MKUTANO MKUU WA 10 WA KAUKI

MKUTANO MKUU WA 10 WA KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

KAUKI-Kidamali, Iringa

KAUKI-Kidamali, Iringa
Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Thursday, August 15, 2013

MKUTANO MKUU WA SITA WA KAUKI-MAGUBIKE, IRINGA



MKUTANO MKUU WA SITA WA UMOJA WA UKOO WA KIVENULE (KAUKI)

 

Kuhusu KAUKI

KAUKI  ni Umoja wa Ukoo wa Kivenule, ulioanzishwa rasmi, katika Mkutano Mkuu wa Kwanza Ukoo wa Kivenule; uliofanyika kwa siku mbili, Kijijini Kidamali, tarehe 17 -18, mwezi Desemba, 2005. Harakati za kuanzishwa kwa KAUKI zilianza mwezi Februari 06, 2005 Jijini Dar es Salaam kwa kufanya mkutano mkuu wa kwanza wa mashauriano. Mikutano 10 ya mashauriano ilifanyika kutoka mwezi Februari hadi Novemba, 2005.

Dira ya KAUKI
Kuwa na jamii elewa, angavu na inayowajibika kwa kujitegemea.

Maono ya KAUKI
Kujengeana uwezo kwa kutumia raslimali, stadi, ujuzi, maarifa na weledi, kupitia mafunzo, kongamano, mijadala na mikutano ili kuboresha maisha.

Malengo ya KAUKI
Lengo Kuu
Kuinua na kuboresha maisha ya wanaukoo wa Kivenule, kielimu, kiuchumi na kimaisha kwa kutumia ujuzi, maarifa na raslimali zinazotunguka.

Malengo mengine mahsusi
1.    Kuujua na kuuelewa kwa kina Chimbuko na Historia ya Ukoo wa Kivenule;
2.    Kuzikusanya, kuratibu na kuhifadhi kumbukumbu mbalimbali za Ukoo wa Kivenule.
3.    Wanaukoo kufahamiana na kutambuana;
4.    Kufanya senza ya ndugu/wanaukoo wanaounda Ukoo wa Kivenule kila inapobidi kufanya hivyo na Senza hiyo itajumuisha watu waliohai na wafu;
5.    Kuanzisha Mfuko wa Ukoo wa Kivenule utakaosaidia kuinua kiwango cha Elimu na pia kusomesha wanaukoo wasio na uwezo wa kumudu kulipa ada za shule au vyuo;
6.    Kuboresha Elimu ndani ya Ukoo wa Kivenule ili ndugu/wanaukoo wawe na uelewa wa hali juu na kumudu mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia katika Dunia ya Utandawazi;
7.    Kusuluhisha na kutatua matatizo yanayojitokeza katika Ukoo wa Kivenule kwa kupitia vikao vinavyokubalika;
8.    Kuelimisha Wanaukoo/ndugu kuhusiana na madhara ya ugonjwa wa UKIMWI, matumizi ya Madawa ya Kulevya na Ulevi wa kupindukia;
9.    Kuinua viwango vya maisha vya wanaukoo wa Kivenule na kuishi maisha mbadala yenye milo kamili, furaha na nyumba bora na nadhifu;
10.           Kuongeza na kuimarisha mahusiano mazuri ndani na nje ya ukoo kwa kushirikiana katika matatizo mfano raha, ugonjwa, misiba pamoja na majanga makubwa;
11.           Kuwa na nguvu ya kurekebisha tabia zisizostahili kwa wanaukoo/ndugu ndani ya Ukoo na kutafuta suluhu ya migogoro/migongano baina ya mtu au jamii inayotuzunguka;
12.           Wanaukoo kuutambua na kuuelewa mtawanyiko/mgawanyiko wa Ukoo wa Kivenule;
13.           Wanaukoo/ndugu kushirikiana katika shughuli za uzalishaji mali pamoja na utendaji kazi wa kila siku;
14.           Kushirikiana na umoja au vikundi vingine vilivyoungana ili kuuletea Ukoo wa Kivenule maendeleo endelevu;
15.           Kuanzisha Mfuko wa kukopeshana (SACOSS);
16.           Kupunguza au kuondoa kabisa tabia ya uvivu na uzembe ndani ya Ukoo wa Kivenule; na
Kuanzishwa kwa KAUKI
Harakati za kuanzishwa kwa KAUKI zilianza kwa kuratibu mawazo ya wana-ukoo wawili, yaani Ndugu Faustino Kivenule na Ndugu Christian Kivenule mwezi Desemba 2004. Mawazo hayo yalifanyiwa kazi kwa kumshirikisha Ndugu Adam Kivenule, ambaye bila kuchelewa, waliweza kuandaa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mashauriano, jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa River Side, tarehe 6 Februari, 2005 – jijini Dar es Salaam.

