MKUTANO MKUU WA 10 WA KAUKI

MKUTANO MKUU WA 10 WA KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

KAUKI-Kidamali, Iringa

KAUKI-Kidamali, Iringa
Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Thursday, March 28, 2013

RIPOTI YA MKUTANO MKUU WA KWANZA WA UKOO WA KIVENULE - 2005















RIPOTI
 YA
 MKUTANO MKUU WA KWANZA WA
UMOJA WA UKOO WA KIVENULE



 17 – 18 DESEMBA 2005
KIDAMALI - IRINGA


Imeandaliwa na:
Adam Alphonce Kivenule
Katibu Mkuu-KAUKI
Kidamali, Iringa Vijijini
E-mail: tagumtwa@gmail.com
                 kauki2006@gmail.com
Tovuti: www.kauki-kauki.blogspot.com



I:    UTANGULIZI
Harakati endelevu za kuleta mabadiliko na maendeleo zinakua kwa kasi kubwa na hivyo kuchochea mabadiliko ya haraka ya hali bora za maisha ulimwenguni kote. Harakati kama hizo zinazotegemea sana uwepo wa Sayansi na Teknolojia, Elimu na Uchumi endelevu; zinatoa fursa na hamasa kwa jamii huria nazo kubuni na kutafuta mbinu mbadala za kuweza kujiinua ili kuweza kukabiliana na hali hiyo. Mabadiliko hayo yanayozungumziwa ni pamoja na kukua kwa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kupitia Kopyuta yaani Internet na simu za mkononi (computer, Internet and cellphones), Soko Huria, Utandawazi na Ubinafsishaji.

Jamii huria kwa upande wake zinapata hamasa na changamoto ya kuweza kutafuta mustakabali wake kutokana na hali halisi ya maendeleo inavyoendelea kukua kwa kasi na athari zake kuonekana moja kwa moja katika maisha yetu ya kila siku kwa upande mmoja; na pia mafanikio kuonekana kwa upande mwingine.
Wimbi la umaskini uliokithiri, janga la UKIMWI, ujinga na rushwa vimekuwa ni vikwazo vikubwa vya maendeleo na ambavyo vinazidi kudidimiza harakati mbalimbali za kuweza kujiinua na kujikwamua katika hali hiyo. Harakati hizi za kutafuta maendeleo zimegawanyika katika makundi mbalimbali ya kijamii hususani makundi ya wasomi, wafanyabiashara, wanawake na wananchi wa kawaida.

Kutokana na harakati hizo, wanajamii wanaounda Ukoo wa Kivenule nao hawako nyuma katika kuhakikisha kuwa jamii yao inaondokana na umaskini, ujinga pamoja na UKIMWI; na hivyo kupata fursa ya kuishi katika Dunia Mbadala [Alternative World] iliyojisheheneza katika sayansi na teknolojia.

Kwa kutambua hilo, wanajamii na ndugu wanaounda UKOO wa KIVENULE, kwa pamoja toka mwezi Februari 06, 2005, walianzisha harakati za kuinasua jamii yao kutoka kwenye lindi la umaskini, ujinga na maradhi kwa kuunda Kamati ya kuuza na kuratibu Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa KIVENULE; ambao ulipangwa kufanyika katika Kijiji cha Kidamali, Wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa, hapo tarehe 17 hadi 18 Desemba 2005. Katika mapendekezo ya awali, Uongozi uliochaguliwa kuunda kamati ya maandalizi na uhamasishaji, ilipanga kuwepo na Kamati Tatu za Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, yaani Kamati iliyopo mkoani Dar es Salaam, Kamati ya Kijijini Kidamali na ya Ilole – Iringa, zote zikiwa zimepewa majukumu mazito ya kusaidia kufanikisha mkutano huo.

Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Kivenule awali ulitegemea kuwaalika ndugu na wageni wapatao mia mbili (200) toka Kijijini Kidamali, Ilole, Nduli, Kihesa, Ilula, Magubike, Kinyamlewa, Nzihi, Iringa Mjini, Kalenga, Ipogolo, Museke, Kitwilu, Igowolo, Kiponzelo, Mafinga, Mufindi, Maduma, Wasa, Ifunda, Tosamaganga, Kilombero, Morogoro, Dodoma na Dar es Salaam; na sehemu nyingine nyingi ambako wanajamii wanaounda ukoo huo wanaishi ili waweze kupata fursa ya kushiriki kikamilifu.

Ukoo wa Kivenule ukiwa umejiwekea malengo mahususi katika kuandaa mkutano huo, pia uliazimia pamoja na mambo mengine, kufundisha jamii inayounda ukoo huo, Mada Tano zenye msukumo wa kimaendeleo. Mada zilizopendekezwa kufundishwa katika siku mbili za mkutano huo zilikuwa ni pamoja na:
1.         HISTORIA NA CHIMBUKO LA UKOO
          Ukoo ni Nini na Unapatikanaje?
          Dhana ya Kuenea na Kukua kwa Ukoo.
          Mgawanyiko wa Ukoo (Chora Mchoro Kuonyesha Ukoo unavyoundwa).
          Kupotea kwa Ukoo.
2.        MAHUSIANO BAINA YA NDUGU NDANI YA UKOO
          Ukaribu wa Wana Ndugu.
          Ushirikiano Katika Nyanja Mbalimbali.
          Kutembeleana kama Sehemu ya Kudumisha Mahusiano.
          Kuondoa Tofauti na Kusaidiana.

3.   ELIMU NA MUSTAKABALI WA UKOO
          Nafasi ya Ukoo wa Kivenule katika Elimu.
          Umuhimu wa Elimu.
          Dunia ya Utandawazi.
          Nini Kifanyike Kuinua Elimu Katika Ukoo Wetu.

4.   UKIMWI NDANI YA UKOO NA ATHARI ZAKE
          UKIMWI ni nini?
          Namna gani UKIMWI unavyoenea/kuambukizwa?
          Njia Mbadala za Kujilinda na Maambukizi?
          Jukumu la Ukoo/Familia Kukabiliana na Janga la UKIMWI.

5. DINI KATIKA UKOO
          Maana ya Dini
          Umuhimu wa Kuwa na Imani
          Maadili na Dini
          Ukoo Uliojengeka katika Misingi ya Dini

Wawezeshaji mbalimbali wenye ujuzi katika mada hizo walipatikana baada ya kamati kuchukua jukumu la kuwatafuta ikiwamo kupata Mtaalam wa UKIMWI toka TAHEA.

Mojawapo ya hamasa kubwa ya kuandaa mkutano huu ilikuwa ni pamoja na suala nzima la mahusiano ndani ya wanandugu, wanaukoo na jamii kwa ujumla. Suala la ELIMU, ATHARI ZA UKIMWI katika jamii ya ukoo wa Kivenule na taifa nzima. Pia haja ya kufahamiana baina ya wanajamii na ndugu wanaounda ukoo, pamoja na kuujua Ukoo kwa ujumla.

Pamoja na mambo mengine, kamati ilifikiria pia uwezekano wa kufanya senza ili kujua idadi ya ndugu wanaounda ukoo husika toka kona mbalimbali hapa Tanzania; kujua nini wanakifanya na kujua idadi sahihi ya wanandugu ambao wanahitaji msaada wa namna moja au nyingine.
Katika suala nzima la Kufahamu Historian na Chimbuko la Ukoo, Mahusiano baina ya wanandugu ndani ya ukoo, Elimu, Maadili na Dini na gonjwa hatari la UKIMWI, Kamati ilionelea kuwa ni mojawapo ya mambo msingi sana kuyaangalia katika shughuli nzima ya maandalizi na wakati wa Mkutano Mkuu.

Changamoto zitakazopatikana baada ya kuyagusia mambo haya ya msingi na hivyo kuwawezesha washiriki wa mkutano mkuu kujenga ajenda mpya.

Mahusiano duni baina ya wana ndugu, kukosekana kwa ushirikiano katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo, hali duni ya kiuchumi na kijamii, matatizo ya kifamilia na kiukoo ni kati ya masuala ya msingi yaliyofikiriwa sana kabla ya kuanza kufanya maandalizi ya Mkutano Mkuu.

Mwelekeo na nafasi ya ukoo wa Kivenule katika suala nzima la Elimu hasa katika dunia hii ya Utandawazi (Globalization). Maendeleo ya sayansi na teknolojia ambapo yameifanya dunia kuwa kama kijiji kisicho na mipaka na kila mtu anaruhusiwa kuingia na kutoka; kuongezeka kwa viwanda vinavyotumia teknolojia ya hali ya juu; kuongezeka kwa teknolojia ya habari na mawasiliano (Internet); kupanuka na kujengeka kwa miji, pamoja na soko huria.

Mambo yote haya ndiyo yanayoweza kuonyesha mustakabali na nafasi ya ukoo wa Kivenule kwa maisha ya baadaye. Ilionekana kuwa ukoo wetu upo nyuma sana katika suala nzima la elimu, hii linajidhihirisha kutokana na kuwa na ndugu wachache sana ambao wameweza kupata elimu kwa kiwango kinachostahili.

Hii ni hatari kwa sababu tunajenga ukoo tegemezi ambayo baadaye utakosa mwelekeo. Mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia yanayojitokeza kila kukicha yanaibadili dunia na hivyo kutulazimisha nasi katika ukoo wa Kivenule kubadilika. Matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano katika simu za mikononi, Internet, kompyuta, redio na satelaiti ni changamoto kubwa katika Ukoo wa Kivenule.

Maambukizo ya ugonjwa wa UKIMWI ambayo kwa kiasi kikubwa yameathiri familia nyingi zikiwemo familia zetu sisi wana ukoo, yanapaswa kutopuuzwa bali kuwekewa mikakati madhubuti. Ufahamu kuhusiana na gonjwa lenyewe livyoenea na madhara yake katika jamii, njia mbadala za kujilinda na maambukizi ya ugonjwa wenyewe pamoja na kuitikia mialiko mbalimbali ya wanajamii wanaopambana na janga hili ni mambo ya msingi sana ambayo yalijadiliwa kwa kina kwenye mkutano huo.

Ilipendekezwa kuwa, wakati wa mkutano huo kutakuwa na nafasi kutoa uzoefu katika mambo mbalimbali ya kitaalum na maendeleo. Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Ukoo yalianza mapema ili kumpa fursa kila mwanajamii/mwanaukoo kutafakari na kujadili kwa kina, kujiandaa pamoja na kuwasilisha mchango wake wa mawazo kwa kamati husika za kuratibu maandalizi.

Mkutano Mkuu wa Ukoo umeazimia kutoka na kitu muhimu ambacho ndicho kitakuwa mwongozo na dira ya shughuli mbalimbali zitakazokuwa zinafanyika katika ukoo.

Licha ya kuwa na malengo na makusudio mbalimbali, pia tunategemea mwisho wa mkutano kutakuwa na mambo kadhaa ambayo yatakuwa ni makubaliano kutoka pande mbalimbali za ukoo wa Kivenule. Yote hayo kwa pamoja yatakuwa ni maazimio ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule.

Kati ya Maazimio ambayo Kamati iliyategemea kuyatekeleza katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ni pamoja na:
1.        Kufanyika kwa Senza ya Ukoo wa Kivenule ili kupata idadi kamili ya ndugu.
2.      Kuanzisha Mfuko wa Ukoo ambao utasaidia katika kusomesha watoto wanaofaulu pamoja na kusaidia katika matatizo mbalimbali yanayojitokeza au uhitaji wa msaada.
3.      Kuchagua Viongozi wa Ukoo pamoja na Wajumbe Wawakilishi watakaounda Kamati ya Ukoo ya Kuratibu mambo mbalimbali ya ukoo. Nafasi za Viongozi watakaochaguliwa zitajumuisha Mwenyekiti, Makamu wa Mwenyekiti, Katibu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina na Msaidizi wake pamoja na Walezi Watatu wa kushauri uongozi uliopo madarakani.
4.      Kuzitaja/kutamka bayana kazi/majukumu mbalimbali ambayo Uongozi utakaoundwa utakuwa unazifanya mfano kufanya mashauriano na usuluhishi wa matatizo mbalimbali ya ukoo yaliyojitokeza. Lakini pia jukumu lao kubwa ni kuongoza na kusimamia majukumu mbalimbali yanayojitokeza au kuhitaji usimamizi ndani ya ukoo.
5.      Kukusanya taarifa mbalimbali za ukoo; na
6.      Kuangalia na Kutathmini usalama wa mali mbalimbali zinazomilikiwa na ukoo nk.

II: UUNDAJI WA KAMATI ZA MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA
     KWANZA WA UKOO
Kamati mbili za kuratibu Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ziliundwa. Kamati ya Kwanza ilikuwa ni Kamati ya Dar eS Salaam ambayo uliundwa mwezi Februari 06, 2005 na Kamati ya Pili kuundwa ni ile ya Kidamali ambayo iliundwa mwezi Mei 2005. Uundaji wa Kamati ya Dar es Salaam na ile ya Kidamali uliendana na uchaguzi wa viongozi wa kuziendesha na kuzisima-mia kamati hizo. Kwa upande wa wanaukoo na ndugu wanaoishi Dar es Salaam na mikoa ya karibu kama Morogoro, Dodoma na Mikumi waliingia kwenye Kamati ya Dar es Salaam.

Kamati ya Kidamali iliwaunganisha wanaukoo na ndugu wote wanaoishi maeneo ambayo yapo karibu na Kidamali mfano Magubike, Nzihi, Kalenga, Nyamihuu, Idete na kwingineko.

Kwa upande wa Kamati ya Dar es Salaam, viongozi walikuwa kama ifuatavyo:-
1.        Christian             Kivenule                    Mwenyekiti
2.      Adam                   Kivenule                    Katibu
3.      Athuman             Mtono                                    Makamu Mwenyekiti
4.      Edgar                   Kivenule                    Mshauri wa Kamati
5.      Innocent             Kivenule                    Mweka Hazina        
6.      Ignas                     Kivenule                    Mshauri Kamati ya Ilole

Na kwa upande wa Kamati ya Kidamali, viongozi waliochaguliwa walikuwa kama ifuatavyo:-
1.        Faustin                 Kivenule                    Mwenyekiti  
2.      Augen                  Kivenule                    Makamu Mwenyekiti         
3.      Jovin                     Kivenule                    Katibu
4.      Carolina               Kivenule                    Katibu Msaidizi
5.      Justin                    Kivenule                    Mweka Hazina
6.      Donati                 Mhapa                       Mshauri
7.      Pyela                    Kivenule                    Mshauri
8.      Daniel                  Kivenule                    Mshauri         

Kamati zote mbili zilikuwa na washauri, ambao nao pia walichaguliwa siku hiyo hiyo ya kuwachagua viongozi. Kazi ya washauri ilikuwa ni kuzishauri Kamati zote mbili katika kutekeleza majukumu yake.


A:     KUHAMASISHA/UHAMASISHAJI
Mwezi Mei 2005, viongozi wanaounda Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule toka Dar es Salaam, walisafiri kwenda Kidamali – Iringa wakiwa na lengo mahsusi la Kuhamasisha wanaukoo wanaoishi Kidamali na maeneo ya Karibu kuhusiana na Maandalizi ya Mkutano wa Ukoo.
Tendo la Uhamasishaji lilienda sambamba na kuundwa kwa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule kwa Upande wa Kidamali. Jukumu la Kamati hiyo iliyoundwa ilikuwa ni:
Kuhamasisha wanaukoo toka maeneo mbalimbali yanayozunguka Kidamali kujitokeza kwa wingi siku ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule;
Kutoa michango ili kufanikisha maandalizi ya Mkutano Mkuu; na
Kusambaza kadi za michango kwa wanandugu na wadau mbalimbali ambao wanaweza kusaidia kuchangia maandalizi ya Mkutano Mkuu.

B:      UCHANGAJI WA MICHANGO
Kamati zote mbili ya Kidamali na Dar es Salaam zilitekeleza ipasavyo jukumu la uchangiaji wa michango. Kwa upande wa Kamati ya Dar es Salaam, zoezi la uchangiaji michango halikuwa na mafanikio sana ukilinganisha na mafanikio yaliyojitokeza upande wa Kidamali.

Ukusanyaji wa michango ulifanyika kwa kusambaza kadi za kuomba mchango wa kufanikisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Viwango wa vichango vilitofautiana kwa wale wanaoishi mijini na pia kwa wale wanaoishi vijijini.

Kwa wanandugu wanaoishi mijini waliombwa wachangie shilingi Elfu Kumi na Tano tu (15,000/=); na kwa wenzetu wanaoishi maeneo ya vijijini waliombwa wachangie shilingi Elfu Tano tu (5,000) au kitu chochote chenye thamani ya fedha hiyo mfano kutoa kuku au mazao (mahindi au maharage).
C:      MWITIKIO KATIKA UCHANGAJI MICHANGO
Wanaukoo wanaoishi Kidamali na maeneo ya karibu walionyesha mwitikio wa hali juu sana kwa kutoa michango yao kwa moyo. Karibu robo tatu ya michango iliyofanikisha Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ilitoka Kidamali na maeneo yake ya Karibu. Jamii kuna sehemu kadhaa zilionyesha kusita katika kutoa michango yao katika kipindi cha awali, ilibadili msimamo wake katika dakika za mwisho.

Kamati iliamini kuwa kutokuwa na hamasa wakati wa awali pengine ilitokana na kutoelewa dhumuni la michango hiyo. Mara baada ya kubandika matangazo ya kuutangaza Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, wanaukoo wengi toka maeneo mbalimbali walijitokeza kutoa michango yao.

Wanaukoo wanaoishi Dar es Salaam hawakufanya vizuri katika kutoa michango. Ni ndugu wachache tu ndio waliojitokeza kutoa michango yao. Wengi wa wanandugu/wanaukoo walitoa sababu mbalimbali za matatizo mfano kutokuwa na ajira na pia kutomudu kutoa kiasi hicho cha pesa. Tatizo la utoaji wa michango lilienda sambamba na mahudhurio duni kwenye vikao vilivyoitishwa. Hadi dakika za mwisho za maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, ni wanaukoo chini ya kumi ndiyo waliokuwa wametoa michango yao.

III:   TATHMINI YA MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA KWANZA WA
        UKOO KIVENULE
Kamati zote mbili za maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ile ya Kidamali nay a Dar es Salaam, zilikaa pamoja ili kuweza kufanya tathmini ya shughuli nzima ya maandalizi ya Mkutano Mkuu yaliyofanyika kati ya mwezi Februari na Novemba 2005.

