Ndugu Mgeni Rasmi,
Ndugu
Wageni Waalikwa;
Wanaukoo
na Jamii yote inayounda KAUKI;
Ndugu
Majirani, Marafiki na Jamii yote Iliyojumuika Nasi;
Mabibi
na Mabwana;
Kamwene…, Munogage…, Makasi…,
Awali ya yote, nimwombe Mwenyezi
Mungu, Mwingi wa Rehema, uzima na Baraka, awape nguvu, afya na amani, wote
mliokusanyika katika Mkutano huu wa 9 wa KAUKI.
Pili, nimwombe Mwenyezi Mungu,
awaepushe na hatari, rapsah na ubaya wowote ulioelekezwa kwenu; awalinde kutoka
saa hii ya ufunguzi wa Mkutano hadi kesho wakati wa kuhitimisha shughuli hii
muhimu kwa mwaka huu 2013.
Tatu, nawaomba wote tusimame kwa
dakika moja (1) kuwakumbuka ndugu zetu ambao wametangulia mbele ya haki kutoka mwaka
jana hadi mwezi Juni mwaka 2013. Ndugu waliotangulia mbele za haki ni:
- Luhanage Ponsiano Sigatambule Kivenule
- Flomina Pangalas Kivenule
- Gidagumhindi (Cecilia) Sigatambule Kivenule
- Atanas
- Mzee wetu Babu Hussein Tavimyenda Tagumtwa Kivenule
Mwenyezi Mungu azilaze Roho za
Marehemu mahali pema peponi, Amina.
Baada ya utangulizi huo mfupi, ni
furaha kubwa kujumuika na hadhara hii siku ya leo. Ni matumaini yangu kuwa wote ni wazima wa
afya na pia uwepo wenu unaonesha namna mnavyothamini shughuli hii muhimu
itakayofanyika kwa muda wa siku mbili; yaani leo na kesho, hali kadhalika
kuhakikisha kuwa Mkutano Mkuu wa 9 wa KAUKI unafakiwa.
Ni furaha iliyoje kuwa nanyi katika
hadhara hii. Ni matumaini yangu kuwa, wote ni wazima wa afya na kuwepo kwenu
pia kuonesha jinsi mnavyothamini shughuli ambayo tutaifanya kwa siku mbili,
yaani leo na kesho katika kuhakikisha kuwa Mkutano Mkuu wa Tisa wa KAUKI
unafanikiwa.
Ndugu Mgeni Rasmi; nianze kutoa historia fupi ya umoja huu. KAUKI
ni Umoja wa Ukoo wa Kivenule, ulioanzishwa rasmi mwaka 2005, kukabiliana na
changamoto mbalimbali za maendeleo, zinazoikabili jamii inayounda umoja huu;
hususani katika kujikwamua na ugumu wa maisha na pia kutumia fursa
zinazopatikana ili kukabiliana na kuondokana na wimbi la umaskini, ujinga,
maradhi na utegemezi. Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI), ulianzishwa rasmi mnamo
Desemba 17 - 18, 2005 Kijijini Kidamali. Harakati za kuanzishwa kwa KAUKI zilianza
mwezi Februari 06, 2005 Jijini Dar es Salaam kwa kufanya mkutano wa kwanza wa
mashauriano. Harakati nyingine na kuunda kamati za maandalizi zilielekezwa
upande wa Kidamali, Ilole na Nduli. Kwa upande wa Kidamali, Mkutano wa kwanza
wa maandalizi ya Mkutano Mkuu ulifanyika mwezi Mei ambapo wajumbe toka Dar es
Salaam walishiriki katika majadiliano, kuchagua viongozi wa kuunda kamati ya
maandalizi na kuhamasisha.
Ndugu Mgeni Rasmi; Umoja wa Ukoo wa
Kivenule ulizinduliwa rasmi mwaka 2006, katika Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo wa
Kivenule uliofanyika tarehe 24 – 25 Juni 2006 katika Ukumbi wa Sanga Kijijini
Kidamali, Iringa. Kuzinduliwa kwa Umoja wa Ukoo wa Kivenule, kulienda sambamba
na uzinduzi wa Mfuko wa Ukoo pamoja na Kuipitisha Rasimu ya Katiba ya Umoja wa
Ukoo wa Kivenule na kuwa Katiba Rasmi; hivyo kutoa fursa ya kuanza kwa utekelezaji
wa shughuli na mipango mbalimbali ya maendeleo. Pia, pamoja na mambo mengine,
katika Mkutano Mkuu wa Pili wa Ukoo, kulifanyika uchaguzi wa Viongozi wa Kanda,
uchaguzi wa Walezi wa Ukoo na hivyo utendaji rasmi wa KAUKI kuruhusiwa kuanza.
