RIPOTI
YA
MKUTANO
MKUU WA KWANZA WA
UMOJA WA
UKOO WA KIVENULE
17 – 18
DESEMBA 2005
KIDAMALI -
IRINGA
Imeandaliwa na:
Adam Alphonce Kivenule
Katibu Mkuu-KAUKI
Kidamali, Iringa Vijijini
E-mail: tagumtwa@gmail.com
kauki2006@gmail.com
Tovuti: www.kauki-kauki.blogspot.com
Adam Alphonce Kivenule
Katibu Mkuu-KAUKI
Kidamali, Iringa Vijijini
E-mail: tagumtwa@gmail.com
kauki2006@gmail.com
Tovuti: www.kauki-kauki.blogspot.com
I: UTANGULIZI
Harakati
endelevu za kuleta mabadiliko na maendeleo zinakua kwa kasi kubwa na hivyo
kuchochea mabadiliko ya haraka ya hali bora za maisha ulimwenguni kote.
Harakati kama hizo zinazotegemea sana uwepo wa Sayansi na Teknolojia, Elimu na
Uchumi endelevu; zinatoa fursa na hamasa kwa jamii huria nazo kubuni na
kutafuta mbinu mbadala za kuweza kujiinua ili kuweza kukabiliana na hali hiyo.
Mabadiliko hayo yanayozungumziwa ni pamoja na kukua kwa Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano kupitia Kopyuta yaani Internet na simu za mkononi (computer,
Internet and cellphones), Soko Huria, Utandawazi na Ubinafsishaji.
Jamii
huria kwa upande wake zinapata hamasa na changamoto ya kuweza kutafuta mustakabali
wake kutokana na hali halisi ya maendeleo inavyoendelea kukua kwa kasi na
athari zake kuonekana moja kwa moja katika maisha yetu ya kila siku kwa upande
mmoja; na pia mafanikio kuonekana kwa upande mwingine.
Wimbi
la umaskini uliokithiri, janga la UKIMWI, ujinga na rushwa vimekuwa ni vikwazo
vikubwa vya maendeleo na ambavyo vinazidi kudidimiza harakati mbalimbali za
kuweza kujiinua na kujikwamua katika hali hiyo. Harakati hizi za kutafuta maendeleo
zimegawanyika katika makundi mbalimbali ya kijamii hususani makundi ya wasomi,
wafanyabiashara, wanawake na wananchi wa kawaida.
Kutokana
na harakati hizo, wanajamii wanaounda Ukoo wa Kivenule nao hawako nyuma katika
kuhakikisha kuwa jamii yao
inaondokana na umaskini, ujinga pamoja na UKIMWI; na hivyo kupata fursa ya
kuishi katika Dunia Mbadala [Alternative World] iliyojisheheneza katika sayansi
na teknolojia.
Kwa
kutambua hilo, wanajamii na ndugu wanaounda UKOO wa KIVENULE, kwa pamoja toka
mwezi Februari 06, 2005, walianzisha harakati za kuinasua jamii yao kutoka
kwenye lindi la umaskini, ujinga na maradhi kwa kuunda Kamati ya kuuza na kuratibu
Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa KIVENULE; ambao ulipangwa
kufanyika katika Kijiji cha Kidamali, Wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa,
hapo tarehe 17 hadi 18 Desemba 2005. Katika mapendekezo ya awali, Uongozi
uliochaguliwa kuunda kamati ya maandalizi na uhamasishaji, ilipanga kuwepo na Kamati
Tatu za Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, yaani Kamati
iliyopo mkoani Dar es Salaam,
Kamati ya Kijijini Kidamali na ya Ilole – Iringa, zote zikiwa zimepewa majukumu
mazito ya kusaidia kufanikisha mkutano huo.
Mkutano
Mkuu wa Ukoo wa Kivenule awali ulitegemea kuwaalika ndugu na wageni wapatao mia
mbili (200) toka Kijijini Kidamali, Ilole, Nduli, Kihesa, Ilula,
Magubike, Kinyamlewa, Nzihi, Iringa Mjini, Kalenga, Ipogolo, Museke, Kitwilu,
Igowolo, Kiponzelo, Mafinga, Mufindi, Maduma, Wasa, Ifunda, Tosamaganga,
Kilombero, Morogoro, Dodoma na Dar es Salaam; na sehemu nyingine nyingi ambako
wanajamii wanaounda ukoo huo wanaishi ili waweze kupata fursa ya kushiriki
kikamilifu.
Ukoo
wa Kivenule ukiwa umejiwekea malengo mahususi katika kuandaa mkutano huo, pia uliazimia
pamoja na mambo mengine, kufundisha jamii inayounda ukoo huo, Mada Tano zenye
msukumo wa kimaendeleo. Mada zilizopendekezwa kufundishwa katika siku mbili za
mkutano huo zilikuwa ni pamoja na:
1. HISTORIA NA CHIMBUKO LA UKOO
• Ukoo ni Nini na Unapatikanaje?
• Dhana ya Kuenea na Kukua kwa Ukoo.
• Mgawanyiko
wa Ukoo (Chora Mchoro Kuonyesha Ukoo unavyoundwa).
• Kupotea kwa Ukoo.
2. MAHUSIANO BAINA YA NDUGU NDANI YA UKOO
• Ukaribu wa Wana Ndugu.
• Ushirikiano Katika Nyanja Mbalimbali.
• Kutembeleana kama Sehemu ya Kudumisha
Mahusiano.
• Kuondoa Tofauti na Kusaidiana.
3. ELIMU NA MUSTAKABALI WA UKOO
• Nafasi ya Ukoo wa Kivenule katika
Elimu.
• Umuhimu wa Elimu.
• Dunia ya Utandawazi.
• Nini Kifanyike Kuinua Elimu Katika
Ukoo Wetu.
4. UKIMWI NDANI YA UKOO NA ATHARI ZAKE
• UKIMWI ni
nini?
• Namna
gani UKIMWI unavyoenea/kuambukizwa?
• Njia
Mbadala za Kujilinda na Maambukizi?
• Jukumu la
Ukoo/Familia Kukabiliana na Janga la UKIMWI.
5. DINI
KATIKA UKOO
• Maana ya
Dini
• Umuhimu
wa Kuwa na Imani
• Maadili
na Dini
• Ukoo
Uliojengeka katika Misingi ya Dini
Wawezeshaji mbalimbali wenye ujuzi katika mada hizo walipatikana
baada ya kamati kuchukua jukumu la kuwatafuta ikiwamo kupata Mtaalam wa UKIMWI toka
TAHEA.
Mojawapo ya hamasa kubwa ya kuandaa mkutano huu ilikuwa ni
pamoja na suala nzima la mahusiano ndani ya wanandugu, wanaukoo na jamii kwa
ujumla. Suala la ELIMU, ATHARI ZA UKIMWI katika jamii ya ukoo wa Kivenule na
taifa nzima. Pia haja ya kufahamiana baina ya wanajamii na ndugu wanaounda
ukoo, pamoja na kuujua Ukoo kwa ujumla.
Pamoja na mambo mengine, kamati ilifikiria pia uwezekano
wa kufanya senza ili kujua idadi ya ndugu wanaounda ukoo husika toka kona
mbalimbali hapa Tanzania; kujua nini wanakifanya na kujua idadi sahihi ya
wanandugu ambao wanahitaji msaada wa namna moja au nyingine.
Katika suala nzima la Kufahamu Historian na Chimbuko la
Ukoo, Mahusiano baina ya wanandugu ndani ya ukoo, Elimu, Maadili na Dini na
gonjwa hatari la UKIMWI, Kamati ilionelea kuwa ni mojawapo ya mambo msingi sana
kuyaangalia katika shughuli nzima ya maandalizi na wakati wa Mkutano Mkuu.
Changamoto zitakazopatikana baada ya kuyagusia mambo haya
ya msingi na hivyo kuwawezesha washiriki wa mkutano mkuu kujenga ajenda mpya.
Mahusiano duni baina ya wana ndugu, kukosekana kwa
ushirikiano katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo, hali duni ya kiuchumi na
kijamii, matatizo ya kifamilia na kiukoo ni kati ya masuala ya msingi
yaliyofikiriwa sana kabla ya kuanza kufanya maandalizi ya Mkutano Mkuu.
Mwelekeo na nafasi ya ukoo wa Kivenule katika suala nzima
la Elimu hasa katika dunia hii ya Utandawazi (Globalization). Maendeleo ya
sayansi na teknolojia ambapo yameifanya dunia kuwa kama kijiji kisicho na
mipaka na kila mtu anaruhusiwa kuingia na kutoka; kuongezeka kwa viwanda
vinavyotumia teknolojia ya hali ya juu; kuongezeka kwa teknolojia ya habari na
mawasiliano (Internet); kupanuka na kujengeka kwa miji, pamoja na soko huria.
Mambo yote haya ndiyo yanayoweza kuonyesha mustakabali na
nafasi ya ukoo wa Kivenule kwa maisha ya baadaye. Ilionekana kuwa ukoo wetu upo
nyuma sana katika suala nzima la elimu, hii linajidhihirisha kutokana na kuwa
na ndugu wachache sana ambao wameweza kupata elimu kwa kiwango kinachostahili.
Hii ni hatari kwa sababu tunajenga ukoo tegemezi ambayo
baadaye utakosa mwelekeo. Mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia yanayojitokeza
kila kukicha yanaibadili dunia na hivyo kutulazimisha nasi katika ukoo wa
Kivenule kubadilika. Matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano katika
simu za mikononi, Internet, kompyuta, redio na satelaiti ni changamoto kubwa
katika Ukoo wa Kivenule.
Maambukizo ya ugonjwa wa UKIMWI ambayo kwa kiasi kikubwa
yameathiri familia nyingi zikiwemo familia zetu sisi wana ukoo, yanapaswa
kutopuuzwa bali kuwekewa mikakati madhubuti. Ufahamu kuhusiana na gonjwa
lenyewe livyoenea na madhara yake katika jamii, njia mbadala za kujilinda na
maambukizi ya ugonjwa wenyewe pamoja na kuitikia mialiko mbalimbali ya
wanajamii wanaopambana na janga hili ni mambo ya msingi sana ambayo yalijadiliwa
kwa kina kwenye mkutano huo.
Ilipendekezwa kuwa, wakati wa mkutano huo kutakuwa na
nafasi kutoa uzoefu katika mambo mbalimbali ya kitaalum na maendeleo.
Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Ukoo yalianza mapema ili kumpa fursa kila
mwanajamii/mwanaukoo kutafakari na kujadili kwa kina, kujiandaa pamoja na
kuwasilisha mchango wake wa mawazo kwa kamati husika za kuratibu maandalizi.
Mkutano Mkuu wa Ukoo umeazimia
kutoka na kitu muhimu ambacho ndicho kitakuwa mwongozo na dira ya shughuli
mbalimbali zitakazokuwa zinafanyika katika ukoo.
Licha ya kuwa na malengo na
makusudio mbalimbali, pia tunategemea mwisho wa mkutano kutakuwa na mambo
kadhaa ambayo yatakuwa ni makubaliano kutoka pande mbalimbali za ukoo wa
Kivenule. Yote hayo kwa pamoja yatakuwa ni maazimio ya Mkutano Mkuu wa Kwanza
wa Ukoo wa Kivenule.
Kati ya Maazimio ambayo Kamati
iliyategemea kuyatekeleza katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ni
pamoja na:
1.
Kufanyika kwa Senza ya Ukoo wa Kivenule ili kupata idadi
kamili ya ndugu.
2.
Kuanzisha Mfuko wa Ukoo ambao utasaidia katika kusomesha
watoto wanaofaulu pamoja na kusaidia katika matatizo mbalimbali yanayojitokeza
au uhitaji wa msaada.
3.
Kuchagua Viongozi wa Ukoo pamoja na Wajumbe Wawakilishi watakaounda
Kamati ya Ukoo ya Kuratibu mambo mbalimbali ya ukoo. Nafasi za Viongozi
watakaochaguliwa zitajumuisha Mwenyekiti, Makamu wa Mwenyekiti, Katibu, Katibu
Msaidizi, Mweka Hazina na Msaidizi wake pamoja na Walezi Watatu wa kushauri
uongozi uliopo madarakani.
4.
Kuzitaja/kutamka bayana kazi/majukumu mbalimbali ambayo
Uongozi utakaoundwa utakuwa unazifanya mfano kufanya mashauriano na usuluhishi
wa matatizo mbalimbali ya ukoo yaliyojitokeza. Lakini pia jukumu lao kubwa ni
kuongoza na kusimamia majukumu mbalimbali yanayojitokeza au kuhitaji usimamizi
ndani ya ukoo.
5.
Kukusanya taarifa mbalimbali za ukoo; na
6.
Kuangalia na Kutathmini usalama wa mali mbalimbali
zinazomilikiwa na ukoo nk.
II: UUNDAJI WA KAMATI ZA
MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA
KWANZA WA UKOO
Kamati mbili za kuratibu Maandalizi ya Mkutano Mkuu
wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ziliundwa. Kamati ya Kwanza ilikuwa ni Kamati ya
Dar eS Salaam ambayo uliundwa mwezi Februari 06, 2005 na Kamati ya Pili kuundwa
ni ile ya Kidamali ambayo iliundwa mwezi Mei 2005. Uundaji wa Kamati ya Dar es
Salaam na ile ya Kidamali uliendana na uchaguzi wa viongozi wa kuziendesha na
kuzisima-mia kamati hizo. Kwa upande wa wanaukoo na ndugu wanaoishi Dar es
Salaam na mikoa ya karibu kama Morogoro, Dodoma na Mikumi waliingia kwenye
Kamati ya Dar es Salaam.
Kamati ya Kidamali iliwaunganisha wanaukoo na ndugu wote
wanaoishi maeneo ambayo yapo karibu na Kidamali mfano Magubike, Nzihi, Kalenga,
Nyamihuu, Idete na kwingineko.
Kwa upande wa Kamati ya Dar es Salaam, viongozi walikuwa
kama ifuatavyo:-
1.
Christian Kivenule Mwenyekiti
2.
Adam Kivenule Katibu
3.
Athuman Mtono Makamu
Mwenyekiti
4.
Edgar Kivenule Mshauri wa Kamati
5.
Innocent Kivenule Mweka Hazina
6.
Ignas Kivenule Mshauri
Kamati ya Ilole
Na kwa upande wa Kamati ya Kidamali, viongozi
waliochaguliwa walikuwa kama ifuatavyo:-
1.
Faustin Kivenule Mwenyekiti
2.
Augen Kivenule Makamu Mwenyekiti
3.
Jovin Kivenule Katibu
4.
Carolina Kivenule Katibu
Msaidizi
5.
Justin Kivenule Mweka Hazina
6.
Donati Mhapa Mshauri
7.
Pyela Kivenule Mshauri
8.
Daniel Kivenule Mshauri
Kamati zote
mbili zilikuwa na washauri, ambao nao pia walichaguliwa siku hiyo hiyo ya
kuwachagua viongozi. Kazi ya washauri ilikuwa ni kuzishauri Kamati zote mbili
katika kutekeleza majukumu yake.
A: KUHAMASISHA/UHAMASISHAJI
Mwezi Mei 2005, viongozi wanaounda Kamati ya
Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule toka Dar es Salaam, walisafiri kwenda Kidamali –
Iringa wakiwa na lengo mahsusi la Kuhamasisha wanaukoo wanaoishi Kidamali na
maeneo ya Karibu kuhusiana na Maandalizi ya Mkutano wa Ukoo.
Tendo
la Uhamasishaji lilienda sambamba na kuundwa kwa Kamati ya Maandalizi ya
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule kwa
Upande wa Kidamali. Jukumu la Kamati hiyo iliyoundwa ilikuwa ni:
Kuhamasisha
wanaukoo toka maeneo mbalimbali yanayozunguka Kidamali kujitokeza kwa wingi siku
ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule;
Kutoa
michango ili kufanikisha maandalizi ya Mkutano Mkuu; na
Kusambaza
kadi za michango kwa wanandugu na wadau mbalimbali ambao wanaweza kusaidia
kuchangia maandalizi ya Mkutano Mkuu.
B: UCHANGAJI
WA MICHANGO
Kamati
zote mbili ya Kidamali na Dar es
Salaam zilitekeleza ipasavyo jukumu la uchangiaji wa
michango. Kwa upande wa Kamati ya Dar es Salaam, zoezi la uchangiaji michango
halikuwa na mafanikio sana
ukilinganisha na mafanikio yaliyojitokeza upande wa Kidamali.
Ukusanyaji
wa michango ulifanyika kwa kusambaza kadi za kuomba mchango wa kufanikisha
kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo
wa Kivenule. Viwango wa vichango vilitofautiana kwa wale wanaoishi mijini na
pia kwa wale wanaoishi vijijini.
Kwa
wanandugu wanaoishi mijini waliombwa wachangie shilingi Elfu Kumi na Tano tu
(15,000/=); na kwa wenzetu wanaoishi maeneo ya vijijini waliombwa wachangie
shilingi Elfu Tano tu (5,000) au kitu chochote chenye thamani ya fedha hiyo
mfano kutoa kuku au mazao (mahindi au maharage).
C: MWITIKIO KATIKA UCHANGAJI MICHANGO
Wanaukoo
wanaoishi Kidamali na maeneo ya karibu walionyesha mwitikio wa hali juu sana kwa kutoa michango yao kwa moyo. Karibu robo tatu ya michango
iliyofanikisha Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo
wa Kivenule ilitoka Kidamali na maeneo yake ya Karibu. Jamii kuna sehemu kadhaa
zilionyesha kusita katika kutoa michango yao
katika kipindi cha awali, ilibadili msimamo wake katika dakika za mwisho.
Kamati
iliamini kuwa kutokuwa na hamasa wakati wa awali pengine ilitokana na kutoelewa
dhumuni la michango hiyo. Mara baada ya kubandika matangazo ya kuutangaza
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, wanaukoo wengi toka maeneo
mbalimbali walijitokeza kutoa michango yao.
Wanaukoo
wanaoishi Dar es Salaam
hawakufanya vizuri katika kutoa michango. Ni ndugu wachache tu ndio
waliojitokeza kutoa michango yao.
Wengi wa wanandugu/wanaukoo walitoa sababu mbalimbali za matatizo mfano kutokuwa
na ajira na pia kutomudu kutoa kiasi hicho cha pesa. Tatizo la utoaji wa michango
lilienda sambamba na mahudhurio duni kwenye vikao vilivyoitishwa. Hadi dakika
za mwisho za maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, ni
wanaukoo chini ya kumi ndiyo waliokuwa wametoa michango yao.
III: TATHMINI YA MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA KWANZA WA
UKOO KIVENULE
Kamati
zote mbili za maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ile ya
Kidamali nay a Dar es Salaam,
zilikaa pamoja ili kuweza kufanya tathmini ya shughuli nzima ya maandalizi ya
Mkutano Mkuu yaliyofanyika kati ya mwezi Februari na Novemba 2005.
Lengo
la kuzikutanisha Kamati zote mbili ilikuwa ni kufanya tathmini ya hatua za
maandalizi zilizofikiwa kwa ajili ya kufanikisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Ilionekana dhahiri kuwa
Kamati ya Maandalizi ya Kidamali ilifanya vizuri zaidi, huku Kamati ya
Maandalizi toka Dar es Salaam – ikionyesha kuelemewa kutokana na mwitikio duni
wa wanaukoo waishio eneo hilo
la mjini.