Lengo la kuzikutanisha Kamati zote mbili ilikuwa ni kufanya tathmini ya hatua za maandalizi zilizofikiwa kwa ajili ya kufanikisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Ilionekana dhahiri kuwa Kamati ya Maandalizi ya Kidamali ilifanya vizuri zaidi, huku Kamati ya Maandalizi toka Dar es Salaam – ikionyesha kuelemewa kutokana na mwitikio duni wa wanaukoo waishio eneo hilo la mjini.
Kamati zote mbili za Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ya Kidamali na Dar es Salaam, zilifanikiwa kukusanya jumla ya shilingi 345,350.00 mpaka siku ya mwisho ilipofanyika tathmini ya ukusanyaji wa michango wa Kamati zote mbili.
Kamati ya Dar es Salaam ilijitahidi kufanya maandalizi ya moja kwa moja katika harakati za Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Maandalizi hayo yalihusisha uandalizi wa Kadi za Michango (Kadi za Kawaida na Kadi Maalum). Kadi za kawaida ziligawanyika katika makundi mawili, yaani kadi za Shilingi Elfu Kumi na Tano (15,000/=) na kadi za Shilingi Elfu Tano (5,000/=). Kadi Maalum zilikuwa mahsusi kwa watu au taasisi maalum zilizoombwa kuuchangia Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule.
Jukumu jingine lilifanyika na Kamati ya Dar es Salaam ilikuwa ni uandaaji na uchapaji wa minitisi za vikao mbalimbali na kuzisambaza, uandaaji wa Mabango ya kuutangaza Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule kwa ajili ya kubandikwa maeneo mbalimbali.
Pia Kamati ya Dar es Salaam iliandaa vitambulisho kwa ajili ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Lengo ilikuwa ni kuhakikisha kuwa kila mshiriki anakuwa na kitambulisho wakati Mkutano ukiendelea.


IV: UUNDAJI WA KAMATI ZA KURATIBU MKUTANO
Kamati mbalimbali ziliundwa ili kuweza kufanikisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Kamati kadhaa ziliundwa ili kuratibu shughuli na majukumu mbalimbali wakati Mkutano ukiendelea. Kamati hizo zilizoundwa ni pamoja na:
1.        Kamati ya Chakula
2.      Kamati ya Ulinzi
3.      Kamati ya Vinywaji
4.      Kamati ya Mapokezi
5.      Kamati ya Burudani

Kila Kamati ilikuwa na msimamizi wake ili kuhakikisha kuwa kila jambo linafanyika kama ilivyopangwa katika Ratiba. Kwa kiwango kikubwa, kila Kamati iliyopewa jukumu la kutekeleza wakati wa Mkutano Mkuu ilifanya vizuri na kwa ufanisi wa hali ya juu. Kamati zilizoundwa zilishirikisha wanaukoo, majirani na marafiki na hivyo kutoa hamasa kubwa katika kutekeleza majukumu. Majirani na marafiki waliwaomba wanandugu/wanaukoo toka Ukoo wa Kivenule kuwa mstari wa mbele katika kutekeleza majukumu yao ili wawe chacho kwa wengine wasio wanaukoo.

V: UTEUZI WA WAWEZESHAJI WA MADA
Wawezeshaji mbalimbali waliteuliwa na Kamati zote mbili, yaani Kamati ya Dar es Salaam na ile ya Kidamali kuwa Wawezeshaji wa Mada Tano zilizopendekezwa kuwasilishwa kwenye Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Baadhi ya Wawezeshaji hao pamoja na Mada walizopewa kuwasilisha ni:
1.         CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOOO
§        Christian              J.          Kivenule
§        Augustino                       Kivenule
§        Daniel                  S.         Kivenule
2.        MAHUSIANO YA NDUGU NDANI YA UKOO
§        Stephan                          Mhapa
§        Ignas                    P.        Kivenule
§        John                     S.         Kivenule
3.        ELIMU NA MUSTAKABALI WA UKOO WA KIVENULE
§        Christian              J.          Kivenule
§        Donath                           Mhapa

4.        UKIMWI NA ATHARI ZAKE NDANI YA UKOO
§        Maria                               Milimo
§        Adam                  A.        Kivenule
5.        DINI KATIKA UKOO
§        Jovin                    D.        Kivenule
§        George                S.         Kivenule
§        Stephan                          Mhapa



VI: MIALIKO KWA WANANDUGU, WANAUKOO PAMOJA NA WASHIRIKI WENGINE
Mialiko ya wanandugu pamoja na wanaukoo kwa ujumla, kuhudhuria MKutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ilifanyika wazi kwa kila mtu bila upendeleo, kila mwanaukoo alipewa taarifa za kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Ukoo na kuombwa kuhudhuria. Aidha kamati zote mbili za maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, zilikubaliana kwamba, kila mwanandugu au mwanaukoo anapaswa kuhudhuria mkutano huo bila kukosa.

Mialiko ilifanyika kwa namna mbalimbali ikiwemo ile ya mdomo. Yaani kumwalika mwanaukoo au ndugu moja kwa moja kwa kumpa maelekezo kuhusiana na mahali unapofanyika mkutano mkuu, tarehe pamoja na muda. Familia yote, yaani baba, mama na watoto, wote walipaswa kuhudhurio mkutano mkuu huo.

Pia mialiko ilifanyika kwa kubandika matangazo ya kuutangaza Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule sehemu mbalimbali Kijijini Kidamali pamoja na maeneo mengine ambako Kamati ziliamini ndugu na wanaukoo wanaishi kule.
Kila ndugu aliyefika na kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, alipewa kitambulisho cha kuweza kumtambulisha kwa ndugu wengine. Kitambulisho hicho kilionyesha namba ya kitambulisho, jina la ndugu, mahali anapoishi na simu au sanduku la posta. Kamati ziliepuka ile hali ya kuulizana maswali ya kuwa wewe unaitwa nani, unaishi wapi na simu yako iko wapi? Hii ilikuwa ni sababu ya msingi ya kutoa kitambulisho kwa kila mwanaukoo au ndugu.

VII: UBANDIKAJI WA MATANGAZO
Ubandikaji wa matangazo ya kuutangaza Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ulifanyika sehemu mbalimbali Kijijini Kidamali pamoja na maeneo mengine ambako Kamati ziliamini ndugu na wanaukoo wanaishi kule, ulifanyika kwa lengo la kuwajulisha ndugu kuhusu uwepo wa Mkutano Mkuu na wapi unafanyika.

Baadhi ya sehemu kulikobandikwa matangazo ni pamoja na Kidamali, Magubike, Nzihi, Nyamihuu, Ipogolo na Nyamihono. Ubandikaji wa matangazo ya Mkutano Mkuu wa Ukoo, uliibua hisia ya kushawishika kuhudhuria kwa wanaukoo na wasio wanaukoo kuhusiana na kufanyika kwa Mkutano huo. Wapo majirani, marafiki na watu wasio wanaukoo waliokuwa na shauku kubwa ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule.

VIII:  SIKU YA KWANZA YA MKUTANO MKUU WA KWANZA WA UKOO WA
          KIVENULE, DESEMBA 17, 2006
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ulifunguliwa na Mgeni Rasmi Ndugu Daima Luvanda, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kidamali.

Awali kabla ya yote, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Mkuu wa Ukoo Ndugu Faustino Kivenule, aliwakaribisha ndugu, jamaa na wanaukoo kwa ujumla kwenye mkutano huo.

Kabla ya kusoma hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Ukoo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo, alimkaribisha Ndugu George Kivenule, kuuombea Mkutano Mkuu kwa sala.

Baada ya Sala ya kuuombea Mkutano Mkuu, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Ukoo, alitumia fursa hiyo kuisoma Hotuba ya Ufunguzi.

Alianza kwa kuwajulisha ndugu, wanaukoo na wageni waalikuwa kuwa, lengo la Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ni kuwaunganisha wanaukoo wote, wanaoishi sehemu mbalimbali hapa Tanzania, ili wafahamiane, waelimishane na kupeana ujuzi katika nyanja mbalimbali za maendeleo na kupeana uzoefu.

Pia, lengo jingine la Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ilikuwa ni kutolewa na kufundishwa kwa Mada kadhaa zenye nia ya kuujengea ukoo na kuwa na msimamo imara. Kwa kuwakusanya ndugu pamoja, Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu, iliamini itasaidia kuujenga Ukoo katika misingi ya Ushirikiano na Upendo na hiyvo kuwa na ukoo wenye umoja.
Lengo jingine la kufanya mkutano mkuu wa ukoo ilikuwa ni kufanya senza ili kujua idadi ya wanaukoo na mwishoni kufanya uchaguzi wa viongozi, watakaunda Uongozi wa Ukoo na pia watashirikiana na Kamati ya Ukoo wa Kivenule katika kutekeleza majukumu mbalimbali.
Kamati itakayoundwa itakuwa na jukumu la kuratibu mambo mbalimbali na matatizo yanayohusu ukoo.

Jumla ya Mada Tano ziliwasilishwa na kufundishwa katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Mada zilizowasilishwa ni pamoja na:
1.          CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO;
2.         MAHUSIANO BAINA YA NDUGU NDANI YA UKOO;
3.         ELIMU NA MUSTKABALI KATIKA UKOO;
4.         UKIMWI NDANI YA UKOO NA ATHARI ZAKE; NA
5.         DINI KATIKA UKOO.

Harakati za maandalizi ya Mkutano Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, zilianza toka mwezi Februari 05, 2005. Harakati hizi zilifanyika Kijijini Kidamali kwa upande mmoja na kwa upande mwingine jijini Dar es Salaam.

Kamati zote mbili zilizoundwa zilijipa majukumu mbalimbali, likiwemo lile la kuwaalika na kuwashirikisha ndugu na wanaukoo katika suala zima la maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Ukoo katika vikao, na pia utoaji wa michango.

Katika harakati za maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa UKoo wa Kivenule, kamati zote mbili zilizipata vikwazo mbalimbali likiwemo tatizo la mwitikio duni katika kulipokea wazo hili. Kwa ujumla, katika kuliuza suala/wazo hili la kuandaa na kuwa na Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, kamati ilibidi zitumiea nguvu na mbinu za ziada ili kuweza kufanikiwa.

Mahudhurio duni yalitoa changamoto kwa Kamati za Maandalizi ya Mkutano Mkuu, kuongeza juhudi/jitihada na kutafuta njia mbadala za kufikia lengo. Kwa upande wa Kijijini Kidamali, ushawishi ulizaa matunda, kwa sababu ongezeko la wanaukoo na ndugu kuliunga mkono wazo la kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo lilivuna washiriki wengi.
Kwa upande wa Dar es Salaam, suala la mahudhurio duni, liliendelea kuwa ni kikwazo kwa kipindi chote cha maandilizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Wapo waliodiliki kusema Mkutano Mkuu wa Ukoo ufanyike kwanza Dar es Salaam na ndipo ufanyike na kijijini Kidamali. Licha ya kupewa sababu na maelezo ya kina ya kuufanya Mkutano huo ufanyike Kijijini Kidamali, hawakutilia maanani.

Katika suala la utoaji wa michango, watu wamekuwa na ari na mwitikio wa hali ya juu hapa Kijijini Kidamali, na kwa kiwango kikubwa ndio waliosaidia kufanikisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule.
Licha ya wanaukoo waishio Dar es Salaam kuchangia, lakini mchango wao umesaidia kidogo sana, kwa sababu kiwango kikubwa cha fedha pamoja na mahitaji mengine, yamepatikana hapa.

Sehemu nyingine, nje ya Kidamali, utoaji wa michango hapo mwanzo ulikuwa wa wastani, lakini kadiri siku zilivyokuwa zinakaribia, ari na kasi mpya ilijitokeza na kuwa kubwa hasa toka sehemu za Magubike pamoja na Nyamihuu.

Majirani na watu wengine wasio wanaukoo wamejitolea kutoa michango katika kuusaidia Ukoo wa Kivenule, kufanikisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Majirani na marafiki waliojitokeza kwa hali na mali katika kutoa fedha, vyombo na vifaa mbalimbali.

IX: HOTUBA YA MGENI RASMI
Mgeni Rasmi aliishukuru Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule kwa kumwalika kuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Kivenule. Alisisitiza kwa kusema kuwa, kuna watu wengi muhimu ambao tumewaacha na kuamua kwenda kumwalika yeye.

Mgeni Rasmi alisema amefarijika sana kutokana na kuwashirikisha jamaa/wanaukoo wote. Pia alisisitiza kuwa anahisi yupo karibu na ukoo wa Kivenule kutokana na baadhi ya jamaa zake wa karibu kuwepo kwenye mkutano huo. Pia hata rafiki zake nao walihudhuria kwenye Mkutano Mkuu wa Ukoo; hii ilimpa faraja sana.

Kutokana na ukoo kuwa na mtandao mkubwa sana, ni muhimu kukawa na shughuli za pamoja kama hizi. Wakati anaongea na Mwenyekiti, amefurahi sana kusikia mikakati ya wanaukoo hasa lile la kufanya senza na pia mkakati wa kufahamiana zaidi.

Mgeni Rasmi aliwashukuru wale wote waliotoa wazo la kuwepo kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule na jinsi walivyoshirikisha wanaukoo katika shughuli hii.
Katika shughuli yoyote ile, vikwazo vipo, suala la msingi ni kuelimishana na kuwashawishi wale ambao hawakuhudhuria ili kuwepo na umoja na mshikamano. Suala mshikamano na umoja ni muhimu sana katika jamii yetu kwani itasaidia kuleta maendeleo na wana-ndugu wanatakuwa karibu. Pia, kuwa pamoja kunasaidia kushirikiana katika magonjwa, furaha na matatizo mbalimbali ya kila siku. Mgeni Rasmi, alitoa mfano wa Abraham na Lutha katika ugomvi wao wa mifugo, lakini mwisho walijaliana katika shida licha ya kutengana. Ndugu ni muhimu sana na hawawezi kutengana.

Mkutano huu unatoa changamoto ya kuwa na mshikamano na kuwa na nguvu zaidi katika kuleta maendeleo. Mgeni Rasmi aliushukuru Ukoo wa Kivenule kwa kuelimishana kuhusu umuhimu wa kuwa na ushirikiano wakati wote nasi tu wakati wa matatizo. Huu ni mfano mzuri kwa jamii nyingine. Mgeni Rasmi aliutakia kila la kheri Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, na kuahidi kuwa yuko nyuma ya wanaukoo sambamba wakati wote wa Mkutano huo.
Baada ya hotuba ya Mgeni Rasmi, MKUTANO MKUU WA KWANZA WA UKOO WA KIVENULE, ulitangazwa Kufunguliwa Rasmi Mnamo saa 4:45 Asubuhi, Siku ya Jumamosi, tarehe 17 Desemba 2005

X: UTAMBULISHO WA WANAUKOO
Kwa mujibu wa ratiba ya siku ya kwanza ya MKUTANO MKUU WA KWANZA WA UKOO WA KIVENULE, utambulisho wa Wanaukoo ulifanyika kwa kila ndugu/mwanaukoo kujitambulisha mwenyewe. Mwenyekiti aliwaelewesha washiriki wote jinsi ambavyo wanapaswa kujitambulisha.

Kila anajitambulisha alipaswa/alitakiwa kutaja jina lake la mwanzo, jina la baba yake, babu na jina la mwisho la ukoo. Lakini, pia wanaukoo walijitambulisha kwa kutaja majina ya Mama zao, Waume au Wake zao.

Kila mshiriki katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, alipewa kitambulisho cha kumtambulisha kwa ndugu wengine. Kitambulisho hicho kilionyesha jina lake kamili, mahali anapoishi, namba ya simu pamoja na sanduku la posta. Hii ilifanyika makusudi ili kupunguza kuulizana majina kutokana na washiriki kuwa wengi.
Yafuatayo hapa chini ni majina ya wanaukoo waliojitambulisha siku/ kwenye Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. (refer registration forms).

XI: UWASILISHAJI WA MADA KATIKA MKUTANO MKUU WA UKOO
Katika MKUTANO MKUU WA KWANZA WA UKOO WA KIVENULE, jumla ya Mada Tano ziliwasilishwa. Mada ya kwanza kuwasilishwa katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ilikuwa ni “CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO”. Wawasilishaji wa Mada hii walikuwa ni ndugu:
1.          Christian        J.          Kivenule [Toka Kidamali]
2.         Augustino                  Kivenule [toka Nduli (Kigonzile)]

MADA YA KWANZA

CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO WA KIVENULE
Maana ya Ukoo (Tafsiri)
Ukoo ni muungano wa familia kadhaa zenye utambulisho fulani, aidha wa jina, alama au mwelekeo mmoja. Tunapozungumzia utambulisho fulani uwe wa jina,alama au mwelekeo mmoja; tunamaanisha kwamba ukoo wa Kivenule unatambulika kati ya jamii nyingine mbalimbali kwa jina la “KIVENULE”, jina ambalo linatuunganisha na jamii nyingine au ndugu kujiona sisi ni kitu kimoja.

Tunapomuona mtu mgeni machoni petu lakini ana mweleko wa ukoo wa Kivenule, tunamwuliza, mwenzetu mwiko wako ni nini kwa upande aidha wa chakula. Bila shaka akitueleza kuwa hali nyama ya Mbawala “Asisile Ukulya Mato” yaani mwiko wake ni kula nyama ya Mbawala, basi sote tunaafikiana kuwa huyu ni ndugu yetu.

Hivyo Ukoo wa Kivenule uzila kula nyama ya Mbawala, na huu ndiyo mwiko mkubwa au alama ya utambulisho tuliyorithishwa na Babu zetu.

Alama nyingine ndani ya Ukoo wa Kivenule ni ile ya Mwitikio, kwa lugha ya fasaha ya asili yaani Kihehe toka kwa wakazi wa mkoa wa Iringa tunaita MWIDIKISO. Mwitikio wa Ukoo wa Kivenule ni MLIGO. Hii ni alama nyingine nyeti inayotambulisha Ukoo wa Kivenule.

Chimbuko la Ukoo wa Kivenule
Chimbuko la Ukoo wa KIVENULE ni kutoka sehemu ya Malangali iliyopo katika Wilaya ya Mufindi, kusini mwa mkoani Iringa. Asili ya ukoo wa KIVENULE ni mchanganyiko wa WAHEHE na WABENA; ambapo mchanganyiko huu hujulikana kama WABENAMANGA.

WABENAMANGA wapo katika maeneo mbalimbali mkoniani Iringa ikiwemo Mgololo, Mtwangu, Idunda, Ilole na kadhalika.

Historia inaonyesha kwamba, Ubini wa KIVENULE ilikuwa ni zawadi iliyotolewa kwa Ukoo wa MWIBALAMA au BALAMA kutokana na umaarufu na uhodari wao katika kulenga shabaha wakati wa mapigano vitani (KWIMIGOHA). MWIBALAMA walikuwa ni Mashujaa katika Shabaha ya Mishale (MIGOHA) kutokana na kuwatekeleza (kuwaua) maadui katika hali isiyo ya kawaida tofauti na wapiganaji wengine.
Kitendo cha kulenga shabaha kikamilifu bila kukosea walikiita KUVENULA. Uhalisia wa KUVENULA ni kuua kikamilifu maadui katika vita. Kwa hiyo KIVENULE limetokana na neno KUVENULA na lilipatikana kama Zawadi toka kwa Wakubwa wa Vita siku hizo za mapigano vitani. KIVENULE ni jina la sifa ya kuwa na uwezo wa kumvua adui kwa kutumia shabaha ya Mishale (Migoha) bila vikwazo.