Harakati nyingine za maandalizi zilielekezwa upande wa Kidamali, Ilole na Nduli. Kwa upande wa Kidamali, Mkutano wa kwanza wa mashauriano kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule, ulifanyika mwezi Mei ambapo wajumbe toka Dar es Salaam walisafiri kwenda huko ili kuwasilisha hoja, kufanya mashauriano na majadiliano, kuchagua viongozi wa kusimamia uratibu na kuunda kamati ya maandalizi.

Maeneo mengine kama Nduli na Ilole hazikuweza kufanya maandalizi ya moja kwa moja japo taarifa toka Dar es Salaam ziliweza kufikishwa na baadhi ya wanaukoo wanaishi huko. Mjumbe mmoja tu ndugu Augustino Kivenule, toka Mgongo ndiye aliyeweza kumudu kushiriki katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule.

Mkutano Mkuu wa Sita wa KAUKI
Huu ni Mkutano Mkuu wa Sita wa KAUKI; na tayari mikutano mingine mitano imekwisha fanyika, mitatu kijijini Kidamali na mkutano moja kijijini Irole na Nduli. Kwa utaratibu uliokubalika katika Mkutano Mkuu wa Pili na wa Tatu wa KAUKI, kuwa itabidi mikutano hii pia ifanyike sehemu nyingine. Na leo hii ni zamu yenu na ndiyo maana mkutano huu wa sita unafanyika hapa Magubike. Katika Mkutano Mkuu wa Tano wa KAUKI uliofanyika Nduli, washiriki wa mkutano huo kwa pamoja walikubaliana kuwa Mkutano Mkuu wa Sita ufanyike Magubike, leo tarehe 26 na 27 ya Mwezi Juni mwaka 2010.

Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Sita wa KAUKI - Magubike
Ili kuhakikisha kuwa Mkutano Mkuu wa Sita unafanyika na kufanikiwa, kila Kanda ililazimika kufanya maandalizi kwa utaratibu wake. Kwa hiyo kulikuwa na kanda za Kidamali, Magubike, Irole, Nduli na Dar es Salaam ambazo mara nyingi Uongozi umekuwa ukipokea taarifa zake. Kila kanda inaelewa majukumu yake ambayo ni pamoja na kukusanya michango, kuhamasisha ushiriki wa  wanandugu katika Mkutano wa Sita wa KAUKI huko Magubike na pia utoaji wa michango.

Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Sita wa KAUKI ilibidi yaanze mapema tu mara baada ya kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Tano wa KAUKI. Maandalizi ya mkutano huu ni jukumu la kila mwana-ukoo ambapo atashiriki kwa kutoa mchango, nafaka, mfugo au nguvu zake katika kuhakikisha kuwa maandalizi ya mkutano yanaenda vizuri.

Shughuli za KAUKI zinafanyika chini ya mwongozo ambao ni Katiba ya Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI). Katiba hii ilishaanza kutumika mara tu baada ya Mkutano Mkuu wa Pili wa KAUKI uliofanyika tarehe 24 na 25 Juni 2006. Nakala kadhaa za KAUKI tayari zimetolewa, kusambazwa na zinaendelea kutumika.

