuona
umuhimu wa kujiunga na Dini ili kuona Upendo wa MUNGU (ALLAH) kwani kujiunga
katika Dini zilizo za kweli kutawafanya watu waishi kwa Amani na Upendo hapa.
Duniani na huko Mbinguni aliko MWENYEZI MUNGU.
UMUHIMU
WA KUWA NA IMANI
Umuhimu wa kuwa na Imani (Dini)
unajengeka katika maeneo mbalimbali. Kuwa na Imani kuna faida zake ambazo
mshika Imani hufaidi, hii ni pamoja na:
1. Dini huondoa tofauti zetu.
2. Dini huondoa chuki, fitina na unafiki.
3. Dini hutoa elimu ya ufahamu wa mambo
mengi.
4. Dini hujenga tabia ya kusaidiana,
kuondoa chuki, kuondo tofauti.
5. Dini hujenga uhusiano mkubwa baina ya
Mungu na Binadamu.
6. Dini hupunguza ushirikina.
7. Dini hupunguza woga wa
kuogopa mtu kutokana na uwezo, uchawi na kadhalika.
8. Kuishi kwa imani hata
kama una matatizo mfano kufiwa; humfanya aamini kuwa Mungu ndiye mweza.
9. Dini humfanya mtu kuwa
na mtazamo baadaye baada ya kifo hivyo anakuwa Mnyenyekevu.
MAADILI NA DINI
Dini, Imani, Dhehebu
na Maadili huenda pamoja. Dini ni Imani. Msingi wa Dini ni Imani. Kila mtu ana
Dini. Mtu anayeamini kukaa peke ndiyo dini yake. Imani ni tabia ya ndani
aliyonayo mtu. Imani ya ndani huzaa tabia. Tabia huonekana nje. Dhehebu ni
muunganiko wa watu wenye tabia ya aina mmoja. Kama ukoo tutengeneze dhehebu
letu ambalo sisi kama wafuasi wake tutakuwa na matarajio fulani. Liwe ni
dhehebu la kuwajali waumini wake, dhehebu lenye kuheshimu na dhehebu lenye
kujengea uwezo wa kiuchumi, kiakili na kiafya.
Maadili nayo hujengwa
kwa msingi wa imani na dini. Watu walio katika imani hujijengea maadili fulani
ambayo huweza kuwatofautisha na jamii nyingine. Kwa mfano maadili fulani ambayo
hufuatwa na waumini wa dini fulani, huwafanya watembee bila ya kuvaa viatu,
wale mlo kwa siku, kujitolea muda wao wote kuwatumikia watu wengine, kukesha
usiku kucha kanisani wakiomba na kadhalika. Haya huwa ni maadili yanayoridhiwa na
kukubaliwa na kundi fulani la watu au jamii, wayafuate.
Maadili ni miiko
ambayo huweza kufuatwa na jamii fulani ili kuweza kutimiza malengo yao. Kwa
mfano katika makanisa mbalimbali ya Kikristo kuna Amri za Mungu au Kanisa
ambazo tunaweza kuzifananisha na Maadili katika maisha yetu ya kila siku. Kwa
mfano katika Kanisa Katoliki kuna Amri Kumi za Mungu, ambapo kina mwanakatoliki
anawajibu wa kuzitimiza. Amri hizo tukizileta katika maisha yetu ya kawaida ya
kibinadamu tunaweza kuziita ni maadili, kwa sababu zipinga tabia zile ambazo
hazikubaliki na jamii zetu. Kwa mfano baadhi ya Amri za Mungu zinasema
yafuatayo : Usiibe, Usiue, Usiseme Uwongo, Usitamani Mali ya Mtu, Usimtamani
Mwanamke Asiye Mke wako, Usizini, Umpende Jirani Yako kama unavyojipenda na
kadhalika.
