Uongozi wa Umoja Wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI), kwa niaba
ya Wana Ukoo wote, unawashukuru wote waliofanikisha Mkutano Mkuu wa 11 wa
KAUKI, uliofanyika Vilalo, Kanda ya Irore, Mkoani Iringa, tarehe 2 Julai 2016.
Tunatambua kuandaa mkutano wowote ni gharama, hivyo tunawapongeza kwa kujitoa
kwao. Ni shughuli inayohitaji raslimali watu, fedha na
zana ili kuweza kufikia lengo. Ni jambo la kujivunia na pia kutia moyo kwa wale
wote ambao wameshiriki kikamilifu na kwa hali na mali katika jukumu hili. Licha
ya kuwepo kwa watu wachache walioshiriki katika maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 11
wa KAUKI, lakini umeweza kufanyika kwa mafanikio.
KAUKI pia inatoa shukrani za pekee kwa Uongozi wa KAUKI Kanda
ya Irore, kwa kuhamasisha Wana Ukoo kushiriki kikamilifu katika maandalizi na
pia kushiriki katika Mkutano Mkuu wa 11 wa KAUKI. Shukrani
za pekee ziwaendee Ndugu Castory Kivenule, Pius Kivenule, Benard Kivenule,
Amalia Kivenule, Michael Mateka na Wanaukoo kwa ujumla kwa moyo wao wa upendo
na ukarimu, kwa kuamua kubeba jukumu hili. Uongozi wa KAUKI unawashukuru pia wanaukoo
wote toka Kanda nyingine za Kidamali, Dar es Salaam na Kalenga kwa ushiriki
wao. Pengine, kutokuwepo kwao, Mkutano huo usingeweza kufanikiwa.
Mwisho, shukrani za pekee ziwaendee ndugu zetu walioshiriki
Mkutano Mkuu wa 11 kwa mara ya kwanza. Hii inaonesha dhamira yao ya dhati ya
kuendelea kushirikiana na Wana Ukoo wenzao. Hali kadhalika wameonesha shauku ya
kutaka kuujua ukoo na kuwafahamu wenzao.
Asante,
Imeandaliwa na:
Adam Kivenule
Katibu Mkuu, KAUKI
No comments:
Post a Comment