Kamati
zote mbili za Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ya
Kidamali na Dar es Salaam,
zilifanikiwa kukusanya jumla ya shilingi 345,350.00
mpaka siku ya mwisho ilipofanyika tathmini ya ukusanyaji wa michango wa Kamati
zote mbili.
Kamati
ya Dar es Salaam ilijitahidi kufanya maandalizi ya moja kwa moja katika
harakati za Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa kwanza wa Ukoo wa Kivenule.
Maandalizi hayo yalihusisha uandalizi wa Kadi za Michango (Kadi za Kawaida na
Kadi Maalum). Kadi za kawaida ziligawanyika katika makundi mawili, yaani kadi
za Shilingi Elfu Kumi na Tano (15,000/=) na kadi za Shilingi Elfu Tano
(5,000/=). Kadi Maalum zilikuwa mahsusi kwa watu au taasisi maalum zilizoombwa
kuuchangia Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa
Kivenule.
Jukumu
jingine lilifanyika na Kamati ya Dar es Salaam ilikuwa ni uandaaji na uchapaji
wa minitisi za vikao mbalimbali na kuzisambaza, uandaaji wa Mabango ya
kuutangaza Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule kwa ajili ya kubandikwa
maeneo mbalimbali.
Pia
Kamati ya Dar es Salaam iliandaa vitambulisho kwa ajili ya washiriki wa Mkutano
Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Lengo
ilikuwa ni kuhakikisha kuwa kila mshiriki anakuwa na kitambulisho wakati
Mkutano ukiendelea.
IV: UUNDAJI WA
KAMATI ZA KURATIBU MKUTANO
Kamati
mbalimbali ziliundwa ili kuweza kufanikisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Kamati kadhaa ziliundwa ili
kuratibu shughuli na majukumu mbalimbali wakati Mkutano ukiendelea. Kamati hizo
zilizoundwa ni pamoja na:
1.
Kamati ya Chakula
2.
Kamati ya Ulinzi
3.
Kamati ya Vinywaji
4.
Kamati ya Mapokezi
5.
Kamati ya Burudani
Kila
Kamati ilikuwa na msimamizi wake ili kuhakikisha kuwa kila jambo linafanyika kama ilivyopangwa katika Ratiba. Kwa kiwango kikubwa,
kila Kamati iliyopewa jukumu la kutekeleza wakati wa Mkutano Mkuu ilifanya
vizuri na kwa ufanisi wa hali ya juu. Kamati zilizoundwa zilishirikisha
wanaukoo, majirani na marafiki na hivyo kutoa hamasa kubwa katika kutekeleza
majukumu. Majirani na marafiki waliwaomba wanandugu/wanaukoo toka Ukoo wa
Kivenule kuwa mstari wa mbele katika kutekeleza majukumu yao ili wawe chacho kwa wengine wasio
wanaukoo.
V: UTEUZI WA WAWEZESHAJI WA MADA
Wawezeshaji
mbalimbali waliteuliwa na Kamati zote mbili, yaani Kamati ya Dar es Salaam na
ile ya Kidamali kuwa Wawezeshaji wa Mada Tano zilizopendekezwa kuwasilishwa
kwenye Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa
Kivenule. Baadhi ya Wawezeshaji hao pamoja na Mada walizopewa kuwasilisha ni:
1. CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOOO
§
Christian J. Kivenule
§
Augustino Kivenule
§
Daniel S. Kivenule
2. MAHUSIANO YA NDUGU NDANI YA UKOO
§
Stephan Mhapa
§
Ignas P. Kivenule
§
John S. Kivenule
3. ELIMU NA MUSTAKABALI WA UKOO WA KIVENULE
§
Christian J. Kivenule
§
Donath Mhapa
4. UKIMWI NA ATHARI ZAKE NDANI YA UKOO
§
Maria Milimo
§
Adam A. Kivenule
5. DINI KATIKA UKOO
§
Jovin D. Kivenule
§
George S. Kivenule
§
Stephan Mhapa
VI: MIALIKO KWA WANANDUGU, WANAUKOO PAMOJA NA WASHIRIKI
WENGINE
Mialiko
ya wanandugu pamoja na wanaukoo kwa ujumla, kuhudhuria MKutano Mkuu wa Kwanza
wa Ukoo wa Kivenule ilifanyika wazi kwa kila mtu bila upendeleo, kila mwanaukoo
alipewa taarifa za kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Ukoo na kuombwa kuhudhuria.
Aidha kamati zote mbili za maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza
wa Ukoo wa Kivenule, zilikubaliana kwamba, kila mwanandugu au mwanaukoo anapaswa
kuhudhuria mkutano huo bila kukosa.
Mialiko
ilifanyika kwa namna mbalimbali ikiwemo ile ya mdomo. Yaani kumwalika mwanaukoo
au ndugu moja kwa moja kwa kumpa maelekezo kuhusiana na mahali unapofanyika
mkutano mkuu, tarehe pamoja na muda. Familia yote, yaani baba, mama na watoto,
wote walipaswa kuhudhurio mkutano mkuu huo.
Pia
mialiko ilifanyika kwa kubandika matangazo ya kuutangaza Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule sehemu mbalimbali Kijijini
Kidamali pamoja na maeneo mengine ambako Kamati ziliamini ndugu na wanaukoo wanaishi
kule.
Kila
ndugu aliyefika na kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Kwanza
wa Ukoo wa Kivenule, alipewa kitambulisho cha kuweza kumtambulisha kwa ndugu
wengine. Kitambulisho hicho kilionyesha namba ya kitambulisho, jina la ndugu,
mahali anapoishi na simu au sanduku la posta. Kamati ziliepuka ile hali ya
kuulizana maswali ya kuwa wewe unaitwa nani, unaishi wapi na simu yako iko
wapi? Hii ilikuwa ni sababu ya msingi ya kutoa kitambulisho kwa kila mwanaukoo
au ndugu.
VII: UBANDIKAJI WA MATANGAZO
Ubandikaji
wa matangazo ya kuutangaza Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ulifanyika
sehemu mbalimbali Kijijini Kidamali pamoja na maeneo mengine ambako Kamati
ziliamini ndugu na wanaukoo wanaishi kule, ulifanyika kwa lengo la kuwajulisha
ndugu kuhusu uwepo wa Mkutano Mkuu na wapi unafanyika.
Baadhi
ya sehemu kulikobandikwa matangazo ni pamoja na Kidamali, Magubike, Nzihi,
Nyamihuu, Ipogolo na Nyamihono. Ubandikaji wa matangazo ya Mkutano Mkuu wa
Ukoo, uliibua hisia ya kushawishika kuhudhuria kwa wanaukoo na wasio wanaukoo
kuhusiana na kufanyika kwa Mkutano huo. Wapo majirani, marafiki na watu wasio
wanaukoo waliokuwa na shauku kubwa ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule.
VIII: SIKU YA KWANZA YA MKUTANO MKUU WA KWANZA WA UKOO WA
KIVENULE, DESEMBA 17, 2006
Mkutano
Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule
ulifunguliwa na Mgeni Rasmi Ndugu Daima Luvanda, ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Kijiji cha Kidamali.
Awali
kabla ya yote, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Mkuu wa
Ukoo Ndugu Faustino Kivenule, aliwakaribisha ndugu, jamaa na wanaukoo kwa
ujumla kwenye mkutano huo.
Kabla
ya kusoma hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Ukoo, Mwenyekiti wa Kamati ya
Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo,
alimkaribisha Ndugu George Kivenule, kuuombea Mkutano Mkuu kwa sala.
Baada
ya Sala ya kuuombea Mkutano Mkuu, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano
Mkuu wa Ukoo, alitumia fursa hiyo kuisoma Hotuba ya Ufunguzi.
Alianza
kwa kuwajulisha ndugu, wanaukoo na wageni waalikuwa kuwa, lengo la Mkutano Mkuu
wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ni kuwaunganisha wanaukoo wote, wanaoishi sehemu
mbalimbali hapa Tanzania, ili wafahamiane, waelimishane na kupeana ujuzi katika
nyanja mbalimbali za maendeleo na kupeana uzoefu.
Pia,
lengo jingine la Mkutano Mkuu wa Kwanza wa
Ukoo wa Kivenule ilikuwa ni kutolewa na kufundishwa kwa Mada kadhaa zenye nia
ya kuujengea ukoo na kuwa na msimamo imara. Kwa kuwakusanya ndugu pamoja,
Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu, iliamini itasaidia kuujenga Ukoo katika
misingi ya Ushirikiano na Upendo na hiyvo kuwa na ukoo wenye umoja.
Lengo
jingine la kufanya mkutano mkuu wa ukoo ilikuwa ni kufanya senza ili kujua
idadi ya wanaukoo na mwishoni kufanya uchaguzi wa viongozi, watakaunda Uongozi
wa Ukoo na pia watashirikiana na Kamati ya Ukoo wa Kivenule katika kutekeleza
majukumu mbalimbali.
Kamati
itakayoundwa itakuwa na jukumu la kuratibu mambo mbalimbali na matatizo
yanayohusu ukoo.
Jumla
ya Mada Tano ziliwasilishwa na kufundishwa katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Mada zilizowasilishwa ni
pamoja na:
1. CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO;
2. MAHUSIANO BAINA YA NDUGU NDANI YA UKOO;
3. ELIMU NA
MUSTKABALI KATIKA UKOO;
4. UKIMWI
NDANI YA UKOO NA ATHARI ZAKE; NA
5. DINI
KATIKA UKOO.
Harakati za maandalizi ya Mkutano Mkutano Mkuu wa Kwanza
wa Ukoo wa Kivenule, zilianza toka mwezi Februari 05, 2005. Harakati hizi
zilifanyika Kijijini Kidamali kwa upande mmoja na kwa upande mwingine jijini
Dar es Salaam.
Kamati zote mbili zilizoundwa zilijipa majukumu mbalimbali,
likiwemo lile la kuwaalika na kuwashirikisha ndugu na wanaukoo katika suala
zima la maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Ukoo katika vikao, na pia utoaji wa
michango.
Katika harakati za maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza
wa UKoo wa Kivenule, kamati zote mbili zilizipata vikwazo mbalimbali likiwemo
tatizo la mwitikio duni katika kulipokea wazo hili. Kwa ujumla, katika kuliuza
suala/wazo hili la kuandaa na kuwa na Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa
Kivenule, kamati ilibidi zitumiea nguvu na mbinu za ziada ili kuweza
kufanikiwa.
Mahudhurio duni yalitoa changamoto kwa Kamati za
Maandalizi ya Mkutano Mkuu, kuongeza juhudi/jitihada na kutafuta njia mbadala
za kufikia lengo. Kwa upande wa Kijijini Kidamali, ushawishi ulizaa matunda,
kwa sababu ongezeko la wanaukoo na ndugu kuliunga mkono wazo la kufanyika kwa
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo lilivuna washiriki wengi.
Kwa upande wa Dar es Salaam, suala la mahudhurio duni,
liliendelea kuwa ni kikwazo kwa kipindi chote cha maandilizi ya Mkutano Mkuu wa
Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Wapo waliodiliki kusema Mkutano Mkuu wa Ukoo
ufanyike kwanza Dar es Salaam na ndipo ufanyike na kijijini Kidamali. Licha ya
kupewa sababu na maelezo ya kina ya kuufanya Mkutano huo ufanyike Kijijini
Kidamali, hawakutilia maanani.
Katika suala la utoaji wa michango, watu wamekuwa na ari
na mwitikio wa hali ya juu hapa Kijijini Kidamali, na kwa kiwango kikubwa ndio
waliosaidia kufanikisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa
Kivenule.
Licha ya wanaukoo waishio Dar es Salaam kuchangia, lakini
mchango wao umesaidia kidogo sana, kwa sababu kiwango kikubwa cha fedha pamoja
na mahitaji mengine, yamepatikana hapa.
Sehemu nyingine, nje ya Kidamali, utoaji wa michango hapo
mwanzo ulikuwa wa wastani, lakini kadiri siku zilivyokuwa zinakaribia, ari na
kasi mpya ilijitokeza na kuwa kubwa hasa toka sehemu za Magubike pamoja na
Nyamihuu.
Majirani na watu wengine wasio wanaukoo wamejitolea kutoa
michango katika kuusaidia Ukoo wa Kivenule, kufanikisha kufanyika kwa Mkutano
Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Majirani na marafiki waliojitokeza kwa hali
na mali katika kutoa fedha, vyombo na vifaa mbalimbali.
IX: HOTUBA YA MGENI RASMI
Mgeni Rasmi aliishukuru Kamati ya Maandalizi ya Mkutano
Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule kwa kumwalika kuwa Mgeni Rasmi katika
Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Kivenule. Alisisitiza kwa kusema kuwa, kuna watu wengi
muhimu ambao tumewaacha na kuamua kwenda kumwalika yeye.
Mgeni Rasmi alisema amefarijika sana kutokana na
kuwashirikisha jamaa/wanaukoo wote. Pia alisisitiza kuwa anahisi yupo karibu na
ukoo wa Kivenule kutokana na baadhi ya jamaa zake wa karibu kuwepo kwenye
mkutano huo. Pia hata rafiki zake nao walihudhuria kwenye Mkutano Mkuu wa Ukoo;
hii ilimpa faraja sana.
Kutokana na ukoo kuwa na mtandao mkubwa sana, ni muhimu
kukawa na shughuli za pamoja kama hizi. Wakati anaongea na Mwenyekiti,
amefurahi sana kusikia mikakati ya wanaukoo hasa lile la kufanya senza na pia
mkakati wa kufahamiana zaidi.
Mgeni Rasmi aliwashukuru wale wote waliotoa wazo la
kuwepo kwa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule na jinsi
walivyoshirikisha wanaukoo katika shughuli hii.
Katika shughuli yoyote ile, vikwazo vipo, suala la msingi
ni kuelimishana na kuwashawishi wale ambao hawakuhudhuria ili kuwepo na umoja
na mshikamano. Suala mshikamano na umoja ni muhimu sana katika jamii yetu kwani
itasaidia kuleta maendeleo na wana-ndugu wanatakuwa karibu. Pia, kuwa pamoja
kunasaidia kushirikiana katika magonjwa, furaha na matatizo mbalimbali ya kila
siku. Mgeni Rasmi, alitoa mfano wa Abraham na Lutha katika ugomvi wao wa
mifugo, lakini mwisho walijaliana katika shida licha ya kutengana. Ndugu ni
muhimu sana na hawawezi kutengana.
Mkutano huu unatoa changamoto ya kuwa na mshikamano na
kuwa na nguvu zaidi katika kuleta maendeleo. Mgeni Rasmi aliushukuru Ukoo wa
Kivenule kwa kuelimishana kuhusu umuhimu wa kuwa na ushirikiano wakati wote
nasi tu wakati wa matatizo. Huu ni mfano mzuri kwa jamii nyingine. Mgeni Rasmi
aliutakia kila la kheri Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, na kuahidi
kuwa yuko nyuma ya wanaukoo sambamba wakati wote wa Mkutano huo.
Baada ya hotuba ya
Mgeni Rasmi, MKUTANO MKUU WA KWANZA WA
UKOO WA KIVENULE, ulitangazwa Kufunguliwa
Rasmi Mnamo saa 4:45 Asubuhi, Siku ya Jumamosi, tarehe 17 Desemba 2005
X: UTAMBULISHO WA WANAUKOO
Kwa mujibu wa ratiba ya siku ya kwanza ya MKUTANO MKUU WA KWANZA WA UKOO WA KIVENULE,
utambulisho wa Wanaukoo ulifanyika kwa kila ndugu/mwanaukoo kujitambulisha
mwenyewe. Mwenyekiti aliwaelewesha washiriki wote jinsi
ambavyo wanapaswa kujitambulisha.
Kila
anajitambulisha alipaswa/alitakiwa kutaja jina lake la mwanzo, jina la baba
yake, babu na jina la mwisho la ukoo. Lakini, pia wanaukoo walijitambulisha kwa
kutaja majina ya Mama zao, Waume au Wake zao.
Kila
mshiriki katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo
wa Kivenule, alipewa kitambulisho cha kumtambulisha kwa ndugu wengine.
Kitambulisho hicho kilionyesha jina lake
kamili, mahali anapoishi,
namba ya simu pamoja na sanduku la posta. Hii ilifanyika makusudi ili kupunguza
kuulizana majina kutokana na washiriki kuwa wengi.
Yafuatayo
hapa chini ni majina ya wanaukoo waliojitambulisha siku/ kwenye Mkutano Mkuu wa
Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. (refer registration forms).
XI: UWASILISHAJI WA MADA KATIKA MKUTANO MKUU WA
UKOO
Katika MKUTANO
MKUU WA KWANZA WA UKOO WA KIVENULE, jumla ya Mada Tano
ziliwasilishwa. Mada ya kwanza kuwasilishwa katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa
Kivenule ilikuwa ni “CHIMBUKO NA
HISTORIA YA UKOO”. Wawasilishaji wa Mada hii walikuwa ni ndugu:
1. Christian J. Kivenule
[Toka Kidamali]
2. Augustino Kivenule [toka Nduli (Kigonzile)]
MADA
YA KWANZA
CHIMBUKO
NA HISTORIA YA UKOO WA KIVENULE
Maana
ya Ukoo (Tafsiri)
Ukoo ni muungano wa familia
kadhaa zenye utambulisho fulani, aidha wa jina, alama au mwelekeo mmoja.
Tunapozungumzia utambulisho fulani uwe wa jina,alama au mwelekeo mmoja;
tunamaanisha kwamba ukoo wa Kivenule unatambulika kati ya jamii nyingine
mbalimbali kwa jina la “KIVENULE”, jina ambalo linatuunganisha na jamii
nyingine au ndugu kujiona sisi ni kitu kimoja.
Tunapomuona mtu mgeni machoni
petu lakini ana mweleko wa ukoo wa Kivenule, tunamwuliza, mwenzetu mwiko wako
ni nini kwa upande aidha wa chakula. Bila shaka akitueleza kuwa hali nyama ya
Mbawala “Asisile Ukulya Mato” yaani mwiko wake ni kula nyama ya Mbawala, basi
sote tunaafikiana kuwa huyu ni ndugu yetu.
Hivyo Ukoo wa Kivenule uzila kula
nyama ya Mbawala, na huu ndiyo mwiko mkubwa au alama ya utambulisho
tuliyorithishwa na Babu zetu.
Alama nyingine ndani ya Ukoo wa
Kivenule ni ile ya Mwitikio, kwa lugha ya fasaha ya asili yaani Kihehe toka kwa
wakazi wa mkoa wa Iringa tunaita MWIDIKISO. Mwitikio wa Ukoo wa Kivenule ni
MLIGO. Hii ni alama nyingine nyeti inayotambulisha Ukoo wa Kivenule.
Chimbuko la Ukoo wa Kivenule
Chimbuko
la Ukoo wa KIVENULE ni kutoka sehemu ya Malangali iliyopo katika Wilaya ya
Mufindi, kusini mwa mkoani Iringa. Asili ya ukoo wa KIVENULE ni mchanganyiko wa
WAHEHE na WABENA; ambapo mchanganyiko huu hujulikana kama
WABENAMANGA.
WABENAMANGA
wapo katika maeneo mbalimbali mkoniani Iringa ikiwemo Mgololo, Mtwangu, Idunda,
Ilole na kadhalika.