Katika maisha yetu ya
kila siku Amri hizo za Mungu ni mfano wa Maadili Mema ambayo kila mtu au ndugu
analazimika kuyafuata ili kuweza kukubalika katika jamii yake. Kwa mfano tabia za uongo, uzinzi
na uasherati, wivu mbaya, tamaa mbaya, wizi, kuua ni baadhi ya tabia mbaya ambazo
hazikubaliki kabisa na ni kinyume cha maadili. Kwa hiyo Dini na Maadili vina
mahusiano makubwa na ya muhimu sana. Kama jamii, tuna jukumu la kuhakikisha
kuwa wanaukoo wanakuwa waumini wazuri katika Dini zao, kwani kwa kufanya hivyo
tutajenga jamii yenye maadili mema.
UKOO ULIOJENGEKA KATIKA MISINGI YA DINI
1. Ukoo uliojengeka
katika misingi ya dini unakuwa hauna ubinafsi.
2. Ukoo uliojengeka
katika dini utakuwa ni ukoo unajaliana katika matatizo kutokana na imani
walionayo kutokana na Dini zao.
3. Watu Kuheshimiana: Dini inafundisha mambo mema;
Kwa hiyo ukoo utakapokuwa na mwamko wa dini hakutakuwa na matatizo ya
kudharauliana.
4. Kuheshimika kwa Ukoo: Kwa kuwa utakuwa na sifa
nzuri basi hata koo nyingine zitapata hamasa ya kujiunga na ukoo.
5. Ukoo unapunguza imani potofu : Kwa mfano kama wanaukoo watafuata misingi ya dini zao, hawawezi
kuwa na imani za kishirikiano au kufikiria kwenda kwa waganga wa jadi ili
kutatua matatizo yao.
MAJADILIANO KWENYE MAKUNDI
KUNDI
NA. 1
Maana ya Dini
Ni Imani aliyonayo mtu
juu ya jambo fulani. Pia ni Msingi fulani ambao mwanadamu anaufuata.
KUNDI
NA. 2
Umuhimu wa Kuwa na Imani
1. Umuhimu wa Kuwa na
Imani ni pamoja na kutoogopa kitu chochote kwa kuwa una Imani.
2. Utakuwa na imani ya jambo lolote lile.
3. Kila jambo utakalolifanya utakuwa na
Imani nalo.
4. Ukiwa na Imai
utajulikana na mtu yeyote.
5. Imani itajenga
mahusiano ndani ya familia, ndugu, jamaa, majirani, marafiki nk.
KUNDI NA. 3
Maadili
na Dini
1. Dini ianzie kwenye familia
2. Familia ikia na maadili mema ya Dini
itakuwa sambamba.
3. Wazazi wawe mstari wa mbele kuelimisha
familia
4. Wazazi wawe mfano kwa familia
5. Wazazi wawe wasikivu (kuwasikiliza)
watoto wanapohitaji kusikilizwa.
KUNDI
NA. 4
Ukoo Uliojengeka katika Misingi ya Dini
6. Ubinafsi: Ukoo uliojengeka katika misingi ya dini unakuwa hauna
ubinafsi.
7. Ukoo uliojengeka
katika dini utakuwa ni ukoo utakaokuwa unajaliana katika matatizo kutokana na
imani walionayo kutokana na Dini.
8. Watu Kuheshimiana: Dini inafundisha mambo mema;
Kwa hiyo ukoo utakapokuwa na mwamko wa dini hakutakuwa na matatizo ya
kudharauliana.
9. Kuheshimika kwa Ukoo: Kwa kuwa utakuwa na sifa
nzuri basi hata koo nyingine zitapata hamasa ya kujiunga na ukoo.
