MADA YA CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO
Wawezeshaji
1.
William Kivenule
2.
Augustino Kivenule
3.
Benard Kivenule
TAARIFA YA
UJUMLA YA CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO
Mada hii Historia na Chimbuko la
Ukoo wa Kivenule, iliwasilishwa na Ndugu
William Sigatambule Kivenule kutoka Kidamali kwa kushirikiana na Ndugu Augustino Kivenule kutoka Nduli na
Bwana Benard Kivenule wa Ilole. Wote kwa ujumla wao walijitahidi kueleza na
kufafanua Kiini na Chimbuko la Ukoo huu. Kwa kuanza Mwezeshaji kutoka Kidamali
Ndugu William, aliwaeleza washiriki wa mkutano huo kuwa Babu MTELINGOMA BALAMA
ndiye aliyekuwa mwanzilishi halisia wa ukoo wa Kivenule. MTELINGOMA ndiye aliyemzaa Babu TAGUMTWA BALAMA (KIVENULE).
Babu TAGUMTWA BALAMA (KIVENULE) ndiye aliyewazaa Babu TAVIMYENDA KIVENULE
na Babu KALASI KIVENULE. Ikumbukwe
kuwa, jina halisi la ukoo wa Kivenule ni BALAMA.
Kama ilivyokwisha julikana katika mada iliyowasilishwa katika Mkutano Mkuu wa
Kwanza na wa Pili wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule, ambapo ilielezwa kuwa, neno KIVENULE linamaanisha sifa ya kuwa jasiri Vitani na hasa katika kutumia
silaha za Mishale na Mikuki yaani kwa Lugha Asilia ya Kihehe
“KUMIGOHA”. Yaani kwa maana nyingine LIGALU yenye maana ya Kwihoma
Imigoha – Kuhoma Watavangu au Kuvenula
Avatawangu. LIGALU maana yake Vita. Kuhoma maana yake Kuchoma na Migoha maana
yake Mikuki. Venula maana yake ua, fyeka
maadui.
LIGALU ndiyo iliyochangia kuzaliwa
kwa jina la Ukoo la KIVENULE. KIVENULE maana yake ni Ushujaa kutokana na Shabaha ya Mikuki.
KUVENULA likiwa na maana halisi ya kuwa
na shabaha ya kuwaangamiza maadui kwa kutumia silaha ya Mishale na Mikuki. Babu
zetu akina TAGUMTWA BALAMA
walilidhihirisha hili katika Vita na Watavangu na hivyo kusababisha kuzawadiwa
kwa jina la KIVENULE kama jina la sifa
kutokana na ushujaa katika Vita.
Baada ya kuwazaa watoto hawa
wawili yaani TAVIMYENDA na KALASI, walisafiri na kufika hadi sehemu ya KALENGA,
wakiwa katika harakati za kutafuta maisha. Ndipo Babu TAVIMYENDA KIVENULE
alipoombwa na Mzee MYINGA aende akamsaidie kumchungia mifugo yake eneo la
MAGUBIKE na pia Babu KALASI KIVENULE naye kuamua kwenda eneo la ILOLE kutafuta
maisha.
Akiwa eneo la MAGUBIKE, Babu
Tavimyenda Kivenule akafanikiwa kupata watoto Saba (7), yaani BABU KAVILIMEMBE
KIVENULE, BABU MGAYAFAIDA KIVENULE, BABU SIGATAMBULE KIVENULE, BIBI MGASI
KIVENULE, BIBI MALIBORA KIVENULE, BIBI SIGINGULIMEMBE KIVENULE, BABU ABDALAH
KIVENULE NA BIBI SIKIMBILAVI SEMABIKI.
Huyu Bibi Sikimbilavi Semabiki hakuwa mtoto wa Babu Tavimyenda ila
alikuwa ni mtoto wa kufikia kwa Bibi
yetu.
Baadhi ya akina Babu
walifanikiwa kuwa na wake zaidi ya mmoja na hawa walikuwa ni Babu SIGATAMBULE
KIVENULE, ambaye mke wake wa kwanza alikuwa anaitwa SIWANGUMHAVI SINGAILE, mke
wake wa pili alikuwa anaitwa
NYANYILIMALE SINGAILE na mke wa Tatu, PANGULIMALE SETWANGA. Mke wa pili
na tatu wa Babu Sigatambule bado wapo hai.
Babu HUSEIN KIVENULE naye
alikuwa na wake wawili ambao ni YIMILENGERESA SEMSISI na DALIKA SETALA. Taarifa
za wake wa Babu wengine bado zinaendelea kufanyiwa utafiti. Babu MGAYAFAIDA
KIVENULE yeye hakubahatika kuoa wala kuwa na mtoto. Alikuwa ni mlemavu na ndiyo
maana ya jina lake
MGAYAFAIDA .