Historia
inaonyesha kwamba, Ubini wa KIVENULE ilikuwa ni zawadi iliyotolewa kwa Ukoo wa
MWIBALAMA au BALAMA kutokana na umaarufu na uhodari wao katika kulenga shabaha
wakati wa mapigano vitani (KWIMIGOHA). MWIBALAMA walikuwa ni Mashujaa katika
Shabaha ya Mishale (MIGOHA) kutokana na kuwatekeleza (kuwaua) maadui katika
hali isiyo ya kawaida tofauti na wapiganaji wengine.
Kitendo
cha kulenga shabaha kikamilifu bila kukosea walikiita KUVENULA. Uhalisia wa
KUVENULA ni kuua kikamilifu maadui katika vita. Kwa hiyo KIVENULE limetokana na
neno KUVENULA na lilipatikana kama Zawadi toka
kwa Wakubwa wa Vita siku hizo za mapigano vitani. KIVENULE ni jina la sifa ya
kuwa na uwezo wa kumvua adui kwa kutumia shabaha ya Mishale (Migoha) bila
vikwazo.
Mzee
TAGAMTWA ambaye alitoka katika Ukoo wa MWIBALAMA alikuwa ni ni mtu na Kaka na TAVIMYENDA
KIVENULE. TAGAMTWA alifia vitani na mwili wake haukuweza kupatikana. Mzee
TAGAMTWA ndiye aliyemzaa SALAMALENGA aliyekwenda kueneza Ukoo wa Kivenule
maeneo ya ILOLE. Kwa maana hiyo, Mzee TAGAMTWA alikuwa ni Baba yake
SALAMALENGA.
Historia
inaonyesha kuwa, Mzee TAVIMYENDA na Mzee SALAMALENGA wakitokea maeneo ya Malangali - Mufindi
walifikia Kalenga, ambapo walikutana na Mzee KIKOTI. KIKOTI alikuwa ana mifugo
yake eneo la MAGUBIKE na ULEFI. Hivyo, KIKOTI alimwomba TAVIMYENDA aende
MAGUBIKE ili aweze kumwangalia mifugo yake. Hali kadhalika Mzee SALAMALENGA
katika kutafuta maisha, aliamua kwenda ILOLE.
TAVIMYENDA
ndiye alieneza ukoo kwa upande wa KIDAMALI na hali kadhalika SALAMALENGA
alifanya hivyo kwa upande wa ILOLE.
Babu
TAVIMYENDA yeye alikuja upande wa Magubike yaani ULEFI enzi hizo. Babu TAVIMYENDA
KIVENULE na Mke wa wake MKAMI waliishi ULEFI na baada ya kufa walizikwa pale
pale ULEFI. Babu SIGATAMBULE KIVENULE pamoja na Babu wengine KAVILIMEMBE
KIVENULE, MGAYIFAIDA KIVENULE, HUSENI KIVENULE na BIBI MGASI walizaliwa katika
eneo la ULEFI - MAGUBIKE. Katika uhai wao muda mwingi waliishi eneo la ULEFI
kabla ya Wazungu kufika wakitafuta eneo la kuishi na wakapewa sehemu ya ULEFI.
Mzungu huyo alikuwa ni JIM, Mgiriki wa kwanza kufika eneo la ULEFI.
Kutokana
na hali hiyo, Babu SIGATAMBULE KIVENULE alihamia sehemu ya MLAFU pamoja na Babu
mwingine MGAYAFAIDA. Kufika MLAFU, Babu SIGATAMBULE alikuna na Mzungu mwingine
aliyeitwa SPELO. Kwa hiyo Wazungu hao wakampimia eneo la MLAFU na hivyo akawa
amepakana na wazungu pande zote. Kwa chini akawa amepakana na Giriki MICHO.
Babu HUSENI KIVENULE yeye alihamia MAGUBIKE.
Maana
halisi ya MAGUBIKE ni kuwa kuna jiwe liliwafunika watu hapo siku za mwanza
ambapo watu walikuwa wanaishi mapangoni.
KIVENULE
waliopo ILOLE na NDULI wa wale waliopo KIDAMALI na MAGUBIKE wote ni asili moja.
MGAWANYIKO WA UKOO WA KIVENULE
1.
Kavilimembe Kivenule Kazikwa Magubike (Me)
2.
Myagafaida Kivenule Kazikwa Mlafu (Me)
3.
Sigatambule Kivenule Kazikwa Mlafu (Me)
4.
Huseni Kivenule Anaishi
Magubike (Me)
5.
Abdalah Kivenule Kazikwa Mlafu (Me)
6.
Sikimbilavi Semabiki Kazikwa Mlafu (Ke)
7.
Mgasi Kivenule Kazikwa Mlafu (Ke)
8.
Sigungilimembe Kivenule Kazikwa Mjini (Ke)
9.
Malibora Kivenule Kazikwa Mkimbizi (Ke)
A: WATOTO WA BABU KAVILIMEMBE KIVENULE
1.
Salikuwaganga Kivenule Anaishi
Nzihi (Ke)
2.
Dalikimali Kivenule Anaishi Nzihi (Ke)
3.
Francis Kivenule Amezikwa Mlafu (Me) (Monica Kivenule)
4.
Pangalasi Kivenule Anaishi Ilula (Me)
5.
Sandra Kivenule Amezikwa
(Ke) (Mama Mapembe)
6.
Elizabert Kivenule Amezikwa (Ke)
B: WATOTO WA BABU MGAYAFAIDA KIVENULE HAKUWA NA FAMILIA
C: WATOTO WA BABU
SIGATAMBULE KIVENULE
WATOTO WA BABU SIGATAMBULE |
||
Bibi SIWANGUMHAVI SINGAILE
|
Bibi NYANYIMALE SINGAILE
|
Bibi PANGULIMALE SETWANGA
|
1.
Gidagumhindi
(Cecilia) Kivenule (Ke)
2. Semyamba (Khadija) Kivenule
(Ke)
3. Sivinitu (Alphonce) Kivenule
(Me)
4. Kadungu (William) Kivenule
(Me)
5. Fibumo (Zavery) Kivenule (Me)
6. Mlagile (Anyesi) Kivenule
(Ke)
7. John Kivenule (Me)
|
1.
Mgulwa
(Mama Agatha) Kivenule(Ke)
2. Luhanage (Ponsiano) Kivenule
(Me)
3. Mgendwa (Eusebio)
Kivenule(Me) Baba Kaini
4. Msinziwa (Daniel)
Kivenule(Me)
5. Kanolo (Edward) Kivenule(Me)
|
1.
Conjeta
Kivenule – Magubike
2. Pyela Kivenule
3. Faustino Kivenule
4. George Kivenule
5. Carolina Kivenule
|
D: WATOTO WA BABU
HUSENI KIVENULE
WATOTO WA BABU HUSEN |
|
Bibi
YIMILENGERESA (Mume yuko) Vitani) SEMSISI
|
Bibi
DALIKA SETALA
|
1.
Nyakudila (Benjamin)
Kivenule(Me) – Gangimali
2.
Sekiyavile (Modesta) (Ke)
Kivenule – Magubike
3.
Dominikus Kivenule (Me) –
Magubike
4.
Emmanuel Kivenule
5.
Luciana Kivenule (Dead)
|
1.
Kabogo (Bernardi) Kivenule
(Me) – Magubike
2.
Sembata (Josephina) Kivenule
(Ke) – Nyamahana
3.
Brandino Kivenule (Me) –
Kidamale
4.
Batromeo Kivenule (Me) (Dead)
5.
Tavina Kivenule (Ke) –
Nyamahana
6.
Masikitiko Kivenule (Dead)
|
1.
Gisapa Kigereso (Ke) [dead]
2.
Sinatoga Kigereso (Ke)
3.
Mtogapawene Kigereso
(Ke) [dead]
4.
Chesilemungu Kigereso
(Ke) [dead]
5.
Ronjino Kigereso (Me) [dead]
MGAWANYIKO WA UKOO WA TAGAMTWA
MWIBALAMA
1.
CHOGAVANU KIVENULE
2.
PANGAYENA KIVENULE
3.
JONAS KIVENULE
4.
SAMWEL KIVENULE
5.
MUNGUATOSA KIVENULE
6.
GALASAMANENO KIVENULE
7.
WILLIAM KIVENULE
8.
TINDASULANGA KIVENULE
9.
GUNGAMESA KIVENULE
10.
SIGONGOLA KIVENULE
11.
SHABAN KIVENULE
12.
BARTON KIVENULE
1.
CHAGAVANU S. KIVENULE
1.
NOSOLO C. KIVENULE
2.
MADESTUS C. KIVENULE
3.
PAULINA C. KIVENULE
2. PANGAYENA S. KIVENULE
1.
GWELINO P. KIVENULE
2.
PASCAL P. KIVENULE
3.
STELINA P. KIVENULE
4.
PAUSTINA P. KIVENULE
5.
BERNADI P. KIVENULE
6.
CHELINA P. KIVENULE
7.
IGNUS P. KIVENULE
8.
CONSOLATA P. KIVENULE
9.
RAPHAEL P. KIVENULE
1. GWELINO P. KIVENULE
1.
Fausta G. Kivenule
2.
Julius G. Kivenule
3.
Delia G. Kivenule
4.
Vasisile G. Kivenule
5.
Christopher G. Kivenule
6.
Farida G. Kivenule
7.
Michael G. Kivenule
8.
Machelina G. Kivenule
9.
Stumai G. Kivenule
10.
Philimon G. Kivenule
11.
Lugina G. Kivenule
12.
Agnes G. Kivenule
13.
Anitha G. Kivenule
14.
Frola G. Kivenule
15.
Bosco G. Kivenule
16.
Olive G. Kivenule
17.
Tegemeo G. Kivenule
18.
Yovita G. Kivenule
2. PASCAL P. KIVENULE
1.
Mage P. Kivenule
2.
Seuginge P. Kivenule
3. STELINA P. KIVENULE
1.
Eluda Nyemba
2.
Anjila Nyemba
4. PAUSTINA P. KIVENULE
1.
Yudita Kiteve
2.
Daniel Kiteve
3.
Etta Kiteve
4.
Wuliana Kiteve
5.
Kalumelita Mkeng’e
6.
Charles Kiteve
7.
Valendino Mkeng’e
5. BERNADI P. KIVENULE
1.
Damas B. Kivenule
2.
Kamimi B. Kivenule
3.
Laheli B. Kivenule
4.
Kalo B. Kivenule
5.
Kulwa B. Kivenule
Damas B. Kivenule
·
Nasuma D. Kivenule
6. CHELINA P. KIVENULE
1.
Tecla Kisumbe
2.
Gibson Kitu
3.
Carson Kisumbe
4.
Lilian Kisumbe
5.
Elasto Kisumbe
7. CONSOLATA P. KIVENULE
1.
Colado Ngwenga
2.
Sixtus Ngwenga
3.
Thdey Ngwenga
4.
Felista Ngwenga
5.
Stani Ngwenga
8. IGNUS P. KIVENULE
1.
Pelis I. Kivenule
2.
Bernadelt I. Kivenule
3.
Theopista I. Kivenule
4.
Vestina I. Kivenule
5.
Lilian I. Kivenule
9. RAPHAEL P. KIVENULE
1.
Geofrey R. Kivenule
2.
Muhomela R. Kivenule
3. SAMWEL S. KIVENULE
1.
MARTIN S. KIVENULE
2.
LUCAS S. KIVENULE
3.
ALOYCE S. KIVENULE
4.
ERENESTO S. KIVENULE
5.
INNOCENT S. KIVENULE
6.
MICHAEL S. KIVENULE
7.
MONICA S. KIVENULE
8.
ANNA S. KIVENULE
9.
ANNETA S. KIVENULE
10.
FELINA S. KIVENULE
1. MARTIN S. KIVENULE
1.
Anesia M. Kivenule
2.
Festo M. Kivenule
3.
Msso M. Kivenule
4.
Nelson M. Kivenule
5.
Saida M. Kivenule
6.
Neema M. Kivenule
7.
Faraja M. Kivenule
8.
Teresia M. Kivenule
2. LUCAS S. KIVENULE
1.
Efrehem L. Kivenule
2.
Uzuni L. Kivenule
3.
Kibanile L. Kivenule
3. ALOIS S. KIVENULE
1.
Kissa A. Kivenule
2.
Zawadi A. Kivenule
3.
Siwazuki A. Kivenule
4.
Sitamini A. Kivenule
5.
Levina A. Kivenule
6.
Asha A. Kivenule
4. ERENESTO S. KIVENULE
5. INNOCENT S. KIVENULE
1.
Vicky I. Kivenule
2.
Frank I. Kivenule
3.
Magreth I. Kivenule
4.
Grace I. Kivenule
5.
Emmanuel I. Kivenule
6. MICHAEL S. KIVENULE
7. MONIKA S. KIVENULE
8. ANNA S. KIVENULE
9. ANNETA S. KIVENULE
10. FELINA S. KIVENULE
4. JONAS S. KIVENULE
1.
TITUS J. KIVENULE
2.
PAULO J. KIVENULE
3.
EMMNUEL J. KIVENULE
4.
ANALOIDA J. KIVENULE
5.
ARDO J. KIVENULE
6.
EMILYANA J. KIVENULE
7.
GWIDO J. KIVENULE
8.
JONISIA J. KIVENULE
9.
PIUS J. KIVENULE
10.
EMILYO J. KIVENULE
1. TITUS J. KIVENULE
1.
Yustina T. Kivenule
2.
Evaristo T. Kivenule
3.
Castory T. Kivenule
4.
Atanasi T. Kivenule
5.
Patricia T. Kivenule
6.
Jachinda T. Kivenule
7.
Johakimu T. Kivenule
8.
Letisia T. Kivenule
2. EMILYO J. KIVENULE
1.
Jamila E. Kivenule
2.
Dolla E. Kivenule
3.
Mwahen E. Kivenule
3. PIUS J. KIVENULE
1.
Frank P Kivenule
2.
Fotte P. Kivenule
3.
Verlo P. Kivenule
4.
Mkutwa P. Kivenule
5.
Niva P. Kivenule
4. PAULO J. KIVENULE
1.
Costandino P. Kivenule
2.
Lenzia P. Kivenule
5. ARDO J. KIVENULE
1.
Lembula A. Kivenule
2.
Kandia A. Kivenule
6. EMMANUEL J. KIVENULE
1.
Mgilinde E. Kivenule
7. GWIDO J. KIVENULE
1.
Sikweli G. Kivenule
2.
Frida G. Kivenule
3.
Reginandi G. Kivenule
ANALOIDA J. KIVENULE
1.
Fahamu A. Kivenule
2.
Rojasi A. Kivenule
5. MUNGUATOSA S. KIVENULE
1.
MARIAM M. KIVENULE
2.
6. GALASAMANENO S. KIVENULE
1.
CHELINA G. KIVENULE
2.
DOMINICUS G. KIVENULE
3.
DAVID G. KIVENULE
7.
WILLIAM S. KIVENULE
1.
MUSA W. KIVENULE
2.
HASSAN W. KIVENULE
3.
ANSEREM W. KIVENULE
4.
PAULINA W. KIVENULE
5.
YESOFINA W. KIVENULE
6.
RIDIA W. KIVENULE
8.
TINDASULANGA S. KIVENULE
9.
GUNGAMESA S. KIVENULE
10.
SIGONGOLA S. KIVENULE
11. SHABAN S. KIVENULE
1.
AUGUSTINO S. KIVENULE
12. BURTON S. KIVENULE
1.
MASUDI B. KIVENULE
2.
STEPHAN B. KIVENULE
3.
JOHN B. KIVENULE
4.
BONIPHASI B. KIVENULE
5.
FABIAN B. KIVENULE
6.
LOSINA B. KIVENULE
7.
MALUKUS B. KIVENULE
8.
JULIO B. KIVENULE
MALUKUSI B. KIVENULE
1.
Jalibu M. Kivenule
2.
Kulwa M. Kivenule
3.
Doto M. Kivenule
4.
Fatuma M. Kivenule
JULIO B. KIVENULE
1.
Siyaleo J. Kivenule
2.
Gude J. Kivenule
3.
Tuma J. Kivenule
4.
Monika J. Kivenule
5.
Pelida J. Kivenule
6.
Kulusumu J. Kivenule
7.
Ajina J. Kivenule
8.
Vailes J. Kivenule
MASUDI B. KIVENULE
1.
Evaristo M. Kivenule
2.
Shedlack M. Kivenule
STEPHAN B. KIVENULE
1.
Aida S. Kivenule
2.
Rajabu S. Kivenule
3.
Kimbembe S. Kivenule
4.
Ambaa S. Kivenule
5.
Fanula S. Kivenule
JOHN B. KIVENULE
1.
Wick J. Kivenule
2.
Simbion J. Kivenule
3.
Mtitu J. Kivenule
KUPOTEA KWA UKOO
Siku
zote katika harakati za kutafuta maisha, ukoo hujikuta unajitenga na mazingira
yake ya asili, yaani nyumbani na kujikuta ukoo husika upo sehemu nyingine.
Sababu kubwa ya ukoo kuwa sehemu nyingine ni kutafuta mkate wa kila siku;
lakini pia kutafuta unafuu wa uchumi na kupata maendeleo ya kuendesha familia
zao.
Siwezi
kusema moja kwa moja kuwa kuna kupotea kwa ukoo; isipokuwa wanandugu siku zote
hupuuzia mawasiliano baina ya wanandugu na kuweka/kujenga ukuta baina yao na hivyo kufanya ndugu
wawe na mfumo mbaya wa mawasiliano. Kutokuwa na mawasiliano huleta matatizo
mengine kama vile kutosaidiana pindi shida
zinapotokea na pia kutokujua upande mwingine wanafanya nini!
Mfumo
huu dume wa kutotafuta mtandao wa mawasiliano na kutokuwa karibu baina ya
wanandugu huleta mgawanyiko, na tabaka ndani ya ukoo, lakini mbaya ziaid
kutakuwa na pengo kubwa la maendeleo baina ndugu yaani wenye nacho na wasio
nacho. Hivyo basi japokuwa wanandugu tunaishi maeneo tofauti tofauti hatuna
budi kuimarisha mtandao wa mawasiliano na kuwa karibu siku zote. Kuna usemi wa
Kiingereza usemao: “People are lonely because they build walls instead of
bridges”. Kwa lugha rahisi ya hapa kwetu ni kwamba “Avanu vakivakwa kuva
vasengite ulukanzi badala ya kisumbo au kilowoko”!!!... Na kwa nini tujenge
ukuta baina yetu?!!!. Hatuna budi tujenge daraja litakalotuunganisha yaani
tuweze kuvuka kutoka upande mmoja hadi mwingine ili tuweze kufahamu upande
mwingine wanafanya nini cha katika kujiletea maendeleo.
HASARA ZA KUPOTEA KWA UKOO
Kuna
hasara nyingi zipo ambazo tunaweza kuzipata endapo ukoo utapotea; kati ya
hasara hizo ni pamoja na:
§
Kuleta umaskini na
ndugu/mwanaukoo kuwa tegemezi; kwa mfano ndugu aliyetoka nyumbani kwenda Kigoma
au popote kwa miaka mingi; hivyo anapoteza mawasiliano na wenzake, pindi maisha
yanapomuelemea basi anaanza kuwa omba omba. Kwa sababu hana msaada wa karibu
kutoka kwa wanandugu.