XII: RATIBA YA MKUTANO MKUU WA KWANZA WA UKOO WA KIVENULE,
DESEMBA 17 – 18, 2005
Siku ya Kwanza ya Mkutano Mkuu wa Ukoo wa KIVENULE |
||
Tarehe
17 Des. 2005 Muda
|
Shughuli/Jukumu
|
Wahusika
|
12:00–12:45
|
Wageni Wote
Kuamka na Kufanya Maandalizi ya Kuingia kwenye Mkutano
|
Wote |
12:45–1:45
|
Kupata
Kifungua Kinywa
|
Wote
|
1:45 – 2:45
|
Kuwasili
Mkutanoni na Kujisajili
|
Wote
|
2:45 – 3:15
|
Ufunguzi wa
Mkutano na Mgeni Rasmi
|
Mgeni Rasmi
|
3:15 – 4:00
|
Utambulisho
baina wa wana Ndugu
|
Wote
|
4:00 – 4:45
|
Pumziko la Chai / Kahawa/Maji
|
Wote
|
4:45 – 5:30
|
Mada ya Kwanza: CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO |
1. Christian J. Kivenule2. Augustino Kivenule |
5:30 – 6:00
|
Majadiliano
katika Makundi
|
Makundi 4
|
6:00 – 6:20
|
Murejesho
na Majumuisho
|
Vikundi na
Mwezeshaji
|
6:30 – 8:00
|
CHAKULA CHA
MCHANA
|
Wote
|
8:00 – 8:45
|
Mada ya
Pili: MAHUSIANO BAINA YA NDUGU NDANI YA UKOO WA KIVENULE
|
1. John S. Kivenule
2. Ignas P. Kivenule
3. Stephan Mhapa
|
8:45 – 9:15
|
Majadiliano
katika Makundi
|
Makundi 4
|
9:15 – 9:45
|
Murejesho
na Majumuisho
|
Vikundi na
Mwezeshaji
|
9:45– 10:45
|
Pumziko la Chai/Kahawa/Maji |
Wote
|
10:45-1:30
Usiku
|
Mapumziko
Marefu (Kusalimiana na Kufahamiana zaidi)
|
Ndugu na
Wageni Wote
|
1:30 – 2:30
|
Chakula cha Usiku na Vinjwaji
|
Ndugu Wote
|
2:30 – 6:30
|
Burudani
(Muziki wa Kisasa na Ngoma za Asili)
|
Wote
|
Siku ya Pili ya Mkutano Mkuu wa Ukoo wa KIVENULE |
||
Tarehe
18 Des. 2005 Muda
|
Shughuli/Jukumu
|
Wahusika
|
12:00–
12:45
|
Kuamuka na
Kufanya Maandalizi ya Mkutano
|
Wote |
12:45 –
1:45
|
Kifungua
Kinywa
|
Wote
|
1:45 – 2:15
|
Kuwasili
Mkutanoni na Kujisajili
|
Ndugu wote |
2:15 – 2:45
|
Mada Ya
Tatu: ELIMU NA MUSTAKABILI WA UKOO WA KIVENULE
|
1. Christian J. Kivenule
2.
Donat Mhapa
|
2:45 – 3:15
|
Majadiliano
kwenye Makundi
|
Makundi 4
|
3:15 – 3:45
|
Murejesho
na Majumuisho
|
Vikundi na
Mwezeshaji
|
3:45 – 4:30
|
Pumziko la Chai/Kahawa/Maji
|
Wote
|
4:30 – 5:00
|
Mada ya Nne: UKIMWI NDANI YA UKOO NA ATHARI ZAKE |
1.
Maria
Milimo
2.
Adam
A. Kivenule
|
5:00 – 5:30
|
Majadiliano kwenye Makundi |
Makundi 4 |
5:30 – 6:00
|
Murejesho na Majumuisho |
Vikundi na Mwezeshaji |
6:00 – 7:15
|
CHAKULA CHA
MCHANA
|
Wote |
7:15 – 7:45
|
Mada ya Tano: DINI KATIKA UKOO |
1. Jovin D. Kivenule
2.
Stephan
Mhapa
3. George Kivenule |
7:45 – 8:15
|
Majadiliano kwenye Makundi |
Makundi 4 |
8:15 – 8:45
|
Murejesho na Majumuisho |
Vikundi na Mwezeshaji |
8:45 – 9:45
|
Majumuisho:1. Yote Yaliyojitokeza
2.