Kwa upande wa ILOLE, Babu
KALASI KIVENULE alibahatika kuwa na watoto watatu ambao ni Babu SALAMALENGA
(KAHENGULA) KIVENULE, MGUBIKILA (NYAKUNGA) KIVENULE NA SEKINYAGA KIVENULE.
BABU SALAMALENGA KIVENULE
alikuwa mwanaume peke yake na wawili waliobaki walikuwa ni wanawake. Babu
Salamalenga Kivenule alioa wake watatu ambao ni Bibi NYANGALI, BIBI SEMFILINGE MHENGAATOSA NA BIBI
SEMKONDA CHOGAVANU.
Kupitia kwa wake zake watu, Babu Salamalenga ndiye aliyeeneza Ukoo wa Kivenule
katika maeneo ya Nduli, Ilole, Mgongo na Kigonzile.
MABORESHO YA TAARIFA ZILIZOPO KUHUSU
HISTORIA YA UKOO WA KIVENULE
Kwa mujibu wa taarifa za
kihistoria kutoka eneo la ILOLE
inaonesha kuwa, Babu Salamalenga
alitokea Magubike na kuelekea eneo la Kaskazini. Baadaye kulitokea ugomvi baina
ya makabila, na hivyo kusababisha vita. Salamalenga
akapelekwa eneo la Pawaga Vitani, ambako alipigana mpaka vita ilipoisha. Baada
ya kurudi toka Vitani, Babu Salamalenga alifanikiwa kupata wake watatu, yaani Bibi Nyangali, Bibi Semfilinge na Bibi
Semkonda. Hawa wake zake wote wa watatu alifanikiwa kuzaa nao watoto.
Awali, Bibi Semkonda aliolewa
na Mwamatagi na kuzaa mtoto
analiyeitwa Sipanganakumutwa Sematagi. Semnyawanu wapo Kalenga na ni watoto wa Sipanganakumtwa.
Watoto wa kila mke wake wameooneshwa kama ifuatavyo:
1.
Bibi Semkonda
- Pangayena
Kivenule
- Jonas
Kivenule
- Samwel Kivenule
- Balasamaneno
Kivenule
- Daud
(William) Kivenule
- Barton
Kivenule
- Chogavanu Kivenule
- Munguatosa Kivenule
- Mwilimilisa
(Gungamesa) mtoto wa Sekinyaga
- Tindasulanga Kivenule
- Sigondola
Kivenule
- Shaban
Kivenule
- Gungamesa Kivenule
Katika Mkutano Mkuu wa Tatu wa KAUKI,
wawezeshaji wa Mada ya Chimbuko na Historia ya Ukoo, bado hakujawa na taarifa
rasmi zinazojitosheleza kuhusiana na mtiririko wa kizazi hiki cha Ukoo wa
Kivenule. Katika mkutano wa Tatu wa KAUKI, wawezeshaji walibainisha kuwa,
muundo wa Ukoo kwa upande wa Kidamali na Magubike upo kama
ifuatavyo:
Babu Mtengelingoma Balama alimzaa Babu Tagumtwa.
Pia, Babu Tagumtwa alikuwa na wake
wawili (2); yaani Bibi Sesambagi na
mwingine ambaye jina lake
halikuweza kuandikwa
(patikana) ambaye alimzaa Babu Kalasi.
Babu Tavimyenda ambaye ni mtoto wa Babu
Mtelingoma, alikuwa na wake watatu (3) ambapo mmoja wa wake zake alikuwa anaitwa
Bibi Mkami Sekabogo. Bibi Mkami Sekabogo alikuwa na mtoto wake wa kwanza ambaye aliitwa Sikimbilavi Semabiki. Mtoto huyu alimzaa kwa mme mwingine. Baadaye
alipokuja kuolewa na Babu Tavimyenda, aliweza kuwazaa watoto
wafuatao:
1.
Myumbila
(Kavilimembe)
Kivenule
2. Mgaifaida Kivenule
3. Sigatambule (Matesagasi) Kivenule
4. Hussein Kivenule
Abdalah Kivenule
Sigungilimembe Kivenule
Malibora Kivenule
Nao watoto wa Babu Tavimyenda kwa Mke wake
Bibi Mkami Sekabogo walijaliwa kuwa na familia zao isipokuwa kwa Babu Mgaifaida
ambaye hakubahatika kupata familia. Babu Mgaifaida pia alikuwa mlemavu.
Babu Kavilimembe ambaye pia ni mtoto wa
kwanza wa Babu Tavimyenda Kivenule, alijaliwa kuwa na wake wawili na kuzaa nao
watoto. Mke wa kwanza wa Babu Kavilimembe
alikuwa anaitwa Bibi Sekusiga ambaye alizaa watoto wafuatao:
1.