§
Kudumaa kimaendeleo kwa sababu
ya kuridhika na mfumo mmoja wa maisha. Hakuna ushindani wa maendeleo kwa sababu
hajifunzi kwa ndugu wenine kutokana na hatua za maendeleo walizozifikia.
Matokeo yake ndugu anaridhika na kujipa moyo eti kwa sababu yupo ugenini na
hana shida.
§
Kuna hatari kubwa ya kujiingiza
katika matukio mabaya mfano ujambazi, utumiaji wa madawa ya kulevya kama bangi, cocaine, mandrax na kujidunga sindano. Pia
ndugu huwa katika nafasi ya kujihusisha na uasherati au umalaya katika
madangulo (kasino).
§
Hukosa msaada tosha wa mawazo na
hata jeki ya kujiletea maendeleo
§
Kutokea kwa mgongano wa mapenzi.
Hii inamaanisha kwambaa vijana ndani ya ukoo wanaweza kujikuta wanatafutana wao
kwa wao ndani ya ukoo, kwa sababu wote wapo ugenini kwa muda mrefu na hawana
mawasiliano na nyumbani kwao.
FAIDA ZA WANAUKOO KUWA KARIBU
Faida
ambazo wanaukoo wanaweza kuzipata kama
watakuwa karibu ni pamoja na:
§
Kudumisha undugu na upendo baina
ya wanandugu ndani ya ukoo.
§
Huchochea maendeleo ya kasi
ndani ya wanaukoo kwa kuangalia ndugu mwingine anafanya nini, na pia ndugu nao kujifunza
kutoka kwake na kuomba mawazo kutoka kwake au kwa wengine.
§
Hupunguza ugumu wa tatizo, na
kuonekana tatizo ni dogo na lenye kutatulika endapo kuna ushirikiano wa dhati
ndani ya wanandugu. Hii ni kwa sababu wanandugu ni kitu kimoja na mtu
kuchukulia tatizo la mwenzake kuwa lake
mfano wa jamii zilizopiga
hatua katika hili ni Wahindi, Waarabu na hapa nyumbani kwetuTanzania ni
Wachaga. Familia nyingi katika jamii hii wamepiga hatua katika maendeleo.
§
Ni rahisi kuanzisha miradi ya
pamoja ya maendeleo kwa kuwa tunakuwa na itikadi zenye mlengo mmoja na wa
kufanana; tofauti na kuwa na mradi na mtu tofauti msiyejuana, inaleta utata na
ugumu zaidi.
Ni
vizuri wanaukoo wakaanza kuwa kitu kimoja kuanzia sasa. Tuache tofauti baina
yetu. Tumwombe Mwenyezi Mungu atujalie roho ya kuwapenda wengine na kuwapenda
ndugu zetu kama tunavyojipenda sisi. Tuwe tayari
kuwasaidia ndugu wanaoelemewa na maisha, tuwape fara na msaada wa vitu na hata
mawazo katika kuhakikisha kila mmoja anapta unafuu wa maisha.
MAJADILIANO YA KWENYE VIKUNDI
KUNDI
NA. 1
Ukoo
ni Nini?
Ukoo huanza na mtu mmoja, ambaye huzaa watoto na pia watoto
nao kuwa na familia zao (yaani nao kuzaa watoto). Mwishoni muunganiko huu huwa
ni kitu kimoja ambacho ni Ukoo.
§
Kuoa au
kuolewa ndiyo msingi mkubwa wa kuwa au kuunda Ukoo kwa sababu kuoa au kuolewa
ndiko kunakojenga familia ambazo zinachangia kupatikana kwa Ukoo.
§
Ukoo pia
unaweza kuenea hata nje ya mipaka mfano Ulaya, America na kwingineko
ulimwenguni.
KUNDI
NA. 2
Kuenea
kwa Ukoo
Maana yake ni
§
Mtu yupo
mahali fulani, ukamtembelea mfano Mbeya, Dar es Salaam, Kenya na kwingineko.
§
Mtu yupo
mahali fulani lakini usitake kumtembelea.
Kuenea/Kukua
kwa Ukoo
§
Kuoa au Kuolewa
§
Kufahamiana
§
Elimu/Kusoma kutapelekea
kujulikana
§
Kusaidiana na kushirikiana
§
Mawasiliano, mfano mtu wa
Mwanza, alioa na akaleta mawasiliano kuwa ana mtoto Mwanza na kumleta.
KUNDI NA. 3
Mgawanyiko wa Ukoo
|
|
§
Watoto kujaliana upande wa mama
na si upande wa baba ambaye ni mwanzo wa ukoo.
§
Kuongeza matawi na Kidamali pawe
ni mzizi wa ukoo.
§
Wanawake wapunguze tofauti kwani
wao ndiyo chanzo cha kuugawa ukoo.l
Katika
kuunganisha mgawanyiko huu wa Ukoo ni Mawasiliano baina ndugu wanaoishi sehemu
mbalimbali. Mfano katika kipindi hiki mawasiliano ya simu za mkononi yameenea
kila mahali, cha msingi ni kuwa na mkakati thabiti katika kuhakikisha kuwa
ndugu wanakuwa na mawasiliano yaliyo sahihi. Bila kuwa na mawasiliano ina maana
kuwa tunakuwa tumejiwekea ukuta mnene wa kututenganisha wanaukoo.
KUNDI NA. 4
Kupotea kwa Ukoo
Kupotea
kwa ukoo husababishwa na sababu kadha wa kadha mojawapo zikiwa zimeainishwa
hapa chini:
§
Kutosaidiana katika shida
mbalimbali mfano misiba na ugonjwa.
§
Kutotembeleana toka sehemu moja
hadi sehemu nyingine mfano ndugu mmoja anakaa Morogoro na ndugu mwingine anakaa
Dar es Salaam,
Tabora na kadhalika.
§
Kudharauliana kutokana na
kutofautiana katika kipato (fedha), umaskini, utajiri na elimu.
§
Kukosekana kwa mawasiliano mfano
kupigiana simu; kutotambulishana na kutotembeleana.
§
Watoto kutotembelea kwa ndugu.
§
Wanawake wanaoolewa kwenye ukoo
kutotembeleana
§
Maskini wasio na kipato (hana
kitu) kuona aibu kufika kwa ndugu mwenye uwezo (kipato kizuri) bila ya kufahamu
kuwa wote ni ndugu wa ukoo mmoja.
§
Kupeana taarifa mapema za
matatizo kwa ndugu wote ili tuwe kitu kimoja.
Jambo
la msingi kufanyika katika kuhakikisha kuwa Ukoo haupotei ni kuundwa kwa Kamati
itakayoratibu matatizo ya Ukoo pamoja na wanandugu.
MADA
YA PILI
MAHUSIANO BAINA YA WANANDUGU
NDANI YA UKOO
Utangulizi
Maana
ya Mahusiano ni hali ya ukaribu, ujirani, urafiki, umoja au ushirikiano
unaojengeka baina ya Ndugu, Jamaa au Marafiki. Mahusiano ni hali ya kuwa pamoja
Kifikra, Kimwili, Kimawasiliano, Kiimani, Kiitikadi, Kimaendeleo, Kikazi,
Kijamii na Kimichezo.
Mahusiano
hujengwa kwa misingi/namna mbalimbali. Baadhi ya njia au vitu vinavyosababisha
kukawepo na mahusiano ni pamoja na:
1. Ujirani: Ujirani mara nyingi katika
jamii zetu huchangia sana
katika kujenga Mahusiano. Mahusiano yenyewe huonekana katika sura mbili
tofauti. Yaani Mahusiano Mazuri kwa maana ya Sura Nzuri au Mahusiano Mabaya kwa
maana ya Sura ya Ubaya.
2. Undugu: Hii ni aina ya nyingine ya
Mahusiano ambapo ndugu wa Damu Moja au wanachangia damu, hujenga Mahusiano ya Moja
kwa Moja (Automatic Relationship). Mara nyingi Mahusiano ya aina hii huwa na
Sura ya Uzuri zaidi (Mahusiano Mazuri). Japo kuna kipindi Fulani hata Sura ya
Ubaya (Mahusiano Mabaya) hujitokeza.
3. Imani: Pia watu huweza kujenga
Mahusiano kupitia Imani zao, mfano watu wanaoabudu katika dhehebu moja huweza
kujenga mahusiano ya aina yao
tofauti na dhehebu jingine. Mara nyingi Mahusiano ya Kiimani huwa na mwelekeo
wa Mahusiano mema. Mahusiano mabaya mara nyingine hutokea na hata kusababisha
vita vya kiimani (dini).
4. Itikadi: Mahusiano ya Kiitikadi nayo
hujengeka kwa kufuata Mlengo wa Vyama Vyao. Na zaidi Mahusiano ya Kiitikadi
huegemea zaidi kwenye siasa na hupungua au kutoweka kabisa baada ya mmoja wao
kubadili Itikadi yake yaani kuhama toka chama cha kimoja cha siasa na kwenye
chama kingine cha siasa. Mahusiano ya Kiitikadi hujengwa kwa misingi ya Chuki,
Fitina na Vitisho baina wa watu wa Itikadi moja na wale wa Itikadi nyingine.
5. Maendeleo: Watu wenye hali fulani ya
kimaendeleo huweza kujenga aina fulani ya mahusiano yenye nia ya kuinuia hali
zao za kimaisha. Na mara nyingi wanaojumuika hapa ni wale ambao tayari
wameonesha nia na mwelekeo. Lakini pia hata wale waliopiga hatua kimaendeleo
huweza kuja mahusiano yao
yakiwa nia ya kuimarisha hali walizonazo. Msingi mkubwa wa mahusiano ya aina
hii huwa ni kupeana mbinu na mikakati ya kuleta au kujiimarisha zaidi katika
maendeleo ambayo wanayatarajia au ambayo wamekwisha yapata.
Pia
hata kwa upande wa wale wenye hali duni ya kimaendeleo nao hujenga aina Fulani
ya mahusiano kulingana na hali na uwezo wao. Kasoro ambayo hujitokeza hapa huwa
ni mahusiano duni baina wenye uwezo (matajiri) na wale na wasio na uwezo
(maskini). Katika kujiimarisha zaidi kimaendeleo, maskini huwa mtumishi
(kibarua) na tajiri huwa mtumikiwa (mtwana).
6. Elimu: Watu wenye elimu nao mara
nyining hujenga mahusiano yao.
Mara nyingi katika mahusiano yao
huwatenga wale wenye elimu kidogo au wasio na elimu kabisa. Hii hutokea zaidi
kwa wale waliobahatika kupata Elimu ya Juu mfano Chuo Kikuu. Mazungumzo na
mipango yao
huwatenga zaidi wale wenye elimu kidogo. Kuwatenga hujitokeza katika matumizi
ya lugha za kigeni, kutowashirikisha katika mawazo mbalimbali ambayo wanadhani
yanaweza kuwainua watu wa hali zote (wasomi na wasio wsomi).
AINA ZA MAHUSIANO
Kuna
aina mbalimbali za mahusiano, lakini tunaweza kugawanya mahusiano haya katika
sehemu kuu mbili.
1. Mahusiano Mazuri; na
2. Mahusiano Mabaya.
Aina
mbalimbali za mahusiano ambayo yapo katika jamii zetu ni pamoja na mahusiano
ya:
§
Kikazi;
§
Kijamii;
§
Kisiasa; na
§
Kiuchumi.
MAHUSIANO MAZURI
Mahusiano
Mazuri ni hali ya kuwa pamoja kwa kushirikiana katika nyanja mbalimbali za
maisha. Mahusiano Mazuri huwa katika shida au raha. Raha hujumuisha hali zozote
zenye kuashiria mafanikio na maendeleo katika maisha ya binadamu. Hii ni pamoja
na kufaulu mitihani mbalimbali ya darasani na ya maisha; kujenga nyumba,
kununua gari, kapata kazi nzuri, kufanikiwa katika kilimo, Jubilei, kupandishwa
cheo pamoja na kupata nishani.
Shida
huwa ni hali ya kuwa na mashaka, kutokuwa na uhakika wa maisha, kutokuwa na
kipato, kutofanikiwa katika elimu, ugonjwa, misongamano (Depression), misusuko
(stress), kutokuwa na ajira, kutofadhiliwa kwa hali yoyote (Promotion au
Scholarship) na kadhalika.
MAHUSIANO MABAYA
Mahusiano
Mabaya ni hali ya kutokuwa na ushirikiano, huruma au wema katika nyanja
mbalimbali za maisha. Mahusiano Mabaya nayo hali kadhalika huwa katika ubaya au
uzuri au shida na raha. Tofauti na katika Mahusiano Mazuri, Mahusiano Mabaya
hubaki kuwa ni swa katika shida na raha. Kwa ujumla ushirikiano na mawasiliano
hukosekana kabisa. Huwa hakuna huruma, maelewano, kuvumiliana na kuwasiliana.
Kikubwa
ambacho hujengeka ni chuki, majivuno, wivu, ugomvi na kutakiana shari. Hamna
hata mmojawapo ambaye huombewa kheri. Kwa yule aliyenacho, huombea au hutamaini
yeye aendelee kuwa nacho peke yake na kutomwombea kheri ya kupata yule ambaye
hana kitu.
Na
kwa yule ambaye hana, humwombea shari, bahati mbaya kupotteza au kwa namna
yoyote ambayo haina kheri kwa yule ambaye anacho. Baadhi huomba mfano kama ni
gari lipate ajari, nyumba iungue na kama
anasoma anafeli. Katika aina hii ya mahusiano hakuna nafasi ya kutakiana mema
au maendeleo.
MAHUSIANO BAINA YA NDUGU NDANI
YA UKOO
Ukoo
wa Kivenule ni mkubwa sana
na kwa haraka unakadiriwa kuwa na ndugu karibia elfu mbili (2000). Ni ukoo
ambao unaweza kufanya mambo makubwa na ya kimaendeleo kama
utaungana na kuwa kitu kimoja.
Tatizo
kubwa ambalo linaonekana kwa wanaukoo ni kuwa na mwamko mdogo. Kwa mfano
wanaukoo wanaohudhuria Mkutano Mkuu wa Kwanza
wa Ukoo wa Kivenule ni theluthi au robot u ya wanaukoo wote. Tumaini la Kamati
za Maandalizi ya MKutano Mkuu ni kuhudhuriwa na Ndugu pamoja na Wanaukoo wa
Kivenule kwa wingi zaidi.
Kwa
upande wa Dar es Salaam, mwamko wao ni mdogo sana. Tumaini na tegemeo
la awali ilikuwa Dar es Salaam
ingekuwa ni mfano, lakini imeshindika na hii ndiyo hali halisi. Tunasikitika na
Kamati ya maandalizi ya Dar es Salaam
inaomba samahani.
Kwa
wanaukoo toka Ilole, nao wamesema tatizo kubwa kwao ni suala na nauli kuwa ni kubwa.
Lakini cha msingi kufanyika ni kuzidi kuwahamasisha na kuwapa mojyo wa kutambua
umuhimu wa Mkutano Mkuu wa Ukoo pamoja na mikutano mingine.
Katika
suala zima la mahusiano, ukaribu wa wanandugu na wanaukoo linaangaliwa kwa
karibu zaidi. Mahusiano yanagusa mambo muhimu katika maisha ya kila siku mfano
Elimu, Ugonjwa, Vifo pamoja na Starehe (Harusi, Send-Off, Kipaimara na
Komunio). Elimu ni muhimu sana
kwani inaongeza upeo na ufahamu wa kuweza kukabiliana na matatizo ya maisha ya
kila siku.
Suala
jingine ni ushirikiano katika nyanja mbalimbali mfano Biashara, kazi na kilimo.
Hapa tunamaanisha kuunda kikundi ambacho kitakuwa na mfuko utakaokuwa
unachangiwa na watu mbalimbali kulingana na shughuli na kipato.
Katika
kujenga mahusiano imara, kutembeleana ni muhimu sana. Faida ya kutembeleana ni kujuliana
hali, kusaidiana, kushauriana na kupeana mbinu na mwongozo wa kufauli katika
maisha. Pia katika kutembeleana huwapa fursa wanaukoo/ndugu kuangalia mazingira
mapya anayotembelea kama yanaweza kumfaa
kuishi akilinganisha na mazingira aliyotoka.
Pia
katika kushirikiana kuna haja ya kuwashawishi na kuwabembeleza wale wasio na
uwezo ikiwa ni pamoja na kuwapa moyo, kuwashauri waondoe aibu na wajenge tabia
ya kushirikiana. Katika kushirikiana inakuwa ni rahisi kuweza kutatua matatizo
mbalimbali baina ya wenye nacho na wasionacho.
Kwa
mfano katika shughuli nzima ya kuandaa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa
Kivenule, inakuwa kitu kizuri na mfano kwa wengine kama
tutaonyesha kwa vitendo haya tunayozungumza hapa. Hii utaufanya Mkutano Mkuu
kuwa na maana sana.
Kivenule kwa tabia ni wapole sana
na wenye huruma. Ni vizuri tuwajali wenzetu kwa sababu hali zetu zinajulikana.
Cha msingi ni kuwa karibu na kusaidiana.
Mahusiano
ambayo ukoo wa Kivenule utarajie ni kama haya ya kuitikia kuja kwenye Mkutano
Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Bila kuwa
na hatua madhubuti ukoo utaparaganyika. Katika vitabu vya dini kuna mfano mmoja
unasema “Mtu mmoja aliandaa sherehe na akaalika watu kwenda kula, lakini watu
wakakataa”. Kwa nini watu walikataa kwenda kula. Kila mmoja ana sababu zake.
Mungu awabariki kwa kukubali mwaliko huu.
Tafsiri
sahihi ya mahusiano ipo katika maeneo mbalimbali kama
ilivyoainishwa pale mwanzo. Kila mwanaukoo anawajibika na anawajibu kushiriki
kikamilifu katika hilo.
Mahusiano mazuri huleta upendano ambao huwa ni chachu ya maendeleo.
Umuhimu
wa kuwa na mahusiano mazuri baina ya wanandugu ni kuulinda ukoo na kupunguza
maingiliano kutokana na wanaukoo kutawanyika maeneo mbalimbali ndani ya mipaka
na nje ya mipaka. Katika Mkutano huu Mkuu wa Kwanza
wa Ukoo wa Kivenule, ndugu na wanaukoo kwa ujumla ni walengwa na wanufaikaji.
Katika
suala zima la mahusiano ndani ya Ukoo wa Kivenule, kinachoepukwa hapa ni
mgawanyiko wenye mwenendo wa tofauti ya kipato. Lengo mahsusi ni kuangalia kwa
nini tunafanya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo
wa Kivenule? Hapa tunachoangalia ni mguso wa kila hali baina ya wanandugu na
wanaukoo kwa ujumla kuwa sisi wote wanaukoo ni kitu kimoja. Hivyo tuwe wepesi
katika kutoa misaada wakati wenzetu wana matatizo ya ugonjwa, njaa na vifo.
Lakini pia, ni vema kushirikiana na kutoa misaada katika shughuli za furaha kama kufanya harusi, kipaimara na komunio.
Wanaukoo
wote wanatahadharishwa, baada ya mwaka mmoja wasipotee kwa sababu na visingizio
mbalimbali. Tutumie chombo hiki cha Mkutano wa Ukoo kutoa michango yetu ya
mawazo, dukuduku na hamasa ya kuwa na ukoo imara.
