Wahamishiwa Kijijini Magubike Kumuenzi Mzee Hussein Tavimyenda Kivenule
Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) umefanya Mkutano
wake Mkuu wa 9 wa umoja huo katika eneo la Magubike. Mkutano huo ulifanyika
siku ya Jumamosi eneo la Magubike tofauti na Kidamali, kama ilivyopangwa katika
Mkutano Mkuu wa 8 wa KAUKI.
Sababu za msingi za kuhamishia Mkutano Magubike
ilikuwa ni kumuenzi muasisi pekee ya Ukoo wa Kivenule aliyekuwa amebaki, ambaye
aliaga dunia siku ya Jumatano ya tarehe 25 Juni 2013, katika hospitali ya
Ipamba, iliyopo Iringa.
Kwa kuzingatia umuhimu wake kwa ukoo wa Kivenule na
pia kumpa heshima, Uongozi wa KAUKI ulibadilisha mahali pa kufanyia Mkutano
ikiwa ni muhsusi ya kuuheshimu mchango wake na juhudi kubwa aliyoifanya
kuunganisha ukoo wa Kivenule.
Mzee Hussein Sigatambuli Tavimyenda Tagumtwa
Kivenule, alizikwa siku ya Alhamisi katika makaburi yaliyopo eneo la Magubike,
karibu kabisa na nyumbani kwake. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali
pema peponi, Amina.
Kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa 9 wa KAUKI, kulienda
sambamba na kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Viongozi wa KAUKI, ambao walikuwa
wanamaliza muda wao. Uchaguzi huo uliwarudisha katika uongozi baadhi ya
viongozi wake waliokuwa madarakani; akiwemo Katibu Mkuu Ndugu Adam Alphonce
Sigatambule Tavimyenda Tagumtwa Kivenule, Makamu wa Mwenyekiti Ndugu Christian
John Kivenule, Mweka Hazina Ndugu Justin Daniel Kivenule, Mweka Hazina Msaidizi
Ndugu Caroline Sigatambule Kivenule na Jermana Peter Mhapa.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa 8 wa KAUKI uliofanyika Jijini Dar es Salaam, mwaka 2012 |
Hali kadhalika, Mwenyekiti Mwasisi wa KAUKI
alirudishwa katika madaraka kwa kuchukua nafasi ya Mwenyekiti aliyemaliza muda
wake, Ndugu Donath Peter Mhapa. Mwenyekiti wa sasa wa KAUKI ni Ndugu Faustino
Sigatambule Tavimyenda Tagumtwa Kivenule, ambaye makazi yake ni Kidamali.
Aliyekuwa Kiongozi wa Kanda ya Magubike Ndugu Vitus
Nzala alichaguliwa kuwa Makamu wa Katibu wa KAUKI.
Ifuatayo ni safu ya viongozi wa KAUKI:
1. Mwenyekiti Ndugu Faustino Sigatambule Kivenule
2. Makamu Mwenyekiti Ndugu Christian John Kivenule
3. Katibu Mkuu Ndugu Adam Alphonce Kivenule
4. Makamu Katibu Mkuu Ndugu Vitus Nzala
5. Mweka Hazina Ndugu
Justin Daniel Kivenule
6. Mweka Hazina Msaidizi Ndugu Carolina Sigatambule Kivenule
7. Mweka Hazina Msaidizi Ndugu Jermana Peter Mhapa
Sambamba na uchaguzi wa Viongozi wa KAUKI, mkutano
uliwachagua Walezi wa Kanda na kubainisha majukumu yao.
Majukumu Makuu ya Walezi ni:
1. Kuhamasisha Wana-KAUKI katika Kanda ili wawe na mwamko
katika masuala mbalimbali yanayohusiana na maendeleo ya KAUKI. Kumekuwepo na
kususua sua kwa shughuli za KAUKI katika Kanda iwepo kushindwa kubisa
kutekelezwa kwa shughuli za maendeleo. Kuwepo kwa Walezi kutasaidia katika
kuwahimiza viongozi waliopewa majukumu kuwajibika kikamilifu, na pia kuishauri
jamii inayounda KAUKI katika maeneo hayo, kujitoa kwa hali na mali.
2. Kuwahimiza viongozi kuwajibika kwa mujibu wa nafasi zao.
Majukumu yote ya viongozi yapo katika Katiba ya KAUKI. Hivyo pale Ambato
itaonekana uongozi unazembea, Mlezi wa Kanda ana jukumu la kuwahimiza viongozi
husika kujiwabika kwa mujibu wa majukumu yake ya kazi.
3. Kuhudhuria vikao vyote vya Kanda ambavyo vitaitishwa na
Viongozi wa Kanda wa KAUKI au vile vya Kamati mbalimbali za KAUKI katika Kanda.
4. Kuitisha kikao/vikao katika Kanda kama kuna suala la msingi
ambalo linapaswa kuzunguzwa na kujadiliwa kwa maendeleo ya KAUKI.
Viongozi Walezi wa Kanda waliochaguliwa ni pamoja
na:
1. Ndugu Innocent Samwel Kivenule (Kanda ya Dar es
Salaam)
2. Ndugu Amalia Kivenule (Kanda ya Irore)
3. Ndugu Augustino Kivenule (Kanda ya Nduli)
4. Ndugu Happy Kivenule (Kanda ya Mufindi)
5. Ndugu Benard Kivenule (Kanda ya Magubike)
6. Ndugu Donath Peter Mhapa (Kanda ya Kidamali)
Wa kwanza kushoto, Mwenyekiti Mpya wa KAUKI aliyerejea tena madarakani, kuongoza KAUKI kwa kipindi cha miaka 3. |
Mkutano Mkuu wa 9 wa KAUKI uliwaelekeza wajumbe wa
Mkutano huo kwenda kuwachagua viongozi wa Kanda katika Kanda zao.
Sambamba na yote hayo kufanyika, Mkutano Mkuu wa 9
wa KAUKI ulitangaza tarehe ya Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI kuwa ni tarehe 28 -
29 Juni 2014; utakaofanyika katika Kijiji cha Kidamali, Mkoani Iringa.
Imeandaliwa na:
Adam A. Kivenule
Katibu Mkuu - KAUKI
+255 713 270364
No comments:
Post a Comment