MKUTANO MKUU WA 10 WA KAUKI

MKUTANO MKUU WA 10 WA KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

KAUKI-Kidamali, Iringa

KAUKI-Kidamali, Iringa
Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Friday, May 3, 2013

BI GIDAGAMHINDI CECILIA SIGATAMBULE KIVENULE AMEFARIKI



TANZIA
Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI) kwa masikitiko makubwa unawatangazia Wana-KAUKI, ndugu, jamaa, marafiki na wanaukoo kwa ujumla, kifo cha Bi. Gidagamhindi Cecilia Sigatambule Kivenule, kilichotokea tarehe usiku wa kuamukia tarehe 18 Aprili 2013, huko Magubike, Iringa Vijijini, Mkoani Iringa.

Marehemu Gidagamhinda Kivenule alikuwa akiumwa kwa muda mrefu na hasa akisumbuliwa na tatizo la upofu wa macho, homa, miguu na uzee. Kabla ya mauti kumkuta, Marehemu alilazwa kwa muda wa wiki mbili katika hospitali ya Ipamba, na hali yake kupata auheni lakini siku ya Jumatano tarehe 17 Aprili 2013 akiwa nyumbani hali ilibadilika na hatimaye kumpelekea mauti kumfika usiku wa tarehe 18 Aprili 2013.

Bi Gidagamhindi ni Mtoto wa Kwanza kwa Bibi Siwangamhavi Singaile, ambaye alikuwa Mke Mkubwa wa Sigatambu Tavimyenda Tagumtwa Kivenule. Bibi Siwangumhavi alikuwa na watoto 7 ambapo mpaka sasa wamebaki watoto 3 tu. Wengine waliomfuata Bi Gidagamhindi ni Semyamba Khadija Kivenule, Sivanitu Alphonce Kivenule, Kadungu Wiliam Kivenule, Fibumo Xavery Kivenule, Mlagile Anyesi Kivenule na John Kivenule.

Mazishi yake yalifanyika tarehe 18 Aprili 2013, eneo la Magubike katika Makaburi ya Ukoo wa akina Nyangalima. Bi Gidagamhindi ataendelea kukumbukwa kwa upendo, mshikamano na hamasa yake katika kuhakikisha kuwa KAUKI inaendelea kuwa imara hususani katika eneo la Magubike.

Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi, Amina.

Imeandaliwa na:


Adam Alphonce Kivenule
Katibu Mkuu - KAUKI

No comments:

Post a Comment