Ndugu Mgeni Rasmi; Huu ni Mkutano
Mkuu wa Tisa wa KAUKI; na tayari mikutano mingine Nane imekwisha fanyika,
mitatu kijijini Kidamali na mkutano moja kijijini Irole, Nduli Magubike,
Igowole-Mufindi na Jijini Dar es Salaam. Huu ni mzunguko mwingine tena baada ya
kumaliza kanda zote. Pengine mkutano huu utashauri namna nyingine ya uendeshaji
wa mikutano ya namna hii.
Malengo ya KAUKI
Ndugu Mgeni Rasmi; malengo makuu ya
KAUKI ni kujaribu kwa kila hali kwa kutumia ujuzi na maarifa, kuinua uwezo wa
kielimu, kiuchumi na kimaendeleo, kwa wanajamii wanaounda umoja huo, kwa
kutumia rasilimali mbalimbali zinazopatika katika nchi ya Tanzania na hususani
katika maeneo wanayoishi; ikiwa ni pamoja kuihamasisha jamii hii kufanya kazi
kwa juhudi na maarifa ili kupunguza umaskini unaowakabili.
KAUKI imeanzishwa kukidhi shida na
mahitaji ya jamii iliyounda umoja huu na hususani katika maeneo lengwa ya
elimu, afya, uchumi na maendeleo, kwa kushirikisha mawazo, fikra, ujuzi na
maarifa ya kila mwanaukoo, katika mikutano mikuu na mikutano midogo midogo,
ambayo inaandaliwa na wanaukoo wenyewe. Kwa kukutana pamoja, fikra za kujenga,
ujuzi, uzoefu, kujengewa uwezo na maarifa, huunganishwa pamoja na kisha kupanga
mikakati mbadala ya kuweza kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika
maisha.
Ndugu Mgeni Rasmi; malengo KAUKI ni
mengi na baadhi yake ni:
·
kuwa na ofisi yake Kijijini
Kidamali na pia sehemu nyingine za Kanda
·
Kuisajili KAUKI na kuwa na mfuko wa
kusaidia ndugu katika elimu, afya na matatizo mengine. Tayari mfuko umeanzishwa
na unaendelea kuchangiwa.
·
kuwa na sanduku lake la posta,
tovuti. Kwa sasa ina tovuti inayopatika
kupitia www.tagumwafoundation.wetpaint.com
na inaboreshwa kupitia www.tagumtwa.blogoak.com
na www.kauki-kauki.blogspot.com
·
Kuwa na Akaunti katika Benki –
tayari imefungua katika Benki ya NMB, Iringa Mjini
·
kuwa na vitendea kazi mfano
Kompyuta, Printa, Simu, Meza na Viti
·
kuanza kutoa elimu mbalimbali kwa
wadau wake. Inatoa elimu katika mikutano yake
·
kubuni na kutekeleza miradi ambayo
itawasadia wanajamii. Mpango wa Mradi wa Alizeti-Irole, ambao bado haujaanza
kutekelezwa.
·
kuwa na kitengo cha Utaalam wa
Kitaaluma na Kiujuzi ambacho kitafanya shughuli za kuiletea fedha KAUKI, pamoja
na miradi mbalimbali. Ipo katika mchakato.
·
Kuchapisha kitabu toleo la kwanza
cha Umoja wa Ukoo wa Kivenule kwa kipindi cha mwaka 2009-2013. Kazi inaendelea
na taarifa mbalimbali zinaendelea kukusanywa.
Mafanikio
Ndugu Mgeni Rasmi; KAUKI imefanikiwa
kufanya yafuatayo:
·
kuendelea kufanyika kwa mikutano
mkuu. Mikutano Mikuu nane tayari imefanyika Kidamali mara tatu, Irole, Nduli,
Magubike, Igowole-Mufindi na mara moja moja.
·
kupanua wigo wa ushiriki kutoka
Irole, Nduli, Itagutwa, Mgongo na Mufindi; Kilimanjaro, Dar es Salaam, Morogoro
na maeneo mengine.
·
Kuongezeka kwa ufahamu na uelewa wa
watu kuhusu KAUKI na mada zinazofundishwa
·
Kufahamiana baina ya wana-KAUKI
kumeongezeka mara dufu
·
Kuanzishwa kwa Mfuko wa KAUKI
·
Imeanzisha blogs ambazo zinabeba taarifa
mbalimbali za KAUKI na wana-KAUKI kwa ujumla.
Changamoto
Ndugu Mgeni Rasmi; Changamoto
zinazoikabili KAUKI ni pamoja na
·
Ushiriki duni wa wanaukoo katika
mikutano mikuu.