MAJADILIANO KWENYE MAKUNDI
KUNDI NA. 1
Ukaribu wa Wanandugu
1.
Ushirikiano wa wanandugu upo katika
shida mbalimbali
2.
Kujitolea na kujituma kama
mwanandugu kusaidia na kuchangia kwa hali na mali
shughuli mbalimbali za Ukoo mfano misiba, ugonjwa na maandalizi ya mikutano kama huu Mkuu.
3.
Kushawishi ndugu wengine ambao
hawajawa na mwamko au habari kuhusiana na kuwepo kwa Mkutano Mkuu wa Ukoo wa
Kivenule
4.
Kudumisha mahusiano mema baina
ya wanandugu
KUNDI NA. 2
Ushirikiano
katika Nyanja Mbalimbali
1.
Elimu:
Tuaangalie uwezekano wa kusaidiana katika kupata na kuinue kiwango cha Elimu
katika Ukoo bila kujali kipato kwa kujitoa zaidi.
2.
Tuondoe
aibu ya kuomba msaada. Toa shida zako kwa ndugu zako ili tusaidiane katika
kuzitatua.
3.
Tuondoe
ukiritimba katika kuchangia hasa katika ugonjwa. Tusaidiane
katika ugonjwa.
4.
Iundwe Kamati ili iwe na
mwelekeo kamili wa kuuinua ukoo.
5.
Tupeane taarifa wakati wa
matatizo ili kila ndugu awe na taarifa na ashiriki kikamilifu.
6.
Hata katika
starehe zetu pia tusaidiane mfano Harusi.
7.
Tutangulize
utu mioyoni mwetu kabla ya pesa (tuwe na moyo wa kusaidiana na kufarijiana)
8.
Tusibaguane,
tusiangalie kipato. Wewe mwenye kipato tumie muda wako kumsaidia asiye na
kipato.
KUNDI
NA. 3
Kusaidiana na
Kutembeleana
1.
Huwezi kumfahamu au kumjua ndugu
yako kama ana matatizo au la hasha kama
hujamtembelea.
2.
Ujali zaidi ndugu kuliko kujali kipato
chao
3.
Eleza hali halisi ya matatizo
uliyonayo hasa pale ukitemblewa na ndugu zako.
4.
Ukiona ndugu yako anadorora
katika maisha, hasa pale unapomtembelea basi mpe mawazo ya kumjenga ili naye
apige hatua ya maendeleo.
KUNDI
NA. 4
Kuondoa Tofauti Baina ya
Ndugu
1.
Matatizo yanayoleta migogoro
ndani ya ukoo yatatuliwe mapema zaidi.
2.
Tupanue wigo wa kusaidiana ndani
ya familia bila kujali huyu tupo tumbo moja au hapana.
3.
Kila eneo liwe na kamati ya
mipango ya kuratibu matatizo ndani ya ukoo.
4.
Kuacha ubinafsi; tuache ubinafsi
ndani ya ukoo.
5.
Mtu alishukuru kwa kusaidiwa
ndani ya ukoo, jambo hili litusaidie hata kwa sisi wanaukoo kuwasaidia wengine.
6.
Haki itendeke sawa katika
kupanga maamuzi bila kujali huyu ni msomi, hana kipato, mzuri n.k. tukifanikiwa
hili, ukoo utakwenda mbali.
7.
Wazazi wawe waangalifu katika
kutoa maamuzi kwa watoto wao, bila kupendelea mtoto na kadhalika.
8.
Tuwekane sawa bila kujali huyu
ni nani, tuambiane ukweli katika mkutano huu.
9.
Watu ndani ya ukoo wanene kwa
vinywa vyao kama kuna tofauti baina ya ndugu
ili tuweze kuondoa tofauti ndani ya Mkutano huu.
10.
Tutoe matatizo yetu leo, ili
kesho tupate majumuisho. Hivyo mtu (mwanandugu) awe huru kuongea na awe huru
katika maisha yake ya kila siku.
MAJUMUISHO
§
Tusaidiane katika nyanja mbalimbali iwe katika
Elimu, Ajira, maisha na kwingineko. Tuige mfano wa Wachaga katika kusaidiana.
§
Tofauti ya maisha baina ya
wanandugu ni kitu cha kawaida, hata vidole havipo sawa.
§
Tunapojenga nguvu ya wanandugu
tuondoe matabaka.
§
Hapa hapa Kidamali ndugu
hawaelewani, tatizo hili ni kubwa sana, hata
ndugu yako wa karibu hawezi akasema, leta watoto wapate chakula kwangu kama ilivyokuwa siku za nyuma.
MADA
YA TATU
ELIMU NA MUSTAKABALI WA UKOO
Elimu
ni kitu cha msingi sana
katika maisha ya binadamu. Elimu ni mwongozo wa fikra za binadamu katika
kuyamudu, kuyatambua, kuyadhibiti na kuyatawala mazingira ya aina yoyote
yanayomzunguka. Elimu ni dira katika maisha yetu ya kila siku. Elimu inasaidia
katika utambuzi na ufahamu wa mambo mengi katika maisha yetu ya kila siku.
Zamani
koo nyingi hapa kwetu zilipuuza sana
Elimu. Umuhimu wa Elimu haukuzingatiwa kabisa. Idadi ya watu waliosoma kadri
siku zinavyozidi kwenda mbele ilipungua na imeendelea kupungua sana na hivyo kufanya
kiwango cha elimu pia kupungua katika jamii zetu. Kukosa Elimu kumewakosesha
wanaukoo nafasi katika sekta mbalimbali za kimaendeleo mfano sekta ya binafsi,
sekta ya umma (serikali) na sekta za kijamii (jamii huria).
Ukoo
wa Kivenule una vipaji vingi, lakini Elimu inaweza kuwa ni kikwazo cha
mafanikio. Kukosekana kwa elimu pengine kunasababisha jamii ya Kivenule kushindwa
kuwa mahusiano (interaction) na jamii nyingine katika kujiletea maendeleo na
hasa kutokana na kukua kwa Sayansi na Teknolojia au vinginevyo. Mabadiliko ya
sayansi na teknolojiayanauweka Ukoo wa Kivenule njiapanda na hivyo kupoteza
mwelekeo.
NAFASI YA UKOO WA KIVENULE KATIKA ELIMU
1.
Tumegundua kuwa
nafasi ya ukoo wa Kivenule katika elimu ni mdogo au upo chini kwa sababu:
·
Nafasi za ajira
katika maofisi makubwa serikalini ni mdogo.
·
Wanaukoo wachache
wamepaa ajira katika mashirika makubwa (umma au binafsi) yanayozingatia kiwango
elimu katika ajira.
2.
Kuwa na idadi
ndogo ya wanaukoo waliofikia elimu ya kiwango cha juu mfano kidato cha 4, 6
mpaka vyuo vikuu.
3.
Wanaukoo kutojua
umuhimu wa elimu.
Ili ukoo uwe na nafasi elimu tufanyaje?
·
Tujitahidi
kusomesha watoto wetu hadi elimu ya juu.
·
Elimu ya ufundi
pia ni muhimu ndani ya ukoo.
·
Tuunde kamati
katika ukoo itkayoratibu sula zima la ukoo.
·
Kukusaya michango
kuwasaidia waso na uwezo wa kusomesha.
·
Kuwasaidia kusoma
watoto wa ukoo wasio na msaada.
·
Kuwatafutia watoto
wafadhili ili kupata elimu.
·
Kubuni miradi ya
kusaidia kukua kwa elimu
UMUHIMU WA ELIMU
1.
Umuhimu wa elimu ni
kuondoa umaskini ndani ya familia na jamii kwa ujumla.
2.
Mtu mwenye elimu
anaweza kusaidia kuinua maisha ya mtu yeyote ambaye hana elimu katika familia.
3.
Mtu mwenye elimu
anaweza kubuni mbinu yeyote itakayomwezesha kuyamudu maisha katika:
·
Kilimo
·
Biashara
·
Ufundi
·
Uongozi katika sekta
mbalimbali nk.
4.
Umuhimu wa elimu ni
kupanua upeo wa akili
·
Kimawazo
·
Kifikra
·
Kujiamini katika
mambo yake unayoyapanga
·
Unakuwa na haiba
·
Kujulikana mbele ya
watu
DUNIA YA UTANDAWAZI
Utangulizi
Dhana
ya utandawazi inahusu kuwepo kwa ulimwengu usio na mipaka katika maingiliano ya
jamii mbalimbali katika shughuli zao za kiuchumi na kisiasa licha ya kuwepo kwa
mipaka ya kijiografia. Dhana ya "utandawazi" katika kiingereza
inaitwa "globalisation", neno ambalo linatokana na "globe",
kwa maana ya umbile la dunia yetu. Kama
tunavyofahamu dunia yetu ina umbile la tufe.
Kwa
karne nyingi, walimwengu walitengenishwa na mipaka ya kimaumbile ya dunia kama
vile mito,
milima, mabonde na bahari. Kabla havijaundwa vyombo vya usafiri vyenye mwendo
wa kasi kuliko wanyama kama vile punda na farasi, jamii nyingi zilkaa peke yake
bila kufahamu kama kuna jamii nyingine nyingi
katika uso wa dunia. Na kwa sababu hiyo jamii ziligawanyika katika makundi
madogo madogo mengi, yenye tamaduni tofauti; kwa maana ya lugha, mila na
desturi. Haya ndiyo makabila ambayo yalikuwepo katika mabara yote ulimwenguni.
Kutokana
na kukosekana aina yeyote ya mawasiliano ya lugha, au maingiliano yoyote ya
kijamii, jamii nyingi zilizokuwa jirani ziliishi kwa uadui. Kila mmoja
akimshuku mwenzake ni mbaya au hana thamani. Matokeo yake yalikuwa vita baina
ya jamii hizi, mwenye nguvu alimuua mwenzake, au alimteka kuwa mtumwa au
alimgeuza kitoweo.
Kwa
jamii nyingi ulimwengu wao ulikuwa ni kijiji chao. Watu, ni wale wa kabila lao tu - wengine wote ni
"washenzi, wanyika, vyasaka, wanyamahanga, n.k." (Hii ni mifano ya
hapa kwetu Tanzania, lakini
hata katika mabara ya Ulaya na Asia hali ilikuwa
ni hiyo hiyo).
Baada
ya jamii kuanza kutengeneza vyombo vya usafiri, hasa vile vya majini, ulimwengu
ukaanza kupanuka watu wakaweza kusafiri sio tu baina ya vijiji na miji ya
karibu bali walivuka bahari kubwa na kwenda kwenye mabara mbali mbali. Huo ndiyo
ulikuwa mwanzo wa Utandawazi.
Watu
wa jamii mbalimbali walianza kueneza tamaduni zao huku na kule. Hapa kwetu
Afrika tulipata watalii wa kwanza kabisa kutoka jamii za Wayunani, Waarabu na
Wachina kame nyingi kabla ya Wareno (hawa ndiyo wazungu wa kwanza huku Afrika
Mashariki.
Hata
hivyo maingiliano baina ya jamii katika mabara mbalimbali yaliendelea kwa kasi
ya wastani tu, kwani nyenzo za usafiri na kupeleka habari zilikuwa hazina kasi
kubwa. Bado safari za meli zilichukua miezi au miaka baina ya bara na bara na
safari za gari moshi pia zilikuwa za polepole.
Uliundwa
mfumo wa Posta wa kimataifa uliowezesha watu kupashana habari kwa maandishi
(barua, magazeti n.k.) lakini nao pia haukuwa wa haraka sana. Kwa hiyo basi, bado jamii nyingi
ziliendelea kuwa na lugha zao na tamaduni zao ambazo hazijaguswa na mabadiliko
kutoka nje ya jamii zao. Lakini katika kame za 19 na 20 yametokea maendeleo
makubwa ya kitekinolojia ambayo yamesababisha mageuzi makubwa katika
maingiliano ya kijamii: usafiri wa anga, simu, radio, cinema, televisheni na
kompyuta. Tekinolojia hizi mpya zimefanya mipaka ya kijiografia kuwa haina
uzito tena.
Watu
wanaweza kusafiri popote duniani kwa muda mfupi tena kwa raha na starehe zaidi,
taarifa za habari zinaweza kufikishwa kwa mamilioni ya watu kwa sauti na picha
kwa wakati mmoja katika muda wa sekunde tu. Huu ndiyo uUandawazi. Huu ndiyo
ulimwengu usio na mipaka.
Je,
katika ulimwengu huu ulio wazi, tunahitaji elimu ya namna gani? Tunasema kuwa
elimu ni utaratibu wa kurithisha kutoka kizazi kimoja hadi kingine, maarifa,
ujuzi, utamaduni na ustaarabu wa jamii iIi kuidumisha, kuistawisha na
kuiendeleza jamii ile.
Changamoto
iliyo kwetu ni kuyaelewa vema mapana na marefu ya dhana hii ya Utandawazi,
kubaini kwa usahihi jamii tunayoikusudia ni ipi - Tanzania, Afrika Mashariki, SADC au
dunia nzima? Na kuafikiana kitaifa ni maarifa gani, ujuzi gani, utamaduni gani,
na ustaarabu gani tunaotaka kuwarithisha watoto wetu.
UTANDAWAZI
KATIKA KARNE VA ISHIRINI NA MOJA
Choy (2004) anatoa maana ya Utandawazi kwa kusema kuwa
Utandawazi ni kasi ya kusambaa kwa watu, mawazo, huduma, mitaji, bidhaa na
mambo mengine kutoka nchi moja kwenda nyingine. Hali hii inasababishwa na kukua
kwa sayansi na teknolojia. Kwa kifupi Utandawazi unasukumwa na ushindani wa
kibiashara ambao umeruhusu utaratibu wa soko huria ambao umesababisha kupanuka
haraka kwa sekta binafsi katika uendeshaji wa uchumi na kupanua biashara ya
kimataifa.
Utandawazi unaendeshwa na soko Iinalopanuka kwa bidhaa za
kila aina kuvuka mipaka ya kitaifa. Uwekezaji, biashara na habari vimefunguliwa
mipaka ya kitaifa. Ripoti ya shirika la Maendeleo la Kimataifa (UNDP) ya
Maendeleo ya Binadamu (1999) inaeleza kasi ya kuenea kwa utandawazi kwa kusema
kuwa "soko likitawala kijamii na kisiasa matokeo yake utandawazi
unawanufaisha wachache wenye nguvu za kumiliki mali wakati wengine wakiendelea
kuwekwa kando katika ushindani". Ripoti ya UNDP ya mwaka 2004
inathibitisha haya kwa kubainisha kuwa Marekani pekee inamiliki asilimia 85 ya
viwanda vyote duniani vya filamu.
Ripoti hiyo pia imetoa mfano wa umiliki na matumizi ya
mtandao wa Kompyuta duniani na kubainisha kuwa nchi maskini zina sehemu ndogo
sana. Kwa mfano mwaka 1997 nchi maskini zilikuwa zinatumia asilimia 0.2 ya
mtandao wa Kompyuta ukilinganishwa na asilimia 93.3 katika nchi tajiri. Katika
mgawanyo wa namna hii ni dhahiri kuwa hakutakuwa na usawa katika dunia ya
utandawazi.
FAIDA ZA
UTANDAWAZI
Utandawazi umefungua milango na kutoa nafasi kwa
mamilioni ya watu duniani kunufaika katika nyanja mbalimbali, kama vile, Kukua
kwa biashara, maendeleo ya kiteknolojia, uwekezaji nje ya nchi na kukua kwa
mawasiliano "na mitandao ambavyo vimechochea kukua kwa uchumi na kuleta
maendeleo kwa jamii. Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (1999) linaripoti
kuwa dunia ya sasa ina utajiri mwingi na teknolojia ya hali ya juu kushinda
wakati wowote ule. Aidha utandawazi umesababisha mataifa kuwa karibu na kufanya
dunia kuwa kama kijiji kimoja. Siku hizi ni rahisi kutoka nchi moja na kwenda
nchi nyingine kufanya kazi au biashara. Aidha, bila hata kwenda unaweza kusoma
au kufanya biashara na nchi nyingine kwa kutumia mitandao.
Kukua kwa mwingiliano wa watu duniani kumeleta mfumo wa
kimataifa ambao unathamini maendeleo ya watu wote. Masuala ya maendeleo
yanajadiliwa na kuwekewa mikakati kimataifa. Hii inasaidia hata nchi maskini
kutoa hoja zake na maslahi yake kulindwa kimataifa. Mwingiliano wa watu duniani
unajaribu kuleta maendeleo katika nchi zote na kuondoa tofauti zilizopo ili
ushirikiano uwe rahisi. Iii tunufaike na fursa hizi zinazoletwa na utandawazi
ni lazima tuwape vijana wetu elimu itakayowawezesha kuelewa majukumu yao katika
jamii yenye amani na utulivu, inayozingatia haki za binadamu na kudhamini
tofauti za mataifa mbalimbali.
USHINDANI
UNAOSABABISHWA NA UTANDAWAZI
Kuenea kwa teknolojia kumepunguza mahitaji ya wafanyakazi
wanaotumia nguvu tu bila ujuzi na stadi katika uzalishaji. Kwa hiyo tunahitaji
wasomi wenye ujuzi na stadi za kutosha iIi nchi yetu isiwe soko la bidhaa za
watu wengine. Ni lazima tulenge katika kujiongezea uwezo wa kunufaika na fursa
zinazoletwa na utandawazi. Kwanza kabisa tunahitaji kuimarisha elimu ya sayansi
na hisabati, kwani masomo haya ndiyo msingi wa teknolojia; iwe ni teknolojia ya
mawasiliano (ICT) au teknolojia ya uzalishaji viwandani.
Kwa hiyo uimarishaji wa masomo ya sayansi na hisabati ni
lazima uanzie
shule za msingi. Na vivyo hivyo tuendeleze katika
madarasa mengine. Wataalamu wa masuala ya maendeleo wanasema "tofauti ya
utajiri kati ya Kaskazini (Ulaya_ na Kusini (Nchi zinazoendelea) ni Sayansi na
teknolojia".
Elimu pia ni nyenzo ya kuwajenga watoto katika ujasiri,
kujiamini na kuthubutu. Hizi ni hulka ambazo zinaweza kujengwa shuleni kupitia
mbinu mbalimbali. Hulka hizi ni misingi imara ya ubunifu na ushindani hata
katika biashara za kimataifa.
ELIMU YENYE
MWELEKEO WA UTANDAWAZI
Tujiulize, je ni elimu gani inayotakiwa iIi kukabiliana
na athari za utandawazi katika jamii yetu? Hili ni swali kwa kila mdau wa
elimu. Kila mmoja wetu ajaribu kujibu swali hili kwa ufasaha. Mimi nitadokezea
tu yale ambayo tunaweza kuyafanya.
Elimu itolewayo haina budi kuwa yenye misingi ya sayansi
na teknolojia. Hivyo ni lazima kuimarisha ufundishwaji na usomaji sayansi na
hisabati kuanzia elimu ya msingi. Hali hii inahitaji kubadilisha mitaala yetu
iIi iweze kutoa maarifa ujuzi na stadi zinazotakiwa, na kumwezesha mhitimu
kukabiliana na utandawazi
Sambamba na ubadilishaji wa mitaala ya shule itabidi
kuimarisha mafunzo ya elimu ya ualimu kwa sababu, pamoja na maendeleo na
mabadiliko ya tekinolojia hakuna mbadala ya mwalimu darasani. Wote tunafahamu
kuwa vitabu na mbinu mbalimbali za kufundishia na kujifunzia anazotumia mwalimu
darasani ni bora kuliko matumizi ya televisheni na kompyuta. Ni kweli kuwa
pamoja na utandawazi, kwa miaka mingi ijayo mwalimu atakuwa hana mbadala
darasani.