Mzee TAGAMTWA ambaye alitoka katika Ukoo wa MWIBALAMA alikuwa ni ni mtu na Kaka na TAVIMYENDA KIVENULE. TAGAMTWA alifia vitani na mwili wake haukuweza kupatikana. Mzee TAGAMTWA ndiye aliyemzaa SALAMALENGA aliyekwenda kueneza Ukoo wa Kivenule maeneo ya ILOLE. Kwa maana hiyo, Mzee TAGAMTWA alikuwa ni Baba yake SALAMALENGA.

Historia inaonyesha kuwa, Mzee TAVIMYENDA na Mzee SALAMALENGA  wakitokea maeneo ya Malangali - Mufindi walifikia Kalenga, ambapo walikutana na Mzee KIKOTI. KIKOTI alikuwa ana mifugo yake eneo la MAGUBIKE na ULEFI. Hivyo, KIKOTI alimwomba TAVIMYENDA aende MAGUBIKE ili aweze kumwangalia mifugo yake. Hali kadhalika Mzee SALAMALENGA katika kutafuta maisha, aliamua kwenda ILOLE.

TAVIMYENDA ndiye alieneza ukoo kwa upande wa KIDAMALI na hali kadhalika SALAMALENGA alifanya hivyo kwa upande wa ILOLE.

Babu TAVIMYENDA yeye alikuja upande wa Magubike yaani ULEFI enzi hizo. Babu TAVIMYENDA KIVENULE na Mke wa wake MKAMI waliishi ULEFI na baada ya kufa walizikwa pale pale ULEFI. Babu SIGATAMBULE KIVENULE pamoja na Babu wengine KAVILIMEMBE KIVENULE, MGAYIFAIDA KIVENULE, HUSENI KIVENULE na BIBI MGASI walizaliwa katika eneo la ULEFI - MAGUBIKE. Katika uhai wao muda mwingi waliishi eneo la ULEFI kabla ya Wazungu kufika wakitafuta eneo la kuishi na wakapewa sehemu ya ULEFI. Mzungu huyo alikuwa ni JIM, Mgiriki wa kwanza kufika eneo la ULEFI.
Kutokana na hali hiyo, Babu SIGATAMBULE KIVENULE alihamia sehemu ya MLAFU pamoja na Babu mwingine MGAYAFAIDA. Kufika MLAFU, Babu SIGATAMBULE alikuna na Mzungu mwingine aliyeitwa SPELO. Kwa hiyo Wazungu hao wakampimia eneo la MLAFU na hivyo akawa amepakana na wazungu pande zote. Kwa chini akawa amepakana na Giriki MICHO. Babu HUSENI KIVENULE yeye alihamia MAGUBIKE.

Maana halisi ya MAGUBIKE ni kuwa kuna jiwe liliwafunika watu hapo siku za mwanza ambapo watu walikuwa wanaishi mapangoni.

KIVENULE waliopo ILOLE na NDULI wa wale waliopo KIDAMALI na MAGUBIKE wote ni asili moja.

MGAWANYIKO WA UKOO WA KIVENULE


WATOTO WA BABU TAVIMYENDA
1.        Kavilimembe                              Kivenule        Kazikwa Magubike (Me)
2.      Myagafaida                                Kivenule        Kazikwa Mlafu (Me)
3.      Sigatambule                               Kivenule        Kazikwa Mlafu (Me)
4.      Huseni                                          Kivenule        Anaishi Magubike (Me)
5.      Abdalah                                      Kivenule        Kazikwa Mlafu (Me)
6.      Sikimbilavi                                  Semabiki       Kazikwa Mlafu (Ke)


7.      Mgasi                               Kivenule        Kazikwa Mlafu (Ke)
8.      Sigungilimembe                         Kivenule        Kazikwa Mjini (Ke)
9.      Malibora                          Kivenule        Kazikwa Mkimbizi (Ke)

A:        WATOTO WA BABU KAVILIMEMBE KIVENULE

1.        Salikuwaganga  Kivenule       Anaishi Nzihi (Ke)
2.      Dalikimali                       Kivenule        Anaishi Nzihi (Ke)
3.      Francis                             Kivenule        Amezikwa Mlafu  (Me) (Monica Kivenule)
4.      Pangalasi                                    Kivenule        Anaishi Ilula (Me)
5.      Sandra                             Kivenule        Amezikwa (Ke) (Mama Mapembe)
6.      Elizabert                          Kivenule        Amezikwa (Ke)

B:        WATOTO WA BABU MGAYAFAIDA KIVENULE HAKUWA NA FAMILIA

C:        WATOTO WA BABU SIGATAMBULE KIVENULE

WATOTO WA BABU SIGATAMBULE

Bibi SIWANGUMHAVI SINGAILE
Bibi NYANYIMALE SINGAILE
Bibi PANGULIMALE SETWANGA
1.        Gidagumhindi (Cecilia) Kivenule (Ke)
2.       Semyamba (Khadija) Kivenule (Ke)
3.       Sivinitu (Alphonce) Kivenule (Me)
4.    Kadungu (William) Kivenule (Me)
5.       Fibumo (Zavery) Kivenule (Me)
6.       Mlagile (Anyesi) Kivenule (Ke)
7.       John            Kivenule (Me)
1.        Mgulwa (Mama Agatha) Kivenule(Ke)
2.       Luhanage (Ponsiano) Kivenule (Me)
3.       Mgendwa (Eusebio) Kivenule(Me) Baba Kaini
4.       Msinziwa (Daniel) Kivenule(Me)
5.       Kanolo (Edward) Kivenule(Me)
1.        Conjeta Kivenule – Magubike
2.       Pyela Kivenule
3.       Faustino Kivenule
4.       George Kivenule
5.       Carolina Kivenule
D:       WATOTO WA BABU HUSENI KIVENULE

WATOTO WA BABU HUSEN

Bibi YIMILENGERESA (Mume yuko) Vitani) SEMSISI
Bibi DALIKA SETALA
1.        Nyakudila (Benjamin) Kivenule(Me) – Gangimali
2.      Sekiyavile (Modesta) (Ke) Kivenule – Magubike
3.      Dominikus Kivenule (Me) – Magubike
4.      Emmanuel Kivenule
5.      Luciana Kivenule (Dead)
1.        Kabogo (Bernardi) Kivenule (Me) – Magubike
2.      Sembata (Josephina) Kivenule (Ke) – Nyamahana
3.      Brandino Kivenule (Me) – Kidamale
4.      Batromeo Kivenule (Me) (Dead)
5.      Tavina Kivenule (Ke) – Nyamahana
6.      Masikitiko Kivenule (Dead)

WATOTO WA BIBI MGASI KIVENULE
1.        Gisapa                             Kigereso (Ke) [dead]
2.      Sinatoga                          Kigereso (Ke)
3.      Mtogapawene                Kigereso (Ke) [dead]
4.      Chesilemungu                 Kigereso (Ke) [dead]
5.      Ronjino                            Kigereso (Me) [dead]

MGAWANYIKO WA UKOO WA TAGAMTWA MWIBALAMA
1.             CHOGAVANU                                  KIVENULE
2.           PANGAYENA                                     KIVENULE
3.           JONAS                                                  KIVENULE
4.           SAMWEL                                              KIVENULE
5.           MUNGUATOSA                                   KIVENULE
6.           GALASAMANENO                             KIVENULE
7.           WILLIAM                                              KIVENULE
8.           TINDASULANGA                                KIVENULE
9.           GUNGAMESA                                     KIVENULE
10.        SIGONGOLA                                       KIVENULE
11.          SHABAN                                              KIVENULE
12.         BARTON                                              KIVENULE

1. CHAGAVANU       S.         KIVENULE
1.             NOSOLO           C.        KIVENULE
2.           MADESTUS       C.        KIVENULE
3.           PAULINA          C.        KIVENULE

2. PANGAYENA    S.        KIVENULE
1.             GWELINO         P.        KIVENULE
2.           PASCAL                        P.        KIVENULE
3.           STELINA           P.        KIVENULE
4.           PAUSTINA        P.        KIVENULE
5.           BERNADI          P.        KIVENULE
6.           CHELINA          P.        KIVENULE
7.           IGNUS               P.        KIVENULE
8.           CONSOLATA   P.        KIVENULE
9.           RAPHAEL         P.        KIVENULE

1. GWELINO                      P.       KIVENULE
1.             Fausta               G.        Kivenule
2.           Julius                  G.        Kivenule
3.           Delia                  G.        Kivenule
4.           Vasisile              G.        Kivenule
5.           Christopher      G.        Kivenule
6.           Farida               G.        Kivenule
7.           Michael              G.        Kivenule
8.           Machelina         G.        Kivenule
9.           Stumai              G.        Kivenule
10.        Philimon           G.        Kivenule
11.          Lugina               G.        Kivenule
12.         Agnes                G.        Kivenule
13.         Anitha               G.        Kivenule
14.        Frola                  G.        Kivenule
15.         Bosco                 G.        Kivenule
16.        Olive                  G.        Kivenule
17.         Tegemeo           G.        Kivenule
18.         Yovita               G.        Kivenule

2. PASCAL                 P.       KIVENULE
1.        Mage                    P.        Kivenule
2.      Seuginge  P.        Kivenule

3. STELINA             P.       KIVENULE
1.        Eluda                   Nyemba
2.      Anjila                   Nyemba

4. PAUSTINA                     P.       KIVENULE
1.        Yudita                  Kiteve
2.      Daniel                  Kiteve
3.      Etta                      Kiteve
4.      Wuliana               Kiteve
5.      Kalumelita          Mkeng’e
6.      Charles                 Kiteve
7.      Valendino           Mkeng’e

5. BERNADI                       P.       KIVENULE
1.        Damas                 B.        Kivenule
2.      Kamimi                B.        Kivenule
3.      Laheli                   B.        Kivenule
4.      Kalo                     B.        Kivenule
5.      Kulwa                  B.        Kivenule
Damas         B.       Kivenule
·        Nasuma   D.        Kivenule

6. CHELINA           P.       KIVENULE
1.        Tecla                    Kisumbe
2.      Gibson                 Kitu
3.      Carson                 Kisumbe
4.      Lilian                    Kisumbe
5.      Elasto                   Kisumbe

7. CONSOLATA     P.       KIVENULE
1.        Colado                 Ngwenga
2.      Sixtus                    Ngwenga
3.      Thdey                   Ngwenga
4.      Felista                  Ngwenga
5.      Stani                    Ngwenga

8. IGNUS                 P.       KIVENULE
1.        Pelis                     I.          Kivenule
2.      Bernadelt                        I.          Kivenule
3.      Theopista                        I.          Kivenule
4.      Vestina                 I.          Kivenule
5.      Lilian                    I.          Kivenule

9. RAPHAEL                     P.       KIVENULE
1.        Geofrey               R.        Kivenule
2.      Muhomela           R.        Kivenule
3. SAMWEL             S.        KIVENULE
1.             MARTIN                        S.         KIVENULE
2.           LUCAS               S.         KIVENULE
3.           ALOYCE                       S.         KIVENULE
4.           ERENESTO       S.         KIVENULE
5.           INNOCENT       S.         KIVENULE
6.           MICHAEL          S.         KIVENULE
7.           MONICA           S.         KIVENULE
8.           ANNA               S.         KIVENULE
9.           ANNETA           S.         KIVENULE
10.        FELINA             S.         KIVENULE

1. MARTIN                 S.         KIVENULE
1.        Anesia                  M.        Kivenule
2.      Festo                    M.        Kivenule
3.      Msso                     M.        Kivenule
4.      Nelson                  M.        Kivenule
5.      Saida                    M.        Kivenule
6.      Neema                 M.        Kivenule
7.      Faraja                  M.        Kivenule
8.      Teresia                 M.        Kivenule

2. LUCAS                   S.         KIVENULE
1.        Efrehem               L.         Kivenule
2.      Uzuni                   L.         Kivenule
3.      Kibanile               L.         Kivenule

3. ALOIS                    S.         KIVENULE
1.        Kissa                     A.        Kivenule
2.      Zawadi                 A.        Kivenule
3.      Siwazuki              A.        Kivenule
4.      Sitamini               A.        Kivenule
5.      Levina                 A.        Kivenule
6.      Asha                     A.        Kivenule

4. ERENESTO           S.         KIVENULE

5. INNOCENT           S.         KIVENULE
1.        Vicky                    I.          Kivenule
2.      Frank                   I.          Kivenule
3.      Magreth              I.          Kivenule
4.      Grace                   I.          Kivenule
5.      Emmanuel          I.          Kivenule

6. MICHAEL              S.         KIVENULE

7. MONIKA               S.         KIVENULE

8. ANNA                   S.         KIVENULE

9. ANNETA               S.         KIVENULE

10. FELINA                S.         KIVENULE

4. JONAS                   S.         KIVENULE
1.             TITUS                 J.          KIVENULE
2.           PAULO             J.          KIVENULE
3.           EMMNUEL        J.          KIVENULE
4.           ANALOIDA      J.          KIVENULE
5.           ARDO                J.          KIVENULE
6.           EMILYANA       J.          KIVENULE
7.           GWIDO             J.          KIVENULE
8.           JONISIA             J.          KIVENULE
9.           PIUS                  J.          KIVENULE
10.        EMILYO             J.          KIVENULE

1. TITUS                     J.          KIVENULE
1.             Yustina              T.         Kivenule
2.           Evaristo             T.         Kivenule
3.           Castory              T.         Kivenule
4.           Atanasi              T.         Kivenule
5.           Patricia             T.         Kivenule
6.           Jachinda            T.         Kivenule
7.           Johakimu          T.         Kivenule
8.           Letisia                T.         Kivenule

2. EMILYO                 J.          KIVENULE
1.             Jamila                E.         Kivenule
2.           Dolla                 E.         Kivenule
3.           Mwahen            E.         Kivenule

3. PIUS                      J.          KIVENULE
1.             Frank                P         Kivenule
2.           Fotte                 P.        Kivenule
3.           Verlo                 P.        Kivenule
4.           Mkutwa            P.        Kivenule
5.           Niva                  P.        Kivenule

4. PAULO                 J.          KIVENULE
1.             Costandino       P.        Kivenule
2.           Lenzia               P.        Kivenule

5. ARDO                    J.          KIVENULE
1.             Lembula           A.        Kivenule
2.           Kandia              A.        Kivenule


6. EMMANUEL         J.          KIVENULE
1.             Mgilinde            E.         Kivenule

7. GWIDO                 J.          KIVENULE
1.             Sikweli               G.        Kivenule
2.           Frida                  G.        Kivenule
3.           Reginandi         G.        Kivenule

ANALOIDA              J.          KIVENULE
1.             Fahamu                        A.        Kivenule
2.           Rojasi                 A.        Kivenule

5. MUNGUATOSA    S.         KIVENULE
1.             MARIAM           M.        KIVENULE
2.            

6. GALASAMANENO          S.         KIVENULE
1.             CHELINA          G.        KIVENULE
2.           DOMINICUS     G.        KIVENULE
3.           DAVID              G.        KIVENULE

7. WILLIAM               S.         KIVENULE
1.             MUSA                W.       KIVENULE
2.           HASSAN           W.       KIVENULE
3.           ANSEREM         W.       KIVENULE
4.           PAULINA          W.       KIVENULE
5.           YESOFINA        W.       KIVENULE
6.           RIDIA                 W.       KIVENULE

8. TINDASULANGA S.         KIVENULE
9. GUNGAMESA      S.         KIVENULE


10. SIGONGOLA       S.         KIVENULE


11. SHABAN               S.         KIVENULE
1.             AUGUSTINO    S.         KIVENULE

12. BURTON              S.         KIVENULE
1.             MASUDI                        B.        KIVENULE
2.           STEPHAN         B.        KIVENULE
3.           JOHN                 B.        KIVENULE
4.           BONIPHASI      B.        KIVENULE
5.           FABIAN             B.        KIVENULE
6.           LOSINA             B.        KIVENULE
7.           MALUKUS         B.        KIVENULE
8.           JULIO                 B.        KIVENULE

MALUKUSI                B.        KIVENULE
1.             Jalibu                 M.        Kivenule
2.           Kulwa                M.        Kivenule
3.           Doto                  M.        Kivenule
4.           Fatuma             M.        Kivenule

JULIO             B.        KIVENULE
1.             Siyaleo               J.          Kivenule
2.           Gude                 J.          Kivenule
3.           Tuma                 J.          Kivenule
4.           Monika              J.          Kivenule
5.           Pelida                J.          Kivenule
6.           Kulusumu          J.          Kivenule
7.           Ajina                  J.          Kivenule
8.           Vailes                 J.          Kivenule

MASUDI         B.        KIVENULE
1.             Evaristo             M.        Kivenule
2.           Shedlack           M.        Kivenule

STEPHAN     B.        KIVENULE
1.             Aida                   S.         Kivenule
2.           Rajabu              S.         Kivenule
3.           Kimbembe        S.         Kivenule
4.           Ambaa              S.         Kivenule
5.           Fanula               S.         Kivenule

JOHN             B.        KIVENULE
1.             Wick                  J.          Kivenule
2.           Simbion             J.          Kivenule
3.           Mtitu                 J.          Kivenule

KUPOTEA KWA UKOO
Siku zote katika harakati za kutafuta maisha, ukoo hujikuta unajitenga na mazingira yake ya asili, yaani nyumbani na kujikuta ukoo husika upo sehemu nyingine. Sababu kubwa ya ukoo kuwa sehemu nyingine ni kutafuta mkate wa kila siku; lakini pia kutafuta unafuu wa uchumi na kupata maendeleo ya kuendesha familia zao.

Siwezi kusema moja kwa moja kuwa kuna kupotea kwa ukoo; isipokuwa wanandugu siku zote hupuuzia mawasiliano baina ya wanandugu na kuweka/kujenga ukuta baina yao na hivyo kufanya ndugu wawe na mfumo mbaya wa mawasiliano. Kutokuwa na mawasiliano huleta matatizo mengine kama vile kutosaidiana pindi shida zinapotokea na pia kutokujua upande mwingine wanafanya nini!

Mfumo huu dume wa kutotafuta mtandao wa mawasiliano na kutokuwa karibu baina ya wanandugu huleta mgawanyiko, na tabaka ndani ya ukoo, lakini mbaya ziaid kutakuwa na pengo kubwa la maendeleo baina ndugu yaani wenye nacho na wasio nacho. Hivyo basi japokuwa wanandugu tunaishi maeneo tofauti tofauti hatuna budi kuimarisha mtandao wa mawasiliano na kuwa karibu siku zote. Kuna usemi wa Kiingereza usemao: “People are lonely because they build walls instead of bridges”. Kwa lugha rahisi ya hapa kwetu ni kwamba “Avanu vakivakwa kuva vasengite ulukanzi badala ya kisumbo au kilowoko”!!!... Na kwa nini tujenge ukuta baina yetu?!!!. Hatuna budi tujenge daraja litakalotuunganisha yaani tuweze kuvuka kutoka upande mmoja hadi mwingine ili tuweze kufahamu upande mwingine wanafanya nini cha katika kujiletea maendeleo.