Matarajio
3. Tarehe ya Mkutano Mwingine |
Mwezeshaji |
9:45 –
10:15
|
Shukurani
toka kwa Ndugu Mbalimbali
|
|
10:15–11:00
|
KUCHAGUA
VIONGOZI WA KUUNDA KAMATI YA UKOO
|
Ndugu Wote
|
11:00
|
Kufunga
Mkutano
|
Mgeni Rasmi
|
XIII:
KAMATI ILIYORATIBU SHUGHULI KATIKA MKUTANO MKUU WA
KWANZA WA UKOO WA KIVENULE
A: Wawezeshaji
Wa Mada Mbalimbali
1. Christian J. Kivenule
2. Augustino Kivenule
3. Stephan Mhapa
4. Maria Milimo
5. Adam A. Kivenule
6. Jovin D. Kivenule
7. George S. Kivenule
8. John S. Kivenule
9. Ignas P. Kivenule
B: Wawezeshaji
Wasaidizi
1. Lesandu Mhapa
2. Adam A. Kivenule
3. Faustin S. Kivenule
4. Christian J. Kivenule
5. Donath Mhapa
C: Msimamizi wa Vyombo vya Matangazo
1. Lesandu Mhapa
2. Justo Chavala
D: Muda
wa Kuwasilisha Mada
·
Muda
wa dakika 45 ulitumika kuwasilisha Mada moja.
·
Majadiliano
katika Makundi yalifanyika kwa dakika kumi; na
·
Uwasilishaji
wa hoja kutoka katika makundi ulitumia dakika tano hadi nane.
Kuwasilisha
Mada[dak.45]; Majadiliano [dak. 10]; Kuwasilisha na Majumuisho [dak.10]
E: Uteuzi
wa Makundi ya Majadiliano
[Namna
gani makundi yalivyokuwa yanaundwa]
Makundi Manne ya Majadiliano yaliundwa
kwa kila Mada iliyowasilishwa kwenye Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa
Kivenule. Uundwaji wa Makundi ya Majadiliano ulifanyika kwa kila mshiriki
kuhesabu namba, yaani moja mpaka nne na kisha kila mshiriki kukariri namba
yake. Baadaye washiriki wote waliohesabu namba moja walikaa kwenye kundi la
kwanza, namba mbili kundi la pili, namba tatu kundi la tatu na kisha namba nne kundi
nne.
Kila mada iliyowasilishwa kwenye Mkutano
Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ilikuwa na dondoo nne. Hivyo makundi
yaligawanywa kutokana na idadi ya hizo dondoo nne.
XIV:
TATHMINI YA MKUTANO MKUU WA KWANZA WA UKOO WA KIVENULE
Wanaukoo walizishukuru na kuzipongeza
Kamati zote za maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule kwa
kufanya kazi nzuri. Walibainisha furaha yao kwa kusema haya yafuatayo:
1. Tunawashukuru Wawezeshaji kwa kujiandaa
barabara na pia Waratibu wa shughuli hii wameiratibu vizuri sana.
- Mpangilio wa Ratiba ulikuwa ni mzuri sana.
- Washiriki wamefanikiwa kuchangia vema kutokana na mpangilio mzuri wa Mada na Wawezeshaji.
2. Mwitikio wa wanandugu
na wanaukoo umetia moyo sana na hivyo kupiga hatua mbele katika Mikutano
mingine ijayo.
3. Shukrani ziwaendelee
wale wote waliochangia gharama za kuweza kufanikisha Mkutano huu. Tunawashukuru
pia wale ambao hawakuchangia gharama lakini kuja kwao kwenye kikao kumetia
hamasa kubwa.
4. Tunawashukuru wale
wote waliotusaidia kuandaa chakula (katika mapishi)…. Na Kamati za maandalizi wa ujumla.
5. Tunaushukuru uongozi wa kijiji cha
Kidamali kwa kuuthamini mkutano wetu; tumeshuhudia Mwenyekiti tukiwa naye siku
zote mbili za Mkutano huu.
6. Tunamshukuru mwenye nyumba (Bwana Sanga)
kwa kutukodisha ukumbi kwani umetusaidia sana.
XV:
MAPENDEKEZO/MAONI YALIYOJITOKEZA WAKATI WA MKUTANO
MKUU WA UKOO
1. Iundwe Kamati Kuu ya Ukoo, Kamati Ndogo
na Uongozi wa Ukoo na pia wachaguliwe Wawakilishi kulingana na maeneo husika
mfano Magubike, Kidamali, Nyamahana, Nzihi na kadhalika. Wawakilishi
watakaochaguliwa watakuwa wanafanya mawasiliano na Uongozi wa toka sehemu zao
husika. Watatoa taarifa za matatizo au furaha, watatekeleza maagizo toka kwa
Viongozi wa Ukoo na Kamati Kuu ya Ukoo. Lakuzingatia:
Wanaukoo wawachague wanaukoo wenye mwelekeo na moyo wa kujituma na kujitolea na
wenye uchungu na maendeleo ya ukoo.