ATHARI ZA
UTANDAWAZI
Hatari ya kutoweka Utamaduni wa kitaifa: Utandawazi
hufungua milango ya kuingiza mawazo na utamaduni wa kigeni unaotoka zaidi
katika nchi zilizoendelea kwenda nchi zinazoendelea. Hii inahatarisha utamaduni
wa nchi zinazoendelea kutoweka. Kwa mfano inasemekana kuwa mwaka 1998 asilimia
80 ya bidhaa za kiutamaduni duniani zilitokea katika nchi 13 tu duniani
zikiongozwa na zile za Hollywood (UNDP, 2004). Hali hii ni ushahidi kuwa nchi
zinazoendelea hupokea sehemu kubwa ya utamaduni kutoka nje ya nchi zao. Ni
jukumu letu kubuni mbinu na mikakati sahihi na kuhakikisha kuwa utamaduni wetu
ulio bora unadumishwa kwa manufaa ya vizazi vijavyo na maendeleo ya nchi yetu
kwa ujumla.
Uharibifu wa mazingira: Matumizi makubwa ya rasilimali
katika nchi zilizoendelea yamesababisha nchi maskini kuharibu mazingira. Kwa
mfano karatasi, samaki, madini na bidhaa nyingine zinazotokana na maliasili
zimevunwa kiasi kwamba zjnasababisha kuharibika kwa mazingira na
Baioanuai. Haya yanathibitishwa na ripoti ya UNDP ya
mwaka 2004 inayobaini kuwa kati ya mwaka 1990 na 1997 uwekezaji katika
uchimbaji wa madini barani Afrika uliongezeka maradufu.
Mada ya Elimu na Dunia ya Utandawazi imeletwa kwenye
Mkutano huu iIi tuweze kujiandaa vizuri kukabiliana na utandawazi ambao
hatuwezi kuukwepa. pamoja na mabadiliko mengi tunayotegemea lakini tuwe na
msimamo. Pale ambapo tunaona kuwa misingi yetu kama taifa itabomolewa, tuchukue
hatua za binafsi na za pamoja kuhakikisha kuwa maadili yetu na utamaduni wetu
unadumishwa kwa vijana wetu na jumuiya nzima. Utandawazi usitufanye tuharibu
yale mazuri tuliyo nayo.
NINI KIFANYIKE KUINUA ELIMU KATIKA UKOO WETU
Umoja wa Ukoo wa Kivenule una jukumu la kuona kuwa vijana
wetu ni rasilimali na nguvu kazi inayotayarishwa kwa ajili ya ushindani katika
dunia ya utandawazi. IIi kufikia azma hii ni lazima tuwe wabunifu na wepesi
kukabiliana na mabadiliko ambayo yatajitokeza kila mara. Ujuzi na maarifa viwe
ndiyo ngao yetu kubwa. Hatimaye matokeo halisi ya kazi yetu tutayaona
tutakapofuatilia vijana wetu waliopitia kwenye mfumo wetu wa elimu na kuona
kuwa wanao ujuzi na stadi za kuwawezesha kupata ajira katika dunia ya
ushindani. Tutakuwa tumefanikiwa kama tutawakuta wanafunzi wetu wameajiriwa na
ni watu wa kutegemewa ndani na nje ya nchi.
Mikakati ambayo inaandaliwa na Umoja wa Ukoo wa Kivenule
katika kuinua elimu katika ukoo ni pamoja na kuanzisha mfuko ambao utachangiwa
na wanaukoo ili kuwasaidia ndugu/wanaukoo ambao hawana uwezo wa kuwasomesha
watoto. Pia, mfuko huo utasaidia kuwaendeleza ndugu/wanaukoo ambao wamefaulu na
hawana uwezo wa kujisomesha. Mambo mengine muhimu kama sara za shule, vitabu,
kalamu za risasi na wino, ada na vifaa vitatolewa na Umoja wa Ukoo wa Kivenule
pindi pale hali ya mfuko itaboreka.
MAJADILIANO KWENYE MAKUNDI
KUNDI NA. 1
Nafasi ya
Ukoo wa Kivenule katika Elimu
4.
Tumegundua
kuwa nafasi ya ukoo wa Kivenule katika elimu ni mdogo au upo chini kwa sababu:
·
Nafasi za
ajira katika maofisi makubwa serikalini ni mdogo.
·
Wanaukoo
wachache wamepaa ajira katika mashirika makubwa (umma au binafsi)
yanayozingatia kiwango elimu katika ajira.
5.
Kuwa na
idadi ndogo ya wanaukoo waliofikia elimu ya kiwango cha juu mfano kidato cha 4,
6 mpaka vyuo vikuu.
6.
Wanaukoo
kutojua umuhimu wa elimu.
Ili ukoo uwe na nafasi elimu tufanyaje?
·
Tujitahidi
kusomesha watoto wetu hadi elimu ya juu.
·
Elimu ya
ufundi pia ni muhimu ndani ya ukoo.
·
Tuunde
kamati katika ukoo itkayoratibu sula zima la ukoo.
·
Kukusaya
michango kuwasaidia waso na uwezo wa kusomesha.
·
Kuwasaidia
kusoma watoto wa ukoo wasio na msaada.
·
Kuwatafutia
watoto wafadhili ili kupata elimu.
·
Kubuni
miradi ya kusaidia kukua kwa elimu
KUNDI
NA. 2
Umuhimu wa Elimu
4.
Umuhimu wa elimu ni kuondoa
umaskini ndani ya familia na jamii kwa ujumla.
5.
Mtu mwenye elimu anaweza
kusaidia kuinua maisha ya mtu yeyote ambaye hana elimu katika familia.
6.
Mtu mwenye elimu anaweza kubuni
mbinu yeyote itakayomwezesha kuyamudu maisha katika:
·
Kilimo
·
Biashara
·
Ufundi
·
Uongozi katika sekta mbalimbali
nk.
5.
Umuhimu wa elimu ni kupanua upeo
wa akili
·
Kimawazo
·
Kifikra
·
Kujiamini katika mambo yake
unayoyapanga
·
Unakuwa na haiba
·
Kujulikana mbele ya watu
KUNDI
NA. 3
Dunia ya Utawandazi
Vigezo:
Elimu ili tuweze kwenda sambamba na wenzetu katika dunia ya Utandawazi.
Utandawazi unafanya dunia kuwa kama kijiji.
·
Kupitia elimu watu wanawezeshwa
kupambana katika mazuri na mabaya.
·
Wenye mwanga kidogo katika elimu
wawasaidie wengine kuifafanua elimu ya Utandawazi kwa kubainisha faida na
hasara zake.
Udhibiti
Mienendo
ya watoto iangaliwe ili kuona kuwa haiharibiwi na Utandawazi. Kazi za watoto
zifuatiliwe kwa karibuni na wazazi ili wasipate muda mwingi wa kuangalia mambo
yasiyowahusu.
Elimu
ya Utandawazi kwa walioipata na umri (wote tuna haki ya elimu, aliyeo na umri
mkubwa.
KUNDI
NA. 4
Nini kifanyike ili kuinua Elimu
katika Ukoo
1.
Watoto wetu wapelekwe shule kwa
wakati unaostahili (Awali, msingi, sekondari nk).
2.
Kudhibiti tabia za watoto wetu
ili waweze kusoma vizuri (tabia mbaya).
3.
Wazazi wawe wapesi kutoa msaada
unaohitajika kwa watoto (mahiaji ya msingi) kuwajenea mazingira mazuri ya elimu.
4.
Mtoto akifaulu kwenda sekondari
mzazi atoe taarifa kwa wenzetu ili waone uwezekano wa kusaidia mtoto huyo aene
shuleni.
5.
Ndugu wawe walinzi wa kila mtoto
wa ndugu anayefanya mambo ya ajabu mitaani.
6.
Kubuni mfuko maalum wa elimu ili
kusaidia mapema watoto wanaofaulu, lakini mtoto anaweza kufaulu na
asichaguliwe.
MAJUMUISHO
1.
Katika dunia ya leo, mambo mengi
yamemezwa na Utandawazi. Jambo la
msingi la kuzingatia ni kupata Elimu. Wanaukoo wote wajitahidi kupata elimu
pamoja na kujiendeleza hadi kupata elimu ya juu.
2.
Wanaukoo
inabidi tuelekeze (tuwekeze) nguvu na rasilimali zetu katika Elimu.
MADA YA NNE
UKIMWI
NDANI YA UKOO NA ATHARI ZAKE
UKIMWI ni
nini?
UKIMWI ni Upungufu wa Kinga Mwilini mwa binadamu. Kwa
lugha ya kigeni, Upungufu wa Kinga Mwilini hujulikana kama AIDS; yaani kirefu
chake “Acquired Immuno Deficiency Syndrome. Na virusi vinavyoeneza ugonjwa wa
UKIMWI kwa lugha ya kigeni hujulikana kama Human Infection Virus (HIV). Kwa
lugha rahisi, neno UKIMWI linaweza kunyumbulishwa au kumegwa katika herufi za
kujitegemea kama tatu hivi; yaani
U – inasimama badala ya Upungufu;
KI – inasimama badala ya Kinga; na
MWI – inasimama badala ya Mwili.
Mwili wa binadamu umeumbwa na seli za aina mbili; yaani
§
Seli
Nyekundi za Damu (Red Blood Cells); na
§
Seli Nyeupe za Damu (White Blood
Cells).
Kinga
za mwili ambazo huulinda mwili wa binadamu kutokana na maambuki ya maradhi
mbalimbali hutengenezwa kwenye Seli Nyeupe za Damu (White Blood Cells). Kwa
lugha ya kigeni kinga hizi huitwa Antibodies.
Virusi
vinavyoeneza ugonjwa wa UKIMWI hukaa muda mrefu sana mwilini mwa binadamu hadi kufikia hatua
ya kuweza kutambulika. Mgonjwa aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI huweza kukao
hadi miaka kumi bila kuleta athari yoyote. Mara nyingi, mgonjwa aliyeambukizwa
virusi vya UKIMWI anaweza kuishi kwa muda mrefu bila kupata madhara yoyote
kutokana na afya ya awali ya mgonjwa, pamoja na aina za vyakula anavyokula.
Kwa
wagonjwa ambao afya zao siyo madhubuti, madhara ya maambukizi ya virusi vya
UKIMWI huweza kujitokeza katika kipindi cha miezi sita (6) au pungufu ya hapo.
Dalili mbalimbali ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI huweza kuanza kujitokeza baada ya kipindi hicho cha miezi sita. Dalili
hizo huwa ni pamoja na:
§
Kushambulia na magonjwa
mbalimbali ya maambukizi mfano Kifua Kikuu (Tuberclosis);
§
Kupungukiwa
na uzito mara kwa mara;
§
Kupata mkanda wa jeshi; na
§
Kutapika na kuharisha.
NJIA MBALIMBALI ZINAZOCHANGIA
MAAMBUKIZI/KUENEA KWA VIRUSI VYA UKIMWI
Kuna haja kwa wanaukoo wa Ukoo wa Kivenule pamoja na jamii
inayowazunguka kutilia umuhimu suala la kupata Elimu ya kujua jinsi maambukizi
na kuenea kwa virusi vya UKIMWI kunavyotokea, hii itasaidia jamii yetu na
wanaukoo/familia kwa ujumla kuzifahamu njia mbalimbali mbadala ambazo
zinachangia kwa kiwango kikubwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Baadhi ya njia
hizo zinazosaidia/changia maambukizi ya virusi vya UKIMWI ni pamoja na:
1.
Kufanya ngoo holela
na zisizo salama;
2.
Kutochukua hatua
madhubuti za kupima afya na kujitambua/kujijua kiafya kabla ya kufunga ndoa;
3.
Kushambuliwa na
magonjwa mbalimbali ya zinaa bila kwenda hospitalini kutibiwa;
4.
Kuchangia katika
matumizi ya vifaa vya kutogea mfano nyembe, sindano za mahospitalini, miswaki,
mikasi ya mahospitalini na kushika vidondo vya mgonjwa aliyeambukizwa na virusi
vya UKIMWI bila kutumia kinga (gloves);
5.
Kuwekewa damu yenye
virusi vya UKIMWI;
6.
Mtoto kuambukizwa
virusi vya ugonjwa wa UKIMWI toka kwa mama yake wakati wa kujifungua;
7.
Mama Mjamzito
kutochukua hatua madhubuti/tahadhari ya kupima afya yake ili kujua kama ana maambukizo ya virusi vya UKIMWI au hapana;
8.
Kurithi wajane;
9.
Wanaukoo/familia kutokuwa waaminifu katika ndoa zao; na
10.
Mama aliyeathirika na virusi vya UKIMWI kumnyonyesha mtoto ambaye
hajaathirika na virusi vya UKIMWI.
NJIA
MBADALA ZA KUJILINDA NA MAAMBUKIZI
WAnaukoo/familia baada ya kuzifahamu njia
mbalimbali mbadala zinazochangia maambukizi ya virusi vya UKIMWI; sasa wajibu
wao mkubwa ni kuielimisha jamii yao kuzitambua njia kadhaa zinazosaidia
kujilinda na maambukizi ya virusi vinavyoleta upungufu wa kingi mwilini yaani
UKIMWI. Hatua hizo madhubuti ambazo ukoo na jamii yetu kwa ujumla inapaswa
kuzichukua ni kutoa elimu kuhusu umuhimu wa:
1.
Kupima afya na kujitambua kama umeambukizwa virusi vya UKIMWI toka katika
vituo mbalimbali vya afya mfano ANGAZA na mahospitalini;
2.
Kufanya ngono salama kwa kutumia njia mbadala zinazoshauriwa na wataalamu
au kuacha kabisa mpaka muda muafaka utakapofika;
3.
Waathirika wa virusi vya UKIMWI kutojihusisha katika ngono au hali yoyote
ambayo inaweza kuchangia maambukizi ya virusi vya UKIMWI:
4.
Wanaukoo/familia kuwa waaminifu katika ndoa zao;
5.
Kwenda hospitali kutibu dalili zozote za maambukizi ya magonjwa ya zinaa.
Magonjwa ya zinaa huchangia sana katika maambukizi ya virusi vya UKIMWI;
6.
Mama Wajawazito kupima afya zao kabla ya kujifungua ili kuwanusuru watoto
wanaozliwa wasiathirike na virusi vya UKIMWI kama mama hao watakuwa
wameambukizwa na virusi vya UKIMWI;
7.
Mama aliyeathirika na virusi vya UKIMWI, kutomnyonyesha mwanae ili
kupunguza uwezekano wa kumwambukiza mtoto kama atathibitika kuwa ameambukizwa;
8.
kuacha kurithi wajane;
na
9.
Kuacha mila potofu
zinazopotosha mfano kupiga ramli.
JUKUMU LA
UKOO/FAMILIA KUKABILIANA NA JANGA LA UKIMWI
Jukumu la Ukoo/Familia katika kukabiliana na virusi vya
maambukizi vinavyoeneza ugonjwa wa UKIMWI ni pamoja na:
1.
Kutoa na
kueneza elimu ihusuyo maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa watoto na vijana
wenye ufahamu na uelewa na hali hali kadhalik kwa watu wazima;
2.
Kuwaelimisha
wanaukoo/familia kuzifahamu njia mbadala za kujikina na kujilinda a maambukizi
ya virusi vya UKIMWI;
3.
Kuwaelimisha
wanaukoo/familia kuzifahamu njia mbalimbali zinazochangia maambukizi na kuenea
kwa virusi vya UKIMWI;
4.
Kuwaelimisha
wanaukoo/familia kujenga tabia ya kupenda kupima afya zao na kujua kama
wameambukizwa virusi vya UKIMWI au hapana;
5.
Kuwaelimisha
wanaukoo/familia kuwa waaminifu katika ndoa zao ili kupunguza hatari ya
maambukizi ya virusi vya UKIMWI; na
6.
Kuwaelimisha
wanaukoo/familia kuishi katika misingi ya Dini na Maadili mema.
Pia muhimu sana kukatolewa Elimu ya kujua jinsi
maambukizi na kuenea kwa virusi vya UKIMWI kunavyotokea, hii itasaidia jamii
yetu na wanaukoo/familia kwa ujumla kuzifahamu jia mbalimbali mbadala ambazo
zinachangia kwa kiwango kikubwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Baadhi ya njia
hizo zinazosaidia/changia maambukizi ya virusi vya UKIMWI ni pamoja na:
1.
Kufanya ngoo holela na zisizo
salama;
2.
Kutochuku hatua madhubuti za
kupima afya na kujitambua/kujijua kiafya kabla ya kufunga ndoa;
3.
Kushambuliwa na magonjwa
mbalimbali ya zinaa bila kwenda hospitalini kutibiwa;
4.
Kuchangia katika matumizi ya
vifaa vya kutogea mfano nyembe, sindano za mahospitalini, miswaki, mikasi ya
mahospitalini na kushika vidondo vya mgonjwa aliyeambukizwa na virusi vya
UKIMWI bila kutumia kinga (gloves);
5.
Kuwekewa damu yenye virusi vya
UKIMWI;
6.
Mtoto kuambukizwa virusi vya
ugonjwa wa UKIMWI toka kwa mama yake wakati wa kujifungua;
7.
Mama Mjamzito kutochukua hatua
madhubuti/tahadhari ya kupima afya yake ili kujua kama
ana maambukizo ya virusi vya UKIMWI au hapana;
8.
Kurithi wajane;
9.
Wanaukoo/familia
kutokuwa waaminifu katika ndoa zao; na
10.
Mama
aliyeathirika na virusi vya UKIMWI kumnyonyesha mtoto ambaye hajaathirika na
virusi vya UKIMWI.
WAnaukoo/familia baada ya kuzifahamu njia mbalimbali
mbadala zinazochangia maambukizi ya virusi vya UKIMWI; sasa wajibu wao mkubwa
ni kuielimisha jamii yao kuzitambua njia kadhaa zinazosaidia kujilinda na
maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Hatua hizo madhubuti ambazo ukoo na jaii yetu
kwa ujumla inapaswa kuzichukua ni kutoa elimu kuhusu umuhimu wa:
1.
Kupima afya
na kujitambua kama umeambukizwa virusi vya UKIMWI toka katika vituo mbalimbali
vya afya mfano ANGAZA na mahospitalini;
2.
Kufanya
ngono salama kwa kutumia njia mbadala zinazoshauriwa na wataalamu au kuacha
kabisa mpaka muda muafaka utakapofika;
3.
Waathirika
wa virusi vya UKIMWI kutojihusisha katika ngono au hali yoyote ambayo inaweza
kuchangia maambukizi ya virusi vya UKIMWI:
4.
Wanaukoo/familia
kuwa waaminifu katika ndoa zao;
5.
Kwenda
hospitali kutibu dalili zozote za maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Magonjwa ya
zinaa huchangia sana katika maambukizi ya virusi vya UKIMWI;
6.
