MKUTANO MKUU WA 10 WA KAUKI

MKUTANO MKUU WA 10 WA KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

KAUKI-Kidamali, Iringa

KAUKI-Kidamali, Iringa
Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Friday, May 3, 2013

TAARIFA KWA UMMA WA WANA-KAUKI NA JAMII KWA UJUMLA



Uongozi wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) kwa heshima na taadhima unautambua na pia kuwapongeza wote waliojitoa kwa hali na mali katika kipindi cha miaka 8 tangu mikutano hii ilipoanza kufanyika mwaka 2005. Thamani ya mchango wao ni kubwa katika jamii yetu na ulimwengu kwa ujumla.

Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 9 wa KAUKI, unaenda sambamba na kuangalia mafanikio na changamoto mbalimbali ambazo KAUKI inaendelea kukumbana nazo. Lakini katika maisha yeyote ya binadamu, mafanikio na changamoto huenda pamoja.

Mafanikio makubwa ambayo KAUKI imeyapata kwa kipindi cha miaka 8 ni pamoja na:
1.   Kuwaunganisha Wanaukoo kutoka maeneo ya Kidamali, Nduli, Magubike, Igominyi, Nduli, Ilalasimba, Kalenga, Mufindi, Irore, Nyamahana, Mgongo, Nyamihuu, Idodi, Idete, Mufindi, Iringa Mjini, Itagutwa, Mtera, Morogoro, Kilombero, Dar es Salaam na Dodoma. Watu wengi wameweza kufahamiana tofauti na mwanzo.

2.   Kufahamiana baina yetu pia kumetufanya tujitambue na pia kuona athari ya kuingiliana majina kutokana na uwingi wetu. Ushirikiano umeanza kuonekana katika matukio mbalimbali ya Kijamii. Blogu yetu ya http://www.tagumtwa.blogoak.com imekuwa ni kiunganishi kikubwa kwa sababu taarifa mbalimbali zimeanza kusambazwa. Hali kadhalika, blogu nyingine zimeandaliwa ili kuwahabarisha wanaukoo

3.   Ushirikiano na upendo wa dhati baina yetu sasa umeanza kuonekana, na tunashirikiana katika shida na raha.

4.   Wachache wetu wamekuwa mstari wa mbele katika kuchangia Mfuko wa KAUKI na Mikutano Mikuu. Ombi letu ni kuwahamasisha wengine nao wachangie Mfuko wa KAUKI na hususani Mkutano Mkuu wa Tisa wa KAUKI, ambapo kwa mwaka huu utafanya uchaguzi wa viongozi na pia kuzindua ofisi yake Kidamali kama mipango ya ujenzi itaenda vizuri kama ilivyokubalika katika Mkutano Mkuu wa 8 wa KAUKI uliofanyika Jijini  Dar es Salaam, mwezi Juni 2012.

5.   Fanikio jingine muhimu ni kufanikiwa kutengeneza Muundo wa Ukoo (Clan Structure) yenye kurasa karibu ya 80. Kila mwana KAUKI atapata nakala yake Wakati wa Mkutano Mkuu wa 9 wa KAUKI itakayofanyika Kijijini Kidamali. Inaonesha toka kizazi hiki kilipoanza hadi sasa…, pamoja na taarifa mbalimbali kuhusiana na Kabila la Wahehe zitatolewa.

Hima tunawaomba ndugu, jamaa na marafiki wenye moyo wa kweli wa kuisaidia jamii inayotahidi kujisaidia kutuunga mkono katika mchakato huu. Mfuko wa KAUKI una malengo mengi, ripoti zilizomo kwenye blogu zinaeleza vizuri. Lakini pia unaweza kuwasiliana na viongozi wa KAUKI kupitia anuani yao:
kauki206@gmail.com
tagumtwa@yahoo.com
na
simu 0713 270364

Kwa taarifa mbalimbali unaweza kuzipata kupitia blogu http://www.tagumtwa.blogoak.com
http://www.kauki-kauki.blogspot.com
http://www.tagumtwafoundation.wetpaint.com
http://www.adamkivenule.blogspot.com

Imeandaliwa na kutolewa kwa niaba ya uongozi na:



Adam Alphonce Sigatambule Tavimyenda Tagumtwa Kivenule
KATIBU KAUKI

No comments:

Post a Comment