Kwa mujibu wa Katiba ya KAUKI, kuna viongozi mbalimbali waliochaguliwa katika Mkutano Mkuu wa Pili. Viongozi hao wanajulikana kama Viongozi wa Kanda. Kila Kanda ambayo ilikubalika kuwepo, katika Mkutano Mkuu wa Pili wa KAUKI, ina viongozi siyo zaidi ya mmoja. Viongozi hawa, wanawajibika kwa wanaukoo wanaotoka katika Kanda husika.

Wajibu wa viongozi hawa, ni kushirikiana pamoja na Viongozi wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule katika kutekeleza masuala mbalimbali ya maendeleo yanayouhusu ukoo. Pia, ni wajibu wa viongozi hawa, kuwashauri Viongozi wa KAUKI katika masuala mbambali yanayoukabili ukoo wetu kwa mfano masuala ya ugonjwa, elimu, uchumi na maendeleo.

Viongozi wa Kanda wana nguvu ya Kikatiba katika kutimiza wajibu wao na pia wana wajibu wa kuhakikisha kuwa mipango mbalimbali inayopangwa kupitia Kamati Kuu au Mkutano Mkuu wa KAUKI inatekelezwa.

Viongozi wa ngazi nyingine za juu kama Katibu, Mwenyekiti, Makamu wa Katibu, Makamu wa Mwenyekiti, Mweka Hazina na Msaidizi wake, wana wajibu wa kuwahimiza viongozi wa Kanda, kushirikiana baina yao wenyewe na pia kushirikiana na viongozi wakuu kutekeleza wajibu na majukumu mbalimbali ambayo yanatukabili.

Kwa mujibu wa KAUKI, viongozi wa Kanda, wana wajibu kuhudhuria vikao mbalimbali kama inavyoainishwa kwenye Katiba ya KAUKI. Wajibu huo pia unawagusa viongozi wengine wa KAUKI na wanawajibika ipasavyo kutekeleza na kutimiza wajibu wao.

MICHANGO YA MFUKO WA KAUKI

Kama ilivyokubaliwa kwenye Mkutano Mkuu wa Pili wa KAUKI na kama Katiba inavyoeleza, kila mwanaukoo, anawajibika kulipa michango kama inavyoanishwa kwenye Katiba ya KAUKI . Katiba ya KAUKI inafafanua kwa mapana kuhusiana na michango hiyo ya kila mwezi. Katiba ya KAUKI, inaeleza wazi kuhusiana na wajibu wa kila mwanaukoo kuchangia maandalizi ya Mkutano Mkuu wa KAUKI (Ibara ya 5:3(ii). Matumizi ya michango hiyo ni kuwasaidia wanaukoo katika matatizo mbalimbali ya ugonjwa, masomo na pia kiuchumi pindi mfuko huo utakuwa umetuna kutokana na kila mwanaukoo kuuchangia ipasavyo. Pia michango hiyo itasaidia gharama mbalimbali mfano kufanya mikutano.

Viongozi wa Kanda, walipewa jukumu la kukusanya michango hiyo. Kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa katika Mkutano Mkuu wa Tatu wa KAUKI, stakabadhi zikiwa na mhuri wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI), zilisambazwa kwa viongozi husika wa Kanda kwa ajili ya shughuli za ukusanyaji wa michango hiyo. Kila anayetoa mchango ni lazima apewe stakabadhi ya malipo halali na si vinginevyo.

Taarifa kuhusiana na suala la michango, viongozi wa kanda watatoa taarifa zaidi.

Lakini viwango hivi vinavyotajwa kwenye Katiba havimfungi mwanaukoo kutoa zaidi. Mara nyingi katika utoaji wa michango kwa ajili ya maandalizi ya Mikutano Mikuu, kadi huandaliwa na kusambazwa kwa wana ndugu mbalimbali na pia kwa jamaa na marafiki zetu. Jambo hili ni nzuri kwa sababu linaonyesha heshima kwa yule unayemwomba atoe mchango wako. Kwa sababu hiyo, kadi maalum huandaliwa na kila mmoja wetu ambaye anahitaji kadi hupewa kwa kiwango kile kinachotakiwa.