Mama
Wajawazito kupima afya zao kabla ya kujifungua ili kuwanusuru watoto wanaozliwa
wasiathirike na virusi vya UKIMWI kama mama hao watakuwa wameambukizwa na
virusi vya UKIMWI;
7.
Mama
aliyeathirika na virusi vya UKIMWI, kutomnyonyesha mwanae ili kupunguza
uwezekano wa kumwambukiza mtoto kama atathibitika kuwa ameambukizwa;
8.
kuacha kurithi wajane; na
9.
Kuacha mila potofu zinazopotosha
mfano kupiga ramli.
Wanaukoo/familia
wana jukuu pia la kuwahudumia wale ambao tayari wameambukizwa na virusi vya
UKIMWI ili waendelee kujihusisha na shughuli za uzalishaji mali na kupunguza utegemezi. Baadhi
ya majukuu hayo ya wanaukoo/familia ni pamoja na:
1.
Kuwapenda na kuwasaidia wagonjwa
wote waliathirika na virusi vya UKIMWI;
2.
Kutowanyanyapa wagonjwa
walioathirika na virusi vya UKIMWI;
3.
Kuchukua hatua madhubuti za
kuwasaidia waathirika wa virusi vya UKIMWI kupata dawa za kurefusha maisha.
Mfano wa dawa hizo ni RVA,
4.
Kuwathamini wagonjwa
waliambukizwa na virusi vya UKIMWI; na
5.
Kuwasaidia wagonjwa
waliambukizwa na virusi vya UKIMWI kupata vyakula vya kuujenga na kuulinda
mwili.
Kuna
Hamasa, Mbinu au Falsafa mbalimbali ambazo wanaukoo/familia wanaweza kuzitumia
katika kupambana na gonjwa hili. Hii ni pamoja na kuzingatia matumizi ya
J&; yaani waone umuhimu wa:
1. KUJITAMBUA;
2. KUJIHESHIMU;
3. KUJIPENDA;
4. KUJITHAMINI;
5. KUJIAMINI;
6. KUJILINDA; na
7. KUJIDHIBITI.
Medani
kadhaa ambazo wanaukoo/familia wanaweza kuzitumia kuepukana au kuwa mbali na
maambukizi ya virusi vya UKIMWI ni pamoja na:
1. Kusema hapana (kukataa) ushawishi wa
aina yoyote;
2. Kuongea na kutokukubali kuburuzwa;
3. Kuondoa woga na kupima afya yako;
4. Kupunguza
matumizi ya vileo au kuacha kabisa;
5. Wanaukoo/familia
kuwa waaminifu katika ndoa zao;
6. Wanaukoo/familia kujiepusha na
vishawishi;
7. Wanaukoo/familia kuulinda ujana na utu
uzima wao;
8. Kujibidisha katika kazi na hivyo
kupunguza fikra zisizo za msingi; na
9. Kusoma vitabu na magazeti baada ya
kazi.
Kwa
kufanya hivyo, yote hayo yaliyopendekezwa katika makala hii, nafasi hii, nafasi
ya jaii hii ya ukoo wa KIVENULE itakuwa imepiga hatua muhimu katika kukabiliana
na kupambana na maambukizi ya virusi vinavyoeneza gonjwa la UKIMWI.
MAJADILIANO KWENYE MAKUNDI
KUNDI NA. 1
UKIMWI ni nini?
1.
Maana:
Upungufu wa Kinga Mwilini
2.
Upungufu wa kinga unasababisha
kukosekana au kuuawawa kwa chembechembe nyeupe za damu (white blood cells)
ambazo husaidia kuzuia maambukizo ya magonjwa mbalimbali mwilini
3.
Kinga hiyo inapopungua mwilini
husababisha mtu kuugua magonjwa mbalimbali mfano malaria, TB Kifua Kikuu,
Kuharisha na kadhalika.
KUNDI NA. 2
Namna gani
UKIMWI unavyoweza kuenea
1.
Kurithi wajane
2.
Ngono uzembe
3.
Ulevi wa kupindukia
4.
Kutokuwa waaminifu katika ndoa
5.
Kukosa maadili ya dini
6.
Michilizi ya damu
7.
Kushirikiana katika matumizi ya
sindano na vifaa vya kutibia visivyo salama.
8.
Kuongezewa damu yenye virusi.
9.
Kwa njia ya kunyonyesha.
10.
Wakati wa kujifungua
11.
Kwa njia ya kushirikiana
miswaki.
KUNDI NA. 3
Njia
Mbadala za Kujilinda na Maambukizi ya UKIMWI
1.
Kuanzisha shughuli mbalimbali.
2.
Kupunguza ulevi wa kupindukia
mfano: mtu alisema kunywa Pombe si starehe ila kwenye Pombe kun starehe.
3.
Wanandoa kuwa waaminifu.
4.
Kuepukana na utumiaji wa vifaa
visivyo salama.
5.
Kufuata Maadili ya Mungu.
6.
Kuwa wazi katika mazungumzo
yanayohusu UKIMWI.
7.
Kupima afya.
8.
Kutumia zana za kujilinda na
maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.
9.
Kukimbilia mijini.
10.
Kutumia Madawa ya Kulevya.
11.
Wazazi na wakubwa kuwa wazi kwa
watoto wao.
12.
Kuepuka vishawishi mbalimbali.
13.
Kurithi wajane au kurithiwa.
14.
Kuweka wazi mtu akifariki.
KUNDI
NA. 4
Jukumu la
Ukoo/Familia Kukabiliana na Janga la UKIMWI
1.
Elimu
itolewe kwa wana ndugu wote juu ya UKIMWI.
2.
Wanandoa
kuwa waaminifu katika ndoa zao.
3.
Wanandugu
kujihusisha katika kazi na kushiriki michezo mbalimbali.
4.
Kuhimiza
matumizi ya mipira ya plastiki (gloves) katika uoshaji wa maiti, nguo na
kadhalika.
5.
Kuwatimizia
watoto wanaosoma mahitaji yao mfano fedha nk.
6.
Kutozalia majumbani (Wakunga)
7.
Ukeketaji ukomeshwe
8.
Kubusu maiti.
9.
Kuficha maradhi.
MADA
YA TANO
DINI
KATIKA UKOO
UTANGULIZI
Tuna msemo unaotukumbusha hivi, hakuna mtu anayependa kuishi peke
yake, au aliye kama kisiwa na hakika kweli.
Hatuishi wala hatuwezi kuishi hivyo, yaani kuishi watu pekee, watu waliotengwa
na wenzao kama vile kisiwa kilichotengwa na
nchi kavu.
Twawahitji wengine wengi ili tujisikie tumeungana na watu tumkuwa
kitu kimoj na wanadau wenzetu.
Tunaangalia maisha yetu ya kila siku tunaona mifano mingi. Nikiona
furaha nahitaji kushirikiana na mtu mwingine. Tukipatwa na misib, magonjwa
tunahitji kutulizwa, kufarijiwa na kusaidiwa na wengine.
Tena kuna vifungo vinavyotuunganisha vyaweza kuwa ni urafiki,
ujamaa, ujirani uhusiano wa kikazi na kadhalika. Kati yangu na watu wengine.
Pamoja na vifungo hivyo tulivyovitaja vinavyotuunganisha katika
maisha ya kawaida, kuna kifungo kikuu ambacho kinaweza kutuunganisha au
kuniunganisha mimi, na hicho kifungo si mwingine ila ni Mungu. Mungu ndiye
kifungo pekee kinachotulte uhusiano wa kawaida uliopo kati ya Mungu na Mimi au
wewe, ndio tunachokiita Dini.
NINI MAANA YA DINI?
Neno
hili Dini ni neno ambalo pengine
umelisikia mara nyingi, na pengine hatuelewi maana yake lakini linaweza kuwa na
maana nyingi sana.
Endapo ukimwuliza ndugu yeyote maana ya dini, natumaini utapata majibu mengi sana na yote yatakuwa yanaelezea
maana halisi ya dini.
Dini ni Imani ya Kuamini kitu au jambo fulani
kuwa linaweza kumsaidia binadamu kupata mahitaji yake. Ndani ya Dini kuna kitu
ambacho huwa ni nguzo kwa yule anayeamua kuwa katika dini fulani. Nguzo hiyo ni
Imani. Imani inampelekea binadamu kuweza kujitengenezea utaratibu wa kutolea
heshima, kufanya ibada ikibidi hata kuitolea Sadaka.
Maana
hii ya pili; Dini ina maana hasa ya kufungamana na kuhusiana. Kwa maneno
mengine Dini ni uhusiano, urafiki, ushirikiano uliopo Kati ya Mungu na
Binadamu. Maana hii ya pili inamweleza hasa Mungu Mmoja Muumba Mbingu na Nchi.
Maana
hii ya pili inaonyesha utofauti wa maana ya kwanza ambayo inaonyesha inaweza
kuhusisha Miungu zaidi ya mmoja. Maana ya pili ya dini ndiyo inayoaminiwa na
watu wengi au mamilioni ya watu katika ulimwengu huu.
Msingi mkuu wa Dini ni Imani. Kila mtu ana dini. Mtu
mwingine anaamini kukaa peke yake na hiyo ndiyo
dini yake. Imani ni tabia ya ndani aliyonayo mtu. Imani ya ndani huzaa
tabia. Tabia huonekana nje. Dhehebu ni muunganiko wa watu wenye tabia. Kama
ukoo tunaweza kutengeneza dhehebu letu.
Dini
ilianza lini
Hili linaweza kuwa ni swali karibu kwa mmoja wetu kuwa
Dini ilianza lini? Kwa kweli Dini imeanza zama za kale kabisa, binadamu
alipoanza kuwa binadamu.
Watu wa Sayansi walichunguza mianzo ya binadamu,
wanatuambia kwamba binadamu alipovumbua ulimwengu na kujitambua mwenyewe, pale
pale alitamua pia mtu aliye mkubwa kuliko binadamu, na huyo si mwingine ila ni
Mungu.
Aina ya
Miungu
Kabla ya Mungu hajajionyesha, kuna Miungu ambayo watu wa
kale waliiabudu na kuitumikia Miungu hiyo ni ile iliyotokana na vitu vilivyoumbwa
na Mungu navyo ni:
ANU Mungu
Mbingu
EA Mungu
Maji
ENIL Mungu
Upepo
SHAMASH Mungua Juan a Dunia na kadhalika
Hii
ndiyo Miungu waliyoiabudu hapo kale lakini haikuwa Miungu ya Kweli.
Dini za Kiulimwengu
Baada
ya kuona Miungu waliyoiabudu hapo kale imepitwa na wakati, hapo baadaye watu
walianzisha Dini za Kiulimwengu ambazo zilianza huku Bara la ASIA katika nchi
za China na India.
Mawazo hayo yaliyojitokeza kabla Mungu hajajifunua au kujionyesha kuanzisha
dini yake Mungu. Mawazo yao
juu ya kumtafuta Mungu yalikuwa mazuri isipokuwa namna zao zilikuwa kinyume na
Mungu.
Dini Zenyewe za Kiulimwengu
Dini
ya Kihindu ilianza mwaka 2500 KK. Imani ya Dini hiyo waliamini uwepo wa Mungu
katika kila kiumbe kilicho hai mfano……. Hivyo kutokana na Imani hiyo walithamini
sana Uhai wa
kila Kiumbe.
Dini
ni KIBUDHA hii ilianzishwa mwaka 560 KK. Imani yao waliamini kuwa maisha ya binadamu ni
mateso, mateso kutokana na kutamani mambo yasiyo kidhi mahitaji ya Roho.
Hivyo
walijitahidi kuepuka mates ohayo kwa kutimiza maneno nan. Maoni halisi – misemo
halisi - mndo mzuri wa maisha – amaa
nzuri – na kadhalika. Hivyo walijitahidi sana
kuongea na kutenda vizuri kila wakati.
Dini ya Mungu
Baada
ya dini hizo za kiulimwengu Mungu saa anajionyesha au kujifunua, japo hakujifunu
katika kila taifa. Alijifunua katika taifa la Israel kwa KUMWITA IBRAHIMU. MUNGU
alijionyesha kwa mpango huo ili watu wamtambue jinsi alivyo, watu waone kuwa
yeye ni Mungu wa namna gani mwa 12 – 13.
Mungu
alijitambulisha kwa Ibrahi katika Taifa la Israel kwa msimamo huu kuwa
MUNGU
NI MOJA NA HAKUNA MWINGINE; ila ni yeye tu, nah ii ndiyo imani kwa Israel
kuwa Mungu I mmoja tu.
Msingi
huo wa Imani kwa Israel
uliandikwa katika maandiko ya Kiyahudi na iliitwa kifungu cha Sikiliza Ee Israel.
Hili ilikuwa SALA ya Asubuhi kila siku na ni muhimu waifahamu na kuisali.
SALA
YENYEWE: Sikiliza Ee Israel Bwana Mungu ni mmoja. Nawe umpende Bwana Mungu wako
kwa moyo wake wote na kwa Roho yako yote, na kwa Nguvu zako zote… Kumb 6:4 – 5,
13 – 14.
Dini Kubwa zinazofuata Mpango wa
Mungu Mmoja
1. Dini ya Kikristo
Dini
hii Asili yake na Mpango wake ni Mungu Mmoja Muumba Mbingu na Nchi. Tukianzia
na Ibrahim pamoja na historia nzima ya Ukoo wa Yesu na Kanisa lake yaani
Mitume.
Dini
hii ya Kikristo ina madhehebu yake ambayo yanamwamini MUNGU mmoja kwa njia ya
Yesu Kristo. Na kila anayemwamini MUNGU hana budi kufuat Mwongozo wake kwa
kushika NENO LA MUNGU kulifuaa na kuwa na maisha nao, kwa kushika kiaminifu
Amri 10 za Mungu na sheria zake. Pamoja na hayo kumheshimu, kumwabudu,
kumwomba, kumpenda katika siku zote za maisha.
2. Dini ya Kiislamu
Hii
pia inamwamini Mungu Mmoja ALLAH, na mjumbe wake ni Mtume MOHAMED SALLALEI
WASALAM Dini hii pia ina madhehebu yake. Dini hii inahimiza kila Mwislamu
anayemwamini MUNGU (ALLAH) anahimizwa kuisoma KORAN au MSAHAFU na kushika
maagizo ya Mungu (ALLAH) kutoka kwa mjumbe wake aliyefunuliwa Mtume MOHAMED,
pamoja na kufuata Nguzo Tano (5) za Uislamu.
Dini
hizi mbili na madhehebu yake zinazomwamini Mungu Mmoja, zinawahimiza waamini
wake pamoja na watu wote kuona umuhimu wa kujiunga na Dini ili kuona Upendo wa
MUNGU (ALLAH) kwani kujiunga katika Dini zilizo za kweli kutawafanya watu
waishi kwa Amani na Upendo hapa. Duniani na huko Mbinguni aliko MWENYEZI MUNGU.
UMUHIMU WA KUWA NA IMANI
Umuhimu
wa kuwa na Imani (Dini) unajengeka katika maeneo mbalimbali. Kuwa na Imani kuna
faida zake ambazo mshika Imani hufaidi, hii ni pamoja na:
1.
Dini huondoa tofauti zetu.
2.
Dini huondoa chuki, fitina na
unafiki.
3.
Dini hutoa elimu ya ufahamu wa
mambo mengi.
4.
Dini hujenga tabia ya
kusaidiana, kuondoa chuki, kuondo tofauti.
5.
Dini hujenga uhusiano mkubwa
baina ya Mungu na Binadamu.
6.
Dini hupunguza ushirikina.
7.
Dini
hupunguza woga wa kuogopa mtu kutokana na uwezo, uchawi na kadhalika.
8.
Kuishi kwa
imani hata kama una matatizo mfano kufiwa; humfanya aamini kuwa Mungu ndiye
mweza.
9.
Dini
humfanya mtu kuwa na mtazamo baadaye baada ya kifo hivyo anakuwa Mnyenyekevu.
MAADILI NA
DINI
Dini, Imani, Dhehebu na Maadili huenda pamoja. Dini ni Imani. Msingi wa Dini ni Imani. Kila mtu ana
Dini. Mtu anayeamini kukaa peke ndiyo dini yake. Imani ni tabia ya ndani
aliyonayo mtu. Imani ya ndani huzaa tabia. Tabia huonekana nje. Dhehebu ni
muunganiko wa watu wenye tabia ya aina mmoja. Kama ukoo tutengeneze dhehebu
letu ambalo sisi kama wafuasi wake tutakuwa na matarajio fulani. Liwe ni
dhehebu la kuwajali waumini wake, dhehebu lenye kuheshimu na dhehebu lenye
kujengea uwezo wa kiuchumi, kiakili na kiafya.
Maadili nayo hujengwa kwa msingi wa imani na dini. Watu
walio katika imani hujijengea maadili fulani ambayo huweza kuwatofautisha na
jamii nyingine. Kwa mfano maadili fulani ambayo hufuatwa na waumini wa dini
fulani, huwafanya watembee bila ya kuvaa viatu, wale mlo kwa siku, kujitolea
muda wao wote kuwatumikia watu wengine, kukesha usiku kucha kanisani wakiomba na
kadhalika. Haya huwa ni maadili yanayoridhiwa na kukubaliwa na kundi fulani la
watu au jamii, wayafuate.
Maadili ni miiko ambayo huweza kufuatwa na jamii fulani
ili kuweza kutimiza malengo yao. Kwa mfano katika makanisa mbalimbali ya
Kikristo kuna Amri za Mungu au Kanisa ambazo tunaweza kuzifananisha na Maadili
katika maisha yetu ya kila siku. Kwa mfano katika Kanisa Katoliki kuna Amri
Kumi za Mungu, ambapo kina mwanakatoliki anawajibu wa kuzitimiza. Amri hizo
tukizileta katika maisha yetu ya kawaida ya kibinadamu tunaweza kuziita ni
maadili, kwa sababu zipinga tabia zile ambazo hazikubaliki na jamii zetu. Kwa
mfano baadhi ya Amri za Mungu zinasema yafuatayo : Usiibe, Usiue, Usiseme
Uwongo, Usitamani Mali ya Mtu, Usimtamani Mwanamke Asiye Mke wako, Usizini, Umpende
Jirani Yako kama unavyojipenda na kadhalika.
Katika maisha yetu ya kila siku Amri hizo za Mungu ni mfano
wa Maadili Mema ambayo kila mtu au ndugu analazimika kuyafuata ili kuweza
kukubalika katika jamii yake. Kwa mfano
tabia za uongo, uzinzi na uasherati, wivu mbaya, tamaa mbaya, wizi, kuua ni
baadhi ya tabia mbaya ambazo hazikubaliki kabisa na ni kinyume cha maadili. Kwa
hiyo Dini na Maadili vina mahusiano makubwa na ya muhimu sana. Kama jamii, tuna
jukumu la kuhakikisha kuwa wanaukoo wanakuwa waumini wazuri katika Dini zao,
kwani kwa kufanya hivyo tutajenga jamii yenye maadili mema.
UKOO
ULIOJENGEKA KATIKA MISINGI YA DINI
1.
Ukoo
uliojengeka katika misingi ya dini unakuwa hauna ubinafsi.
2.
Ukoo
uliojengeka katika dini utakuwa ni ukoo unajaliana katika matatizo kutokana na
imani walionayo kutokana na Dini zao.
3.