HASARA ZA KUPOTEA KWA UKOO
Kuna hasara nyingi zipo ambazo tunaweza kuzipata endapo ukoo utapotea; kati ya hasara hizo ni pamoja na:
§        Kuleta umaskini na ndugu/mwanaukoo kuwa tegemezi; kwa mfano ndugu aliyetoka nyumbani kwenda Kigoma au popote kwa miaka mingi; hivyo anapoteza mawasiliano na wenzake, pindi maisha yanapomuelemea basi anaanza kuwa omba omba. Kwa sababu hana msaada wa karibu kutoka kwa wanandugu.
§        Kudumaa kimaendeleo kwa sababu ya kuridhika na mfumo mmoja wa maisha. Hakuna ushindani wa maendeleo kwa sababu hajifunzi kwa ndugu wenine kutokana na hatua za maendeleo walizozifikia. Matokeo yake ndugu anaridhika na kujipa moyo eti kwa sababu yupo ugenini na hana shida.
§        Kuna hatari kubwa ya kujiingiza katika matukio mabaya mfano ujambazi, utumiaji wa madawa ya kulevya kama bangi, cocaine, mandrax na kujidunga sindano. Pia ndugu huwa katika nafasi ya kujihusisha na uasherati au umalaya katika madangulo (kasino).
§        Hukosa msaada tosha wa mawazo na hata jeki ya kujiletea maendeleo
§        Kutokea kwa mgongano wa mapenzi. Hii inamaanisha kwambaa vijana ndani ya ukoo wanaweza kujikuta wanatafutana wao kwa wao ndani ya ukoo, kwa sababu wote wapo ugenini kwa muda mrefu na hawana mawasiliano na nyumbani kwao.

FAIDA ZA WANAUKOO KUWA KARIBU
Faida ambazo wanaukoo wanaweza kuzipata kama watakuwa karibu ni pamoja na:
§        Kudumisha undugu na upendo baina ya wanandugu ndani ya ukoo.
§        Huchochea maendeleo ya kasi ndani ya wanaukoo kwa kuangalia ndugu mwingine anafanya nini, na pia ndugu nao kujifunza kutoka kwake na kuomba mawazo kutoka kwake au kwa wengine.
§        Hupunguza ugumu wa tatizo, na kuonekana tatizo ni dogo na lenye kutatulika endapo kuna ushirikiano wa dhati ndani ya wanandugu. Hii ni kwa sababu wanandugu ni kitu kimoja na mtu kuchukulia tatizo la mwenzake kuwa lake mfano wa jamii zilizopiga hatua katika hili ni Wahindi, Waarabu na hapa nyumbani kwetuTanzania ni Wachaga. Familia nyingi katika jamii hii wamepiga hatua katika maendeleo.
§        Ni rahisi kuanzisha miradi ya pamoja ya maendeleo kwa kuwa tunakuwa na itikadi zenye mlengo mmoja na wa kufanana; tofauti na kuwa na mradi na mtu tofauti msiyejuana, inaleta utata na ugumu zaidi.

Ni vizuri wanaukoo wakaanza kuwa kitu kimoja kuanzia sasa. Tuache tofauti baina yetu. Tumwombe Mwenyezi Mungu atujalie roho ya kuwapenda wengine na kuwapenda ndugu zetu kama tunavyojipenda sisi. Tuwe tayari kuwasaidia ndugu wanaoelemewa na maisha, tuwape fara na msaada wa vitu na hata mawazo katika kuhakikisha kila mmoja anapta unafuu wa maisha.
MAJADILIANO YA KWENYE VIKUNDI

KUNDI NA. 1
Ukoo ni Nini?
Ukoo huanza na mtu mmoja, ambaye huzaa watoto na pia watoto nao kuwa na familia zao (yaani nao kuzaa watoto). Mwishoni muunganiko huu huwa ni kitu kimoja ambacho ni Ukoo.
§         Kuoa au kuolewa ndiyo msingi mkubwa wa kuwa au kuunda Ukoo kwa sababu kuoa au kuolewa ndiko kunakojenga familia ambazo zinachangia kupatikana kwa Ukoo.
§         Ukoo pia unaweza kuenea hata nje ya mipaka mfano Ulaya, America na kwingineko ulimwenguni.

KUNDI NA. 2
Kuenea kwa Ukoo
Maana yake ni
§        Mtu yupo mahali fulani, ukamtembelea mfano Mbeya, Dar es Salaam, Kenya na kwingineko.
§        Mtu yupo mahali fulani lakini usitake kumtembelea.
Kuenea/Kukua kwa Ukoo
§        Kuoa au Kuolewa
§        Kufahamiana
§        Elimu/Kusoma kutapelekea kujulikana
§        Kusaidiana na kushirikiana
§        Mawasiliano, mfano mtu wa Mwanza, alioa na akaleta mawasiliano kuwa ana mtoto Mwanza na kumleta.

KUNDI NA. 3
Mgawanyiko wa Ukoo
Dodoma
 
Iringa
 
Ukoo unaweza kugawanyika kutokana na ndugu au wanaukoo kuamua kuishi sehemu fulani kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo zile za kiuchumi, hali ya hewa nzuri na maendeleo.

















§        Watoto kujaliana upande wa mama na si upande wa baba ambaye ni mwanzo wa ukoo.
§        Kuongeza matawi na Kidamali pawe ni mzizi wa ukoo.
§        Wanawake wapunguze tofauti kwani wao ndiyo chanzo cha kuugawa ukoo.l

Katika kuunganisha mgawanyiko huu wa Ukoo ni Mawasiliano baina ndugu wanaoishi sehemu mbalimbali. Mfano katika kipindi hiki mawasiliano ya simu za mkononi yameenea kila mahali, cha msingi ni kuwa na mkakati thabiti katika kuhakikisha kuwa ndugu wanakuwa na mawasiliano yaliyo sahihi. Bila kuwa na mawasiliano ina maana kuwa tunakuwa tumejiwekea ukuta mnene wa kututenganisha wanaukoo.

KUNDI NA. 4
Kupotea kwa Ukoo
Kupotea kwa ukoo husababishwa na sababu kadha wa kadha mojawapo zikiwa zimeainishwa hapa chini:
§        Kutosaidiana katika shida mbalimbali mfano misiba na ugonjwa.
§        Kutotembeleana toka sehemu moja hadi sehemu nyingine mfano ndugu mmoja anakaa Morogoro na ndugu mwingine anakaa Dar es Salaam, Tabora na kadhalika.
§        Kudharauliana kutokana na kutofautiana katika kipato (fedha), umaskini, utajiri na elimu.
§        Kukosekana kwa mawasiliano mfano kupigiana simu; kutotambulishana na kutotembeleana.
§        Watoto kutotembelea kwa ndugu.
§        Wanawake wanaoolewa kwenye ukoo kutotembeleana
§        Maskini wasio na kipato (hana kitu) kuona aibu kufika kwa ndugu mwenye uwezo (kipato kizuri) bila ya kufahamu kuwa wote ni ndugu wa ukoo mmoja.
§        Kupeana taarifa mapema za matatizo kwa ndugu wote ili tuwe kitu kimoja.

Jambo la msingi kufanyika katika kuhakikisha kuwa Ukoo haupotei ni kuundwa kwa Kamati itakayoratibu matatizo ya Ukoo pamoja na wanandugu.
MADA YA PILI
MAHUSIANO BAINA YA WANANDUGU NDANI YA UKOO
Utangulizi
Maana ya Mahusiano ni hali ya ukaribu, ujirani, urafiki, umoja au ushirikiano unaojengeka baina ya Ndugu, Jamaa au Marafiki. Mahusiano ni hali ya kuwa pamoja Kifikra, Kimwili, Kimawasiliano, Kiimani, Kiitikadi, Kimaendeleo, Kikazi, Kijamii na Kimichezo.

Mahusiano hujengwa kwa misingi/namna mbalimbali. Baadhi ya njia au vitu vinavyosababisha kukawepo na mahusiano ni pamoja na:
1.          Ujirani: Ujirani mara nyingi katika jamii zetu huchangia sana katika kujenga Mahusiano. Mahusiano yenyewe huonekana katika sura mbili tofauti. Yaani Mahusiano Mazuri kwa maana ya Sura Nzuri au Mahusiano Mabaya kwa maana ya Sura ya Ubaya.
2.         Undugu: Hii ni aina ya nyingine ya Mahusiano ambapo ndugu wa Damu Moja au wanachangia damu, hujenga Mahusiano ya Moja kwa Moja (Automatic Relationship). Mara nyingi Mahusiano ya aina hii huwa na Sura ya Uzuri zaidi (Mahusiano Mazuri). Japo kuna kipindi Fulani hata Sura ya Ubaya (Mahusiano Mabaya) hujitokeza.
3.         Imani: Pia watu huweza kujenga Mahusiano kupitia Imani zao, mfano watu wanaoabudu katika dhehebu moja huweza kujenga mahusiano ya aina yao tofauti na dhehebu jingine. Mara nyingi Mahusiano ya Kiimani huwa na mwelekeo wa Mahusiano mema. Mahusiano mabaya mara nyingine hutokea na hata kusababisha vita vya kiimani (dini).
4.         Itikadi: Mahusiano ya Kiitikadi nayo hujengeka kwa kufuata Mlengo wa Vyama Vyao. Na zaidi Mahusiano ya Kiitikadi huegemea zaidi kwenye siasa na hupungua au kutoweka kabisa baada ya mmoja wao kubadili Itikadi yake yaani kuhama toka chama cha kimoja cha siasa na kwenye chama kingine cha siasa. Mahusiano ya Kiitikadi hujengwa kwa misingi ya Chuki, Fitina na Vitisho baina wa watu wa Itikadi moja na wale wa Itikadi nyingine.
5.         Maendeleo: Watu wenye hali fulani ya kimaendeleo huweza kujenga aina fulani ya mahusiano yenye nia ya kuinuia hali zao za kimaisha. Na mara nyingi wanaojumuika hapa ni wale ambao tayari wameonesha nia na mwelekeo. Lakini pia hata wale waliopiga hatua kimaendeleo huweza kuja mahusiano yao yakiwa nia ya kuimarisha hali walizonazo. Msingi mkubwa wa mahusiano ya aina hii huwa ni kupeana mbinu na mikakati ya kuleta au kujiimarisha zaidi katika maendeleo ambayo wanayatarajia au ambayo wamekwisha yapata.

Pia hata kwa upande wa wale wenye hali duni ya kimaendeleo nao hujenga aina Fulani ya mahusiano kulingana na hali na uwezo wao. Kasoro ambayo hujitokeza hapa huwa ni mahusiano duni baina wenye uwezo (matajiri) na wale na wasio na uwezo (maskini). Katika kujiimarisha zaidi kimaendeleo, maskini huwa mtumishi (kibarua) na tajiri huwa mtumikiwa (mtwana).

6.         Elimu: Watu wenye elimu nao mara nyining hujenga mahusiano yao. Mara nyingi katika mahusiano yao huwatenga wale wenye elimu kidogo au wasio na elimu kabisa. Hii hutokea zaidi kwa wale waliobahatika kupata Elimu ya Juu mfano Chuo Kikuu. Mazungumzo na mipango yao huwatenga zaidi wale wenye elimu kidogo. Kuwatenga hujitokeza katika matumizi ya lugha za kigeni, kutowashirikisha katika mawazo mbalimbali ambayo wanadhani yanaweza kuwainua watu wa hali zote (wasomi na wasio wsomi).

AINA ZA MAHUSIANO
Kuna aina mbalimbali za mahusiano, lakini tunaweza kugawanya mahusiano haya katika sehemu kuu mbili.
1.          Mahusiano Mazuri; na
2.         Mahusiano Mabaya.
Aina mbalimbali za mahusiano ambayo yapo katika jamii zetu ni pamoja na mahusiano ya:
§        Kikazi;
§        Kijamii;
§        Kisiasa; na
§        Kiuchumi.

MAHUSIANO MAZURI
Mahusiano Mazuri ni hali ya kuwa pamoja kwa kushirikiana katika nyanja mbalimbali za maisha. Mahusiano Mazuri huwa katika shida au raha. Raha hujumuisha hali zozote zenye kuashiria mafanikio na maendeleo katika maisha ya binadamu. Hii ni pamoja na kufaulu mitihani mbalimbali ya darasani na ya maisha; kujenga nyumba, kununua gari, kapata kazi nzuri, kufanikiwa katika kilimo, Jubilei, kupandishwa cheo pamoja na kupata nishani.

Shida huwa ni hali ya kuwa na mashaka, kutokuwa na uhakika wa maisha, kutokuwa na kipato, kutofanikiwa katika elimu, ugonjwa, misongamano (Depression), misusuko (stress), kutokuwa na ajira, kutofadhiliwa kwa hali yoyote (Promotion au Scholarship) na kadhalika.

MAHUSIANO MABAYA
Mahusiano Mabaya ni hali ya kutokuwa na ushirikiano, huruma au wema katika nyanja mbalimbali za maisha. Mahusiano Mabaya nayo hali kadhalika huwa katika ubaya au uzuri au shida na raha. Tofauti na katika Mahusiano Mazuri, Mahusiano Mabaya hubaki kuwa ni swa katika shida na raha. Kwa ujumla ushirikiano na mawasiliano hukosekana kabisa. Huwa hakuna huruma, maelewano, kuvumiliana na kuwasiliana.

Kikubwa ambacho hujengeka ni chuki, majivuno, wivu, ugomvi na kutakiana shari. Hamna hata mmojawapo ambaye huombewa kheri. Kwa yule aliyenacho, huombea au hutamaini yeye aendelee kuwa nacho peke yake na kutomwombea kheri ya kupata yule ambaye hana kitu.

Na kwa yule ambaye hana, humwombea shari, bahati mbaya kupotteza au kwa namna yoyote ambayo haina kheri kwa yule ambaye anacho. Baadhi huomba mfano kama ni gari lipate ajari, nyumba iungue na kama anasoma anafeli. Katika aina hii ya mahusiano hakuna nafasi ya kutakiana mema au maendeleo.

MAHUSIANO BAINA YA NDUGU NDANI YA UKOO
Ukoo wa Kivenule ni mkubwa sana na kwa haraka unakadiriwa kuwa na ndugu karibia elfu mbili (2000). Ni ukoo ambao unaweza kufanya mambo makubwa na ya kimaendeleo kama utaungana na kuwa kitu kimoja.

Tatizo kubwa ambalo linaonekana kwa wanaukoo ni kuwa na mwamko mdogo. Kwa mfano wanaukoo wanaohudhuria Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ni theluthi au robot u ya wanaukoo wote. Tumaini la Kamati za Maandalizi ya MKutano Mkuu ni kuhudhuriwa na Ndugu pamoja na Wanaukoo wa Kivenule kwa wingi zaidi.

Kwa upande wa Dar es Salaam, mwamko wao ni mdogo sana. Tumaini na tegemeo la awali ilikuwa Dar es Salaam ingekuwa ni mfano, lakini imeshindika na hii ndiyo hali halisi. Tunasikitika na Kamati ya maandalizi ya Dar es Salaam inaomba samahani.

Kwa wanaukoo toka Ilole, nao wamesema tatizo kubwa kwao ni suala na nauli kuwa ni kubwa. Lakini cha msingi kufanyika ni kuzidi kuwahamasisha na kuwapa mojyo wa kutambua umuhimu wa Mkutano Mkuu wa Ukoo pamoja na mikutano mingine.

Katika suala zima la mahusiano, ukaribu wa wanandugu na wanaukoo linaangaliwa kwa karibu zaidi. Mahusiano yanagusa mambo muhimu katika maisha ya kila siku mfano Elimu, Ugonjwa, Vifo pamoja na Starehe (Harusi, Send-Off, Kipaimara na Komunio). Elimu ni muhimu sana kwani inaongeza upeo na ufahamu wa kuweza kukabiliana na matatizo ya maisha ya kila siku.

Suala jingine ni ushirikiano katika nyanja mbalimbali mfano Biashara, kazi na kilimo. Hapa tunamaanisha kuunda kikundi ambacho kitakuwa na mfuko utakaokuwa unachangiwa na watu mbalimbali kulingana na shughuli na kipato.

Katika kujenga mahusiano imara, kutembeleana ni muhimu sana. Faida ya kutembeleana ni kujuliana hali, kusaidiana, kushauriana na kupeana mbinu na mwongozo wa kufauli katika maisha. Pia katika kutembeleana huwapa fursa wanaukoo/ndugu kuangalia mazingira mapya anayotembelea kama yanaweza kumfaa kuishi akilinganisha na mazingira aliyotoka.

Pia katika kushirikiana kuna haja ya kuwashawishi na kuwabembeleza wale wasio na uwezo ikiwa ni pamoja na kuwapa moyo, kuwashauri waondoe aibu na wajenge tabia ya kushirikiana. Katika kushirikiana inakuwa ni rahisi kuweza kutatua matatizo mbalimbali baina ya wenye nacho na wasionacho.

Kwa mfano katika shughuli nzima ya kuandaa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, inakuwa kitu kizuri na mfano kwa wengine kama tutaonyesha kwa vitendo haya tunayozungumza hapa. Hii utaufanya Mkutano Mkuu kuwa na maana sana. Kivenule kwa tabia ni wapole sana na wenye huruma. Ni vizuri tuwajali wenzetu kwa sababu hali zetu zinajulikana. Cha msingi ni kuwa karibu na kusaidiana.

Mahusiano ambayo ukoo wa Kivenule utarajie ni kama haya ya kuitikia kuja kwenye Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Bila kuwa na hatua madhubuti ukoo utaparaganyika. Katika vitabu vya dini kuna mfano mmoja unasema “Mtu mmoja aliandaa sherehe na akaalika watu kwenda kula, lakini watu wakakataa”. Kwa nini watu walikataa kwenda kula. Kila mmoja ana sababu zake. Mungu awabariki kwa kukubali mwaliko huu.

Tafsiri sahihi ya mahusiano ipo katika maeneo mbalimbali kama ilivyoainishwa pale mwanzo. Kila mwanaukoo anawajibika na anawajibu kushiriki kikamilifu katika hilo. Mahusiano mazuri huleta upendano ambao huwa ni chachu ya maendeleo.

Umuhimu wa kuwa na mahusiano mazuri baina ya wanandugu ni kuulinda ukoo na kupunguza maingiliano kutokana na wanaukoo kutawanyika maeneo mbalimbali ndani ya mipaka na nje ya mipaka. Katika Mkutano huu Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, ndugu na wanaukoo kwa ujumla ni walengwa na wanufaikaji.

