MKUTANO MKUU WA 10 WA KAUKI

MKUTANO MKUU WA 10 WA KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

KAUKI-Kidamali, Iringa

KAUKI-Kidamali, Iringa
Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Thursday, April 11, 2013

MAHUSIANO BAINA YA WANANDUGU NDANI YA UKOO



Maana ya Mahusiano ni hali ya ukaribu, ujirani, urafiki, umoja au ushirikiano unaojengeka baina ya Ndugu, Jamaa au Marafiki. Mahusiano ni hali ya kuwa pamoja Kifikra, Kimwili, Kimawasiliano, Kiimani, Kiitikadi, Kimaendeleo, Kikazi, Kijamii na Kimichezo.

Mahusiano hujengwa kwa misingi/namna mbalimbali. Baadhi ya njia au vitu vinavyosababisha kukawepo na mahusiano ni pamoja na:
1.    Ujirani: Ujirani mara nyingi katika jamii zetu huchangia sana katika kujenga Mahusiano. Mahusiano yenyewe huonekana katika sura mbili tofauti. Yaani Mahusiano Mazuri kwa maana ya Sura Nzuri au Mahusiano Mabaya kwa maana ya Sura ya Ubaya.
2.    Undugu: Hii ni aina ya nyingine ya Mahusiano ambapo ndugu wa Damu Moja au wanachangia damu, hujenga Mahusiano ya Moja kwa Moja (Automatic Relationship). Mara nyingi Mahusiano ya aina hii huwa na Sura ya Uzuri zaidi (Mahusiano Mazuri). Japo kuna kipindi Fulani hata Sura ya Ubaya (Mahusiano Mabaya) hujitokeza.
3.    Imani: Pia watu huweza kujenga Mahusiano kupitia Imani zao, mfano watu wanaoabudu katika dhehebu moja huweza kujenga mahusiano ya aina yao tofauti na dhehebu jingine. Mara nyingi Mahusiano ya Kiimani huwa na mwelekeo wa Mahusiano memo. Mahusiano mabaya mara nyingine hutokea na hata kusababisha vita vya kiimani (dini).
4.    Itikadi: Mahusiano ya Kiitikadi nayo hujengeka kwa kufuata Mlengo wa Vyama Vyao. Na zaidi Mahusiano ya Kiitikadi huegemea zaidi kwenye siasa na hupungua au kutoweka kabisa baada ya mmoja wao kubadili Itikadi yake yaani kuhama toka chama cha kimoja cha siasa na kwenye chama kingine cha siasa. Mahusiano ya Kiitikadi hujengwa kwa misingi ya Chuki, Fitina na Vitisho baina wa watu wa Itikadi moja na wale wa Itikadi nyingine.
5.    Maendeleo: Watu wenye hali fulani ya kimaendeleo huweza kujenga aina fulani ya mahusiano yenye nia ya kuinuia hali zao za kimaisha. Na mara nyingi wanaojumuika hapa ni wale ambao tayari wameonesha nia na mwelekeo. Lakini pia hata wale waliopiga hatua kimaendeleo huweza kuja mahusiano yao yakiwa nia ya kuimarisha hali walizonazo. Msingi mkubwa wa mahusiano ya aina hii huwa ni kupeana mbinu na mikakati ya kuleta au kujiimarisha zaidi katika maendeleo ambayo wanayatarajia au ambayo wamekwisha yapata.

Pia hata kwa upande wa wale wenye hali duni ya kimaendeleo nao hujenga aina Fulani ya mahusiano kulingana na hali na uwezo wao. Kasoro ambayo hujitokeza hapa huwa ni mahusiano duni baina wenye uwezo (matajiri) na wale na wasio na uwezo (maskini). Katika kujiimarisha zaidi kimaendeleo, maskini huwa mtumishi (kibarua) na tajiri huwa mtumikiwa (mtwana).

6.    Elimu: Watu wenye elimu nao mara nyining hujenga mahusiano yao. Mara nyingi katika mahusiano yao huwatenga wale wenye elimu kidogo au wasio na elimu kabisa. Hii hutokea zaidi kwa wale waliobahatika kupata Elimu ya Juu mfano Chuo Kikuu. Mazungumzo na mipango yao huwatenga zaidi wale wenye elimu kidogo. Kuwatenga hujitokeza katika matumizi ya lugha za kigeni, kutowashirikisha katika mawazo mbalimbali ambayo wanadhani yanaweza kuwainua watu wa hali zote (wasomi na wasio wasomi).

AINA ZA MAHUSIANO
Kuna aina mbalimbali za mahusiano, lakini tunaweza kugawanya mahusiano haya katika sehemu kuu mbili.
1.    Mahusiano Mazuri; na
2.    Mahusiano Mabaya.

Aina mbalimbali za mahusiano ambayo yapo katika jamii zetu ni pamoja na mahusiano ya:
§        Kikazi;
§        Kijamii;
§        Kisiasa; na
§        Kiuchumi.