Pia, viongozi wa KAUKI walipendekeza wanaukoo kuwa wabunifu katika kutoa michango yao, hii ni pamoja na kutoa bidhaa au mazao ambayo yatajulikana kama mchango. Kama ni nafaka au mifugo, inaweza kutumika kama chakula moja kwa moja au ikauzwa na zikapatikana fedha ambazo zitajumuishwa kwenye bajeti inayoandaliwa.

MICHANGO TOKA VYANZO VINGINE

Tubuni miradi ambayo inaweza kutuboreshea mapato ya KAUKI na pia kila mwana-ukoo ahusike kikamilifu. Pia, hii kazi kwa viongozi wa mipango ya maendeleo kuwa wabunifu wa shughuli mbalimbali za uzalishaji mali. Tunaweza kubuni miradi ya maandazi, chapati, mama lishe, kilimo au miradi yoyote ambayo mnadhani itatusadia kupata fedha kwa ajili ya kuweza kufanikisha mikutano kama hii.

TAREHE YA MKUTANO MKUU WA SITA WA KAUKI

Tarehe 26 ya Jumamosi na 27 Jumapili Juni 2010, ilipendekezwa kuwa ndiyo siku ambapo Mkutano Mkuu wa Sita wa KAUKI utafanyike Magubike.

YATAKAYOJIRI KATIKA MKUTANO MKUU WA SITA WA KAUKI

Kwa mujibu wa ratiba ya mkutano, kutakuwa na shughuli mbalimbali katika siku mbili za mkutano. Pamoja na mambo mengine, kutakuwepo na uwasilisha wa mada kadhaa na pia taarifa mbalimbali kutoka kwa wana-KAUKI na viongozi, mfano:
·         Mada:   1.CHIMBUKO NA HISTORIA YA UKOO WA KIVENULE
2. CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI KAUKI KUJILETEA MAENDELEO
3. HISTORIA YA WAHEHE
·         TAARIFA YA UTENDAJI WA KAUKI
·         TAARIFA YA SHUGHULI ZA MAENDELEO KATIKA KANDA
·         KUSOMA RIPOTI YA MKUTANO MKUU WA TANO WA KAUKI
·         UZOEFU WA WANAUKOO KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO
·         MAJADILIANO YA HOJA MBALIMBALI AMBAZO ZIMEWASILISHWA NA WASHIRIKI KATIKA MKUTANO
·         MAHITAJI YA KAUKI NA JINSI YA KUFANIKISHA KUPATIKANA KWA MAHITAJI HAYO: Huu ni mjadala wa jumla na kila mjumbe wa mkutano anashiriki moja kwa moja kutoa mawazo yake. Katibu na watendaji wengine wa KAUKI wana jukumu ya kuyanakili maswali na majibu yote kwa ajili ya kufanyiwa kazi
·         MAJUMUISHO NA TATHMINI YA MKUTANO
·         MIPANGO NA MIKAKATI YA MBELENI
·         KUTANGAZWA KWA TAREHE YA MKUTANO MKUU WA SABA
·         SHUKRANI
·         KUFUNGA MKUTANO

Utambulisho baina ya wanaukoo utafanyika kwa kina na kila ndugu/mwanaukoo atakuwa na kitambulisho ambacho atakivaa kifuani kwake. Kutakuwa na fursa mbalimbali kwa wanandugu kupeana uzoefu mbalimbali wa utafutaji wa maisha bora. Mbinu za kujiinua kimaisha zitafundishwa na wadau wenye uzoefu pamoja na aina mbalimbali za miradi ambayo ndugu wanaweza kufanya.