Katika suala zima la mahusiano ndani ya Ukoo wa Kivenule, kinachoepukwa hapa ni mgawanyiko wenye mwenendo wa tofauti ya kipato. Lengo mahsusi ni kuangalia kwa nini tunafanya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule? Hapa tunachoangalia ni mguso wa kila hali baina ya wanandugu na wanaukoo kwa ujumla kuwa sisi wote wanaukoo ni kitu kimoja. Hivyo tuwe wepesi katika kutoa misaada wakati wenzetu wana matatizo ya ugonjwa, njaa na vifo. Lakini pia, ni vema kushirikiana na kutoa misaada katika shughuli za furaha kama kufanya harusi, kipaimara na komunio.

Wanaukoo wote wanatahadharishwa, baada ya mwaka mmoja wasipotee kwa sababu na visingizio mbalimbali. Tutumie chombo hiki cha Mkutano wa Ukoo kutoa michango yetu ya mawazo, dukuduku na hamasa ya kuwa na ukoo imara.

MAJADILIANO KWENYE MAKUNDI

KUNDI NA. 1
Ukaribu wa Wanandugu
1.        Ushirikiano wa wanandugu upo katika shida mbalimbali
2.      Kujitolea na kujituma kama mwanandugu kusaidia na kuchangia kwa hali na mali shughuli mbalimbali za Ukoo mfano misiba, ugonjwa na maandalizi ya mikutano kama huu Mkuu.
3.      Kushawishi ndugu wengine ambao hawajawa na mwamko au habari kuhusiana na kuwepo kwa Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Kivenule
4.      Kudumisha mahusiano mema baina ya wanandugu

KUNDI NA. 2
Ushirikiano katika Nyanja Mbalimbali
1.        Elimu: Tuaangalie uwezekano wa kusaidiana katika kupata na kuinue kiwango cha Elimu katika Ukoo bila kujali kipato kwa kujitoa zaidi.
2.      Tuondoe aibu ya kuomba msaada. Toa shida zako kwa ndugu zako ili tusaidiane katika kuzitatua.
3.      Tuondoe ukiritimba katika kuchangia hasa katika ugonjwa. Tusaidiane katika ugonjwa.
4.      Iundwe Kamati ili iwe na mwelekeo kamili wa kuuinua ukoo.
5.      Tupeane taarifa wakati wa matatizo ili kila ndugu awe na taarifa na ashiriki kikamilifu.
6.      Hata katika starehe zetu pia tusaidiane mfano Harusi.
7.      Tutangulize utu mioyoni mwetu kabla ya pesa (tuwe na moyo wa kusaidiana na kufarijiana)
8.      Tusibaguane, tusiangalie kipato. Wewe mwenye kipato tumie muda wako kumsaidia asiye na kipato.

KUNDI NA. 3
Kusaidiana na Kutembeleana
1.        Huwezi kumfahamu au kumjua ndugu yako kama ana matatizo au la hasha kama hujamtembelea.
2.      Ujali zaidi ndugu kuliko kujali kipato chao
3.      Eleza hali halisi ya matatizo uliyonayo hasa pale ukitemblewa na ndugu zako.
4.      Ukiona ndugu yako anadorora katika maisha, hasa pale unapomtembelea basi mpe mawazo ya kumjenga ili naye apige hatua ya maendeleo.

KUNDI NA. 4
Kuondoa Tofauti Baina ya Ndugu
1.        Matatizo yanayoleta migogoro ndani ya ukoo yatatuliwe mapema zaidi.
2.      Tupanue wigo wa kusaidiana ndani ya familia bila kujali huyu tupo tumbo moja au hapana.
3.      Kila eneo liwe na kamati ya mipango ya kuratibu matatizo ndani ya ukoo.
4.      Kuacha ubinafsi; tuache ubinafsi ndani ya ukoo.
5.      Mtu alishukuru kwa kusaidiwa ndani ya ukoo, jambo hili litusaidie hata kwa sisi wanaukoo kuwasaidia wengine.
6.      Haki itendeke sawa katika kupanga maamuzi bila kujali huyu ni msomi, hana kipato, mzuri n.k. tukifanikiwa hili, ukoo utakwenda mbali.
7.      Wazazi wawe waangalifu katika kutoa maamuzi kwa watoto wao, bila kupendelea mtoto na kadhalika.
8.      Tuwekane sawa bila kujali huyu ni nani, tuambiane ukweli katika mkutano huu.
9.      Watu ndani ya ukoo wanene kwa vinywa vyao kama kuna tofauti baina ya ndugu ili tuweze kuondoa tofauti ndani ya Mkutano huu.
10.   Tutoe matatizo yetu leo, ili kesho tupate majumuisho. Hivyo mtu (mwanandugu) awe huru kuongea na awe huru katika maisha yake ya kila siku.

MAJUMUISHO
§        Tusaidiane katika nyanja mbalimbali iwe katika Elimu, Ajira, maisha na kwingineko. Tuige mfano wa Wachaga katika kusaidiana.
§        Tofauti ya maisha baina ya wanandugu ni kitu cha kawaida, hata vidole havipo sawa.
§        Tunapojenga nguvu ya wanandugu tuondoe matabaka.
§        Hapa hapa Kidamali ndugu hawaelewani, tatizo hili ni kubwa sana, hata ndugu yako wa karibu hawezi akasema, leta watoto wapate chakula kwangu kama ilivyokuwa siku za nyuma.

MADA YA TATU
ELIMU NA MUSTAKABALI WA UKOO
Elimu ni kitu cha msingi sana katika maisha ya binadamu. Elimu ni mwongozo wa fikra za binadamu katika kuyamudu, kuyatambua, kuyadhibiti na kuyatawala mazingira ya aina yoyote yanayomzunguka. Elimu ni dira katika maisha yetu ya kila siku. Elimu inasaidia katika utambuzi na ufahamu wa mambo mengi katika maisha yetu ya kila siku.

Zamani koo nyingi hapa kwetu zilipuuza sana Elimu. Umuhimu wa Elimu haukuzingatiwa kabisa. Idadi ya watu waliosoma kadri siku zinavyozidi kwenda mbele ilipungua na imeendelea kupungua sana na hivyo kufanya kiwango cha elimu pia kupungua katika jamii zetu. Kukosa Elimu kumewakosesha wanaukoo nafasi katika sekta mbalimbali za kimaendeleo mfano sekta ya binafsi, sekta ya umma (serikali) na sekta za kijamii (jamii huria). 

Ukoo wa Kivenule una vipaji vingi, lakini Elimu inaweza kuwa ni kikwazo cha mafanikio. Kukosekana kwa elimu pengine kunasababisha jamii ya Kivenule kushindwa kuwa mahusiano (interaction) na jamii nyingine katika kujiletea maendeleo na hasa kutokana na kukua kwa Sayansi na Teknolojia au vinginevyo. Mabadiliko ya sayansi na teknolojiayanauweka Ukoo wa Kivenule njiapanda na hivyo kupoteza mwelekeo.

NAFASI YA UKOO WA KIVENULE KATIKA ELIMU
1.        Tumegundua kuwa nafasi ya ukoo wa Kivenule katika elimu ni mdogo au upo chini kwa sababu:
·        Nafasi za ajira katika maofisi makubwa serikalini ni mdogo.
·        Wanaukoo wachache wamepaa ajira katika mashirika makubwa (umma au binafsi) yanayozingatia kiwango elimu katika ajira.
2.      Kuwa na idadi ndogo ya wanaukoo waliofikia elimu ya kiwango cha juu mfano kidato cha 4, 6 mpaka vyuo vikuu.
3.      Wanaukoo kutojua umuhimu wa elimu.
Ili ukoo uwe na nafasi elimu tufanyaje?
·        Tujitahidi kusomesha watoto wetu hadi elimu ya juu.
·        Elimu ya ufundi pia ni muhimu ndani ya ukoo.
·        Tuunde kamati katika ukoo itkayoratibu sula zima la ukoo.
·        Kukusaya michango kuwasaidia waso na uwezo wa kusomesha.
·        Kuwasaidia kusoma watoto wa ukoo wasio na msaada.
·        Kuwatafutia watoto wafadhili ili kupata elimu.
·        Kubuni miradi ya kusaidia kukua kwa elimu

UMUHIMU WA ELIMU
1.        Umuhimu wa elimu ni kuondoa umaskini ndani ya familia na jamii kwa ujumla.
2.      Mtu mwenye elimu anaweza kusaidia kuinua maisha ya mtu yeyote ambaye hana elimu katika familia.
3.      Mtu mwenye elimu anaweza kubuni mbinu yeyote itakayomwezesha kuyamudu maisha katika:
·        Kilimo
·        Biashara
·        Ufundi
·        Uongozi katika sekta mbalimbali nk.
4.      Umuhimu wa elimu ni kupanua upeo wa akili
·        Kimawazo
·        Kifikra
·        Kujiamini katika mambo yake unayoyapanga
·        Unakuwa na haiba
·        Kujulikana mbele ya watu

DUNIA YA UTANDAWAZI
Utangulizi
Dhana ya utandawazi inahusu kuwepo kwa ulimwengu usio na mipaka katika maingiliano ya jamii mbalimbali katika shughuli zao za kiuchumi na kisiasa licha ya kuwepo kwa mipaka ya kijiografia. Dhana ya "utandawazi" katika kiingereza inaitwa "globalisation", neno ambalo linatokana na "globe", kwa maana ya umbile la dunia yetu. Kama tunavyofahamu dunia yetu ina umbile la tufe.

Kwa karne nyingi, walimwengu walitengenishwa na mipaka ya kimaumbile ya dunia kama vile mito, milima, mabonde na bahari. Kabla havijaundwa vyombo vya usafiri vyenye mwendo wa kasi kuliko wanyama kama vile punda na farasi, jamii nyingi zilkaa peke yake bila kufahamu kama kuna jamii nyingine nyingi katika uso wa dunia. Na kwa sababu hiyo jamii ziligawanyika katika makundi madogo madogo mengi, yenye tamaduni tofauti; kwa maana ya lugha, mila na desturi. Haya ndiyo makabila ambayo yalikuwepo katika mabara yote ulimwenguni.
Kutokana na kukosekana aina yeyote ya mawasiliano ya lugha, au maingiliano yoyote ya kijamii, jamii nyingi zilizokuwa jirani ziliishi kwa uadui. Kila mmoja akimshuku mwenzake ni mbaya au hana thamani. Matokeo yake yalikuwa vita baina ya jamii hizi, mwenye nguvu alimuua mwenzake, au alimteka kuwa mtumwa au alimgeuza kitoweo.

Kwa jamii nyingi ulimwengu wao ulikuwa ni kijiji chao. Watu, ni wale wa kabila lao tu - wengine wote ni "washenzi, wanyika, vyasaka, wanyamahanga, n.k." (Hii ni mifano ya hapa kwetu Tanzania, lakini hata katika mabara ya Ulaya na Asia hali ilikuwa ni hiyo hiyo).

Baada ya jamii kuanza kutengeneza vyombo vya usafiri, hasa vile vya majini, ulimwengu ukaanza kupanuka watu wakaweza kusafiri sio tu baina ya vijiji na miji ya karibu bali walivuka bahari kubwa na kwenda kwenye mabara mbali mbali. Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa Utandawazi.

Watu wa jamii mbalimbali walianza kueneza tamaduni zao huku na kule. Hapa kwetu Afrika tulipata watalii wa kwanza kabisa kutoka jamii za Wayunani, Waarabu na Wachina kame nyingi kabla ya Wareno (hawa ndiyo wazungu wa kwanza huku Afrika Mashariki.

Hata hivyo maingiliano baina ya jamii katika mabara mbalimbali yaliendelea kwa kasi ya wastani tu, kwani nyenzo za usafiri na kupeleka habari zilikuwa hazina kasi kubwa. Bado safari za meli zilichukua miezi au miaka baina ya bara na bara na safari za gari moshi pia zilikuwa za polepole.

Uliundwa mfumo wa Posta wa kimataifa uliowezesha watu kupashana habari kwa maandishi (barua, magazeti n.k.) lakini nao pia haukuwa wa haraka sana. Kwa hiyo basi, bado jamii nyingi ziliendelea kuwa na lugha zao na tamaduni zao ambazo hazijaguswa na mabadiliko kutoka nje ya jamii zao. Lakini katika kame za 19 na 20 yametokea maendeleo makubwa ya kitekinolojia ambayo yamesababisha mageuzi makubwa katika maingiliano ya kijamii: usafiri wa anga, simu, radio, cinema, televisheni na kompyuta. Tekinolojia hizi mpya zimefanya mipaka ya kijiografia kuwa haina uzito tena.

Watu wanaweza kusafiri popote duniani kwa muda mfupi tena kwa raha na starehe zaidi, taarifa za habari zinaweza kufikishwa kwa mamilioni ya watu kwa sauti na picha kwa wakati mmoja katika muda wa sekunde tu. Huu ndiyo uUandawazi. Huu ndiyo ulimwengu usio na mipaka.

Je, katika ulimwengu huu ulio wazi, tunahitaji elimu ya namna gani? Tunasema kuwa elimu ni utaratibu wa kurithisha kutoka kizazi kimoja hadi kingine, maarifa, ujuzi, utamaduni na ustaarabu wa jamii iIi kuidumisha, kuistawisha na kuiendeleza jamii ile.

Changamoto iliyo kwetu ni kuyaelewa vema mapana na marefu ya dhana hii ya Utandawazi, kubaini kwa usahihi jamii tunayoikusudia ni ipi - Tanzania, Afrika Mashariki, SADC au dunia nzima? Na kuafikiana kitaifa ni maarifa gani, ujuzi gani, utamaduni gani, na ustaarabu gani tunaotaka kuwarithisha watoto wetu.

UTANDAWAZI KATIKA KARNE VA ISHIRINI NA MOJA
Choy (2004) anatoa maana ya Utandawazi kwa kusema kuwa Utandawazi ni kasi ya kusambaa kwa watu, mawazo, huduma, mitaji, bidhaa na mambo mengine kutoka nchi moja kwenda nyingine. Hali hii inasababishwa na kukua kwa sayansi na teknolojia. Kwa kifupi Utandawazi unasukumwa na ushindani wa kibiashara ambao umeruhusu utaratibu wa soko huria ambao umesababisha kupanuka haraka kwa sekta binafsi katika uendeshaji wa uchumi na kupanua biashara ya kimataifa.

Utandawazi unaendeshwa na soko Iinalopanuka kwa bidhaa za kila aina kuvuka mipaka ya kitaifa. Uwekezaji, biashara na habari vimefunguliwa mipaka ya kitaifa. Ripoti ya shirika la Maendeleo la Kimataifa (UNDP) ya Maendeleo ya Binadamu (1999) inaeleza kasi ya kuenea kwa utandawazi kwa kusema kuwa "soko likitawala kijamii na kisiasa matokeo yake utandawazi unawanufaisha wachache wenye nguvu za kumiliki mali wakati wengine wakiendelea kuwekwa kando katika ushindani". Ripoti ya UNDP ya mwaka 2004 inathibitisha haya kwa kubainisha kuwa Marekani pekee inamiliki asilimia 85 ya viwanda vyote duniani vya filamu.

Ripoti hiyo pia imetoa mfano wa umiliki na matumizi ya mtandao wa Kompyuta duniani na kubainisha kuwa nchi maskini zina sehemu ndogo sana. Kwa mfano mwaka 1997 nchi maskini zilikuwa zinatumia asilimia 0.2 ya mtandao wa Kompyuta ukilinganishwa na asilimia 93.3 katika nchi tajiri. Katika mgawanyo wa namna hii ni dhahiri kuwa hakutakuwa na usawa katika dunia ya utandawazi.

FAIDA ZA UTANDAWAZI
Utandawazi umefungua milango na kutoa nafasi kwa mamilioni ya watu duniani kunufaika katika nyanja mbalimbali, kama vile, Kukua kwa biashara, maendeleo ya kiteknolojia, uwekezaji nje ya nchi na kukua kwa mawasiliano "na mitandao ambavyo vimechochea kukua kwa uchumi na kuleta maendeleo kwa jamii. Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (1999) linaripoti kuwa dunia ya sasa ina utajiri mwingi na teknolojia ya hali ya juu kushinda wakati wowote ule. Aidha utandawazi umesababisha mataifa kuwa karibu na kufanya dunia kuwa kama kijiji kimoja. Siku hizi ni rahisi kutoka nchi moja na kwenda nchi nyingine kufanya kazi au biashara. Aidha, bila hata kwenda unaweza kusoma au kufanya biashara na nchi nyingine kwa kutumia mitandao.
Kukua kwa mwingiliano wa watu duniani kumeleta mfumo wa kimataifa ambao unathamini maendeleo ya watu wote. Masuala ya maendeleo yanajadiliwa na kuwekewa mikakati kimataifa. Hii inasaidia hata nchi maskini kutoa hoja zake na maslahi yake kulindwa kimataifa. Mwingiliano wa watu duniani unajaribu kuleta maendeleo katika nchi zote na kuondoa tofauti zilizopo ili ushirikiano uwe rahisi. Iii tunufaike na fursa hizi zinazoletwa na utandawazi ni lazima tuwape vijana wetu elimu itakayowawezesha kuelewa majukumu yao katika jamii yenye amani na utulivu, inayozingatia haki za binadamu na kudhamini tofauti za mataifa mbalimbali.

USHINDANI UNAOSABABISHWA NA UTANDAWAZI
Kuenea kwa teknolojia kumepunguza mahitaji ya wafanyakazi wanaotumia nguvu tu bila ujuzi na stadi katika uzalishaji. Kwa hiyo tunahitaji wasomi wenye ujuzi na stadi za kutosha iIi nchi yetu isiwe soko la bidhaa za watu wengine. Ni lazima tulenge katika kujiongezea uwezo wa kunufaika na fursa zinazoletwa na utandawazi. Kwanza kabisa tunahitaji kuimarisha elimu ya sayansi na hisabati, kwani masomo haya ndiyo msingi wa teknolojia; iwe ni teknolojia ya mawasiliano (ICT) au teknolojia ya uzalishaji viwandani.
Kwa hiyo uimarishaji wa masomo ya sayansi na hisabati ni lazima uanzie
shule za msingi. Na vivyo hivyo tuendeleze katika madarasa mengine. Wataalamu wa masuala ya maendeleo wanasema "tofauti ya utajiri kati ya Kaskazini (Ulaya_ na Kusini (Nchi zinazoendelea) ni Sayansi na teknolojia".

Elimu pia ni nyenzo ya kuwajenga watoto katika ujasiri, kujiamini na kuthubutu. Hizi ni hulka ambazo zinaweza kujengwa shuleni kupitia mbinu mbalimbali. Hulka hizi ni misingi imara ya ubunifu na ushindani hata katika biashara za kimataifa.

ELIMU YENYE MWELEKEO WA UTANDAWAZI
Tujiulize, je ni elimu gani inayotakiwa iIi kukabiliana na athari za utandawazi katika jamii yetu? Hili ni swali kwa kila mdau wa elimu. Kila mmoja wetu ajaribu kujibu swali hili kwa ufasaha. Mimi nitadokezea tu yale ambayo tunaweza kuyafanya.