Elizabert
Kivenule
2. Dalikimale Kivenule
3. Sandra Kivenule
4. Pangalasi Kivenule
1.
Salikuvaganga Kivenule; na
2. Francis Kivenule
Mada ya Historia na Chimbuko la
Ukoo, pia ilileta mjadala ni namna gani tutahifadhi kumbukumbu za ukoo; na pia
njia mbadala za kutunza taarifa zinazohusiana na Ukoo. Wana-KAUKI kwa ujumla
wao walikuja na hoja mbalimbali zikiwemo hizi zifuatazo:
Kuwepo na viongozi (uongozi) wenye jukumu
la kufuatilia taarifa mbalimbali zinazohusiana na ukoo katika maeneo mbalimbali
ambapo wanadhani zinaweza kupatikana. Pia pawepo na mfumo unaoeleweka wa
kuhifadhi kumbukumbu aidha katika maandishi au namna nyingine yeyote. Pia
ilipendekezwa pawepo na taarifa za mara kwa mara katika maandishi ambazo
zitakuwa zinawasilishwa wakati wa mikutano mikuu ya KAUKI.
Wajumbe wa mkutano walipendekeza umuhimu
wa kumtumia Babu Hussein ambaye bado yupo hai kwa sababu ana taarifa nyingi zinazohu
ukoo wa Kivenule. Pia ilikubaliwa na wana-KAUKI kuwa licha ya kuwepo kwa majina
ya kisasa na ya Ubatizo ambayo walipewa hawa Babu na Bibi zetu; ni vyema pia
majina yote yakajumuishwa kwenye makaburi yao
ikiwa ni sehemu mojawapo ya kutunza kumbukumbu. Majina mapya siyo maarufu (au
hayafahamiki sana );
kwa hiyo ni vyema bado tukaendelea kutumia majina yote ili tusipoteze
kumbukumbu.
Wana-KAUKI pia walipendekeza yachongwe
mawe yenye majina ya marehemu ambapo tutayaweka katika makaburi kwa sababu siyo
rahisi kufutika na kupotea. Taarifa za historia ya ukoo ni muhimu ziwekwe
kwenye maandishi hususani vijitabu vidogo vidogo ambavyo vitasambwa kwa
wanaukoo mbalimbali na kuweza kujisomea.
Mada hii ya Chimbuko na Historia ya Ukoo
wa Kivenule, ni mwendelezo wa taarifa mbalimbali ambazo tumekuwa tukizitafuta
na kuziwasilisha katika Mikutano kama hii.
Katika Mkutano Mkuu wa Kwanza , wa Pili na pia
huu wa tatu Mada ya Chimbuko na Historia ya Ukoo iliwasilishwa. Kinachofanyika
kwa hivi sasa ni kuzidi kuiboresha na kuziongeza taarifa kwenye taarifa za
awali ambazo tayari tulikwisha zipata.
Tafsiri za Majina Mbalimbali yaliyopo
katika Ukoo wa Kivenule
Kidagamhindi Heka heka za
kukimbia kodi wakati wa mkoloni
Tunyahindi Kupigwa pigwa na wakoloni
Mwanitu Alizaliwa kweusi (kwa kutumia lung’ali). Kuwasha
moto ili kupata mwanga kwa kutumia kuni au aina fulani ya nyasi. Mara nyingi
ving’ali vinakuwa vinazimika.
Kadungu Kuwa na Dungu kubwa (kuwa na kitovu kikubwa)
Kibumo Mvefi (Mtu anayelialia)
Mlagile Alizaliwa wakati Bibi yake hayupo. Wakati
anaonyeshwa Bibi yake akisema Mlagile akaitwa Mlagile.
Fatamali Alifuata mali
Yamkopita Bibi alipomzaa mtoto wa kwanza na kisha kufariki,
akapata jina la ya Mkopite
Luhanage Wakati Bibi anazaa watoto wanakufa, alipomzaa
mtoto na akaugua sana
basi akaitwa Luhanage. Luhanage maana yake ni kuugua sana .
Mgendwa Alizaliwa kwa taabu. Alizaliwa kwa waganga wa
kienyeji kwa tabu wakiwa safarini
Msinziwa
Kanolo Wakati ameugua, anapiga ramli huki akitembea
kwa waganga.
Yimilengeresa Mzee Babu Husein alichukuliwa kwenye Vita ya Pili ya
Dunia. Wahindi walikufa sana
na Waingereza wakashinda Vita.
Misamiti ya Lugha
ya Kihehe
Mhisive Binamu
Nyavana Degedege
Ligalu Vita
Watavangu Wakubwa (Wakuu wa Nchi) kabla ya Ukoloni
No comments:
Post a Comment