Tutakuwa na kipindi cha kupeana uzoefu wa shughuli mbalimbali za kiuchumi kutoka katika maeneo mbalimbali ambako ndugu wanaishi. Kama ilivyofanyika katika Mkutano Mkuu wa Tatu wa KAUKI, maeneo yatakayotolewa uzoefu Kilimo, biashara na ajira kutoka katika maeneo mbalimbali. Kwa kupeana elimu ya ujasiliamali itasaidia kutufungua macho na hivyo kuongeza uwezo wa kufikiri na kwenda kutafuta maisha katika maeneo ambayo ni mbadala kwetu. Pia taarifa hizi zitawasaidia wanandugu toka maeneo mengine kupata mwanga wa shughuli mbadala zitakazosaidia kupata kipato na kuboresha maisha.

Pia huu ni mwaka wa uchaguzi. Tunategemea kuwa wana-ukoo wataitumia fursa hii ipasavyo kuwachangua viongozi wanaoona wanafaa kuiongoza jumuiya yetu.

UCHAGUZI MKUU WA VIONGOZI WA KAUKI
Taarifa kuhusu uchaguzi wetu tayari ilikwisha tolewa kwenye tovuti yetu inayoitwa: http://www.tagumtwafoundation.wetpaint.com . Natumaini ni watu wachache tu wamemudu kuiangalia na lakini bado kama viongozi tuna wajibu wa kuwatambulisha katika mkutano huu. Wafuatao ni viongozi wapya waliochaguliwa:

VIONGOZI WAKUU WA KAUKI
1.    Mwenyekiti                    Donath Mhapa
2.    Makamu Mwenyekiti              
3.    Katibu Mkuu                  Adam Kivenule
4.    Katibu Msaidizi                       Christian Kivenule
5.    Mweka Hazina                        Justine Kivenule
6.    Mweka Hazina Msaidizi           

UCHAGUZI WA WALEZI WA KAUKI
Wafuatao ni Walezi wa KAUKI………………………………….

VIONGOZI WA KANDA
Kila Kanda itakuwa na wawakilishi wawili
1.    Mwenyekiti                   
2.    Katibu                          
3.    Mweka Hazina                       

Kutakuwa na Viongozi wa Kamati mbalimbali
A. Mipango na Maendeleo
  1. Mwenyekiti:      
  2. Katibu:     
B. Mahesabu na Fedha
  1. Mwenyekiti:      
  2. Katibu:     
C. Maafa na Matatizo
  1. Mwenyekiti:      
  2. Katibu:     

D. Nidhamu na Maadili
  1. Mwenyekiti:      
  2. Katibu:             

Angalizo: Viongozi wa Kamati ya Mahesabu na Fedha, watashirikiana na Mweka Hazina katika kuratibu shughuli zote za ukusanyaji wa michango mbalimbali, wakati wa maafa, wakati wa mkutano mkuu, mikutano na pia mchango wa kila mwezi.