Elimu itolewayo haina budi kuwa yenye misingi ya sayansi na teknolojia. Hivyo ni lazima kuimarisha ufundishwaji na usomaji sayansi na hisabati kuanzia elimu ya msingi. Hali hii inahitaji kubadilisha mitaala yetu iIi iweze kutoa maarifa ujuzi na stadi zinazotakiwa, na kumwezesha mhitimu kukabiliana na utandawazi

Sambamba na ubadilishaji wa mitaala ya shule itabidi kuimarisha mafunzo ya elimu ya ualimu kwa sababu, pamoja na maendeleo na mabadiliko ya tekinolojia hakuna mbadala ya mwalimu darasani. Wote tunafahamu kuwa vitabu na mbinu mbalimbali za kufundishia na kujifunzia anazotumia mwalimu darasani ni bora kuliko matumizi ya televisheni na kompyuta. Ni kweli kuwa pamoja na utandawazi, kwa miaka mingi ijayo mwalimu atakuwa hana mbadala darasani.

ATHARI ZA UTANDAWAZI
Hatari ya kutoweka Utamaduni wa kitaifa: Utandawazi hufungua milango ya kuingiza mawazo na utamaduni wa kigeni unaotoka zaidi katika nchi zilizoendelea kwenda nchi zinazoendelea. Hii inahatarisha utamaduni wa nchi zinazoendelea kutoweka. Kwa mfano inasemekana kuwa mwaka 1998 asilimia 80 ya bidhaa za kiutamaduni duniani zilitokea katika nchi 13 tu duniani zikiongozwa na zile za Hollywood (UNDP, 2004). Hali hii ni ushahidi kuwa nchi zinazoendelea hupokea sehemu kubwa ya utamaduni kutoka nje ya nchi zao. Ni jukumu letu kubuni mbinu na mikakati sahihi na kuhakikisha kuwa utamaduni wetu ulio bora unadumishwa kwa manufaa ya vizazi vijavyo na maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla.

Uharibifu wa mazingira: Matumizi makubwa ya rasilimali katika nchi zilizoendelea yamesababisha nchi maskini kuharibu mazingira. Kwa mfano karatasi, samaki, madini na bidhaa nyingine zinazotokana na maliasili zimevunwa kiasi kwamba zjnasababisha kuharibika kwa mazingira na

Baioanuai. Haya yanathibitishwa na ripoti ya UNDP ya mwaka 2004 inayobaini kuwa kati ya mwaka 1990 na 1997 uwekezaji katika uchimbaji wa madini barani Afrika uliongezeka maradufu.

Mada ya Elimu na Dunia ya Utandawazi imeletwa kwenye Mkutano huu iIi tuweze kujiandaa vizuri kukabiliana na utandawazi ambao hatuwezi kuukwepa. pamoja na mabadiliko mengi tunayotegemea lakini tuwe na msimamo. Pale ambapo tunaona kuwa misingi yetu kama taifa itabomolewa, tuchukue hatua za binafsi na za pamoja kuhakikisha kuwa maadili yetu na utamaduni wetu unadumishwa kwa vijana wetu na jumuiya nzima. Utandawazi usitufanye tuharibu yale mazuri tuliyo nayo.

NINI KIFANYIKE KUINUA ELIMU KATIKA UKOO WETU
Umoja wa Ukoo wa Kivenule una jukumu la kuona kuwa vijana wetu ni rasilimali na nguvu kazi inayotayarishwa kwa ajili ya ushindani katika dunia ya utandawazi. IIi kufikia azma hii ni lazima tuwe wabunifu na wepesi kukabiliana na mabadiliko ambayo yatajitokeza kila mara. Ujuzi na maarifa viwe ndiyo ngao yetu kubwa. Hatimaye matokeo halisi ya kazi yetu tutayaona tutakapofuatilia vijana wetu waliopitia kwenye mfumo wetu wa elimu na kuona kuwa wanao ujuzi na stadi za kuwawezesha kupata ajira katika dunia ya ushindani. Tutakuwa tumefanikiwa kama tutawakuta wanafunzi wetu wameajiriwa na ni watu wa kutegemewa ndani na nje ya nchi.

Mikakati ambayo inaandaliwa na Umoja wa Ukoo wa Kivenule katika kuinua elimu katika ukoo ni pamoja na kuanzisha mfuko ambao utachangiwa na wanaukoo ili kuwasaidia ndugu/wanaukoo ambao hawana uwezo wa kuwasomesha watoto. Pia, mfuko huo utasaidia kuwaendeleza ndugu/wanaukoo ambao wamefaulu na hawana uwezo wa kujisomesha. Mambo mengine muhimu kama sara za shule, vitabu, kalamu za risasi na wino, ada na vifaa vitatolewa na Umoja wa Ukoo wa Kivenule pindi pale hali ya mfuko itaboreka.

MAJADILIANO KWENYE MAKUNDI

KUNDI NA. 1
Nafasi ya Ukoo wa Kivenule katika Elimu
4.      Tumegundua kuwa nafasi ya ukoo wa Kivenule katika elimu ni mdogo au upo chini kwa sababu:
·        Nafasi za ajira katika maofisi makubwa serikalini ni mdogo.
·        Wanaukoo wachache wamepaa ajira katika mashirika makubwa (umma au binafsi) yanayozingatia kiwango elimu katika ajira.
5.      Kuwa na idadi ndogo ya wanaukoo waliofikia elimu ya kiwango cha juu mfano kidato cha 4, 6 mpaka vyuo vikuu.
6.      Wanaukoo kutojua umuhimu wa elimu.
Ili ukoo uwe na nafasi elimu tufanyaje?
·        Tujitahidi kusomesha watoto wetu hadi elimu ya juu.
·        Elimu ya ufundi pia ni muhimu ndani ya ukoo.
·        Tuunde kamati katika ukoo itkayoratibu sula zima la ukoo.
·        Kukusaya michango kuwasaidia waso na uwezo wa kusomesha.
·        Kuwasaidia kusoma watoto wa ukoo wasio na msaada.
·        Kuwatafutia watoto wafadhili ili kupata elimu.
·        Kubuni miradi ya kusaidia kukua kwa elimu

KUNDI NA. 2
Umuhimu wa Elimu
4.      Umuhimu wa elimu ni kuondoa umaskini ndani ya familia na jamii kwa ujumla.
5.      Mtu mwenye elimu anaweza kusaidia kuinua maisha ya mtu yeyote ambaye hana elimu katika familia.
6.      Mtu mwenye elimu anaweza kubuni mbinu yeyote itakayomwezesha kuyamudu maisha katika:
·        Kilimo
·        Biashara
·        Ufundi
·        Uongozi katika sekta mbalimbali nk.
5.      Umuhimu wa elimu ni kupanua upeo wa akili
·        Kimawazo
·        Kifikra
·        Kujiamini katika mambo yake unayoyapanga
·        Unakuwa na haiba
·        Kujulikana mbele ya watu

KUNDI NA. 3
Dunia ya Utawandazi
Vigezo: Elimu ili tuweze kwenda sambamba na wenzetu katika dunia ya Utandawazi. Utandawazi unafanya dunia kuwa kama kijiji.
·        Kupitia elimu watu wanawezeshwa kupambana katika mazuri na mabaya.
·        Wenye mwanga kidogo katika elimu wawasaidie wengine kuifafanua elimu ya Utandawazi kwa kubainisha faida na hasara zake.
Udhibiti
Mienendo ya watoto iangaliwe ili kuona kuwa haiharibiwi na Utandawazi. Kazi za watoto zifuatiliwe kwa karibuni na wazazi ili wasipate muda mwingi wa kuangalia mambo yasiyowahusu.
Elimu ya Utandawazi kwa walioipata na umri (wote tuna haki ya elimu, aliyeo na umri mkubwa.


KUNDI NA. 4
Nini kifanyike ili kuinua Elimu katika Ukoo
1.        Watoto wetu wapelekwe shule kwa wakati unaostahili (Awali, msingi, sekondari nk).
2.      Kudhibiti tabia za watoto wetu ili waweze kusoma vizuri (tabia mbaya).
3.      Wazazi wawe wapesi kutoa msaada unaohitajika kwa watoto (mahiaji ya msingi) kuwajenea mazingira mazuri ya elimu.
4.      Mtoto akifaulu kwenda sekondari mzazi atoe taarifa kwa wenzetu ili waone uwezekano wa kusaidia mtoto huyo aene shuleni.
5.      Ndugu wawe walinzi wa kila mtoto wa ndugu anayefanya mambo ya ajabu mitaani.
6.      Kubuni mfuko maalum wa elimu ili kusaidia mapema watoto wanaofaulu, lakini mtoto anaweza kufaulu na asichaguliwe.

MAJUMUISHO
1.        Katika dunia ya leo, mambo mengi yamemezwa na Utandawazi. Jambo la msingi la kuzingatia ni kupata Elimu. Wanaukoo wote wajitahidi kupata elimu pamoja na kujiendeleza hadi kupata elimu ya juu.
2.      Wanaukoo inabidi tuelekeze (tuwekeze) nguvu na rasilimali zetu katika Elimu.


MADA YA NNE
UKIMWI NDANI YA UKOO NA ATHARI ZAKE
UKIMWI ni nini?
UKIMWI ni Upungufu wa Kinga Mwilini mwa binadamu. Kwa lugha ya kigeni, Upungufu wa Kinga Mwilini hujulikana kama AIDS; yaani kirefu chake “Acquired Immuno Deficiency Syndrome. Na virusi vinavyoeneza ugonjwa wa UKIMWI kwa lugha ya kigeni hujulikana kama Human Infection Virus (HIV). Kwa lugha rahisi, neno UKIMWI linaweza kunyumbulishwa au kumegwa katika herufi za kujitegemea kama tatu hivi; yaani
U – inasimama badala ya Upungufu;
KI – inasimama badala ya Kinga; na
MWI – inasimama badala ya Mwili.

Mwili wa binadamu umeumbwa na seli za aina mbili; yaani
§        Seli Nyekundi za Damu (Red Blood Cells); na
§        Seli Nyeupe za Damu (White Blood Cells).

Kinga za mwili ambazo huulinda mwili wa binadamu kutokana na maambuki ya maradhi mbalimbali hutengenezwa kwenye Seli Nyeupe za Damu (White Blood Cells). Kwa lugha ya kigeni kinga hizi huitwa Antibodies.

Virusi vinavyoeneza ugonjwa wa UKIMWI hukaa muda mrefu sana mwilini mwa binadamu hadi kufikia hatua ya kuweza kutambulika. Mgonjwa aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI huweza kukao hadi miaka kumi bila kuleta athari yoyote. Mara nyingi, mgonjwa aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI anaweza kuishi kwa muda mrefu bila kupata madhara yoyote kutokana na afya ya awali ya mgonjwa, pamoja na aina za vyakula anavyokula.

Kwa wagonjwa ambao afya zao siyo madhubuti, madhara ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI huweza kujitokeza katika kipindi cha miezi sita (6) au pungufu ya hapo. Dalili mbalimbali ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI huweza kuanza kujitokeza  baada ya kipindi hicho cha miezi sita. Dalili hizo huwa ni pamoja na:
§        Kushambulia na magonjwa mbalimbali ya maambukizi mfano Kifua Kikuu (Tuberclosis);
§        Kupungukiwa na uzito mara kwa mara;
§        Kupata mkanda wa jeshi; na
§        Kutapika na kuharisha.

NJIA MBALIMBALI ZINAZOCHANGIA MAAMBUKIZI/KUENEA KWA VIRUSI VYA UKIMWI
Kuna haja kwa wanaukoo wa Ukoo wa Kivenule pamoja na jamii inayowazunguka kutilia umuhimu suala la kupata Elimu ya kujua jinsi maambukizi na kuenea kwa virusi vya UKIMWI kunavyotokea, hii itasaidia jamii yetu na wanaukoo/familia kwa ujumla kuzifahamu njia mbalimbali mbadala ambazo zinachangia kwa kiwango kikubwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Baadhi ya njia hizo zinazosaidia/changia maambukizi ya virusi vya UKIMWI ni pamoja na:
1.                    Kufanya ngoo holela na zisizo salama;
2.                  Kutochukua hatua madhubuti za kupima afya na kujitambua/kujijua kiafya kabla ya kufunga ndoa;
3.                  Kushambuliwa na magonjwa mbalimbali ya zinaa bila kwenda hospitalini kutibiwa;
4.                  Kuchangia katika matumizi ya vifaa vya kutogea mfano nyembe, sindano za mahospitalini, miswaki, mikasi ya mahospitalini na kushika vidondo vya mgonjwa aliyeambukizwa na virusi vya UKIMWI bila kutumia kinga (gloves);
5.                  Kuwekewa damu yenye virusi vya UKIMWI;
6.                  Mtoto kuambukizwa virusi vya ugonjwa wa UKIMWI toka kwa mama yake wakati wa kujifungua;
7.                  Mama Mjamzito kutochukua hatua madhubuti/tahadhari ya kupima afya yake ili kujua kama ana maambukizo ya virusi vya UKIMWI au hapana;
8.                  Kurithi wajane;
9.                  Wanaukoo/familia kutokuwa waaminifu katika ndoa zao; na
10.               Mama aliyeathirika na virusi vya UKIMWI kumnyonyesha mtoto ambaye hajaathirika na virusi vya UKIMWI.

NJIA MBADALA ZA KUJILINDA NA MAAMBUKIZI
WAnaukoo/familia baada ya kuzifahamu njia mbalimbali mbadala zinazochangia maambukizi ya virusi vya UKIMWI; sasa wajibu wao mkubwa ni kuielimisha jamii yao kuzitambua njia kadhaa zinazosaidia kujilinda na maambukizi ya virusi vinavyoleta upungufu wa kingi mwilini yaani UKIMWI. Hatua hizo madhubuti ambazo ukoo na jamii yetu kwa ujumla inapaswa kuzichukua ni kutoa elimu kuhusu umuhimu wa:
1.                    Kupima afya na kujitambua kama umeambukizwa virusi vya UKIMWI toka katika vituo mbalimbali vya afya mfano ANGAZA na mahospitalini;
2.                  Kufanya ngono salama kwa kutumia njia mbadala zinazoshauriwa na wataalamu au kuacha kabisa mpaka muda muafaka utakapofika;
3.                  Waathirika wa virusi vya UKIMWI kutojihusisha katika ngono au hali yoyote ambayo inaweza kuchangia maambukizi ya virusi vya UKIMWI:
4.                  Wanaukoo/familia kuwa waaminifu katika ndoa zao;
5.                  Kwenda hospitali kutibu dalili zozote za maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Magonjwa ya zinaa huchangia sana katika maambukizi ya virusi vya UKIMWI;
6.                  Mama Wajawazito kupima afya zao kabla ya kujifungua ili kuwanusuru watoto wanaozliwa wasiathirike na virusi vya UKIMWI kama mama hao watakuwa wameambukizwa na virusi vya UKIMWI;
7.                  Mama aliyeathirika na virusi vya UKIMWI, kutomnyonyesha mwanae ili kupunguza uwezekano wa kumwambukiza mtoto kama atathibitika kuwa ameambukizwa;
8.                  kuacha kurithi wajane; na
9.                  Kuacha mila potofu zinazopotosha mfano kupiga ramli.
JUKUMU LA UKOO/FAMILIA KUKABILIANA NA JANGA LA UKIMWI
Jukumu la Ukoo/Familia katika kukabiliana na virusi vya maambukizi vinavyoeneza ugonjwa wa UKIMWI ni pamoja na:
1.                    Kutoa na kueneza elimu ihusuyo maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa watoto na vijana wenye ufahamu na uelewa na hali hali kadhalik kwa watu wazima;
2.                  Kuwaelimisha wanaukoo/familia kuzifahamu njia mbadala za kujikina na kujilinda a maambukizi ya virusi vya UKIMWI;
3.                  Kuwaelimisha wanaukoo/familia kuzifahamu njia mbalimbali zinazochangia maambukizi na kuenea kwa virusi vya UKIMWI;
4.                  Kuwaelimisha wanaukoo/familia kujenga tabia ya kupenda kupima afya zao na kujua kama wameambukizwa virusi vya UKIMWI au hapana;
5.                  Kuwaelimisha wanaukoo/familia kuwa waaminifu katika ndoa zao ili kupunguza hatari ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI; na
6.                  Kuwaelimisha wanaukoo/familia kuishi katika misingi ya Dini na Maadili mema.

Pia muhimu sana kukatolewa Elimu ya kujua jinsi maambukizi na kuenea kwa virusi vya UKIMWI kunavyotokea, hii itasaidia jamii yetu na wanaukoo/familia kwa ujumla kuzifahamu jia mbalimbali mbadala ambazo zinachangia kwa kiwango kikubwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Baadhi ya njia hizo zinazosaidia/changia maambukizi ya virusi vya UKIMWI ni pamoja na:
1.                    Kufanya ngoo holela na zisizo salama;
2.                  Kutochuku hatua madhubuti za kupima afya na kujitambua/kujijua kiafya kabla ya kufunga ndoa;
3.                  Kushambuliwa na magonjwa mbalimbali ya zinaa bila kwenda hospitalini kutibiwa;
4.                  Kuchangia katika matumizi ya vifaa vya kutogea mfano nyembe, sindano za mahospitalini, miswaki, mikasi ya mahospitalini na kushika vidondo vya mgonjwa aliyeambukizwa na virusi vya UKIMWI bila kutumia kinga (gloves);
5.                  Kuwekewa damu yenye virusi vya UKIMWI;
6.                  Mtoto kuambukizwa virusi vya ugonjwa wa UKIMWI toka kwa mama yake wakati wa kujifungua;
7.                  Mama Mjamzito kutochukua hatua madhubuti/tahadhari ya kupima afya yake ili kujua kama ana maambukizo ya virusi vya UKIMWI au hapana;
8.                  Kurithi wajane;
9.                  Wanaukoo/familia kutokuwa waaminifu katika ndoa zao; na
10.               Mama aliyeathirika na virusi vya UKIMWI kumnyonyesha mtoto ambaye hajaathirika na virusi vya UKIMWI.

WAnaukoo/familia baada ya kuzifahamu njia mbalimbali mbadala zinazochangia maambukizi ya virusi vya UKIMWI; sasa wajibu wao mkubwa ni kuielimisha jamii yao kuzitambua njia kadhaa zinazosaidia kujilinda na maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Hatua hizo madhubuti ambazo ukoo na jaii yetu kwa ujumla inapaswa kuzichukua ni kutoa elimu kuhusu umuhimu wa:
1.                    Kupima afya na kujitambua kama umeambukizwa virusi vya UKIMWI toka katika vituo mbalimbali vya afya mfano ANGAZA na mahospitalini;
2.                  Kufanya ngono salama kwa kutumia njia mbadala zinazoshauriwa na wataalamu au kuacha kabisa mpaka muda muafaka utakapofika;
3.                  Waathirika wa virusi vya UKIMWI kutojihusisha katika ngono au hali yoyote ambayo inaweza kuchangia maambukizi ya virusi vya UKIMWI:
4.                  Wanaukoo/familia kuwa waaminifu katika ndoa zao;
5.                  Kwenda hospitali kutibu dalili zozote za maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Magonjwa ya zinaa huchangia sana katika maambukizi ya virusi vya UKIMWI;
6.                  Mama Wajawazito kupima afya zao kabla ya kujifungua ili kuwanusuru watoto wanaozliwa wasiathirike na virusi vya UKIMWI kama mama hao watakuwa wameambukizwa na virusi vya UKIMWI;
7.                  Mama aliyeathirika na virusi vya UKIMWI, kutomnyonyesha mwanae ili kupunguza uwezekano wa kumwambukiza mtoto kama atathibitika kuwa ameambukizwa;
8.                  kuacha kurithi wajane; na
9.                  Kuacha mila potofu zinazopotosha mfano kupiga ramli.