·
Kasi ndogo na moyo wa kuchangia
mfuko wa kusaidia wanaukoo
·
Kutokidhi gharama za kuandaa mikutano
hii kwa sababu michango inakuwa ni kidogo
·
Kutofikia malengo ya mipango
tunayojiwekea
·
Ndugu wa mijini kuwa na mwamko
mdogo wa kuunga mkono jitihada hizi
Matarajio katika Mkutano Mkuu wa Tisa wa KAUKI
Ndugu Mgeni Rasmi; Kama Ratiba
inavyoonesha, hayo ndiyo yatakayofanyika katika siku mbili za Mkutano Mkuu wa Tisa
wa KAUKI. Lakini, tunategemea kuwa na Mada kadhaa ikiwemo ya Chimbuko Historia
ya Ukoo ambapo tutaijadili kwa undani zaidi. Lakini pia, masuala mengine mfano
elimu, maendeleo na ushirikiano wa dhati baina ya wanandugu yatapewa kipaumbele.
Utambulisho baina ya wanaukoo
utafanyika kwa kina na kila ndugu/mwanaukoo atakuwa na kitambulisho ambacho
atakivaa kifuani kwake. Kutakuwa na fursa mbalimbali kwa wanandugu kupeana
uzoefu mbalimbali wa utafutaji wa maisha bora. Mbinu za kujiinua kimaisha
zitafundishwa na wadau wenye uzoefu pamoja na aina mbalimbali za miradi ambayo
ndugu wanaweza kufanya.
Tutakuwa na kipindi cha kupeana
uzoefu wa shughuli mbalimbali za kiuchumi kutoka katika maeneo mbalimbali
ambako ndugu wanaishi. Kama ilivyofanyika katika Mkutano Mkuu wa Tatu, Nne,
Tano, Sita, Saba na Nane wa KAUKI, maeneo yatakayotolewa uzoefu Kilimo,
biashara na ajira kutoka katika maeneo mbalimbali. Kwa kupeana elimu ya
ujasiliamali itasaidia kutufungua macho na hivyo kuongeza uwezo wa kufikiri na
kwenda kutafuta maisha katika maeneo ambayo ni mbadala kwetu. Pia taarifa hizi
zitawasaidia wanandugu toka maeneo mengine kupata mwanga wa shughuli mbadala
zitakazosaidia kupata kipato na kuboresha maisha.
Matarajio ya Mbeleni
Ndugu Mgeni Rasmi; Mipango ya KAUKI
kwa mwaka uliopita 2011 na 2012
·
Kuendeleza jitihada za kufungua
ofisi Kidamali na kununua vifaa vya ndani ya ofisi kama vile kompyuta, printa
na fenicha.
·
Kuchapisha kitabu cha historia ya wahehe
ambapo ndani yake pia kutakuwa na taarifa za KAUKI.
·
Kuongeza wigo wa ushiriki katika
mikutano; na
·
Kuhamasisha wana-KAUKI kuchangia
mfuko
Hitimisho
Ndugu Mgeni Rasmi; KAUKI imeendelea
kujikita katika kuongeza uangavu na weledi kwa wanaukoo kutokana na kutambua
changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika dunia hii ya ushindani. Ugumu wa
maisha, mfumuko wa bei, ukosefu wa ajira, na changamoto mbalimbali ambazo kila mwana-KAUKI
anaiona, ameguswa nayo au kuathiriwa nayo. Tatizo la ufisadi wa raslimali za watanzania,
rushwa katika huduma za jamii mfano kukosa dawa hospitalini, maji safi na salama,
elimu duni na ukosefu wa ajira, vyote vinatuathiri sisi. KAUKI inaamini kuwa
mwana-KAUKI mwenyewe ndiye mwenye uamuzi wa mwisho ya kuamua hatma na mustakabali
wa maisha yake ya sasa na baadaye. KAUKI haitarajii maisha bora kwa kila
mwana-KAUKI au mtanzania mwingine yataletwa na wanasiasa au watu baki waliopo
nje ya nchi yetu. Jukumu la maendeleo ni letu sisi wenyewe. Ndio maana
tunahimiza watu kujitoa kwa hali na mali kuuchangia mfuko wetu ili uweze
kuisaidia jamii yetu katika nyanja zote za kiuchumi, elimu, afya na maendeleo.
Ndugu Mgeni Rasmi, baada ya kusema
hayo machache, kwa niaba ya Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu ya Kidamali, Iringa,
inakuomba Ufungue Rasmi Mkutano Mkuu wa Tisa wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule
(KAUKI).
Karibu Sana
Imetolewa na:
Ndugu Donath Mhapa
Mwenyekiti wa KAUKI
Kwa Niaba ya Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Tisa wa KAUKI