MIPANGO YA KAUKI

KAUKI inajikita kujiimarisha katika ngazi zote za kiutendaji, kiuendeshaji na kuleta mabadiliko ya kiuchumi, kielimu, kisiasa, kimaendeleo, na kimapinduzi. Baadhi ya mikakati KAUKI ni pamoja na:
1.    KAUKI kuwa na ofisi yake Kijijini Kidamali na pia sehemu nyingine za Kanda ambapo wanaukoo wanadhani ni muhimu kuwa na ofisi. Jambo hili lilishaanza kufanyiwa kazi na pia eneo ambalo inabidi ofisi iwepo lilishapatikana katika majadilian ya awali ya mwaka 2008. Viongozi toka eneo ambalo ofisi inabidi ifunguliwe watatuhabarisha zaidi wapi wamefikia.
2.    Suala na pili ni kupata usajili ili tuwe na fursa ya kufanya shughuli kubwa zaidi. Bado suala hili lipo katika mchakato, na taratibu nyingine zote za namna ya kupata usajili zilikwisha fuatiliwa. Ni matumaini yetu uongozi mpya uliochaguliwa, unalifanyia kazi kazi jukumu hili muhimu.
3.    KAUKI kuwa na sanduku lake la posta. Bado jambo hili halijatekelezwa na natumaini hatua za makusudi inabidi zichukuliwe. Hakuna masharti makubwa zaidi ya kulipa fedha tu. Ni changamoto kwa viongozi wa KAUKI na nadhani hatuna haja ya kusubiri zaidi ya kuchukua hatua zinazostahili kulikamilisha hili.
4.    Kuwa na Akaunti katika Benki yeyote. Ufunguzi wa Akaunti ulikwisha fanyika kabla ya Mkutano Mkuu wa Nne wa KAUKI uliofanyika Irole. Hima wanaukoo tutoe michango yetu na pia tusaidie kuitunisha akaunti yetu. Wangapi wanalipa mia tano za kila mwezi? Mnapata stakabadhi? Wangapi bado hawajalipa? Kwa nini? Hizi ndizo changamoto kwetu. Bila kujitoa hatuwezi kufanikiwa. Msitegemea watu wachache tu ndio wanaoweza kubadili maisha ya wanaukoo wote. Inabidi tuunganishe nguvu zetu wote. Wahenga walisema, ‘Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu’.
5.    KAUKI kuwa na vitendea kazi mfano Kompyuta, Printa, Simu, Meza na Viti. Bado kutekelezwa kutokana na uhaba wa fedha na pia bado wanaukoo hawajaonesha mwito wa kutoa michango ya kila mwezi. Hivyo tunawahimiza kutoa michango hiyo ili baadhi ya mipango na malengo ya KAUKI yakamilike. Tutafanya harambee ili tuweze kununua vifaa hivyo, mfano Kompyuta na printa yake. Wangapi mpo tayari kuchangia?
6.    KAUKI kuanza kutoa elimu mbalimbali kwa wadau wake. Tumeanza na sehemu ndogo na mojawapo ni wakati wa mikutano hii. Lakini bado tunadhani inabidi tutafute fursa nyingine. Kama tungekamilisha suala la ofisi, natumaini fursa nyingi za kupata masomo kwa wana-ukoo zingetafutwa kwa hali na mali.
7.    KAUKI kubuni na kutekeleza miradi mbalimbali ambayo itawasadia wanajamii. Sijapata taarifa rasmi labda viongozi wa Irole wanaweza kutupa taarifa. Mwenyekiti wa kipindi kilichopita Bwana Nyakunga aliahidi kuwa wangeanzisha mradi wa alizeti, Sijui walifikia wapi? Tupatieni taarifa. Tuanzishe mashamba ya KAUKI na kila kanda iwe na shamba lake. Mazao yatakayopatikana yatatumika kama sehemu ya chakula wakati wa mikutano hii. Na pia iliyobaki itauzwa na fedha kuwekwa katika mfuko wa KAUKI.
8.    KAUKI kuwa na kitengo cha Utaalam wa Kitaaluma na Kiujuzi ambacho kitafanya shughuli za kuiletea fedha KAUKI, pamoja na miradi mbalimbali. Tunasubiri kukamilika kwa ofisi na kazi itaanza mara moja. Binafsi nipo tayari kujitolea kuhakikisha tunafanikiwa katika suala hili.
9.    KAUKI kujitangaza kwa asasi nyingine za ndani ya nchi na nje kwa kutumia teknolojia ya kisasa yaani kuwa na tovuti. Tumeanzisha tovuti (blog) na natumaini bado haijafikiwa na wengi. Mpango mzuri ni sisi wenyewe kulisajili jina la KAUKI (Domain Registration) kwa wamiliki wa mitandao na kuiweka hewani tovuti yetu kwa watoa huduma za mawasiliano ya tovuti na mitandao.
10.           Kuchapisha kitabu toleo la kwanza cha Umoja wa Ukoo wa Kivenule kwa kipindi cha mwaka 2008 – 2009. Kamati iliyoundwa imeshindwa kukutana na kuikamilisha kazi hiyo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za:
  • Kukosa pesa
  • Mtawanyiko wa wajumbe
  • Shughuli yenyewe inahitaji pesa kwa mfano kazi ya uhariri na uchapishaji
Kutokana shughuli kuwa ngumu na kushindwa kufanyika kama ilivyopangwa, inabidi kamati iwasilishe taarifa na mapendekezo kwa wajumbe kuhusu hatua ambazo imechukua na nini imekifanya; na pia nini kifanyike, kwa kurejea hadidu zake na pia majukumu yaliyopaswa kufanyika kabla ya mkutano huu wa tano.