Wanaukoo/familia wana jukuu pia la kuwahudumia wale ambao tayari wameambukizwa na virusi vya UKIMWI ili waendelee kujihusisha na shughuli za uzalishaji mali na kupunguza utegemezi. Baadhi ya majukuu hayo ya wanaukoo/familia ni pamoja na:
1.                    Kuwapenda na kuwasaidia wagonjwa wote waliathirika na virusi vya UKIMWI;
2.                  Kutowanyanyapa wagonjwa walioathirika na virusi vya UKIMWI;
3.                  Kuchukua hatua madhubuti za kuwasaidia waathirika wa virusi vya UKIMWI kupata dawa za kurefusha maisha. Mfano wa dawa hizo ni RVA,
4.                  Kuwathamini wagonjwa waliambukizwa na virusi vya UKIMWI; na
5.                  Kuwasaidia wagonjwa waliambukizwa na virusi vya UKIMWI kupata vyakula vya kuujenga na kuulinda mwili.

Kuna Hamasa, Mbinu au Falsafa mbalimbali ambazo wanaukoo/familia wanaweza kuzitumia katika kupambana na gonjwa hili. Hii ni pamoja na kuzingatia matumizi ya J&; yaani waone umuhimu wa:
1.          KUJITAMBUA;
2.         KUJIHESHIMU;
3.         KUJIPENDA;
4.         KUJITHAMINI;
5.         KUJIAMINI;
6.         KUJILINDA; na
7.         KUJIDHIBITI.

Medani kadhaa ambazo wanaukoo/familia wanaweza kuzitumia kuepukana au kuwa mbali na maambukizi ya virusi vya UKIMWI ni pamoja na:
1.          Kusema hapana (kukataa) ushawishi wa aina yoyote;
2.         Kuongea na kutokukubali kuburuzwa;
3.         Kuondoa woga na kupima afya yako;
4.         Kupunguza matumizi ya vileo au kuacha kabisa;
5.         Wanaukoo/familia kuwa waaminifu katika ndoa zao;
6.         Wanaukoo/familia kujiepusha na vishawishi;
7.         Wanaukoo/familia kuulinda ujana na utu uzima wao;
8.         Kujibidisha katika kazi na hivyo kupunguza fikra zisizo za msingi; na
9.         Kusoma vitabu na magazeti baada ya kazi.
Kwa kufanya hivyo, yote hayo yaliyopendekezwa katika makala hii, nafasi hii, nafasi ya jaii hii ya ukoo wa KIVENULE itakuwa imepiga hatua muhimu katika kukabiliana na kupambana na maambukizi ya virusi vinavyoeneza gonjwa la UKIMWI.

MAJADILIANO KWENYE MAKUNDI

KUNDI NA. 1
UKIMWI ni nini?
1.        Maana: Upungufu wa Kinga Mwilini
2.      Upungufu wa kinga unasababisha kukosekana au kuuawawa kwa chembechembe nyeupe za damu (white blood cells) ambazo husaidia kuzuia maambukizo ya magonjwa mbalimbali mwilini
3.      Kinga hiyo inapopungua mwilini husababisha mtu kuugua magonjwa mbalimbali mfano malaria, TB Kifua Kikuu, Kuharisha na kadhalika.

KUNDI NA. 2
Namna gani UKIMWI unavyoweza kuenea
1.        Kurithi wajane
2.      Ngono uzembe
3.      Ulevi wa kupindukia
4.      Kutokuwa waaminifu katika ndoa
5.      Kukosa maadili ya dini
6.      Michilizi ya damu
7.      Kushirikiana katika matumizi ya sindano na vifaa vya kutibia visivyo salama.
8.      Kuongezewa damu yenye virusi.
9.      Kwa njia ya kunyonyesha.
10.   Wakati wa kujifungua
11.     Kwa njia ya kushirikiana miswaki.

KUNDI NA. 3
Njia Mbadala za Kujilinda na Maambukizi ya UKIMWI
1.        Kuanzisha shughuli mbalimbali.
2.      Kupunguza ulevi wa kupindukia mfano: mtu alisema kunywa Pombe si starehe ila kwenye Pombe kun starehe.
3.      Wanandoa kuwa waaminifu.
4.      Kuepukana na utumiaji wa vifaa visivyo salama.
5.      Kufuata Maadili ya Mungu.
6.      Kuwa wazi katika mazungumzo yanayohusu UKIMWI.
7.      Kupima afya.
8.      Kutumia zana za kujilinda na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.
9.      Kukimbilia mijini.
10.   Kutumia Madawa ya Kulevya.
11.     Wazazi na wakubwa kuwa wazi kwa watoto wao.
12.    Kuepuka vishawishi mbalimbali.
13.    Kurithi wajane au kurithiwa.
14.   Kuweka wazi mtu akifariki.

KUNDI NA. 4
Jukumu la Ukoo/Familia Kukabiliana na Janga la UKIMWI
1.        Elimu itolewe kwa wana ndugu wote juu ya UKIMWI.
2.      Wanandoa kuwa waaminifu katika ndoa zao.
3.      Wanandugu kujihusisha katika kazi na kushiriki michezo mbalimbali.
4.      Kuhimiza matumizi ya mipira ya plastiki (gloves) katika uoshaji wa maiti, nguo na kadhalika.
5.      Kuwatimizia watoto wanaosoma mahitaji yao mfano fedha nk.
6.      Kutozalia majumbani (Wakunga)
7.      Ukeketaji ukomeshwe
8.      Kubusu maiti.
9.      Kuficha maradhi.
MADA YA TANO
DINI KATIKA UKOO
UTANGULIZI
Tuna msemo unaotukumbusha hivi, hakuna mtu anayependa kuishi peke yake, au aliye kama kisiwa na hakika kweli. Hatuishi wala hatuwezi kuishi hivyo, yaani kuishi watu pekee, watu waliotengwa na wenzao kama vile kisiwa kilichotengwa na nchi kavu.

Twawahitji wengine wengi ili tujisikie tumeungana na watu tumkuwa kitu kimoj na wanadau wenzetu.

Tunaangalia maisha yetu ya kila siku tunaona mifano mingi. Nikiona furaha nahitaji kushirikiana na mtu mwingine. Tukipatwa na misib, magonjwa tunahitji kutulizwa, kufarijiwa na kusaidiwa na wengine.

Tena kuna vifungo vinavyotuunganisha vyaweza kuwa ni urafiki, ujamaa, ujirani uhusiano wa kikazi na kadhalika. Kati yangu na watu wengine.

Pamoja na vifungo hivyo tulivyovitaja vinavyotuunganisha katika maisha ya kawaida, kuna kifungo kikuu ambacho kinaweza kutuunganisha au kuniunganisha mimi, na hicho kifungo si mwingine ila ni Mungu. Mungu ndiye kifungo pekee kinachotulte uhusiano wa kawaida uliopo kati ya Mungu na Mimi au wewe, ndio tunachokiita Dini.

NINI MAANA YA DINI?
Neno hili Dini ni neno ambalo pengine umelisikia mara nyingi, na pengine hatuelewi maana yake lakini linaweza kuwa na maana nyingi sana. Endapo ukimwuliza ndugu yeyote maana ya dini, natumaini utapata majibu mengi sana na yote yatakuwa yanaelezea maana halisi ya dini.

Dini ni Imani ya Kuamini kitu au jambo fulani kuwa linaweza kumsaidia binadamu kupata mahitaji yake. Ndani ya Dini kuna kitu ambacho huwa ni nguzo kwa yule anayeamua kuwa katika dini fulani. Nguzo hiyo ni Imani. Imani inampelekea binadamu kuweza kujitengenezea utaratibu wa kutolea heshima, kufanya ibada ikibidi hata kuitolea Sadaka.

Maana hii ya pili; Dini ina maana hasa ya kufungamana na kuhusiana. Kwa maneno mengine Dini ni uhusiano, urafiki, ushirikiano uliopo Kati ya Mungu na Binadamu. Maana hii ya pili inamweleza hasa Mungu Mmoja Muumba Mbingu na Nchi.

Maana hii ya pili inaonyesha utofauti wa maana ya kwanza ambayo inaonyesha inaweza kuhusisha Miungu zaidi ya mmoja. Maana ya pili ya dini ndiyo inayoaminiwa na watu wengi au mamilioni ya watu katika ulimwengu huu.

Msingi mkuu wa Dini ni Imani. Kila mtu ana dini. Mtu mwingine anaamini kukaa peke yake na hiyo ndiyo  dini yake. Imani ni tabia ya ndani aliyonayo mtu. Imani ya ndani huzaa tabia. Tabia huonekana nje. Dhehebu ni muunganiko wa watu wenye tabia. Kama ukoo tunaweza kutengeneza dhehebu letu.

Dini ilianza lini
Hili linaweza kuwa ni swali karibu kwa mmoja wetu kuwa Dini ilianza lini? Kwa kweli Dini imeanza zama za kale kabisa, binadamu alipoanza kuwa binadamu.

Watu wa Sayansi walichunguza mianzo ya binadamu, wanatuambia kwamba binadamu alipovumbua ulimwengu na kujitambua mwenyewe, pale pale alitamua pia mtu aliye mkubwa kuliko binadamu, na huyo si mwingine ila ni Mungu.

Aina ya Miungu
Kabla ya Mungu hajajionyesha, kuna Miungu ambayo watu wa kale waliiabudu na kuitumikia Miungu hiyo ni ile iliyotokana na vitu vilivyoumbwa na Mungu navyo ni:
ANU               Mungu Mbingu
EA                   Mungu Maji
ENIL               Mungu Upepo
SHAMASH     Mungua Juan a Dunia na kadhalika

Hii ndiyo Miungu waliyoiabudu hapo kale lakini haikuwa Miungu ya Kweli.

Dini za Kiulimwengu
Baada ya kuona Miungu waliyoiabudu hapo kale imepitwa na wakati, hapo baadaye watu walianzisha Dini za Kiulimwengu ambazo zilianza huku Bara la ASIA katika nchi za China na India. Mawazo hayo yaliyojitokeza kabla Mungu hajajifunua au kujionyesha kuanzisha dini yake Mungu. Mawazo yao juu ya kumtafuta Mungu yalikuwa mazuri isipokuwa namna zao zilikuwa kinyume na Mungu.

Dini Zenyewe za Kiulimwengu
Dini ya Kihindu ilianza mwaka 2500 KK. Imani ya Dini hiyo waliamini uwepo wa Mungu katika kila kiumbe kilicho hai mfano……. Hivyo kutokana na Imani hiyo walithamini sana Uhai wa kila Kiumbe.

Dini ni KIBUDHA hii ilianzishwa mwaka 560 KK. Imani yao waliamini kuwa maisha ya binadamu ni mateso, mateso kutokana na kutamani mambo yasiyo kidhi mahitaji ya Roho.

Hivyo walijitahidi kuepuka mates ohayo kwa kutimiza maneno nan. Maoni halisi – misemo halisi  - mndo mzuri wa maisha – amaa nzuri – na kadhalika. Hivyo walijitahidi sana kuongea na kutenda vizuri kila wakati.

Dini ya Mungu
Baada ya dini hizo za kiulimwengu Mungu saa anajionyesha au kujifunua, japo hakujifunu katika kila taifa. Alijifunua katika taifa la Israel kwa KUMWITA IBRAHIMU. MUNGU alijionyesha kwa mpango huo ili watu wamtambue jinsi alivyo, watu waone kuwa yeye ni Mungu wa namna gani mwa 12 – 13.

Mungu alijitambulisha kwa Ibrahi katika Taifa la Israel kwa msimamo huu kuwa
MUNGU NI MOJA NA HAKUNA MWINGINE; ila ni yeye tu, nah ii ndiyo imani kwa Israel kuwa Mungu I mmoja tu.

Msingi huo wa Imani kwa Israel uliandikwa katika maandiko ya Kiyahudi na iliitwa kifungu cha Sikiliza Ee Israel. Hili ilikuwa SALA ya Asubuhi kila siku na ni muhimu waifahamu na kuisali.

SALA YENYEWE: Sikiliza Ee Israel Bwana Mungu ni mmoja. Nawe umpende Bwana Mungu wako kwa moyo wake wote na kwa Roho yako yote, na kwa Nguvu zako zote… Kumb 6:4 – 5, 13 – 14.

Dini Kubwa zinazofuata Mpango wa Mungu Mmoja
1. Dini ya Kikristo
Dini hii Asili yake na Mpango wake ni Mungu Mmoja Muumba Mbingu na Nchi. Tukianzia na Ibrahim pamoja na historia nzima ya Ukoo wa Yesu na Kanisa lake yaani Mitume.

Dini hii ya Kikristo ina madhehebu yake ambayo yanamwamini MUNGU mmoja kwa njia ya Yesu Kristo. Na kila anayemwamini MUNGU hana budi kufuat Mwongozo wake kwa kushika NENO LA MUNGU kulifuaa na kuwa na maisha nao, kwa kushika kiaminifu Amri 10 za Mungu na sheria zake. Pamoja na hayo kumheshimu, kumwabudu, kumwomba, kumpenda katika siku zote za maisha.

2. Dini ya Kiislamu
Hii pia inamwamini Mungu Mmoja ALLAH, na mjumbe wake ni Mtume MOHAMED SALLALEI WASALAM Dini hii pia ina madhehebu yake. Dini hii inahimiza kila Mwislamu anayemwamini MUNGU (ALLAH) anahimizwa kuisoma KORAN au MSAHAFU na kushika maagizo ya Mungu (ALLAH) kutoka kwa mjumbe wake aliyefunuliwa Mtume MOHAMED, pamoja na kufuata Nguzo Tano (5) za Uislamu.

Dini hizi mbili na madhehebu yake zinazomwamini Mungu Mmoja, zinawahimiza waamini wake pamoja na watu wote kuona umuhimu wa kujiunga na Dini ili kuona Upendo wa MUNGU (ALLAH) kwani kujiunga katika Dini zilizo za kweli kutawafanya watu waishi kwa Amani na Upendo hapa. Duniani na huko Mbinguni aliko MWENYEZI MUNGU.

UMUHIMU WA KUWA NA IMANI
Umuhimu wa kuwa na Imani (Dini) unajengeka katika maeneo mbalimbali. Kuwa na Imani kuna faida zake ambazo mshika Imani hufaidi, hii ni pamoja na:
1.        Dini huondoa tofauti zetu.
2.      Dini huondoa chuki, fitina na unafiki.
3.      Dini hutoa elimu ya ufahamu wa mambo mengi.
4.      Dini hujenga tabia ya kusaidiana, kuondoa chuki, kuondo tofauti.
5.      Dini hujenga uhusiano mkubwa baina ya Mungu na Binadamu.
6.      Dini hupunguza ushirikina.
7.      Dini hupunguza woga wa kuogopa mtu kutokana na uwezo, uchawi na kadhalika.
8.      Kuishi kwa imani hata kama una matatizo mfano kufiwa; humfanya aamini kuwa Mungu ndiye mweza.
9.      Dini humfanya mtu kuwa na mtazamo baadaye baada ya kifo hivyo anakuwa Mnyenyekevu.


MAADILI NA DINI
Dini, Imani, Dhehebu na Maadili huenda pamoja. Dini ni Imani. Msingi wa Dini ni Imani. Kila mtu ana Dini. Mtu anayeamini kukaa peke ndiyo dini yake. Imani ni tabia ya ndani aliyonayo mtu. Imani ya ndani huzaa tabia. Tabia huonekana nje. Dhehebu ni muunganiko wa watu wenye tabia ya aina mmoja. Kama ukoo tutengeneze dhehebu letu ambalo sisi kama wafuasi wake tutakuwa na matarajio fulani. Liwe ni dhehebu la kuwajali waumini wake, dhehebu lenye kuheshimu na dhehebu lenye kujengea uwezo wa kiuchumi, kiakili na kiafya.

Maadili nayo hujengwa kwa msingi wa imani na dini. Watu walio katika imani hujijengea maadili fulani ambayo huweza kuwatofautisha na jamii nyingine. Kwa mfano maadili fulani ambayo hufuatwa na waumini wa dini fulani, huwafanya watembee bila ya kuvaa viatu, wale mlo kwa siku, kujitolea muda wao wote kuwatumikia watu wengine, kukesha usiku kucha kanisani wakiomba na kadhalika. Haya huwa ni maadili yanayoridhiwa na kukubaliwa na kundi fulani la watu au jamii, wayafuate.

Maadili ni miiko ambayo huweza kufuatwa na jamii fulani ili kuweza kutimiza malengo yao. Kwa mfano katika makanisa mbalimbali ya Kikristo kuna Amri za Mungu au Kanisa ambazo tunaweza kuzifananisha na Maadili katika maisha yetu ya kila siku. Kwa mfano katika Kanisa Katoliki kuna Amri Kumi za Mungu, ambapo kina mwanakatoliki anawajibu wa kuzitimiza. Amri hizo tukizileta katika maisha yetu ya kawaida ya kibinadamu tunaweza kuziita ni maadili, kwa sababu zipinga tabia zile ambazo hazikubaliki na jamii zetu. Kwa mfano baadhi ya Amri za Mungu zinasema yafuatayo : Usiibe, Usiue, Usiseme Uwongo, Usitamani Mali ya Mtu, Usimtamani Mwanamke Asiye Mke wako, Usizini, Umpende Jirani Yako kama unavyojipenda na kadhalika.

Katika maisha yetu ya kila siku Amri hizo za Mungu ni mfano wa Maadili Mema ambayo kila mtu au ndugu analazimika kuyafuata ili kuweza kukubalika katika  jamii yake. Kwa mfano tabia za uongo, uzinzi na uasherati, wivu mbaya, tamaa mbaya, wizi, kuua ni baadhi ya tabia mbaya ambazo hazikubaliki kabisa na ni kinyume cha maadili. Kwa hiyo Dini na Maadili vina mahusiano makubwa na ya muhimu sana. Kama jamii, tuna jukumu la kuhakikisha kuwa wanaukoo wanakuwa waumini wazuri katika Dini zao, kwani kwa kufanya hivyo tutajenga jamii yenye maadili mema.

