TANZIA
Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) kwa masikitiko makubwa
unawatangazia Wana-KAUKI, ndugu, jamaa, marafiki na wanaukoo kwa ujumla, kifo cha
Bi. Gidagamhindi Cecilia Sigatambule Kivenule, kilichotokea tarehe usiku wa
kuamukia tarehe 18 Aprili 2013, huko Magubike, Iringa Vijijini, Mkoani Iringa.
Marehemu Gidagamhinda Kivenule alikuwa akiumwa kwa
muda mrefu na hasa akisumbuliwa na tatizo la upofu wa macho, homa, miguu na
uzee. Kabla ya mauti kumkuta, Marehemu alilazwa kwa muda wa wiki mbili katika
hospitali ya Ipamba, na hali yake kupata auheni lakini siku ya Jumatano tarehe
17 Aprili 2013 akiwa nyumbani hali ilibadilika na hatimaye kumpelekea mauti
kumfika usiku wa tarehe 18 Aprili 2013.
Bi Gidagamhindi ni Mtoto wa Kwanza kwa Bibi
Siwangamhavi Singaile, ambaye alikuwa Mke Mkubwa wa Sigatambu Tavimyenda Tagumtwa
Kivenule. Bibi Siwangumhavi alikuwa na watoto 7 ambapo mpaka sasa wamebaki
watoto 3 tu. Wengine waliomfuata Bi Gidagamhindi ni Semyamba Khadija Kivenule,
Sivanitu Alphonce Kivenule, Kadungu Wiliam Kivenule, Fibumo Xavery Kivenule,
Mlagile Anyesi Kivenule na John Kivenule.
Mazishi yake yalifanyika tarehe 18 Aprili 2013, eneo
la Magubike katika Makaburi ya Ukoo wa akina Nyangalima. Bi Gidagamhindi ataendelea
kukumbukwa kwa upendo, mshikamano na hamasa yake katika kuhakikisha kuwa KAUKI
inaendelea kuwa imara hususani katika eneo la Magubike.
Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi,
Amina.
Imeandaliwa na:
Adam Alphonce Kivenule
Katibu Mkuu - KAUKI
No comments:
Post a Comment