Uongozi wa Umoja wa Ukoo wa
Kivenule (KAUKI) kwa heshima na taadhima unautambua na pia kuwapongeza wote
waliojitoa kwa hali na mali katika kipindi cha miaka 8 tangu mikutano hii
ilipoanza kufanyika mwaka 2005. Thamani ya mchango wao ni kubwa katika jamii
yetu na ulimwengu kwa ujumla.
Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 9
wa KAUKI, unaenda sambamba na kuangalia mafanikio na changamoto mbalimbali
ambazo KAUKI inaendelea kukumbana nazo. Lakini katika maisha yeyote ya
binadamu, mafanikio na changamoto huenda pamoja.
Mafanikio makubwa ambayo KAUKI
imeyapata kwa kipindi cha miaka 8 ni pamoja na:
1.
Kuwaunganisha Wanaukoo kutoka
maeneo ya Kidamali, Nduli, Magubike, Igominyi, Nduli, Ilalasimba, Kalenga,
Mufindi, Irore, Nyamahana, Mgongo, Nyamihuu, Idodi, Idete, Mufindi, Iringa
Mjini, Itagutwa, Mtera, Morogoro, Kilombero, Dar es Salaam na Dodoma. Watu
wengi wameweza kufahamiana tofauti na mwanzo.
2.
Kufahamiana baina yetu pia
kumetufanya tujitambue na pia kuona athari ya kuingiliana majina kutokana na
uwingi wetu. Ushirikiano umeanza kuonekana katika matukio mbalimbali ya
Kijamii. Blogu yetu ya http://www.tagumtwa.blogoak.com
imekuwa ni kiunganishi kikubwa kwa sababu taarifa mbalimbali zimeanza
kusambazwa. Hali kadhalika, blogu nyingine zimeandaliwa ili kuwahabarisha
wanaukoo
3.
Ushirikiano na upendo wa dhati
baina yetu sasa umeanza kuonekana, na tunashirikiana katika shida na raha.
4.
Wachache wetu wamekuwa mstari wa
mbele katika kuchangia Mfuko wa KAUKI na Mikutano Mikuu. Ombi letu ni
kuwahamasisha wengine nao wachangie Mfuko wa KAUKI na hususani Mkutano Mkuu wa
Tisa wa KAUKI, ambapo kwa mwaka huu utafanya uchaguzi wa viongozi na pia
kuzindua ofisi yake Kidamali kama mipango ya ujenzi itaenda vizuri kama
ilivyokubalika katika Mkutano Mkuu wa 8 wa KAUKI uliofanyika Jijini Dar es Salaam, mwezi Juni 2012.
5.
Fanikio jingine muhimu ni
kufanikiwa kutengeneza Muundo wa Ukoo (Clan Structure) yenye kurasa karibu ya
80. Kila mwana KAUKI atapata nakala yake Wakati wa Mkutano Mkuu wa 9 wa KAUKI
itakayofanyika Kijijini Kidamali. Inaonesha toka kizazi hiki kilipoanza hadi
sasa…, pamoja na taarifa mbalimbali kuhusiana na Kabila la Wahehe zitatolewa.
Hima tunawaomba ndugu, jamaa na
marafiki wenye moyo wa kweli wa kuisaidia jamii inayotahidi kujisaidia kutuunga
mkono katika mchakato huu. Mfuko wa KAUKI una malengo mengi, ripoti zilizomo
kwenye blogu zinaeleza vizuri. Lakini pia unaweza kuwasiliana na viongozi wa
KAUKI kupitia anuani yao:
kauki206@gmail.com
tagumtwa@yahoo.com
na
simu 0713 270364
Kwa taarifa mbalimbali unaweza
kuzipata kupitia blogu http://www.tagumtwa.blogoak.com
http://www.kauki-kauki.blogspot.com
http://www.tagumtwafoundation.wetpaint.com
http://www.adamkivenule.blogspot.com
Imeandaliwa
na kutolewa kwa niaba ya uongozi na:
Adam Alphonce Sigatambule
Tavimyenda Tagumtwa Kivenule
KATIBU KAUKI
No comments:
Post a Comment