MAPUNGUFU YA KAUKI NA WATENDAJI WAKE
Uongozi wa KAUKI bado umeonyesha mapungufu na hii pia inaathiri mfumo mzima wa utendaji kazi zake. Baadhi ya mapungufu hayo ni pamoja na kushindwa kubisa kutekeleza baadhi ya mikakati ambayo ilikuwa ni sehemu ya makubaliano na pia mipango ya mbeleni ya maendeleo ya KAUKI. Kwa mfano baadhi ya majukumu ambayo bado hayajatekelezwa ni pamoja na:-
1.    Kutokuwa na Kalenda ya Shughuli za Mwaka;
2.    Kushindwa kufanya vikao vya Kamati Kuu;
3.    Ushirikiano finyu baina ya viongozi wa ngazi mbalimbali wa KAUKI kutokuwepo kwa mpango-kazi, tathmini ya utendaji kazi na utekelezaji wa mipango ya maendeleo;
4.    Viongozi wengi wa KAUKI kushindwa kutekeleza wajibu wao;
5.    Makusanyo hafifu ya michango; Wangapi wamelipa mpaka muda huu?
6.    Viongozi kutokuwa mfano mzuri katika kutoa michango. Tunaamini kiongozi lazima awe ni mfano wa kuigwa; Je viongozi wote mnatoa michango ya kila mwezi. Wangapi wamelipa mpaka muda huu?
7.    Wanaukoo kuonesha mwitikio duni katika ushiriki wa Mikutano Mikuu. Mfano wa Wanaukoo kutoka Dar es Salaam; na
8.    KAUKI kutokuwa na ofisi. Ni mwaka wa pili sasa jambo hili ilibidi liwe limekamilika lakini mpaka sasa bado ofisi haijaanza kufanya kazi. Hii ni changamoto kwa viongozi wetu.

VIONGOZI WAKUU WA KAUKI

1.    Mwenyekiti                    Donath      P.     Mhapa
2.    Makamu Mwenyekiti              
3.    Katibu Mkuu                  Adam                A.     Kivenule
4.    Makamu Katibu                     
5.    Mhasibu Mkuu                        Justin         D.     Kivenule

Walezi

1.    Stephan        Mhapa
2.    John             Kivenule
3.    Augustino              Kivenule

HITIMISHO
K
AUKI imeendelea kujikita katika kuongeza uangavu na weledi kwa wanaukoo kutokana na kutambua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika dunia hii ya utandawazi. Mazingira na hali halisi iliyopo ambayo kila mwana-KAUKI anaiona, ameguswa nayo au kuathiriwa nayo ni vigezo tosha. Propaganda na kejeli kama kauli mbiu kutoka kwa watu mbalimbali duniani hususiani kwa wanasiasa wetu yameendelea kuwaathiri wana-KAUKI na watanzania kwa ujumla. Tatizo la ufisadi wa raslimali za watanzania mkiwemo ninyi, rushwa katika huduma za jamii mfano kukosa dawa hospitalini, maji safi ya kunywa, elimu duni na ukosefu wa ajira, vyote vinamwathiri sisi. KAUKI inaamini kuwa mwana-KAUKI mwenyewe ndiye mwenye uamuzi wa mwisho ya kuamua hatma na mustakali wa maisha yake ya sasa na baadaye. KAUKI haitarajii maisha bora kwa kila mwana-KAUKI au mtanzania mwingine yataletwa na wanasiana au watu baki waliopo nje ya nchi yetu. Jukumu la maendeleo ni letu sisi wenyewe. Ndio maana tunahimiza watu kujitoa kwa hali na mali kuuchangia mfuko wetu ili uweze kuisaidia jamii yetu katika nyanja zote za kiuchumi, elimu, afya na maendeleo.

