Kama Mwenyekiti, ninayo heshima kubwa sana kuandika
ujumbe huu kwenu wapendwa wana ukoo. Nina amini wote mliofika kwenye mkutano huo
ni kutokana na moyo wa dhati kabisa mlio nao kwa ajili ya kujenga umoja na
mshikamano wa ukoo wetu ili jina hili kubwa na lenye hadhi lisipoteee bure.
Naleta ujumbe huu kuomba msamaha kwa kushindwa
kuhudhuria mkutano kutokana na kuumwa. Inaniumiza sana kutoonana na ndugu zangu
mlio wengi, wapo ambao sijaonana nao tangia mkutano uliopita, wapo ambao ni
miezi kadhaa. Lakini najua Mungu ni mwema
- atatukutanisha tena.
Kama Mwenyekiti najua kuna mambo ambayo tumeshindwa
kutekeleza ndani ya makubaliano ya mikutano mbalimbali, hii ni kutokana na
mwaka huu kuwa mgumu sana. Kikazi na kiuchumi. Sipendi nionekane kama najitetea
ila kwa niaba ya viongozi wenzangu naomba tusamehewe.
Naomba wana ukoo mtuamini ya kwmaba mwaka huu
tutajitahidi kufanya kadri ya yote yatakayoongelewa kwenye mkutano huu.
Nawatakia Mkutano Mwema.
Na Mungu Awatangulie
Donath Mhapa
Mwenyekiti - KAUKI
No comments:
Post a Comment