MAHUSIANO MAZURI
Mahusiano Mazuri ni hali ya kuwa pamoja kwa kushirikiana katika nyanja mbalimbali za maisha. Mahusiano Mazuri huwa katika shida au raha. Raha hujumuisha hali zozote zenye kuashiria mafanikio na maendeleo katika maisha ya binadamu. Hii ni pamoja na kufaulu mitihani mbalimbali ya darasani na ya maisha; kujenga nyumba, kununua gari, kapata kazi nzuri, kufanikiwa katika kilimo, Jubilei, kupandishwa cheo pamoja na kupata nishani.

Shida huwa ni hali ya kuwa na mashaka, kutokuwa na uhakika wa maisha, kutokuwa na kipato, kutofanikiwa katika elimu, ugonjwa, misongamano (Depression), misusuko (stress), kutokuwa na ajira, kutofadhiliwa kwa hali yoyote (Promotion au Scholarship) na kadhalika.

MAHUSIANO MABAYA
Mahusiano Mabaya ni hali ya kutokuwa na ushirikiano, huruma au wema katika nyanja mbalimbali za maisha. Mahusiano Mabaya nayo hali kadhalika huwa katika ubaya au uzuri au shida na raha. Tofauti na katika Mahusiano Mazuri, Mahusiano Mabaya hubaki kuwa katika shida na raha. Kwa ujumla ushirikiano na mawasiliano hukosekana kabisa. Huwa hakuna huruma, maelewano, kuvumiliana na kuwasiliana.

Kikubwa ambacho hujengeka ni chuki, majivuno, wivu, ugomvi na kutakiana shari. Hamna hata mmojawapo ambaye huombewa kheri. Kwa yule aliyenacho, huombea au hutamaini yeye aendelee kuwa nacho peke yake na kutomwombea kheri ya kupata yule ambaye hana kitu.

Na kwa yule ambaye hana, humwombea shari, bahati mbaya kupoteza au kwa namna yoyote ambayo haina kheri kwa yule ambaye anacho. Baadhi huomba mfano kama ni gari lipate ajari, nyumba iungue na kama anasoma anafeli. Katika aina hii ya mahusiano hakuna nafasi ya kutakiana mema au maendeleo.

MAHUSIANO BAINA YA NDUGU NDANI YA UKOO
Ukoo wa Kivenule ni mkubwa sana na kwa haraka unakadiriwa kuwa na ndugu karibia elfu mbili (2000). Ni ukoo ambao unaweza kufanya mambo makubwa nay a kimaendeleo kama utaungana na kuwa kitu kimoja.

Tatizo kubwa ambalo linaonekana kwa wanaukoo ni kuwa na mwamko mdogo. Kwa mfano wanaukoo wanaohudhuria Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule ni theluthi au robo tu ya wanaukoo wote. Tumaini la Kamati za Maandalizi ya MKutano Mkuu ni kuhudhuriwa na Ndugu pamoja na Wanaukoo wa Kivenule kwa wingi zaidi.

Kwa upande wa Dar es Salaam, mwamko wao ni mdogo sana. Tumaini na tegemeo la awali ilikuwa Dar es Salaam ingekuwa ni mfano, lakini imeshindika na hii ndiyo hali halisi. Tunasikitika na Kamati ya maandalizi ya Dar es Salaam inaomba samahani.

Kwa wanaukoo toka Irore, nao wamesema tatizo kubwa kwao ni suala na nauli kuwa ni kubwa. Lakini cha msingi kufanyika ni kuzidi kuwahamasisha na kuwapa moyo wa kutambua umuhimu wa Mkutano Mkuu wa Ukoo pamoja na mikutano mingine.

Katika suala zima la mahusiano, ukaribu wa wanandugu na wanaukoo linaangaliwa kwa karibu zaidi. Mahusiano yanagusa mambo muhimu katika maisha ya kila siku mfano Elimu, Ugonjwa, Vifo pamoja na Starehe (Harusi, Send-Off, Kipaimara na Komunio). Elimu ni muhimu sana kwani inaongeza upeo na ufahamu wa kuweza kukabiliana na matatizo ya maisha ya kila siku.

Suala jingine ni ushirikiano katika nyanja mbalimbali mfano Biashara, kazi na kilimo. Hapa tunamaanisha kuunda kikundi ambacho kitakuwa na mfuko utakaokuwa unachangiwa na watu mbalimbali kulingana na shughuli na kipato.

Katika kujenga mahusiano imara, kutembeleana ni muhimu sana. Faida ya kutembeleana ni kujuliana hali, kusaidiana, kushauriana na kupeana mbinu na mwongozo wa kufauli katika maisha. Pia katika kutembeleana huwapa fursa wanaukoo/ndugu kuangalia mazingira mapya anayotembelea kama yanaweza kumfaa kuishi akilinganisha na mazingira aliyotoka.

Pia katika kushirikiana kuna haja ya kuwashawishi na kuwabembeleza wale wasio na uwezo ikiwa ni pamoja na kuwapa moyo, kuwashauri waondoe aibu na wajenge tabia ya kushirikiana. Katika kushirikiana inakuwa ni rahisi kuweza kutatua matatizo mbalimbali baina ya wenye nacho na wasionacho.

Kwa mfano katika shughuli nzima ya kuandaa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Ukoo wa Kivenule, inakuwa kitu kizuri na mfano kwa wengine kama tutaonyesha kwa vitendo haya tunayozungumza hapa.

No comments:

Post a Comment