2. Iundwe Kamati ya Ukoo (Yenye Uwakilishi
wa Wajumbe) toka sehemu mbalimbali itakayoratibu shughuli kadhaa za ukoo mfano
Uanzishwaji wa Mfuko wa kuchangia kutatua matatizo ya wanandugu kama vile
ugonjwa, elimu na vifo. Pia inapendekezwa kuwa wanaukoo wanaoishi vijijini
wachangie shilingi 500/= kila mwezi; lakini kila mwanaukoo awe huru kuchangia
zaidi. Watumishi na walio mjini wenye vipato wachangie shilingi 1000/= kila
mwezi.
3. Wanaukoo wanashauriwa wawe na imani kwa
mwanaukoo yeyote atakayepewa jukumu la usimamizi wa fedha. Suala la ufunguzi wa
Akaunti ni muhimu likazingatiwa.
4. Iundwe Kamati ya Usuluhishi ya Ukoo
itakayotatua matatizo ya Wanaukoo wote, na iundwe na watu kutoka maeneo
mbalimbali wanakoishi. Kazi yake kubwa itakuwa ni kupokea taarifa za matatizo
na kuyatafutia ufumbuzi.
5. Michango ianze kuchangwa mara moja na
iachwe ikae angalau mwaka mmoja kabla hajaanza kutumika kuwasaidia wale wenye
matatizo ya ugonjwa, kufiwa na pia kupangwe viwango mahsusi vya kuwasaidia hao
wenye matatizo.
6. Mfuko utakaoanzishwa kwa ajili ya
kusaidia kwa upande wa Elimu, uegemee zaidi kuwasaidia wale wasio na uwezo.
Wenye uwezo watumie gharama zao kuwasomesha watoto au jamaa. Lakini katika
ugonjwa au misiba basi ndugu wa hali
zote wanufaike.
7. Achaguliwe mwakilishi wa wanaukoo
kutokana maeneo mbalimbali wanakoishi ili awe anafanya mawasiliano kwa
wanandugu kuhusiana na matatizo au furaha katika maisha yao ya kila siku.
8. Je wanaukoo mnadhani ni hatua gani
zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya wanandugu/wanaukoo ambao hawaridhii kuuchangia
mfuko huu? Katiba ikitungwa itakuwa na kipengele cha kuwabana wale ambao
hawatoi michango yao. Mweka Hazina atakuwa na kipengele cha kumbana kuhusiana
na utunzaji wa fedha za michango mbalimbali.
XVI:
UCHAGUZI WA VIONGOZI WA UKOO
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoowa
Kivenule ulifanya uchaguzi wa viongozi wa ukoo katika ngazi zifuatazo kama
inavyobainishwa hapa chini:
1.
Viongozi wa Ukoo
- Faustin S. Kivenule Mwenyekiti
- Donath Mhapa Makamu Mwenyekiti
- Christian J. Kivenule Katibu
- Severin Nyangalima Katibu Msaidizi
- Justin D. Kivenule Mweka Hazina
- Carolina S. Kivenule Mweka Hazina Msaidizi
2. Washauri wa Uongozi wa Ukoo
- John S. Kivenule Morogoro
- Stephan Mhapa Kidamali
- Edgar S. Kivenule Dar eS Salaam
- Pius Kivenule Ilole
3.