UKOO ULIOJENGEKA KATIKA MISINGI YA DINI
1.        Ukoo uliojengeka katika misingi ya dini unakuwa hauna ubinafsi.
2.      Ukoo uliojengeka katika dini utakuwa ni ukoo unajaliana katika matatizo kutokana na imani walionayo kutokana na Dini zao.
3.      Watu Kuheshimiana: Dini inafundisha mambo mema; Kwa hiyo ukoo utakapokuwa na mwamko wa dini hakutakuwa na matatizo ya kudharauliana.
4.      Kuheshimika kwa Ukoo: Kwa kuwa utakuwa na sifa nzuri basi hata koo nyingine zitapata hamasa ya kujiunga na ukoo.
5.      Ukoo unapunguza imani potofu : Kwa mfano kama wanaukoo watafuata misingi ya dini zao, hawawezi kuwa na imani za kishirikiano au kufikiria kwenda kwa waganga wa jadi ili kutatua matatizo yao.


MAJADILIANO KWENYE MAKUNDI

KUNDI NA. 1
Maana ya Dini
Ni Imani aliyonayo mtu juu ya jambo fulani. Pia ni Msingi fulani ambao mwanadamu anaufuata.

KUNDI NA. 2
Umuhimu wa Kuwa na Imani
1.        Umuhimu wa Kuwa na Imani ni pamoja na kutoogopa kitu chochote kwa kuwa una Imani.
2.      Utakuwa na imani ya jambo lolote lile.
3.      Kila jambo utakalolifanya utakuwa na Imani nalo.
4.      Ukiwa na Imai utajulikana na mtu yeyote.
5.      Imani itajenga mahusiano ndani ya familia, ndugu, jamaa, majirani, marafiki nk.

KUNDI NA. 3
Maadili na Dini
1.        Dini ianzie kwenye familia
2.      Familia ikia na maadili mema ya Dini itakuwa sambamba.
3.      Wazazi wawe mstari wa mbele kuelimisha familia
4.      Wazazi wawe mfano kwa familia
5.      Wazazi wawe wasikivu (kuwasikiliza) watoto wanapohitaji kusikilizwa.

KUNDI NA. 4
Ukoo Uliojengeka katika Misingi ya Dini
6.      Ubinafsi: Ukoo uliojengeka katika misingi ya dini unakuwa hauna ubinafsi.
7.      Ukoo uliojengeka katika dini utakuwa ni ukoo utakaokuwa unajaliana katika matatizo kutokana na imani walionayo kutokana na Dini.
8.      Watu Kuheshimiana: Dini inafundisha mambo mema; Kwa hiyo ukoo utakapokuwa na mwamko wa dini hakutakuwa na matatizo ya kudharauliana.
9.      Kuheshimika kwa Ukoo: Kwa kuwa utakuwa na sifa nzuri basi hata koo nyingine zitapata hamasa ya kujiunga na ukoo.

XII: RATIBA YA MKUTANO MKUU WA KWANZA WA UKOO WA KIVENULE,

        DESEMBA 17 – 18, 2005


Siku ya Kwanza ya Mkutano Mkuu wa Ukoo wa KIVENULE

Tarehe
17 Des. 2005 Muda
Shughuli/Jukumu
Wahusika
12:00–12:45
Wageni Wote Kuamka na Kufanya Maandalizi ya Kuingia kwenye Mkutano

Wote

12:45–1:45
Kupata Kifungua Kinywa
Wote
1:45 – 2:45
Kuwasili Mkutanoni na Kujisajili
Wote
2:45 – 3:15
Ufunguzi wa Mkutano na Mgeni Rasmi
Mgeni Rasmi
3:15 – 4:00
Utambulisho baina wa wana Ndugu
Wote
4:00 – 4:45
Pumziko la Chai / Kahawa/Maji
Wote
4:45 – 5:30

Mada ya Kwanza: CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO

1.       Christian J. Kivenule

2.       Augustino Kivenule

5:30 – 6:00
Majadiliano katika Makundi
Makundi 4
6:00 – 6:20
Murejesho na Majumuisho
Vikundi na Mwezeshaji
6:30 – 8:00
CHAKULA CHA MCHANA
Wote
8:00 – 8:45
Mada ya Pili: MAHUSIANO BAINA YA NDUGU NDANI YA UKOO WA KIVENULE
1.       John S. Kivenule
2.       Ignas P. Kivenule
3.       Stephan Mhapa
8:45 – 9:15
Majadiliano katika Makundi
Makundi 4
9:15 – 9:45
Murejesho na Majumuisho
Vikundi na Mwezeshaji
9:45– 10:45

Pumziko la Chai/Kahawa/Maji

Wote
10:45-1:30 Usiku
Mapumziko Marefu (Kusalimiana na Kufahamiana zaidi)
Ndugu na Wageni Wote
1:30 – 2:30
Chakula cha Usiku na Vinjwaji
Ndugu Wote
2:30 – 6:30
Burudani (Muziki wa Kisasa na Ngoma za Asili)
Wote

Siku ya Pili ya Mkutano Mkuu wa Ukoo wa KIVENULE

Tarehe
18 Des. 2005 Muda
Shughuli/Jukumu
Wahusika
12:00– 12:45
Kuamuka na Kufanya Maandalizi ya Mkutano

Wote

12:45 – 1:45
Kifungua Kinywa
Wote
1:45 – 2:15
Kuwasili Mkutanoni na Kujisajili

Ndugu wote

2:15 – 2:45
Mada Ya Tatu: ELIMU NA MUSTAKABILI WA UKOO WA KIVENULE

1.       Christian J. Kivenule

2.      Donat         Mhapa
2:45 – 3:15
Majadiliano kwenye Makundi
Makundi 4
3:15 – 3:45
Murejesho na Majumuisho
Vikundi na Mwezeshaji
3:45 – 4:30
Pumziko la Chai/Kahawa/Maji
Wote
4:30 – 5:00

Mada ya Nne: UKIMWI NDANI YA UKOO NA ATHARI ZAKE

1.       Maria Milimo
2.      Adam A. Kivenule
5:00 – 5:30

Majadiliano kwenye Makundi

Makundi 4

5:30 – 6:00

Murejesho na Majumuisho

Vikundi na Mwezeshaji

6:00 – 7:15
CHAKULA CHA MCHANA

Wote

7:15 – 7:45

Mada ya Tano: DINI KATIKA UKOO

1.       Jovin D. Kivenule

2.       Stephan Mhapa

3.       George Kivenule

7:45 – 8:15

Majadiliano kwenye Makundi

Makundi 4

8:15 – 8:45

Murejesho na Majumuisho

Vikundi na Mwezeshaji

8:45 – 9:45

Majumuisho:

1.       Yote Yaliyojitokeza

2.      Matarajio

3.      Tarehe ya Mkutano Mwingine

Mwezeshaji

9:45 – 10:15
Shukurani toka kwa Ndugu Mbalimbali
Mgeni Rasmi, Ndugu
10:15–11:00
KUCHAGUA VIONGOZI WA KUUNDA KAMATI YA UKOO
Ndugu Wote
11:00
Kufunga Mkutano
Mgeni Rasmi


XIII: KAMATI ILIYORATIBU SHUGHULI KATIKA MKUTANO MKUU WA
         KWANZA WA UKOO WA KIVENULE

A:        Wawezeshaji Wa Mada Mbalimbali
1.          Christian        J.          Kivenule
2.         Augustino                  Kivenule
3.         Stephan                     Mhapa
4.         Maria                         Milimo
5.         Adam             A.        Kivenule
6.         Jovin               D.        Kivenule
7.         George           S.         Kivenule
8.         John                S.         Kivenule
9.         Ignas               P.        Kivenule

B:        Wawezeshaji Wasaidizi
1.          Lesandu                     Mhapa
2.         Adam             A.        Kivenule
3.         Faustin           S.         Kivenule
4.         Christian        J.          Kivenule
5.         Donath                      Mhapa

C:        Msimamizi wa Vyombo vya Matangazo
1.          Lesandu                     Mhapa
2.         Justo                           Chavala

D:       Muda wa Kuwasilisha Mada
·        Muda wa dakika 45 ulitumika kuwasilisha Mada moja.
·        Majadiliano katika Makundi yalifanyika kwa dakika kumi; na
·        Uwasilishaji wa hoja kutoka katika makundi ulitumia dakika tano hadi nane.
Kuwasilisha Mada[dak.45]; Majadiliano [dak. 10]; Kuwasilisha na Majumuisho [dak.10]

E:        Uteuzi wa Makundi ya Majadiliano
[Namna gani makundi yalivyokuwa yanaundwa]
Makundi Manne ya Majadiliano yaliundwa kwa kila Mada iliyowasilishwa kwenye Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Uundwaji wa Makundi ya Majadiliano ulifanyika kwa kila mshiriki kuhesabu namba, yaani moja mpaka nne na kisha kila mshiriki kukariri namba yake. Baadaye washiriki wote waliohesabu namba moja walikaa kwenye kundi la kwanza, namba mbili kundi la pili, namba tatu kundi la tatu na kisha namba nne kundi nne.

Kila mada iliyowasilishwa kwenye Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ilikuwa na dondoo nne. Hivyo makundi yaligawanywa kutokana na idadi ya hizo dondoo nne.

XIV: TATHMINI YA MKUTANO MKUU WA KWANZA WA UKOO WA KIVENULE
Wanaukoo walizishukuru na kuzipongeza Kamati zote za maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule kwa kufanya kazi nzuri. Walibainisha furaha yao kwa kusema haya yafuatayo:
1.        Tunawashukuru Wawezeshaji kwa kujiandaa barabara na pia Waratibu wa shughuli hii wameiratibu vizuri sana.
·        Mpangilio wa Ratiba ulikuwa ni mzuri sana.
·        Washiriki wamefanikiwa kuchangia vema kutokana na mpangilio mzuri wa Mada na Wawezeshaji.
2.      Mwitikio wa wanandugu na wanaukoo umetia moyo sana na hivyo kupiga hatua mbele katika Mikutano mingine ijayo.
3.      Shukrani ziwaendelee wale wote waliochangia gharama za kuweza kufanikisha Mkutano huu. Tunawashukuru pia wale ambao hawakuchangia gharama lakini kuja kwao kwenye kikao kumetia hamasa kubwa.
4.      Tunawashukuru wale wote waliotusaidia kuandaa chakula (katika mapishi)…. Na Kamati za maandalizi wa ujumla.
5.      Tunaushukuru uongozi wa kijiji cha Kidamali kwa kuuthamini mkutano wetu; tumeshuhudia Mwenyekiti tukiwa naye siku zote mbili za Mkutano huu.
6.      Tunamshukuru mwenye nyumba (Bwana Sanga) kwa kutukodisha ukumbi kwani umetusaidia sana.

XV: MAPENDEKEZO/MAONI YALIYOJITOKEZA WAKATI WA MKUTANO
       MKUU WA UKOO

1.        Iundwe Kamati Kuu ya Ukoo, Kamati Ndogo na Uongozi wa Ukoo na pia wachaguliwe Wawakilishi kulingana na maeneo husika mfano Magubike, Kidamali, Nyamahana, Nzihi na kadhalika. Wawakilishi watakaochaguliwa watakuwa wanafanya mawasiliano na Uongozi wa toka sehemu zao husika. Watatoa taarifa za matatizo au furaha, watatekeleza maagizo toka kwa Viongozi wa Ukoo na Kamati Kuu ya Ukoo. Lakuzingatia: Wanaukoo wawachague wanaukoo wenye mwelekeo na moyo wa kujituma na kujitolea na wenye uchungu na maendeleo ya ukoo.  
2.      Iundwe Kamati ya Ukoo (Yenye Uwakilishi wa Wajumbe) toka sehemu mbalimbali itakayoratibu shughuli kadhaa za ukoo mfano Uanzishwaji wa Mfuko wa kuchangia kutatua matatizo ya wanandugu kama vile ugonjwa, elimu na vifo. Pia inapendekezwa kuwa wanaukoo wanaoishi vijijini wachangie shilingi 500/= kila mwezi; lakini kila mwanaukoo awe huru kuchangia zaidi. Watumishi na walio mjini wenye vipato wachangie shilingi 1000/= kila mwezi.
3.      Wanaukoo wanashauriwa wawe na imani kwa mwanaukoo yeyote atakayepewa jukumu la usimamizi wa fedha. Suala la ufunguzi wa Akaunti ni muhimu likazingatiwa.
4.      Iundwe Kamati ya Usuluhishi ya Ukoo itakayotatua matatizo ya Wanaukoo wote, na iundwe na watu kutoka maeneo mbalimbali wanakoishi. Kazi yake kubwa itakuwa ni kupokea taarifa za matatizo na kuyatafutia ufumbuzi.
5.      Michango ianze kuchangwa mara moja na iachwe ikae angalau mwaka mmoja kabla hajaanza kutumika kuwasaidia wale wenye matatizo ya ugonjwa, kufiwa na pia kupangwe viwango mahsusi vya kuwasaidia hao wenye matatizo.
6.      Mfuko utakaoanzishwa kwa ajili ya kusaidia kwa upande wa Elimu, uegemee zaidi kuwasaidia wale wasio na uwezo. Wenye uwezo watumie gharama zao kuwasomesha watoto au jamaa. Lakini katika ugonjwa au misiba  basi ndugu wa hali zote wanufaike.
7.      Achaguliwe mwakilishi wa wanaukoo kutokana maeneo mbalimbali wanakoishi ili awe anafanya mawasiliano kwa wanandugu kuhusiana na matatizo au furaha katika maisha yao ya kila siku.
8.      Je wanaukoo mnadhani ni hatua gani zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya wanandugu/wanaukoo ambao hawaridhii kuuchangia mfuko huu? Katiba ikitungwa itakuwa na kipengele cha kuwabana wale ambao hawatoi michango yao. Mweka Hazina atakuwa na kipengele cha kumbana kuhusiana na utunzaji wa fedha za michango mbalimbali.

XVI: UCHAGUZI WA VIONGOZI WA UKOO
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoowa Kivenule ulifanya uchaguzi wa viongozi wa ukoo katika ngazi zifuatazo kama inavyobainishwa hapa chini:
1.      Viongozi wa Ukoo
1.        Faustin           S.         Kivenule                    Mwenyekiti
2.      Donath                      Mhapa                       Makamu Mwenyekiti
3.      Christian        J.          Kivenule                    Katibu
4.      Severin                      Nyangalima              Katibu Msaidizi
5.      Justin              D.        Kivenule                    Mweka Hazina
6.      Carolina        S.         Kivenule                    Mweka Hazina Msaidizi

2.  Washauri wa Uongozi wa Ukoo
1.        John                S.         Kivenule                    Morogoro
2.      Stephan                     Mhapa                       Kidamali
3.      Edgar             S.         Kivenule                    Dar eS Salaam
4.      Pius                            Kivenule                    Ilole
3.   Wajumbe wa Kamati Kuu ya Ukoo ambao pia ni Wawakilishi wa
      Kamati toka sehemu mbalimbali hapa Tanzania
1.        Adam             A.        Kivenule        Dar es Salaam
2.      Ignas               P.        Kivenule        Dar es Salaam
3.      Jovin               D.        Kivenule        Kidamali
4.      Justin              D.        Kivenule        Kidamali
5.      Faustin           S.         Kivenule        Kidamali
6.      Donati                       Mhapa           Kidamali
7.      Carolina        S.         Kivenule        Kidamali
8.      Zavary           S.         Kivenule        Mufindi
9.      Florian           A.        Kivenule        Mafinga
10.   Augustino                  Kivenule        Nduli
11.     Martin                                   Kivenule        Nduli
12.    Vitus                          Nzala             Magubike
13.    Romanus                   Kivenule        Ibogo
14.   Severin                      Nyangalima  Ilalasimba
15.    Marco                        Kivenule        Ilalasimba
16.   Fabian                       Kivenule        Nyamihuu
17.    Christopher               Kivenule        Ilole
18.    Titus                           Kivenule        Igominyi
19.   Alexander                 Nyangalima  Morogoro (Mikumi)
20. Christian                    Kivenule        Morogoro Mjini


XVII: SHUKRANI

Ndugu Ignas Kivenule ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Ukoo wa Kivenule, aliwashukuru wanaukoo wote waliotoa ushirikiano na kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, kwa kuwa wameonyesha umoja wa hali ya juu sana. Binafsi yeye anaamini jamii inayounda Ukoo wa Kivenule ni wapole na wasio na majivuno. Ila angefurahi sana kama jamii inayounda ukoo huu itajitokeza kwa wingi zaidi katika Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo wa Kivenule, utakaofanyika mwakani 2006.

Ukoo wa Kivenule una zaidi ya ndugu 2000 kutoka pande zote za Kidamali, Ilole, Nduli, Magubike na kwingineko. Ni wajibu wa kila mwanaukoo kuhamasisha watu wengine wajitokeze kuhudhuria Mkutano Mkuu ujao. Sambamba na hilo, pia aliiomba jamii ya Ukoo wa Kivenule ikalipa umuhimu suala la kusomesha watoto ili kupunguza utegemezi na pia kuwaandalia hali bora za maisha hapo baadaye.

Alisikitika kwa wanaukoo toka Ilole kutohudhuria Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, ila angefurahi sana kama jamii hiyo ya Ilole ingeshiriki mkutano huo. Kuna sababu nyingi zimetolewa, likiwemo suala la Nauli. Lakini, kama kila mwanaukoo atakuwa anajali ni jambo la msingi sana wangejiandaa kikamilifu kuhudhuria Mkutano ujao.

Wanaukoo wengi wa kutoka Dar es Salaam wamekuwa ni wazito na hii pia inakatisha tamaa. Kama ni matatizo ni vyema jamii yote ikashirikiana. Mojawapo ya mambo mazuri na ya msingi ya kufanya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ni kuiwezesha jamii inayounda ukoo huu, kuwa na uwezo wa kukabiliana na matatizo ya kila siku. Mwishoni aliwashukuru wanaukoo wote wa Kidamali kwa moyo wa ukarimu waliouonyesha


XVIII: KUFUNGA MKUTANO
Mgeni Rasmi Daima Luvanda (Mwenyekiti ya Serikali ya Kijiji cha Kidamali) alifunga rasmi Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule mnamo saa 3.30 usiku kwa kuzishukuru Kamati za Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo kwa kufanikisha kufanyika kwa mkutano huo.

Pia, aliwashukuru viongozi wapya waliochaguliwa kuuongoza Ukoo wa Kivenule na kuahidi kuwa atawapa ushirikiano wa hali na mali kuhakikisha kuwa wanafanikiwa katika utendaji wao wa kazi. Mgeni Rasmi kwa mara nyingine alitoa shukrani zake kwa viongozi, Umoja wa Ukoo wa Kivenule kwa ujumla kwa kumteua kuwa Mgeni Rasmi.

Kwake binafsi ilisema ilikuwa ni fursa tosha kujifunza mambo mbalimbali ambayo alikuwa hayajui, na pia kupata somo la kuweza kulifanyia kazi au kuionyesha jamii yake umuhimu wa kuwa na mkutano wa pamoja kama ulivyofanyika huu wa Ukoo wa Kivenule.













No comments:

Post a Comment