Yote yanayofanyika katika mikutano hii ni sehemu ndogo ya jitihada kubwa zinazofanywa na KAUKI. Ahadi za wanasiasa ni za mdomoni tu na hatuamini hata siku moja kama wana-KAUKI mtayafurahia maisha bora kwa kukaa mtu moja moja au kwa kutounganisha nguvu zenu. Wanasiasa wana-agenda zao ambazo mara nyingi huwa kuangalia maslahi yao na kuyalinda. Mfano wa hivi karibuni kwa Wabunge wameomba kujiongezea mshahara hadi kufikia milioni kumi na mbili kutoka milioni saba (7) wanazolipwa sasa. Mishahara hiyo ni kodi za maskini sisi wana-KAUKI na wenzetu ambao hawapo hapa. Kwa hiyo suala la kujikwamua kimaendeleo la kila mmoja wetu hapa na si vinginevyo. Hizi ni mojawapo ya harakati za kujikwamua na lindi la umaskini unaotukabili. Lakini harakati nyingine unazifanya wewe kama mwana-KAUKI wakati wa kupiga kura yako kumchagua kiongozi. Msilemae na rushwa. Tumieni vizuri fursa yenu kwa kuchagua viongozi bora. Pengine hata katika chaguzi wa viongozi wa KAUKI watu wanaweza kutoa rushwa ili wachaguliwe! Tumieni fursa zinazopatikana kwa kuwahoji wale wanaotaka nafasi za uongozi, nini kimewatuma kugombea nafasi hizo, na sisi kama wana-KAUKI tutarajie nini. Jamii yetu ni maskini wa kila kitu, wataisaidiaje?

Siasa za porojo zimepitwa na wakati. Kama wana-KAUKI inabidi kuhimiza mabadiliko ya kiitikadi na kimaendeleo. Wajibu watu ni kuwadhihirishia nini tunakusudia kukifanya ili kuboresha maisha yetu. Maisha bora kwa kila mtanzania kama mnavyoahidiwa katika kampeni za uchaguzi ni ndoto tu.

Kwa mfano huu ni mwaka wa tano toka uchaguzi mkuu ufanyike na wananchi mliahidiwa maisha bora kwa kila mtanzania. Je haya maisha mnayoishi kweli ni maisha bora ukilinganisha na maisha mliyokuwa mnaishi siku za nyuma. Mfumuko wa bei, kupanda kwa bei za mafuta kila wakati, njaa, ufisadi, dhuluma na kejeli na hata vifo kwa wapigania haki za wanyonge. Hii ni hali ya kukatisha tamaa na sisi wana-KAUKI tuna kila wajibu na kukabiliana na hali hii.

Tukikaa pembeni na kuacha yatokee basi nasi tutaangamia kwani kinachofanyika kinatuathiri sisi. Ufisadi na wizi wa mali ya umma unatuathiri sisi. Kwa mfano kukosekana kwa huduma za msingi mfano huduma za afya, shule bora, maji na bei kubwa ya umeme ni matokeo ya dhuluma hizi. Hivyo kama wana-KAUKI bado tuna jukumu kubwa la kukabiliana na kila aina ya uozo, na adui wa maisha na maendeleo yetu.

Mbadala ya maendeleo ya nchi ya Tanzania unakutegemea wewe mwana-KAUKI, dhima, uamuke toka sasa na uelekeze nguvu zako katika kuiboresha KAUKI ili jamii yetu ipate maendeleo.

Mwisho
Imetolewa na:

___________________________               ___________________________
Donath Mhapa                                           Adam A. Kivenule

Mwenyekiti – KAUKI                                      Katibu - KAUKI

No comments:

Post a Comment