Wajumbe wa Kamati Kuu ya Ukoo ambao pia
ni Wawakilishi wa
Kamati toka sehemu mbalimbali hapa
Tanzania
- Adam A. Kivenule Dar es Salaam
- Ignas P. Kivenule Dar es Salaam
- Jovin D. Kivenule Kidamali
- Justin D. Kivenule Kidamali
- Faustin S. Kivenule Kidamali
- Donati Mhapa Kidamali
- Carolina S. Kivenule Kidamali
- Zavary S. Kivenule Mufindi
- Florian A. Kivenule Mafinga
- Augustino Kivenule Nduli
- Martin Kivenule Nduli
- Vitus Nzala Magubike
- Romanus Kivenule Ibogo
- Severin Nyangalima Ilalasimba
- Marco Kivenule Ilalasimba
- Fabian Kivenule Nyamihuu
- Christopher Kivenule Ilole
- Titus Kivenule Igominyi
- Alexander Nyangalima Morogoro (Mikumi)
- Christian Kivenule Morogoro Mjini
XVII: SHUKRANI
Ndugu Ignas Kivenule ambaye ni Mjumbe wa
Kamati Kuu ya Ukoo wa Kivenule, aliwashukuru wanaukoo wote waliotoa ushirikiano
na kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, kwa kuwa wameonyesha
umoja wa hali ya juu sana. Binafsi yeye anaamini jamii inayounda Ukoo wa
Kivenule ni wapole na wasio na majivuno. Ila angefurahi sana kama jamii
inayounda ukoo huu itajitokeza kwa wingi zaidi katika Mkutano Mkuu wa Pili wa
Ukoo wa Kivenule, utakaofanyika mwakani 2006.
Ukoo wa Kivenule una zaidi ya ndugu 2000
kutoka pande zote za Kidamali, Ilole, Nduli, Magubike na kwingineko. Ni wajibu
wa kila mwanaukoo kuhamasisha watu wengine wajitokeze kuhudhuria Mkutano Mkuu
ujao. Sambamba na hilo, pia aliiomba jamii ya Ukoo wa Kivenule ikalipa umuhimu
suala la kusomesha watoto ili kupunguza utegemezi na pia kuwaandalia hali bora
za maisha hapo baadaye.
Alisikitika kwa wanaukoo toka Ilole
kutohudhuria Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, ila angefurahi sana
kama jamii hiyo ya Ilole ingeshiriki mkutano huo. Kuna sababu nyingi
zimetolewa, likiwemo suala la Nauli. Lakini, kama kila mwanaukoo atakuwa
anajali ni jambo la msingi sana wangejiandaa kikamilifu kuhudhuria Mkutano
ujao.
Wanaukoo wengi wa kutoka Dar es Salaam
wamekuwa ni wazito na hii pia inakatisha tamaa. Kama ni matatizo ni vyema jamii
yote ikashirikiana. Mojawapo ya mambo mazuri na ya msingi ya kufanya Mkutano
Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ni kuiwezesha jamii inayounda ukoo huu, kuwa
na uwezo wa kukabiliana na matatizo ya kila siku. Mwishoni aliwashukuru
wanaukoo wote wa Kidamali kwa moyo wa ukarimu waliouonyesha
XVIII:
KUFUNGA MKUTANO
Mgeni Rasmi Daima Luvanda (Mwenyekiti ya
Serikali ya Kijiji cha Kidamali) alifunga rasmi Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo
wa Kivenule mnamo saa 3.30 usiku kwa kuzishukuru Kamati za Maandalizi ya
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo kwa kufanikisha kufanyika kwa mkutano huo.
Pia, aliwashukuru viongozi wapya
waliochaguliwa kuuongoza Ukoo wa Kivenule na kuahidi kuwa atawapa ushirikiano
wa hali na mali kuhakikisha kuwa wanafanikiwa katika utendaji wao wa kazi.
Mgeni Rasmi kwa mara nyingine alitoa shukrani zake kwa viongozi, Umoja wa Ukoo
wa Kivenule kwa ujumla kwa kumteua kuwa Mgeni Rasmi.
Kwake binafsi ilisema ilikuwa ni fursa
tosha kujifunza mambo mbalimbali ambayo alikuwa hayajui, na pia kupata somo la
kuweza kulifanyia kazi au kuionyesha jamii yake umuhimu wa kuwa na mkutano wa
pamoja kama ulivyofanyika huu wa Ukoo wa Kivenule.
XIX:
MATUKIO KATIKA PICHA SIKU YA MKUTANO MKUU WA UKOO