Watu Kuheshimiana: Dini inafundisha mambo mema; Kwa hiyo ukoo utakapokuwa
na mwamko wa dini hakutakuwa na matatizo ya kudharauliana.
4.
Kuheshimika kwa Ukoo: Kwa kuwa utakuwa na sifa nzuri basi hata koo nyingine
zitapata hamasa ya kujiunga na ukoo.
5.
Ukoo unapunguza imani potofu : Kwa mfano
kama wanaukoo watafuata misingi ya dini zao, hawawezi kuwa na imani za
kishirikiano au kufikiria kwenda kwa waganga wa jadi ili kutatua matatizo yao.
MAJADILIANO KWENYE MAKUNDI
KUNDI NA. 1
Maana ya
Dini
Ni Imani aliyonayo mtu juu ya jambo fulani. Pia ni Msingi
fulani ambao mwanadamu anaufuata.
KUNDI NA. 2
Umuhimu wa
Kuwa na Imani
1.
Umuhimu wa
Kuwa na Imani ni pamoja na kutoogopa kitu chochote kwa kuwa una Imani.
2.
Utakuwa na imani ya jambo lolote
lile.
3.
Kila jambo utakalolifanya
utakuwa na Imani nalo.
4.
Ukiwa na
Imai utajulikana na mtu yeyote.
5.
Imani
itajenga mahusiano ndani ya familia, ndugu, jamaa, majirani, marafiki nk.
KUNDI
NA. 3
Maadili na Dini
1.
Dini ianzie kwenye familia
2.
Familia ikia na maadili mema ya
Dini itakuwa sambamba.
3.
Wazazi wawe mstari wa mbele
kuelimisha familia
4.
Wazazi wawe mfano kwa familia
5.
Wazazi wawe wasikivu
(kuwasikiliza) watoto wanapohitaji kusikilizwa.
KUNDI NA. 4
Ukoo Uliojengeka
katika Misingi ya Dini
6.
Ubinafsi: Ukoo
uliojengeka katika misingi ya dini unakuwa hauna ubinafsi.
7.
Ukoo
uliojengeka katika dini utakuwa ni ukoo utakaokuwa unajaliana katika matatizo
kutokana na imani walionayo kutokana na Dini.
8.
Watu Kuheshimiana: Dini inafundisha mambo mema; Kwa hiyo ukoo utakapokuwa
na mwamko wa dini hakutakuwa na matatizo ya kudharauliana.
9.
Kuheshimika kwa Ukoo: Kwa kuwa utakuwa na sifa nzuri basi hata koo nyingine
zitapata hamasa ya kujiunga na ukoo.
XII: RATIBA YA MKUTANO MKUU WA KWANZA WA UKOO WA KIVENULE,
DESEMBA 17 – 18, 2005
Siku ya Kwanza ya Mkutano Mkuu wa Ukoo wa KIVENULE |
||
Tarehe
17 Des. 2005 Muda
|
Shughuli/Jukumu
|
Wahusika
|
12:00–12:45
|
Wageni Wote Kuamka na Kufanya Maandalizi ya Kuingia kwenye Mkutano
|
Wote |
12:45–1:45
|
Kupata Kifungua Kinywa
|
Wote
|
1:45 – 2:45
|
Kuwasili Mkutanoni na Kujisajili
|
Wote
|
2:45 – 3:15
|
Ufunguzi wa Mkutano na Mgeni Rasmi
|
Mgeni Rasmi
|
3:15 – 4:00
|
Utambulisho baina wa wana Ndugu
|
Wote
|
4:00 – 4:45
|
Pumziko la Chai / Kahawa/Maji
|
Wote
|
4:45 – 5:30
|
Mada ya Kwanza: CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO |
1. Christian J. Kivenule2. Augustino Kivenule |
5:30 – 6:00
|
Majadiliano katika Makundi
|
Makundi 4
|
6:00 – 6:20
|
Murejesho na Majumuisho
|
Vikundi na Mwezeshaji
|
6:30 – 8:00
|
CHAKULA CHA MCHANA
|
Wote
|
8:00 – 8:45
|
Mada ya Pili: MAHUSIANO BAINA YA NDUGU NDANI YA UKOO WA KIVENULE
|
1. John S. Kivenule
2. Ignas P. Kivenule
3. Stephan Mhapa
|
8:45 – 9:15
|
Majadiliano katika Makundi
|
Makundi 4
|
9:15 – 9:45
|
Murejesho na Majumuisho
|
Vikundi na Mwezeshaji
|
9:45– 10:45
|
Pumziko la Chai/Kahawa/Maji |
Wote
|
10:45-1:30 Usiku
|
Mapumziko Marefu (Kusalimiana na Kufahamiana zaidi)
|
Ndugu na Wageni Wote
|
1:30 – 2:30
|
Chakula cha Usiku na Vinjwaji
|
Ndugu Wote
|
2:30 – 6:30
|
Burudani (Muziki wa Kisasa na Ngoma za Asili)
|
Wote
|
Siku ya Pili ya Mkutano Mkuu wa Ukoo wa KIVENULE |
||
Tarehe
18 Des. 2005 Muda
|
Shughuli/Jukumu
|
Wahusika
|
12:00– 12:45
|
Kuamuka na Kufanya Maandalizi ya Mkutano
|
Wote |
12:45 – 1:45
|
Kifungua Kinywa
|
Wote
|
1:45 – 2:15
|
Kuwasili Mkutanoni na Kujisajili
|
Ndugu wote |
2:15 – 2:45
|
Mada Ya Tatu: ELIMU NA MUSTAKABILI WA UKOO WA KIVENULE
|
1. Christian J. Kivenule
2.
Donat
Mhapa
|
2:45 – 3:15
|
Majadiliano kwenye Makundi
|
Makundi 4
|
3:15 – 3:45
|
Murejesho na Majumuisho
|
Vikundi na Mwezeshaji
|
3:45 – 4:30
|
Pumziko la Chai/Kahawa/Maji
|
Wote
|
4:30 – 5:00
|
Mada ya Nne: UKIMWI NDANI YA UKOO NA ATHARI ZAKE |
1. Maria Milimo
2.
Adam A. Kivenule
|
5:00 – 5:30
|
Majadiliano kwenye Makundi |
Makundi 4 |
5:30 – 6:00
|
Murejesho na Majumuisho |
Vikundi na Mwezeshaji |
6:00 – 7:15
|
CHAKULA CHA MCHANA
|
Wote |
7:15 – 7:45
|
Mada ya Tano: DINI KATIKA UKOO |
1. Jovin D. Kivenule
2. Stephan Mhapa
3. George Kivenule |
7:45 – 8:15
|
Majadiliano kwenye Makundi |
Makundi 4 |
8:15 – 8:45
|
Murejesho na Majumuisho |
Vikundi na Mwezeshaji |
8:45 – 9:45
|
Majumuisho:1. Yote Yaliyojitokeza
2.
Matarajio
3. Tarehe ya Mkutano Mwingine |
Mwezeshaji |
9:45 – 10:15
|
Shukurani toka kwa Ndugu Mbalimbali
|
|
10:15–11:00
|
KUCHAGUA VIONGOZI WA KUUNDA KAMATI YA UKOO
|
Ndugu Wote
|
11:00
|
Kufunga Mkutano
|
Mgeni Rasmi
|
XIII: KAMATI ILIYORATIBU
SHUGHULI KATIKA MKUTANO MKUU WA
KWANZA WA UKOO WA KIVENULE
A: Wawezeshaji
Wa Mada Mbalimbali
1. Christian J. Kivenule
2. Augustino Kivenule
3. Stephan Mhapa
4. Maria Milimo
5. Adam A.
Kivenule
6. Jovin D. Kivenule
7. George S. Kivenule
8. John S. Kivenule
9. Ignas P. Kivenule
B: Wawezeshaji Wasaidizi
1. Lesandu Mhapa
2. Adam A. Kivenule
3. Faustin S. Kivenule
4. Christian J. Kivenule
5. Donath Mhapa
C: Msimamizi wa Vyombo vya Matangazo
1. Lesandu Mhapa
2. Justo Chavala
D: Muda wa Kuwasilisha Mada
·
Muda wa dakika 45 ulitumika
kuwasilisha Mada moja.
·
Majadiliano katika Makundi
yalifanyika kwa dakika kumi; na
·
Uwasilishaji wa hoja kutoka
katika makundi ulitumia dakika tano hadi nane.
Kuwasilisha
Mada[dak.45]; Majadiliano [dak. 10]; Kuwasilisha na Majumuisho [dak.10]
E: Uteuzi wa Makundi ya Majadiliano
[Namna gani makundi yalivyokuwa
yanaundwa]
Makundi
Manne ya Majadiliano yaliundwa kwa kila Mada iliyowasilishwa kwenye Mkutano
Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule. Uundwaji
wa Makundi ya Majadiliano ulifanyika kwa kila mshiriki kuhesabu namba, yaani moja
mpaka nne na kisha kila mshiriki kukariri namba yake. Baadaye washiriki wote
waliohesabu namba moja walikaa kwenye kundi la kwanza, namba mbili kundi la
pili, namba tatu kundi la tatu na kisha namba nne kundi nne.
Kila
mada iliyowasilishwa kwenye Mkutano Mkuu wa Kwanza
wa Ukoo wa Kivenule ilikuwa na dondoo nne. Hivyo makundi yaligawanywa kutokana
na idadi ya hizo dondoo nne.
XIV: TATHMINI YA MKUTANO
MKUU WA KWANZA WA UKOO WA KIVENULE
Wanaukoo
walizishukuru na kuzipongeza Kamati zote za maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule kwa kufanya kazi nzuri.
Walibainisha furaha yao
kwa kusema haya yafuatayo:
1.
Tunawashukuru Wawezeshaji kwa
kujiandaa barabara na pia Waratibu wa shughuli hii wameiratibu vizuri sana.
·
Mpangilio
wa Ratiba ulikuwa ni mzuri sana.
·
Washiriki
wamefanikiwa kuchangia vema kutokana na mpangilio mzuri wa Mada na Wawezeshaji.
2.
Mwitikio wa
wanandugu na wanaukoo umetia moyo sana na hivyo kupiga hatua mbele katika
Mikutano mingine ijayo.
3.
Shukrani
ziwaendelee wale wote waliochangia gharama za kuweza kufanikisha Mkutano huu.
Tunawashukuru pia wale ambao hawakuchangia gharama lakini kuja kwao kwenye
kikao kumetia hamasa kubwa.
4.
Tunawashukuru
wale wote waliotusaidia kuandaa chakula (katika mapishi)…. Na
Kamati za maandalizi wa ujumla.
5.
Tunaushukuru uongozi wa kijiji
cha Kidamali kwa kuuthamini mkutano wetu; tumeshuhudia Mwenyekiti tukiwa naye
siku zote mbili za Mkutano huu.
6.
Tunamshukuru mwenye nyumba
(Bwana Sanga) kwa kutukodisha ukumbi kwani umetusaidia sana.
XV: MAPENDEKEZO/MAONI
YALIYOJITOKEZA WAKATI WA MKUTANO
MKUU WA UKOO
1.
Iundwe Kamati Kuu ya Ukoo,
Kamati Ndogo na Uongozi wa Ukoo na pia wachaguliwe Wawakilishi kulingana na
maeneo husika mfano Magubike, Kidamali, Nyamahana, Nzihi na kadhalika.
Wawakilishi watakaochaguliwa watakuwa wanafanya mawasiliano na Uongozi wa toka
sehemu zao husika. Watatoa taarifa za matatizo au furaha, watatekeleza maagizo
toka kwa Viongozi wa Ukoo na Kamati Kuu ya Ukoo. Lakuzingatia: Wanaukoo wawachague wanaukoo wenye mwelekeo na moyo
wa kujituma na kujitolea na wenye uchungu na maendeleo ya ukoo.
2.
Iundwe Kamati ya Ukoo (Yenye
Uwakilishi wa Wajumbe) toka sehemu mbalimbali itakayoratibu shughuli kadhaa za
ukoo mfano Uanzishwaji wa Mfuko wa kuchangia kutatua matatizo ya wanandugu kama vile ugonjwa, elimu na vifo. Pia inapendekezwa kuwa
wanaukoo wanaoishi vijijini wachangie shilingi 500/= kila mwezi; lakini kila
mwanaukoo awe huru kuchangia zaidi. Watumishi na walio mjini wenye vipato
wachangie shilingi 1000/= kila mwezi.
3.
Wanaukoo wanashauriwa wawe na
imani kwa mwanaukoo yeyote atakayepewa jukumu la usimamizi wa fedha. Suala la
ufunguzi wa Akaunti ni muhimu likazingatiwa.
4.
Iundwe Kamati ya Usuluhishi ya
Ukoo itakayotatua matatizo ya Wanaukoo wote, na iundwe na watu kutoka maeneo
mbalimbali wanakoishi. Kazi yake kubwa itakuwa ni kupokea taarifa za matatizo
na kuyatafutia ufumbuzi.
5.
Michango ianze kuchangwa mara
moja na iachwe ikae angalau mwaka mmoja kabla hajaanza kutumika kuwasaidia wale
wenye matatizo ya ugonjwa, kufiwa na pia kupangwe viwango mahsusi vya
kuwasaidia hao wenye matatizo.
6.
Mfuko utakaoanzishwa kwa ajili
ya kusaidia kwa upande wa Elimu, uegemee zaidi kuwasaidia wale wasio na uwezo.
Wenye uwezo watumie gharama zao kuwasomesha watoto au jamaa. Lakini katika
ugonjwa au misiba basi ndugu wa hali
zote wanufaike.
7.
Achaguliwe mwakilishi wa
wanaukoo kutokana maeneo mbalimbali wanakoishi ili awe anafanya mawasiliano kwa
wanandugu kuhusiana na matatizo au furaha katika maisha yao ya kila siku.
8.
Je wanaukoo mnadhani ni hatua
gani zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya wanandugu/wanaukoo ambao hawaridhii
kuuchangia mfuko huu? Katiba ikitungwa itakuwa na kipengele cha kuwabana wale
ambao hawatoi michango yao.
Mweka Hazina atakuwa na kipengele cha kumbana kuhusiana na utunzaji wa fedha za
michango mbalimbali.
XVI: UCHAGUZI WA VIONGOZI WA UKOO
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoowa Kivenule ulifanya uchaguzi
wa viongozi wa ukoo katika ngazi zifuatazo kama
inavyobainishwa hapa chini:
1. Viongozi wa Ukoo
1.
Faustin S. Kivenule Mwenyekiti
2.
Donath Mhapa Makamu
Mwenyekiti
3.
Christian J. Kivenule Katibu
4.
Severin Nyangalima Katibu Msaidizi
5.
Justin D. Kivenule Mweka
Hazina
6.
Carolina S. Kivenule Mweka
Hazina Msaidizi
2. Washauri wa Uongozi wa Ukoo
1.
John S. Kivenule Morogoro
2.
Stephan Mhapa Kidamali
3.
Edgar S. Kivenule Dar eS Salaam
4.
Pius Kivenule Ilole
3. Wajumbe wa Kamati Kuu ya Ukoo ambao pia ni
Wawakilishi wa
Kamati toka sehemu mbalimbali hapa
Tanzania
1.
Adam A. Kivenule Dar
es Salaam
2.
Ignas P. Kivenule Dar
es Salaam
3.
Jovin D. Kivenule Kidamali
4.
Justin D. Kivenule Kidamali
5.
Faustin S. Kivenule Kidamali
6.
Donati Mhapa Kidamali
7.
Carolina S. Kivenule Kidamali
8.
Zavary S. Kivenule Mufindi
9.
Florian A. Kivenule Mafinga
10.
Augustino Kivenule Nduli
11.
Martin Kivenule Nduli
12.
Vitus Nzala Magubike
13.
Romanus Kivenule Ibogo
14.
Severin Nyangalima Ilalasimba
15.
Marco Kivenule Ilalasimba
16.
Fabian Kivenule Nyamihuu
17.
Christopher Kivenule Ilole
18.
Titus Kivenule Igominyi
19.
Alexander Nyangalima Morogoro
(Mikumi)
20. Christian
Kivenule Morogoro Mjini
XVII: SHUKRANI
Ndugu
Ignas Kivenule ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Ukoo wa Kivenule, aliwashukuru
wanaukoo wote waliotoa ushirikiano na kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo
wa Kivenule, kwa kuwa wameonyesha umoja wa hali ya juu sana. Binafsi yeye
anaamini jamii inayounda Ukoo wa Kivenule ni wapole na wasio na majivuno. Ila
angefurahi sana kama
jamii inayounda ukoo huu itajitokeza kwa wingi zaidi katika Mkutano Mkuu wa
Pili wa Ukoo wa Kivenule, utakaofanyika mwakani 2006.
Ukoo
wa Kivenule una zaidi ya ndugu 2000 kutoka pande zote za Kidamali, Ilole,
Nduli, Magubike na kwingineko. Ni wajibu wa kila mwanaukoo kuhamasisha watu
wengine wajitokeze kuhudhuria Mkutano Mkuu ujao. Sambamba na hilo, pia aliiomba jamii ya Ukoo wa Kivenule
ikalipa umuhimu suala la kusomesha watoto ili kupunguza utegemezi na pia
kuwaandalia hali bora za maisha hapo baadaye.
Alisikitika
kwa wanaukoo toka Ilole kutohudhuria Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa
Kivenule, ila angefurahi sana kama
jamii hiyo ya Ilole ingeshiriki mkutano huo. Kuna sababu nyingi zimetolewa,
likiwemo suala la Nauli. Lakini, kama kila mwanaukoo atakuwa anajali ni jambo
la msingi sana
wangejiandaa kikamilifu kuhudhuria Mkutano ujao.
Wanaukoo
wengi wa kutoka Dar es Salaam
wamekuwa ni wazito na hii pia inakatisha tamaa. Kama
ni matatizo ni vyema jamii yote ikashirikiana. Mojawapo ya mambo mazuri na ya
msingi ya kufanya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa
Ukoo wa Kivenule ni kuiwezesha jamii inayounda ukoo huu, kuwa na uwezo wa kukabiliana
na matatizo ya kila siku. Mwishoni aliwashukuru wanaukoo wote wa Kidamali kwa
moyo wa ukarimu waliouonyesha
XVIII: KUFUNGA MKUTANO
Mgeni Rasmi Daima Luvanda (Mwenyekiti ya Serikali ya Kijiji
cha Kidamali) alifunga rasmi Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule mnamo
saa 3.30 usiku kwa kuzishukuru Kamati za Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo kwa kufanikisha kufanyika kwa mkutano huo.
Pia,
aliwashukuru viongozi wapya waliochaguliwa kuuongoza Ukoo wa Kivenule na
kuahidi kuwa atawapa ushirikiano wa hali na mali kuhakikisha kuwa wanafanikiwa
katika utendaji wao wa kazi. Mgeni Rasmi kwa mara nyingine alitoa shukrani zake
kwa viongozi, Umoja wa Ukoo wa Kivenule kwa ujumla kwa kumteua kuwa Mgeni
Rasmi.
Kwake
binafsi ilisema ilikuwa ni fursa tosha kujifunza mambo mbalimbali ambayo
alikuwa hayajui, na pia kupata somo la kuweza kulifanyia kazi au kuionyesha
jamii yake umuhimu wa kuwa na mkutano wa pamoja kama
ulivyofanyika huu wa Ukoo wa Kivenule.